Welcome, Guest |
You have to register before you can post on our site.
|
Online Users |
There are currently 70 online users. » 0 Member(s) | 68 Guest(s) Bing, Facebook
|
Latest Threads |
Buy Vilitra 60 Mg |【Get E...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-24-2023, 11:45 AM
» Replies: 0
» Views: 0
|
How to take Cenforce50?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-19-2023, 12:59 PM
» Replies: 0
» Views: 0
|
About the Vidalista 60 Mg...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-04-2023, 04:07 PM
» Replies: 0
» Views: 0
|
What Is Vidalista 60?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-03-2023, 10:49 AM
» Replies: 0
» Views: 0
|
How to take Cenforce 100 ...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
03-29-2023, 02:37 PM
» Replies: 0
» Views: 66
|
How is Vidalista 10 Mg us...
Forum: Watunzi wa Kiswahili
Last Post: Kieth_winsett
03-27-2023, 01:26 PM
» Replies: 0
» Views: 117
|
Obtain Thesis Paper Assis...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Minny02
03-24-2023, 03:01 PM
» Replies: 0
» Views: 200
|
SEO services for sports f...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Maria Poland
03-17-2023, 01:51 PM
» Replies: 1
» Views: 223
|
NUKUU ZA KISWAHILI DARASA...
Forum: Nukuu
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:31 PM
» Replies: 0
» Views: 788
|
NECTA K4 2022
Forum: Mitihani
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:25 PM
» Replies: 0
» Views: 403
|
|
|
SHAIRI: KUTUNGA |
Posted by: MwlMaeda - 08-14-2021, 08:17 AM - Forum: Ushairi
- No Replies
|
|
KUTUNGA
Ewe kaka ewe dada, ninakuomba sikiya,
Somo lisilo na ada, kwa utuvu zingatiya,
Nataka nikupe rada, ikufae kwenye ndiya,
Itakupa msaada, safari kutokawiya,
kutunga kwataka mada, tamu zilizotuliya,
Mtunga ni yake ada, wazo kujitafutiya,
Kwazo tele jitihada, ndipo sasa hutungiya,
Tamu mithili ya bada, mengi zinaangaziya,
Si pekee za mawada, katika yake jamiya,
kutunga kwataka mada, tamu zilizotuliya.
Somo naweka bayana, wewe kukusaidiya,
Chukua bila hiyana, mtunga tamthiliya,
Riwaya zitazofana, ngano, mashairi piya,
Tumia lugha nyanana, ile inayovutiya,
Kutunga kwataka sana, lugha iliyo sawiya.
Uwe mtunzi mwanana, si wale wakupupiya,
Misamiati hawana, kazi yao kurudiya,
Maneno yafuatana, neno moja mara miya,
Kazi unapoiyona, inakutia udhiya,
Kutunga kwataka sana, lugha iliyotuliya.
Ndipo mimi mtetezi, leo hii nakwambiya,
Kwani kuketi siwezi, tungo nikashuhudiya,
Zilizo tele telezi, uchungu zinazotiya,
Pamwe nacho kigegezi, unapo ziangaliya,
Kutunga kwataka mada, kutunga kwataka lugha.
Tama wangu uamuzi, haya kukufikishiya,
Alinambia mjuzi, aliye na njema niya,
lengo kutumia uzi, ufaao kutungiya,
Utunge kama wa juzi, zile zilizotimiya,
kutunga kwataka mada, kutunga kwataka lugha.
Mshairi Machinga,
mfaumehamisi@gmail.com,
+255716541703/752795964,
Dar es salaam, Kkoo.
|
|
|
SHAIRI: NI HERI NINGEKUROGA |
Posted by: MwlMaeda - 08-13-2021, 11:43 PM - Forum: Ushairi
- Replies (1)
|
|
NI HERI NINGEKUROGA
Mara ngapi nakuonya, uwe wangu peke yangu,
Haya uliyoyafanya, yamenitia uchungu,
Vile nilivyokuonya, ni bure maneno yangu,
Kwa haya uliyofanya, ni heri ningekuroga.
Sikuthubutu limbwata, moyo wako kuushika,
Niliepuka matata, usije ukawehuka,
Leo haya kunipata, na mimi nimegutuka,
Kwa haya uliyofanya, ni heri ningekuroga.
Mara kadha niliwaza, nende kwa Kalumanzila,
Mawazo nikapuuza, chanzo cha haya madhila,
Sasa kimetua kiza, siwezi tena kulala,
Kwa haya uliyofanya, ni heri ningekuroga.
Sasa mbali umekwenda, kurudi umekaidi,
Ili unitoe chonda, utimize makusudi,
Nimebakia kukonda, pamwe na zangu juhudi,
Kwa haya uliyofanya, ni heri ningekuroga.
Yako simu ninapiga, haupokei mwendani,
Nimebaki kichwa boga, sijui nifanye nini,
Au chupa ningesaga, nitoweke duniani,
Kwa haya uliyofanya, ni heri ningekuroga.
Nakumbuka ile juzi, na ulivyonitukana,
Umezidi siku hizi, tena mapenzi hakuna,
Nalia sitokwi chozi, ninabaki kujikuna,
Kwa haya uliyofanya, ni heri ningekuroga.
Beti chache nasimama, sili ugali kushiba,
Unionee huruma, uchungu unanikaba,
Kwa raha imegoma, zimepita siku saba,
Kwa haya uliyofanya, ni heri ningekuroga.
Mtunzi Filieda Sanga Mama B
Mabibo Dsm
0753738704
|
|
|
SHAIRI: HASARA YA KIWAKACHO |
Posted by: MwlMaeda - 08-13-2021, 11:24 PM - Forum: Ushairi
- No Replies
|
|
HASARA YA KIWAKACHO
Kiwakacho huzimika, zii kisiwake tena,
Waja wanaposhituka, kiza kinasemezana,
Hakuna wa kuinuka, aweke nuru bayana,
Hasara ya kiwakacho, huwaka na kuzimika.
Huwaka kwa kuripuka, ripuripu kusongana,
Mwisho wake ukifika, muwako wake hakuna,
Wenye subira kushika, hubaki kukonyezana,
Hasara ya kiwakacho, huwaka na kuzimika.
Ukingoni ukifika, moto ulowaka sana,
Hapo inathibitika, muwako huna maana,
Moto ukisha zimika, huna thamani bayana,
Hasara ya kiwakacho, huwaka na kuzimika.
Hata uvuke mipaka, iwe umeshindikana,
Kwa mafuta ya Merika, au Kusini ya China,
Mwisho ukisha wadika, waja watasemezana,
Hasara ya kiwakacho, huwaka na kuzimika.
Mtunzi Filieda Sanga
Mama B
Mabibo Dsm
0753738704
|
|
|
SHAIRI: KISU |
Posted by: MwlMaeda - 08-13-2021, 06:10 PM - Forum: Ushairi
- No Replies
|
|
KISU
Pokea zino salamu,msomaji msifika
Leo nashika kalamu, ninalo lakuandika
Kwani nina kubwa hamu,tungo ipate someka
Sifa ya kali makali,wala usambe umbile
Si hoja wake muundo,hivyo usirubunike
Utakupata mfundo,mwishowe ufedheheke
Utembee kwa vishindo,kukata visikatike
Sifa ya kisu makali,wala usambe umbile
Japo kiwe kama panga,hima chungua makali
Kama butu hata kanga,kumchinja ni muhali
Watu watakusimanga,ziruke zako akili
Sifa ya kisu makali,wala usambe umbile
Nakitoke uhabeshi,ala iwe ya dhahabu
Watakiona bileshi,bure upate aibu
Tena hata kwa mapishi,ni kujitia adhabu
Sifa ya kisu makali,wala usambe umbile
Kaditama tambueni,vingine havinoleki
Uwe na tupa dazeni,ukali hawongezeki
Jisu hili kuwa ndani,ni kujitia hamaki
Sifa ya kisu makali, wala usambe umbile
Abdul Ndembo
Mburahati Sekondari
|
|
|
MULIKA : MAELEKEZO KWA WAANDISHI WA MAKALA |
Posted by: MwlMaeda - 08-13-2021, 05:29 PM - Forum: Uandishi/Utungaji
- No Replies
|
|
MULIKA ni jarida la taaluma ya Lugha na Fasihii ya Kiswahili. Jukumu lake kuu ni kukusanya na kusambaza maarifa yanayohusu Lugha na Fasihi ya Kiswahili yaliyokitwa katika utafiti mpevu. MULIKA limeendelea kuwa daraja kati ya watumiaji wa Kiswahili popote walipo, na wataalamu wa Kiswahili katika Sekondari na Vyuo vya Elimu ya Juu Afrika ya Mashariki.
Kamati ya Uhariri
Dkt. Ernesto
Mosha
– Mkurugenzi, Taasisi ya Taaluma za Kiswahili
Prof. Mugyabuso
Mulokozi – Mhariri Mkuu
Dkt. Mussa
Hans
– Mhariri Msaidizi
Dkt. Lutz
Diegner
– Chuo
Kikuu cha Humboldt,Ujerumani
Dkt. Athumani
Ponera
– Chuo Kikuu cha Dodoma, Tanzania
Dkt. Miriam Kenyani
Osore
– Chuo Kikuu
cha Kenyatta, Kenya
Washauri wa wahariri
Prof. Cyprean
Niyomugabo
– Chuo
Kikuu cha Rwanda, Rwanda
Prof. Sangai Mohochi
– Chuo
Kikuu cha Rongo, Kenya
Dkt. Abel Mreta
– Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania
Dkt. Joseph Nyehita
Maitaria
– Chuo Kikuu cha Karatina, Kenya
Dkt. Selemani
Sewangi
– Baraza la Kiswahili la Taifa, Tanzania
Prof. Ipara
Odeo
– Chuo Kikuu cha Kibabii, Kenya
Dkt. Wael Nabil
Ibrahim
– Chuo Kikuu cha Al Azhar, Misri
MAELEKEZO KWA WAANDISHI
WA MAKALA
MULIKA ni jarida la
taaluma ya Lugha na Fasihii ya Kiswahili. Jukumu lake kuu ni kukusanya na
kusambaza maarifa yanayohusu Lugha na Fasihi ya Kiswahili yaliyokitwa katika
utafiti mpevu. MULIKA limeendelea kuwa daraja katti ya watumiaji wa Kiswahili
popote walipo, na wataalamu wa Kiswahili katika Sekondari ba Vyuo vya Elimu ya
Juu Afrika ya Mashariki.
Jarida huchapishwa mara
moja kwa mwaka.
Jarida linapokea Makala
yaliyoandikwa kwa Kiswahili TU. Makala yapigwe chapa kwenye karatasi za A4,
mistari ikitengwa kwa kipimo cha nafasi mbili. Upande mmoja tu wa karatasi
utumiwe.
Mwandishi awasilishe
kwa Mhariri, nakala tatu za muswada wake, pamoja na nakala tepe iliyowekwa katika mfumo wa kikompyuta
katika muundo wa Microsoft WORD.
Ukurasa wa kwanza wa
Makala uoneshe jina la Makala, jina kamili la mwandishi (au waandishi) wa
Makala (Ikiwa ni pamoja na wwadhifa wake) na anuani yake.
Ukurasa wa pili uoneshe
jina la Makala na ufupisho wa Makala (Ikisiri) kwa maneno yasiyozidi 300. Jina
la mwandishi lisiandikwe.
Unapotaja marejeleo
kwenye matini taja jina l mwisho la mwandishi, likifuatiwa katika mabano na
tarehe ya chapisho lake na kurasa zilizorejelewa, k.m. Yahya (1983:139). Kwenye
orodha ya marejeleo au bibliografia majina ya marejelewa yapangwe kialfabeti.
Tanbihi ziwekwe namba
na zitumike pale tu inapobidi. Maelezo ya tanbihi yatolewe kwenye ukurasa wa
pekee mwisho wa Makala, yaani ya kuorodhesha marejeleo.
Makala yatatathiminiwa
na walau wasomaji wawili, bila ya wao kujua mwandishi ni nani. Waandishi waepuke
kuweka utambulisho wowote katika Makala zao ilo wanaosoma Makala hayo na
kuyatathmini wafanye kazi yao kwa uyakinifu. Waandishi ambao Makala yao
yatakubaliwa kuchapishwa watapatiwa NAKALA MOJA YA Jarida lenye Makala
yao pamoja na malopoo kumi ya Makala yao.
Makala yapelekwe kwa:
Mhariri
MULIKA
Taasisi ya Taaluma za
Kiswahili
Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam
CHANZO >>>>>>>
|
|
|
UTENZI WA FURAHA |
Posted by: MwlMaeda - 08-13-2021, 05:54 AM - Forum: Ushairi
- No Replies
|
|
UTENZI WA FURAHA
Kwakowe Mola Wadudi,
Utenzi naabtadi,
Unipe kujitahidi,
Tenzi iwe kitabuni.
Safusafu beti hizi,
Nisitunge nisihizi,
Nipe yako maongozi,
Uliye wangu Manani.
Nishike palipo nibu,
Unifungue ububu,
Nandike yaso harabu,
Yawafae duniani.
Dunia utenzi huu,
Uwe breviari kuu,
Wazee na vitukuu,
Uwaache furahani.
Utenzi wa manukato,
Kwa wakubwa na watoto,
Na beti zenye mnato,
Viwashike akilini.
Mabeti jozi kwa jozi,
Wazaliwa na wazazi,
Utungo huu kuhozi,
Wakautia thamani.
Ewe Mola wa Mbawazi,
Niongeze shinikizi,
Situnge ya uchokozi,
Nihasiri majirani.
Bali uwe yangu taa,
Nendapo njia kung’aa,
Hata chini nikikaa,
Nibaki mwako nuruni.
Pia nina maombezi,
Kwa mama yangu mzazi,
Mlaze basi mwenyezi,
Palipo pako peponi.
Peponi awe mkazi,
Malaika watetezi,
Ndio wakawe walezi,
Mama awe farajani.
Nikakufuru wakati,
Nikwone Wabarakati,
Wewe nduli kama nyati,
Nakuomba samahani.
Nisamehe Mola wangu,
Kwa hasira za uchungu,
Msiba wa mama yangu,
Mungu nikuone nyani.
Nimetambua najua,
Muumba na muumbua,
Utoaye na kutwaa,
Anayekupinga nani?
Miaka kumi kutimu,
Tangu awe marehemu,
Mama yangu Mariamu,
Namuweka utenzini.
Mola una maajabu,
Mambo unayaratibu,
Pamwe nilipata tabu,
Ukanikuza thamani.
Hivihivi ukiwani,
Ukanitia shuleni,
Nikafika na chuoni,
Chuo hapo Mlimani.
Ukiwani nikasoma,
Ukanipa na uzima,
Pia marafiki wema,
Nikabaki farajani.
Yupo Ntambi wa Stella,
Wa Kagera si Mwela,
Naye huyu sikulala,
Tulikesha darasani.
Ni mapenzi nikahozi,
Yakanifuta machozi,
Nikazimaliza kozi,
Kufundishwa darasani.
Umenituza kipaji,
Kutunga nikawa gwiji,
Ni rahisi kama uji,
Nikorogavyo mekoni.
Kipaji chaninyanyua,
Sasa ninainukia,
Nawe wanongoza njia,
Wengine hunitamani.
Huniuliza maswali,
Naipataje sahali,
Nikatunga bulibuli,
Pasi sumbuo kichwani?
Hata mwenyewe sijui,
Ni kama maruirui,
Hii fani sikatai,
Naiweza kama nini.
Japo sipendi kutuna,
None wengine hawana,
Ukweli wanauona,
Wanafumbia moyoni.
Dibaji naterekeza,
Kueleza nakatiza,
Nisijefanya ajiza,
Wanione majununi.
Naikabili furaha,
Kinyume chake karaha,
Hapa sileti mizaha,
Naiweka upeoni.
Furaha ijapo kwetu,
Sisi hujiona watu,
Huwa sio mali kwetu,
Inapokuja huzuni.
Furaha kama yakuti,
Kuipata ni bahati,
Tasifu Wabarakati,
Kumuweka masifuni.
Pia ni kama feruzi,
Kuwa nayo ni ujuzi,
Shida hazifululizi,
Hiki ni kitu thamani.
Tena ni kama dhahabu,
Inayokimbiza tabu,
Yende mbali jitanibu,
Furaha kwetu jubuni.
Kama maua waridi,
Harufuye maridadi,
Tutamani ikarudi
Iendapo ghaibuni.
Twaona mithili riha,
Harufu iso karaha,
Katu huwezi kuhaha,
Ikufikapo moyoni.
Furaha ya uzeeni,
Tajiona utotoni,
Ukumbuke ujanani,
Ubakie kushaini.
Furaha inahuisha,
Kicho kufa hufufusha,
Maisha kuyarefusha,
Ifananishwe na nini?
Kila mja duniani,
Furaha huitamani,
Hutafuta masokoni,
Ikae mwao fukoni.
Husakwa madarasani,
Kwa kisomo vitabuni,
Maandiko kurasani,
Furaha kuipateni.
Mafyatu majalalani,
Ni watupu maungoni,
Kucha huchakura chini,
Furaha kuishikeni.
Hutafutwa migodini,
Waja huzama shimoni,
Huko huwa hatarini,
Na kujiweka kufani.
Pia huko mashambani,
Mkulima na mpini,
Kusiha na mavunoni,
Furaha maandamoni.
Hata na mama ntilie,
Chakula ajipikie,
Walaji awauzie,
Furaha iwe fukoni.
Machinga barabarani,
Kutwa hushinda juani,
Na bidhaa mikononi,
Furaha kuiauni.
Cherehani yu kitini,
Habanduki mashononi,
Anachowaza moyoni,
Furaha iwe kichwani.
Waashi nao sawia,
Hujenga na kubomoa,
Huku wakitia nia,
Watulie furahani.
Wahunzi vyuma hufua,
Bidhaa kujiundia,
Haja yao hutambua,
Furaha mwao nyumbani.
Mangi naye yu gengeni,
Haondoki mauzoni,
Hung’ang’ana dirishani,
Furaha kuitamani.
Na wagonjwa vitandani,
Ijapo huwa tabani,
Wanamuomba Manani,
Wabakie furahani.
Waumini kanisani,
Na kule misikitini,
Magoti altareni,
Mola raha kuwapeni.
Waandishi kama mimi,
Nasi japo hatuvumi,
Lakini tunajihami,
Tusitoke furahani.
Mapadiri, mashemasi,
Askofu, makasisi,
Furaha wakaihisi,
Haja yao fuadini.
Wafanyakazi nyumbani,
Kutwa apo shughulini,
Halali kibaruani,
Lengo awe furahani.
Walinzi huliwa mbu,
Ila yao kumbukumbu,
Wakiyafanya malumbu,
Furaha iwe nguoni.
Rais naye kitini,
Kutwa huomba Manani,
Furaha iwe nchini,
Pia na mwake moyoni.
Makatibu na wabunge,
Na hao wasijitenge,
Bila raha wasiringe,
Japo washinda bungeni.
Furaha twaitafuta,
Ni tunu hii kupata,
Kiu zetu kuzikata,
Tuondoke matatani.
Pasi furaha sumbuko,
Tusombwe na nung’uniko,
Tubadili miondoko,
Twende kwa mwendo wa nyani.
Pasi furaha kilio,
Hakuna tena pumuo,
Na maisha huwa sio,
Kwetu huwa msibani.
Furaha rafiki shibe,
Tule matumbo tuzibe,
Kingine tukakibebe,
Twende kula majiani.
Tena nduguye sherehe,
Tuimbe tusherekehe,
Zile nyimbo za kihehe,
Kadhalika za wangoni.
Swahiba wake mapenzi,
Waja mapenzi twaenzi,
Kama kidonda na nzi,
Abakivyo furahani.
Tena jiraniye pesa,
Paso pesa anasusa,
Pesa huja kutakasa,
Palipo jaa huzuni.
Amani ni wake mbasi,
Bila amani kuhisi,
Furaha huwa tatasi,
Ikimbiavyo vitani.
Huketi pamwe malazi,
Si kulala kwenye zizi,
Furaha kamwe kuhozi,
Hapati hiyo zizini.
Pia huketi na vazi,
Ikiwa hatupendezi,
na mwili husitirizi,
twaondokewa jubuni.
Na tuwe na marafiki,
Wema sio wazandiki,
Furaha haiondoki,
Daima huwa moyoni.
Pasipo na maonevu,
Na kuitwa mpumbavu,
Hata ukiwa shupavu,
Hufurahi dharauni.
Haitadumu furaha,
Popote penye karaha,
Tajionea udhiha,
Tahamia kwa jirani.
Furaha penye shutumu,
Hapo huwa marehemu,
Ama penye madhulumu,
Na hapo huwa tabani.
Furaha hudhoofika,
Pa vijembe na dhihaka,
Njaa na kuhangaika,
Raha wenda ghaibuni.
Tuondokewapo ndugu,
Hapo huota magugu,
Mioyo huzuka sugu,
Furaha huwa kandoni.
Furaha kwa tegemezi,
Kuwa nayo huiwezi,
Upewe kwa simangizi,
Utapata raha gani?
Furaha na matatizo,
Hawamalizi mizozo,
Hutofauti mawazo,
Hawa kamwe wapatani
Furaha na tafrani,
Mithili moto na kuni,
Furaha huwa kinywani,
Humezwa na tafrani.
Furaha penye mabavu,
Ja samaki nchi kavu,
Kadhalika na pa wivu,
Haiwi pumzikoni.
Fura ni kitu bora,
Kizidicho njema sura,
Hupendwa kila idara,
Kila rika kila dini.
Furaha kila kiumbe,
Mola wake amuombe,
Hawezi huyu atambe,
Sipo kuwa furahani.
Furaha zama na zama,
Ndo kilicho kitu chema,
Ndanimwe ikikuhama,
Bora wende kaburini.
Kukikosa kitu hiki,
Mwenyewe tajidhihaki,
Ujione hujitaki,
Vile hauna thamani.
Penye chuki na madhila,
Furaha hapo pahala,
Kamwe hawezi kulala,
Ijapopita njiani.
Na pale penye izara,
Na maudhi ya kukera,
Hata kwa mja sogora,
Raha huwa hatarini.
Furaha kwa masikini,
Hata atie makini,
Na hapo nikabaini,
Furaha huwa kufani.
Kadhalika penye gubu,
Furaha hupata tabu,
Kuishi haijaribu,
Huishia maozoni.
Penye ghiliba na wizi,
Uchawi na uchochezi,
Pa maudhi na machozi,
Furaha yenda zikoni.
Furaha pasi uzazi,
Uzae Juma na Rozi,
Kuzaa kuwe tatizi,
Furaha hauioni.
Furaha mali ghalani,
Sio kuwa utumwani,
Waja wakuone nyani,
Furaha hapo shakani.
Furaha penye kushindwa,
Na moyowe ukadundwa,
Hofu woga ukapandwa,
Utaambua huzuni.
Furaha mali ya Mungu,
Pasi yeye ni uchungu,
Hata uwe kwa mzungu,
Sifanye ya ushetani.
Shetani yeye balozi,
Anayeunda machozi,
Dhiki na maangamizi,
Kaviweka duniani.
Taifa bila furufu,
Hulega kama mkufu,
Hilo taifa dhaifu,
Hata liwe uzunguni.
Dunia bila jubuni,
Tungekuwa kama mbuni,
au kwale wa nyikani,
tubakie mawindoni.
Koo bila kitu hiki,
Kamwe wasingeshiriki,
Vikao kuvimiliki,
Wabaki matenganoni.
Familia nayo pia,
Bila raha ni mdhia,
Waja wangeomba njia,
Ukimbizi majiani.
Darasa bila furaha,
Wanafunzi tungehaha,
Kufunzwa kwetu fadhaha,
Tenge pata raha gani.
Watoto bila jubuni,
Nini wangekithamini?
Kuishi pao nyumbani,
Kamwe wasingetamani.
Furaha hushika dira,
Tunapotaka kugura,
Tukikosa twazurura,
Hakwendeki mahalani.
Na wapishi majikoni,
Wao huchochea kuni,
Chakula kupakuani,
Chenye furaha yakini.
Lolote lenye mwenendo,
Kadhalika na matendo,
Yaliyo yetu mapendo,
Litufurahi moyoni.
Wengine hutaka ndoa,
Na wengine hukia,
Hao walitambua,
I wapi raha yakini.
Mtunzi Filieda Sanga
Mabibo Dsm
0753738704
|
|
|
UTENZI: NAKUPENDA |
Posted by: MwlMaeda - 08-13-2021, 05:52 AM - Forum: Ushairi
- No Replies
|
|
NAKUPENDA
Ewe pepo za bahari nibarizi,
Umenipa yako shwari, sinihizi,
Mapenzi yako fahari, mtulizi,
Moyo umekufiri,muokozi,
Nakupenda!
Ewe wangu nyota njema, asubuhi,
Umenipa kutazama, nifurahi,
Alfajiri na mapema na sikahi,
Kusinzia nimegoma na walahi,
Nakupenda!
Ewe wangu njiwa dume, niimbie,
Uniondoke ukame, unijie,
Utokako nitazame, nitulie,
Sadirini nikaseme, nifurahie,
Nakupenda!
Tabibu wa moyo na mwili huu,
Yashushe mapigo yasende juu,
Unipe mapenzi yale makuu,
Yasiwake na kuzima,Ile vuu,
Nakupenda!
Ewe jua la machweo niangaze,
Na upepo wa jioni nipulize,
Taratibu masikio, nong'oneze,
Kwa tamu yako sauti, niambilize,
Nakupenda!
Mafuriko ya mahaba niogolee,
Unipe basi kushiba yaninogee,
Tamaa yangu kuziba usipotee,
Hapo nitakuwa zoba, nikapotee,
Nakupenda!
Ewe usiku mtulivu, unilaze,
Macho yangu matulivu, yafumbilize,
Niwe wako msikivu, nibembeleze,
Niondolee makovu, nipendekeze,
Nakupenda!
Mtunzi Filieda Sanga
Mabibo Dsm
0753738704
|
|
|
SHAIRI: MAHABA YAKICHACHA |
Posted by: MwlMaeda - 08-13-2021, 05:51 AM - Forum: Ushairi
- No Replies
|
|
*Mahaba yakichacha*
Kama sikio la kufa,
Lisivyosikia dawa,
Nayo Mahaba yakifa,
Mambo yote huuawa,
Hata uyatwike sifa,
Muhali kufufuliwa,
Mahaba yakishachacha, ndimu haiyachachui.
Yakizikwa yamezikwa,
Kaburile hufukui,
Hata kama yangepikwa,
Kwa mafuta kwa karai,
Ni kama mtu kutekwa,
Kafishwa si kuzirai,
Mahaba yakishachacha, ndimu haiyachachui.
Kutwa nilibembeleza,
Machozi nikamwagia,
Nikambiwa yameoza,
Tabu bure najitia,
Maneno sikuyasaza,
Kitu sikuambulia,
Mahaba yakishachacha, ndimu haiyachachui.
Nalia sina bahati,
Kwa penzi mimi yatima,
Nipo kwenye hatihati,
Mapenzi yamenihama,
Nipo kwenye kavu kuti,
Moyo waenda mrama,
Mahaba yakishachacha, ndimu haiyachachui.
Ninahitaji kiota,
Ndege nipate kutua,
Nikilala ninaota,
Ndoto za kunisumbua,
Niwezesheni kupata,
Stara nipate tua.
Mahaba yakishachacha, ndimu haiyachachui.
*Shaaban Mwinyikayoka*
(Mwanaupwa)
Iringa
0715439740
|
|
|
SHAIRI: NIMEONJA LADHA YAKE |
Posted by: MwlMaeda - 08-12-2021, 06:27 PM - Forum: Ushairi
- No Replies
|
|
NIMEONJA LADHA YAKE
Mfano wake halua, kabichi na bilingani,
Hapana nimekosea, niseme ja kitu gani?
Vile mmeniambia, nifananishe na nini?
Amezidi nizuzua, maana namwita honey.
Yule bwana anajua, kunipa nyama laini,
Anipavyo kwa hatua, basi mie taabani,
Ai nimemzimia, kunishika niacheni,
Amezidi nizuzua, maana namwita honey.
Sio kujiropokea, nipeni heko jamani,
Siku hizi nasinzia, hali mwepesi mwilini,
Kama katoka Asia, penzi lake la fasheni,
Amezidi nizuzua, maana namwita honey.
Nyie mnojisifia, makelele mtaani,
Mnajipiga vifua, wachovu nimebani,
Amewazidi hatua, huyu kijana jamani,
Amezidi nizuzua, maana namwita honey.
Na huyu kumfikia, Kuna kazi tambueni,
Ni bado kumfikia, nendeni bara na pwani,
Mana nawasimulia, Kuna wajuzi jamani,
Amezidi nizuzua, maana namwita honey.
Ukimwona amepoa, yake kazi kitandani,
Kweli watu wanajua, na leo nimeamini,
Mtunzi namsifia, Wala haya si matani,
Amezidi nizuzua, Mana namwita honey.
Leo ninamuimbia, ameniweza fanani,
Ai ninawaambia, wake utamu acheni,
Kama wali kwa bamia, sijui niseme nini?
Amezidi nizuzua, maana namwita honey.
Mumeshikwa na tamaa, yenu macho yaoneni,
Mnaanza kulegea, hebu nenda kalaleni,
Nataka kumpigia, niongee na mwendani,
Amezidi nizuzua, maana namwita honey.
Mtunzi Filieda Sanga
Mama B
Mabibo Dsm
0753738704
|
|
|
SHAIRI: YA KESHO YA MCHIMBAKA |
Posted by: MwlMaeda - 08-11-2021, 10:41 PM - Forum: Ushairi
- No Replies
|
|
YA KESHO YA MCHIMBAKA
Naanza kwa Subuhana, aliye wangu Jalali,
Nongoze nipange vina, vya mwisho na vya awali,
Bila wewe mi tumbili,
Tumbili wao hawana, kijiko wala ugali,
Yao kazi kubebana, wende misitu ya mbali,
Ya kesho ya mchimbaka, mimi natunga kabisa.
Wangapi tunawaona, wanayo macho mawili,
Tuamkapo hawana, hubaki viwiliwili,
Huzidiwa na tumbili,
Tumbili yeye huona, vivyo karibu na mbali,
Na wao hupapasana, japo kuwa kandambili,
Ya kesho ya mchimbaka, mimi natunga kabisa.
Mola ajua Lijana, lini huko nawasili,
Kifo hakina azana, tena huoni dalili,
Sio mithili ya meli,
Meli moshi tukaona, tukaanza kushakili,
Tuanze kukimbizana, kuinusuru miili,
Ya kesho ya mchimbaka, mimi natunga kabisa.
Mifuko imenituna, kuishi kwangu sahali,
Kesho nanza kujikuna, nifikwapo udhalili,
Nisile uji na wali,
wali sio kwamba kana, sivitaki vitu bali,
Ila ndo chochote sina, imekatika salali,
Ya kesho ya mchimbaka, mimi natunga kabisa.
Ja watoto wa watwana, waishio bora hali,
Wasojua kubanana, pa kunguni hawalali,
Kesho wazazi ajali,
Ajali huvunjikana, kifo kwao huwasili,
Watoto raha hawana, hakuna mwenye kujali,
Ya kesho ya mchimbaka, mimi natunga kabisa.
Japo leo pesa sina, kutunga sina zohali,
Sipuuzi vyangu vina, nayatunga bulibuli,
Anayejua Jalali,
Jalali kaumba jana, leo na hata azali,
Lailati na mchana, sipumzishi akili,
Ya kesho ya mchimbaka, mimi natunga kabisa.
Wangapi wenye majina, wakwasi na majalili,
Walijigeuza nduna, wawe hawana akili,
Zilipukutika mali,
Malizo sasa hawana, hivi wana mbaya hali,
Wadhoofu wa kunona, wamekondeana mwili,
Ya kesho ya mchimbaka, mimi natunga kabisa.
Kwa nini natunga sana, mwaniuliza maswali,
Dahari ya Maulana, kwaye ninatawakali,
Amependa Subuhana,
Subuhana akinena, lolote jambo hajali,
Ni nani atapingana, na roho asiye mwili,
Ya kesho ya mchimbaka, mimi natunga kabisa.
Kaditamati amina, nakushukuru Jalali,
Haki umenipa vina, nivyokuomba awali,
Mithili nafunga goli,
Goli wanavyofungana, wanayanga na lipuli,
Wengine waseme mbona, hatukuona dalili,
Ya kesho ya mchimbaka, mimi natunga kabisa.
Mtunzi Filieda Sanga
Mama B
Mabibo Dsm
0753738704
|
|
|
|