MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

SHAIRI: YA KESHO YA MCHIMBAKA

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
SHAIRI: YA KESHO YA MCHIMBAKA
#1
YA KESHO YA MCHIMBAKA
Naanza kwa Subuhana, aliye wangu Jalali,
Nongoze nipange vina, vya mwisho na vya awali,
              Bila wewe mi tumbili,
Tumbili wao hawana, kijiko wala ugali,
Yao kazi kubebana, wende misitu ya mbali,
Ya kesho ya mchimbaka, mimi natunga kabisa.

Wangapi tunawaona, wanayo macho mawili,
Tuamkapo hawana, hubaki viwiliwili,
                Huzidiwa na tumbili,
Tumbili yeye huona, vivyo karibu na mbali,
Na wao hupapasana, japo kuwa kandambili,
Ya kesho ya mchimbaka, mimi natunga kabisa.

Mola ajua Lijana, lini huko nawasili,
Kifo hakina azana, tena huoni dalili,
                Sio mithili ya meli,
Meli moshi tukaona, tukaanza kushakili,
Tuanze kukimbizana, kuinusuru miili,
Ya kesho ya mchimbaka, mimi natunga kabisa.

Mifuko imenituna, kuishi kwangu sahali,
Kesho nanza kujikuna, nifikwapo udhalili,
                Nisile uji na wali,
wali sio kwamba kana, sivitaki vitu bali,
Ila ndo chochote sina, imekatika salali,
Ya kesho ya mchimbaka, mimi natunga kabisa.

Ja watoto wa watwana, waishio bora hali,
Wasojua kubanana, pa kunguni hawalali,
                Kesho wazazi ajali,
Ajali huvunjikana, kifo kwao huwasili,
Watoto raha hawana, hakuna mwenye kujali,
Ya kesho ya mchimbaka, mimi natunga kabisa.

Japo leo pesa sina, kutunga sina zohali,
Sipuuzi vyangu vina, nayatunga bulibuli,
              Anayejua Jalali,
Jalali kaumba jana, leo na hata azali,
Lailati na mchana, sipumzishi akili,
Ya kesho ya mchimbaka, mimi natunga kabisa.

Wangapi wenye majina, wakwasi na majalili,
Walijigeuza nduna, wawe hawana akili,
                Zilipukutika mali,
Malizo sasa hawana, hivi wana mbaya hali,
Wadhoofu wa kunona, wamekondeana mwili,
Ya kesho ya mchimbaka, mimi natunga kabisa.

Kwa nini natunga sana, mwaniuliza maswali,
Dahari ya Maulana, kwaye ninatawakali,
              Amependa Subuhana,
Subuhana akinena, lolote jambo hajali,
Ni nani atapingana, na roho asiye mwili,
Ya kesho ya mchimbaka, mimi natunga kabisa.

Kaditamati amina, nakushukuru Jalali,
Haki umenipa vina, nivyokuomba awali,
Mithili nafunga goli,
Goli wanavyofungana, wanayanga na lipuli,
Wengine waseme mbona, hatukuona dalili,
Ya kesho ya mchimbaka, mimi natunga kabisa.

Mtunzi Filieda Sanga
Mama B
Mabibo Dsm
0753738704
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)