Welcome, Guest
You have to register before you can post on our site.

Username
  

Password
  

Search Forums

(Advanced Search)

Forum Statistics
» Members: 381
» Latest member: ayuxofefaoy
» Forum threads: 1,942
» Forum posts: 2,003

Full Statistics

Online Users
There are currently 57 online users.
» 0 Member(s) | 56 Guest(s)
Bing

Latest Threads
ETIMOLOJIA YA NENO 'AHERA...
Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili
Last Post: MwlMaeda
54 minutes ago
» Replies: 0
» Views: 2
ETIMOLOJIA YA NENO 'AHSAN...
Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili
Last Post: MwlMaeda
Yesterday, 02:16 PM
» Replies: 0
» Views: 6
SHAIRI: HISIA ZANGU
Forum: Ushairi
Last Post: John John
01-15-2022, 08:51 PM
» Replies: 1
» Views: 25
ETIMOLOJIA YA NENO 'AHADI...
Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili
Last Post: MwlMaeda
01-14-2022, 09:08 AM
» Replies: 0
» Views: 23
MUUNDO WA VITENZI, VIVUMI...
Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha
Last Post: MwlMaeda
01-14-2022, 07:56 AM
» Replies: 0
» Views: 22
KIMYA CHENYE KELELE NYING...
Forum: Hadithi
Last Post: MwlMaeda
01-13-2022, 01:25 PM
» Replies: 0
» Views: 22
SHAIRI: MFAUME
Forum: Ushairi
Last Post: MwlMaeda
01-12-2022, 09:13 PM
» Replies: 0
» Views: 28
SHAIRI: SIJAFAHAMU
Forum: Ushairi
Last Post: MwlMaeda
01-11-2022, 04:50 PM
» Replies: 0
» Views: 43
DUNIA KOKWA YA FURU: AMAL...
Forum: Fasihi kwa ujumla
Last Post: MwlMaeda
01-11-2022, 04:08 PM
» Replies: 0
» Views: 44
TUZO YA KISWAHILI: USHAIR...
Forum: Ushairi
Last Post: MwlMaeda
01-11-2022, 03:39 PM
» Replies: 0
» Views: 37

 
  ETIMOLOJIA YA NENO 'AHERA/AKHERA'
Posted by: MwlMaeda - 54 minutes ago - Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili - No Replies

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AHERA/AKHERA'

Neno *ahera/akhera* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: i-/-zi*] yenye maana ya:

1. Mahali panapoaminiwa kuwa ndiko roho za wafu zinakoenda.

2. Maskani ya roho za wanadamu baada ya mauti/kifo.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *ahera/akhera*( *soma: aakhiratun/aakhiratan/,aakhiratin آخرة )* ni nomino ya Kiarabu yenye maana zifuatazo:

1. Kinyume cha Dunia. Kuna aya katika Qur'aan Tukufu isemayo: "Miongoni mwenu wapo wanaoitaka Dunia, na miongoni mwenu wapo wanaoitaka Akhera." (Qur'aan Tukufu, Sura ya 3 (Surat Aali Imraan, Aya ya 152).

2. Kinyume cha mwanzoni; mwishoni.

3. Maskani ya roho za wanadamu baada ya kifo.

Kinachodhihiri ni kuwa neno hili *aakhira* lilipoingia katika  Kiswahili na kutoholewa limezoeleka kutamkwa *ahera* na *akhera* likibeba maana moja ya maskani ya roho za wanadamu baada ya kifo.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*

Print this item

  ETIMOLOJIA YA NENO 'AHSANTE'
Posted by: MwlMaeda - Yesterday, 02:16 PM - Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili - No Replies

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AHSANTE'

Neno ahsante katika lugha ya Kiswahili ni kihisishi: tamko analotoa mtu wakati wa kushukuru.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili ahsante( soma: ahsanta/ahsanti/ahsantumaa/ahsantum/ahsantunna ) احسنت/احسنتما/احسنتم/احسنتن) ni kitenzi cha Kiarabu chenye maana ya kufanya vizuri.
Ahsanta = Wewe mwanamume umefanya vizuri.
Ahsanti = Wewe mwanamke umefanya vizuri.
Ahsantumaa = Nyinyi wawili mmefanya vizuri.
Ahsantum = Nyinyi wanaume wengi mmefanya vizuri.
Ahsantunna = Nyinyi wanawake wengi mmefanya vizuri.

Neno hili, kwa wazungumzaji wa pwani, wamezoea kulichukua kama lilivyo katika Kiarabu kwa  mwanamume mmoja kumwambia ahsanta , mwanamke mmoja kumwambia ahsanti , watu wawili kuwaambia ahsantumaa , wanaume wengi kuwaambia ahsantum , na wanawake wengi kuwaambia ahsantunna.

Kinachodhihiri ni kuwa neno hili ahsante ambalo hutumika bila ya kuzingatia jinsia, ambalo kwa watu wengi huwa ahsanteni, halikutumika sana kwa Waswahili wa pwani ambao walizowea kulitumia kama linavyotumika katika lugha ya Kiarabu. 

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.

Print this item

  SHAIRI: HISIA ZANGU
Posted by: MwlMaeda - 01-14-2022, 10:28 AM - Forum: Ushairi - Replies (1)

HISIA ZANGU
Nilijaribu kuficha, niwe Kama simpendi,
Moyo unanichokocha, kumpata yule fundi,
Naona huku kuficha, kunanifanya siwandi,
Natangaza nampenda,  mpeni habari hizi.

Hisia zanifumuka, moyoni kunikeketa,
Ni yule ninamtaka, mwambe aache matata,
Ninamtaka haraka, tafurahi kumpata,
Natangaza nampenda, mpeni habari hizi.

Ninaomba samahani, kiwa nimevunja mwiko,
Kwa wetu utamaduni, niendako mie siko,
Sema nampenda Nani, inazua chokochoko,
Natangaza nampenda, mpeni habari hizi.

Mkisema naigiza, eti tulivyo malenga,
Bure mtanipoteza, mniue mie Sanga,
Leo ninamtangaza, nimepagawa mkinga,
Natangaza nampenda, mpeni habari hizi.

Kwanza nimependa ndevu, sharubu nazo sharafa,
Na macho yake makavu, yaniletea maafa,
Mwambieni Nina wivu, kumkosa nitakufa,
Natangaza nampenda, mpeni habari hizi.

Si mweusi si mweupe, bwana yupo katikati,
Kijana Hana mapepe, Wala Hana hatihati,
Mwambieni hata lepe, siku hizi silipati,
Natangaza nampenda, mpeni habari hizi.

Ni mrefu wa kadiri, si mnene si mwembamba,
Kumpata ni fahari, mtaani nitatamba,
Nimemuomba Kahari, ake kwangu huyu mwamba,
Natangaza nampenda, mpeni habari hizi.

Siendelezi kutunga, nimeanza kumuwaza,
Machozi yananilenga, namlilia Hamza,
Amini akinitenga, binti mtanipoteza,
Natangaza nampenda, mpeni habari hizi.

Mtunzi Filieda Sanga
Mama b
Mabibo Dsm
0753738704

Print this item

  ETIMOLOJIA YA NENO 'AHADI'
Posted by: MwlMaeda - 01-14-2022, 09:08 AM - Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili - No Replies

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AHADI'

Neno ahadi katika lugha ya Kiswahili lina maana zifuatazo:

1. Nomino: [Ngeli: i-/-zi] mwisho wa uhai wa kiumbe aghalabu mwanadamu; mauti.

2 - Nomino: [Ngeli: i-/-zi] makubaliano yaliyofikiwa baina ya pande mbili au zaidi.

3 - Nomino: [Ngeli: i-/-zi] hakikisho la utekelezaji wa jambo ambalo mtu au watu hujipa jukumu la kutimiza.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili ahadi( soma: ahdun/ahdan/ahdin عهد ) ni nomino ya Kiarabu yenye maana zifuatazo:

1. Ahadi : tendo-jina kutokana na kitenzi cha Kiarabu ahida عهد ameahidi.

2. Utekelezaji wa jambo fulani.

3. Dhamana.

4. Amani.

5. Mapenzi.

6. Dhima.

7. Azimio; makubaliano.

8. Wasia/wosia, usia.

9. Kiapo.

10. Andiko la uhawilishaji wa madaraka.

11. Zama/wakati, ahdush shabaabi عهد الشباب wakati wa ujana.

12. Mrithi wa ufalme, ikitanguliwa na neno waliyuu, waliyyul Ahdi ولي العهد.

13 -  Agano la Kale, likiambatana na neno Al-Qadiim, Al-Ahdul Qadiim العهد القديم، maandiko matakatifu kabla ya ujio wa Masihi Issa Mwana wa Maryam (Yesu Kristo).

14 -  Agano la Jipya, likiambatana na neno Al-Jadiid, Al-Ahdul Jadiid العهد الجديد، maandiko matakatifu yanayohusu wakati wa Masihi Issa Mwana wa Maryam (Yesu).

Kinachodhihiri ni kuwa neno hili ahadi ( soma: ahdun/ahdan/ahdin عهد ) lilipoingia katika  Kiswahili lilichukua baadhi ya maana zake katika lugha ya asili- Kiarabu na kuacha maana zingine.

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.

Print this item

  MUUNDO WA VITENZI, VIVUMISHI, VIBAINISHI, NUMERALI/NAMBA NA VIELEZI KATIKA KISWAHILI
Posted by: MwlMaeda - 01-14-2022, 07:56 AM - Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha - No Replies


.pdf   MUUNDO_WA_VITENZI_VIVUMISHI_VIBAINISHI_N.pdf (Size: 119.98 KB / Downloads: 0)

Print this item

  KIMYA CHENYE KELELE NYINGI
Posted by: MwlMaeda - 01-13-2022, 01:25 PM - Forum: Hadithi - No Replies

KIMYA CHENYE KELELE NYINGI
Akulumbale huwa hapendi kupuuzwa hata kidogo, kwa sababu hiyo,  alikata shauri la kurudi huko pasipojulikana .  Kwa hakika, kusikojulikana ndiko pahala waishipo watu wasiojulikana pia. Watu hao aghalabu huwa hawana sio tu anwani za makazi  lakini pia hata  majina yao hayatambuliki kiwepesi.
Hata hivyo,  pamoja na yote hayo, huko kusikojulikana ni tofauti kabisa na kule kimya, ambako huenda watu walioharibikiwa mambo yao.
Utasikia,  hivi bwana fulani siku hizi yuko wapi?  Iwapo bwana fulani mwenyewe anayezungumziwa  atakuwa ameharibikiwa na mambo yake, majibu huwa, '  bwana yule, yupo kimya ' ikisemwa hivyo mara nyingi huwa inaeleweka kuwa,  ingawa mambo ya huyo bwana fulani yapo msegemnege lakini uhakika uliyopo  ni kwamba, walau  huko aliko yuko hai.
Hii ni kinyume kabisa na kule kusikojulikana. Huko ikiachiliwa mbali kutojulikana kwake na kwenda bila utayari wala hiyari hakuna kikingine kinachojulikana na wengi.
Ni muhimu kufahamu kuwa,  si kila mtu aliyeharibikiwa ama kuharibiwa mambo yake huchagua kwenda huko kimya.  Kuchagua kuishi huko hutegemea ubora wa ama busara na hekima au silka na hulka zilizomkuza mtu mwenyewe.
Jambo muhimu kuliko yote katika muktadha huu,  ni kule kuweza kung'amua nyakati za mapito ya kimaisha ya mwanadamu. 
Hivyo, ni muhimu kabisa kujua, ni wakati gani  mtu aende huko kimya na muda gani achague kwenda pasipojulikana kama itaonekana inafaa.
Akichagua kwenda kimya huenda akavikwa nguo upya siku za usoni. Hata hivyo,  uamuzi wowote baina ya hiyari hizi mbili ni mgumu.  Ingawa ni bora katika mazingira fulani kupoteza pua ili kuulinda wajihi. Kwani! Kama hapana budi lisilobudi hufanywa! Uamuzi wa mithili hii ndiyo hasa huitwa uamuzi wa kukata jongoo kwa meno.  Wakati fulani kimya ni kelele lakini si kila kiza ni shari.
Si budi kuzipima vizuri nyakati ili ifanyike itihari sahihi ya mtindo wa maisha kwa kuzingatia mazingira ya wakati unaohusika. Hata kiza si shari tupu na si kila kilichopinda ni kibaya.
soma_useme
********
A. A. Majid Mswahili
Chang'ombe,  Kisarawe_ Pwani
Usipitwe na Hadithi Fupi kwa Ufupi za Majid Mswahili,  kuanzia Februari Mosi, 2022, In Shaa Allah.
Anuanipepe: majidkiswahili@gmail.com

Print this item

  SHAIRI: MFAUME
Posted by: MwlMaeda - 01-12-2022, 09:13 PM - Forum: Ushairi - No Replies

MFAUME
vya kale ndio dhahabu, hebu kuwa mchunguzi,
Imekushuka ghadhabu, kakupiku kwa ujuzi,
Langu donda hunitibu, kwa sirinja na mizizi,
Chambo yako sikuila, na babu yako ninae.

Kijana uache gumu, huiwezi hii kazi,
Wawezaje kunitibu, unashindia viazi?
Mwishowe unipe tabu, iwe kazi huiwezi,
Chambo yako sikuila, na babu yako ninae.

Shairi ninakujibu, Mfaume nenda kozi,
Siku ulipojaribu, nikabaini huwezi,
Nenda kashike Kitabu, walimu wakupe kwizi,
Chambo yako sikuila, na babu yako ninae.

Nikwambe yalo nisibu, kuwa na huyu lazizi,
Naamini utatubu, akusamehe Mwenyezi,
Anajua huyu babu, Kama katoka Shirazi,
Chambo yako sikuila, na babu yako ninae.

Tena ushike adabu, mepata wapi makuzi?
Babu ana maajabu, mweledi wa upembuzi,
Jambo unalojaribu, taambua kikohozi,
Chambo yako sikuila, na babu yako ninae.

Ukimuona shaibu, kwa penzi hana ajizi,
Wewe tastaajabu, mfano sikuelezi,
Mapenzi ni mahesabu, uyajue matatuzi,
Chambo yako sikuila, na babu yako ninae.

Kijana unaharibu, na ujue sikuwazi,
Unajitia aibu, hali huna utatuzi,
Hauishiwi sababu, mithili yake mbaazi,
Chambo yako sikuila, na babu yako ninae.

Shairi ulipojibu, nilibaki bumbuwazi,
Unamtania babu, kwenye kilo hakujazi,
Yatakupata majibu, na mie simkatazi,
Chambo yako sikuila, na babu yako ninae.

Ninafunua Kitabu, zangu beti sikatizi,
Nikushikishe adabu, uache wako utozi,
Ona unapata tabu, ulivyoishiwa pozi,
Chambo yako sikuila, na babu yako ninae.

Mitindo ya Kiarabu, babu anipayo dozi,
Wala sisumbui nibu, niitwe muongopezi,
Mashine yake ajabu! Ni muhogo si kiazi,
Chambo yako sikuila, na babu yako ninae.

Na muda unanisibu, nende kwa babu mlezi,
Sasa naifunga nibu, ukweli mekupa wazi,
Umeyapata majibu, hoja na ufafanuzi,
Chambo yako sikuila, na babu yako ninae.

Mtunzi Filieda Sanga
Mama B
Mabibo Dsm
0753738704

Print this item

  SHAIRI: SIJAFAHAMU
Posted by: MwlMaeda - 01-11-2022, 04:50 PM - Forum: Ushairi - No Replies

SIJAFAHAMU
Maamuzi na hukumu, kipawa cha subuhana.
Namshukuru Karimu, kwa kunifadhili sana:
Mambo ni zamu kwa zamu, apendapo maulana,
Uzuri wake naona, ujane sijafahamu.

Pumu maradhi ya Mola, anipapo sitakana,
Kama anipavyo kula, na kuwaza na kunena:
Alipendalo si ila, kwa mtu kutendekana,
Uzuri wake naona, ujane sijafahamu.
Omba dua la maradhi, nipate kila namna,
Ikiwa Mungu haridhi, kazi bure hutavuna,
Pabakie kujiudhi, wala pato jema huna,
Uzuri wake naona, ujane sijafahamu.
©Shaaban bin Robert

Print this item

  DUNIA KOKWA YA FURU: AMALI YA MISEMO YA KIPEMBA
Posted by: MwlMaeda - 01-11-2022, 04:08 PM - Forum: Fasihi kwa ujumla - No Replies


.pdf   DUNIA KOKWA YA FURU AMALI YA MISEMO YA KIPEMBA.pdf (Size: 241.09 KB / Downloads: 1)

Print this item

  TUZO YA KISWAHILI: USHAIRI
Posted by: MwlMaeda - 01-11-2022, 03:39 PM - Forum: Ushairi - No Replies

Print this item