MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

SHAIRI: NI HERI NINGEKUROGA

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
SHAIRI: NI HERI NINGEKUROGA
#1
NI HERI NINGEKUROGA
Mara ngapi nakuonya, uwe wangu peke yangu,
Haya uliyoyafanya, yamenitia uchungu,
Vile nilivyokuonya, ni bure maneno yangu,
Kwa haya uliyofanya, ni heri ningekuroga.

Sikuthubutu limbwata, moyo wako kuushika,
Niliepuka matata, usije ukawehuka,
Leo haya kunipata, na mimi nimegutuka,
Kwa haya uliyofanya, ni heri ningekuroga.

Mara kadha niliwaza, nende kwa Kalumanzila,
Mawazo nikapuuza, chanzo cha haya madhila,
Sasa kimetua kiza, siwezi tena kulala,
Kwa haya uliyofanya, ni heri ningekuroga.

Sasa mbali umekwenda, kurudi umekaidi,
Ili unitoe chonda, utimize makusudi,
Nimebakia kukonda, pamwe na zangu juhudi,
Kwa haya uliyofanya, ni heri ningekuroga.

Yako simu ninapiga, haupokei mwendani,
Nimebaki kichwa boga, sijui nifanye nini,
Au chupa ningesaga, nitoweke duniani,
Kwa haya uliyofanya, ni heri ningekuroga.

Nakumbuka ile juzi, na ulivyonitukana,
Umezidi siku hizi, tena mapenzi hakuna,
Nalia sitokwi chozi, ninabaki kujikuna,
Kwa haya uliyofanya, ni heri ningekuroga.

Beti chache nasimama, sili ugali kushiba,
Unionee huruma, uchungu unanikaba,
Kwa raha imegoma, zimepita siku saba,
Kwa haya uliyofanya, ni heri ningekuroga.

Mtunzi Filieda Sanga Mama B
Mabibo Dsm
0753738704
Mwl Maeda
Reply
#2
Kunywa maji yatulie,tumlani ibilisi
Mie sipendi ulie,ichomwe yako nafusi
Filieda nisikie,penzi letu sijepesi
Umeniroga kitambo,si mizizi ni mahaba

Hakufiki Balkisi,mrembo wazama zile
Wote nawaona ngisi,sitamani nende kule
Ukutoke wasiwasi,wadharau misukule
Umeniroga kitambo,si mizizi ni mahaba

Sikuisikia simu,ulipopiga mwandani
Usikupate wazimu,nilikuwepo bafuni
Usifanye ninywe sumu,roho niweke rehani
Umeniroga kitambo,si mizizi ni mahaba

Upesi ninarejea,ziara ninakatisha
Naja hima kukulea,maneno yamenitisha
Moyo wangu waelea,imenihama bashasha
Umeniroga kitambo,si mizizi ni mahaba

Abdul Ndembo
Mburahati Sekondari
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)