![]() |
MULIKA : MAELEKEZO KWA WAANDISHI WA MAKALA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Uandishi/Utungaji (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=12) +--- Thread: MULIKA : MAELEKEZO KWA WAANDISHI WA MAKALA (/showthread.php?tid=831) |
MULIKA : MAELEKEZO KWA WAANDISHI WA MAKALA - MwlMaeda - 08-13-2021 MULIKA ni jarida la taaluma ya Lugha na Fasihii ya Kiswahili. Jukumu lake kuu ni kukusanya na kusambaza maarifa yanayohusu Lugha na Fasihi ya Kiswahili yaliyokitwa katika utafiti mpevu. MULIKA limeendelea kuwa daraja kati ya watumiaji wa Kiswahili popote walipo, na wataalamu wa Kiswahili katika Sekondari na Vyuo vya Elimu ya Juu Afrika ya Mashariki. Kamati ya Uhariri
Dkt. Ernesto
Mosha – Mkurugenzi, Taasisi ya Taaluma za Kiswahili Prof. Mugyabuso
Mulokozi – Mhariri Mkuu Dkt. Mussa
Hans – Mhariri Msaidizi Dkt. Lutz
Diegner – Chuo Kikuu cha Humboldt,Ujerumani Dkt. Athumani
Ponera – Chuo Kikuu cha Dodoma, Tanzania Dkt. Miriam Kenyani
Osore – Chuo Kikuu cha Kenyatta, Kenya Washauri wa wahariri
Prof. Cyprean
Niyomugabo – Chuo Kikuu cha Rwanda, Rwanda Prof. Sangai Mohochi
– Chuo Kikuu cha Rongo, Kenya Dkt. Abel Mreta
– Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania Dkt. Joseph Nyehita
Maitaria – Chuo Kikuu cha Karatina, Kenya Dkt. Selemani
Sewangi – Baraza la Kiswahili la Taifa, Tanzania Prof. Ipara
Odeo – Chuo Kikuu cha Kibabii, Kenya Dkt. Wael Nabil
Ibrahim – Chuo Kikuu cha Al Azhar, Misri MAELEKEZO KWA WAANDISHI
WA MAKALA MULIKA ni jarida la
taaluma ya Lugha na Fasihii ya Kiswahili. Jukumu lake kuu ni kukusanya na kusambaza maarifa yanayohusu Lugha na Fasihi ya Kiswahili yaliyokitwa katika utafiti mpevu. MULIKA limeendelea kuwa daraja katti ya watumiaji wa Kiswahili popote walipo, na wataalamu wa Kiswahili katika Sekondari ba Vyuo vya Elimu ya Juu Afrika ya Mashariki. Jarida huchapishwa mara
moja kwa mwaka. Jarida linapokea Makala
yaliyoandikwa kwa Kiswahili TU. Makala yapigwe chapa kwenye karatasi za A4, mistari ikitengwa kwa kipimo cha nafasi mbili. Upande mmoja tu wa karatasi utumiwe. Mwandishi awasilishe
kwa Mhariri, nakala tatu za muswada wake, pamoja na nakala tepe iliyowekwa katika mfumo wa kikompyuta katika muundo wa Microsoft WORD. Ukurasa wa kwanza wa
Makala uoneshe jina la Makala, jina kamili la mwandishi (au waandishi) wa Makala (Ikiwa ni pamoja na wwadhifa wake) na anuani yake. Ukurasa wa pili uoneshe
jina la Makala na ufupisho wa Makala (Ikisiri) kwa maneno yasiyozidi 300. Jina la mwandishi lisiandikwe. Unapotaja marejeleo
kwenye matini taja jina l mwisho la mwandishi, likifuatiwa katika mabano na tarehe ya chapisho lake na kurasa zilizorejelewa, k.m. Yahya (1983:139). Kwenye orodha ya marejeleo au bibliografia majina ya marejelewa yapangwe kialfabeti. Tanbihi ziwekwe namba
na zitumike pale tu inapobidi. Maelezo ya tanbihi yatolewe kwenye ukurasa wa pekee mwisho wa Makala, yaani ya kuorodhesha marejeleo. Makala yatatathiminiwa
na walau wasomaji wawili, bila ya wao kujua mwandishi ni nani. Waandishi waepuke kuweka utambulisho wowote katika Makala zao ilo wanaosoma Makala hayo na kuyatathmini wafanye kazi yao kwa uyakinifu. Waandishi ambao Makala yao yatakubaliwa kuchapishwa watapatiwa NAKALA MOJA YA Jarida lenye Makala yao pamoja na malopoo kumi ya Makala yao. Makala yapelekwe kwa:
Mhariri
MULIKA
Taasisi ya Taaluma za
Kiswahili Chuo Kikuu cha Dar es
CHANZO >>>>>>>
Salaam |