MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

SHAIRI: HASARA YA KIWAKACHO - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
SHAIRI: HASARA YA KIWAKACHO - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6)
+---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50)
+---- Thread: SHAIRI: HASARA YA KIWAKACHO (/showthread.php?tid=833)

SHAIRI: HASARA YA KIWAKACHO - MwlMaeda - 08-13-2021

HASARA YA KIWAKACHO
Kiwakacho huzimika, zii kisiwake tena,
Waja wanaposhituka, kiza kinasemezana,
Hakuna wa kuinuka, aweke nuru bayana,
Hasara ya kiwakacho, huwaka na kuzimika.

Huwaka kwa kuripuka, ripuripu kusongana,
Mwisho wake ukifika, muwako wake hakuna,
Wenye subira kushika, hubaki kukonyezana,
Hasara ya kiwakacho, huwaka na kuzimika.

Ukingoni ukifika, moto ulowaka sana,
Hapo inathibitika, muwako huna maana,
Moto ukisha zimika, huna thamani bayana,
Hasara ya kiwakacho, huwaka na kuzimika.

Hata uvuke mipaka, iwe umeshindikana,
Kwa mafuta ya Merika, au Kusini ya China,
Mwisho ukisha wadika, waja watasemezana,
Hasara ya kiwakacho, huwaka na kuzimika.

Mtunzi Filieda Sanga
Mama B
Mabibo Dsm
0753738704