UTENZI: NAKUPENDA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: UTENZI: NAKUPENDA (/showthread.php?tid=829) |
UTENZI: NAKUPENDA - MwlMaeda - 08-13-2021 NAKUPENDA Ewe pepo za bahari nibarizi, Umenipa yako shwari, sinihizi, Mapenzi yako fahari, mtulizi, Moyo umekufiri,muokozi, Nakupenda! Ewe wangu nyota njema, asubuhi, Umenipa kutazama, nifurahi, Alfajiri na mapema na sikahi, Kusinzia nimegoma na walahi, Nakupenda! Ewe wangu njiwa dume, niimbie, Uniondoke ukame, unijie, Utokako nitazame, nitulie, Sadirini nikaseme, nifurahie, Nakupenda! Tabibu wa moyo na mwili huu, Yashushe mapigo yasende juu, Unipe mapenzi yale makuu, Yasiwake na kuzima,Ile vuu, Nakupenda! Ewe jua la machweo niangaze, Na upepo wa jioni nipulize, Taratibu masikio, nong'oneze, Kwa tamu yako sauti, niambilize, Nakupenda! Mafuriko ya mahaba niogolee, Unipe basi kushiba yaninogee, Tamaa yangu kuziba usipotee, Hapo nitakuwa zoba, nikapotee, Nakupenda! Ewe usiku mtulivu, unilaze, Macho yangu matulivu, yafumbilize, Niwe wako msikivu, nibembeleze, Niondolee makovu, nipendekeze, Nakupenda! Mtunzi Filieda Sanga Mabibo Dsm 0753738704 |