08-13-2021, 06:10 PM
KISU
Pokea zino salamu,msomaji msifika
Leo nashika kalamu, ninalo lakuandika
Kwani nina kubwa hamu,tungo ipate someka
Sifa ya kali makali,wala usambe umbile
Si hoja wake muundo,hivyo usirubunike
Utakupata mfundo,mwishowe ufedheheke
Utembee kwa vishindo,kukata visikatike
Sifa ya kisu makali,wala usambe umbile
Japo kiwe kama panga,hima chungua makali
Kama butu hata kanga,kumchinja ni muhali
Watu watakusimanga,ziruke zako akili
Sifa ya kisu makali,wala usambe umbile
Nakitoke uhabeshi,ala iwe ya dhahabu
Watakiona bileshi,bure upate aibu
Tena hata kwa mapishi,ni kujitia adhabu
Sifa ya kisu makali,wala usambe umbile
Kaditama tambueni,vingine havinoleki
Uwe na tupa dazeni,ukali hawongezeki
Jisu hili kuwa ndani,ni kujitia hamaki
Sifa ya kisu makali, wala usambe umbile
Abdul Ndembo
Mburahati Sekondari
Pokea zino salamu,msomaji msifika
Leo nashika kalamu, ninalo lakuandika
Kwani nina kubwa hamu,tungo ipate someka
Sifa ya kali makali,wala usambe umbile
Si hoja wake muundo,hivyo usirubunike
Utakupata mfundo,mwishowe ufedheheke
Utembee kwa vishindo,kukata visikatike
Sifa ya kisu makali,wala usambe umbile
Japo kiwe kama panga,hima chungua makali
Kama butu hata kanga,kumchinja ni muhali
Watu watakusimanga,ziruke zako akili
Sifa ya kisu makali,wala usambe umbile
Nakitoke uhabeshi,ala iwe ya dhahabu
Watakiona bileshi,bure upate aibu
Tena hata kwa mapishi,ni kujitia adhabu
Sifa ya kisu makali,wala usambe umbile
Kaditama tambueni,vingine havinoleki
Uwe na tupa dazeni,ukali hawongezeki
Jisu hili kuwa ndani,ni kujitia hamaki
Sifa ya kisu makali, wala usambe umbile
Abdul Ndembo
Mburahati Sekondari
Mwl Maeda