MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI

Welcome, Guest
You have to register before you can post on our site.

Username
  

Password
  





Search Forums

(Advanced Search)

Forum Statistics
» Members: 5,481
» Latest member: Kundlimatching
» Forum threads: 2,178
» Forum posts: 2,256

Full Statistics

Online Users
There are currently 140 online users.
» 0 Member(s) | 138 Guest(s)
Bing, Google

Latest Threads
Buy Vilitra 60 Mg |【Get E...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-24-2023, 11:45 AM
» Replies: 0
» Views: 0
How to take Cenforce50?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-19-2023, 12:59 PM
» Replies: 0
» Views: 0
About the Vidalista 60 Mg...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-04-2023, 04:07 PM
» Replies: 0
» Views: 0
What Is Vidalista 60?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-03-2023, 10:49 AM
» Replies: 0
» Views: 0
How to take Cenforce 100 ...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
03-29-2023, 02:37 PM
» Replies: 0
» Views: 66
How is Vidalista 10 Mg us...
Forum: Watunzi wa Kiswahili
Last Post: Kieth_winsett
03-27-2023, 01:26 PM
» Replies: 0
» Views: 117
Obtain Thesis Paper Assis...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Minny02
03-24-2023, 03:01 PM
» Replies: 0
» Views: 200
SEO services for sports f...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Maria Poland
03-17-2023, 01:51 PM
» Replies: 1
» Views: 223
NUKUU ZA KISWAHILI DARASA...
Forum: Nukuu
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:31 PM
» Replies: 0
» Views: 788
NECTA K4 2022
Forum: Mitihani
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:25 PM
» Replies: 0
» Views: 403

 
  KWA MKAPA HATOKI MTU
Posted by: MwlMaeda - 06-14-2021, 08:05 AM - Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili - No Replies

KWA MKAPA HATOKI MTU-KAULIMBIU YA SIMBA ILIYOWAFIKISHA HATUA YA ROBO FAINALI-KONGOLENI KWA KUTUHOMBORA-UCHAMBUZI WA MISEMO AU KAULIMBIU 7 ZA SIMBA

Anaandika PhD Dkt. Ahmad Sovu

Ndugu zanguni. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania-Kazi iendelee.

Kwa wale wapenzi wa makala zetu ambao wengi wamezoea makala zetu zilizo nyingi huwa zikichambua masuala anuwai yahusuyo hotuba za viongozi wetu, lugha yetu adhimu ya Kiswahili na siasa.

Uchambuzi wetu wa leo umejikita katika suala la michezo, lakini kwa muktadha wa namna matumizi ya lugha za hamasa (kaulimbiu au misemo) zinavyosaidia kuchagiza mafanikio ya timu fulani au chama au asasi nyingine yoyote ile ya kijamii.

Kaulimbiu kama tulivyowahi kufafanua katika makala zetu huko nyuma. Ni misemo rahisi inayotumiwa zaidi na wanasiasa au asasi fulani kwa lengo la kujenga hamasa yenye madhumuni ya kufikia malengo fulani.

Makala haya maarubu yake makuu, ni kutaka kuonesha namna Timu ya Simba ya Kariakoo, Dar es salaam -Tanzania ilivyoweza kufikia hatua ya juu ya mashindano ya Klabu bingwa barani Afrika pamoja na mambo mengine lakini kwa umuhimu wa misemo au kaulimbiu mbalimbali.

Pamoja na kujizatiti kwa maandalizi mengine ya kuimarisha kikosi kama klabu ya mpira wa miguu, Simba pia walitumia kaulimbiu mbalimbali kwa lengo la kujenga morali na kutia shime wachezaji, viongozi na mashabiki ili kufikia malengo yao.

Hivyo basi, msingi wa makala haya mwega wake upo kwenye kaulimbiu naweza kuiita kaulimbiu kuu ya *Kwa Mkapa hatoki Mtu*

Uwanja wetu mkuu wa michezo umepewa jina la aliyekuwa Rais wa awamu ya 3, hayati Mzee Benjamini Wiliam Mkapa. Kwa hivyo kaulimbiu ya Simba ililenga kuonesha kuwa mechi zote zitakazochezwa kwenye uwanja wa nyumbani hakuna timu itakayoshinda mchezo ndani ya dimba hilo. Yaani kwa Mkapa hatoki mtu. Wakimaanisha katika uwanja wa nyumbani Tanzania hatutafungwa na timu  yoyote ile katika uwanja huo.

Ilianza kama mzaha, lakini hadi jana  imethibitika kuwa kwa Mkapa hakutoka mtu.

Jana timu ya Simba ilitolewa kwenye mashindano hayo na timu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini kwa ushindi mwembamba wa goli 1. Yaani 4 kwa 3.

Ufuatao ni baadhi ya uchambuzi wa kaulimbiu au misemo 7 maarufu ya Simba zilivyoichagiza kaulimbiu kuu ya kwa Mkapa hatoki mtu.

Ingawa misemo hii iliyo mingi imebuniwa katika lugha ya Kingereza rahisi. Kiingereza ambacho Watanzania wengi wanakifahamu maana yake.
Misemo hii ilichagizwa na mbwembwe, madoido, ukabobo, kujishongondoa, kujitanibu na hata kujifaragua kwa mnenaji wa timu hiyo Ndugu Haji Manara. Uwasilishaji wa Manara kwa misemo na kaulimbiu hizi ulisaidia sana kutamalaki kwake.

Ukiachilia mazonge au ukayeye wetu wa Usimba na Uyanga Manara naweza kusema aliifanya kazi yake vilivyo.

Sasa hebu tuiduruusu misemo au kaulimbiu hizo hapa chini:

1. Simba Next Level
Msemo huu ambao una maana ya TIMU ya Simba ni ya Kiwango kingine cha juu. Msemo huu ulilenga kuwajenga kisaikolojia wachezaji, viongozi wa Simba na hata MASHABIKI kuwa TIMU yao ni ya kiwango cha juu ukilinganisha pengine na timu nyingine za Tanzania. Haya tuliyashuhudia hata pale ambapo mashabiki wa Simba wakihojiwa walikuwa wakitamba na kujimwambafai kuwa wao ni wa kiwango cha juu. Saikolojia katika msemo huu ulisaidia sana kuifanya timu ya Simba kujiamini na kusonga mbele katika kila hatua. Wachezaji walijiona wao ni timu kubwa na wanastahiki kuchukua ubingwa.

2. Do or Die
Kaulimbiu au msemo mwingine ulikuwa ni huu wa 'Do or Die' ukiwa na maana ya kufa au kupona. Kama kumbukumbu zangu ziko sawa msemo huu ulichagizwa wakati wa mechi ya marudio baina ya Simba na timu ya AS Vita ya Congo. Kufa au kupona unaweza ukaona ni maneno machache na mepesi? lakini yalisaidia kuijenga saikolojia ya wachezaji wa Simba.

Kufa au kupona, yaani liwalo na liwe USHINDI lazima. Hii ni kauli inayoongeza ari ya kujituma kwa hali zote kuhakikisha ushindi unapatikana. Kaulimbiu hii ilizaa matunda na kuifanya Simba kuendelea kujizolea alama Katika hatua za makundi. Msemo huu pia ulisikika ukitolewa na MASHABIKI wa Simba kuwa na wao walikuwa wakisema tu  ni kufa au kupona leo.


3. War in Dar (WIDAR)
Msemo au kaulimbiu hii ambayo ina maana ya Vita ndani ya Dar es Salaam. Kama asemavyo Mtangazaji wa Azam, Baraka Mpenja. Msemo huu haukumaanisha vita ya vifaru, bunduki za SMG au AK 47 wala mabomu na kuuuwa watu la hasha. Ni vita ya kisoka, ni vita pira biriani, pira sambusa. Msemo huu ulihanikiza mechi ya marudio kati ya Simba na Platinum. Nakumbuka Simba aliibuka na ushindi wa bao nne katika uwanja wa Mkapa. Ilikuwa vita kweli, wachezaji walijituma wakapambana vilivyo na kuishinda vita ya kisoka. Msemo 'war in Dar' unaifanya Simba kubakia kileleni mwa kundi lake.

4. Total war Point of no return
Kaulimbiu au msemo mwingine ulikuwa  ni huu, msemo huu ulimaanisha _vita kamili kwa hatua hii hakuna kurudi nyuma_ .

Ama kwa hakika misemo hii ni muhimu sana kwani huongeza siha na afya kwa wachezaji  na wadau wote wa timu inayohusika. Kuwaambia wachezaji sasa ni vita kamili na hakuna kurudi nyuma ni jambo linalowapa ukakamavu, uimara na linalotia nguvu kukabiliana na timu pinzani. Katika hali hiyohiyo tulishuhudia vita kamili na Simba kuendelea kujinyakulia alama muhimu dhidi ya Al Ahly na kuzidi kusogea mbele zaidi katika mashindano hayo. Ambapo Simba ilimaliza Michezo yake katika hatua za makundi. Simba iliibuka ikiwa kinara katika kundi lake kwa alama 13 dhidi ya wababe kama Al Ahly ya Misri. Vita kamili waliyoinadi iliwafanya Simba wasirudi nyuma.

5. Visit Tanzania
Msemo mwingine ni huu wa Visit Tanzania, ukimaanisha tembelea Tanzania. Simba baada ya kusogea katika hatua zaidi katika mashindano hayo, walianza kuiona fursa ya kuitangaza nchi yetu ya Tanzania. Wakaona pia hatuwezi kuitangaza nchi tu hivihivi wakaamua kubuni msemo wa Tembelea Tanzania huku usawiriwa na picha za Mlima Kilimanjaro. Ingawa kwa maoni yangu ingekuwa tembelea Tanzania hakuna matata. Msemo huu ulihanikizwa katika fulana zao, mabegi, barakoa na vifaa vyao mbalimbali. Mawaziri wenye dhamana nao kwa wakati  huo waliiunga Simba mkono. Kwani msemo huo ulichagiza uchumi katika kukuza utalii wetu. Simba walisafiri Congo, Sudan, Misri na  Afrika Kusini. wakiwahamasisha kila wanayekutana naye kutembelea Tanzania. Maana waliwahimiza wageni kuja kutembelea nchini mwetu. Tembelea Tanzania Simba Sports Club.

6. Pira Biriani
Msemo mwingine ni huu wa pira biriani. Msemo huu ulikuwa na maana ya Mpira wa Biriani. Biriani ni aina upishi wa wali ambao kwa siku za hivi karibuni chakula hiki kimepata umaarufu sana hasa katika majiji ya Dar es salaam, Mwanza, Tanga, Unguja, Dodoma na kwenye miji mbalimbali. Chakula cha biriani kimetengewa siku mahsusi ambayo huliwa kwa wingi. Mathalan, kwa Dar es salaam watu wengi hutoka katika ofisi zao siku za Ijumaa na kwenda kwenye vijiwe, nyumba, migahawa, hoteli mbalimbali kwenda kula Biriani kwa lengo la kukidhi  haja ya mioyo na mitima yao.?? mambo ya Dar na Biriani ?.

Katika hali kama hiyo timu ya Simba inataka kuonesha aina ya mchezo wanaoucheza. Wanatafuta msemo rahisi wa kuwaelewesha mashabiki wao na wanaamua kubuni msemo *pira biriani* kwa mujibu wa mchambuzi wa masuala ya Michezo ndugu Ali Kamwe katika makala  yake ya "mambo 10 niliyoyaona Simba Vs Kaizer Chiefs" anaelezea  namna pira Biriani lilivyotamalaki pale kwa Mkapa Simba walipocheza na klabu ya Kaizer Chiefs anaposema,

Simba wamepiga mashuti 32 na on target 10, Chama aliutembeza mpira hakuna na mambo mengi, Boko kaweka kamba 2 muhimu, sub ya Muzamir na Morisson na Asante kwa Thabalala aliyekuwa akitoa  superb sana kwenye kuipandisha timu na kuidumbukia vyema katikati muda ambao viuongo wake walivamia zone ya Kaizer...

uchambuzi huu wa Alikamwe unaonesha namna msemo wa Pira Biriani ulivyooneshwa na timu ya Simba katika dimba la kwa Mkapa.

7. Ama zetu ama zao Do or Die season 2
Msemo mwingine ambao unaweza kuuita wa mwisho katika mashindano haya, ni huu msemo wa ama zetu ama zao, kufa au kupona msimu wa 2.

Msemo huu umekuwa muhimu sana na umedhihirisha kuwa kwa Mkapa hatoki mtu. Kila shabiki  wa michezo ambaye anajua namna ambavyo mchezo wa marudio kati ya Simba na Kaizer Chiefs ulikuwa mchezo mgumu na wenye presha na msisimko wa aina yake. Basi anaweza kubaini ni kwa namna gani Simba walipambana hadi kushinda mchezo huo.

Simba walipoteza mchezo wao wa awali wa robo fainali dhidi ya timu hii Kaizer Chiefs kwa kufungwa bao 4 kwa nunge.

Kama ilivyo ada yao Simba wanasema pamoja na kipigo hicho waliiendeleza kaulimbiu yao kuwa *kwa Mkapa hatoki mtu* na wakahanikiza kwa kaulimbiu ya ama zetu ama zao kufa au kupona msimu wa pili. Simba wanapambana vilivyo kuonesha kuwa ni ama zetu au ama zao, jasho la mapambano linawavuja.
Kwa Mkapa hatoki mtu Simba wanaibuka na Ushidi wa GOLI 3 kwa nunge. Ingawa wanatolewa kutoka Robo Fainali ya 2020/21 kila shabiki wa Simba anaondoka Kwa Mkapa, akijipiga kifuani kwake na kusema HATUWADAI CHOCHOTE.

Huku wachambuzi, wadau wa soka wakitoa sifa kedekede kuwa Simba imepiga hatua kubwa sana. Nikakumbuka  msemo wa Next level Hivi ndivyo Simba walivyoiishi kaulimbiu ya ama zetu ama zao kwa Mkapa hatoki mtu.

Simba anaondolewa kwenye mashindano akiwa kwenye hatua ya robo fainali. Katika robo fainali hii akiwa ameiingia kibabe kwa kuongoza kundi na akikutana na miamba mingine ya soka kama vile Mamelodi Sundawns ya Afrika Kusini, Al Ahly ya Misri, Waydad Casablanca ya Moroko, Esperance de Tunis ya Tunisia na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.

Hivi ndivyo ambayo kaulimbiu kuu ya kwa Mkapa hatoki mtu na misemo mbalimbali ilivyochagiza mafanikio makubwa ya soka kwa timu ya Simba.

Kaulimbiu na misemo hiyo imetuacha na hadithi ya vipigo kwa timu kama Plateau United, Platnum FC, AS Vita, Al Merrikh na Al Ahly.

Simba anafikia mwisho wa mashindano haya akiwa amecheza michezo 12, akishinda mechi 7, akipoteza 3 akitoka sare mechi 2, akiwa na magoli ya kufunga 17 na kufungwa  9 na akipata hati/mkeka safi (clean sheet) katika mechi 8.

Kongole sana Mohammed Dewji (Mo) mwekezaji thabiti maana tija na rajua imepatikana.

Pia, Mwandada Barbara Gonzalez, mwanamke wa shoka na mtendaji Mkuu wa klabu kwa ubunifu na usimamizi mahiri bila kuwasahau Mwalimu Didier Gomes Da Rosa na Msaidizi wake Seleman Matola (Veron) mtoto wa nyumbani, viongozi wengine,wadau, wanachama, mashabiki wa Simba na wengineo.

Ama kwa hakika tumeona kwa Mkapa hakutoka mtu. Nikakumbuka maneno ya Baraka Mpenja, siku Simba walipocheza na  Platimum aliposema; _Kwa Mkapa ni uwanja ambao hakuna kisichowezekana, uwanja ambao Simba wanabadilisha yasiyowezekana yakawezekana, yasiyotarajiwa yakatarajiwa, yasiyotabirika yakatabirika na usiyoyaamini ukayaamini...This is another level_. Kwa hakika Kwa Mkapa hatoki mtu.

Kwa kuhitimisha niseme tu,  pengine hii ni fursa ya vilabu vingine kama Yanga, Azam F.C, Namuongo, Mtibwa n.k kujiimarisha zaidi ili kuendelea kuliinua soka letu  la Bongo. Nadiriki kusema Simba wametuhombora, yaani wametuinua kiinchi katika medani za soka la Kimataifa. Kongoleni sana wekundu wa Msimbazi.
kwamkapahatokimtu

0713400079
sovu82@gmail.com
Mshititi Dokta Ahmad Sovu.
Mhadhiri Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni DSM.

Print this item

  NAFASI YA VYAMA NA TAASISI MBALIMBALI KATIKA MAKUZI YA KISWAHILI
Posted by: MwlMaeda - 06-14-2021, 07:19 AM - Forum: Taasisi za kukuza lugha - No Replies

Kwa Mukhtasari

IKIWA idara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI), awali ikiitwa Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI) ni miongoni mwa taasisi kongwe zaidi za lugha nchini Tanzania na Afrika Mashariki. Madhumuni yake ni kusimamia usanifishaji na maendeleo ya Kiswahili.

Japo Kiswahili kimeendelea kubaki nembo ya Afrika, mjadala usio na mwisho kuhusiana na ni ipi lugha ya kufundishia katika shule na vyuo nchini Tanzania ni ithibati kwamba Kiswahili hakijapokezwa hadhi inayostahiki katika mengi ya mataifa ya Afrika Mashariki na Kati.

TUKI, kwa sasa TATAKI, ilianzishwa mnamo 1930 ikijulikana kama International-Territorial Language (Swahili) Committee kwa nchi tatu za Afrika Mashariki na baadaye ikaitwa Kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki.

Mnamo 1964, kamati ilifanywa kuwa sehemu ya UDSM na baadaye ikaitwa Chuo cha Uchunguzi wa Kiswahili. Tangu 1970 kimepewa jina la Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI). Mwaka 2009, TUKI iliungana na iliyokuwa Idara ya Kiswahili ya UDSM na kuunda taasisi kubwa zaidi inayoitwa TATAKI.

Majukumu ya taasisi hii awali yalikuwa ni kutafiti nyanja zote za lugha ya Kiswahili, fasihi na utamaduni na kuchapisha matokeo ya utafiti huo.

Hivyo pamoja na Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA), TUKI ni mlinzi wa usanifu wa lugha ya Kiswahili katika Tanzania. Baada ya kuungana na Idara ya Kiswahili, sasa TATAKI inafundisha Isimu, Fasihi na Historia ya Lugha ya Kiswahili.

Inafundisha Kiswahili kama lugha ya pili hasa kwa wageni kutoka nje ya ulimwengu wa Waswahili na kuendeleza utungaji wa kamusi mbalimbali zinazohusiana na Kiswahili.

BAKITA

Ni taasisi ya serikali iliyoundwa kwa sheria ya Bunge Na.27 ya mwaka 1967 kwa madhumuni ya kukuza Kiswahili. Kutokana na sheria hii, Baraza ndilo mratibu wa kusimamia asasi zote na mawakala wote wanaokuza Kiswahili katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

BAKITA imekuwa na mchango mkubwa katika ukuzaji na uenezaji wa lugha ya Kiswahili kupitia majukumu yake.

Miongoni mwa majukumu ya Baraza hili kama yalivyofafanuliwa katika sheria hiyo ni kuratibu na kusimamia maendeleo na matumizi ya Kiswahili nchini pamoja na kushirikiana na vyombo vingine vinavyojihusisha na maendeleo ya Kiswahili.

Huhimiza matumizi ya Kiswahili katika shughuli rasmi na za kawaida, huandaa vipindi mbalimbali redioni ili kuhimiza matumizi sahihi ya lugha ya Kiswahili, hushirikiana na mamlaka zinazohusika kuthibitisha tafsiri sanifu za istilahi, hutoa huduma za tafsiri na ukalimani kwa serikali, mashirika ya serikali na yasiyo ya serikali na asasi nyingine pamoja na kuidhinisha vitabu vya Kiswahili vitakavyotumika shuleni na vyuoni kabla havijachapishwa.

TAKILUKI

Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kigeni (TAKILUKI) ilianzishwa mnamo 1979 kwa lengo la kukuza na kueneza Kiswahili ndani na nje ya Zanzibar.

Inajishughulisha na kuratibu, kuendesha mafunzo ya Kiswahili visiwani Zanzibar, kuhariri miswada mbalimbali ili kuthibitisha ufasaha wa Kiswahili na kufanya tafiti za Kiswahili katika nyanja zake zote, hususan sarufi na fasihi.

TAKILUKI inatoa ushauri wa kitaaluma kwa watunzi wa vitabu ili waweze kuandika kazi zenye ubora, na kushirikiana na wadau wengine wa Kiswahili kuandaa na kuendesha semina, warsha na kozi fupifupi za Kiswahili.

CHAUKIDU

Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) kina makao makuu katika Chuo Kikuu cha Wisconsin-Madison, Marekani.

Madhumuni yake ni kuwajumuisha pamoja wakuzaji wa Kiswahili duniani kote kwa lengo la kuchochea kasi ya malengo mahususi kama vile kukuza Kiswahili katika nyanja zote ambamo lugha hii inatumika na kuongeza ufanisi wa mawasiliano katika ufundishaji na utafiti wa maarifa ya aina zote mathalan uandishi na utangazaji wa habari, uandishi na uchapishaji wa vitabu na majarida pamoja na utayarishaji wa safari za mafunzo katika Afrika Mashariki na Kati.


Husambaza habari na matokeo ya utafiti kwa kutumia machapisho mbalimbali na teknolojia ya mtandao wa kompyuta kuhusu vipengele mbalimbali vya Kiswahili na masuala yanayohusiana na Kiswahili. CHAUKIDU inaelimisha umma juu ya umuhimu wa kujivunia, kuendeleza, na kuheshimu Kiswahili.

Vilevile inashauri ama kushinikiza serikali za nchi ambamo Kiswahili kinazungumzwa kutambua thamani iliyobebwa na maliasili hii ili kuunda sera mwafaka za kukiendeleza kadri ya uwezo wake kwa manufaa ya maendeleo ya serikali na watu wake kijamii, kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni na kielimu.

CHAWAKAMA

Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili katika vyuo vikuu vya Afrika Mashariki (CHAWAKAMA), kilianzishwa mnamo 2004 kwa lengo la kukuza na kueneza Kiswahili katika eneo lote la Afrika Mashariki kupitia kwa wanafunzi wanaosoma Kiswahili vyuoni.

Wanachama wa chama hiki ni wale wanaosomea taaluma za Kiswahili ila wapenzi wa Kiswahili pia wanaweza kujiunga nacho.

Mara kwa mara, CHAWAKAMA huandaa makongamano kwa lengo la kuwapa wanachama nafasi ya kujadili, kuimarisha, kuendeleza na kukuza vipawa vyao vya lugha na fasihi ya Kiswahili, kuamsha ari ya mapinduzi ya utamaduni wa Kiswahili, kueneza Kiswahili ndani na nje ya nchi, kushirikiana na vyama vingine katika juhudi za kuendeleza na kuimarisha Kiswahili ndani na nje ya nchi wanachama, kuwaunganisha wanafunzi wa Kiswahili Afrika Mashariki na Kati katika kukikuza Kiswahili pamoja na kushirikiana na asasi mbalimbali zinazojihusisha na ukuzaji na uenezaji wa Kiswahili.

CHAKAMA

Chama cha Kiswahili Afrika Mashariki (CHAKAMA) ndicho cha tatu kwa umaarufu zaidi miongoni mwa wasomi, wataalamu na wahadhiri wa vyuo vikuu baada ya CHAUKIDU na Chama cha Walimu wa Lugha za Kiafrika (ALTA) ambacho haundaa makongamano yake jijini Bayreuth, Ujerumani.

Kwa pamoja na Chama cha Kiswahili cha Taifa (CHAKITA), CHAKAMA huchapisha jarida la chama na machapisho mengine ili kusaidia kueneza taaluma za Kiswahili.

Aidha, huhifadhi kumbukumbu za wataalamu wa Kiswahili kwa nia ya kutumia katika kufanikisha malengo ya chama na wadau wa Kiswahili pamoja na kuratibu makongamano na mijadala mbalimbali inayohusiana na taaluma za Kiswahili.

Chama huandaa makongamano kila mwaka ambalo linawakutanisha wanachama wote katika vyuo mbalimbali katika nchi husika.

Katika makongamano hayo, mada mbalimbali zinazohusu Kiswahili na mustakabali wake hujadiliwa lakini pia maazimio mbalimbali huchukuliwa kuhusu maendeleo ya chama. Makala mbalimbali huandikwa na kuchapishwa kwa minajili ya kusomwa na watu mbalimbali.

Print this item

  SHAIRI LA KUMUENZI HAJI GORA HAJI
Posted by: MwlMaeda - 06-14-2021, 07:11 AM - Forum: Watunzi wa Kiswahili - No Replies

Tangao la nuru yako, limezunguka bahari
Kimbunga kwenye maeko, kimetulia shuwari
Yamepita maandiko, kwa kalamu ya kahari
Umekwisha mzunguko, kuishi kwenye sayari
Lala salama habibi, kipenzi cha washairi

Andiko la maajabu, labubujika bongoni
Ni andiko la dhahabu, si la kusoma chuoni
Ni tunu yake Wahabu, hidaya yenye thamani
Alitunukiwa babu, Gora pomoni moyoni
Lala salama habibi, kipenzi mwanafasihi

Unaishi vitabuni, umelala mioyoni
Maisha ya hali duni, uliishi duniani
Ni duni tulivyodhani, ila duni ya thamani
Naamini kwa Manani, maisha yako peponi
Lala salama habibi, kipenzi mwanachuoni

Nikuzungumze vipi, hata niishe kalima
Niziseme mara ngapi, sifa kwa yako heshima
Nikazitafute wapi, hadithi za kukusema
Yatosha japo makapi, bora niweke khatima
Lala salama habibi, kipenzi cha kila mtu

Ali Hilal
Zanzibar.
13.6.2021

Print this item