SHAIRI: KISU - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: KISU (/showthread.php?tid=832) |
SHAIRI: KISU - MwlMaeda - 08-13-2021 KISU Pokea zino salamu,msomaji msifika Leo nashika kalamu, ninalo lakuandika Kwani nina kubwa hamu,tungo ipate someka Sifa ya kali makali,wala usambe umbile Si hoja wake muundo,hivyo usirubunike Utakupata mfundo,mwishowe ufedheheke Utembee kwa vishindo,kukata visikatike Sifa ya kisu makali,wala usambe umbile Japo kiwe kama panga,hima chungua makali Kama butu hata kanga,kumchinja ni muhali Watu watakusimanga,ziruke zako akili Sifa ya kisu makali,wala usambe umbile Nakitoke uhabeshi,ala iwe ya dhahabu Watakiona bileshi,bure upate aibu Tena hata kwa mapishi,ni kujitia adhabu Sifa ya kisu makali,wala usambe umbile Kaditama tambueni,vingine havinoleki Uwe na tupa dazeni,ukali hawongezeki Jisu hili kuwa ndani,ni kujitia hamaki Sifa ya kisu makali, wala usambe umbile Abdul Ndembo Mburahati Sekondari |