Utata ni hali ya neno au sentensi kuwa na maana zaidi ya moja. Kwa hiyo tungo tata ni tungo ambayo inaweza kuwa na maana zaidi ya moja.
Sababu za Utata Elezea Sababu za Utata
Utata katika tungo hutokea kwa sababu zifuatazo:
Neno kuwa na maana zaidi ya moja, kwa mfano neno mbuzi, kata n.k.
Kutozingatia taratibu za uandishi, Mfano; Tulimkuta Nyammy na rafiki yake, Mazala vs Tulimkuta Nyammy na rafiki yake Mazala. Katika sentensi hizi alama (,) ndio huleta tofauti, sentensi ya kwanza inamaana kulikuwa na watu wawili Nyammy na rafiki yake aitwaye Mazala na sentensi ya pili isiyo na alama (,) inamaanisha kulikuwa na watu wawili Nyammy na mtu mwingine ambaye ni rafiki yake Mazala
Kutumia maneno bila kuzingatia muktadha wa matumizi ya maneno hayo.
Utamkaji wa maneno. Wakati mwingine utata unaweza kujitokeza katika matamshi tu, ili hali katika maandishi utata hauonekani. Kwa mfano; Mimina wewe, katika maandishi linaweza kuandikwa mimi na wewe, na hivyo kuondoa utata.
Mjengo wa maneno. Utata huu huzuka katika vitenzi kama pigia. Chanzo cha utata katika kitenzi hiki ni kiambishi –i-. Kiambishi hiki kinaweza kumaanisha: kwa ajili ya…, kwa sababu ya.., kwa kutumia chombo fulani.., au mahali fulani.
Mfano:
Alimpigia ukorofi wake (kwa sababu ya)
Alimpigia kiatu (kifaa)
Alimpigia ndani (mahali)
Mifano ya utata katika tungo
Patience amemwandikia Lilian barua:Sentensi hii huweza kuwa na maana kuwa Patience ameandika barua kwenda kwa Lilian au Patience ameandika barua kwa niaba ya Lilian
Umefanikiwa kununua mbuzi?Sentensi hii huweza kumaanisha ununuzi wa mbuzi mnyama au mbuzi kifaa cha kukunia nazi.
Alimkuta amelala kwenye nyumba ya wageni:Sentensi hii huweza kumaanisha, nyumba ya mtu lakini inatumika kwa ajili ya wageni kwa malipo au ni nyumba inayomilikiwa na watu ambao ni wageni katika eneo lile.
Attu ametumwa na Aritamba:Sentensi hii inaweza kueleweka kumaanisha, Aritamba amemtuma Attu au Attu na Aritamba wametumwa wote kwa pamoja.
ZOEZI Zifuatazo ni sababu za utata, isipokuwa:
A Kutumia maneno ya picha
B Neno kuwa na maana zaidi ya moja
C kutumia maneno bila kuzingatia muktadha husika
D Umahiri wa lugha
Neno ‘mbuzi’ ni tata, kwa sababu___
A Lina maana moja tu
B Lina maana zaidi ya moja
C Lina maana iliyofichika
D Ni neno la Kiswahili
Utata unaojitokeza katika mazungumzo pekee husababishwa na nini?
A Mjengo wa maneno
B Maana zaidi ya moja katika neno
C Utamkaji wa maneno
D Kutozingatia taratibu za uandishi
Utata katika matumizi ya vitenzi kama vile ‘pigia’ husababishwa na___
A Neno kuwa na maana zaidi ya moja
B Utamkaji wa neno
C Kutozingatia taratibu za uandishi
D Mjengo wa neno
“Juma ametumwa na Rama” Utata wa tungo hii ni wa kutozingatia nini?
Ufahamu ni dhana inayorejelea kujua na kulielewa jambo kwa usahihi na kuweza kulielezea upya kwa usahihi bila kupoteza maana yake ya msingi. Ufahamu wa mtu waweza kupimwa katika kusikiliza jambo au katika kusoma.
Kusikiliza
Ufahamu wa kusikiliza ni zaidi ya kusikiliza tu kile kilichosemwa; badala yake ni uwezo wa mtu kuelewa maana ya maneno anayoyasikia na kuweza kuhusiana nayo kwa namna fulani. Kwa mfano mwanafunzi anaposikiliza hadithi, ufahamu mzuri wa kusikiliza humsaidia kuielewa hadithi hiyo, kuikumbuka, kuijadili, na hata kuisimulia tena kwa maneno yake mwenyewe.
Mambo ya Kuzingatia katika Ufahamu wa Kusikiliza
Elezea mambo ya kuzingatia katika ufahamu wa kusikiliza
Ufahamu wa kusikiliza unahusisha michakato kadhaa katika kuelewa na kupata maana ya kile kinachozungumzwa. Michakato hii inahusisha:
Kuelewa vizuri sarufi ya lugha ile inayozungumzwa
Kuelewa vyema maana ya maneno ya mhusiaka anayezungumza
Kuelewa sintaksia (muundo wa maneno) ya sentensi kwa namna zinavyowasilishwa.
Katika ufahamu wa kusikiliza, msikilizaji hana budi kuzingatia mambo yafutayo:
Kuwa makini na kuelekeza akili yote kwa mzungumzaji ili kuweza kusikia kila anachokisema.
Kutilia maanani vidokezo vya maana ili kubaini iwapo msemaji anaongeza jambo jipya, anatofautisha, anafafanua au anahitimisha hoja.
Msomaji anatakiwa kuandika baadhi ya mambo anayoona kuwa ni ya muhimu ili kumasidia kukumbuka hapo baadae.
Kuwa makini na ishara mbambali za mwili kama vile kurusha mikono, kutingisha kichwa, kutingisha mabega au hata kupepesa macho. Ishara hizi huwa zinachangia kwa kiasi kikubwa kupata maana katika mazungumzo.
ZOEZI
Lipi kati ya haya halifanyiki katika ufahamu wa
kusikiliza?
A
Kuzingatia vidokezi vya maana
B
Kuzingatia ishara
C
Kuzingatia matini
D
Kuandika kwa ufupi yasemwayo
___siyo ishara ya mwili inayopaswa kuzingatiwa na
msikilizaji ili kujibu maswali ya habari iliyosikilizwa?
A
Kutingisha kichwa
B
Kutembea
C
Kutingisha mabega
D
Kupepesa macho
Ni kipi kifanyike ili msikilizaji aweze kubaini mawazo
Kusoma kwa sauti ni namna ya kuyaangalia maandishi na kuyatamka kwa sauti inayosikika.
Mambo ya Kuzingatia katika Ufahamu wa Kusoma
Elezea mambo ya Kuzingatia katika ufahamu wa kusoma kwa sauti
Kuna vipengele viwili vinavyounda mchakato wa ufahamu wa kusoma:
Uelewa wa msamiati na
Uelewa wa matini
Ili kuilelewa habari/matini ni lazima msomaji awe na uwezo wa kuelewa msamiati uliotumika katika matini hiyo. Endapo maneno yaliyotumika hayataeleweka vilevile matini yote haitaeleweka.
Katika ufahamu wa kusoma, msomaji anatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo:
Kubaini mawazo makuu; msomaji anaposoma habari fulani au kitabu inatakiwa ajiulize, Je, kinachoongelewa hapa ni nini? Ni jambo gani hasa analolizungumzia mwandishi? Msomaji akiwa na maswali haya akilini mwake basi itakuwa rahisi kwake kuielewa habari hiyo.
Kuzingatia alama za uakifishi; msomaji ni lazima azingatie alama za uakifishi, kwa kufanya hivyo itamsaidia kuelewa ujumbe wa habari hiyo na endapo hatazingatia alama za uakifishaji anaweza kupotosha maana ya mwandishi.
Kubaini maana ya maneno na misemo mbalimbali; habari nyingine huwa zina maneno ya kisanaa hivyo ni muhimu msomaji kubaini maana ya maneno hayo katika muktadha wa habari hiyo, hii itamsaidia kuelewa vyema maana ya mwandishi.
Kwa kuzingatia haya yote msomaji atakuwa na uelewa mzuri juu ya habari aliyoisoma na pia anaweza kufupisha habari hiyo aliyoisoma.
ZOEZI
Alama za uakifishi zisipozingatiwa katika ufahamu wa kusoma
hupelekea___.
A
Kuwa makini
B
Kuongeza maneno
C
Kubaini mawazo makuu
D
Kupotosha maana
Ipi siyo kazi ya vidokezi vya maana anavyopaswa kuzingatia
msomaji katika ufahamu wa kusoma?
A
Kuhitimisha
B
Kutofautisha
C
Kuongeza jambo
D
Kutia chumvi
___siyo jambo la kuzingatia katika ufahamu wa kusoma.
A
Kuzingatia alama za uakifishi
B
Kubaini mawazo makuu
C
Kubaini misemo mbalimbali
D
Kufupisha ufahamu
Zifuatazo ni alama za uakifishi zinazopaswa kuzingatiwa katika
ufahamu wa kusoma, isipokuwa:
A
Kistari
B
Mubalagha
C
Nukta
D
Alama ya mshangao
Katika ufahamu wa kusoma, msomaji anatakiwa kuandika
pembeni mambo muhimu ili kumsadia___.
A
Kuuliza maswali
B
Kufupisha ufahamu
C
Kukosoa
D
Kukumbuka
Kujibu Maswali kutokana na Habari uliyosoma
Jibu maswali kutokana na habari uliyosoma
Kazi 2
Jibu maswali kutokana na habari uliyosoma
Kusoma Kimya
Kujibu Maswali kutokana na Habari uliyoisoma
Jibu maswali kutokana na habari uliyosoma
Katika usomaji huu, msomaji hufumba kinywa na kupitisha macho katika kila mstari harakaharaka. Macho hayo huunganisha neno lililotangulia na lile linalofuata. Ubongo wake huchambua mambo muimu yanayojitokeza, huku akiyahifadhi kichwani. Mtu akijizoeza kusoma kimya, ananufaika ifuatavyo:
Hupata nafasi ya kupima mwendo wake na kiasi cha welewa
Hujiepusha na lawama ya kusumbua wengine
Hukwepa kuzingatia kanuni za matamshi
Huweza kusoma maandishi mengi kuliko ambavyo angesoma kwa sauti
ZOEZI
Ni kipi kati ya hivi husababisha kushindwa kujibu maswali ya habari
uliyoisoma?
A
Kutoelewa maana ya misemo
B
Kuelewa swali
C
Kusoma kwa makini
D
Kusoma kwa utulivu
Ili kujibu maswali ya habari uliyoisoma ni muhimu kujibu kwa ufupi.
Hii husaidia___.
A
Kuwa makini
B
Kuokoa muda
C
Kujibu maswali yote
D
Kutambua maswali magumu
Ili kujibu maswali ya habari uliyoisoma ni sharti kuzingatia yafuatayo,
isipokuwa:
A
Kuwa mtulivu
B
Kujibu kwa ufupi
C
Kusoma kwa makini
D
Kuunganisha mawazo makuu
Kufahamu maana ya maneno na misemo katika kujibu maswali ya
habari uliyoisoma inahitaji kuelewa___.
A
Habari nzima
B
Swali lililoulizwa
C
Matamshi
D
Lugha iliyotumika
Nini kifanyike ili kuweza kuelewa uhusiano uliopo kati ya habari
uliyoisoma na maswali?
A
Kusoma kwa makini
B
Kufafanua maana ya maneno
C
Kujibu kwa ufupi
D
Kuuliza maswali
Kusoma kwa Burudani
Huu ni usomaji ambao lengo lake kuu huwa ni kujiburudisha tu. Katika usomaji wa aina hii, msomaji hujisomea zaidi magazeti, majarida na vitabu tofauti na vile vinavyotumika darasani.
Mambo ya Kuzingatiwa katika Ufahamu wa Kusoma kwa Burudani
Fafanua mambo ya kuzingatiwa katika ufahamu wa kusoma kwa burudani
Wakati mwingine sio lazima msomaji awe na vitabu vyote ambavyo anahitaji kuvisoma au magazeti na majarida. Inapotokea hivyo, msomaji anaweza kwenda maktaba kuazima kitabu nachokihitaji.
Ingawa lengo la msomaji huwa ni kujiburudisha tu, lakini pia hujiongezea maarifa. Hii ni kwa sababu, magazeti, majarida na vitabu sambamba na kutuamia lugha sanifu huelezea mambo mabalimbali yanayoihusu jamii.
Hivyo msomaji kutokana na kusoma vitabu na majarida mbalimbali hujiongezea kiwango cha welewa wa lugha na mambo mengine ya kijamii yanayojadiliwa humo.
Ni jambo zuri kwa msomaji kujijengea tabia ya kujipima ili aweze kuelewa kiwango cha maarifa aliyopata katika kujisomea. Kujipima huku kunaweza kufanywa kwa kujiundia utaratibu wa kuweka kumbukumbu ya vitu au makala zilizosomwa na kufanya ufupisho wa kila makala.
Utaratibu unaopendekezwa katika kujipima na kujiwekea kumbukumbu ya usomaji wa burudani ni kama ufuatao:
Tarehe…
Jina la kitabu/makala/gazeti….
Mchapishaji……
Mwaka/tarehe ya uchapishaji…..
Ufupisho wa habari(yasizidi maneno 20)
Fundisho/ujumbe mkuu ni…..
Jambo lililokuvutia sana……
Maoni kwa ujumla kama yapo….
ZOEZI
Lipi kati ya haya ni jambo la kuzingatia katika ufahamu wa kusoma kwa
burudani?
A
Kujibu maswali
B
Kujinufaisha
C
Kuweka kumbukumbu
D
Kuongeza maarifa
___siyo mojawapo ya kipengele cha kujiwekea kumbukumbu katika
ufahamu wa kusoma kwa burudani.
A
Jina la kitabu
B
Ujumbe mkuu
C
Kiini cha habari
D
Tarehe
Lengo kuu katika ufahamu wa kusoma kwa burudani ni___.
A
Kuongeza maarifa
B
Kujinufaisha
C
Kuweka kumbukumbu
D
Kujiburudisha
Katika ufahamu wa kusoma kwa burudani msomaji anaweza kujisomea
vitabu vifuatavyo, isipokuwa:
A
Makala
B
Vitabu vya ziada
C
Majarida
D
Vitabu vya kiada
Ufupisho wa kile kinachosomwa katika ufahamu wa kusoma kwa burudani
Katika lugha ya Kiswahili kuna angalau aina nane za maneno ambazo wataalamu wengi wa lugha wanakubaliana hivyo. Katika mada hii utaweza kujifunza na kubainisha aina zote nane za maneno na jinsi zinvyotumika katika sentensi. Utaweza pia kujifunza namna ya kutofautisha aina za maneno ambazo zimeleta ubishi miongoni mwa wataalamu wengi hususani katika Viunganishi na Vihusishi.
Ubainishaji wa aina Saba za Maneno
Aina Saba za Maneno ya Kiswahili
Bainisha aina saba za maneno ya Kiswahili
Aina za maneno katika lugha ya Kiswahili ni pamoja na hizi zifuatazo:
Nomino (N)
Viwakilishi (W)
Vitenzi (T)
Vivumishi (V)
Vielezi (E)
Viunganishi (U)
Vihusishi (H)
Vihisishi (I)
Ufafanuzi wa aina za Maneno
Maana ya kila aina ya Neno
Eleza maana ya kila aina ya neno
Nomino (N)
Nomino ni maneno yanayotaja vitu, watu, na hali kadhalika. Kuna aina mbali mbali za maneno ambazo ni pamoja na hizi zifuatazo:
Nomino za pekee:Nomino za pekee hutaja na kutambulisha nomino mahsusi na za kipekee. Yaani kuwa kitu ni hicho na wala si kingine chochote. Hizi ni nomino zinazohusisha majina kama vile ya watu, nchi, miji, mito, milima, maziwa na bahari. Herufi za kwanza za nomino za pekee huwa kubwa hata kama nomino hizi zinapatikana katikati ya sentensi.
Nomino za kawaida:Hizi kwa jina jingine huitwa nomino za jumla. Nomino hizi hazibainishi wazi wazi vitu ambavyo habari zake zinatolewa. Kwa mfano ikiwa ni mtu, mahsusi hatambuliwi. Haituambii kama ni Bahati, Bite ama Neema. Ikiwa ni mlima hautambuliwi kama ni Meru , Kilimanjaro au Evarest, yaani hutaja vitu bila kutaja umahususi wake kama ilivyo katika nomino za pekee.Hizi zinapoandikwa si lazima zianze na kwa herufi kubwa ispokuwa zimetumiwa mwanzoni mwa sentensi au zimetumika kama anuani ya kutajia kitu kama vile Mkuu wa Sheria. Katika mfano huu ‘sheria’ kwa kawaida ni nomino ya kawaida, lakini hapa inaanza kwa herufi kubwa kwani inataja anuwani ya kipekee.
Nomino za mguso:Nomino za mguso hurejelea vitu vinavyoweza kuhusika na mwanadamu kupitia milango ya hisia kama macho, mapua, masikio vidole na ulimi- yaani vitu vinavyoweza kushikika, kuonekana, kunusika na kuonjeka.
Nomino za jamii:Hizi ni nomino ambazo zinawakilisha vitu vingi katika jina moja, yaani nimino zinazotaja umla ya vitu vingi. Mfano; jozi ya viatu, umati wa watu, bustani ya maua, bunga ya wanyama
Nomiono dhahania:Kundi hili la nomino hutumia kigezo cha uwezekano wa kuhesabika kuziainisha. Hapa tunatofautisha kati ya nomino zinazowakilisha vitu vinavyohesabika kwa upande mmoja, na vile visivyohesabika kwa upande mwengine. Nomino ya vitu vinavyohesabikavitanda, nyumba,vikombe vitabu na kadhalika.Zile zisizohesabika hurejelea vitu ambavyo hutokea kwa wingi na haviwezi kugawika, kwa mfano maji, mate, makamasi, maziwa, moshi, mafuta. Aghalabu nomino hizo huwa sawa katika umoja na wingi.
Nomino za kitenzi jina:Hizi ni nomino zinazohusu vitenzi. Huundwa kwa kuongezwa kiambishi {ku-} cha unominishaji kwenye mzizi wa kitenzi cha kitendo halisi ili kukifanya kiwe nomino.
Vivumishi (V)
Vivimishi ni maneno yanayoelezea zaidi juu ya nomino, aghalabu vivumishi hutanguliwa na nomino. Kuna aina kadhaa za vivumushi, miongoni mwa hivyo ni pamoja na hivi vifuatavyo.
Vivumishi: vinaweza kujitokeza katika aina tatu ndogondogo.
Vivumishi vya sifa:hutoa sifa za nomino /kiwakilishi cha nomino. Sifa hizi huweza kuwa nzuri, mbaya au yoyote ile.
Vivumishi vya idadi;vivumishi vya aina hii hutoa taarifa kuhusu idadi ya nomino. Kuna vivumishi vya idadi vinavyoweza kuvumisha nomino kwa kutaja idadi ya nomino hizo kiujumla jumla bila kudhihirisha idadi halisi.
Vivumishi vya idadiambavyo huonyesha nafasi iliyochukuliwa na nomino fulani katika orodha.
Vivumishi vya kumiliki:-Ni vivumishi vinavyoonesha kuwa kitu fulani kina milikiwa na mtu au kitu kingine.
Vivumishi Vioneshi:vivumishi vya aina hii huonyesha mahali au upande kitu kilipo. Vivumishi vya aina hii hujengwa na mzizi{h}kwa vitu vilivyopo karibu na mzizi{le}kwa vitu vilivyo mbali.
Vivumishi vya kuuliza:Hivi ni vivumishi ambavyo hufafanua nomino kwa kuuliza habari zake. Hujibu swali “gani?ipi? ngapi?”
Vivumishi vya A- unganifu:Vivumishi vya aina hii huundwa kwa mzizi wa kihusishi a- unganifu. Kihusishi hiki huandamana na nomino kuunda kirai husishi ambacho huvumisha nomino iliyotajwa awali.Vivumishivya aina hii hutumika kuleta dhana za–Umilikaji, -Nafasi katika orodha.
Vivumishi vya jina kwa jina:Hizi ni nomino zinazotumika kama vivumishi ambazo hutumika kufafanua nomino
Vivumishi vya pekee:Vivumishi hivi huitwa vya pekee kwa sababu kila kimojawapo huwa na maana maalumu. Pia kila kimojawapo huchukua upatanisho wake wa kisarufi kulingana na ngeli ya nomino ambayo kinaivumisha.
Mizizi vivumishi hivi niote, o-ote, -enye, -enyewe, -ingine, -ingineo.
-ote:Huonyesha ujumla wa kitu au vitu
-o-ote:Kivumishi cha aina hii kina maana ya “kila”, “bila kubagua”
– enye:Kivumishi cha aina hii hutumika kuleta dhanna ya umilikishaji nomino fulani.
-enyewe:Kivumishi cha aina hii hutumika kuisisitiza nomino fulani.
– ingine:Kivumishi cha aina hii huonyesha/huonesha ‘tofauti na’ au ‘zaidi ya’ kitu fulani
– ingineo:Kivumishi cha aina hii hutumika kuonesha/kuonyesha ziadi.
Vielezi(E)
Vielezi ni maneno yanayofafanua vitenzi, vivumishi au vielezi vingine. Huweza kuarifu kitendo kilichotendeka kilitendeka wapi, namna gani na hata mara ngapi.
Aina za vielezi
Vielezi vya Mahali
Vielezi vya mahali hutoa habari kuhusu mahali ambapo kitendo kilifanyika. Aghalabu vielezi hivi huundwa kwa kutumia jina la mahali au kwa kuongeza kiungo -NI mwishoni mwa neno linaloashiria mahali.Kwa mfano:nyumbani, kazini, shuleni
Mfano: 1
Mtoto huyo hajatulia nyumbani tangu alipotoka Mombasa.
Msipitie sokoni mkienda kanisani.
Vielezi vya wakati
Huelezea zaidi kuhusu wakati kitendo kinapofanyika; kwa mfano: jioni, jana, asubuhi, saa saba, mwaka juzi.
Mfano: 2
Mzee Kasorogani amesema kwamba ataoga mwaka ujao
Musa alilazimishwa kuchimba mtaro saa sita usiku
Kisaka na Musa watakutana kesho
Vielezi vya Idadi
Vielezi vya idadi hutulezea kitendo kilifanyika mara ngapi.
Idadi Kamili:Vielezi vya Idadi Kamili hutaja idadi kamili ya mara ngapi kitendo kilifanyika. Kwa mfano:mara mbili, siku mbili kwa juma, mara kumi
Mfano: 3
Gibi alimzaba kofi mara tatu na kisha akakimbia
Daktari alimwagiza mama huyo achukue dawa mara tatu kwa siku na arudi hospitalini siku mbili kwa mwezi
Idadi Isiyodhihirika:Vielezi vya Idadi Isiyodhirika huelezea kiasi ambacho kitendo kilifanyika bila kutaja kiasi kamili kwa mfano:chache, nyingi, kadhaa, kidogo, wastani.
Mfano: 4
Mwizi wa kuku alipigwa mara kadhaa kabla ya kuokolewa na polisi.
Yeye hunipigia simu mara kwa mara.
Vielezi vya namna au jinsi
Vielezivya namna hii huonyesha jinsi au namna kitendo kilivyotendeka. Vielezi vya namna vipo vya aina kadhaa.
Vielezi vya namna halisi
Hivi ni vielezi vinavyotumia maneno ambayo kimsingi yana sura ya vielezi moja kwa moja katika uainishaji wa aina za maneno.
Vielezi vya namna mfanano
Hivi ni vieleziambavyo hutumika kufananisha vitendo na vivumishi au nomino mbalimbali. Hujengwa kwa kuongeza kiambishi(ki-)au kiambishi(vi-).Viambishi hivi hujulikana kwa jina la viambishi vya mfanano. Mfano; Ulifanyavizurikumsaidia mwanangu.
Vielezi vya namna vikariri
Hivi ni vielezi ambavyo hufafanua vitenzi kwa kurudiarudia neno moja mara mbili.
Vielezi vya namna hali
Hivi nivieleziambavyo hufafanua juu ya kitendo kilichotendeka kimetendeka katika hali gani.
Vielezi vya namna ala/kitumizi
Hivi ni vielezi vinavyotaja vitu ambavyo hutumika kutendea kitendo
Vielezi vya namna viigizi
Hivi vinaelezea zaidi jinsi tendo lilivyofanyika kwa kuigiza au kufuatisha sauti inayojitokeza wakati tendo linapofanyika au kutokea.
Vielezi vya wakati
Vielezivya namna hii huonyesha wakati wa kutendeka kwa kitendo.Huweza kutokea kama maneno kamili au hodokezwa kwa kiambishi{po.}
Vitenzi
Kitenzi ni neno linaloeleza jambo lililotendwa au lililotendeka. Kitenzi huarifu lililofanyika au lililofanywa na kiumbe hai chochote kinachoweza kutenda jambo
Kitenzi cha Kiswahili huundwa na mzizi pamoja na viambishi vyenye uamilifu wa aina tofauti
Aina za vitenzi
Vitenzi vikuu:Vitenzi vikuu ni vile ambavyo hubeba ujumbe muhimu wa kiarifu cha sentensi.
Vitenzi visaidizi:Hivi hutoa taarifa ya kusaidia vitenzi vikuu. Hutoa taarifa kama vile uwezekano , wakati, hali n.k.Vitenzi visaidizi daima hutumika na vitenzi vikuu, ndivyo vinavyobeba viambishi vya wakati.
Vitenzi vishirikishi: Hivi ni vitenzi vishirikishi ambavyo havichukui viambishi vya nafsi, njeo ama hali. Vitenzi vishirikishi vipungufu ni vya aina mbili, ambavyo ni kitenzi kishirikishi“ni” cha uyakinishina kitenzi shirikishi “si” si cha ukanushi.
Vitenzi vishirikishi vikamilifu:Hivi huchukuwa viambishi viwakilishi vya nafsi, njeo na hata hali. Kwa mfano;ndiye, ndio, ndipo.
Kazi za kitenzi kikuu
Kueleza tendo linalofanywa na mtenda/mtendwa.
Kuonyesha wakati tendo linapotendeka
Kuonyesha hali ya tendo
Kuonyesha nafsi
Kuonyesha kauli mbali mbali za tendo
Kuonyesha urejeshi wa mtenda/mtendwa/ mtendewa/ kujitendea
Kazi za kitenzi kishirikishi
Kushirikisha vipashio vingine katika sentensi
Kuonyesha tabia fulani iliyopo au isiyokuwepo ya mtu fulani au kitu fullani.
Kuonyesha cheo au kazi anayofanya mtu.
Kuonyesha sifa za mtu.
Kuonyesha umoja wa vitu au watu
Kuonyesha mahali
Kuonyesha msisitizo
Kuonyesha umilikishi wa kitu chochote.
Aina za wakati katika kitenzi
Wakati uliopita
Wakati uliopo
Wakati ujao
Hali mbalimbali za kitenzi
Hali ya masharti
Hali ya kuendelea kwa tendo
Hali ya kutarajia, kuamuru na kuhimiza
Viwakilishi
Viwakilishi ni aina ya neno linaloweza kutumika badala ya jina/nomino .
Aina za viwakilishi
Viwakilishi vioneshi au viwakilishi vya kuonesha:Viwakilishi vionyeshi hutumika badala ya nomino kwa kutumia kuonyesha nomino inayorejelewa bila kuitaja. Kwa mfano; huyu, yule, hapo, kule, humo. Huyu si mwenzetu kabisa; kule hakufai kwenda watoto.
Viwakilishi vya nafsi: Kwa mfano:mimi, wewe, yeye, sisi, nyinyi, wao
Viwakilishi vya kuuliza/viwakilishi viuliziambavyo huashiriwa na mofu /kiambishi{-pi}ambavyo katika tungo hutanguliwa na kiambishi ngeli cha jina husika. Kwa mfano, Wangapi wameondoka? Kipi kimekosewa?
Wiwakilishi vya urejeshiambavyo vinajengwa na shinaambapamoja na vipande vidogo vidogo –ye-, -o-, -cho-, vyo, lo, po, mo, kon.k ambavyo vinachaguliwa kulingana na ngeli ya majina yanayorejeshwa navyo. Mfano; aliyeondoko hatapewa chake.
Viwakilishi vya idadi:Viwakilishi hivi hutuarifu kuhusu idadi ya nomino hiyo huweza kuwa kamili (halisi) au ya jumla.
Viwakilishi vya pekee/vimilikishi:-Hivi ni aina ya vivumishi vya pekee kuwakilisha nomino. Hufuata sheria za upatanisho za nomino zinazowakilishwa. Mfano; '-angu, -ako, -ake, -etu, -enu, -ao '. kwangu haingii megini, chako haikna thamani.
Viwakilishi vya A-unganifu:- Viwakilishi hivi huundwa kwa kihusishi chaA-unganifukusimamia nomino iliyomilkiwa, inayochukuwa nafasi fulani katika orodha au nomino ya aina fulani. Kihusishi a-unganifu huandamana na nomino kuunda kirai husishi ambacho husimama mahali pa nomino. Mfano;ya kwakeyamemshinda,vya wazeehaviguswi.
Viwakilishi vya sifa:Haya ni maneno ya sifa ambayo huchukua nafasi ya nomino katika setensi. Kwa mfano -eupe, -janja, -tamu
Viwakilishi vya Idadi;Idadi Kamili- hutumia namba kuelezea idadi ya nomino. 'saba, mmoja, ishirini' -Hutumika kusimama badala ya nomino kwa kurejelea idadi yake. Idadi Isiyodhihirika- huelezea kiasi cha nomino kwa ujumla, bila kutaja idadi kamili: 'chache, nyingi, kadhaa, kidogo, wastani'
Viunganishi
Ni maneno, kikundi cha maneno au kiambishi chenye kuunganisha maneno, kirai, kishazi au sentensi.Dhima ya kiunganishi ni kuunga vipashio viwili au zaidi vyenye hadhi sawa kisarufi.
Aina za viunganishi
Viunganishi huru:hivi ni viunganishi vinavyosimama pekee katika tungo, katikati ya vipashio vinavyoungwa.Viunganishi huru hujumuisha:
Viunganishi nyongeza/vya kuongeza, kama vile, na, pia, pamoja. Baba na mwanae wanacheza mpira, Alichukua chakula chote pamoja na akiba iliyokuwepo.
Viunganishi vya sababu/visababishi, mfano, kwa sababu, kwa kuwa, kwa vile, madhali, ili. Alimsogelea karibu ila ambusu, Atatumikia kifungo madhali amebainika kuwa na hatia.
Viunganishi vya uteuzi/chaguo. Mfano; au, Naweza kwenda nyumani au shuleni.
Viunganishi vya kutofautisha/vya kinyume:ila, lakini, kinyume na, japokuwa, ingawa, ilihali. Mfano; Mkumbatie lakini usimbusu.
Viunganishi vya wakati.Wakati mfano; Mwalimu aliuliza swali wakati yeye amesinzia.
Viunganishi vya masharti;ikiwa, iwapo, hadi. Mfano; utaruhusiwa kuingia hapa ikiwa umevaa mavazi yanaostahili.
Viunganishi vihusishi; miongoni mwa, kati ya; mfano: Jane alikuwa miongoni mwa washindi kumbi bora kitaifa.
Viunganishi tegemezi:ni viambishi ambavyo hutiwa katika kitenzi cha kishazi tegemezi ili kukiunga na kitenzi kikuu cha kishazi huru ambavyo kwa pamoja huunda sentensi changamano au shurtia. Mfano; -po-, -cho-, -o- Nili-po-amka…, Ali-cho-mwelez…, alizo-o-neshwa…n.k
Vihusishi
Ni maneno ambayo huonyesha uhusiano uliopo baina ya neno moja na jingine. Vihusishi aghlabu huonyesha uhusiano kati ya nomino au kirai nomino na maneno mengine.
Mambo yanayoweza kuonyeshwa na vihusishi
Huonyesha uhusiano wa kiwakati; Mfano, ni vizuri kupiga mswakibaada yachakula.
huonyesha uhusiano wa mahali: mfano, Ninaishikaribu nakwa Mtogole
huonyesha uhusiano wa kulinganisha: Amekulazaidi yauwezo wake.
huonyesha uhusiano wa umilikaji: Usiguse hicho kitabu nicha kwangu
huonyesha uhusiano wa sababu/kiini: nimerudi kwaajili yakuonana na mkuu wa shule.
Aina za vihusishi
vihusishi vya wakati
vihusishi vya mahali
vihusishi vya vya kulinganisha
vihusishi vya sababu
vihusishi vya ala/kifaa mfano; -kwa
vihusishi vimilikishi
vihusishi vya namna; Kichwacha mviringo
vihusishi ‘na’ cha mtenda mfano, amepigwana Juma.
Matumizi ya kihusishi “kwa”
huonyesha mahali au upande: Mfano, amekwenda kwa mjomba wake.
huonyesha sababu au kisababishi cha jambo: mfano; ninaishi kwa ajili yako.
huonyesha wakati: mfano; sina nafasi kwa sasa.
huonyesha sehemu fulani ya kitu kikubwa, mfano: Mpira umekwisha wakiwa wamefungana nne kwa tatu.
huonyesha jinsi kitendo kilivyotendeka: Mfano; alimvuta kwa nguvu sana ndo maana limevunjika.
Vihisishi/Viingizi
Ni maneno ambayo hutumiwa kuwakilisha hisia fulani.
Vihusishi vinaweza kugawanywa katika makundi yafuatayo:
Vihisishi vinavyoonyesha mhemko au hisi kali
vihisishi vya furaha
vihisishi vya huzuni
vihisishi vya mshituko
vihisishi vya mshangao
Vihisishi vya maamrisho au msisitizo wa jambo au tukio
vihisishi vya maadili
vihisishi vya mwiitiko
vihisishi vya ombi
vihisishi vya bezo
vihisishi vya kutakia heri
vihisishi vya kukiri afya/jambo
vihisishi vya kiapo
vihisishi vya salamu
ZOEZI
Kuna aina ngapi za vitenzi katika lugha
ya Kiswahili?
A
Tatu
B
Sita
C
Tano
D
Nne
___ni maneno yanayoonyesha kuwapo
kwa hali au tabia kwa mtu au vitu.
A
Vitenzi vikuu
B
Vitenzi visaidizi
C
Viunganishi huru
D
Vitenzi vishirikishi
Ni aina gani ya vivumishi vinavyoonesha
ujirani au umbali wa kitu au mtu?
A
Vivumishi vionyeshi
B
Vivumishi vya idadi
C
Vivumishi vya sifa
D
Vivumishi viulizi
Ni aina gani ya maneno yanapoandikwa
hufuatiwa na alama ya mshangao?
A
Vihisishi
B
Viwakilishi
C
Vihusishi
D
Vitenzi
___ni aina ya maneno yanayotaja watu
au vitu katika makundi.
A
Nomino za kawaida
B
Nomino za jamii
C
Nomino za pekee
D
Nomino dhahani
Matumizi ya Aina za Maneno katika Tungo
Elezea matumizi ya aina za maneno katika tungo
Aina za maneno hutumika katika tungo kwa kutegemeana na lengo la msemaji. Kwa mfano kama lengo la msemaji ni kuonesha aina fulani ya hisia atatumia vihisishi katika tungo yake. Vilevile kama msemaji anahitaji kueleza kuhusu namna nomino inavyotenda, ilivyotendewa au inavyotendwa, atatumia kitenzi.
ETIMOLOJIA YA NENO ' ALHAMISI'.
Alhamisi, katika Lugha ya Kiswahili) ni neno (nomino) lenye maana ya siku ya nne ya wiki kuanzia Jumatatu, siku ya wiki iliyopo baina ya Jumatano na Ijumaa.
Neno hili (Alhamisi) asili yake ni Kiarabu na huko ni 'Alkhamiis الخميس ' neno ambalo mzizi wake ni *nomino ya Kiarabu* *khams* (namba tano #5).
Katika Lugha ya Kiarabu neno (Alkhamiis) lina maana zifuatazo:
1. Sehemu ya tano, moja ya Tano.
2. Siku moja katika wiki, siku ya tano ya wiki kuanzia siku ya Jumapili ambayo Waarabu wanaiita *Al-Ahad* (Siku ya Kwanza).
3. Jeshi lenye idadi kubwa ya wanajeshi, huitwa pia kwa Kiarabu *Al-Jayshu* *Al-Jarrar* *الجيش* *الجرار*. Tunaweza kuliita Jeshi la Pembe Tano kwa kuwa jeshi hili huwa na vikosi vitano: Kikosi cha Mbele, Kikosi cha Kati, Kikosi cha Kulia, Kikosi cha Kushoto na Kikosi cha Nyuma.
4. (Kwa watu) Mkusanyiko wa watu *Khamisun* *Naas* *خميس* *الناس*
5. (Kwa nguo na vitu vingine) ni kile chenye urefu wa dhiraa tano.
Neno hili 'Alkhamiis' lilipoingia katika Lugha ya Kiswahili na kutoholewa na kusanifiwa kuwa (Alhamisi) limejifunga na maana moja tu: siku ya wiki iliyopo baina ya Jumatano na Ijumaa.
Kutumika neno hili (Alhamisi) tunaloweza kulifasiri ' *siku ya tano'* kunafanya ulimwengu wa Kiswahili kuwa na siku mbili ziitwazo 'siku ya tano': siku moja kwa neno lenye asili ya Kibantu (Jumatano) na siku nyingine kwa neno lenye asili ya Kiarabu (Alhamisi/Alkhamis).
Nakusudia kusema kuwa Waswahili wameanza kuhesabu siku za wiki Jumamosi na Waarabu wameanza kuhesabu siku za wiki Jumapili. Muachano huo ndio ulioleta Jumatano (Siku ya 5 ya wiki) na Alhamisi (Siku ya 5 ya wiki).
*Shukran sana.*
Sarufi ya Kiswahili na sintaksia ni kozi inayochambua sarufi ya Kiswahili kwa kuzingatia nadharia za kisintaksia kama zilivyoasisiwa na wanazuoni wa isimu. Sintaksia ni tawi la isimu linalohusu mpangilio na mfuatano wa vipashio vya lugha katika kuunda tungo za darajia mbalimbali, huchunguza mathalan namna maneno yanavyounda virai na sentensi za Kiswahili. Sintaksia inahusu tungo za lugha ambazo zaweza kuwa ni maneno, virai, vishazi na sentensi. Japokuwa neno ni kipashio cha kiumbo, linasadifu kuingia katika sintaksia ya lugha kwani lenyewe lina muundo wake unaotokana na viambajengo vinavyoliunda ambavyo ni mzizi na viambishi.
Baada ya ufafanuzi huo kwa kifupi sasa unakaribishwa kwenye somo lenyewe. Ni imani yangu kuwa utalifurahia na kulipenda na hatimaye kulifaulu vizuri somo hili.
MAANA YA LUGHA NA SARUFI
Lugha ni nini?
Dhanna ya lugha ni pana sana, hata hivyo kimuundo lugha inafafanuliwa kama “Mfumo wa sauti za nasibu zinazotumiwa na watu ili kupashana habari.”
Hammerley, 1982:26 anasema; Lugha ni mfumo wa mawasiliano wenye ishara za kinasibu, mfumo ambao ni tata, kamilifu na unaobadilika. Mfumo huo humudiwa na hutumiwa na wanajamii wenye utamaduni maalumu.
Kutokana na fasili hiyo tunapata mambo saba ya msingi kuhusu lugha:
Lugha ni kamilifu; Lugha ni kamilifu kwa kuwa inahimili matakwa ya jamii kimawasiliano. Kila jamii hutosheka inapotumia lugha yake kuelezea hisia zake kisiasa, kiutamaduni na kiuchumi pamoja na matakwa mengine ya kijamii. Panapotokea dhanna mpya lugha hujiongezea msamiati kwa njia mbalimbali.
Lugha ni tata; Kisintaksia lugha ni tata kwa sababu inaundwa na vipashio vidogo ambavyo huweza kubainishwa katika viwango mbalimbali kama vile; fonimu ambazo huunda mofimu, mofimu huunda maneno, maneno huunda virai, virai huunda vishazi na vishazi huunda sentensi.
(d) Fonimu 18: M + t + o + t + o + a + n + a + o + m +
b + a +m + a + z + i + w + a
Vipashio vyote hapo juu hushonana kwa kanuni maalumu
ambazo hutofautiana kati ya lugha na lugha.
Lugha hubadilika; Lugha hupokea mabadiliko kulingana na mahitaji ya jamii kwa wakati husika. Baadhi ya maneno hutoweka katika matumizi na misamiati mipya huibuka na mingine hubadili maana ya awali.
Lugha ina mfumo; Lugha ni matokeo ya mfumo ambao hujibainisha katika kiwango cha muundo na pia maana.
(i) Kiwango cha muundo (sintaksia); Lugha ina utaratibu maalumu wa mfuatano wa maneno (mofolojia) na mshonano wa sauti (fonolojia). Katika kiwango hiki mpangilio wa vipashio husimamiwa katika namna inayokubalika ili vilete maana inayokubalika au iliyokusudiwa.
Mfano: – Mdogo baba analima shamba (sio
sahihi)
– Baba mdogo analima shamba (sahihi)
(ii) Kiwango cha maana; Kiswahili kwa mfano kina namna ya kupambanua maana za maneno kwa njia mbalimbali. Mathalan Upambanuzi wa maneno kwa njia ya kutoa maana iliyo kinyume cha maneno ya awali.
Lugha hasa ni ya mazungumzo; Uasilia wa lugha ni mazungumzo tangu mwanadamu alipoanza kutumia lugha kuwasiliana. Lugha hutegemea sauti za kutamkwa toka kinywani mwa mwanadamu kwa kutumia ala za sauti. Lugha ya mazungumzo maneno yake hubeba maana nyingi na pana sana kuliko yakiwa katika maandishi. Ni dhahiri kuwa maandishi ni namna tu ya kuwasilisha yale yote yaliyo katika mazungumzo. Wapo watu wengi ambao humudu lugha ya mazungumzo lakini hawawezi kuandika lugha hizo.
Lugha humudiwa/hufunzwa; Pamoja na ukweli kwamba kila mtu anapozaliwa huzaliwa na uwezo wa kumudu lugha, uwezo huo ni sawa na uwezo mwingine tu kama kuendesha gari, kunyonya, kutambaa au kutembea. Kila mwanadamu hupaswa kutumia uwezo alionao kujifunza na kuimudu lugha yake kama ilivyo kwa mambo mengine. Juhudi hizi huanzia pale mtu anapojifunza lugha yake ya kwanza katika jamii inayomzunguka.
– Baada ya kumudu lugha ya kwanza mtu huyo huweza kujifunza lugha ya pili akiwa shuleni au kupitia njia zozote za mawasiliano.
Lugha hufungamana na utamaduni wa jamii; Kila lugha hueleza mambo yanayoihusu jamii yake kwa wakati wote wa historia ya jamii hiyo. Hivyo lugha na utamaduni ni vitu visivyoweza kutenganishwa. Kwa mantiki hii kumbe kuijua lugha kunahitaji ujuzi wa utamaduni wa wanalugha husika. Hii ni kwa sababu maneno ya lugha hubeba vionjo vya wanalugha na huambatana na ishara na maana mbalimbali zinazofungamana na utamaduni wa jamii husika.
Kwa mfano:
– Mchele kwa mswahili
– Migomba kwa mchaga/mhaya
– Samaki kwa mpare,n.k
LUGHA KAMA MFUMO BUNIFU
Uwezo wa kuimudu lugha uko katika sehemu ya ubongo na hushamirishwa na jamii ya wazungumza lugha ambao humsaidia mtu kuimarisha uwezo huo. Kuimarika uwezo wa kumudu lugha huongezeka kutokana na ujuzi anaoupata mwanadamu katika harakati za kupambana na mazingira yanayomzunguka.
Kila mtumia lugha hubuni lugha inayokidhi mazingira fulani. Hivyo lugha hubuniwa wakati wote na ubunifu huu hutofautiana kati ya lugha moja na ingine.
Katika mifano hiyo msemaji ametumia mbinu gani kuunda msamiati huo?
DHANNA YA SARUFI
Sarufi ni mfumo wa taratibu na kanuni zinazomuongoza mtumiaji wa lugha ili aweze kuitumia lugha yake kwa usanifu na ufasaha.
Ni uwezo wa wazungumzaji wa lugha kuunda na kufasili kanuni za usahihi au kutokuwa sahihi kwa maneno au sentensi za lugha yao. Sarufi kwa ujumla inajumuisha vipengele vya lugha kama vile: fonetiki, fonolojia, mofolojia, sintaksia na semantiki.
SIFA ZA JUMLA ZA KISARUFI
Lugha zote zina sarufi; kila lugha duniani inatawaliwa na sarufi ingawa sarufi za lugha hutofautiana.
Mfano:
Kiingereza
The two boys now see several dogs
This boy is incredible
Kiswahili
Boys two see now dogs several
Vijana wawili sasa wanaona mbwa wengi
Boys two see dogs several
Sasa vijana wawili wanaona mbwa wengi
This boy is incredible
Huyu kijana ni mkorofi (sio sahihi)
Kijana huyu ni mkorofi (sahihi)
Kwa mifano hiyo ni dhahiri kuwa kila lugha ina sarufi yake na haiwezekani sarufi ya lugha fulani ikawa ndio msingi wa sarufi za lugha nyingine.
Sarufi za lugha hufanana; sarufi za lugha hufanana ingawa ndani ya lugha moja jambo fulani huweza kuelezwa kwa namna tofauti. Utofauti huo haumaanishi namna fulani ni bora zaidi ya ingine. (rejelea mifano ya hapo juu).
MUHADHARA WA KUMI : AINA ZA MANENO NA UAINISHAJI WAKE
Nomino
Maana ya Nonimo :
Nomino ni istilahi inayopewa maneno yanayotaja vitu, hali, mahali au viumbe ili kuviainisha na kuvitofautisha.
Aina za nomino:
Nomino za pekee: Nomino za pekee hutaja na kutambulisha nomino mahsusi na za kipekee. Yaani kuwa kitu ni hicho na wala si kingine chochote. Hizi ni nomino zinazohusisha majina kama vile ya watu, nchi, miji, mito, milima, maziwa na bahari. Herufi za kwanza za nomino za pekee huwa kubwa hata kama nomino hiyo inapatikana katikati ya sentensi.
Nomino za kawaida: Hizi kwa jina lingine huitwa nomino za jumla. Nomino hizi hazibainishi waziwazi vitu ambavyo habari zake zinatolewa. Kwa mfano ikiwa ni mtu, mahsusi hatambuliwi. Haituambii kama ni Kelvin, Aisha ama Zawadi. Ikiwa ni ziwa halitambuliwi kama ni Tanganyika, Viktoria au Nyasa, yaani hutaja vitu bila kutaja umahususi wake kama ilivyo katika nomino za pekee. Nomino Hizi zinapoandikwa si lazima zianze kwa herufi kubwa isipokuwa zimetumiwa mwanzoni mwa sentensi au zimetumika kama anuani ya kutajia kitu kama vile Mkuu wa Sheria. Katika mfano huu ‘sheria’ kwa kawaida ni nomino ya kawaida, lakini hapa inaanza kwa herufi kubwa kwani inataja anuwani ya kipekee.
Nomino za jamii: Hizi ni nomino ambazo zinawakilisha vitu vingi katika jina moja, yaani nimino zinazotaja umla wa vitu vingi.
Nomiono dhahania: Kundi hili hubeba nomino ambazo zipo kwa kudhani tu. Nomino hizi hutaja vitu, viumbe au hali ambazo hazishikiki wala kuonekana. Mf. Mungu, shetani, malaika, upendo, uchoyo, hasira, peponi, n.k
Nomino za kitenzi jina: Hizi ni nomino zinazohusu vitenzi. Huundwa kwa kuongezwa kiambishi {ku-} cha unominishaji kwenye mzizi wa kitenzi cha kitendo halisi ili kukifanya kiwe nomino.
Nomino za wingi: Hizi hutaja vitu katika wingi japo vitajwa havina umoja wala wingi. Mf. Maji, manukato, mapenzi, mawasiliano, n.k
Vivumishi
Maana ya kivumishi:
Vivumishi ni maneno yanayofanya maneno mengine yavume. Vivumishi huvumisha kuhusu sifa, idadi, mahali, n.k kuhusu nomino.
Aina za vivumishi.
Vivumishi vya sifa: hutoa sifa za nomino /kiwakilishi cha nomino. Sifa hizi huweza kuwa nzuri, mbaya au yoyote ile.
Vivumishi vya idadi: vinaweza kujitokeza katika aina tatu ndogondogo.
Vivumishi vya aina hii hutoa taarifa kuhusu idadi ya nomino ambazo kiwango chake kimetajwa.
Vivumishi vya idadi vinavyoweza kuvumisha nomino kwa kutaja idadi ya nomino hizo kiujumlajumla bila kudhihirisha idadi halisi.
Vivumishi vya idadi ambavyo huonesha nafasi iliyochukuliwa na nomino fulani katika orodha.
Vivumishi vya kumiliki:- Ni vivumishi vinavyoonesha kuwa kitu fulani kinamilikiwa na mtu au kitu kingine.
Vivumishi Vioneshi:- vivumishi vya aina hii huonesha mahali au upande kitu kilipo. Vivumishi vya aina hii hujengwa na mzizi {h} kwa vitu vilivyopo karibu na mzizi {le} kwa vitu vilivyo mbali.
Vivumishi vya kuuliza Hivi ni vivumishi ambavyo hufafanua nomino kwa kuuliza habari zake. Hujibu maswali kama “gani? ipi? ngapi?”
Vivumishi vya pekee: Vivumishi hivi huitwa vya pekee kwa sababu kila kimojawapo huwa na maana maalumu. Pia kila kimojawapo huchukua upatanisho wake wa kisarufi kulingana na ngeli ya nomino ambayo kinaivumisha. Mizizi ya vivumishi hivi ni ote, o-ote, -enye, -enyewe, – ingine, -ingineo. –ote. Huonesha ujumla wa kitu au vitu -o-ote Kivumishi cha aina hii kina maana ya “kila”, “bila kubagua” – enye Kivumishi cha aina hii hutumika kuleta dhanna ya umilikishaji nomino fulani. – enyewe Kivumishi cha aina hii hutumika kuisisitiza nomino fulani. – ingine Kivumishi cha aina hii huonesha ‘tofauti na’ au ‘zaidi ya’ kitu fulani – ingineo Kivumishi cha aina hii hutumika kuonesha/kuonesha ziadi.
Vivumishi vya A- unganifu Vivumishi vya aina hii huundwa kwa mzizi wa kihusishi a- unganifu. Kihusishi hiki huandamana na nomino kuunda kirai husishi ambacho huvumisha nomino iliyotajwa awali. Vivumishi vya aina hii hutumika kuleta dhanna zifuatazo:- -Umilikaji -Nafasi katika orodha
Vivumishi vya jina kwa jina huwa ni nomino zinazotumika kama vivumishi ambazo hutumika kufafanua nomino ingine.
Vielezi
Maana ya vielezi:
Vielezi ni maneno yanayofafanua vitenzi, vivumishi au vielezi vingine. Huweza kuarifu kitendo kilichotendeka kilitendeka wapi, namna gani na hata mara ngapi?
Aina za vielezi
Vielezi vya namna au jinsi. Vielezi vya namna hivi huonesha jinsi au namna kitendo kilivyotendeka. Vielezi vya namna vipo vya aina kadhaa.
Vielezi vya namna halisi. Hivi ni vielezi vinavyotumia maneno ambayo kimsingi yana sura ya vielezi moja kwa moja katika uainishaji wa aina za maneno.
Vielezi vya namna. Hivi ni vielezi ambavyo hutumika kufananisha vitendo na vivumishi au nomino mbalimbali. Hujengwa kwa kuongeza kiambishi (ki-) au kiambishi (vi-). Viambishi hivi hujulikana kwa jina la viambishi vya mfanano. Ulifanya vizuri kumsaidia mwanangu. -Vielezi vya namna vikariri, hivi ni vielezi ambavyo hufafanua vitenzi kwa kurudiarudia neno moja mara mbili. – Vielezi vya namna hali, Hivi ni vieelezi ambavyo hufafanua juu ya kitendo kilichotendeka kimetendeka katika hali gani. – Vielezi vya namna ala/kitumizi Hivi ni vielezi vinavyotaja vitu ambavyo hutumika kutendea kitendo. – Vielezi vya namna viigizi. Hivi vinaelezea zaidi jinsi tendo lilivyofanyika kwa kuigiza au kufuatisha sauti inayojitokeza wakati tendo linapofanyika au kutokea.
Vielezi vya idadi: hivi huonesha kuwa kitendo kilitendeka mara fulani au kwa kiasi fulani.
Vielezi vya mahali. Vielezi vya namna hii huonesha mahali ambapo kitendo kinatokea.Huweza kudokezwa kwa viambishi au kwa maneno kamili.
Vielezi vya wakati: Vielezi vya namna hii huonesha wakati wa kutendeka kwa kitendo.Huweza kutokea kama maneno kamili au kudokezwa kwa kiambishi {po.}
Vitenzi
Maana ya vitenzi:
Kitenzi ni neno linaloeleza jambo lililotendwa au lililotendeka. Kitenzi huarifu tendo lililofanyika au lililofanywa na kiumbe hai chochote kinachoweza kutenda jambo.
Muundo wa kitenzi cha Kiswahili
Kitenzi cha Kiswahili huundwa na mzizi pamoja na viambishi vyenye uamilifu wa aina tofauti.
Aina za vitenzi
v Vitenzi halisi: Hivi ni vitenzi ambavyo huonesha kutendeka kwa kitendo.Wakati mwingine vitenzi hivi huitwa vitenzi vya kutenda.
vitenzi elekezi: Hivi ni vitnzi vya ambavyo vinaweza kuchukuwa kitendwa/kitendewa (Yambwa/Yambiwa). Muundo wake unadokeza kuwa, kuna kitendwa au kitu kinachoelezea tendo hilo.
vitenzi sielekezi: Hivi ni vitenzi ambavyo havichukuwi kitendwa/kitendewa (Yambwa/Yambiwa). Muundo wake haudokezi uwezekano wa kuwepo kwa yambwa/yambiwa. Tendo halielekezwi kwa yeyote.
Aina za vitenzi halisi
v Vitenzi vikuu: Vitenzi vikuu ni vile ambavyo hubeba ujumbe muhimu wa kiarifu cha sentensi.
v Vitenzi visaidizi: Hivi hutoa taarifa ya kusaidia vitenzi vikuu. Hutoa taarifa kama vile uwezekano, wakati, hali n.k. Vitenzi visaidizi daima hutumika na vitenzi vikuu, ndivyo vinavyobeba viambishi vya wakati.
v Vitenzi vishirikishi: Hivi ni Vitenzi vishirikishi ambavyo vilevile sielekezi. Vitenzi hivi hufanya kazi ya kuunga sehemu mbili za sentensi.
Aina za vitenzi vishirikishi
Vitenzi vishirikishi vipungufu: Hivi ni vitenzi vishirikishi ambavyo havichukui viambishi vya nafsi, njeo ama hali. Vitenzi vishirikishi vipungufu ni vya aina mbili, ambavyo ni kitenzi kishirikishi “ni” cha uyakinishi na kitenzi shirikishi “si” cha ukanushi.
Vitenzi vishirikishi vikamilifu: Hivi huchukuwa viambishi viwakilishi vya nafsi, njeo na hata hali.
Kazi za kitenzi kikuu:
kueleza tendo linalofanywa na mtenda/mtendwa.
kuonesha wakati tendo linapotendeka
kuonesha hali ya tendo
Kuonesha nafsi
kuonesha kauli mbalimbali za tendo
Kuonesha urejeshi wa mtenda/mtendwa/ mtendewa/ kujitendea
Kazi za kitenzi kishirikishi
kushirikisha vipashio vingine katika sentensi
Kuonesha tabia fulani iliyopo au isiyokuwepo ya mtu fulani au kitu fullani.
Kuonesha cheo au kazi anayofanya mtu.
kuonesha sifa za mtu.
kuonesha umoja wa vitu au watu
kuonesha mahali
kuonesha msisitizo
kuonesha umilikishi wa kitu chochote.
Aina za wakati katika kitenzi.
wakati uliopita
wakati uliopo
wakati ujao
Hali mbalimbali za kitenzi
– Hali ya masharti
– Hali ya kuendelea kwa tendo
– kuamuru na kuhimiza n.k
Viwakilishi
Maana ya kiwakilishi:
kiwakilishi neno linaloweza kutumika badala ya jina. Hutokea nafasi ya nomino pindi nomino inapokosekana.
Aina za viwakilishi
Viwakilishi vioneshi/mahali
Mf. Zile,yule,kule,
Viwakilishi vya nafsi ambavyo vipo vya aina tatu; ambavyo ni:
Viwakilishi vya kuuliza/viwakilishi viulizi ambavyo huashiriwa na mofu/kiambishi {-pi} ambavyo katika tungo hutanguliwa na kiambishi ngeli cha jina husika.
Viwakilishi vya urejeshi ambavyo vinajengwa na shina -amba- pamoja na vipande vidogovidogo kama –ye-, -o-, -cho-, vyo, lo, po, mo, ko n.k ambavyo vinachaguliwa kulingana na ngeli ya majina inayorejeshwa navyo.
Viwakilishi vya idadi: Viwakilishi hivi hutuarifu kuhusu idadi ya nomino, idadi hiyo huweza kuwa kamili (halisi) au ya jumla.
Viwakilishi vya pekee: Hivi ni aina ya vivumishi ambavyo huwakilisha nomino kwa umaalumu wake. Hufuata sheria za upatanisho za nomino zinazowakilishwa.
Viwakilishi vya A-unganifu: Viwakilishi hivi huundwa kwa kihisishi cha A-unganifu kusimamia nomino inayomilikiwa, inayochukuwa nafasi fulani katika orodha au nomino ya aina fulani. kihisishi a-unganifu huandamana na nomino kuunda kirai husishi ambacho husimama mahali pa nomino.
Viwakilishi vya sifa; Haya ni maneno ya sifa ambayo huchukua nafasi ya nomino katika setensi.
Viunganishi
Maana ya viunganishi. Ni maneno, kikundi cha maneno au kiambishi chenye kuunganisha maneno, kirai, kishazi au sentensi. Dhima ya kiunganishi ni kuunga vipashio viwili au zaidi vyenye hadhi sawa kisarufi.
Aina za viunganishi:
v viunganishi huru: hivi ni viunganishi vinavyosimama pekee katika tungo, katikati ya vipashio vinavyoungwa.
Aina za viunganishi huru
Viunganishi nyongeza/vya kuongeza mf. Tena, Na, Zaidi ya n.k.
Viunganishi vya sababu/visababishi Mfano; Kwa kuwa, kwa sababu, kwa vile, kutokana na, n.k.
Viunganishi vya uteuzi/chaguo Mfano; Ingawa, Japokuwa, Lakini n.k.
Viunganishi linganishi/vya kinyume Mfano; Ingawa, Japokuwa, Lakini n.k.
Viunganishi vya wakati Mfano; kisha, baadaye, Halafu, Baada ya n.k.
Viunganishi vya masharti Mfano; Kama, Ikiwa, Iwapo n.k
Viunganishi vihusishi Mfano; Cha, La, Wa, Za n.k.
v Viunganishi tegemezi: ni viambishi ambavyo hutiwa katika kitenzi cha kishazi tegemezi ili kukiunga na kitenzi kikuu cha kishazi huru ambavyo kwa pamoja huunda sentensi changamano au shurtia. Mfano; -ye-, -po-, -ki-, -cho- na -nge-.
Vihusishi: Ni maneno ambayo huonesha uhusiano uliopo baina ya neno moja na lingine. Vihusishi aghalabu huonesha uhusiano kati ya nomino au kirai nomino na maneno mengine.
Mambo mbalimbali yanayoweza kuoneshwa na vihusishi
huonesha uhusiano wa kiwakati
huonesha uhusiano wa mahali
huonesha uhusiano wa kulinganisha
huonesha uhusiano wa umilikaji
huonesha uhusiano wa sababu/kiini
Aina za vihusishi
vihusishi vya wakati Mfano; kabla ya, baada ya n.k
vihusishi vya mahali Mfano; chini ya, juu ya, ndani ya, mbele ya n.k.
vihusishi vya ulinganishi/ vya kulinganisha Mfano; kuliko, zaidi ya n.k.
vihusishi vya sababu/ kusudi/nia Mfano; kwa sababu ya, kwa ajili ya n.k.
vihusishi vya ala (kifaa) Mfano; kwa
vihusishi vimilikishi Mfano; cha, za n.k
vihusishi vya namna/jinsi/hali Mfano; moto wa kuotea mbali, macho yamviringo
vihusishi ‘na’ cha mtenda
Matumizi ya ziada ya kihusishi “kwa”
kihusishi hiki huonesha mahali au upande
kihusishi hiki huonesha sababu au kisababishi cha jambo
kihusishi hiki huonesha wakati
kihusishi hiki huonesha sehemu fulani ya kitu kikubwa
kihusishi hiki hutumika kuonesha ‘nia ya pamoja na’
Kihusishi hiki huonesha jinsi kitendo kilivyotendeka
Viingizi/Vihisishi: Ni maneno ambayo hutumiwa kuwakilisha hisia fulani. Maneno haya huwa na alama ya mguso yatokeapo katika maandishi.
Aina za viingizi:
Viingizi vinaweza kugawanywa kwa kutumia vigezo vya kisemantiki. Mkabala huu unatumika kuvigawa viingizi kulingana na maana zinazowakilishwa na viingizi husika. Maana hizo ni hisia zinazobebwa na viingizi hivyo.
v Viingizi vinavyoonesha mhemko au hisiya kali
viingizi vya furaha
viingizi vya huzuni
viingizi vya mshituko
viingizi vya mshangao
v Viingizi vya maamrisho au msisitizo wa jambo au tukio.
Posted by: MwlMaeda - 12-01-2021, 08:12 AM - Forum: Nukuu
- No Replies
MUHADHARA WA NANE : FONOLOJIA ARUDHI
Fonolojia Arudhi
Maana ya fonolojia arudhi
Hizi ni sifa za kimatamshi zinazoambatanishwa kwenye sauti za lugha ya mwanadamu, sifa hizi huitambulisha sauti kimatamshi zaidi na husaidia kubainisha taarifa za msingi kama hali ya msemaji, hisiya za msemaji, umbali, n.k
Matamshi:
Kifonolojia matamshi ni utaratibu maalum utumikao katika utoaji wa sauti za maneno ya lugha ya binadamu. Matamshi huhusu lugha za wanadamu peke yake.
Utaratibu wa matamshi ya sauti za lugha huzingatia mambo mawili: Mahali pa matamshi, yaani sehemu katika mkondo wa utamkaji wa sauti mbalimbali ambapo sauti fulani hutamkwa. Jambo la pili ni jinsi ya matamshi yaani namna ambavyo sauti fulani hutolewa.
Lafudhi
Lafudhi ni matamshi ya msemaji wa lugha fulani ambayo yanatokana na athari za kimazingira.
Mazingira hayo yanaweza kuwa eneo atokalo mtu, mahali alikosomea, au kiwango chake cha elimu
Shadda/mkazo
Ni utaratibu wa utamkaji wa maneno ambapo silabi fulani hutamkwa kwa nguvu nyingi zaidi kuliko ilivyo katika silabi nyingine za neno hilohilo.
Mkazo unaweza kuchukuliwa kama kilele cha kupanda na kushuka kwa sauti katika utamkaji wa neno.
Silabi yenye mkazo inakuwa na msikiko mzito zaidi kuliko silabi nyingine za neno hilohilo.
Lugha nyingi hasa za kibantu hazitumii mkazo, Lugha nyingi hutumia toni. Kiswahili sanifu hakitumii toni na zaidi hutumia mkazo.
Kidatu:
Kidatu kina maana ya kiwango cha sauti isikikayo, wakati wa utamkaji ama kuwa juu, kuwa katikati au kuwa chini.:
Kiimbo
Ni utaratibu maalum wa upandaji na ushukaji wa mawimbi ya sauti unaojitokeza katika utamkaji wa lugha fulani.
Katika utaratibu wa utamkaji dhanna ya Kiimbo huandamana pia na dhanna ya kidatu (yaani, kiwango cha juu, cha kati au cha chini cha sauti katika usemaji), Kwa hivyo ni muhimu hapa kueleza tofauti zilizopo baina ya kiimbo na kidatu. Wakati kiimbo kina maana ya kupanda na kushuka kwa mawimbi ya sauti ya lugha, kidatu kina maana ya kiwango cha sauti isikikayo, wakati wa utamkaji ama kuwa juu, kuwa katikati au kuwa chini.
Aina za kiimbo
Kiimbo cha maelezo: Kiimbo cha maelezo ni kile ambacho kwa kawaida msemaji wa lugha akiwa kwenye kidatu chochote kile mawimbi sauti ya usemaji wake yanakuwa takriban katika mstari ulionyooka.
Kiimbo cha kuuliza: Kiimbo cha kuuliza hujitokeza kwa kutumia viwango tofauti vya kidatu kutegemeana na aina ya swali linaloulizwa .
Kiimbo cha amri: kiimbo cha amri hakitofautiani sana na kiimbo cha maulizo.Uchunguzi wa kifonetiki, unaonesha kuwa katika kutoa amri, mzungumzaji hutumia kidatu cha juu zaidi kuliko ilivyo katika kiimbo cha maelezo.
Otografia :- Neno otografia lina asili ya kigiriki na maana yake ni utaratibu wa kutumia alama au michoro ya maandishi kuwakilisha sauti zisikikazo katika lugha.
Kila lugha ina mfumo tofauti wa usemaji na hutumia mfumo tofauti wa sauti.
Kila lugha haina budi kubuni mfumo wake wa kuziwakilisha sauti zake katika maandishi.
Mfumo huo wa maandishi ndio ujulikanao kama othografia.
Mfumo huu huwa unawasilisha herufi maalumu zinazobuniwa ili kuwakilisha sauti za lugha inayohusika kimaandishi.
Silabi:
Silabi ni kipashio cha kifonolojia kinachohusu matamshi ambacho kwacho sauti za Lugha hutamkwa mara moja kwa pamoja kama fungu moja la sauti. Kuna aina mbili za silabi, yaani silabi funge na silabi huru. Silabi huru ni zile ambazo huishia na irabu na silabi funge ni zile zinazoishia na konsonanti. Silabi za Kiswahili sanifu mara nyingi huangukia katika kundi la silabi huru.
Miundo asilia ya silabi za Kiswahili
Miundo ya silabi ya irabu peke yake (I).
Mf. A katika Anasoma
Miundo ya silabi ya konsonanti na irabu (KI).
Mf. Ka, ba, ma
Miundo ya silabi ya nazali pekee (N)
Mf. N katika Nta,
M katika Mtoto
Muundo wa silabi wa konsonanti, konsonanti na irabu (KKI)
Mf. Cha, sha,
Muundo wenye konsonanti,konsonanti,kiyeyusho,irabu (KKkI)
Mf. Shwa,
Muundo wa konsonanti,kiyeyusho,irabu (KkI)
Mf. Kwa, mwa
Muundo wa silabi za Kiswahili sanifu zenye asili ya lugha za kigeni
Muundo wa silabi wa Konsonanti, konsonanti na irabu (KKI)
Mf. Labda, leksika, teknolojia
Muundo wa silabi wa kosonanti, consonanti, konsonanti na Irabu (KKKI)