MOFOLOJIA YA KISWAHILI: MUHADHARA WA NANE: UUNDAJI WA MANENO /ISTILAHI/ MSAMIATI - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Chuo (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=3) +---- Forum: Shahada (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=20) +----- Forum: Nukuu (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=22) +----- Thread: MOFOLOJIA YA KISWAHILI: MUHADHARA WA NANE: UUNDAJI WA MANENO /ISTILAHI/ MSAMIATI (/showthread.php?tid=1627) |
MOFOLOJIA YA KISWAHILI: MUHADHARA WA NANE: UUNDAJI WA MANENO /ISTILAHI/ MSAMIATI - MwlMaeda - 12-01-2021 MUHATHARA WA NANE:
NJIA ZA UUNDAJI WA MANENO /ISTILAHI/ MSAMIATI
Uundaji wa maneno ni mchakato unaowezesha lugha kujiongezea msamiati ili kukidhi haja ya mawasiliano na kuendana na mabadiliko yanayotokea kila siku.
Maneno ya lugha ya Kiswahili hayaundwi kiholela bali hufuata taratibu na kanuni zinazokubalika kitaalamu.
Njia zitumikazo kuunda maneno ni kama zifuatazo:
v Unyambuaji
Njia hii inatumia mzizi mmoja wa neno na kuzalisha maneno mapya kwa kupachika viambishi nyambuaji
Mfano
Somo
Kisomo
Msomi
Msomaji
Mkulima
Kilimo
Mlimaji
v Uambatishaji/mwambatano
Hii ni njia ya kuunda maneno mapya kwa kuambatanisha maneno mawili.
Mfano
Mwana+chama – Mwanachama
Askari+kanzu – Askarikanzu
Bwana+shamba – Bwanashamba
v Urudufishaji / Uradidi
Hii ni mbinu ya kurudiarudia neno au sehemu ya neno na kuunda neno jipya ambalo huwa na maana tofauti na maneno yanayorudiwarudiwa.
Mfano
(a) Pole : polepole
(b) Sawa : sawasawa
© Haraka : harakaharaka
v Akronimu/ufupishaji
Ufupishaji ni njia mojawapo ya kuundia maneno mapya,ufupishaji huweza kufanyika kwa namna mbili ambazo ni.
Ø Kufupisha kwa kuchukua herufi za mwanzo
Mfano
CWT (Chama cha Walimu Tanzania)
VVU (Virusi Vya Ukimwi)
Ø Kufupisha kwa kuchukua silabi za mwanzo za maneno yanayo fupishwa
Mfano
BAKITA (Baraza la Kiswahili la Taifa)
TUKI (Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili)
TATAKI (Taasisi ya Taaluma za Kiswahili)
v Uhulutishaji
Ni njia ya kuunda maneno mapya kwa kuchukua vijisehemu vya
neno pasipo kufuata kanuni yoyote.
Mfano
Mnyama mfu – nyamafu
chakula cha jioni – chajio
hati za kukataza – hataza
Mtu asiye kwao – msikwao
v Utohoaji
Ni uchukuaji wa maneno toka lugha moja na kuyatumia kwenye
lugha nyingine baada ya kuyarekebisha kimatamshi na
kimaandishi ili yaendane na sarufi ya lugha inayotohoa.
Mfano
Neno Lugha asilia Kiswahili
Shirt Kiingereza Shati
Schule Kijerumani Shule
Bakura Kiarabu Bakora
Benjera Kireno Bendera
Matching guys Kiingereza Machinga
v Kuchukua
Hii ni mbinu ya kuongenza maneno kwa kuyachukua toka lugha
yake na kuyatumia kama yalivyo. Uchukuaji hufanyika kwa
lugha zinazoendana kisarufi kama Kiswahili na lugha za
kibantu.
Mfano
Kitivo — kisambaa /kipare
Ikulu – kinyamwezi
Kigoda – kizaramo
v kubadili mpangilio wa fonimu
Mfano
Lima – mila – imla – mali
v kufananisha umbo /sauti /tabia
Mfano
kifaru-(mnyama faru)
mkono wa tembo-(mkonga wa tembo)
kidole tumbo-(umbo la kidole)
Ubeberu-(beberu la mbuzi)
Ukupe-(mdudu kupe)
Pikipiki (mlio wa pikipiki)
Mtutu (mlio wa bunduki)
Nyau (mlio wa paka)
Kuku – kokoriko (mlio wa kuku)
v Njia ya udondoshaji
Mfano
mkwe wake – mkwewe
mwana wake – mwanawe
ndugu yake – nduguye
v Kuzingatia matumizi ya kitu
Mfano
Banio – (kubana)
Chanio – (kuchana)
Fyekeo – (kufyeka)
v Kutarjumi/kutafsiri
Mfano;
Fluid – (ugiligili)
Acquired immunal deficiency syndrome (Upungufu wa kinga mwilini)
Human immunal virus – (virusi vya ukimwi)
Anti-rentro-virus – (dawa za kufubaza makali ya ukimwi)
RE: MOFOLOJIA YA KISWAHILI: MUHADHARA WA NANE: UUNDAJI WA MANENO /ISTILAHI/ MSAMIATI - MwlMlela - 01-23-2022 Nimejifunza kitu kipya, kweli elimi Haina mwisho,kila jambo twapaswa kusoma na kupata maarifa mapya |