Welcome, Guest |
You have to register before you can post on our site.
|
Online Users |
There are currently 57 online users. » 0 Member(s) | 55 Guest(s) Applebot, Bing
|
Latest Threads |
Buy Vilitra 60 Mg |【Get E...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-24-2023, 11:45 AM
» Replies: 0
» Views: 0
|
How to take Cenforce50?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-19-2023, 12:59 PM
» Replies: 0
» Views: 0
|
About the Vidalista 60 Mg...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-04-2023, 04:07 PM
» Replies: 0
» Views: 0
|
What Is Vidalista 60?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-03-2023, 10:49 AM
» Replies: 0
» Views: 0
|
How to take Cenforce 100 ...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
03-29-2023, 02:37 PM
» Replies: 0
» Views: 66
|
How is Vidalista 10 Mg us...
Forum: Watunzi wa Kiswahili
Last Post: Kieth_winsett
03-27-2023, 01:26 PM
» Replies: 0
» Views: 117
|
Obtain Thesis Paper Assis...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Minny02
03-24-2023, 03:01 PM
» Replies: 0
» Views: 200
|
SEO services for sports f...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Maria Poland
03-17-2023, 01:51 PM
» Replies: 1
» Views: 223
|
NUKUU ZA KISWAHILI DARASA...
Forum: Nukuu
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:31 PM
» Replies: 0
» Views: 788
|
NECTA K4 2022
Forum: Mitihani
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:25 PM
» Replies: 0
» Views: 403
|
|
|
DHANA ZA MSINGI ZA MOFOLOJIA |
Posted by: MwlMaeda - 12-03-2021, 01:14 PM - Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha
- No Replies
|
|
(a) Mofimu
Kwa mujibu wa Matinde (2012:101) mofimu ni maana inayowakilishwa na mofu. Pia mofimu ni dhana ambayo ni sehemu ya umilisi kwa watumiaji wa lugha husika.
Mofimu ni vipashio vidogo vya msingi vinavyotumika katika kuunda maneno ya lugha. Mofimu ni vipashio vinavyoonyesha uhusiano uliopo kati ya sauti msingi za lugha yaani fonimu na maana maalumu katika sarufi ya lugha (Besha, 1994:52).
Aidha Massamba na wenzake (2013:13) wanaeleza kuwa mofimu ni kipashio kidogo kabisa katika umbo la neno kilicho amilifu (yaani kilicho na kazi ya kisarufi au kileksika) na ambacho hakiwezi kuvunjwa au kugawanywa katika vipande vingine vidogo bila kupoteza uamilifu wake.
Kwa ujumla mofimu ni kipashio kidogo cha lugha chenye maana kisarufi au kileksika.
Aina za Mofimu
Matinde (2012) ameainisha na kuelezea aina kuu mbili za mofimu yaani mofimu huru na mofimu tegemezi.
Mofimu huru. Ni silabi moja au zaidi yenye maana kamili ya neno na inaweza kujisimamia yenyewe bila msaada wa viambishi au silabi nyingine. Aghalabu mofimu huru huwa nomino, vivumishi au vielezi visivyochukua viambishi vya ngeli mfano daktari, ndoa, nyumba.
Mofimu tegemezi. Ni mofimu ambazo huhitaji viambishi ili kukamilisha maana iliyokusudiwa. Mofimu hizi hujumuisha mzizi wa neno au shina la kitenzi, kivumishi, nomino au vielezi ambavyo vinahitaji viambishi viwakilishi vya ngeli ili kutoa maana iliyokusudiwa.
Kwa ujumla mofimu inaweza kujidhihirisha kwa namna kuu tatu tofautitofauti ambazo ni;
(i) mzizi. Mfano; ruk- ruka
Kop- kopa
Pig- piga
Lim- lima
Chez- cheza
(ii) kiambishi. Mfano; a-na-temb-e-a
a-na-lim-a
kop-esh-a
a-na-chez-a
(iii) Neno yaani neno sharti liwe linajitosheleza kimaana mfano Baba, Dirisha, Mama, Kaka, Babu, Asha, Juma na maneno mengineyo mengi ya namna hiyo.
(b) Alomofu
Matinde (2012:100) Alomofu ni maumbo mawili au zaidi yanayowakilisha mofimu moja na hutokea katika mazingira maalum ya utokeaji.
Besha (1994:55) anaeleza kuwa Alomofu za mofimu ambazo zinatokea katika mazingira maalumu ya kifonolojia ya utokeaji wake unaweza kutabirika.
Hivyo basi, Alomofu ni maumbo mawili au zaidi yanayowakilisha mofimu ileile moja na ambayo huweza kutokea katika mazingira maalum.
Kanuni za alomofu katika kauli ya kutendeka.
Matinde (2012:192) anasema kuwa alomofu {-ik-} hutokea katika shina likiwa na irabu mojawapo kati ya a, i au u na mzizi huo huishia na konsonanti ambayo huonyesha ubora wa jambo fulani au uwezekano wa kitu kufanyika.
Mfano; {imb-} + //-ik-// + {-a} = imbika
{umb-} + //-ik-// + {-a} = umbika
{fany¬-} + //-ik-// + {-a} = fanyika
{pit-} + //-ik-// + {-a} = pitika
{tup-} + //-ik-// + {-a} = tupika
Habwe na Karanja (2007:110) anasema alomofu /-ek-/ hutokea iwapo mzizi wa kitenzi ndani yake una irabu e au o na mzizi huo huishia na konsananti na huonyesha ubora wa kitu/jambo kufanyika au uwezekano wa jambo fulani kufanyika.
Mfano; {jeng-} + //-ek-// + {-a} =jengeka
{pony-} + //-ek-// + {-a} = ponyeka
{chom-} + //-ek-// + {-a} = chomeka
{tosh-} + //-ek-// + {-a} = tosheka
{som-} + //-ek-// + {-a} = someka
{tek-} + //-ek-// + {-a} =tekeka
© Mofu
Matinde (2012) akiwanukuu TUKI (1990) wanaeleza kuwa mofu ni kipashio cha isimu maumbo kiwakilishacho mofimu.
Matinde (2012) Mofu ni umbo kamili ambalo huwakilisha mofimu. Umbo hilo hudhihirika kifonolojia na kiothografia (uwezo wa kutamkwa na kuandikwa).
Katika lugha ya kitaalamu umbo linalowakilisha mofimu hujulikana kama mofu (Massamba na Wenzake, 2013:14).
Kwa ujumla mofu ni umbo au maumbo yanayowakilisha mofimu na ambayo yanaweza kudhihirika kwa kutamkwa au kimaandishi.
Aina za Mofu
Matinde (2012) ameainisha mofu kwa kuzingatia vigezo viwili ambavyo ni:
(i) kigezo cha isimu maana
(ii) kigezo cha isimu maumbo
Katika kigezo cha isimu maana tunapata aina kuu tatu za mofu ambazo ni;
(i) Mofu huru
(ii) Mofu funge
(iii) Mofu tata
(i) Mofu huru
Ni mofu ambazo zinaweza kukaa peke yake kama maneno kamili yenye maana inayoeleweka bila kusaidiwa na mofu nyingine. Mofu huru zinaweza kuwa nomino, kivumishi, kiwakilishi, kielezi, kitenzi au kiunganishi.
(ii) Mofu funge au tegemezi
Ni mofu ambayo haiwezi kukaa peke yake kama neno lenye maana kamili. Mofu hizi huhitaji kuambatanishwa na mofu nyingine ili kupata maana sawa au neno kamili.
Mfano: M-toto – w-atoto
Ki-su – vi-su
M-ti – mi-ti
Ji-tu – ki-ji-tu
Wakati mwingine mofu funge inaweza ikatokea katika mizizi ya vitenzi:
Mfano: {-l-} katika neno kula
{-f-} katika neno kufa
{lim-} katika neno lima
{-j-} katika neno kuja
{-nyw-} katika neno kunywa
(iii) Mofu tata
Ni mofu ambayo huwa na maana zaidi ya moja yaani kuanzia mbili na kuendelea. Mofimu tata hutokea katika vitenzi vilivyopo katika kauli ya kutendea.
Mfano: Alimpigia = a-li-m-pig-i-a.
Alimchezea = a-li-m-chez-e-a.
Alimchomekea = a-li-m-chom-ek-e-a.
Hivyo mofu {-i-} na {-e-} ni mofu ambazo zinaonyesha kauli ya kutendea na ndizo zinaleta utata katika vitenzi hivyo.
Kigezo cha isimu maumbo
Matinde (2012) anaeleza kuwa katika kigezo hiki cha isimu maumbo kuna aina kuu mbili za mofu. Aina hizo za mofu ni;
(i) Mofu changamani
(ii) Mofu kappa
(i) Mofu changamani
Ni mofu inayoundwa kutokana na mwambatano wa mizizi miwili ambayo inaweza ikawa ni mizizi sahihi miwili kama vile;
{Askari} + {Kanzu} = Askarikanzu
{Gari} + {Moshi} = Garimoshi
{Fundi} + {Chuma} = Fundichuma
Pia inaweza ikawa mofu funge + mofu huru
Mfano: {Mw-} + {-ana} + {nchi} = Mwananchi
{Mw-} + {-ana} + {hewa} = Mwanahewa
(ii) Mofu kapa
Ni mofu za pekee ambazo hazina umbo. Mofu kapa hazitamkwi wala kuandikwa. Mofu kapa hazionekani katika neno lakini athari zinazotokana na mofu kapa hueleweka.
Mfano; Umoja wingi
U-kucha – ⱷkucha
U-kuta – ⱷkuta
U-funguo – ⱷfunguo
Nomino zilizo na kiambishi cha wingi tu cha umoja hakipo
Mfano; umoja wingi
ⱷkasha Ma – kasha
ⱷdebe Ma – debe
ⱷjembe Ma – jembe
(b) Fasili ya neno kileksika, kimuundo na kisarufi
(i) Fasili ya neno Kileksika
Neno ni kipashio kidogo cha lugha chenye maana. Kwa maana hiyo neno ni lazima liwe na maana inayoeleweka kwa jamii inayotumia lugha hiyo. (Mdee, 1977).
Mfano: Mama- Mzazi wa kike
Ndama- Mtoto wa ng`ombe
Dhana hii ina mashiko kwa sababu maneno mengi katika lugha yana maana ya kueleweka kwa watumiaji wa lugha.
Udhaifu wa fasili hii
Si kila neno linalotumika linaweza kuwa na maana ya wazi au ya kileksika. Mfano baadhi ya maneno hasa viunganishi na vihusishi kama vile ya, kwa, na, wakati ambapo yanakua hayana maana ya kileksika lakini yana uamilifu kisarufi.
(ii) Fasili ya neno kimuundo
Neno ni kipengele kidogo kabisa cha sentensi ambacho kinaweza kuhamishwa kutoka nafasi moja hadi nyingine bila kuathiri sarufi ya lugha katika tungo au sentensi hiyo (cruse, 1986) akinukuliwa na (Mdee, 1997). Kwa ujumla hapa kinachotazamwa zaidi ni kategoria za maneno na mpangilio wake katika tungo.
Mfano: Ali alimuua Ahmed
N T N
Ahmed alimuua Ali
N T N
Hapa N ni nomino na T ni kitenzi japo nomino zimebadilishana nafasi lakini sarufi hiyo haijaathirika. Utaratibu huu husaidia katika kujifunza sarufi ya lugha hasa miundo ya tungo kama kirai, kishazi na sentensi na pia kujua sehemu za tungo kama kiima na kiarifu.
Udhaifu wa fasili hii
• Sio maneno yote yanaweza kuhamishwahamishwa bila kuvuruga sarufi ya lugha
Mfano; Ali alisimama kando ya mto
Amesimama kando ya mto Ali
Kando ya mto Ali amesimama
*Mto Ali amesimama kando ya
*Mto ya kando amesimama
Hivyo sentensi mbili za mwisho hazikidhi haja ya usahihi wa kisarufi.
• Vilevile unapohamisha maneno basi maana ya neno pia hubadilika.
Mfano; Zubeda anampenda Zawadi
Zawadi anampenda Zubeda
Nomino zimebadilishana nafasi hazijaathiri sarufi ya lugha lakini kimaana imebadilika kwa sababu katika sentensi ya kwanza Zubeda ndiye anatenda tendo na katika sentensi ya pili Zawadi ndiye anatenda tendo.
(iii) Fasili ya neno kisarufi
Kwa mujibu wa Katamba (1993:19) ili neno litambulike lazima liwe katika muktadha wa matumizi. Katamba anasema neno moja linaweza kuwa na dhima mbalimbali na dhima hiyo itagundulika tu litakapokuwa ndani ya muktadha wa matumizi kwenye sentensi. Anatoa mfano wa neno la kiingereza “cut” kwamba likiwa kipwekepweke mtu hawezi kutambua linarejelea nini pamoja kwamba neno hilo katika lugha ya kiingereza ni kitenzi yaani ‘kata’ lakini kuna wakati linaweza kutumika kurejelea nomino. Mfano I need my cut na I have cut my fingure. Ukichunguza vizuri mifano hii ‘cut’ katika sentensi ya kwanza hurejelea nomino na katika sentensi ya pili hurejelea kitenzi. Sentensi ya kwanza ilikuwa na maana ‘nahitaji stahiki yangu’ na ya pili ina maana ya ‘nimekata kidole’.
Kigezo hiki huenda mbali kwa kufafanua kuwa pia maneno kama ‘na’, ‘tu’, ‘si’ katika Kiswahili na maneno kama ‘and’, ‘an’, ‘the’ ‘on’ katika kiingereza nayo hayawezi kutambulika yanarejelea nini, lazima yawe katika muktadha wa matumizi ndio tunaweza kusema ni aina gani za maneno na kutambua maana zake.
Udhaifu wa fasili hii
Si lazima maneno yote yawe katika muktadha wa matumizi ndipo tuweze kubaini maana zake kwani kuna baadhi ya maneno huweza kutambulika kuwa yana maana gani hata yasipokuwa katika muktadha wa matumizi katika sentensi. Kwa mfano nomino za mahali kama vile Dodoma, Mwanza na Morogoro na majina ya watu kama vile Amina, Omari, Magreth na Ali.
HITIMISHO
Hivyo basi katika kufasili dhana ya neno ni vyema kuzingatia vigezo vyote vya kisarufi kama vile fonolojia, maana, sarufi ili kupunguza changamoto zinazojitokeza katika kufasili dhana hii kama ilivyobainishwa hapo juu.
MAREJELEO:
Besha, R.M. (2007). Utangulizi wa Lugha na Isimu. Dar es Salaam: Macmillan Aidan Ltd.
Habwe, J. & Karanja, P. (2007). Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Nairobi: Phoenix Publishers.
Katamba, F. (1993). Morphology. London: Macmillan Press Ltd.
Massamba, D.P.B na Wenzake. (2013). Fonolojia ya Kiswahili Sanifu. Dar es Salaam: TUKI.
Matinde, R.S. (2012). Dafina ya Lugha Isimu na Nadharia: Kwa Sekondari, Vyuo vya Kati na Vyuo Vikuu. Mwanza: Serengeti Educational Publishers (T) Ltd.
Mdee, D. (2007). Nadharia za Leksikografia. Dar es Salaam: TUKI.
TUKI. (1990). Kamusi ya Isimu na Lugha. Dar es Salaam: TUKI
|
|
|
USHAMIRISHAJI KATIKA LUGHA YA KISWAHILI |
Posted by: MwlMaeda - 12-03-2021, 01:02 PM - Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha
- No Replies
|
|
Makala hii itaangazia kwa kifupi maana ya ushamilishaji kwa mujibu wa wataalamu wanavyojaribu kuielezea, tutaangalia maana ya uelekezi kwa mujibu wa wataalamu ambao ndio hutupa mwelekeo wa uelewa zaidi dhana nzima na sifa pamoja na viashiria vya ushamirishaji, pia tutaeleza aina za ushamirishaji pamoja na makundi ya ushamilishaji.
Kwa kuanza na maana ya ushamilishaji wataalamu wameifasili kama ifuatavyo;
grammar.about.com/old/dg/complent. Wanaeleza ushamilishaji ni hali ya kishazi tegemezi kusaidia kueleza au kufafanua maana kamili ya nomino au kitenzi katika sentensi. Fasili hii imejikita kuonesha ushamirishaji wa nomino na kitenzi bila kuangalia au kueleza ushamilishaji wa vivumishi, vihusishi na vitenzi kwa hata vivumishi vinaweza kutosheleza na kishazi tegemezi.
O’grady na wenzake (1996) wanaeleza ushamilishaji kwa kutoa maneno ambayo yanaweza kufanyiwa ushamilishaji kama vile nomino, kivumishi, kitenzi, kihusishi ambayo yanaweza kutoshelezwa na vishazi tegemezi. Mapungufu ya hoja hii ni kwamba hawajaonesha ushamirishaji wa kielezi lakini ukweli ni kwamba ni maneno yanaweza kufanyiwa ushamirishaji.
Hivyo tunaweza kusema ushamirishaji ni mchakato unaofanywa na vishazi tegemezi kutosheleza kitenzi, nomino kivumishi kielezi na kihusishi kinachotokea kwenye upande wa kiarifu au kutoa maelezo yaliyo ya lazima kukamilisha taarifa ya za kitenzi, nomino, kivumishi, kihusishi na kielezi.
Baada ya kufasili maana ya ushakilishaji sasa tunaweza kueleza kwa kifupi maana ya uelekezi. Wataalamu wameeleza maana ya uelekezi kama ifuatavyo;
Massamba (2004) anaeleza uelekezi kuwa ni kuwa ni hali ya uhusiano uliopo baina ya kitenzi na vijenzi vingine vya muundo wa sentensi vinavyohusiana nacho. Kiini chake hasa ni kitenzi kuhitaji au kutohitaji yambwa. Hii ina maana kuwa anaposema kuwa kitenzi kuhitaji yambwa ana maana kuwa kitenzi kuambatana na kipashio kingine kilicho cha lazima.
Mfano: mwalimu anasoma kitabu
Juma anacheza mpira
Hivyo katika sentensi hizi vipashio vilivyo vya lazima ni kitabu na mpira.
Katika kutohitaji yambwa (si elekezi) ana maana kuwa kutoandamana na kipashio kingine au kutoandamana lakini hakuna ulazima.
Mfano: Rajabu amelala usingizi.
Hivyo neno “usingizi” si kipashi cha lazima katika sentensi hii.
Habwe na karanja (2004) wanasema kitenzi elekezi ni vitenzi vinavyoashilia vitendwa na hali ambayo huvuka mipaka na kuathiri maneno mengi ya sentensi. Maneno yanayoathiriwa huitwa yambwa tendwa au tendwa.
Mfano: jesse anampiga mama
Baba anakula machungwa.
Hivyo basi kitenzi “anampiga” kinauliza swali la nani na “anakula” swali “nini” hivyo vitenzi hivi ni elekezi ambapo vinaandamana na maneno yaliyo ya lazima kama vile “mama” na “machungwa”.
Pia vitenzi si elekezi, wanaelezea kuwa ni vitenzi ambavyo huwa havihitaji yambwa. Kwa maana kwamba vinajitoshereza katika matumizi yake.
Mfano: jamesi amesinzia
Asha anakimbia
Hivyo vitenzi (amesinzia) na (anakimbia) si elekezi kwa maana havihitaji yambwa. Hivyo basi uelekezi tunaewza kusema ni mchakato wa kitenzi kuchukua au kubeba au kutoandamana na yambwa.
Baada ya kufasili au kueleza maana ya uelekezi tuangalie tuangalie sifa za ushamirishaji: sifa hizo ni kama zifuatazo.
Kishazi tegemezi bebwa, huwa kinafanya kazi ya kuarifu pia kufanya kazi ya kutosheleza kitenzi, nomino, kitenzi na kihusishi. Ni lazima kitokee baada ya maneno haya kwa lengo la kujibu maswali ya kwa nini na nani kama yale yanayotokea kwenye uelekezi.
Hivyo baada ya kuangalia sifa hizi za usharishaji tuangalie viashiria vya ushamiklishaji:
Black (1998) na O’glady na wenzake (1996) wanatueleza kuwa viashiria vya ushamirishaji ni kama vile ya, kuwa, kwamba,kappa, kama lakini kuna kiashiria kingine kama vile (ku). Blacka (1998) amezungumzia suala la ushamirishaji wa vitenzi peke yake hajatuelezea wa vitenzi, nomino,vivumishi, vihusishi na vivumishi kama O’glady na wenzake.
Baaba ya kuangalia viashiria vya ushamirishaji tuangalie ushamirishaji unaweza kujidhihirisha katika vitenzi, nomino, vivumishi, vihusishi na vielezi. Hivyo tukianza na :
Ushamirishaji wa vitenzi, ni ushamirishaji unaotokana na vitenzi vinapohitaji kutoshelezwa si kwa nomino za kawaida bali kishazi tegemezi ambacho lazima kitokee kwa lengo la kitenzi husika kukamilisha taarifa/ utoa taarifa zinazojitosheleza
Mfano: Baba alimwambia [asha] kuwa mama hatarudi nyumbani.
Mwalimu alihuzunika kuwa wanafunzi walifeli somo lake.
Kishazi tegemezi kilichotokea baada ya yambwa “Asha” na kitenzi “alihuzunika” vinafanya kazi ya kutosheleza vitenzi / kukamilisha taarifa ya kitenzi.
Ushamirishaji wa vitenzi umegawanyika katika makundi manne ambayo ni kama ifuatavyo:
Vitenzi vya kusema, ni vile vitenzi ambavyo huwa vinatoa ripoti, matangazo, kuarifu jambo, kuambia au kueleza jambo au tukio fulani.
Mfano: Rais aliwatangazia wananchi kuwa atavunja baraza la mawaziri.
Komba alituambia kwamba wanafunzi wanaojituma kusoma watafaulu.
Katika sentensi hizi kishazi au vishazi vinavyotokea baada ya kitenzi “aliwatangazia” na “alituambia” vinafanya kazi ya kushamirisha vitenzi hivi au kukamilisha taarifa ya vitenzi.
Vitenzi vya kudadisi au kutaka kujua, ni vile vitenzi ambavyo huwa vinafanya kazi ya uchanganuzi, kuuliza na kufanya upelelezi kuhusu kitu fulani au jambo.
Mfano: Juma alitaka kujua kwamba nani anafuja mali za umma
Asha alichunguzakuwa wanafunzi wengi wanaishi kwa kutegemea fedha yamkopo.
Vishazi tegemezi vilivyopigiwa msitari vinafanya kazi ya ushamirishaji wa vitenzi “alitaka” na “alichunguza”.
Vitenzi vya kutendesha, hivi ni vitenzi vya kuamuru, kuagiza, kuruhusu, kulazimisha, au omba kufanyika kwa jambo fulani.
Mfano: Wazazi aliwasihi watoto kusoma kwa bidii ili wafaulu mitihani yao.
Rais aliamuru kwamba wanajeshi walinde mipaka ya nchi.
Hivyo vishazi hivi vinafanya kazi ya kushamirisha “waliwashawishi” na “aliamulu” ambapo vinafanya kazi ya kutoshereza vitenzi.
Vitenzi vya kuhisina kuamua, hivi ni vitenzi vya pande, furahi, kataa, jaribu, thubutu, fikiria na kusudia
Mfano: Wanafunzi walikataa kuwa hawawezi acha kudai haki zao.
Mama alimkataza Juma kuwa asichezee karibu na kisima.
Vishazi hivyo vinafanya ya kutosheleza “walikataa” na “alimkataa”.
Ushamirishaji wa nomino, ni mchakato ambao kishazi tegemezi hufanya kazi ya kuelezea au kufafanua au kutosheleza nomino ambayo inakuwa hijakamilika inayotokea katika sehemu ya kirifu.
Mfano: ameacha maagizo kwamba mwanae amfuate.
Kishazi tegemezi kilichotokea baada ya nomino “maagizo” kinafanya kazi ya kutosheleza namino “maagizo”
Ushamilishaji wa nomino unafanana na ushamilishaji wa vitenzi vya kusema, kudadisi na kutendesha. Hivyo tunaweza kugawa nomino katika makundi matatu. Makundi hayo nia kama vile:
Nomino za kutendesha, ni nomino ambazo huwa ambazo huwa zinaonesha hali ya kuamuru, kuruhusu, kuagiza kutaka, kulazimisha na kuomba.
Mfano: Imetolewa amri kwamba wamanchi wasichechee migomo ya vyimbo vya dola.
Ametoa maagizo kuwa wanafunzi wote tuondoke kesho hapa chuoni.
Vishazi vilivyotokea baada ya nomino “amri”na” maagizo” vinafanya kazi ya kutosheleza nomino hizi.
Nomino za kudadisi au kutaka kujua, ni nomino ambazo huwa ziafanya kazi ya kuchunguza, kuuliza au kuliza jambo fulani.
Mfano: sina uhakika kama maelezo aliyatoa ni ya kweli
Sina mashaka kama maelezo yake si sahihi.
Sina uhakika kama uufafanuzi wako unajitosheleza.
Vishazi vinavyotokea baada ya nomino vinafanya kazi ya kutosheleza nomino “uhakika” na “mashaka”.
Nimino za kusema, ni nomino zinazotoa ripoti, tangaza, arifu, ambia, na eleza jambo au tukio fulani.
Mfano: Ametoa matangazo kwamba watu wote wafike kwenye mkutano.
Tumetoa taarifa kwamba wanawake wengi ni wavivu.
Vishazi vinavyotokea baada ya nomino vinafanya kazi ya kushamirisha nomino husika au kutosheleza nomino hii.
Ushamilishaji wa vivumishi, ni mchakato ambao kishazi tegemezi hufanya kazi ya kutosheleza kivumishi kinachotokea kwenye kiarifu. Ushamilishaji huu hufanana na ushamilishaji wa vitenzi vya kuhisi au kuamuru.
Mfano: haikuwa rahisi kumuua Simba kwa mishale.
Ni vigumu kumwamini msichana ambaye humfahamu historia yake ya maisha.
Hivyo vishazi vinavyotokea baada ya kivumishi “rahisi” na “vigumu” inatumika kutosheleza vivumishi hivi ambavyo havikamilishi maana ya tungo.
Ushamirishaji wa vihusishi, ni mchakato ambao kishazi tegemezi hufanya kazi ya kutosheleza kihusishi kinachotokea upande wa kiarifu ambacho huwa ni lazima kitokee baada ya kihusishi.
Mfano: Juma alifaulu kwa kusoma kwa bidii
Mwalimu alituambia ya kwamba tusipokuwa makini tutafeli vibayamitihani.
Neno la Mungu linasema ya kuwa kumcha bwana ni chanzo chamaarifa.
Hivyo vishazi hivo vinafanya kazi ya kazi ya kutosheleza kihusishi.
Ushamilishaji wa vielezi, ni mchakato ambao kishazi tegemezi hufanya kazi ya kutosheleza kielezi kinachotokea upande wa kiarifu ambacho huwa na lazima kutokea baada ya kihusishi.
Mfano: John anatembea polepole kama mgonjwa anyeumwa miguu.
Asha anakula harakaharaka kama mtu ambaye hajawahi kula siku kumi.
Hivyo vishazi vinafanya kazi ya kutosheleza kielezi.
Hivyo basi ushamirishaji katika Kiswahili unasaidia kuondoa maswali ya nini? Na nani?. Hivyo ushamirishaji unafanya kazi ya kutoa taarifa zilizo kamilika.
MAREJEO
Black, C.A (1998) A step by Introduction to The Government and Biding Theory of Syntax. SIL-
Mexico Branch and Univerisity of North Dakota.
grammar.about.com/od/c/g/complement.
Habwe, J na Karanja, P (2004) Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Nairobi: Phoenix.
Massamba, D.P.B (2004) Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha. Dar es Salaam: TUKI.
|
|
|
VIKOA VYA MAANA: UMUHIMU NA CHANGAMOTO ZAKE KATIKA KUELEZA MAANA YA MAANA |
Posted by: MwlMaeda - 12-03-2021, 12:56 PM - Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha
- No Replies
|
|
Katika makala hii tujadili umuhimu wa vikoa vya maana katika semantiki, yaani kuonesha ni kwa namna gani vikoa vya maana vinaweza kufanikisha suala la kuendeleza taaluma ya semantiki ambayo hujihusisha zaidi na uchunguzi wa maana ya lugha ya binadamu. Pia tutaonyesha changamoto mbalimbali ambazo zinatokea wakati wa kuelezea maana ya maana. Kabla ya kujadili yote hayo ni vyema kwanza kujadili kwa ufupi maana ya vikoa vya maana pamoja na semantiki kutoka kwa wataalamu mbalimbali kusudi uhusiano na utofauti uliopo kati ya semantiki na vikoa vya maana.
Briton (2000) anaihusisha dhana ya vikoa vya maana na dhana ya hiponimia ambapo hiponimia ni uhusiano wa kiuwima ambapo fahiwa ya neno moja hujumuishwa katika fahiwa ya neno jingine mfano fahiwa ya mgomba, mahindi, maharage zimejumuishwa katika mimea. Anahitimisha kwa kusema kuwa maneno katika vikoa vya maana huwa na sifa sawa zinazohusiana.
Wikipedia, wanaeleza kuwa kikoa cha maana ni msamiati wa kiufundi katika taaluma ya isimu ambao unaelezea kikundi cha maneno yanayohusiana kimaana.
Dirk (2010) anaeleza kuwa vikoa vya maana ni jozi za maneno yenye maana zinazohusiana ambazo maana zake zinategemeana, na kwa pamoja zinatoa dhana ya kimuundo yenye uhalisia ndani yake.
Hivyo kikoa cha maana kinaweza kufasiriwa kuwa ni seti yeyote ile ya misamiati ambayo memba wake wanahusiana kiwima na kimlalo. Uhusiano kiwima tunaweza kusema kuwa ni namna maneno yanavyohusiana kiwima, na mlalo ni namna maneno yanavyoweza kuvutana na maneno mengine yanayoelekeana nayo na kuleta maana.
Mifano ya vikoa vya maana nikama vile; “Uandishi wa kubuni” ambapo hujumuisha hadithi fupi, tamthiliya, ushairi na riwaya.
“Michezo”: ambapo hujumuisha; mpira wa miguu, mpira wa kikapu, kuruka kamba, mpira wa pete, mpira wa meza, mpira wa mikono.
“Nguo”: ambapo hujumuisha nguo za wanawake na nguo za wanaume. Nguo za wanawake: sketi, kanga, gauni, sidiria, blauzi.
Baada ya kujadili maana ya vikoa vya maana, ni vema pia kuangalia maana ya semantiki kabla ya kujadili umuhimu wa vikoa vya maana.
Kwa mujibu wa Habwe na Karanja (2004) semantiki ni utanzu wa isimu unaochunguza maana katika lugha ya binadamu, wanaendelea kusema kuwa maana hushughulikiwa katika viwango vyote vya lugha kama vile sauti, maneno na sentensi.
Hivyo tunaona kuwa vipengele muhimu katika lugha ya binadamu ni maana kwa sababu huweza kufanikisha suala la mawasiliano na upashanaji wa habari(ujumbe).
Umuhimu wa vikoa vya maana katika semantiki ni kama ufuatao.
Huonesha uhusiano wa maneno yenye sifa sawa au zinazoelekeana kimaana. Vikoa vya maana humsaidia mwanaisimu kutambua sifa za maana mbalimbali zinazohusiana kimaana kwani huwezi kuweka neno fulani katika kikoa fulani bila kujua sifa zinazotawala neno hilo. Mfano lazima ujue ndege na sifa zake ndipo utaje ndege wanaojenga hicho kikoa kama vile Kanga, Kuku, Njiwa, Bata, Mbuni na Kware.
Hurahisisha mchakato wa ujifunzaji lugha, husaidia kumueleza mtu anayejifunza lugha fulani husika ili kujua vitu mbalimbali vilivyowekwa katika makundi husika. Mfano mtoto au mgeni wa lugha fulani huweza kujifunza dhana mbalimbali kupitia vikoa vya maana. Mfano watoto huweza kujifunza rangi mbalimbali hasa nyeusi na nyeupe kwa kupitia vikoa hivyo.
Hurahisisha mawasiliano, yaani huokoa muda baina ya wazungumzaji, kwa mfano badala ya kutaja kitu kimoja kimoja basi unataja kwa ujumla wake endapo vinahusiana mfano, ukienda sokoni utauliza “una mboga za majani” utajibiwa kuwa kuna, mchicha, chainizi, spinachi, figili na matembele. Ilhali ilitakiwa mnunuaji amuulize muhudumu kwa kutaja jina mojamoja lakini yeye ametaja kwa ujumla na jibu limepatikana na ndipo huweza kutaja kikoa kimoja alichokitarajia.
Hufanya kazi ya kustawisha maana katika tungo au sentensi, utungo huwa na maana iliyojitosheleza kisemantiki(kimaana). Vikoa vya maana vinapotumika katika utungo huo hauwezi kustawisha maana hata kama vitabadilishana nafasi na muda mwingine hupelekea hata maana ya awali kupotea lakini bado utungo utakuwa na maana. Vikoa hivyo vinaweza kujitokeza katika mfumo wa kiwima au kiulalo.
Mfano :
(a) paka amekula nyama yote.
(b) chui amekula nyama yote.
© simba amekula nyama yote.
Maneno yaliyopigiwa mstari yamebadilishana nafasi kiwima lakini maana yake imebaki kama ilivyo na sentensi zimejitosheleza.
Hufanikisha shughuli za utunzi wa leksikografia, Mdee (2010), akimnukuu Wiegand anaeleza kuwa leksikografia ni shughuli au kazi ya kisanaa inayojishughulisha na utunzi wa kamusi. Leksikografia hiyo hujishughulisha na ukusanyajin wa misamiati mbalimbali ya lugha na ndiyo inayosaidia kutungiwa kamusi. Na kamusi ni kipengele cha kisemantiki kwa kuwa hutoa maneno yenye maana kwa watumiaji wa lugha na maneno hayo ndiyo vikoa vyenyewe vya maneno vyenye maana ambazo muda mwingine maana zake zaweza kuwa tofauti hatakama vikoa hivyo vinakuwa na maumbo sawa ya maneno. Mifano ya kamusi zenye vikoa vya maana ni kama vile;
-kamusi ya wanyama
-Kamusi ya mavazi
-Kamusi ya tiba ya magonjwa
-Kamusi za misuko ya nywele
-Kamusi za vyakula
Kikoa kimoja husaidia kujua na kufafanua vikoa vidogo vilivyomo ndani ya vikoa vikubwa mfano kikoa cha vyakula: ugali, ndizi, viazi, ambapo kisemantiki humsaidia mtumiaji wa lugha kuteua kikoa mahususi kwa ajili ya matumizi yake kwa wakati huo.
Husaidia kuonesha umbo la wingi ambalo lina umuhimu kisemantiki hasahasa katika upatanisho wa kisarufi kwa mfano badala ya kusema ‘kikoa cha tunda” tunasema “kikoa cha matunda” “mnyama- wanyama” “mmea- mimea” hivyo basi vikoa hivyo vikitumika kwenye sentensi huwa matunda yameiva badala ya kusema Tunda yameiva, wanyamawanakimbia badala ya kusema wanyama anakimbia.
Vikoa vya maana vina sifa ya kuwa na maana ya kileksimu na kufanya kikoa kimoja kichanuze zaidi na kuweza kupata maneno mengine yenye maana kisemantiki. Mfano kuna kikoa cha masomo ya sayansi, biolojia, fizikia, kemia, kilimo. Kikoa cha biolojia huweza hufasiliwa kuwa ni somo la kisayansi linalohusiana na viumbe hai na visivyo hai. Hivyo tunaona kuwa kikoa cha biolojia kimechanuza zaidi na kuleta maana ya kikoa hicho.
Changamoto ya vikoa vya maana katika kuelezea maana ya maana.
Kuna baadhi ya vikoa havina idadi maalumu na vingine vina idadi maalumu, hii ni kutokana na ukweli kwamba vikoa kama vile vya siku za wiki , idadi ya miezi ya mwaka na siku katika mwezi huwa na idadi maalumu lakini vikoa vya maana vingine havina idadi maalumu mfano vikoa vya matunda, wanyama, mimea. Vikoa vya matunda,wanyama mimea na vinginevyo haviewezi kuwa na idadi maalum kwa kuwa vikoa vyake huweza kujitokeza kutegemeana na mazingira. Wanajamii watatoa majina ya vikoa hivyo baada ya aina fulani kutokea katika jamii yake na hivyo kuacha vionekani kutokuwa na idadi maalumu.
Kuna baadhi ya vikoa ni changamani, hii ni kutokana na kwamba baadhi ya vikoa vya maana vinawakilisha dhana zaidi ya moja na hivyo kumfanya mtumiaji wa lugha apate utata wakati wa uainishaji wake.
Mfano: ndege kama mnyama, na ndege kama kifaa cha usafiri, pia mbuzi kama mnyama na mbuzi kama kifaa. Nyanya kama kiungo na nyanya kama mboga.
Hivyo basi vikoa hivi vya maana huweza kumchanganya mwanasemantiki na kushindwa kupata maana halisi.
Baadhi ya vikoa vya maana vinauhusiano wa karibu kiasi kwamba vinaweza kumchanganya mtu katika kutofautisha dhana mbili mfano Chui na Duma, Mbwa na Mbwa mwitu, Kuku na Kware.
Hakuna nadharia ya jumla inayohusika na upangaji wa vikoa hivi, hii inatokana na ukweli kwamba dhana hizi zipo vichwani mwa watu na kuandikwa kutokana na matumizi yake kimaana
Vilevile uainishaji unahitaji umakini zaidi katika upangaji wa vikoa kwani kuna uchomozi wa vikoa vingine, hii hutokea pale ambapo dhana moja mahususi huwa na dhana ndogondogo ndani yake ambazo nazo huweza kusimama peke yake mfano kikoa cha binadamu tunapata wanaume na wanawake, ambapo ndani ya kikoa cha wanawake tunapata bibi kizee, shangazi, mama, msichana. Pia kikoa cha mwanaume tunapata babu, mjomba, Mvulana.
Vikoa vya maana hutofautiana kutokana na eneo na utamaduni, hii inamaana kuwa kila utamaduni fulani huweza kuwa na vikoa vitumikavyo katika mazungumzo yao ambavyo vinaweza kutofautiana na utamaduni wa jamii nyingine kutokana na aina na idadi ya vitu hivyo katika jamii fulani. Mfano kikoa cha ndizi katika utamaduni wa Wanyakyusa Tukuyu Mbeya kuna vikoa vya majina ya ndizi kama vile; malinda, matoki, mkono wa tembo, haradoni, kaambani na ndyali lakini katika jamii ya Wahaya huko Bukoba kuna vikoa vya majina ya ndizi kama vile; shubili, majivu. Hivyo tunaona kuwa vikoa vya maana katika jamii ya wanyakyusa na wahaya hutofautiana.
Hivyo tunaweza kusema kuwa japokuwa kunachangamoto zinazokabili vikoa vya maana lakini vikoa hivyo vina umuhimu au mchango mkubwa katika kuendeleza taaluma ya semantiki kwa sababu wanasemantiki hufanya uteuzi mzuri wa maneno yenye maana kutoka akilini na kuyatumia katika mazungumzo na hivyo kufanya suala la mawasiliano liendelee kufanikiwa zaidi.
MAREJEO
Brinton L. J (2000) The Structure of Modern English. A Linguistic intro Illustrated Edition. John Benjamini Publishing company.
Dirk, G (2010) Theories of Lexico Semantics. Oxford University Press: New York.
Habwe, J na Karanja, P (2004) Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Phoenix Publishers: Nairobi.
Mdee,J.S, (2010) Nadharia na Historia ya Leksikografia.Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili: Dar es Salaam.
|
|
|
SARUFI MAPOKEO, WANAZUONI WALIVYOCHANGIA KATIKA MAENDELEO YA SARUFI ULIMWENGUNI |
Posted by: MwlMaeda - 12-03-2021, 12:48 PM - Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha
- No Replies
|
|
Kabla ya kueleza mcango wa wanamapokeo ni vema kueleza maana ya sarufi. Dhana ya sarufi imefasiliwa na wataalamu mbalimbali huku kila mmoja akitoa fasili yake, wataalamu hao waliofasili dhana hii ni kama wafuatao.
TUKI (2004) sarufi ni kanuni za lugha zinazotumika ili kupata ufasaha wa usanifu katika lugha.
Massamba (2004) yeye anaeleza kuwa sarufi ni taaluma ya lugha inayohusu uchunguzi na uchanganuzi wa kanuni za n vipengele mbalimbali vya lugha.
Massamba na wenzake (1999) pia wameeleza kuwa sarufi inahusu kanuni, sheria au taratibu zinazotawala kila kimoja kati ya viwango vinne vya lugha ambavyo ni umbosauti (Fonolojia), umbo neno (Mofolojia), Miundo maneno (Sintaksia) na umbo maana (Semantiki).
Katika fasili hizi juu ya dhana ya sarufi wataalamu hawa kila mmoja amejaribu kugusa baadhi ya vipengele katika fasili zao, vipengele hivyo ni kama vile kanuni na vipengele vya lugha. Hivyo tunaweza kufasili sarufi kuwa ni kanuni, sheria na taratibu zinazotawala lugha katika viwango vyote vya lugha yaani kiwango cha fonolojia, mofolojia, sintaksia na semantiki.
Khamisi na Kiango (2002) wanaeleza kuwa sarufi mapokeo ni sarufi ya kale ambayo ilijitokeza kuanzia karne ya 5KK, ambayo ilionekana kutokuwa na msimamo wakisayansi katika kuelezea lugha bali zilikuwa na mwelekeo wa kifalsafa.
Massamba na wenzake (1999) wanafafanua kuwa sarufi mapokeo ni sarufi elekezi iliyosisitiza usahihi wa lugha kwa kuonesha sheria ambazo hazina budi kufuatwa, mathalani, kufanya muundo fulani wa sentensi usemekane kuwa sahihi, au sheria ambazo hazina budi kufuatwa ili kufanya matamshi ya neno fulani yakubalike kuwa ndio sahihi.Sarufi hizo za kimapokeo zilikuwa zikisisitiza jinsi ambavyo lugha haikupaswa kuwa. Kwa mfano sarufi mapokeo ingekubali sentensi (a) mpaka © na kuzikataa (d) mpaka (f) hapa chini.
(a) Kalamu hii ni yangu
(b) Kiti hiki ni chetu
© Mtoto huyu ni wenu
(d) Kalamu hii ni ya mimi
(e) Kiti hiki ni cha sisi
(f) Mtoto huyu ni wa nyinyi
Pia wanasarufi mapokeo waliamini kuwa lugha ya Kilatini ilikuwa ni bora kwa kuwa lugha hii ilikuwa imeenea zaidi. Waandishi wengi walichukulia moja kwa moja kwamba taratibu zilizokuwa zikitumika katika kuainisha au kuchambua sarufi za lugha hiyo ambazo ndizo zilizokuwa sawa na ndizo zilizostahili kutumiwa katika uchambuzi na uainishaji wa lugha yeyote duniani.
Hiyo ndiyo sababu sarufi za lugha nyingine zilizoandikwa hapo zamani zilifuata taratibu na muundo wa sarufi ya Kilatini. Kwa mfano umoja na wingi, kwa kuwa lugha ya kilatini zilikuwa na nomino za umoja na wingi, hivyo basi waliamini kuwa nomino za lugha zote duniani zilikuwa na maumbo ya umoja na wingi.
Sarufi ya kimapokeo ni sarufi kama ilivyokuwa ikichambuliwa kwa kutumia mtazamo na mbinu za kimapokeo, ikitazamwa katika mwelekeo wa kimapokeo, sarufi hii ni taaluma ambayo imekuwepo
kwa muda wa karne nyingi na kuelezwa na wataalamu mbalimbali wa kale kama wafuatao;
Panin, huyu ni mwanasarufi mapokeo ambaye anakumbukwa kwa kuainisha sauti za lugha ya kisansikriti katika karne ya 5, alizigawa sauti hizo katika vokali na konsonanti na neno kama vile majina na vitenzi. Utafiti huu ulifanywa huko india ya kale katika karne ya 5.
Kimsingi Panin alichangia sana katika maendeleo ya sarufi ulimwenguni kwani kategoria za maneno ambazo aliziainisha kama vile majina na vitenzi bado zinatumika katika lugha nyingi duniani ikiwemo Kiswahili,
Plato, naye pia alichangia kwa kuigawa sentensi katika makundi mawili makuu, makundi hayo ni nomino na tendo. Yeye aliamini nomino ni maneno yaliyoweza kufanya kazi ya kiima na tendo ni maneno yenye kueleza matendo au sifa za kiima.
Mfano;
(a)Alinunua saa
(b)Alikimbia sana.
Makundi haya aliyaita kiarifu.katika falsafa sentensi iliundwa na Kiima na Kiarifu. Sentensi haikuwa kamili kama haikudhihilisha vitu hivyo yaani kiima na kiarifu. Mchango wake mkubwa katika dunia yetu ya lugha, maelezo ya sentensi yalitakiwa yaoneshe ukweli wa falsafa ya Kiima na Kiarifu, hivyo sentensi ilitawaliwa na kanuni hii,
S = KM + KF
Ukweli huu haukuwa na mashiko zaidi kwani lugha mara nyingi zilionyesha sulubu tofauti tofauti za kuifanya kanuni isifanye kazi. Pamoja na udhaifu huu Plato amechangia sana katika dhana ya kiima na kiarifu katika lugha nyingi duniani.
Kwa mfano Kiswahili;
(a) Mama anapika ugali
(b) Mama analima shamba
Katika mifano hii “Baba” na “Mama” ni kiima na sehemu ya sentensi anapika ugali na analima shamba ni kiarifu.
Donates, huyu ni mwanamapokeo mwingine. Ni mwanasarufi mapokeo wa karne ya 4, ambaye aligundua mambo mawili ambayo ni tofauti kati ya nomino na kivumishi. Pia aliangalia upatanisho, utawala na mrejeo sawa katika sarufi, kabla ya hapo aliandika sarufi elekezi na pia aliandika sarufi ya jumla ambayo ilikuwa na mantiki ya lugha zote duniani.
Protagoras: Nae alitoa mchango wake katika sarufi mapokeo kwa kutumia kigezo cha maana. Aliainisha aina tatu za sentensi ambazo ni swali, maelezo na amri.
Mfano;
(a) Mwalimu amekuja? (swali)
(b)Mwalimu anfundisha vizuri (maelezo)
© Njoo hapa mara moja (amri)
Udhaifu wake ni kwamba anaainisha sentensi kwa kuzingatia kigezo cha maana bila kuzingatia vigezo vingine kama vile muundo ambapo tunaweza kupata sentensi sahili, changamano na ambatano.
Licha ya udhaifu wake dhana yake ya kuainisha sentensi kwa kigezo cha maana bado inatumika katika lugha mbalimbali kama vile;
Kiingereza.
Mfano
(a) What is he doing? (swali)
(b) Mariam is reading (maelezo)
© Come here (amri)
Kiswahili:
Mfano
(a) Mtoto amekula? (swali)
(b) Mama ameenda sokoni (maelezo)
© Kimbia (amri)
Aristotle: Pia alichangia kwa kuongeza aina ya maneno ambayo ni kiungo na njeo. Aliainisha Kiungo kuwa ni neno lolote ambalo sio Nomino wala Tendo. Akaongezea njeo kwa kuzingatia kuwa zilibadili umbile na kitenzi cha kigiriki. Katika uwanja wa kitenzi alitofautisha mtenda na kitenzi na kutofautisha sentensi na vitenzi hivyohivyo. Pamoja na uainishaji huu aliainisha aina mbili za vitenzi ambavyo ni kitenzi elekezi na si elekezi. Udhaifu wake ni kuwa aliainisha njeo kwa kuzingatia lugha ya kigirikibila kuangalia lugha zingine duniani mfano lugha za kibantu na lugha za kihindi.
Mchango wake mkubwa katika sarufi ya leo dhana za njeo na kiungo bado zinatumika. Mfano katika kiswahili, kiungo ni kiunganishi ambacho kinaunganisha neno na neno, mfano baba na mama, na njeo ni dhana inayoonyesha wakati katika tungo.
Mfano;
-Mama anapika (wakati ujao)
-Mvua itanyesha (wakati ujao)
-Mwalimu alikuja (wakati uliopita)
Mifano hii inapatikana katika lugha ya kiswahili, pia dhana ya uelekezi na si elekezi hujitokeza katika sarufi ya kiswahili.
Mfano; Juma amelala (si elekezi) kwa sababu kitenzi hiki hakihitaji maelezo zaidi.
Mtoto amelalia (elekezi) kwa sababu kitenzi hiki kinahitaji maelezo zaidi ili msikilizaji apate maana iliyokusudiwa.
Dionysius Thrax: Yeye alitenga aina nane za maneno katika lugha ya kigiriki, maneno hayo ni kama vile nomino,kitenzi, faridi peke, kielezi, kiungo,kibainishi, kihusishi, na kibadala.aliona kuwa neno ndio mwanzo na maelezo ya kisarufi na sentensi kuwa ndio kikomo cha maelezo ya sarufi. Pia aliipa sentensi maumbo mawili, umbo la ndani na umbo la nje. Kwake umbo la ndani ndio lenye kufafanua maana ya sentensi na umbo la nje linatokana na mageuzo ya umbo la ndani.
Udhaifu wake ni kuwa hakuangalia kategoria ya kivumishi katika uainishaji wake ambapo lugha nyingi duniani zina aina hii ya maneno.
Licha ya udhaifu huu lakini kimsingi aina hizi alizoziainisha zinatumika katika lugha nyingi dunianiikiwemo lugha ya kiswahili. Pia dhana ya umbo la nje na la ndani linajitokeza katika lugha ya kiswahili.
Mfano; Juma amempiga mtoto (umbo la nje)
Mtoto amepigwa na Juma (umbo la ndani)
Apollonius: Mtaalamuhuyu anaelezea uhusiano kati ya nomino, hasa kati ya kitenzi na nomino na kati ya maneno haya na maneno mengine ambapo lugha nyingi duniani zinaangalia mahusiano ya karibu ya dhana hizi mbili yaani nomino na kitenzi.
Udhaifu wa hoja za mtaalamu huu ni kuwa alijikita zaidi katika kuangalia uhusiano kati ya kitenzi na nomino bila kutilia maanani uhusiano baina ya maneno mengine mfano kivumishi na kielezi.
Licha ya udhaifu wake kimsingi maelezo yake ya uhusiano yalijenga misingi ya ufafanuzi na maana ya miundo ya lugha.
Varro: Ni mmoja ya wanasarufi mashuhuri kabisa wa wakati huo. Anasifika kwa kutenga viambishi na minyumbuliko katika maumbo ya maneno. Udhaifu wake ni kwamba alijikita sana katika minyumbuliko zaidi kuliko dhana nyingine kama vile uambatizi.
Ubora wake ni kuwa dhana ya viambishi na mnyumbuliko bado zinatumika katika sarufi ya kiswahili.
Mfano; M-toto a-na-pik-a (viambishi)
Pika, pikia, pikika (mnyambuliko)
Priscian: Ni mtaalamu aliyekuwa mashuhuri kuliko wote, yeye alitunga vitabu kumi na nane.
Alitafriri msamiati wa sarufi ya kigiriki na kuitumia kuelezea lugha ya kilatini. Pia alitoa maelezo ya kutosheleza na yenye nidhamu kuhusu maumbo.
Udhaifu wa mtaalamu huyu ni kuwa alijikita zaidi katika kutafsiri msamiati wa kigiriki kwenda lugha ya kilatini bila kuangalia lugha nyingine duniani.
Ubora wake ni kwamba kutokana na kuandika vitabu kumi na nane ilisaidia kutoa mwanga kwa waandishi wachanga waliokuwa wakiibuka kwa wakati huo na kupelekea mapinduzi katika sarufi mapokeo na kuibuka kwa sarufi mambo leo.
Kwa kuhitimisha tunaweza kusema kuwa licha ya sarufi mapokeo kuwa na mapungufu lakini sarufi hii ndio chemchem na chachu ya kuibuka kwa sarufi elekezi na fafanuzi ambayo ilifanya wataalamu mbalimbali kujikita katika uwanja huu wa sarufi.
|
|
|
USAYANSI WA ISIMU |
Posted by: MwlMaeda - 12-03-2021, 12:37 PM - Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha
- No Replies
|
|
Wanaisimu waliochunguza lugha waliyumbishwa na mitazamo na mielekeo yao ndipo wakaona haja ya kuichunguza kisayansi.
SIFA ZA UCHAMBUZI WA LUGHA KISAYANSI
(1) Uwazi
Hii inawataka wanaisimu kuweka hoja zao wazi bila hofu yoyote ile. Hii ina maana ya kwamba mada ya uchunguzi yafaa kuelezwa kwa undani kabisa. Yote ambayo wanaisimu watayasema kuhusu mada yawe kwa uwazi na kwa njia ya kueleweka kwa urahisi. Kwa mfano mawanda aliyoyatumia katika kazi yake yawe na uwazi na ukamilifu ambao unafaa kuzingatiwa katika uwekaji wa maneno, utengaji wa hoja na hata uchunguzi wa data.
(2) Upangilifu na utaratibu maalum
Hoja zote zinapaswa kupangwa vizuri katika
taaluma zote za kisayansi, kwa utaratibu maalum mambo yote hufuatwa hatua kwa hatua. Wanaisimu
hufuata utaratibu katika kuchambua kazi yake ifaavyo.Mwanaisimu hatakiwi kufanya
kazi yake kiholela holela.
(3) Uchechefu
Hapa ni pale wanaismu wanapofaulu
kueleza tofauti zote zilizomo katika kongoo linalochunguzwa hatimaye katika
lugha hiyo yote.
(4) Wanaisimu kuweza kuifafanua kazi yao jinsi inavyotakikana
Hii ni hatua ambapo mwanaisimu
anapofanikiwa kuifafanua kazi yake kwa undani kabisa, katika viwango
vyote.Viwango hivi ni kama vile vya kifonolojia, mfumo wa sauti na kimofolojia.
(5) Mwana isimu anafaa kuichunguza kazi yake kwa kina kabisa
Mwanaisimu anapofanikiwa kueleza yale yote ambayo
ametafiti kwa kina, bila kuacha au kupuuza kitu chochote anachochunguza.
|
|
|
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO ' STAHILI' |
Posted by: MwlMaeda - 12-03-2021, 12:11 PM - Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili
- No Replies
|
|
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO ' STAHILI'.
Stahili katika lugha ya Kiswahili ni kitenzi na nomino.
Katika kategoria ya kitenzi, neno hili (stahili) lina maana zifuatazo:
1. Kuwa na sifa ya kupata jambo fulani aghalabu kutokana na hicho ulichokifanya; faa.
2. Wajibika kutokana na jambo ulilolifanya au kulisababisha.
Ima katika kategoria ya nomino, neno hili (stahili) lina maana ya "hali inayomfanya mtu afikwe na jambo jema au baya".
Lakini katika lugha ya Kiarabu, neno hili (stahili) linakuwa na maana mbili tofauti kutokana na utamkaji wa herufi 'h'; pale herufi 'h' inapotamkwa kama 'h' kavu (dry 'h') kama ile iliyopo katika neno 'Alhamdu' na pale inapotamkwa kama herufi 'h' ya kawaida ile iliyopo katika neno 'hujambo'.
Kama ikiwa ni herufi 'h' kavu, basi neno (stahili) linakuwa linatokana na kitenzi cha Kiarabu istahaala (-mekuwa muhali/ugumu,uzito), na ikiwa ni 'h' ya kawaida neno hili linatokana na kitenzi 'ista-a-hala' (amestahiki).
Aidha,neno hili 'stahili' lilipoingia katika lugha ya Kiswahili, limejifunga na ile maana ya kustahiki tu wakati ikiitupa ile maana ya kuwa "muhali".
Shukran sana.
Khamis S.M. Mataka.
|
|
|
DHANA NA HISTORIA YA SARUFI MAPOKEO |
Posted by: MwlMaeda - 12-03-2021, 12:07 PM - Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha
- No Replies
|
|
Dhana na historia ya sarufi mapokeo
Dhana ya Sarufi
Sarufi ni kanuni, sheria au taratibu zinazotawala lugha katika matumizi yake ambayo hujumuisha matamshi, maumbo, miundo na maana (Saluhaya, 2010:72).Massamba na wenzake (1999) Sarufi ni kanuni, sheria au taratibu zinazotawala kila moja kati ya viwango vinne vya lugha ambavyo ni umbo-sauti (fonolojia), umbo-neno (mofolojia), miundo maneno (sintaksia) na umbo maana (semantiki).Matinde (2012:211) Sarufi ni taaluma ya lugha inayochunguza na kuchanganua vipashio na kanuni mbalimbali zinazotawala muundo wa lugha.Massamba (2004) anasema, sarufi ni taaluma ya lugha inayohusu uchunguzi na uchanganuzi wa kanuni za vipengele mbalimbali vya lugha.Kwa ujumla sarufi inaweza kuelezwa kama kanuni, sheria na taratibu zinazomuongoza mzungumzaji au mwandishi kuzungumza au kuandika tungo sahihi zinzoeleweka kwa msikilizaji wa lugha ileile. Kama ni mzawa wa lugha, mtumiaji huwa tayari anazo kanuni hizo (hata katika uzungumzaji), yaani kanuni anakuwa nazo akilini baada ya kusomaau kuishi na watu wa lugha hiyo.
Dhana na historia ya sarufi mapokeo. Kwa mujibu wa Massamba na wenzake (1999) wanaeleza kuwa, sarufi mapokeo ni sarufi elekezi ikisisitiza usahihi wa lugha kwa kuonesha sheria ambazo hazina budi kufuatwa, mathalani kufanya muundo fulani wa sentensi usomeke kwa usahihi au sheria ambazo hazina budi kufuatwa ili kufanya matamshi fulani yakubalike kuwa ndio sahihi.Matinde (2012:211) anaeleza kuwa, mkabala huu wa sarufi mapokeo ni mkabala wa awali ulioshughulikia sarufi ya lugha. Waasisi wake walikuwa wanafalsafa wa Ugiriki. Habwe na Karanja (2004:129) anataja wanafalsafa hao kuwa ni Plato, Aristotle, Dionysus Thrax, na Priscian. Katika kipindi hiki sarufi ilishughulikiwa sambamba na falsafa, dini, fasihi, balagha na mantiki. Plato alikuwa wa kwanza kugawa sentensi katika sehemu kuu mbili mtenda (subject) na kitendwa (object). Hatimaye Aristotle akaendeleza kazi ya mwalimu wake kwa kugawa sentensi katika sehemu kuu tano ambazo pia ndizo aina za maneno; nomino, kitenzi, kivumishi, kiunganishi na kielezi.Miaka ya 100 K.K, mwanasarufi Myunani Dionysus Thrax aliandika kitabu cha sarufi ambacho ni cha awali kabisa kilichoitwa “Techne Grammatike (The Art of Grammar)”. Mwanasarufi huyu aliainisha sehemu saba za sentensi ambazo ni nomino, kitenzi, kivumishi, kiwakilishi, kiunganishi, kielezi na kiingizi.
Dhana ya Neno Habwe na Karanja (2007:71) wanafafanua kuwa, neno ni kipashio cha kiisimu kinachoundwa na mofimu moja au zaidi.Saluhaya (2010:135) anadai kuwa, neno ni mkusanyiko wa sauti zinazotamkwa au kuandikwa kwa pamoja na kuleta maana.Massamba na wenzake (1999:43) katika samikisa wakitilia maanani maelezo ya Lyons (1968:194-208), neno linaweza kufafanuliwa katika misingi ya kiumbo-sauti (yaani, kwa kuchunguza sauti zinazounda umbo zima), kiothografia (yaani kwa kuchunguza herufi zinazotumika katika kuliandika umbo hilo), na kisarufi(yaani kwa kuchunguza kile kinachowakilishwa na umbo husika katika lugha).Hivyo basi, tunaweza kufasili neno kama silabi au mkusanyiko wa silabi (sauti) unaoandikwa au kutamkwa ili kuleta maana. Maana hiyo yaweza kuwa kamili, yaani inayotoa taarifa kamili au isiwe kamili, yaani ambayo haitoi taarifa kamili kwa msomaji au msikilizaji.
Dhana ya Sentensi Matinde (2012:157) anafafanua sentensi kuwa ni neno au fungu la maneno lenye uarifishaji mkamilifu. Sentensi huwa na muundo uliokamilika na hujitegemea kimaana.Kwa ujumla sentensi ni kipashio kikuu katika tungo chenye uwezo wa kutoa taarifa iliyo kamili au isiyo kamili na huwa na muundo wa kiima na kiarifu.Ufafanuzi wa aina za maneno kwa mujibu wa wanasarufi wa kimapokeoWataalamu wengi wa sarufi ya Kiswahili sanifu wanaelekea kukubaliana kwamba katika lugha hii kuna aina za maneno zisizopungua saba. Aina hizi za maneno zimewahi kujadiliwa kwa kina katika vitabu kadhaa vya sarufi vinavyojishughulisha na sarufi miundo na sarufi maumbo. Baadhi ya wataalamu wa sarufi mapokeo waliojadili aina hizo ni Kapinga (1983), Nkwera, Tumi, Mohamed, Massamba na wenzake (1999) na Kihore na wenzake (1999). Aina hizo ni pamoja na:
Nomino
Nomino ni jina linalotaja kitu, kiumbe, hali, dhana au tendo lolote liwalo. Tukiyachunguza kwa makini maelezo haya tunaona kwamba yanaashiria kuwa katika uamilifu wake nomino hufanya kazi ya kukipambanua au kukibainisha kitajwa kwa madhumuni ya kukitofautisha na vitajwa vingine. Kwahiyo nomino si mtajwa tu bali pia ni mtajwa bainishi.Katika sarufi za kimapokeo, nomino zilijulikana kama majina lakini katika sarufi za kisiku hizi neno jina au majina limeonekana kuwa la kawaida mno na kwamba haliwezi kuwa na mashiko yenye kukidhi mahitajio ya kiistilahi. Kwahiyo neno nomino limependekezwa litumike badala yake (Massamba na wenzake, 1999:39 katika Samikisa. Wanasarufi mapokeo wameweka migawanyo ya nomino kama ifuatavyo:a) Nomino jumuishi – hizi ni nomino zinazohusu majina ambayo hayakibainishi wazi kitu kinachotajwa. Kwa mfano mbuzi, gari, chuo, mtu, kalamu na nyumba.b) Nomino mahususi – ni yale majina ambayo yanataja vitu, dhana, na viumbe fulani maalumu na kwa kutoa ubainishi ambao ni wa wazi zaidi. Baadhi ya nomino mahususi ni kama vile Masalu, Ijumaa, Februari, Mwanza, Mariam, Herman, Viktoria, Tanzania na Rufiji.c) Nomino kikundi – hizi ni nimino ambazo huhusu majina yanayotaja vikundi kadhaa vya viumbe. Katika nomino hizi, jina moja huwa linataja jumuiya yenye sifa za namna moja. Kwa mfano baraza, jeshi, familia, shule, bunge, genge, mahakama, kombania na kwaya.d) Nomino dhahania – ni nomino zinazohusu majina ya vitu, dhana, na viumbe ambavyo kiukweli tunaweza kuviona katika akili tu lakini hatuwezi kuvibainisha kwa macho. Kwa mfano Uchawi, uzee, malaika, mizimu, Mungu ,usingizi na uchovu.e) Nomino mguso – ni nomino zinazohusu majina ya vitu ambavyo tunaweza kuviona kwa macho na kuvitambua katika uyakinifu wake, na utambumbuzi huu huweza kutokana na kuvigusa, kuvishika au kuvionja kama vile asali, chumvi, kiti, tofali, na tonge.f) Nomino za hesabu – hili ni kundi la nomino ambalo hutumia kigezo cha uwezekano wa kuhesabika katika uainishaji wake. Hapa tunatofautisha kati ya nomino zinazowakilisha vitu vinavyohesabika na vile visivyohesabika. Nomino za vitu vinavyohesabika ni kama vile watoto, vitu, visu, mifuko na viatu. Nomino zisizohesabika hurejelea vitu ambavyo hutokea kwa wingi na haviwezi kugawika, kwa mfano makamasi, mafuta, maji, matope, sukari, mchanga, uji, na nywele.
Vitenzi
Ni aina ya neno linalotoa taarifa juu ya tendo linalofanyika au linalotendwa na kiumbe au kitu. Wanasarufi mapokeo wamevigawa vitenzi katika aina kuu tatu ambazo ni:a) Kitenzi kikuu – ni kitenzi ambacho kinaweza kujitokeza peke yake katika sentensi. Mfano anakula, anampiga, tunacheza, wamechoka na anaimba.b) Kitenzi kisaidizi – ni kitenzi ambacho kinaandamana na kitenzi kikuu katika sentensi. Kwa mfano alikuwaanalima, tunapenda kusoma, na amechoka kucheza. Hivyo, maneno yaliyo katika hati mlazo ni vitenzi visaidizi.c) Kitenzi kishirikishi – ni kile cha umbo ni na si ambacho kinachukuliwa kuwa kinashirikisha vipashio vingine katika sentensi. Kwa mfano Kahigi ni mwalimu bora, huyu msichana si mwerevu.
Vivumishi
Ni kipashio ambacho hutoa maelezo zaisi juu ya nomino au kiwakilishi chake. Maelezo kama hayo kwa kawaida huwa namna au jinsi nomino ilivyo, yaani inavyoonekana, inavyofikiriwa, tabia, au idadi yake. Mfano wa vivumishi ni kama vile chafu, dogo, refu, vivu, zuri, embamba, na fupi. Vivumishi vimeweza kugawanywa katika aina kuu zifuatazo:a) Vivumishi vya sifa – ni vivumishi vinavyotaja tabia au namna vitu vilivyo au vinavyoonekana. Kwa mfano ema, nyenyekevu, pole na katili.b) Vivumishi vya idadi – ni vivumishi vinavyoonesha jumla au hesabu ya vitu. Aina hii ya vivumishi tunaweza kuigawa katika makundi mawili ambayo ni kundi linaloonesha idadi kwa jumla na kundi linaloonesha idadi kwa hesabu. Kwa mfano ingi, chache, haba na kidogo vilievile tano, tisini, elfu , milioni na tatu.c) Vivumishi viulizi – ni vivumishi vinavyouliza maswali kuhusiana na nomino inayoandamana navyo. Mfano watu wangapi, miti mingapi, mayai mangapi, watoto wangapi, na viti vingapi.d) Vivumishi vya pekee – ni maumbo enye na enyewe ambayo katika Kiswahili ndiyo tu huchanganya aina na viambishi vya upatanisho wa kisarufi vinavyojitokeza navyo kimatumizi. Mfano m-tu m-refu, m-ti mrefu, miti mirefu.
Viwakilishi
Ni aina mojawapo ya maneno katika sarufi ya lugha ambayo uamilifu wake ni kuwakilisha nomino katika miktadha mbalimbali. Kwa mfano viwakilishi nafsi, viwakilishi viashirii, viwakilishi viulizi, viwakilishi vimikilishi, viwakilishi vya idadi na viwakilishi jumla.
Viunganishi
Ni neno linalotumika kuviweka pamoja vipashio mbalimbali ili kuvifanya viwe kipashio kikuu kimoja. Kwa mfano na, au, wala, na lakini katika sentensi zifuatazo:Baba na Mama wanalima.Unapenda chai au uji.Hana huruma wala upendo.Wanasarufi mapokeo wamevigawa viunganishi katika makundi makuu mawili kwa kuzingatia msingi wa kimaana kama vile viunganishi vya hadhi sawa na viunganishi vihusishi.
Vielezi
Ni neno linalotumika kuelezea zaidi juu ya kitenzi. Mfano sana, mno, kabisa, polepole, harakaharaka, zaidi, sawasawa na barabara. Wanasarufi mapokeo wameviainisha vielezi katika aina kuu mbili yaani vielezi halisi na vielezi viingizi. Mfano wa vilelezi halisi ni kama vile mno, sana, bure, hasa, kabisa, ovyo, haraka na sasa. Kwa upande wa vielezi viingizi ni kama vile pu, mwa, na bwe .
Viingizi
Ni aina ya maneno inayodokeza hisia za msemaji kama vile ya hali yake ya kufurahi, kushangaa, kushtuka, na uchungu. Haya ni maneno kama vile Lo! Alaa! Lahaula! na Aa! Maneno kama haya kwa kawaida huwa yanatumika kabla ya sentensi na aghalabu huwa hayana mfungamano wa kisarufi na sentensi inayofuata. Aina hii ya neno pia huitwa vihisishi. Jina vihisishi limekitwa zaidi katika misingi ya kimaana yaani linahusu zaidi hisia mbalimbali zinazobebwa na maneno hayo. Viingizi navyo vimegawanywa katika makundi mawili nayo ni viingizi halisi na viingizi vya taswira.
Ufafanuzi wa aina za sentensi kwa mujibu wa wanasarufi mapokeo
Kwa upande wa sentensi, wanasarufi mapokeo wanaainisha aina tatu za sentensi kwa kuzingatia uamilifu wake. Aina hizo ni kama zifuatazo:i) Sentensi taarifa – hizi ni sentensi zenye kutoa taarifa fulani.Kwa mfano: Kiranja amechelewa kufika shuleni.Kahigi kaandika kitabu cha sarufi ya Kiswahili.ii) Sentensi ulizi – aina hii ya sentensi huwa ina pengo katika sehemu yake ya taarifa. Sentensi hizi hutaka kupata taarifa fulani.Kwa mfano: Adam ameweza kucheza mpira?Kalamu yako ni ipi?iii) Sentensi Agizi – aina hii ya sentensi humuingiza msikilizaji kutenda kitendo fulani. Aghalabu sentensi ya aina hii haina sehemu ya kiima.Kwa mfano: Toka nyuma uende mbele.Mwite kiranja wako.Kwa ujumla, wanasarufi mapokeo kwa kiasi fulani wanatofautiana katika uainishaji wa aina za maneno kwani kuna wengine wametaja aina kumi za maneno badala ya saba. Kwa mfano Habwe na Karanja (2004:130-139) wao wanaainisha aina kumi za maneno ambazo ni nomino, vitenzi, viwakilishi, vivumishi, vielezi, vihusishi, viunganishi, vionyeshi, vihisishi na vibainishi. Hivyo ni vigumu kutambua idadi halisi ya aina za maneno kwa mujibu wa sarufi mapokeo.
MAREJELEO
Habwe, J. & Karanja, P. (2004). Misingi ya Sarufi ya Kiswahili.Nairobi: Phoenix Publishers.Habwe, J. & Karanja, P. (2007). Misingi ya Sarufi ya Kiswahili.Nairobi: Phoenix Publishers.Kapinga, M.C. (1983). Sarufi Maumbo ya Kiswahili Sanifu. Dar es Saalam: TUKI.Massamba, D.P.B na Wenzake (1999). Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu (SAMIKISA); Sekondari na Vyuo. Dar es Saalam: TUKI.Matinde, R.S. (2012). Dafina ya Lugha, Isimu na Nadharia; Kwa Sekondari, Vyuo vya Kati na Vyuo Vikuu. Mwanza: Serengeti Educational Publishers (T) LTD.
|
|
|
Swali: Sarufi miundo virai inatofautianaje na sarufi geuzi? |
Posted by: MwlMaeda - 12-03-2021, 12:01 PM - Forum: Maswali na majibu
- No Replies
|
|
Swali: Sarufi miundo virai inatofautianaje na sarufi geuzi?
DHANA YA SARUFI
Sarufi ni taaluma ya lugha inayochunguza na kuchanganua vipashio na kanuni mbalimbali zinazotawala muundo wa lugha, (Matinde, 2012.
Sarufi ni utaratibu wa kanuni ambazo humwezesha mtumiaji wa lugha kutunga tungo sahihi zinazoeleweka mara zinapotamkwa. (Kapinga, 1983).
Dhana ya sarufi inatafsiriwa katika mitazamo tofauti lakini yenye kuhusiana. Mtazamo wa kwanza tunaweza kusema Sarufi ni taaluma ya uchambuzi walugha inayojumuisha viwango vyote vya uchambnuzi yaani kiwango cha umbo sauti (fonolojia), kiwango cha umbo neno (fonolojia), kiwango cha miundo maneno (sintaksia) na kiwango cha umbo maana(semantiki), (Massamba, 1999).
DHANA YA SARUFI MIUNDO VIRAI
Sarufi muundo virai ni mkabala wa kimapokeo ambao haujihusishi na sarufi miundo katika marefu na mapana yake, ambapo zilijihusisha sana na sentensi sahili, (Massamba 1999).
Sarufi muundo virai ni kitengo cha sarufi geuza maumbo zalishi, ambacho hujikita katika matumizi ya sheria chache kuzalisha sentensi nyingi zisizo na kikomo, ambazo zina usarufi na hata zile ambazo hazijawahi kutungwa, ( Matinde, 2012).
Sarufi muundo virai ni mpangilio wa vitu vidogo vilivyowekwa pamoja na kujenga kitu kikubwa zaidi. Sarufi miundo virai ni mkabala wa kuchambua lugha kwa kuigawa sentensi katika virai vinayoiunda na kasha kuvichanganua zaidi hadi kufikia neno mojamoja lililokiunda kirai, (Massamba, 2001).
DHANA YA SARUFI GEUZI
Ugeuzi ni utaratibu unaotumiwa kubadili umbo la tungo kuwa umbo jingine kwa kutumia kanuni maalumu. Kwa hiyo ugeuzi ni mbinu ya kisarufi ambayo hutumiwa katika sarufi geuza maumbo zalishi kuzalisha sentensi lukuki kwa kufuata sheria mahususi, (Matinde, 2012).
Sarufi geuzi hueleza ujuzi wa lugha ambao msemaji mzawa anao ujuzi anaomwezesha kutumia lugha (Habwe na Karanja,2007).
Sarufi geuzi maumbo ni utaratibu wa kubadili maumbo kuwa maumbo meng kwa kufuata kanuni maalumu (Matinde,2012).
Zifuatazo ni tofauti kati ya sarufi miundo virai na sarufi geuzi:
Hutofautiana katika lengo. Lengo la sarufi muundo lilikuwa halifahamiki zaidi ya kutumia taratibu za kijarabati zinazohusu ukusanyaji wa data na kuzichambua pamoja na kuunda kanuni kwa kutumia data hizo. Lakini,
Lengo la sarufi geuzi liko bayana, hujitokeza dhahiri. Lengo la sarufi hii ni kufafanua umilisi wa ujuzilugha ambao huwa mwanalugha anao. Umilisi huo humfanya mwanalugha kutambua viambajengo kati ka tungo, katika mtazamo wa ndani yaani muundo wa ndani.
Hutofautiana katika miundo. Sarufi miundo virai, hii huwa inajikita katika miundo ya nje, ambayo huchunguza na kuchambua sentensi katika umbo la nje.
Mfano; Mama anakula ugali
Hivyo huonyesha tu aina ya maneno husika katika sentensi au tungo kama vile: Mama- Nomino, Anakula- Kitenzi, na Ugali- Nomino. Ilihali,
Sarufi geuzi, hii huwa imejikita katika kuchungaza sentensi kama umbo la ndani na umbo la nje. Muundo wa ndani ni uchopekwaji katika miundo hiyo ambapo muundo wan je lazima upitie katika muundo wa mofofonemiki na kuweka katika kitengo cha fonolojia.
Hutofautiana katika vitengo. Sarufi geuzi ni sarufi ambayo inafumbata vitengo vyote vya lugha ambavyo ni fonolojia, sintaksia, semantiki, na mofofonemiki ambapo kitengo cha fonolojia hushughulikia sauti za lugha, kitengo cha kisintaksia hushughulika na uundaji wa sentensi, kitengo cha semantiki hushughulika na ufasili wa maana, na kitengo cha mofofonemiki huwa na kazi ya kuibadili njeo za wakati. Ilihali
Sarufi miundo virai hufumbata kitengo cha mofolojia ambapo sentensi iligawanywa katika kiunzi cha aina za maneno kama Nomino, Kitenzi, Kivumishi, Kielezi na kihunzi hicho kilijulikana kama utaratibu wa uchanganuzi wa viambajengo.
Hutofautiana katika uhusiano wa sentensi. Sarufi geuzi ilipiga hatua kubwa, kwanza huonyesha uhusiano uliopo kati ya maumbo mbalimbli ya sentensi au tungo. Na pia kuonyesha uhusiano unaoweza kuwepo baina ya sentensi moja na sentensi nyingine.
Mfano: (1) Mtoto mrefu anacheza, na si kusema kuwa Mtoto anacheza mrefu
Huu ni uhusianao kati ya maumbo.
Mfano: (2) Juma alipiga mpira
Mpira ulipigwa na Juma
Huu ni uhusiano wa sentensi moja na sentensi nyingine. Ilihali
Sarufi miundo virai haionyeshi uhusiano kati ya sentensi moja na sentensi nyingine.
Hutofautiana katika uwazi. Sarufi geuzi huonesha sentensi sahihi na ambazo sio sahihi pia huonesha sentensi ambazo zinakubalika na sentensi zisizokubalika kwa msemaji mzawa. Ilihali
Sarufi miundo virai yenyewe haina uwazi huo.
Hitimisho ni kwamba, Sarufi geuzi ilianzishwa kutokana na mapungufu katika sarufi muundo virai. Sarufi iliyokuwepo, sarufi miundo virai, ilishindwa kuonyesha mahusiano yaliyokuwepo baina ya sentinsi zinazo husiana kimaana. Hivyo kutokana na upungufu huo kulikuwa na haja ya kuonyesha uhusiano huo.
MAREJELEO
Kapinga,M.C.(1983). Sarufi Maumbo ya Kiswahili Sanifu (SAMAKISA). Dar-es-Salaam:
TUKI.
Massamba, D.T., Kihore,M.Y.& Hokororo.(1999). Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu
(SAMIKISA). Dar-es-Salaam: TUKI.
Matinde,S.R.(2012). Dafina ya Lugha Isimu na Nadharia. Mwanza: Serengeti Educational
Publishers (T) LTD.
|
|
|
MATUMIZI YA PO NA JI |
Posted by: MwlMaeda - 12-03-2021, 07:21 AM - Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha
- No Replies
|
|
PO ya Mahali
1. Mahali alipoanguka paliacha kuota nyasi.
2. Hapo ndipo tulipoketi. Jumapili ifikapo tutakwenda Kisetoni.
PO ya Wakati
1. Nilipomlilia aliisikia sauti ya dua langu.
2. Kitumbua kilipikwa mayai yalipoletwa.
3. Zitakaporudishwa tutazificha mbali.
PO ya Hisia (Hasira)
1. Umenikosea sana! Po! Utakiona cha mtema kuni.
Matumizi ya JI
1. Kuunda nomino kutokana na kitenzi.
1. sema => msemaji.
2. kimbia => mkimbiaji
Kuonesha Ukubwa
1. Jikapu lile lina jitunda kubwa.
2. Jito lile limemeza watu wengi.
Kuonesha mtendaji anapokuwa mtendewa (kujitenda, kujitendea)
1. Amejikwaa kidole cha kati.
2. Kitabu kimejifungua chenyewe.
|
|
|
|