UTANGULIZI WA LUGHA NA ISIMU: MUHADHARA WA KUMI : AINA ZA MANENO NA UAINISHAJI WAKE - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Chuo (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=3) +---- Forum: Shahada (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=20) +----- Forum: Nukuu (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=22) +----- Thread: UTANGULIZI WA LUGHA NA ISIMU: MUHADHARA WA KUMI : AINA ZA MANENO NA UAINISHAJI WAKE (/showthread.php?tid=1629) |
UTANGULIZI WA LUGHA NA ISIMU: MUHADHARA WA KUMI : AINA ZA MANENO NA UAINISHAJI WAKE - MwlMaeda - 12-01-2021 MUHADHARA WA KUMI : AINA ZA MANENO NA UAINISHAJI WAKE
Maana ya Nonimo :
Nomino ni istilahi inayopewa maneno yanayotaja vitu, hali, mahali au viumbe ili kuviainisha na kuvitofautisha.
Aina za nomino:
Maana ya kivumishi:
Vivumishi ni maneno yanayofanya maneno mengine yavume. Vivumishi huvumisha kuhusu sifa, idadi, mahali, n.k kuhusu nomino.
Aina za vivumishi.
Vivumishi vya aina hii hutoa taarifa kuhusu idadi ya nomino ambazo kiwango chake kimetajwa.
Vivumishi vya idadi vinavyoweza kuvumisha nomino kwa kutaja idadi ya nomino hizo kiujumlajumla bila kudhihirisha idadi halisi.
Vivumishi vya idadi ambavyo huonesha nafasi iliyochukuliwa na nomino fulani katika orodha.
Maana ya vielezi:
Vielezi ni maneno yanayofafanua vitenzi, vivumishi au vielezi vingine. Huweza kuarifu kitendo kilichotendeka kilitendeka wapi, namna gani na hata mara ngapi?
Aina za vielezi
Vielezi vya namna halisi. Hivi ni vielezi vinavyotumia maneno ambayo kimsingi yana sura ya vielezi moja kwa moja katika uainishaji wa aina za maneno.
Vielezi vya namna. Hivi ni vielezi ambavyo hutumika kufananisha vitendo na vivumishi au nomino mbalimbali. Hujengwa kwa kuongeza kiambishi (ki-) au kiambishi (vi-). Viambishi hivi hujulikana kwa jina la viambishi vya mfanano. Ulifanya vizuri kumsaidia mwanangu. -Vielezi vya namna vikariri, hivi ni vielezi ambavyo hufafanua vitenzi kwa kurudiarudia neno moja mara mbili. – Vielezi vya namna hali, Hivi ni vieelezi ambavyo hufafanua juu ya kitendo kilichotendeka kimetendeka katika hali gani. – Vielezi vya namna ala/kitumizi Hivi ni vielezi vinavyotaja vitu ambavyo hutumika kutendea kitendo. – Vielezi vya namna viigizi. Hivi vinaelezea zaidi jinsi tendo lilivyofanyika kwa kuigiza au kufuatisha sauti inayojitokeza wakati tendo linapofanyika au kutokea.
Vielezi vya idadi: hivi huonesha kuwa kitendo kilitendeka mara fulani au kwa kiasi fulani.
Vielezi vya mahali. Vielezi vya namna hii huonesha mahali ambapo kitendo kinatokea.Huweza kudokezwa kwa viambishi au kwa maneno kamili.
Vielezi vya wakati: Vielezi vya namna hii huonesha wakati wa kutendeka kwa kitendo.Huweza kutokea kama maneno kamili au kudokezwa kwa kiambishi {po.}
Maana ya vitenzi:
Kitenzi ni neno linaloeleza jambo lililotendwa au lililotendeka. Kitenzi huarifu tendo lililofanyika au lililofanywa na kiumbe hai chochote kinachoweza kutenda jambo.
Muundo wa kitenzi cha Kiswahili
Kitenzi cha Kiswahili huundwa na mzizi pamoja na viambishi vyenye uamilifu wa aina tofauti.
Aina za vitenzi
v Vitenzi halisi: Hivi ni vitenzi ambavyo huonesha kutendeka kwa kitendo.Wakati mwingine vitenzi hivi huitwa vitenzi vya kutenda.
vitenzi elekezi: Hivi ni vitnzi vya ambavyo vinaweza kuchukuwa kitendwa/kitendewa (Yambwa/Yambiwa). Muundo wake unadokeza kuwa, kuna kitendwa au kitu kinachoelezea tendo hilo.
vitenzi sielekezi: Hivi ni vitenzi ambavyo havichukuwi kitendwa/kitendewa (Yambwa/Yambiwa). Muundo wake haudokezi uwezekano wa kuwepo kwa yambwa/yambiwa. Tendo halielekezwi kwa yeyote.
Aina za vitenzi halisi
v Vitenzi vikuu: Vitenzi vikuu ni vile ambavyo hubeba ujumbe muhimu wa kiarifu cha sentensi.
v Vitenzi visaidizi: Hivi hutoa taarifa ya kusaidia vitenzi vikuu. Hutoa taarifa kama vile uwezekano, wakati, hali n.k. Vitenzi visaidizi daima hutumika na vitenzi vikuu, ndivyo vinavyobeba viambishi vya wakati.
v Vitenzi vishirikishi: Hivi ni Vitenzi vishirikishi ambavyo vilevile sielekezi. Vitenzi hivi hufanya kazi ya kuunga sehemu mbili za sentensi.
Aina za vitenzi vishirikishi
Vitenzi vishirikishi vipungufu: Hivi ni vitenzi vishirikishi ambavyo havichukui viambishi vya nafsi, njeo ama hali. Vitenzi vishirikishi vipungufu ni vya aina mbili, ambavyo ni kitenzi kishirikishi “ni” cha uyakinishi na kitenzi shirikishi “si” cha ukanushi.
Vitenzi vishirikishi vikamilifu: Hivi huchukuwa viambishi viwakilishi vya nafsi, njeo na hata hali.
Kazi za kitenzi kikuu:
kueleza tendo linalofanywa na mtenda/mtendwa.
kuonesha wakati tendo linapotendeka
kuonesha hali ya tendo
Kuonesha nafsi
kuonesha kauli mbalimbali za tendo
Kuonesha urejeshi wa mtenda/mtendwa/ mtendewa/ kujitendea
Kazi za kitenzi kishirikishi
kushirikisha vipashio vingine katika sentensi
Kuonesha tabia fulani iliyopo au isiyokuwepo ya mtu fulani au kitu fullani.
Kuonesha cheo au kazi anayofanya mtu.
kuonesha sifa za mtu.
kuonesha umoja wa vitu au watu
kuonesha mahali
kuonesha msisitizo
kuonesha umilikishi wa kitu chochote.
Aina za wakati katika kitenzi.
wakati uliopita
wakati uliopo
wakati ujao
Hali mbalimbali za kitenzi
– Hali ya masharti
– Hali ya kuendelea kwa tendo
– kuamuru na kuhimiza n.k
Maana ya kiwakilishi:
kiwakilishi neno linaloweza kutumika badala ya jina. Hutokea nafasi ya nomino pindi nomino inapokosekana.
Aina za viwakilishi
Viwakilishi vioneshi/mahali
Mf. Zile,yule,kule,
Viwakilishi vya nafsi ambavyo vipo vya aina tatu; ambavyo ni:
viwaakilishi nafsi huru mf. Mimi,sisi,wewe,yeye,
viwakilishi nafsi viambata mf. Ni,Tu,U,M,A na Wa
viwakilishi nafsi rejeshi mf. Ambaye,ambalo,ambavyo, n.k
Viwakilishi vya kuuliza/viwakilishi viulizi ambavyo huashiriwa na mofu/kiambishi {-pi} ambavyo katika tungo hutanguliwa na kiambishi ngeli cha jina husika.
Viwakilishi vya urejeshi ambavyo vinajengwa na shina -amba- pamoja na vipande vidogovidogo kama –ye-, -o-, -cho-, vyo, lo, po, mo, ko n.k ambavyo vinachaguliwa kulingana na ngeli ya majina inayorejeshwa navyo.
Viwakilishi vya idadi: Viwakilishi hivi hutuarifu kuhusu idadi ya nomino, idadi hiyo huweza kuwa kamili (halisi) au ya jumla.
Viwakilishi vya pekee: Hivi ni aina ya vivumishi ambavyo huwakilisha nomino kwa umaalumu wake. Hufuata sheria za upatanisho za nomino zinazowakilishwa.
Viwakilishi vya A-unganifu: Viwakilishi hivi huundwa kwa kihisishi cha A-unganifu kusimamia nomino inayomilikiwa, inayochukuwa nafasi fulani katika orodha au nomino ya aina fulani. kihisishi a-unganifu huandamana na nomino kuunda kirai husishi ambacho husimama mahali pa nomino.
Viwakilishi vya sifa; Haya ni maneno ya sifa ambayo huchukua nafasi ya nomino katika setensi.
Maana ya viunganishi. Ni maneno, kikundi cha maneno au kiambishi chenye kuunganisha maneno, kirai, kishazi au sentensi. Dhima ya kiunganishi ni kuunga vipashio viwili au zaidi vyenye hadhi sawa kisarufi.
Aina za viunganishi:
v viunganishi huru: hivi ni viunganishi vinavyosimama pekee katika tungo, katikati ya vipashio vinavyoungwa.
Aina za viunganishi huru
Viunganishi nyongeza/vya kuongeza mf. Tena, Na, Zaidi ya n.k.
Viunganishi vya sababu/visababishi Mfano; Kwa kuwa, kwa sababu, kwa vile, kutokana na, n.k.
Viunganishi vya uteuzi/chaguo Mfano; Ingawa, Japokuwa, Lakini n.k.
Viunganishi linganishi/vya kinyume Mfano; Ingawa, Japokuwa, Lakini n.k.
Viunganishi vya wakati Mfano; kisha, baadaye, Halafu, Baada ya n.k.
Viunganishi vya masharti Mfano; Kama, Ikiwa, Iwapo n.k
Viunganishi vihusishi Mfano; Cha, La, Wa, Za n.k.
v Viunganishi tegemezi: ni viambishi ambavyo hutiwa katika kitenzi cha kishazi tegemezi ili kukiunga na kitenzi kikuu cha kishazi huru ambavyo kwa pamoja huunda sentensi changamano au shurtia. Mfano; -ye-, -po-, -ki-, -cho- na -nge-.
Mambo mbalimbali yanayoweza kuoneshwa na vihusishi
huonesha uhusiano wa kiwakati
huonesha uhusiano wa mahali
huonesha uhusiano wa kulinganisha
huonesha uhusiano wa umilikaji
huonesha uhusiano wa sababu/kiini
Aina za vihusishi
vihusishi vya wakati Mfano; kabla ya, baada ya n.k
vihusishi vya mahali Mfano; chini ya, juu ya, ndani ya, mbele ya n.k.
vihusishi vya ulinganishi/ vya kulinganisha Mfano; kuliko, zaidi ya n.k.
vihusishi vya sababu/ kusudi/nia Mfano; kwa sababu ya, kwa ajili ya n.k.
vihusishi vya ala (kifaa) Mfano; kwa
vihusishi vimilikishi Mfano; cha, za n.k
vihusishi vya namna/jinsi/hali Mfano; moto wa kuotea mbali, macho yamviringo
vihusishi ‘na’ cha mtenda
Matumizi ya ziada ya kihusishi “kwa”
kihusishi hiki huonesha mahali au upande
kihusishi hiki huonesha sababu au kisababishi cha jambo
kihusishi hiki huonesha wakati
kihusishi hiki huonesha sehemu fulani ya kitu kikubwa
kihusishi hiki hutumika kuonesha ‘nia ya pamoja na’
Kihusishi hiki huonesha jinsi kitendo kilivyotendeka
Aina za viingizi:
Viingizi vinaweza kugawanywa kwa kutumia vigezo vya kisemantiki. Mkabala huu unatumika kuvigawa viingizi kulingana na maana zinazowakilishwa na viingizi husika. Maana hizo ni hisia zinazobebwa na viingizi hivyo.
v Viingizi vinavyoonesha mhemko au hisiya kali
viingizi vya furaha
viingizi vya huzuni
viingizi vya mshituko
viingizi vya mshangao
v Viingizi vya maamrisho au msisitizo wa jambo au tukio.
v viingizi vya maadili
viingizi vya mwitiko
viingizi vya ombi
viingizi vya bezo
viingizi vya kutakia heri
viingizi vya kukiri afya/jambo
viingizi vya kiapo
viingizi vya salamu
|