MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
KIDATO CHA KWANZA : UFAHAMU

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
KIDATO CHA KWANZA : UFAHAMU
#1
UFAHAMU
Ufahamu ni dhana inayorejelea kujua na kulielewa jambo kwa usahihi na kuweza kulielezea upya kwa usahihi bila kupoteza maana yake ya msingi. Ufahamu wa mtu waweza kupimwa katika kusikiliza jambo au katika kusoma.
Kusikiliza
Ufahamu wa kusikiliza ni zaidi ya kusikiliza tu kile kilichosemwa; badala yake ni uwezo wa mtu kuelewa maana ya maneno anayoyasikia na kuweza kuhusiana nayo kwa namna fulani. Kwa mfano mwanafunzi anaposikiliza hadithi, ufahamu mzuri wa kusikiliza humsaidia kuielewa hadithi hiyo, kuikumbuka, kuijadili, na hata kuisimulia tena kwa maneno yake mwenyewe.
Mambo ya Kuzingatia katika Ufahamu wa Kusikiliza
Elezea mambo ya kuzingatia katika ufahamu wa kusikiliza
Ufahamu wa kusikiliza unahusisha michakato kadhaa katika kuelewa na kupata maana ya kile kinachozungumzwa. Michakato hii inahusisha:
  • Kuelewa vizuri sarufi ya lugha ile inayozungumzwa
  • Kuelewa vyema maana ya maneno ya mhusiaka anayezungumza
  • Kuelewa sintaksia (muundo wa maneno) ya sentensi kwa namna zinavyowasilishwa.
Katika ufahamu wa kusikiliza, msikilizaji hana budi kuzingatia mambo yafutayo:
  1. Kuwa makini na kuelekeza akili yote kwa mzungumzaji ili kuweza kusikia kila anachokisema.
  2. Kutilia maanani vidokezo vya maana ili kubaini iwapo msemaji anaongeza jambo jipya, anatofautisha, anafafanua au anahitimisha hoja.
  3. Msomaji anatakiwa kuandika baadhi ya mambo anayoona kuwa ni ya muhimu ili kumasidia kukumbuka hapo baadae.
  4. Kuwa makini na ishara mbambali za mwili kama vile kurusha mikono, kutingisha kichwa, kutingisha mabega au hata kupepesa macho. Ishara hizi huwa zinachangia kwa kiasi kikubwa kupata maana katika mazungumzo.
  ZOEZI  
Lipi kati ya haya halifanyiki katika ufahamu wa
 kusikiliza?
A
Kuzingatia vidokezi vya maana
B
Kuzingatia ishara
C
Kuzingatia matini
D
Kuandika kwa ufupi yasemwayo
___siyo ishara ya mwili inayopaswa kuzingatiwa na
msikilizaji ili kujibu maswali ya habari iliyosikilizwa?
A
Kutingisha kichwa
B
Kutembea
C
Kutingisha mabega
D
Kupepesa macho
Ni kipi kifanyike ili msikilizaji aweze kubaini mawazo
 makuu katika ufahamu wa kusikiliza?
A
Kuandika kwa ufupi
B
Kufuatilia ishara
C
Kuuliza maswali
D
Kusikiliza kwa makini
Mambo ya msingi yanayozungumzwa katika ufahamu wa
 kusikiliza na yanapaswa kuzingatiwa huitwa___.
A
Ishara
B
Alama za uakifishi
C
Mawazo makuu
D
Misemo
Nini kitatokea endapo msikilizaji hatazingatia matamshi
 ya mzungumzaji katika ufahamu wa kusikiliza?
A
Kubaini mawazo
B
Kufupisha habari
C
Kupotosha maana ya maneno
D
Kutosikiliza
Kujibu Maswali kutokana na Habari uliyosikiliza
Jibu maswali kutokana na habari uliyosikiliza
Kazi 1
Jibu maswali kutokana na habari uliyosikiliza
Kusoma kwa Sauti
Kusoma kwa sauti ni namna ya kuyaangalia maandishi na kuyatamka kwa sauti inayosikika.
Mambo ya Kuzingatia katika Ufahamu wa Kusoma
Elezea mambo ya Kuzingatia katika ufahamu wa kusoma kwa sauti
Kuna vipengele viwili vinavyounda mchakato wa ufahamu wa kusoma:
  • Uelewa wa msamiati na
  • Uelewa wa matini
Ili kuilelewa habari/matini ni lazima msomaji awe na uwezo wa kuelewa msamiati uliotumika katika matini hiyo. Endapo maneno yaliyotumika hayataeleweka vilevile matini yote haitaeleweka.
Katika ufahamu wa kusoma, msomaji anatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo:
  1. Kubaini mawazo makuu; msomaji anaposoma habari fulani au kitabu inatakiwa ajiulize, Je, kinachoongelewa hapa ni nini? Ni jambo gani hasa analolizungumzia mwandishi? Msomaji akiwa na maswali haya akilini mwake basi itakuwa rahisi kwake kuielewa habari hiyo.
  2. Kuzingatia alama za uakifishi; msomaji ni lazima azingatie alama za uakifishi, kwa kufanya hivyo itamsaidia kuelewa ujumbe wa habari hiyo na endapo hatazingatia alama za uakifishaji anaweza kupotosha maana ya mwandishi.
  3. Kubaini maana ya maneno na misemo mbalimbali; habari nyingine huwa zina maneno ya kisanaa hivyo ni muhimu msomaji kubaini maana ya maneno hayo katika muktadha wa habari hiyo, hii itamsaidia kuelewa vyema maana ya mwandishi.
  4. Vilevile msomaji anatakiwa kumakinikia kile anachokisoma, kila kipengele anachokisoma inampasa akielewe vizuri.
Kwa kuzingatia haya yote msomaji atakuwa na uelewa mzuri juu ya habari aliyoisoma na pia anaweza kufupisha habari hiyo aliyoisoma.
  ZOEZI  
Alama za uakifishi zisipozingatiwa katika ufahamu wa kusoma
 hupelekea___.
A
Kuwa makini
B
Kuongeza maneno
C
Kubaini mawazo makuu
D
Kupotosha maana
Ipi siyo kazi ya vidokezi vya maana anavyopaswa kuzingatia
 msomaji katika ufahamu wa kusoma?
A
Kuhitimisha
B
Kutofautisha
C
Kuongeza jambo
D
Kutia chumvi
___siyo jambo la kuzingatia katika ufahamu wa kusoma.
A
Kuzingatia alama za uakifishi
B
Kubaini mawazo makuu
C
Kubaini misemo mbalimbali
D
Kufupisha ufahamu
Zifuatazo ni alama za uakifishi zinazopaswa kuzingatiwa katika
 ufahamu wa kusoma, isipokuwa:
A
Kistari
B
Mubalagha
C
Nukta
D
Alama ya mshangao
Katika ufahamu wa kusoma, msomaji anatakiwa kuandika
pembeni mambo muhimu ili kumsadia___.
A
Kuuliza maswali
B
Kufupisha ufahamu
C
Kukosoa
D
Kukumbuka
Kujibu Maswali kutokana na Habari uliyosoma
Jibu maswali kutokana na habari uliyosoma
Kazi 2
Jibu maswali kutokana na habari uliyosoma
Kusoma Kimya
Kujibu Maswali kutokana na Habari uliyoisoma
Jibu maswali kutokana na habari uliyosoma
Katika usomaji huu, msomaji hufumba kinywa na kupitisha macho katika kila mstari harakaharaka. Macho hayo huunganisha neno lililotangulia na lile linalofuata. Ubongo wake huchambua mambo muimu yanayojitokeza, huku akiyahifadhi kichwani. Mtu akijizoeza kusoma kimya, ananufaika ifuatavyo:
  1. Hupata nafasi ya kupima mwendo wake na kiasi cha welewa
  2. Hujiepusha na lawama ya kusumbua wengine
  3. Hukwepa kuzingatia kanuni za matamshi
  4. Huweza kusoma maandishi mengi kuliko ambavyo angesoma kwa sauti
  ZOEZI  
Ni kipi kati ya hivi husababisha kushindwa kujibu maswali ya habari
uliyoisoma?
A
Kutoelewa maana ya misemo
B
Kuelewa swali
C
Kusoma kwa makini
D
Kusoma kwa utulivu
Ili kujibu maswali ya habari uliyoisoma ni muhimu kujibu kwa ufupi.
Hii husaidia___.
A
Kuwa makini
B
Kuokoa muda
C
Kujibu maswali yote
D
Kutambua maswali magumu
Ili kujibu maswali ya habari uliyoisoma ni sharti kuzingatia yafuatayo,
 isipokuwa:
A
Kuwa mtulivu
B
Kujibu kwa ufupi
C
Kusoma kwa makini
D
Kuunganisha mawazo makuu
Kufahamu maana ya maneno na misemo katika kujibu maswali ya
 habari uliyoisoma inahitaji kuelewa___.
A
Habari nzima
B
Swali lililoulizwa
C
Matamshi
D
Lugha iliyotumika
Nini kifanyike ili kuweza kuelewa uhusiano uliopo kati ya habari
uliyoisoma na maswali?
A
Kusoma kwa makini
B
Kufafanua maana ya maneno
C
Kujibu kwa ufupi
D
Kuuliza maswali
Kusoma kwa Burudani
Huu ni usomaji ambao lengo lake kuu huwa ni kujiburudisha tu. Katika usomaji wa aina hii, msomaji hujisomea zaidi magazeti, majarida na vitabu tofauti na vile vinavyotumika darasani.
Mambo ya Kuzingatiwa katika Ufahamu wa Kusoma kwa Burudani
Fafanua mambo ya kuzingatiwa katika ufahamu wa kusoma kwa burudani
Wakati mwingine sio lazima msomaji awe na vitabu vyote ambavyo anahitaji kuvisoma au magazeti na majarida. Inapotokea hivyo, msomaji anaweza kwenda maktaba kuazima kitabu nachokihitaji.
Ingawa lengo la msomaji huwa ni kujiburudisha tu, lakini pia hujiongezea maarifa. Hii ni kwa sababu, magazeti, majarida na vitabu sambamba na kutuamia lugha sanifu huelezea mambo mabalimbali yanayoihusu jamii.
Hivyo msomaji kutokana na kusoma vitabu na majarida mbalimbali hujiongezea kiwango cha welewa wa lugha na mambo mengine ya kijamii yanayojadiliwa humo.
Ni jambo zuri kwa msomaji kujijengea tabia ya kujipima ili aweze kuelewa kiwango cha maarifa aliyopata katika kujisomea. Kujipima huku kunaweza kufanywa kwa kujiundia utaratibu wa kuweka kumbukumbu ya vitu au makala zilizosomwa na kufanya ufupisho wa kila makala.
Utaratibu unaopendekezwa katika kujipima na kujiwekea kumbukumbu ya usomaji wa burudani ni kama ufuatao:
  1. Tarehe…
  2. Jina la kitabu/makala/gazeti….
  3. Mchapishaji……
  4. Mwaka/tarehe ya uchapishaji…..
  5. Ufupisho wa habari(yasizidi maneno 20)
  6. Fundisho/ujumbe mkuu ni…..
  7. Jambo lililokuvutia sana……
  8. Maoni kwa ujumla kama yapo….
   ZOEZI  
Lipi kati ya haya ni jambo la kuzingatia katika ufahamu wa kusoma kwa
 burudani?
A
Kujibu maswali
B
Kujinufaisha
C
Kuweka kumbukumbu
D
Kuongeza maarifa
___siyo mojawapo ya kipengele cha kujiwekea kumbukumbu katika
 ufahamu wa kusoma kwa burudani.
A
Jina la kitabu
B
Ujumbe mkuu
C
Kiini cha habari
D
Tarehe
Lengo kuu katika ufahamu wa kusoma kwa burudani ni___.
A
Kuongeza maarifa
B
Kujinufaisha
C
Kuweka kumbukumbu
D
Kujiburudisha
Katika ufahamu wa kusoma kwa burudani msomaji anaweza kujisomea
 vitabu vifuatavyo, isipokuwa:
A
Makala
B
Vitabu vya ziada
C
Majarida
D
Vitabu vya kiada
Ufupisho wa kile kinachosomwa katika ufahamu wa kusoma kwa burudani
 husaidia___.
A
Kujibu maswali
B
Kuweka kumbukumbu
C
Kujiburudisha
D
Kusoma vitabu vingi
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)