UTANGULIZI WA LUGHA NA ISIMU: MUHADHARA WA NANE : FONOLOJIA ARUDHI - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Chuo (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=3) +---- Forum: Shahada (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=20) +----- Forum: Nukuu (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=22) +----- Thread: UTANGULIZI WA LUGHA NA ISIMU: MUHADHARA WA NANE : FONOLOJIA ARUDHI (/showthread.php?tid=1628) |
UTANGULIZI WA LUGHA NA ISIMU: MUHADHARA WA NANE : FONOLOJIA ARUDHI - MwlMaeda - 12-01-2021 MUHADHARA WA NANE : FONOLOJIA ARUDHI
Fonolojia Arudhi
Maana ya fonolojia arudhi
Hizi ni sifa za kimatamshi zinazoambatanishwa kwenye sauti za lugha ya mwanadamu, sifa hizi huitambulisha sauti kimatamshi zaidi na husaidia kubainisha taarifa za msingi kama hali ya msemaji, hisiya za msemaji, umbali, n.k
Matamshi:
Lafudhi
Shadda/mkazo
Kidatu:
Kiimbo
Aina za kiimbo
Kiimbo cha maelezo: Kiimbo cha maelezo ni kile ambacho kwa kawaida msemaji wa lugha akiwa kwenye kidatu chochote kile mawimbi sauti ya usemaji wake yanakuwa takriban katika mstari ulionyooka.
Kiimbo cha kuuliza: Kiimbo cha kuuliza hujitokeza kwa kutumia viwango tofauti vya kidatu kutegemeana na aina ya swali linaloulizwa .
Kiimbo cha amri: kiimbo cha amri hakitofautiani sana na kiimbo cha maulizo.Uchunguzi wa kifonetiki, unaonesha kuwa katika kutoa amri, mzungumzaji hutumia kidatu cha juu zaidi kuliko ilivyo katika kiimbo cha maelezo.
Otografia :- Neno otografia lina asili ya kigiriki na maana yake ni utaratibu wa kutumia alama au michoro ya maandishi kuwakilisha sauti zisikikazo katika lugha.
Silabi:
Silabi ni kipashio cha kifonolojia kinachohusu matamshi ambacho kwacho sauti za Lugha hutamkwa mara moja kwa pamoja kama fungu moja la sauti. Kuna aina mbili za silabi, yaani silabi funge na silabi huru. Silabi huru ni zile ambazo huishia na irabu na silabi funge ni zile zinazoishia na konsonanti. Silabi za Kiswahili sanifu mara nyingi huangukia katika kundi la silabi huru.
Miundo asilia ya silabi za Kiswahili
Mf. A katika Anasoma
Mf. Ka, ba, ma
Mf. N katika Nta,
M katika Mtoto
Mf. Cha, sha,
Mf. Shwa,
Mf. Kwa, mwa
Muundo wa silabi za Kiswahili sanifu zenye asili ya lugha za kigeni
Mf. Labda, leksika, teknolojia
Mf. Asprini, skrini
|