MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI

Welcome, Guest
You have to register before you can post on our site.

Username
  

Password
  





Search Forums

(Advanced Search)

Forum Statistics
» Members: 5,481
» Latest member: Kundlimatching
» Forum threads: 2,178
» Forum posts: 2,256

Full Statistics

Online Users
There are currently 171 online users.
» 0 Member(s) | 169 Guest(s)
Bing, Google

Latest Threads
Buy Vilitra 60 Mg |【Get E...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-24-2023, 11:45 AM
» Replies: 0
» Views: 0
How to take Cenforce50?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-19-2023, 12:59 PM
» Replies: 0
» Views: 0
About the Vidalista 60 Mg...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-04-2023, 04:07 PM
» Replies: 0
» Views: 0
What Is Vidalista 60?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-03-2023, 10:49 AM
» Replies: 0
» Views: 0
How to take Cenforce 100 ...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
03-29-2023, 02:37 PM
» Replies: 0
» Views: 66
How is Vidalista 10 Mg us...
Forum: Watunzi wa Kiswahili
Last Post: Kieth_winsett
03-27-2023, 01:26 PM
» Replies: 0
» Views: 117
Obtain Thesis Paper Assis...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Minny02
03-24-2023, 03:01 PM
» Replies: 0
» Views: 200
SEO services for sports f...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Maria Poland
03-17-2023, 01:51 PM
» Replies: 1
» Views: 223
NUKUU ZA KISWAHILI DARASA...
Forum: Nukuu
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:31 PM
» Replies: 0
» Views: 788
NECTA K4 2022
Forum: Mitihani
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:25 PM
» Replies: 0
» Views: 403

 
  ETIMOLOJIA YA NENO "BURUDAI''
Posted by: MwlMaeda - 09-10-2022, 05:41 PM - Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili - No Replies

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO "BURUDAI''

Neno burudai katika lugha ya Kiswahili ni nomino: [Ngeli: i-/zi-] yenye maana zifuatazo:

1. Kisomo maalumu cha kumsifu Mtume Muhammad (Swalla Llaahu Alayhi Wasallama/Allaah Amrehemu na Ampe Amani); maulidi      ( Chanzo: Kamusi Kuu ya Kiswahili).

2. Jina la kasida mojawapo ya kumsifu Mtume Muhammad (S.A.W) na kueleza maisha yake; maulidi (Chanzo:Kamusi ya Kiswahili Sanifu - TUKI).

3. Wimbo wa kasida ambao ni mashairi ya kumsifu Mtume Muhammad (S.A.W) (Chanzo: Kamusi ya Kiswahili ya Karne ya 21).

Neno hili burudai linatokana na neno la Kiarabu burdah ( soma: burdatun/burdatan/burdatin بردة) lenye maana zifuatazo:

1. Mharuma (Kitambaa chembamba kirefu kinachotupiwa shingoni au begani).

2. Kasida ya kumsifu Mtume Muhammad (Allaah Amrehemu na Ampe Amani) iliyotungwa na Kaab bin Zuheir. Na imeitwa kwa jina hilo kwa kuwa Kaab bin Zuheir alipomaliza kuiimba Mtume alivua mharuma wake na kumtunza.

3. Kasida ya kumsifu Mtume Muhammad (S.A.W) iliyotungwa na Imam Al-Buswiriy.

Kinachodhihiri ni kuwa neno burdatun  بردة lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno burudai halikubadili maana yake ya kasida ya kumsifu Mtume Muhammad (S.A.W) katika lugha ya asili - Kiarabu.

TANBIHI:
Burudai mashuhuri, kwa Waswahili wa Afrika ya Mashariki, ni ile kasida iliyotungwa na mwanachuoni mshairi wa Misri aitwaye Muhammad bin Said bin Hamad  bin Abdillaahi Al-Sanhajii Al-Buswiiriy maarufu kwa jina la Al-Imaam Al-Buswiiriy (Amezaliwa tarehe Mosi Shawwal Mwaka 608 Hijiriyyah sawa na tarehe 7 Machi Mwaka 1213 Miladiyya).

Al-Imaam Al-Buswiiriy ndiye mtunzi wa kasida ya Hamziyya iliyotafsiriwa kwa Kiswahili na Sharif Aidarus na kuitwa Utendi wa Hamziyya.

Al-Imaam Al-Buswiiriy amesimulia kuwa alitunga kasida hii iitwayo ' Burdatu Al-Madiih بردة المديح'  alipopatwa na ugonjwa wa kupooza, akaomba uombezi kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kumsifu Mtume  Muhammad (S A.W) kwa kutunga kasida hii.

Alipolala alimuona Mtume Muhammad (S.A.W) ndotoni, akimfuta mwili wake kwa mkono wake uliobarikiwa na akapata nafuu.

Kulipokucha alipotoka nje ya nyumba yake alikutana na  baadhi ya watu masikini, na mmoja akasema: Ewe Bwana, nataka unipe shairi ulilomsifu Mtume wa Mwenyezi Mungu.
Akamuuliza: shairi lipi? Akasema: Shairi linaloanza na: “ Amin tadhakuri jiiranin..../Je, ni kwa kuwakumbuka majirani…” (Ubeti wa kwanza wa shairi la Burdatu Al-Madiih, ambalo hakumwambia siri yake yeyote), basi akampa.

Habari ya kupona kwake ikaenea na watu wakaanza kutafuta baraka na uponyaji kwa kuisoma kasida hii.

Imesimuliwa kuwa burdah/burudai ni mharuma ambao Al-Imaam Al-Buswiiriy alimuona Mtume Muhammad ndotoni akiutumia kumpagusa mwilini na akaamka hali amepona kabisa maradhi ya kupooza yaliyokuwa yakimsumbua.

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.

Print this item

  ETIMOLOJIA YA NENO "BURIANI''
Posted by: MwlMaeda - 09-08-2022, 10:08 PM - Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili - No Replies

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO "BURIANI''

Neno *buriani* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: i-/zi-*] yenye maana zifuatazo:

1. Maagano yanayoonesha kuwa wanaoagana wataachana kwa muda mrefu au kutoonana kabisa.

2. Salamu za kutakiana heri ambayo watu hupeana wanapoagana.

3. Msamaha au radhi ambayo watu hutakiana huku wakiagana.

*Nahau:*
*Peana buriani:* agana.

Katika lugha ya Kiarabu, hakuna neno *buriani* na neno lililo karibu ni neno *barawah*, neno la msimu lililotumika katika baadhi ya nyimbo za Kiarabu likiwa na maana zifuatazo:

1. Neno la kushukuru; ahsante.

2. Hali ya kukamilika; timamu.

Kinachodhihiri ni kuwa neno *buriani* halina asili ya Kiarabu kinyume na madai yaliyosajiliwa makamusini.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*

Print this item

  SAFARI YA BULICHEKA NA MKE WAKE
Posted by: MwlMaeda - 09-05-2022, 01:07 PM - Forum: Riwaya - No Replies


.pdf   Safari ya Bulicheka na mke wake .pdf (Size: 2.29 MB / Downloads: 37)

Print this item

  NECTA K4 2021
Posted by: MwlMaeda - 09-05-2022, 01:02 PM - Forum: Mitihani - No Replies


.pdf   Kiswahili-F4-2021.pdf (Size: 4.43 MB / Downloads: 18)

Print this item

  ETIMOLOJIA YA NENO "BURUJI''
Posted by: MwlMaeda - 09-05-2022, 12:44 PM - Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili - No Replies

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO "BURUJI''

Neno buruji katika lugha ya Kiswahili ni nomino: [Ngeli: i-/zi-] na pia [Ngeli: a-/wa- kwa mtu]* yenye maana zifuatazo:

1. Ngome iliyo na kuta zenye uwazi juu, boma la ngome lenye kuta zilizo na mapengo kwa juu; sera      ( Vyanzo: Kamusi Kuu ya Kiswahili na Kamusi ya Kiswahili Sanifu - TUKI).

2. Jengo au kitu kirefu kinachowekwa au kujengwa kwa ajili ya kuadhimisha au kuashiria tukio fulani; mnara (Chanzo: Kamusi Kuu ya Kiswahili na Kamusi ya Kiswahili Sanifu-TUKI ).

3. Chombo cha muziki aina ya tarumbeta ambacho mabadiliko ya sauti yake hutokana na kubonyeza vali, tarumbeta ndogo inayopigwa na askari. (Chanzo: Kamusi Kuu ya Kiswahili na Kamusi ya Kiswahili Sanifu-TUKI ).

4. Njia au mashukio ya nyota.(Chanzo: Kamusi Kuu ya Kiswahili na Kamusi ya Kiswahili Sanifu-TUKI ).

5. Nafasi zilizoachwa chini ya ua uliojengwa kwenye maji machache na ambayo nyuma yake huwekwa mitego ya samaki, nafasi inayoachwa katika uzio uliojengwa majini kwa ajili ya kuwekea  mitego ya kunasia samaki. (Chanzo: Kamusi Kuu ya Kiswahili na Kamusi ya Kiswahili Sanifu-TUKI ).

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili buruji linatokana na neno la Kiarabu buruuj ( soma: buruujun/buruujan/buruujin بروج) wingi wa neno la Kiarabu burj (soma: burjun/burjan/burjin برج) lenye maana zifuatazo:

1. Mnara wa kuongozea meli au ndege.

2. Kibanda cha askari kinachojengwa juu aghalabu katika ukuta wa kuingia kwenye mji, kwenye gereza, ukuta au ngome kwa ajili ya kufuatilia kwa mbali.

3. Kasri yenye kulindwa kwa ulinzi madhubuti.

4. Njia ya kushukia nyota 12 katika elimu ya Falaki.

5. Jengo refu kama vile Burju Al-Khalifa nchini Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E).

Kinachodhihiri ni kuwa neno buruujun  بروج lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno buruji lilichukua kutoka Kiarabu baadhi ya maana, kuziacha nyingine na kuchukua maana mpya za nafasi inayoachwa katika uzio uliojengwa majini kwa ajili ya kuwekea  mitego ya kunasia samaki na chombo cha muziki kiitwacho tarumbeta.

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.

Print this item

  ETIMOLOJIA YA NENO "BURUNUSI''
Posted by: MwlMaeda - 09-05-2022, 12:43 PM - Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili - No Replies

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO "BURUNUSI''

Neno burunusi katika lugha ya Kiswahili ni nomino: [Ngeli: i-/zi-] yenye maana ya vazi zito lililounganishwa na kofia.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili burunusi linatokana na neno la Kiarabu burnus ( soma: burnusun/burnusan/burnusin برنس) lenye maana zifuatazo:

1. Vazi lenye mikono miwili linalounganishwa na kofia aghalabu huvaliwa baada ya kukoga.

2. Mji wa mimba.

Kinachodhihiri ni kuwa neno burnus  برنس lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno burunusi halikubadili maana ya vazi linalounganishwa na kofia, katika Kiarabu na liliacha maana ya mji wa mimba.

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.

Print this item

  TATHMINI YA WATAHINI KUHUSU UFAULU WA WATAHINIWA WA KIDATO CHA NNE
Posted by: MwlMaeda - 09-05-2022, 07:45 AM - Forum: Zana za kufundishia - No Replies


.pdf   021_KISWAHILI 2021.pdf (Size: 3.42 MB / Downloads: 1)

Print this item

  ETIMOLOJIA YA NENO "UJUMI''
Posted by: MwlMaeda - 09-03-2022, 10:30 AM - Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili - No Replies

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO "UJUMI''

Neno *ujumi* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: u-/u-*] yenye maana zifuatazo:
1. Kanuni zinazohusu ubora na ubaya wa kazi ya sanaa.(Vyanzo: *Kamusi ya Karne ya 21* na *Kamusi ya Kiswahili Sanifu - TUKI*).

2. Tathmini inayobainisha ubora au ubaya wa kazi za sanaa. (Chanzo: *Kamusi Kuu ya Kiswahili*).

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *ujumi* linatokana na neno la Kiarabu *ujmu* ( *soma: ujmun/ujman/ujmin عجم*) wingi wa neno la Kiarabu *a-ajamiyyu (a-ajamiyyun/a-ajamiyyan/a-ajamiyyin اعجمي)* lenye maana zifuatazo:

1. Mtu asiye fasaha katika kuzungumza aghalabu lugha ya Kiarabu hata kama ni mwarabu.

2. Asiye mwarabu, mtu wa Uajemi (Iran); muajemi.

3. Mtu asiyeweza kusema; bubu.

4. -siyo na mlio/sauti aghalabu mawimbi au bunduki.

Kinachodhihiri ni kuwa neno *ujmun  عجم* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *ujumi* lilichukua maana mpya *kanuni zinazohusu ubora na ubaya wa kazi ya sanaa, tathmini inayobainisha ubora au ubaya wa kazi za sanaa* na kuacha maana za neno hili katika lugha ya Kiarabu.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*

Print this item

  ETIMOLOJIA YA NENO "BULIBULI''
Posted by: MwlMaeda - 08-28-2022, 08:22 AM - Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili - No Replies

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO "BULIBULI''

Neno *bulibuli* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: i-/zi-*] yenye maana ya mtindo mmojawapo wa kofia nyeupe yenye nakshi (viua) inayovaliwa hasa mwambao wa pwani ya Afrika Mashariki, kofia ya kazi.

Pia ni kivumishi kwa maana ya: -zuri, -a kupendeza, bambam, -ema.

Mwanafunzi mwenye tabia bulibuli hufaulu vizuri katika mitihani yake.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *bulibuli* linatokana na nomino ya Kiarabu *bulbulu بلبل* yenye maana zifuatazo:

1. Ndege mdogo aina ya kunega maarufu kwa kuimba vizuri.

2. Sehemu ya kumiminia maji katika birika.

Kinachodhihiri ni kuwa neno *bulbulu  بلبل* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *bulibuli* lilichukua maana mpya ya (nomino) kofia yenye viua inayovaliwa pwani ya Afrika Mashariki na maana ya (kivumishi): -zuri, -a kupendeza, bambam, -ema.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*

Print this item

  ETIMOLOJIA YA NENO "MAHABA''
Posted by: MwlMaeda - 08-23-2022, 09:59 AM - Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili - No Replies

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO "MAHABA''

Neno mahaba katika lugha ya Kiswahili ni nomino: [Ngeli: ya-/ya-] yenye maana zifuatazo:

1. Hisia za mvuto zinazojengeka kwa mtu mwengine kutokana na kupendezwa naye. (Chanzo: Kamusi Kuu ya Kiswahili).

2. Hali ya kuvutiwa na kitu au mtu kutokana na uzuri wake ambao huingia moyoni na kumfanya ampende. (Chanzo: Kamusi ya Karne ya 21).

3. Hali ya kuingiwa moyoni na mtu au kitu na kukuthamini zaidi ya vingine; mapenzi .(Chanzo: Kamusi ya Kiswahili Sanifu - TUKI).

4. Matandu ya wali yaliyoandaliwa maalumu kama tunu kwa mume.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili mahaba linatokana na neno la Kiarabu mahabbah محبة  ( soma: mahabbatun/mahabbatan/mahabbatin محبة) lenye maana zifuatazo:

1. Kupendana na kuthaminiana moyoni.

2. Ashiki inayojenga ubinafsi wa pendo na wivu.

3. Kinachotakiwa na moyo.

4. Ki-Falsafa, mahaba ni sababu inayoleta pamoja vitu mbalimbali.

Kinachodhihiri ni kuwa neno mahabbatun  محبة lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno mahaba lilichukua maana jumla ya mapenzi na kuleta maana mpya ya matandu ya wali yaliyoandaliwa kama tunu kwa mume.

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.

Print this item