MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO "BURIANI'' - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
ETIMOLOJIA YA NENO "BURIANI'' - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16)
+--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO "BURIANI'' (/showthread.php?tid=2825)

ETIMOLOJIA YA NENO "BURIANI'' - MwlMaeda - 09-08-2022

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO "BURIANI''

Neno *buriani* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: i-/zi-*] yenye maana zifuatazo:

1. Maagano yanayoonesha kuwa wanaoagana wataachana kwa muda mrefu au kutoonana kabisa.

2. Salamu za kutakiana heri ambayo watu hupeana wanapoagana.

3. Msamaha au radhi ambayo watu hutakiana huku wakiagana.

*Nahau:*
*Peana buriani:* agana.

Katika lugha ya Kiarabu, hakuna neno *buriani* na neno lililo karibu ni neno *barawah*, neno la msimu lililotumika katika baadhi ya nyimbo za Kiarabu likiwa na maana zifuatazo:

1. Neno la kushukuru; ahsante.

2. Hali ya kukamilika; timamu.

Kinachodhihiri ni kuwa neno *buriani* halina asili ya Kiarabu kinyume na madai yaliyosajiliwa makamusini.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*