MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO "BURUJI''

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO "BURUJI''
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO "BURUJI''

Neno buruji katika lugha ya Kiswahili ni nomino: [Ngeli: i-/zi-] na pia [Ngeli: a-/wa- kwa mtu]* yenye maana zifuatazo:

1. Ngome iliyo na kuta zenye uwazi juu, boma la ngome lenye kuta zilizo na mapengo kwa juu; sera      ( Vyanzo: Kamusi Kuu ya Kiswahili na Kamusi ya Kiswahili Sanifu - TUKI).

2. Jengo au kitu kirefu kinachowekwa au kujengwa kwa ajili ya kuadhimisha au kuashiria tukio fulani; mnara (Chanzo: Kamusi Kuu ya Kiswahili na Kamusi ya Kiswahili Sanifu-TUKI ).

3. Chombo cha muziki aina ya tarumbeta ambacho mabadiliko ya sauti yake hutokana na kubonyeza vali, tarumbeta ndogo inayopigwa na askari. (Chanzo: Kamusi Kuu ya Kiswahili na Kamusi ya Kiswahili Sanifu-TUKI ).

4. Njia au mashukio ya nyota.(Chanzo: Kamusi Kuu ya Kiswahili na Kamusi ya Kiswahili Sanifu-TUKI ).

5. Nafasi zilizoachwa chini ya ua uliojengwa kwenye maji machache na ambayo nyuma yake huwekwa mitego ya samaki, nafasi inayoachwa katika uzio uliojengwa majini kwa ajili ya kuwekea  mitego ya kunasia samaki. (Chanzo: Kamusi Kuu ya Kiswahili na Kamusi ya Kiswahili Sanifu-TUKI ).

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili buruji linatokana na neno la Kiarabu buruuj ( soma: buruujun/buruujan/buruujin بروج) wingi wa neno la Kiarabu burj (soma: burjun/burjan/burjin برج) lenye maana zifuatazo:

1. Mnara wa kuongozea meli au ndege.

2. Kibanda cha askari kinachojengwa juu aghalabu katika ukuta wa kuingia kwenye mji, kwenye gereza, ukuta au ngome kwa ajili ya kufuatilia kwa mbali.

3. Kasri yenye kulindwa kwa ulinzi madhubuti.

4. Njia ya kushukia nyota 12 katika elimu ya Falaki.

5. Jengo refu kama vile Burju Al-Khalifa nchini Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E).

Kinachodhihiri ni kuwa neno buruujun  بروج lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno buruji lilichukua kutoka Kiarabu baadhi ya maana, kuziacha nyingine na kuchukua maana mpya za nafasi inayoachwa katika uzio uliojengwa majini kwa ajili ya kuwekea  mitego ya kunasia samaki na chombo cha muziki kiitwacho tarumbeta.

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)