MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
ETIMOLOJIA YA NENO "BURUDAI''

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO "BURUDAI''
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO "BURUDAI''

Neno burudai katika lugha ya Kiswahili ni nomino: [Ngeli: i-/zi-] yenye maana zifuatazo:

1. Kisomo maalumu cha kumsifu Mtume Muhammad (Swalla Llaahu Alayhi Wasallama/Allaah Amrehemu na Ampe Amani); maulidi      ( Chanzo: Kamusi Kuu ya Kiswahili).

2. Jina la kasida mojawapo ya kumsifu Mtume Muhammad (S.A.W) na kueleza maisha yake; maulidi (Chanzo:Kamusi ya Kiswahili Sanifu - TUKI).

3. Wimbo wa kasida ambao ni mashairi ya kumsifu Mtume Muhammad (S.A.W) (Chanzo: Kamusi ya Kiswahili ya Karne ya 21).

Neno hili burudai linatokana na neno la Kiarabu burdah ( soma: burdatun/burdatan/burdatin بردة) lenye maana zifuatazo:

1. Mharuma (Kitambaa chembamba kirefu kinachotupiwa shingoni au begani).

2. Kasida ya kumsifu Mtume Muhammad (Allaah Amrehemu na Ampe Amani) iliyotungwa na Kaab bin Zuheir. Na imeitwa kwa jina hilo kwa kuwa Kaab bin Zuheir alipomaliza kuiimba Mtume alivua mharuma wake na kumtunza.

3. Kasida ya kumsifu Mtume Muhammad (S.A.W) iliyotungwa na Imam Al-Buswiriy.

Kinachodhihiri ni kuwa neno burdatun  بردة lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno burudai halikubadili maana yake ya kasida ya kumsifu Mtume Muhammad (S.A.W) katika lugha ya asili - Kiarabu.

TANBIHI:
Burudai mashuhuri, kwa Waswahili wa Afrika ya Mashariki, ni ile kasida iliyotungwa na mwanachuoni mshairi wa Misri aitwaye Muhammad bin Said bin Hamad  bin Abdillaahi Al-Sanhajii Al-Buswiiriy maarufu kwa jina la Al-Imaam Al-Buswiiriy (Amezaliwa tarehe Mosi Shawwal Mwaka 608 Hijiriyyah sawa na tarehe 7 Machi Mwaka 1213 Miladiyya).

Al-Imaam Al-Buswiiriy ndiye mtunzi wa kasida ya Hamziyya iliyotafsiriwa kwa Kiswahili na Sharif Aidarus na kuitwa Utendi wa Hamziyya.

Al-Imaam Al-Buswiiriy amesimulia kuwa alitunga kasida hii iitwayo ' Burdatu Al-Madiih بردة المديح'  alipopatwa na ugonjwa wa kupooza, akaomba uombezi kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kumsifu Mtume  Muhammad (S A.W) kwa kutunga kasida hii.

Alipolala alimuona Mtume Muhammad (S.A.W) ndotoni, akimfuta mwili wake kwa mkono wake uliobarikiwa na akapata nafuu.

Kulipokucha alipotoka nje ya nyumba yake alikutana na  baadhi ya watu masikini, na mmoja akasema: Ewe Bwana, nataka unipe shairi ulilomsifu Mtume wa Mwenyezi Mungu.
Akamuuliza: shairi lipi? Akasema: Shairi linaloanza na: “ Amin tadhakuri jiiranin..../Je, ni kwa kuwakumbuka majirani…” (Ubeti wa kwanza wa shairi la Burdatu Al-Madiih, ambalo hakumwambia siri yake yeyote), basi akampa.

Habari ya kupona kwake ikaenea na watu wakaanza kutafuta baraka na uponyaji kwa kuisoma kasida hii.

Imesimuliwa kuwa burdah/burudai ni mharuma ambao Al-Imaam Al-Buswiiriy alimuona Mtume Muhammad ndotoni akiutumia kumpagusa mwilini na akaamka hali amepona kabisa maradhi ya kupooza yaliyokuwa yakimsumbua.

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)