ETIMOLOJIA YA NENO "BULIBULI'' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO "BULIBULI'' (/showthread.php?tid=2815) |
ETIMOLOJIA YA NENO "BULIBULI'' - MwlMaeda - 08-28-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO "BULIBULI'' Neno *bulibuli* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: i-/zi-*] yenye maana ya mtindo mmojawapo wa kofia nyeupe yenye nakshi (viua) inayovaliwa hasa mwambao wa pwani ya Afrika Mashariki, kofia ya kazi. Pia ni kivumishi kwa maana ya: -zuri, -a kupendeza, bambam, -ema. Mwanafunzi mwenye tabia bulibuli hufaulu vizuri katika mitihani yake. Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *bulibuli* linatokana na nomino ya Kiarabu *bulbulu بلبل* yenye maana zifuatazo: 1. Ndege mdogo aina ya kunega maarufu kwa kuimba vizuri. 2. Sehemu ya kumiminia maji katika birika. Kinachodhihiri ni kuwa neno *bulbulu بلبل* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *bulibuli* lilichukua maana mpya ya (nomino) kofia yenye viua inayovaliwa pwani ya Afrika Mashariki na maana ya (kivumishi): -zuri, -a kupendeza, bambam, -ema. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |