HANI NIPO KITANDANI
haloo!hanii halo, Rwaka hani wasikia?
Ndio hapo sawa halo, vipi unaendelea?
Tatizo nililonalo, lazizi ninaugua,
Hani nipo kitandani, taabani hali yangu.
Wala sijahama njia, nitafika huko Rwanda,
Ikinijia afia, na wangu mwili kuwanda,
Basi huko nitatua, unione mie kinda,
Sasa nipo kitandani, taabani hali yangu.
Ila ninayo pumzi, bado moyo unahema,
Bora nikweleze wazi, kinifanyacho kukwama,
Matatizo ya uzazi, ndiyo yaloniandama,
Jua nipo kitandani, taabani hali yangu.
Ina machungu dunia, na mie yamenikuta,
Nusu niage dunia, kwa tumbo kunikeketa,
Japo nimeamkia, bado najivutavuta,
Ila nipo kitandani, taabani hali yangu.
Maradhi yanaghasia, Karagama sikiliza,
Yakishakuangukia, dira unaipoteza,
Mwilini nimelegea, vile nimepata siza,
Love nipo kitandani, taabani hali yangu.
Nitahama nikipona, Tanzania sitarudi,
Na wewe tukionana, itatulia fuadi,
Ila sasa raha sina, Darling I feel bad,
Vile nipo kitandani, taabani hali yangu.
Namshukuru Karima, ningali hai mpenzi,
Ninaungoja uzima, japo kutwa nakuenzi,
Ningelikufa mapema, ungelipata simanzi,
Hapa nipo kitandani, taabani hali yangu.
Na mie napata ganzi, nikikukosa kijana,
Heri kunipiga konzi, utosini nitapona,
Sitahimili majonzi, na wewe tukikosana,
Japo nipo kitandani, taabani hali yangu.
Maumivu yamezidi, yanikataza kutunga,
Kuacha imenibidi, utungo huu kufunga,
Ila ninakuahidi, huko Rwanda nitatinga,
Nikitoka kitandani, iwe njema hali yangu.
Neno *balaghamu/belghamu* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: li-/ya-*] yenye maana ya kioevu kizito kilichochanganyika na utandoute kinachotolewa kwa wingi kwa njia ya kupumulia hususan mtu anapougua mafua au kikohozi, mate mazito yanayokuwa kooni ambayo hutoka mtu anapokohoa.
*Msemo:* *Toa balaghamu zako*: toa hasira zako.
Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *balaghamu/belghamu* limechukuliwa kutoka neno la Kiarabu *'balghamu* *(soma: balghamun/balghaman/balghamin بلغم)** lenye maana ya mate yaliyochanganyika na kamasi na hutoka kwa njia ya upumuaji, dutu laini ya mate iliyochanganyika na kamasi; *kohozi*.
Kinachodhihiri ni kuwa neno *'balghamun بلغم* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *balaghamu/belghamu* halikubadili maana katika lugha asili- Kiarabu.
Posted by: MwlMaeda - 07-29-2022, 08:04 AM - Forum: Semi
- No Replies
MAANA YA METHALI
Wataalamu mbalimbali wamejaribu kutoa fasili ya maana ya methali. Mazrui na Syambo (1992), methali ni misemo mifupi yenye hekima fulani. Wamesisitiza kuwa methali hudhihirisha mkusanyiko wa mafunzo waliyopata watu wa vizazi vingi vya jumuiya wanayoishi katika maisha yao. Aidha, wameongeza kusem kuwa methali ni sehemu moja ya lugha inayoweza kubaini falsafa ya watu fulani kuhusu maisha kwa ujumla.
Ngole na Honero (1981), wamesema kuwa methali ni aina ya usemi mzito na ambao unakusudiwa kusema jambo maalumu kwa njia ya fumbo. Methali hukusudiwa kumuonya, kumuongoza na kumuadilisha mwanadamu katika maisha yake. Aidha, kwa umbile la nje methli huwa na muundo wa pande mbili. Upande mmoja wa methali hueleza mazoea au tabia ya watu au kitu katika utendaji wa jambo. Upande wa pili wa methali hueleza matokeo yaliyosababishw na mazowea au tabia iliyoelezwa katika upande wa kwanza.
Murega (2015), ameona kuwa methali ni semi fupi ya kimapokeo yenye muundo mahsusi na iliyo na fumbo amblo linapofasiliwa hupata maana mbalimbali hutegemea muktadha na hali halisi ya maisha ya watumiaji.
Wamitila (2001), ameeleza kuwa methali ni msemo unaojitosheleza, wenye maana yenye nguvu au uzito, wenye muundo au sifa za kishairi, unaokusudiwa kuadibu au kuelekeza, kuelimisha, kushauri na kadhalika.
Kutokana na fasili za wataalamu hao, tunaweza kusema kuwa methali ni aina ya usemi mzito unaoelezea wazo pana kwa muhtasari ukiwa na umbo mahsusi na unaotumia uzowefu wa jamii kuonya, kuadilisha na kufunza kwa kuzingatia miktadha maalumu. Methali hutumia hekima, uficho wa kauli, usanii w kimsamiati, uzowefu wa matukio katika jamii na falsafa ya jamii katika mitazamo ya masuala mbalimbali ambayo huakisi maisha na utamaduni wa jamii husika.
UCHAWI
Jamani niambieni, akipatapacho mchawi,
Huko awako gizani, mbona ya Mana hayawi,
Pasi na nguo mwilini, lake baridi mchawi,
Jamani niambieni, akipatapacho mchawi.
Mchawi hupenda tabu, hapendi mambo rahisi,
Kona anaziharibu, apite kwa wasiwasi,
Mlangoni hajaribu, apite kwa urahisi,
Jamani niambieni, akipatapacho mchawi.
Yake kazi kuharibu, akageuza kizazi,
Ili unapojaribu, huoni chako kizazi,
Hapo hawana sababu, mambo yao ni ushenzi,
Jamani niambieni, akipatapacho mchawi.
Japo yu mtu mkubwa, chamani kuheshimika,
Tabiaye kama mbwa, anapotaka kuruka,
Na baridi atakumbwa, hana nguo kujivika,
Jamani niambieni, akipatapacho mchawi.
Juzi nilipata kesi, mtu katiwa kifafa,
Matabibu na manesi, wakadhani amekufa,
Mwisho katoa kamasi, tukagundua hajafa,
Jamani niambieni, akipatapacho mchawi.
Mchawi akifahamu, una kitu kumzidi,
Jua umejipa sumu, kukuroga hana budi,
Utateswa kwa awamu, ukuishe ukaidi,
Jamani niambieni, akipatapacho mchawi.
Msiwaone vichaa, kidhani yote ya Mumba,
Wengine tukashangaa, ovyo waanza kuimba,
Wachawi walishakaa, kuchanganya mitishamba,
Jamani niambieni, akipatapacho mchawi.
Mtu umesoma sana, Mara vyeti huvioni,
Kumbe walishagawana, watandike kaburini,
Miaka kazi hauna, uchawi ni ushetani,
Jamani niambieni, akipatapacho mchawi.
Machawi yake hasara, ulie yeye acheke,
Wala haimpi fora, hadharani asifike,
Kiumbe mwenye mikwara, japo asifaidike,
Jamani niambieni, akipatapacho mchawi.
Mchawi mtu wa ila, mambo yake ni kinyume,
Usiku sie twalala, yu uchi atutazame,
Na hawi tajiri wala, kiwa wongo na aseme,
Jamani niambieni, akipatapacho mchawi.
Sasa ninafunga beti, utungo siendelezi,
Msijenishika shati, ati nimewapa kazi,
Naona bora niketi, kuandika nimesizi,
Jamani niambieni, akipatapacho mchawi.
Neno bedui/bedawi katika lugha ya Kiswahili ni nomino: [Ngeli: a-/wa-, wingi: mabedui/mabedawi] yenye maana zifuatazo:
1. Mtu wa jamii ya Waarabu anayeishi jangwani au karibu na jangwa.
2. Mtu katili asiyemwonea mwenzie huruma.
Katika lugha ya Kiarabu, neno hili bedui/bedawi limechukuliwa kutoka neno la Kiarabu 'badawiyyun (soma: badawiyyun/badawiyyan/badawiyyin بدوي)* lenye maana zifuatazo:
1. Mkazi wa eneo la jangwani lililowekwa makazi, malisho na panapopatikana maji.
2. Mtu anayelinda na kuendelea na utamaduni wake wa asili.
Kinachodhihiri ni kuwa neno 'badawiyyun بدوي lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno bedui/bedawi halikubadili maana yake ya mkazi wa jangwani katika lugha asili- Kiarabu, likaacha maana ya mtu anayehifadhi na kuendelea na utamaduni wake wa asili na likachukua maana mpya ya mtu katili asiyemwonea mwenzie huruma.
Posted by: MwlMaeda - 07-24-2022, 09:04 AM - Forum: Tamthiliya
- No Replies
Oktoba, 1966 kulizuka mgogoro mkubwa wa kihistoria kati ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Muhimbili. Wanafunzi hawa walifanya maandamano makubwa hadi Ikulu wakipinga vikali sera ya kuwataka wajiunge na Jeshi la kujenga Taifa (JKT). Wasomi hawa walilalama kwa hasira wakisema, "afadhali wakati wa mkoloni kuliko serekali ya Nyerere. Mkitulazimisha basi tutaenda KIMWILI, lakini MIOYO yetu, asilani, haitaenda JKT..." Katika kuukabili upinzani huu, Mwalimu, katika ile hotuba maarufu: "Tanzania itajengwa na wenye moyo" aliwacharaza viboko baadhi ya wasomi hao kadamnasi na kuwafukuza takribani wanafunzi 400 warudi kwao, wakalime! Mwandishi anatudokeza, miongoni mwa masuala mengine kuwa: Mgogoro huu wa 1966, ulichangia katika kukuza mimba ya safari ya Kanaani nchi ya asali na maziwa.Hapana shaka kuwa tamthiliya hii, iliyoandikwa kwa ustadi kabisa, ni kitabu muhimu kwa wanasiasa, wasomi na wapenzi wote wa fasihi ya Kiswahili.
Neno *bayani* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: i-/i-*] yenye maana ya *stadi mojawapo katika mafunzo ya lugha ya Kiarabu inayohusu ujuzi wa kuzungumza.*
Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *bayani* limechukuliwa kutoka neno la Kiarabu *'bayaan* *(soma: bayaanun/bayaanan/bayaanin بيان/البيان)** lenye maana zifuatazo:
1. Maelezo kuhusu bidhaa anayoyatoa mzalishaji wa bidhaa au wakala/muuzaji wake yanayoweka wazi aina ya bidhaa, kiwango chake, uzito wake na hata utumiaji wake.
2. Ubini wa mtu asiyejulikana asili na nasaba yake; *bin bayyaan بن بيان.*
3. Ufasaha wa kulieleza jambo fulani.
4. Taarifa itolewayo baada ya kikao cha pande mbili, *bayaanum mushtarikun بيان مشترك.*
5. Taaluma ya lugha ya Kiarabu ya kuelezea maana moja kwa njia tofauti kama vile *tashbihiتشبيه , majazi مجاز na kinaya كناية.*
Kinachodhihiri ni kuwa neno *'bayaanun بيان* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *bayani* halikubadili maana yake katika lugha asili- Kiarabu.
*TANBIHI:*
Bayani, Kiarabu *Bayaan/Al-Bayaan البيان* ni moja ya fani za *Balaagha ya Kiarabu*, taaluma ya ufasaha wa kusema na kutia madoido.
Fani nyingine mbali ya *ALBAYAAN البيان (Rhetoric)* , ni *ALMAAN المعاني (Semantic)* na *ALBADII'I البديع (The Art of Figures of Speech/The Art of Metaphors and Stylistics/Good Style).*
Posted by: MwlMaeda - 07-22-2022, 06:23 AM - Forum: Ushairi
- No Replies
NIMPENDE NANI ?
Mwenzenu nipeni rai kwa haya yalonifika
Moyo wangu haukai, kwa hapa nilipofika
Japo naona nishai, moyoni nimewatika
Kati ya hawa wawili, Nipende nani zaidi?
Huyu wa kwanza mpole , tena si muongeaji
Kama simba mwenda pole, kwenye ufatiliaji
Hutembea polepole ,amdake mwiwindwaji
Kati ya huyu nayule jama nimpende nani?
Huyu wa pili mweusi , kapanda juu kidogo
Mwenye pua ya kitusi, mwili mwembamba kidogo
Mtalamu wa kukisi,utadhania mgogo
Kati ya huyu na yule ,jama nimpende nani?
Akili inanituma , wa pili awe mwandani
Ninategemea mema ,sitotoka asilani
Kama ikiwa salama ,nitasota uvunguni
Kati ya hawa wawili Nimpende nani?
Nilikuwa na furaha,nimefika maskani
Nikayaanza madaha, nikavipata vya ndani
Nilishazika karaha,ninapokuwa chumbani
Alivyokuja wa pili , Moyo wangu umeshindwa
Wa pili yeye mcheshi , muda wote tabasamu
Ni kweli kuwa achoshi ,twacheka kama binamu
Kwangu hamu haiishi, jama mpeni salamu
Kati ya Hawa wawili nimpende nani?
Wa kwanza ananijali, kwa pesa nayo mahaba
Nikimuuzi hajali, hunilea kama baba
Na hunijulia hali, upendowe sio haba
Wanagenzi mnijuze nimpende yupi?
Rama karibu javini , unipe jibu murua
Na wengine karibuni, jibu nataka kujua
Nitomuweka moyoni, kofuli kumfungia
Kitendawili tegua Yupi kwangu anafaa?
DINNA ( MOM J )
21/7/22
KUWA TAYARI KUHESABIWA
MPE USHIRIKIANO KARANI WA SENSA??