ETIMOLOJIA YA NENO "UJUMI'' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO "UJUMI'' (/showthread.php?tid=2819) |
ETIMOLOJIA YA NENO "UJUMI'' - MwlMaeda - 09-03-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO "UJUMI'' Neno *ujumi* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: u-/u-*] yenye maana zifuatazo: 1. Kanuni zinazohusu ubora na ubaya wa kazi ya sanaa.(Vyanzo: *Kamusi ya Karne ya 21* na *Kamusi ya Kiswahili Sanifu - TUKI*). 2. Tathmini inayobainisha ubora au ubaya wa kazi za sanaa. (Chanzo: *Kamusi Kuu ya Kiswahili*). Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *ujumi* linatokana na neno la Kiarabu *ujmu* ( *soma: ujmun/ujman/ujmin عجم*) wingi wa neno la Kiarabu *a-ajamiyyu (a-ajamiyyun/a-ajamiyyan/a-ajamiyyin اعجمي)* lenye maana zifuatazo: 1. Mtu asiye fasaha katika kuzungumza aghalabu lugha ya Kiarabu hata kama ni mwarabu. 2. Asiye mwarabu, mtu wa Uajemi (Iran); muajemi. 3. Mtu asiyeweza kusema; bubu. 4. -siyo na mlio/sauti aghalabu mawimbi au bunduki. Kinachodhihiri ni kuwa neno *ujmun عجم* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *ujumi* lilichukua maana mpya *kanuni zinazohusu ubora na ubaya wa kazi ya sanaa, tathmini inayobainisha ubora au ubaya wa kazi za sanaa* na kuacha maana za neno hili katika lugha ya Kiarabu. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |