09-05-2022, 12:43 PM
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO "BURUNUSI''
Neno burunusi katika lugha ya Kiswahili ni nomino: [Ngeli: i-/zi-] yenye maana ya vazi zito lililounganishwa na kofia.
Katika lugha ya Kiarabu, neno hili burunusi linatokana na neno la Kiarabu burnus ( soma: burnusun/burnusan/burnusin برنس) lenye maana zifuatazo:
1. Vazi lenye mikono miwili linalounganishwa na kofia aghalabu huvaliwa baada ya kukoga.
2. Mji wa mimba.
Kinachodhihiri ni kuwa neno burnus برنس lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno burunusi halikubadili maana ya vazi linalounganishwa na kofia, katika Kiarabu na liliacha maana ya mji wa mimba.
Shukran sana.
Khamis S.M. Mataka.

Mwl Maeda