MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'BAYANI'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO 'BAYANI'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'BAYANI'

Neno *bayani* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: i-/i-*] yenye maana ya *stadi mojawapo katika mafunzo ya lugha ya Kiarabu  inayohusu ujuzi wa kuzungumza.*

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *bayani* limechukuliwa kutoka neno la Kiarabu  *'bayaan* *(soma: bayaanun/bayaanan/bayaanin  بيان/البيان)**  lenye maana zifuatazo:

1. Maelezo kuhusu bidhaa anayoyatoa mzalishaji wa bidhaa au wakala/muuzaji wake yanayoweka wazi aina ya bidhaa, kiwango chake, uzito wake na hata utumiaji wake.

2. Ubini wa mtu asiyejulikana asili na nasaba yake; *bin bayyaan بن بيان.* 

3. Ufasaha wa kulieleza jambo fulani.

4.  Taarifa itolewayo baada ya kikao cha pande mbili, *bayaanum mushtarikun بيان مشترك.*

5. Taaluma ya lugha ya Kiarabu ya kuelezea maana moja kwa njia tofauti kama vile *tashbihiتشبيه , majazi مجاز  na kinaya كناية.*

Kinachodhihiri ni kuwa neno *'bayaanun بيان* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *bayani* halikubadili maana yake katika lugha asili- Kiarabu.

*TANBIHI:*
Bayani, Kiarabu *Bayaan/Al-Bayaan البيان* ni moja ya fani za *Balaagha ya Kiarabu*, taaluma ya ufasaha wa kusema na kutia madoido. 

Fani nyingine mbali ya *ALBAYAAN  البيان (Rhetoric)* , ni *ALMAAN المعاني (Semantic)* na *ALBADII'I البديع (The Art of Figures of Speech/The Art of Metaphors and Stylistics/Good Style).*

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)