MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

SHAIRI: NIMPENDE NANI ?

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
SHAIRI: NIMPENDE NANI ?
#1
NIMPENDE NANI ?

Mwenzenu nipeni rai kwa haya yalonifika
Moyo wangu haukai, kwa hapa nilipofika
Japo naona nishai,  moyoni nimewatika
Kati ya hawa wawili, Nipende nani zaidi?

Huyu  wa kwanza mpole ,  tena si muongeaji
Kama simba mwenda pole, kwenye ufatiliaji 
Hutembea polepole ,amdake mwiwindwaji
Kati ya huyu nayule jama  nimpende nani?

Huyu wa pili  mweusi , kapanda juu kidogo
Mwenye pua ya kitusi,  mwili mwembamba kidogo
Mtalamu wa kukisi,utadhania mgogo
Kati ya huyu na yule ,jama  nimpende nani?

Akili inanituma , wa pili awe mwandani
Ninategemea mema ,sitotoka asilani
Kama ikiwa salama ,nitasota uvunguni
Kati ya hawa wawili Nimpende nani?

Nilikuwa na furaha,nimefika maskani
Nikayaanza madaha, nikavipata vya ndani
Nilishazika karaha,ninapokuwa chumbani
Alivyokuja wa pili , Moyo wangu umeshindwa

Wa pili yeye mcheshi , muda wote tabasamu
Ni kweli kuwa achoshi ,twacheka kama binamu
Kwangu hamu haiishi, jama mpeni salamu
Kati ya Hawa wawili nimpende nani?

Wa kwanza ananijali, kwa pesa nayo mahaba
Nikimuuzi hajali,  hunilea kama baba
Na hunijulia hali,  upendowe sio haba
Wanagenzi mnijuze nimpende yupi?

Rama  karibu javini ,  unipe  jibu murua
Na wengine karibuni, jibu nataka kujua
Nitomuweka moyoni,  kofuli kumfungia
Kitendawili tegua  Yupi kwangu anafaa?

DINNA ( MOM J )
21/7/22
KUWA TAYARI KUHESABIWA
MPE USHIRIKIANO KARANI WA SENSA??
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)