ETIMOLOJIA YA NENO 'BALAGHAMU/BELGHAMU' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'BALAGHAMU/BELGHAMU' (/showthread.php?tid=2795) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'BALAGHAMU/BELGHAMU' - MwlMaeda - 07-29-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'BALAGHAMU/BELGHAMU' Neno *balaghamu/belghamu* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: li-/ya-*] yenye maana ya kioevu kizito kilichochanganyika na utandoute kinachotolewa kwa wingi kwa njia ya kupumulia hususan mtu anapougua mafua au kikohozi, mate mazito yanayokuwa kooni ambayo hutoka mtu anapokohoa. *Msemo:* *Toa balaghamu zako*: toa hasira zako. Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *balaghamu/belghamu* limechukuliwa kutoka neno la Kiarabu *'balghamu* *(soma: balghamun/balghaman/balghamin بلغم)** lenye maana ya mate yaliyochanganyika na kamasi na hutoka kwa njia ya upumuaji, dutu laini ya mate iliyochanganyika na kamasi; *kohozi*. Kinachodhihiri ni kuwa neno *'balghamun بلغم* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *balaghamu/belghamu* halikubadili maana katika lugha asili- Kiarabu. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |