MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

SHAIRI: NAINGOJA SIMU YAKO - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
SHAIRI: NAINGOJA SIMU YAKO - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6)
+---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50)
+---- Thread: SHAIRI: NAINGOJA SIMU YAKO (/showthread.php?tid=2791)

SHAIRI: NAINGOJA SIMU YAKO - MwlMaeda - 07-25-2022

NAINGOJA SIMU YAKO
Nimeamka mapema, nimekaa kitandani,
Mawazoni nimezama, ninakuwaza mwandani,
Fikira zimenihama, nipo kwako ewe hani,
Naingoja simu yako!

Mara nasimama wima, ghafla nakaa chini,
Mpenzi nashika tama, bila wewe mimi nyani,
Wewe wangu maulama, wanitia tulizoni,
Naingoja simu yako!

Usidhani nalalama, nijinadani mnadani,
Moyo wangu unauma, Mimi nicheze na nani?
Au simu ulizima, upo kwea kitandani?
Naingoja simu yako!

Sio mwingi wa lawama, nakuomba samahani,
Kwakowe nimetuama, kama somba mtungoni,
Haki kwako nimekwama, mithili mwiba kooni,
Naingoja simu yako!

Basi uamke vema, pasi mavune mwilini,
Nakungoja mtu mwema, unijuze hali gani,
Hamu bado hijakoma, kukusubiri mwendani,
Naingoja simu yako!

Mtunzi Filieda Sanga
Mama B
Mabibo Dsm
0753738704