MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'BEDUI/BEDAWI'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO 'BEDUI/BEDAWI'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'BEDUI/BEDAWI'

Neno bedui/bedawi katika lugha ya Kiswahili ni nomino: [Ngeli: a-/wa-, wingi: mabedui/mabedawi] yenye maana zifuatazo:

1. Mtu wa jamii ya Waarabu anayeishi jangwani au karibu na jangwa.

2. Mtu katili asiyemwonea mwenzie huruma.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili bedui/bedawi limechukuliwa kutoka neno la Kiarabu  'badawiyyun (soma: badawiyyun/badawiyyan/badawiyyin  بدوي)*  lenye maana zifuatazo:

1. Mkazi wa eneo la jangwani lililowekwa makazi, malisho na panapopatikana maji.

2. Mtu anayelinda na kuendelea na utamaduni wake wa asili.   

Kinachodhihiri ni kuwa neno 'badawiyyun بدوي lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno bedui/bedawi halikubadili maana yake ya mkazi wa jangwani katika lugha asili- Kiarabu, likaacha maana ya mtu anayehifadhi na kuendelea na utamaduni wake wa asili na likachukua maana mpya ya mtu katili asiyemwonea mwenzie huruma.

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)