ETIMOLOJIA YA NENO 'BAYANI' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'BAYANI' (/showthread.php?tid=2788) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'BAYANI' - MwlMaeda - 07-24-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'BAYANI' Neno *bayani* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: i-/i-*] yenye maana ya *stadi mojawapo katika mafunzo ya lugha ya Kiarabu inayohusu ujuzi wa kuzungumza.* Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *bayani* limechukuliwa kutoka neno la Kiarabu *'bayaan* *(soma: bayaanun/bayaanan/bayaanin بيان/البيان)** lenye maana zifuatazo: 1. Maelezo kuhusu bidhaa anayoyatoa mzalishaji wa bidhaa au wakala/muuzaji wake yanayoweka wazi aina ya bidhaa, kiwango chake, uzito wake na hata utumiaji wake. 2. Ubini wa mtu asiyejulikana asili na nasaba yake; *bin bayyaan بن بيان.* 3. Ufasaha wa kulieleza jambo fulani. 4. Taarifa itolewayo baada ya kikao cha pande mbili, *bayaanum mushtarikun بيان مشترك.* 5. Taaluma ya lugha ya Kiarabu ya kuelezea maana moja kwa njia tofauti kama vile *tashbihiتشبيه , majazi مجاز na kinaya كناية.* Kinachodhihiri ni kuwa neno *'bayaanun بيان* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *bayani* halikubadili maana yake katika lugha asili- Kiarabu. *TANBIHI:* Bayani, Kiarabu *Bayaan/Al-Bayaan البيان* ni moja ya fani za *Balaagha ya Kiarabu*, taaluma ya ufasaha wa kusema na kutia madoido. Fani nyingine mbali ya *ALBAYAAN البيان (Rhetoric)* , ni *ALMAAN المعاني (Semantic)* na *ALBADII'I البديع (The Art of Figures of Speech/The Art of Metaphors and Stylistics/Good Style).* *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |