NYERERE NA SAFARI YA KANAANI - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi andishi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=7) +---- Forum: Tamthiliya (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=53) +---- Thread: NYERERE NA SAFARI YA KANAANI (/showthread.php?tid=2789) |
NYERERE NA SAFARI YA KANAANI - MwlMaeda - 07-24-2022 Oktoba, 1966 kulizuka mgogoro mkubwa wa kihistoria kati ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Muhimbili. Wanafunzi hawa walifanya maandamano makubwa hadi Ikulu wakipinga vikali sera ya kuwataka wajiunge na Jeshi la kujenga Taifa (JKT). Wasomi hawa walilalama kwa hasira wakisema, "afadhali wakati wa mkoloni kuliko serekali ya Nyerere. Mkitulazimisha basi tutaenda KIMWILI, lakini MIOYO yetu, asilani, haitaenda JKT..." Katika kuukabili upinzani huu, Mwalimu, katika ile hotuba maarufu: "Tanzania itajengwa na wenye moyo" aliwacharaza viboko baadhi ya wasomi hao kadamnasi na kuwafukuza takribani wanafunzi 400 warudi kwao, wakalime! Mwandishi anatudokeza, miongoni mwa masuala mengine kuwa: Mgogoro huu wa 1966, ulichangia katika kukuza mimba ya safari ya Kanaani nchi ya asali na maziwa.Hapana shaka kuwa tamthiliya hii, iliyoandikwa kwa ustadi kabisa, ni kitabu muhimu kwa wanasiasa, wasomi na wapenzi wote wa fasihi ya Kiswahili.
|