Usawiri wa wahusika wa kike katika kazi za zainabu Burhani
Utafiti huu umeshughulikia usawiri wa wahusika wa kike katika kazi za Zainabu Burhani. Mtafiti amehakiki riwaya tatu zake mwandishi huyu. Kazi zilizochanganuliwa ni Mali ya Masikini (1981), Mwisho wa Kosa (1987) na Kipimo cha Mizani (2004).
Burhani katika kuwasawiri wanawake anapiga vita mfumo wa kuumeni ijapokuwa haepuki athari zake kabisa. Hii yatokana na malezi na pia dini yake ya Kfslamu.
Amejitokeza na vizazi tofauti vya wanawake; He kichanga kina shime ya kupambana ili kiweze kujikomboa. Kwa upande mwingine kizazi kikongwe kimekubah hali ilivyo.
Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni kitengo kimoja cha mtazamo-kike ambayo ni nadharia ya unisai wa Kiafrika. Nadharia hii huj aribu kueleza matatizo yanayowakabili wanawake wa Kiafrika, kinachoyasababisha na jinsi wanavyoweza kujiepusha nayo.
Kupitia hii nadharia ni dhahiri kuwa wanawake wa Burhani wamesawiriwa kwa mtazamo hasi na j amii na pia kuwekwa katika nafasi ya pili. Haya yote yanasababishwa na itikadi ya mfumo wa kuumeni inayowafanya hawa wanawake lcuikubali half yao. Hata hivyo kuna matumaini kupitia kizazi kichanga cha wanawake ambao wanajitahidi kuikata hii minyororo. Tasnifu hii imegawanywa katika sura saba.
Sura ya kwanza ni utangulizi wa utafiti ambapo mada ya utafiti, madhumuni ya utafiti, sababu za kuchagua mada pamoja na upeo wa utafiti huu zimeshughulikiwa. Aidha yaliyoandikwa kuhusu mada hii pamoja na nadharia iliyoongoza utafiti huu zimej adiliwa.
Sura ya pili inashughulikia swala la itikadi na sura zake mbalimbali. Tumechunguza ni vipi itikadi hizi zinavyomwathiri mwandishi ambaye ni mzaliwa wa jamii anayoishughulikia. Katika sura ya tatu uhalisi wa mwanamke wa kiafrika umesawiriwa. Nayo sura ya nne imeshughulikia jinsi mwanamke wa Kiafrika alivyo na uwezo wa kujitegemea. Sura ya tano imemsawiri mwanamke wa Kiafrika anavyojitokeza kuwa shujaa na hata mtawala katika j amii.
Sura ya sita imeshughulikia jinsi mwanamke kama mwanamume, alivyo na nafasi katika uj enzi wa j amii.
Sura ya saba ni hitimisho linalotoa muhtasari na matokeo ya utafiti huu, pamoja na mapendekezo ya mtafiti. Mwisho kabisa kuna marej eleo ya utafiti huu.
Jambo linalojitokeza kupitia usawiri wa wahusika wa kike wa mwandishi Burhani ambaye ni mwanamke ni kuwa, katika uandishi mwandishi awe ni wa kiume au kike huathiriwa pakubwa na itikadi ya jamii yake. Hii ni kwa sababu malighafi yake hutokana na mazingira anamoishi. Asasi za kidini na kitamaduni, kwa mfano zina athari kubwa kwa mtazamo wa Zainabu Burhani. Chanzo>>>>>>
Karne ya ishirini na moja kwa hakika imeshuhudia kuingia kwa teknolojia mpya katika nyimbo za Kiswahili. Teknolojia hii ilijiimarisha kwa kiwango cha juu na kupata
mashiko na mwelekeo wa utandawazi. Utandawazi si mfumo mpya katika ulimwengu wa
sayansi ya habari na teknolojia mpya. Mfumo huu umekuwepo kwa karne nyingi japo
kwa viwango tofauti kutoka karne moja hadi nyingine.
Kuingia
kwa dhana ya utandawazi katika fasihi simulizi kumeleta maingiliano na
mabadiliko mengi Kitaifa na hata Kimataifa katika tanzu zake nyingi. Kwa upande
wa mashairi na nyimbo maingiliano haya yanaonekana dhahiri na kuleta mabadiliko
makubwa katika jamii. Vijana wengi hususan wale wa Afrika ya Mashariki
walizitumia mashairi yao kuielezea jamii juu ya matatizo wanayopambana nayo
kila siku. Mathalani ukosefu wa ajira, umaskini waliokuwa nao, athari za
ukosefu wa ajira kwa vijana, uongozi, polisi, mahakama, n.k..
Kutungwa,
kuimbwa na kuonekana majukwaani kwa wasanii na mashairi haya kumewezesha vijana
kuwa wabunifu, wajasiriamali na weledi wa kueleza kero zao na matatizo
wanayopambana nayo katika maisha ya kila siku. Kwa mfano, mashairi ya msanii Ras
Lion katika wimbo Umasikini Huu:
Umaskini
huu (x 3) Utaisha lini
Umaskini
huu (x 3) Utaisha lini
Umasikini
huu (x 3) Utaisha lini
Msanii
analalamikia kwa masikitiko makubwa umasikini uliokithiri tanzania bila ya
kupata jibu ya kuwa mwisho wake ni lini. Kwa upande mwingine anaikejeli nchi za
Tanzania pamoja na viongozi wake ambapo kila siku wanaulalamikia huku nchi ni
inao utajiri mkubwa wa raslimali. Hii inatuonyesha wazi kuwa msanii anaona
uchungu sana juu ya umasikini unaozikumba nchi zetu ilhali viongozi wake ni
matajiri.
Msanii
Jaffer Rhyme yaliyopo wimbo wake wa Niko Bize yaani nina shughuli nyingi,
anasema:
(…)
ndiyo pekee inayonifanya nipate ninachotaka
Umenipata
(brother) kaka ofisini hatujaliwi
Ndio
sababu hasa tunasafa, Kwenye muziki cash tunapata
Niko
Bize naandika rhyme kila time nnayopata
Sio
bize tu for nothing, Bize nageti something
Kwenye
life time hivi sasa kazi ni kazi afisa
Ili
mradi tu inalipa ukiifanya kiuhakika
Ni
mfano mwingine wa kejeli inayowasema viongozi wa siku hizi. Kiongozi kila siku
anakuwa safarini bila kujali nchi yake na wananchi wa eneo lake wanaishi namna
gani. Kila siku kiongozi anapoulizwa jambo fulani yeye anajibu kuwa hana nafasi
kwa kuwa ana kazi nyingi (Niko Bize).
Kuwa bize huko hakumsaidii yeye wala wananchi wake bali hutumika kama fimbo ya
kukwepea majukumu yake.
Kwa
upande mwingine, msanii Jaffer Rhyme anaongeza kwamba wapo viongozi wengine
ambao wako bize kwelikweli. Hawa ni wale waliomeza au walikunywa damu ya
bendera. Viongozi hawa ni wale wenye kuona uchungu kwa wananchi wake. Hawa ni
wale wenye kujitoa mhanga kwa ajili ya kuitetea jamii nzima bila kujali uwezo
walionao wanajamii. Pia hawa ni wale viongozi wanaokosa muda wa kuzurura ovyo
na kupata nafasi ya kuwasikiliza wananchi waliowachagua. Maudhui ya mashairi
haya ndio msingi mkuu wenye kujengwa na utandawazi.
Kwa
upande mwingine tunauona mashairi ya Mr
Ebbo katika wimbo wa Mi Mmasai Bana:
Mi
Mmasai bwana nasema mi Mmasai,
Nadumisha
mila zile wengine walishashindwa,
Mi
Mmasai bwana nasema mi Mmasai.
Naruhusu
kushangaa kwa wageni na wenyeji,
Mi
Mmasai bwana nasema mi Mmasai.
Tamaduni
asilia ilobaki Afirika…
Msanii
anatamba kwa kulisifia kabila lake la Kimasai, mila na desturi za Kimasai
zilizomzunguka na ambazo zinazomshangaza kila mtu. Anasema kuwa hata utandawazi
utandawae namna gani yeye hawezi kuuacha utamaduni wake huo. Mmasai huyu kwa
namna moja au nyingine anawasema wale wote wenye tabia ya kuukana utaifa wao na
kuufurahia utaifa wa wengine kuwa hawatafaidika lolote. Aidha mashairi haya
yanazisema nchi na makabila mengi kuwa yameshindwa kudumisha tamaduni zao na
kuiga tamaduni za kigeni.
Mashairi
ya wasanii wengi yamegubikwa na kasumba waliokuwa nayo wanajamii wengi ya kuwa
Kiingereza ni lugha ya wasomi. Kwa kasumba hiyo wasanii wanachanganya na lugha
za Kiingereza na Kiswahili/Kabila jingine kama mbinu za kuwapata wapenzi wengi
na wasomi. Kwa mfano mashairi ya msanii Lady JayDee katika wimbo wake What I need from you is understanding:
Ninachotaka
kutoka kwako maelewano
What
I need from you is understanding
nakupenda,
nakutaka nakuhitajiii
I
love you, I need you …
Nakupenda,
Nakutaka …
Msanii
huyu pamoja na wengine wamesahau kwamba lugha ni kitu cha kujivunia kwa sababu ndio
kielelezo cha utamaduni wa taifa. Aidha utamaduni ndio msingi na roho ya taifa
lolote. Nchi ambayo haina Utamaduni wake yenyewe ni sawa na mkusanyiko wa watu
Tumeona
kwamba kejeli haitumiki tu katika kuukosoa uongozi katika jamii, ni mzaha wenye
kuweza kuwasema, kuwasengenya, kuwakebehi wanajamii wote kwa lengo la
kuwarekebisha, kuwaonya na kuwaelimisha ili waende sambamba na wanajamii
wengine. Kejeli haitumiki kwa lengo la kuwakosoa viongozi na watu wa tabaka la
chini tu, bali hutumika kuwakosoa hata wanazuoni wenye kwenda kinyume na
taaluma.
Kejeli
ni mojawapo ya mbinu ambazo hutumiwa na wasanii na waandishi katika muktadha wa
kuelimisha, kukosoa na kuburudisha jamii. Aidha, kejeli hutumika kwa malengo ya
kuyaweka wazi mambo yaliyopo katika jamii, kulingana na mabadiliko na matukio
yaliyopo na yanayotokea.
Kejeli
hutoa uhuru wa waandishi na wasanii. Kwa hakika hii ni njia ya pekee sana
ambazo inawapa wanajamii nafasi ya kushiriki kwa katika kuwakosoa walioko
madarakani na kuifanya kazi yao kuwa nyepesi kueleweka.
Katika
kipindi cha ukoloni, kipindi cha baada ya ukoloni na kipindi tulichonacho hivi
sasa cha utandawazi, mbinu za kejeli zimekuwa zikibadilika badilika. Hii
inawezekana kwamba ni kwa sababu kadri ya mfumo wa maisha na mbinu mbalimbali
za kupambana na mabadiliko hayo ya maisha zinavyobadilika, ndivyo na mbinu za
kejeli zinavyobadilika. Kwa mfano hivi asa vijana wamebuni michezo ya
kuchekesha inayorushwa katika baadhi ya vituo vya televisheni vya Tanzania kama
vile Ze Komedi iliyokuwa ikionyeshwa
kwenye EATV chaneli 5, The Original
Komedi inayoonyeshwa na TBC Mizengwe
inayooneshwa kwenye kituo cha ITV; na baadhi ya vituo vya televisheni vya Kenya
kama Vitimbi au Vioja Mahakamani vinavyooneshwa na kituo cha KBC wanaitumia kejeli
kuusema uozo, ufisadi, unyama, udhalilishwaji, unyanyapaa na ukandamizwaji
ulioshika kasi katika jamii. Aidha vikundi hivi hutumia kejeli kuwasema
wafanyakazi, wala-rushwa na wanajamii vigeugeu walioko na wanaoziongoza nchi na
jumuiya mbalimbali. Kufanya hivyo kunaisaidia jamii iliyoko mbali na miji mikuu
kufahamu kinachotokea ndani na nje ya nchi yao.
Vikundi
vya vichekesho na dhana yao ya kejeli husaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza
uchovu wa wanajamii baada ya shughuli nyingi na nzito za mchana kutwa. Hii ina
maana kwamba jamii inapokusanyika pamoja na kuburudishwa kwa kuviangalia
vikundi hivi vya vichekesho, inapunguza uchovu kwa kucheka na kufurahi. Hii pia
ni kwa sababu, maigizo yanayo manufaa kwani yanabeba ujumbe muhimu ambao kwa
hali ya kawaida hauwezi kubebwa na sanaa nyingine. Kwa mfano, suala la UKIMWI
ni vigumu kuliongelea kwa urahisi bila kuigiza au kwa kuonyesha picha. Kwa
kupitia vichekesho vyenye kejeli wana- jamii hujikuta wakiwa na shughuli za
kufanya baada ya kazi na kujiepusha na mambo mengi yenye kusababisha maambukizo
na usambazaji wa Virusi vya UKIMWI.
Ifahamike
wazi kwamba, kejeli katika fasihi ya Kiswahili na kumbo zake hubeba ujumbe
mzima wa kazi ya msanii au mwandishi kisaikolojia, kifani na kimaudhui katika
kujikamilisha kwake.
Kwa
mfano, wanamuziki wetu wa kizazi kipya, wana taarabu, wacheza maigizo,
wachekeshaji, wanakomedia, wanakomiki na vikundi vingine vingi vya kisanii.
hutumia kejeli kuielimisha jamii juu ya janga la madawa ya kulevya. Wasanii
wetu hawa wamefanikiwa kwa kuiangazia misuguano iliyopo katika serikali,
jitihada za kuinua uchumi, maisha bora, n.k..
Hivyo
ni wajibu wa wasanii, waandishi na wanazuoni wengine kuhakikisha kuwa
wanaitumia mbinu hii na kuiendeleza ili kufichua uozo, ubadhirifu, ufisadi,
ufidhuli uliopo, unaojitokeza na unaozidi kujikita katika jamii na taifa zima
kwa ujumla.
MAREJELEO
Balisidya,
M. L. 1982. Uchunguzi katika fasihi simulizivizingiti na mkabala. Katika makala
za
semina
za TUKI na makala mbalimbali. Dar es Salaam. TUKI.
Gibbs,
R. W. 1994. The Poetics of Mind. Figurative thought, Language &
Understanding.
Cambridge:
Cambridge University Press.
Honero,
L. N. na wenzake. 1980. Matunda ya Azimio la Arusha, Mashairi ya Mwamko wa
Siasa.
Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili: Dar es Salaam.
Kezilahabi,
E. 1988. Karibu Ndani. Dar es Salaam: Dar es Salaam University Press.
Kezilahabi,
E. 1999. Kaputula la Marx. Dar es Salaam: Dar es Salaam University Press.
Khatibu,
M. S. 1988. Fungate ya uhuru. Dar es Salaam: Dar es Salaam University Press.
Mbatiah,
M. 2001. Kamusi ya Fasihi. Nairobi: Fotoform Ltd.
Mbogo,
E. 1981. Morani. Dar es Salaam: Dar es Salaam University Press.
Mtesigwa,
P. C. K. 1989. Methali ni nini? Katika Mulika juzuu Na. 56 Dar es Salaam: TUKI.
Muhando,
P. 1984. Lina Ubani. Dar es Salaam: Dar es Salaam University Press.
Mvungi,
T. A. 1985. Chungu Tamu. Dar es Salaam: Tanzania Publishing House.
Mvungi,
T. A. 1978. Raha Karaha. Dar es Salaam: Continental Publishers.
Mvungi,
T. A. 1995. Chekacheka. Dar es Salaam: Continental Publishers.
Mwakyembe,
H. 1980. Pepo ya Mabwege. Dar es Salaam: Longman.
Mulokozi,
M. M. 1989. Tanzu za fasihi simulizi. Katika Mulika juzuu Na. 21 Dar es Salaam:
TUKI.
Ngahyoma,
N. 1975. Kijiji Chetu. Dar es Salaam: Tanzania Publishing House.
Penina,
M. M. 1984. Lina Ubani. Dar es Salaam: Dar es Salaam University Press.
Ruhumbika,
G. 1995. Miradi Bubu ya Wazalendo. Dar es Salaam: Tanzania Publishing House.
Rutashobya,
M. G. R. 1980. Nuru Mpya. Dar es Salaam: Tanzania Publishing House.
Kandoro,
S. 1971 Mashairi ya Saadani. Dar es Salaam: Mwananchi Publishing Ltd
Shaaban,
R. 1951. Kusadikika. Nairobi: Nelson & Sons.
Shaaban,
R. 1968. Kufikirika. Nairobi: OUP.
Short,
M. 1980. Style in Fiction. London: Longman
Wales,
Katie 2001. A Dictionary of Stylistics. Harlow: Personal Education.
Wamitila,
K. W. 2008. Kanzi za Fasihi. Misingi ya Uchanganuzi wa Fasihi: Nairobi Vide Muwa
Publishers Ltd.
Ipo hoja inayosema kwamba waandishi wa jinsia ya kike ni wachache ikilinganishwa na wale wa jinsia ya kiume. Kutokana na hayo, basi wenye kuwachora wanawake kwa mtazamo hasi zaidi ni wanaume, kwani wao ni wengi zaidi. Madai haya yamebainishwa na Simala (2002:72) alipofanya utafiti wake nchini Kenya. Yeye anasema ni jambo la kushangaza sana ni kwamba, mpaka hivi sasa nchi ya Kenya haina waandishi wengi wanawake wa fasihi ya Kiswahili kama ilivyo katika fasihi ya Kiingereza. Anatoa mfano katika majadiliano na waandishi wa Afrika nanukuu: waandishi wa kike waliohojiwa kutoka Afrika Mashariki (A. Mashariki) ni Grace Ogot kutoka Kenya na Penina Mlama (Muhando) kutoka Tanzania. Mjadala wa mwaka 1990 waandishi Muthoni Likamani na Pamela Kola ndio walihojiwa miongoni mwa waandishi wanawaake kutoka Kenya. Hivyo ni dhahiri kwamba wanawake wengi wasomi wamejikita zaidi katika uwanja wa kuhakiki na kuchambua fasihi kuliko kutunga kazi asilia za kubuni. Hata hivyo ni wazi kuwa fani hizi mbili haziwezi kutenganishwa kwani zinakwenda sambamba.
Mbughuni (1979) anasema kuwa katika riwaya za Kiswahili zipo picha mbili zinazokinzana za mwanamke, picha inayotokea mara nyingi ni mwanamke kama Hawa yaani mghilibu, asiyeweza kutawaliwa na mwanamume, mwanamke aliye chombo cha uovu, fujo na anayevuruga taratibu za jamii. Picha nyingine ni ya Maria yaani mama mtiifu, mwenye nyumba, pambo la mhusika mkuu wa kiume. Mwanamume anawakilisha maadili mazuri na anaokoa wanawake kwa njia ya kuoa. Katika riwaya mwanamke anayefanya mambo ya kujitegemea au anayepigania maslahi yake anaadhibiwa.
Mbughuni (1982) anabainisha kuwa uchorwaji wa wahusika unategemea ufafanuzi wa tabia au dhana fulani. Kwa mfano akielezea uchorwaji wa Rosa katika riwaya Rosa Mistika, anasema kuwa uchorwaji wake unasisitiza jinsi mazingira, silika na malezi vinavyomuathiri msichana Rosa. Rosa anachorwa kuanzia utotoni akinyanyaswa na baba yake hadi anapokuwa shuleni ambako anakutana na mwalimu mkuu.
Balisidya (1982:2) anabainisha taswira kadhaa zinazomhusu mwanamke, Taswira hizo alizoziainisha ni mwanamke kama mama, mwanamke kama chombo cha kumstarehesha mwanamume na mwanamke kama chombo cha kumilikiwa na mwanamume. Taswira hizo alizoziainisha Balisidya, zimeangaliwa na waandishi wengine wengi kwa mitizamo tofauti. Ila yeye Balisidya alimaanisha yafuatayo:
Katika taswira ya u-mama, Balisidya anaona kuwa mwanamke ni mlezi wa familia, hulelewa toka utotoni huku akijua jukumu hili la kulea familia. Haya yana uhalisia wake kwani tunawaona watoto wadogo katika michezo yao ya kitoto, wanawake huonekana wakipika, wakiosha vyombo, wakilea watoto, na kadhalika, ilhali wanaume
wakionekana kwenda shambani, kujenga nyumba, na kadhalika. Kwa upande mwingine,
tunakumbana na ukweli kwamba, mafunzo anayopewa mwanamke unyagoni huhusisha
mambo yote muhimu katika kulea familia, kumtunza, kumnyenyekea na kumtii
mwanamume, shughuli za jikoni, na kadhalika.
Balisidya anaona fasihi
kwamba, nayo hujikita kwa namna fulani katika kumpa mwanamke nafasi ileile ya
ulezi kupitia hadithi, michezo ya watoto na nyimbo. Suala la mwanamke
kumstarehesha mwanamume limebainishwa na kujadiliwa na Balisidya. Ameona kuwa,
taswira hii inamdhalilisha mwanamke kwani inamchora kwa undani jinsi anavyotumiwa na mwanamume ili kukidhi
utashi wa haja zake za mapenzi. Mwandishi anaona taswira hii hujengwa kwa
mafunzo yanayotolewa katika jamii hususan miviga wawapo mafunzoni ya unyago,
ambapo wasichana hufundwa jinsi ya kukidhi haja za wanaume.
Mafunzo hayo
yamemsukuma mwandishi kuonesha msimamo wake juu ya manju wanaoendesha mafunzo
hayo na kuyapitisha kwa jamii kama kaida za jamii husika. Jamii imeshindwa
kutambua kuwa jukumu la mafunzo ya miviga huzilenga jinsia zote mbili ili
ziweze kuishi pamoja kwa kusaidiana. Huu ni mfano na msimamo wa mwandishi ambao
unaonesha namna waandishi wa kike wanavyoyaandika haya katika muktadha wa kumdunisha
mwanamke mwenzao katika utanzu huo wa fasihi ilhali waandishi wa kike ndio
tegemeo na msaidizi wa kumtetea mhusika wa kike. Hapa inatubidi kutoa wito kwa
wahusika hawa kujizatiti katika kuandika fasihi yenye malengo ya kuumba upya
uhai na taswira ya mwanamke katika kazi za fasihi.
Muhando (1982: 41)
hayupo nyuma katika kuandika kazi za fasihi, Yeye anamtumia mke wa mwanasiasa
kwa lengo la kubainisha uhalisi huu katika jamii. Mhusika huyu anasawiriwa na
mwandishi kuwa ana wajibu wa kumridhisha na kumfurahisha baba watoto, la sivyo
hatapata chakula. Kwa hakika huu ni udhalilishwaji wa hali ya juu unaofanywa na
jinsia ya kiume. Hali hii inasikitisha kwani kila mtu mwenye uwezo wa kufanya
kazi hana budi kula pia. Wapo wanaume wenye tabia za kuwatesa, kuwadhalilisha,
kuwanyima haki zao na kutoa adhabu dhalilishi kwa wanawake wao. Kosa hili
linasababishwa na mambo mengi ambayo tutayajadili katika kipengele kifuatacho.
Kwa upande mwingine
haya yanatokea kwa sababu ya unyonge wa mwanamke kujiona kiumbe dhaifu mbele ya
wanaume na pia hali halisi za kiuchumi, ambazo husababishwa na wanaume
wasiowaruhusu wanawake wao kufanya shughuli za kujiingizia kipato. Kwa kufanya
hivyo, mwanamke anawajibika kumnyenyekea mwanamume ili mradi apate chakula na
kinga.
Mbilinyi na wenzake
(1991) wanabainisha kwamba nafasi ya wanawake inabadilika mara kwa mara, na
hivyo wajibu wao katika jamii hubadilika pia. Kutokana na hayo, picha na
mwonekano wa wanawake unaoonekana unaowakilishwa katika kazi fasihi kuwa
unabadilika. Picha hiyo ya wanawake inayowakilishwa katika tamthiliya leo
ambayo ni aina mojawapo ya fasihi ya Kiswahili anadai kuwa inatokana na kuwepo
kwa uchumi wa aina mbili: uchumi wa jadi na ule wa kisasa. Ili kuendeleza
uchumi aina hizi mbili bila ya kuathiri au kufifia kwa mfumo wa ukabaila ni
lazima kuleta mabadiliko katika sekta ya kazi kwa wanawake. Pamoja na hayo,
kila mtu katika jamii anatakiwa kuwajibika ipaswavyo katika majukumu ya maisha
ya kila siku.
Balisidya (1982)
anasema kwamba “ukandamizaji wa wanawake na wanaume unategemea sana mahusiano
yao ya mapenzi” Yeye anabainisha dhamira tatu kuu za wanawake katika kazi,
hususan fasihi simulizi. Anamwonesha kama mama watoto, chombo cha kumfurahisha
mwanamume na mwanamke kama mali. Hata hivyo wanawake wachache sana
wanajishughulisha na fasihi simulizi na sanaa au sanaa za maonyesho. Hii ni
kwasababu wanawake hawakupata elimu ya kutosha kama au sawa na wanaume. Pia ni
kwa zile sababu tulizokwisha kuzitaja ya kuwa wanabaguliwa katika elimu.
Ubaguzi huo unawazuia wanawake wasipate vyeo vya juu na wengine wanavunjika
moyo na kukataa kujaribu kazi zinazofanywa na wanaume.
Kwa upande mwingine,
wanawake wanasaidia sana katika kujengwa na kuendelezwa kwa taswira na picha
potofu za wanawake wengine. Hii ndio sababu iliyomsukuma Khonje (1979) kuandika
kuwa wanawake wanasaidia kujenga uovu wa wanawake kwa njia mbalimbali.
Akishadidia hayo, ametoa mfano kuwa, katika familia wanawake wanawafundisha
watoto msingi ya uonevu, nafasi tofauti ya wanawake na wanaume na madaraka ya
mwanamume kama mkuu wa familia. Hivyo wanawake hawajaungana pamoja katika
kuendesha mapambano dhidi ya ubaguzi na kubaguliwa kwao. Badala yake wanasaidia
kujenga wazo kwamba mahali pa mwanamke ni nyumbani kulea familia na sio nje ya
nyumba.
Mwanga (1984) amekwepa
kumsawiri mwanamke katika hali ya kudhalilisha akilinganishwa na Balisidya
katika riwaya ya Shida. Pamoja ukwepaji huo, bado kuna taswira kadhaa
zilizojitokeza katika Hiba ya Wivu, zenye vipengele vya kumdhalisha mwanamke.
Taswira hizi ni utegemezi wa mwanamke kwa mwanamume, mwanamke kuwa kitu adhimu
na laghai.
Swila (2000)
ameichunguza nafasi ya mwanamke katika magazeti ya Kiswahili ya Uhuru na
Majira, haya ni magazeti yanayotolewa kila siku nchini Tanzania. Kwenye
magazeti haya aliangalia hadithi fupi, ambazo hupendwa kusomwa na wasomaji wa
fasihi. Katika uchunguzi wake huo, amegundua kuwa karibu robo tatu ya hadithi
hizo zimemchora mwanamke kwa mtazamo hasi hususan katika matumizi ya lugha na
maudhui. Amemalizia kwa kusema kuwa katika usawiri wa mwanamke kwa kiasi
kikubwa ni hasi, wanamchora mwanamke kama mshawishi aliyewekwa kwa ajili ya
kumvutia mwanamume kimapenzi. Masimulizi haya yameonyesha kuwa mwenye akili na
haki pekee ya kifalme ni mwanamume.
Momanyi (2001)
anabainisha kuwa wanawake wamepewa taswira za aina mbili: taswira ya kwanza ni
ile ya motifu ya Bikira Maria4 na taswira ya pili inayomsawiri mwanamke kama
motifu ya Hawa.5 Kuna waandishi ambao wamekoleza mielekeo ya kifeministi katika
kazi zao ili waufundishe umma kuhusu usawaq na uwezo wa wanadamu wote. Miongoni
mwao ni Momanyi (2004 na 2006) kama alivyoandikwa na Richard na wenzake (2007).
Manufaa ya nadharia hii inayozungumzia masuala ya wanawake ni kupigania usawa
miongoni mwa wanadamu na kuonesha udhahifu wa mfumo dume6 . Pia kutetea uhuru
wa mwanamke katika kufurahia haki zote za binadamu.
Tamathali za usemi ni aina ya matumizi ya lugha yanayohusishwa sana na ushairi hata wakati mwingine waandishi wa nathari.
Ni aina ya msemo fulani kwenye lugha unaojaribu kufupisha maelezo kwa kuchora picha ya aina Fulani wenye kujaribu kushawishi mawasijiano ya kisanaa kwa njia ya kufuma hisia kwa wasomaji au wasikilizaji.
1.Tashbihi.
Hii ni mbinu ya uhusisho baina ya vitu viwili.Pia ni mbinu inayotumia uhamisho wa kimaana;yaani sifa, tabia, umbo, sura, muundo au umbo kutoka kitu kimoja huhamishwa kwenye kitu kingine, lakini hapa uhamisho au uhusisho si wa moja kwa moja, bali hupitia katika maneno kama : mithili, kama, mfano wa, vile, sawa, useme, na maneno mengine ya kuonyesha mlinganisho kati ya vitu mbali mbali. Mifano :
Afya mwilini ni kama mafuta katika utambi wa taa
Ana upara kama jagwa la Sahara
Ali alinguluma useme simba mkali
Alikuwa na midomo mikubwa yenye nyama iliyojikunja kama pua ya nguruwe
Dunia ni kama uwanja wa mpira, kila mmoja anapasua kujua sehemu gani atapigania ushindi maishani mwake
Alikuwa na nyusi mfano wa mwezi mwandamano.
Katika sentensi ya, afya inalinganishwa na utambi wa taa.upara wa mtu fulani unalinganishwa na jangwa la sahara katika sentensi ya
2, katika sentensi ya tatu tunaona mgurumo wa Ali ulilinganishwa na ule wa simba n.k uhusisho huo ambao si wa moja kwa moja unjaotumia maneno kama : kama, mfano wa, useme….kuonyesha mlinganisho kwa vitu mbali mbali ni Tashbihi.
2.Sitiari :
Ni tamathali ya usemi ambayo kwayo kitu matendo ya kitu au vitu kvyenye hulka mbali mbali, hulinganishwa na hali sawasawa ya maumkbile au jinsi ya utendaji.
Katika sitiari, maneno ya mlinganisho hayatumiki.Mlinganisho wa sitiari hufichwa ndani kwa ndani na hufichuliwa kwa hisi tu.
Mifano :
Kamau alikua simba
Mapenzi ni majani huota popote
Kukopa harusi, kulipa matanga
Tabia njema ni mzizi mkuu wa fadhila
Ujana ni moshi, ukenda haurudi tena
Maisha ya duniza ni bahari
3.Tashihisi
Ni thamathali ya usemi ambamo kuna hali ya mlinganisho baina ya vitu viwili lakini sasa kimoja cha vitu hivyo ni chenye uhai na cha pili si kitu chenye uhai. Hiki kitu kisicho na uhai au kisicho na tabia za kibinadamu hupewa sifa, tabia, sura au matendo ya kiuhai, au kiutu na kibinadamu.
Mifano :
Ubaya hatimaye utamezwa na wema na sisi sote tushuhudie.
Wakati ulikua ukipiga mbio huwahi mwisho wa mtu yule.
Katika mfano wa 1, tumeona kwambaq wema unapewa uwezo wa kumeza kama vile mwanadammu anavyomeza kitu.Na katika mfano wa 2 tunaona wakati unapoewa uwezo wa kwenda mbio kama kitu chenye uhai.
3.uhaba una ndwele mbi, una ndele mbi
uhaba Uhaba huleta dhambi, mtu hutamani kuiba
Uhaba hupiga kambi, lango hutia bawaba
Katika ubeti huu kutoka shairi la Mathas E.Mnyampala tunaona kwamba uhaba unapewa uwezo wa kukumbwa na maradhi(ndwele), uwezo wa kumletea dhambi na uwezo wa kupiga kambi.
3.TAASHIRA :
Ni namna ya fani ya usemi, ambao kwao, kwa sababu ya mwambatano wa ujamii au uhusiano mkubwa uliopo kati ya vitu fulani, ishara, alama, dalili, au neno Fulani, hutumika kuwakilisha tendo au kitu tupendacho kutaja, badala ya kueleza wazi wazi .
Mifano :
Shoka la kata miti msituni
Anavaa kanzu za china
kila nyumba ina furaha kubwa ya mazao
Fadhila nyingi na shangwe zilifika siteshoni ya treni mjini Dar es
Salamu
Shoka lakata miti yametumika kawakilisha watu wenye kukata miti Kanzu za china huwakilisha ka knzu zilizotengenjezwa uchina furaha majumbani huwakilisha watu wenye furaha nyumani, n.k
(i) Alama au ishara hutumika kufidisha hali fulani ya utendaji.
(ii)kitu au chombo cha utendaji huwakilisha mtendaji au watendaji (iii) Tendo huakilisha mtendaji.
(iv)mahali kitu kilipotengenezwa huakilisuha kitu kitengenezwacho.
(v)mtendaji huakilisha tendo.
4.Takriri :
Ni kmtindo wa uneni wa fasaha, ambao msemaji kwa makusudi au nia mahsusi, hurudia neno au maneno yale yale ili kutia mkazo au msisitizo zaidi, juu ya jambo asemalo .Mtindo huu wa msemo wa msistitizo, huwa na nia ya kutia nanga jambo Fulani ili liweze kumwingia msikilizaji moyoni apate kulidhibiti vizuri.
Mifano: 1. Kifo hakiogopi kiumbe chochote duniani.Kifo hakimuopi mtawala au raia, Kifo hakina tajiri au maskini, kifo hakichagui mzee au chipukizi .Kifo hakina mkubwa au mdogo. Kila kitu chini ya mazingira kiomesha pigwa muhuri na kifo.
Ni mtindo wa uneni wa fasaha ambao kwao maono au mawazo mbali mbali yenye mgongano na uhitilafiano, huunganishwa pamoja kakika sentensi au kifungu cha maneno ili kufanya mvutano mkubwa zaidi wa mawazo.
Mifano:
Kukonda rahisi kunenepa kugumu
Matengano ni huzuni makumbano ni lfuraha.
Baada ya dhiki, faraja
Hawa wanaingia hawa wanatoka
6.Tabaini:
Ni mmtindo wa uneni wa fasaha, ambao kwao msemaji husisitiza kauli au ukweli na jambo Fulani kwa kutumia maneno yenye ukinzani, aghalabu neno “si”.
Mifano:
Lo, ama kweli Juma anafanana sana na babake, si kuwa, si nywele, si mdomo, si macho, si kichwa, si sauti !Ama baba na mwanawe wako kama pande mbili za sarafu.
Kwake watu wote walikuwa sawa, si mdogo, si mkubwa, si masikini, si tajiri. Kwa kutumia neno “si”siyo kwamba twakanusha au kubomoa kauli tusemayo.
7.Kinaya:
Tamathali hii hutumika kwa kusemea kitu kimoja kwa kumaanisha kingine.Tamathali hii huweza kuonekana katika neno au kauli Fulani katika muktadha Fulani ilimojitokeza, au katika shairi zima.Kwa mmfano, shairi “Bustani”ya S.A.Muhammad, katika mojawapo wa beti zake, latongoa hivi : Yamerudikwa machicha, na maganda ya matunda. Na mwiku uliochacha, na mbali uliovunda. Harufu inopekecha, yanukia naipenda Hakuna inomchusha, bustani ya maua. Kinaya hapa inajengwa kuanzia mustari wa tatu pale ambapo harufu inayopekecha kuwa inasemwa inanukia na kupendwa na hatimaye bustani na taka, machicha, maganda ya matunda ambayo unaambiwa hapana inomchusha.Kinyume kipo pia pale ambapo uchafu wa kupindukia huitwa bustani.
Kejeli:
Hii ni tamathali inayofanyia stihizai, kebehi au dharau.Anayefanyiwa kejeli huwa anasutwa kwa kutupiwa maneno ya kero. Kwa mfano : Wanyakyusa wanaoishi Tanzania Kusini wanawakejeli Wazungu jinsi wapendavyo pesa kwa kutumia dini:
Basikalija anasali wapi?
Kwenye mawe kwenye mawe
Watemi wanasali wapi?
Kwenye mizimu kwenye mizimu
Wazungu jee wanasali wapi?
Kwenye pesa kwenye pesa.
9.Tafsida:
Msemo wa adabu, ambao kwao mambo yasiyopendeza hatamkwi waziwazi, hasa hadharani, hutajwa kwa lugha ya siri bila kuchukiza au kuchafua moyo ili kinyaa au hali m, baya waonayo watu moyoni. Mifano :
Acha naye aone cha mtemakuni, Mungu amemnyoshea kidole.
Mbona mtoto yule ana mkono mrefu vile!
Tafadhali nikumbushe, umenitoka machoni kidogo.
10.Dhihaka:
Ni tamathali ya usemi ambayo inatumiwa kwa kusema maneno ya kumjukumu na kumdhihaki mwingine kisirisiri.
Mfano :
Bwana Bwanyenye wewe ni miongoni mwa matajiri nchini Tanzania, ama labda nikuite kabaila, nanyi makabaila wa siku hizi mu wakarimu sana.Juzi umetoa shilingi mooja kama ya dawa ikiwa ni mchango wako kusaidia ujenzi wa makao makuu ya TANU. Ingawa maneno yaliyoambiwa bwana Bwanyenye juu ya kutoa shilingi ikiwa ni mchango wa kusaidia ujenzi wa makao makuu ya TANU ni ya sukari, lakini yalikuwa machungu moyoni.Msemaji hakuwa na nia ya kumsifu bwana Bwanyenye kama mtu mkarimu, bali nia yake ilikuwa kumdhihaki bwana Bwanyenye kama mtu bahili asiye na moyo wa uzalendo bora.
11.Chuku:
Hii ina maana ya kutia chumvi jambo fulani linapojadiliwa.Kwa mfano, mwimbaji wa taarabu anapomwimbia mpenzi wake kuwa pendo lake lina thamani ya kuti ambayo usiku na mchana linang’aa na kuenea chumba kizima-hii ni chumvi tosha. Pendo nlako nil la kutii moyoni limeshakaa Mchana na lailati, nuru yake huzagaa Ah! Mpenzi nimo peponi.
12.Tanakali sauti :
Huu ni usemi unaoonesha jinsi maneno ya lugha yanavyoweza kuiga sauti halisi. Kwa mfano, fisi anapotandikwa mwangwi wa mjeledi anasikika “chwaaa!” Rangi yake ni nyeupe, ila si nyeupe peee. Alikuwa na weupe, wenye wekundu haba
Njiwa huyu hulia kooo!!
Mazoezi:
Katika maandishi haya onesha tamatali za usemi zilizotumiwa?
Pendo
Pendo, pendo wee!
Mbona huchoki kunisumbua?
Daima waninyanyasa,
Pendo adui ya wanadamu.
2.Mpenzi
Tanzania Tanzania, Tanzania!
Nakupenda kwa moyo wote,
Nchi yangu Tanzania,
Jina lako ni tamu sana!
Nilalapo nakuota wewe,
Niamkapo ni heri mama we!
Tanzania, Tanzania!
Nakupenda, kwa moyo wote!
suu ulimwengu bahali tesi
Kamau alikua simba mkali
mtoto huyo ana macho kama ya kobe
Nakwenda kwa haja kubwa
Ndege walijaa uwanja wote hata sindano haionekani.
Neno ubani [Ngeli: u-/u-] katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana zifuatazo:
1. Utomvu mkavu wa mti wa mbani ambao unapochomwa hutoa moshi na harufu maalumu unaotumiwa kufukiza.
Kuna methali : la kuvunda halina ubani; jambo linapokwenda kombo, huwa limekosa mwongozaji.
Kuna msemo : wangu wa ubani; umpendaye kwa dhati.
Kuna nahau : tia ubani; ombea dua.
2. Kiasi fulani cha pesa anachopewa mfiwa kusaidia shughuli za mazishi au kuwa msaada.
Kuna msemo : toa ubani.
3. Utomvu wa mti fulani unaonatanata ambao unatumiwa kutengeneza vitu vitamu vya kuvutika kama mpira kama vile peremende.
4. Ada anayopewa mwalimu (wa madrasa) au Sheikh ukiwa ushuru wa kazi aliyofanya. Ada hii hulipwa mwanzoni au mwishoni mwa mafunzo.
Katika lugha ya Kiarabu, neno hili ubani (soma: lubanun/lubanan/lubanin لبان) ni nomino yenye maana zifuatazo:
1. Mmea wa familia ya uvumba ambao hutoa utomvu (gundi).
2. Utomvu (gundi) wa mti wa miiba ambao majani yake ni kama mihadasi.
Mhadasi (wingi: mihadasi ) ni aina ya mmea wenye majani mabichi majira yote wenye matunda yenye mchanganyiko wa rangi ya bluu na nyeusi.
3. Maziwa ya mwanamke anayomnyonyesha mtoto; kwa Kiarabu huitwa hasa libanun/libanan/libanin لبان)
4. Kamba nzito ya mkonge ambayo hutumika kuvuta meli wakati wa shwari. Kwa Kiarabu huitwa hasa
(libanun/libanan/libanin لبان).
Katika Kiarabu kisawe cha lubaanun لبان ni kandar كندر neno lenye asili ya kiYunani.
Kinachodhihiri ni kuwa neno ubani ( soma: lubanun/lubanan/lubanin لبان) lilipoingia katika Kiswahili maana yake ya msingi katika lugha yake ya asili - Kiarabu haikubadilika bali lilibeba dhana mpya ya kile kinachotolewa kumuhani mfiwa na ile ada anayopewa mwalimu wa madrasa au sheikh mwanzoni au mwishoni mwa mafunzo.
MASHAIRI YA CHEKA CHEKA ni diwani inayoongelea masuala hayo ni pamoja na uongozi mbaya,mapenzi duni,Ukombozi.Mwandishi Theobald Mvungi amejadili kuwa kwa kinamasuala ya hayo na alipoanza alipendekeza namna ya kukubaliana nayo;mfano katika shairi la CHANZO CHA HUO UOZOamewashauri viongozi wa dini kuhimiza waumini watende matendo mema na wamrudie Mungu badala ya kuhimiza michango kwa ujumla Mvungi ametoa mchango mkubwa katika kujenga jamii mpya. MAUDHUI Maudhui ni mawazo yanayozungumzwa na msanii wa kazi ya kifasihi pamoja mtazamo wa mwandishi au msanii juu ya mawazo hayo. A)DHAMIRA
UKOMBOZI
Mwandishi anazungumzia suala la ukombozi kisiasa ambapo kupitia shairi lake la TAIFA WAMELIZIKA,msanii anaonyesha namna wananchi wasivyo na uhuru katika masuala mbalimbali,msanii anasema; Ni sera zao tukufu, hangaiko la raia Hao ndio maarufu, wajua kuhutubia, Wajumbe mshiriki, katika huo uovu, Pia mshauri anaendelea kusema kuwa hakuna demokrasia ya kweli kwani watu wanaamriwa kila jambo kama ubeti huu usemavyo, Mezikwa demokrasia,chama kimoja ndio ngao Watu hawana nafasi,kutetea nchi yao. Mawazo ya ukakasi, mawazo ya mtitio, Wapenda jibu mkato, wale waongo wa hoja. Aidha mwandishi anaeleza kuwa ukombozi wa kweli utatekelezwa endapo kutakuwa na mshikamano wa dhati baina ya viongozi na wananchi, msanii amedhihirisha hayo kupitia shairi la MWINYI UMEWASHA MOTO:Angalia usizimwe.Hapa mshairi anaeleza kuwa wananchi wanategemea viongozi katika kuleta maendeleo, viongozi ni dira hivyo wapaswa wawe mstari wa mbele kwenye mambo ya maendeleo. Kwa suala la ukombozi kiuchumi mshairi anasema ni vigumu kupata maendeleo kama viongozi wataendelea kutumia madaraka kwa manufaa yao binafsi kama shairi la MTOTO ASO RIZIKI lisemavyo; Taifa wamelizika,mali zetu wamepora, Tena hawa wasifika,tunawapigia kura, Kwa hotuba wasifika,vitabu sura kwa sura, Uchafu ulivyojaa,dawa maji ya tufani
MAPENZI
Mwandishi amejadili dhamira hii kupitia mashairi mbali mbali kama vile NJIWA KIUMBE MTINI,katika shairi hili mshairi anasema katika mahusiano ya kimapenzi kuna umuhim wa watu kuchnguzana na kupeana muda kwani papara husababisha watu kutoa majibu yasiyo sahihi na kama mtu ana mapenzi ya dhati hatakata tamaa asumbuliwapo na ampendaye.Katika ubeti huu msanii asema; Matawi mkiyakwea,njia arukie kule, Si kwamba anakimbia, ni mbinu zake teule, Tabu kaniongezea,hata chakula nisile, Vivyo hivyo katika shairi la PENZI LISILO HESHIMA,mshairi anaonyesha namna mapenzi ya siku hizi yalivyogeuzwa bidhaa; Penzi la umaskini, kwa hii yetu dunia Ni penzi la nuksani,mpendwa hatapokea, Mpendwa hamuelewani,kwa maneno ya kumwambia, Mfukoni huna kitu,mpenda tahangaika.
DEMOKRASIA
Mwandishi amejadili suala la kidemokrasia katika shairi la TAIFA WAMELIZIKA ambapo wanawatumia wakunga na wajumbe mbalimbali wahudhurie vikao mbalimbali vya kujadili masuala ya nchi,lakini wao wasiende kupiga porojo na kufanya mawazo ya wachache bali wawasilisha mawazo ya wananchi Lakini Wabunge na wajumbe husinzia wawapo mikutanoni badala ya kuchangia hoja zenye kuleta tija kwa wananchi wanaowakalisha majumbani wengi hujali posho zao matokeo yake mawazo ya wananchi hupuuzwa. kama ubeti huu usemavyo; Mezikwa demokrasia,chama kimoja ndio ngao, Watu hawana nafasi,kutetea nchi yao, Mawazo ya ukakasi,mawazo ya mtitio, Wapenda jibu mkato,wale waongo wa hoja. Msanii anawataka viongozi wakumbuke kutekeleza majukumu au wajibu wao kwa ufanisi na sio kwenda kusinzia wawapo mikutano kwani wao ni wawakilishi wa watu wao. 4.MATUMIZI MABAYA YA MALI YA UMMA Katika shairi la GUNIA LA MIKUTANO,mwandishi ameonyesha namna ambavyo viongozi wengi hutumia fedha za umma kinyume na utaratibu. mfano; kujilipa posho wawapo vikaoni,hata vikao visivyo vya ulazima.Aidha huandaa sherehe mbalimbali zinazohitaji fedha nyingi na ambazo haziwanufaishi wananchi.msanii anasema; Sherehe zenye utamu,raha ya wachache humu, Ni mateso kwa kaumu, wasoweza kujikimu, Sherehe si kipaumbele, mwelekeo uwe kazi
UZEMBE NA UKASUKU
Katika shairi la NI WAPI USHAURI msanii anakemea uzembe na kwamba watu hawafanyi kazi kwa kujituma bali wanataka wasukumwe,kwa mtazamo wake msanii anaona kufanya kazi kwa kusukumwa ni kama utumwa.Msanii anadhihirisha hili kwa kuwatumia wanaohusika na usafirishaji mazao toka kwa wakulima ambao huzembea na kufanya mazao yaoze mashambani ambapo hali hii huwakatisha tama wakulima ya kuendelea na kilimo.Msanii anasema; Wanawe idadi sita,wakulima maarufu, Pamba mahindi ufuta,tena wana watiifu, Fedha wanazitafuta,wanunue maradufu Mazao yamo nyumbani,hayana mnunuzi. Pia katika shairi la TUAMBAE UKASUKU mwandishi anawaasa watu wanaoishi maisha yakufuata mkumbo kuwa maisha ya namna hiyo hayafai. Katika maisha mtu anatakiwa kuangalia jambo gani lina manufaa na lipi halina,lile lenye manufaa lifuatwe kwa lengo la kuboresha maisha.Hapa msanii anawazungumzia washairi kuwa watunge mashairi yenye lengo la kuleta maendeleo siyo kuwasifia viongozi wafanyapo mambo yasiyofaa kuwasifia.Mwandishi anaona kuwa mshairi bora ni yule anayesema ukweli asiyekubali kuwa kibaraka.Mwandishi anasema; Mshairi uwe huru,upige yako mafumbo, Usiwe kama kunguru,woga umejaa tumbo, Na usitoze ushuru,hapo utakwenda kombo, Wataka wanyonge,so wale waheshimiwa. Mwandishi anawataka waandishi na jamii kwa ujumla waishi kama vile walivyo na si kuishi maisha ya kuigiza kwa lengo la kuwafurahisha watu fulani. 6. DINI Mwandishi katika diwani yake amezungumzia upotofu unaojitokeza kwenye madhehebu yetu ya dini.mfano; Dini ya kikristo madhehebu ya wakatoliki na walutheri viongozi huimiza sana michango badala ya kuimiza matendo mema kwa waumini.Watu wanatakiwa kumrudia Mungu na kuacha dhambi,kuhimiza upendo na mshikamano badala ya kutenda hayo waumini hujazwa chuki kwa kurundukiwa michango.Msanii anasema; Nimechunguza kanisa,luteri na katoliki, Viongozi nawaasa,roho hazimpi chuki, Zile ibada za misa,watu wanajazwa chuki, Padri hanalo jambo,ila kudai michango. kupitia ubeti huo mwandishi wa shairi la CHANZO CHA HUO UOZO anaonesha namna maana ya dini inavyopotoshwa watu wanachukizwa na kuchoshwa na michango na kuona kanisa kama sehemu ya maudhi badala ya faraja.Mwandishi anawataka viongozi wa dini kuwasaidia waumini wao waende mbinguni na sio kudai michango pekee.
SUALA LA UONGOZI
Mwandishi amejadili suala la uongozi kwa kuonesha namna viongozi wetu wengi wasivyo wasikivu na kutotekeleza wajibu wao.Mwandishi ameonesha namna ambavyo viongozi wengi wanavyoweka ahadi ambazo hazitekelezwi,ahadi zao ni za kutaka madaraka wakati wa kampeni za uchaguzi.katika shairi la MTOTO ASO RIZIKI mwandishi ameonesha namna viongozi wanzvotusaliti.Msanii anasema; Wasalitiwa mbali, wala si waamerika Ni hawana wala mali, hatamu walioshika, Weusi kwa kila hali, madaraka waloshika, Si wote hilo ni wazi, lakini ni wamo wengi. Katika shairi la MASHAIRI YA NGULU mwandishi ameonesha namna viongozi wanavyojipendelea na kufanya dhuluma kwa wananchi,wakulima na wafanyakazi hawatendewi haki wanadhulumiwa mazao na mishahara yao.Msanii anasema; Diwani unasaili,falsafa za kukwama, Uongozi usojali,taabu za wakulima, Wale wasio na hali,wanarudishwa nyuma, Waporwa mazao yao,kwa hoja za ulaghai. Tazama mfanyakazi,mshahara wa mwezi, Utani wa uchochezi,hautoshi hata nazi Ni vipi asiwe mwizi,nani asiye mwizi? Ujira wa moja juma, ati ndo wa wote mwezi. Katika ubeti huo hapo juu mwandishi ametoa mfano wa dhuluma hizo wanazofanyiwa wakulima kwa kulaghaiwa bei wauzapo mazao yao (bei hailingani na thamani ya mazao). Pia wafanyakazi wanapata mishahara midogo ambayo haikidhi mahitaji yao na ndiyo maana wengi wanapokea rushwa katika utendaji wao. Vivyo hivyo katika shairi la MUWAPI NAWAULIZA msanii ameeleza namna viongozi wanavyolala na kuacha baadhi ya watu kufanya watakavyo. kwa mfano; Wafanyabiashara kupanga bei za mazao ya wakulima watakavyo kwa madai kuwa biashara ngumu,Aidha wauzapo huuza kwa bei wazipendazo eti biashara huria. Katika shairi la RAIA SI MALI KITU Mshairi ameonesha kuwa viongozi hawashirikishi wananchi katika kutoa maamuzi, mambo mengine huamuliwa na viongozi na wananchi wanaambiwa tu kutekeleza. Mwandishi anawataka viongozi kutekeleza wajibu wao kwa ufanisi hasa ahadi wanazoahidi pindi wanapotaka uongozi. FANI
MUUNDO
Mwandishi amegawa mashairi katika makundi mawili, mashairi ya kawaida na tena ambapo aina zote kwa kuzingatia beti, vina, mizani na vituo. Kwa upande wa beti yapo mashairi yenye beti nyingi na yenye beti beti chache. Mashairi yenye beti nyingi ni pamoja na LAZIMA WAUMINI lenye beti 10, RAIA SI MALI KITU lenye beti 9 na yenye beti chache ni KIMOYO lenye beti 4. Mizani,mwandishi ameunga mkono mashairi kwa idadi ya mizani ambapo mashairi ya kawaida yana mizani 16 kwa mgao wa 8¤8kwa kila shairi, mfano shairi la MWENYEWE UMEWASHAMOTO. Hao wamekuzunguka,walaji hawako mbali, Vipigo vimetukuka,ndilo jina la awali, Hawa ndio wasifika,kwa hidhini na vibali, Usoni tadhani watu,lo aheri mbwa mwitu, Kwa upandewa ametumia mizani nane (8) kwa kila shairi, mfano shairi la SENG’ENGE Nipishe wewe seng’enge, Nipishe kando jitenge, Nipishe usinifunge, Usiwe haambiliki Vina,kwenye mashairi ya kawaida kuna vina vya kati na mwisho.Mfano shairi la CHATU MMEZA MATONGE. Sipendi yanatokea, shirika macho kufumba, Kukataa kusikiya, ya wapangaji wa nyumba, Watu walifikia, shirika la nyumba, Ndilo kimbilio lao, hawa wavuja majasho Katika ubeti huo kuna vina vya kati “a” na vina vya mwisho ni“mba” na upande wa tenzi huwa na vina vya mwisho. Mfano utenzi wa INDIRA Sifazo kwa jitihada, Tuishi kwa kawaida, Kwetu ukawa ushuhuda, Takukumbuka daima. Vituo,mwandishi ametunga mashairi yenye vituo vitoshelezi kwakuwa katika mashairi yake yote kila ubeti una kituo chake 2. MTINDO Mwandishi katika mashairi yake yote yamezingatia urari wa vina na mizani, pia ametumia mtindo na maelezo yaani anaelezea ufahamu alionao juu ya jambo analozungumzia.Aidha ametumia mtindo wa nafsi ambapo nafsi karibu zote zimetumika. Mfano -“Mwinyi amewasha moto” (U-nafsi ya pili umoja-wewe), -“Tuambae ukasuku” (Tu-sisi nafsi ya kwanza wingi), – “lazima mniamini (nyinyi- nafsi ya pili wingi) n.k. 3. LUGHA Mshairi ametumia vipengele mbalimbalivya lugha ili kuifanya kazi yake na mvuto wa kueleweka kwa hadhira, baadhi ya vipengele hivyo ni :- 4. TASWIRA/ PICHA Mshairi ametumia taswira mbalimbali yani zahisi,au za kuonekana.Mfano; -Shairi la KUNA NINI HUKO NDANI inamaanisha matumizi mabaya ya madaraka ), – CHATU MMEZA MATONGE linamaanisha matumizi mabaya ya mali za umma, GUNIA LA MIKUTANO (ufugaji wa fedha) METHALI Mshairi ametumia baadhi ya methali katika mashairi yake mfano –Taratibu ndio mwendo, katika shairi la MOYO, –Umoja ni nguvu, katika shairi la KAZI ZETU HARAKATI. TAMATHALI ZA SEMI Mwandishi ametumia tamathali za semi mbalimbali ili kuongeza mvuto kwenye kazi yake, mfano Ø Tashibisha Ni tamathali inayolinganisha vitu viwili au zaidi kwa kutumia viunganishi.mfano katika shairi la LAZIMA MNIAMINI mandishi anasema; Mlevi akakolea,kama tumbaku ya tozo Miguu ikalegea, katika kuchezacheza, Kaziongeza bia, watu wakatumbuiza, Watoto wakirimu,mradi kiitikio, vile vile katika shairi la MOYO mwandishi anasema; Moyo nimeushauri, lakini umekaidi, Moyo kiburi hatari, mfanowe kama radi, Moyo mefumbata shairi, unayakwepa maradi, Moyo mwilini mwangu,jiradi tuwe pamoja Ø Sitiari Ni tamathali inayounganisha vitu pasipo kutumia viunganishi.Mfano katika shairi la INDIRA Mwandishi anasema; Mwenzetu Gandi kwaheri, Moyo hutuna shwari, Machozi yetu bahari, Gandhi ulitudhamini. Aidha katika shairi la UTU UMEKUWA KIMA mwandishi anasema; Dhuluma ndio hekima, Utu umekuwa kima, Hafai huyo mnyama, Jumlaye ni uhuru. Ø Tashihisi Ni tamathali ivipavyo uwezo vitu visivyo binadamu kutenda matendo ya binadamu. mfano, katika shairi la NJIWA KIUMBE MTINI mwandishi anasema; Mmejaribu kujongea,ndege awe mkononi, Yeye juu hurukia, na muomba samahani, Nyimbo anaziimba, nyimbo zachoma moyoni, Basi mie kaabani, njiwa akitabasamu. Katika shairi ubeti huo njiwa amepewa uwezo wa kumwimbia mwanadamu nyimbo kuomba msamaha na kutabasamu.Matendo hayo kiuhalisia yanatakiwa yatendwe na watu sio ndege (njiwa). Katika shairi la MOYO unaambiwa uache jeuri na ukaidi na ujifunze busara. MKATO WA MANENO Baadhi ya maneno yamekatwa katika diwani hii ili kupata urari wa mizani na vina.Mfano maneno asotaka badala ya asiyetakana walojonea baala ya waliojionea, katika shairi la LAZIMA MNIAMINI na katika shairi la MOYO mwandishi anasemamekuwa badala ya imekuwa. Kwa ujumla Mwandishi amejitahidi sana kutumia utenzi na utumizi wa lugha na hivyo kufanya kazi yake iwe na mvuto.