MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI

Welcome, Guest
You have to register before you can post on our site.

Username
  

Password
  





Search Forums

(Advanced Search)

Forum Statistics
» Members: 5,481
» Latest member: Kundlimatching
» Forum threads: 2,178
» Forum posts: 2,256

Full Statistics

Online Users
There are currently 218 online users.
» 0 Member(s) | 217 Guest(s)
Bing

Latest Threads
Buy Vilitra 60 Mg |【Get E...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-24-2023, 11:45 AM
» Replies: 0
» Views: 0
How to take Cenforce50?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-19-2023, 12:59 PM
» Replies: 0
» Views: 0
About the Vidalista 60 Mg...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-04-2023, 04:07 PM
» Replies: 0
» Views: 0
What Is Vidalista 60?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-03-2023, 10:49 AM
» Replies: 0
» Views: 0
How to take Cenforce 100 ...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
03-29-2023, 02:37 PM
» Replies: 0
» Views: 66
How is Vidalista 10 Mg us...
Forum: Watunzi wa Kiswahili
Last Post: Kieth_winsett
03-27-2023, 01:26 PM
» Replies: 0
» Views: 117
Obtain Thesis Paper Assis...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Minny02
03-24-2023, 03:01 PM
» Replies: 0
» Views: 200
SEO services for sports f...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Maria Poland
03-17-2023, 01:51 PM
» Replies: 1
» Views: 223
NUKUU ZA KISWAHILI DARASA...
Forum: Nukuu
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:31 PM
» Replies: 0
» Views: 788
NECTA K4 2022
Forum: Mitihani
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:25 PM
» Replies: 0
» Views: 403

 
  MISINGI YA UHAKIKI KATIKA FASIHI YA KISWAHILI
Posted by: MwlMaeda - 12-28-2021, 04:10 PM - Forum: Uhakiki wa kazi za fasihi - No Replies

Misingi ya Uhakiki katika Fasihi ya Kiswahili
T.S.Y. Sengo
Madhumuni
Madhumuni ya makala haya ni kujaribu kuitafakari dhana ya uhakiki wa Fasihi ya Kiswahili na misingi inayoitawala na kuisimamia. Katika jaribio hilo, kutafanywa juhudi za kutoa maelezo ya dhana muhimu, kujadili misingi iliyopo na kupendekeza mingine, kudadisi na kueleza nafasi na kazi za mhakiki.
Maelezo
Uhakiki
Uhakiki katika Fasihi ya Kiswahili si taaluma yenye umri mkubwa. Umri wake haufikii hata robo karne. Dhana hii ya uhakiki kwa lugha ya kawaida, ina maana ya “upataji wa hakika au kweli ya jambo; maelezo yanayochambua maandishi kwa kufafanua mambo mbalimbali yaliyomo.”1 Upataji wa hakika au wa kweli ya jambo unahusu ujuzi mkubwa. Ujuzi huu si ule wa kiufundi na kisanii tu bali wa maarifa na hekima. Ajuaye ni yule mwenye uwezo wa kuona tofauti katika vitu vya kufanana na mfanano katika vitu tofauti, imani na itikadi tofauti, mazingira na hali tofauti, dhana na hoja tofauti, kauli na semi tofauti, na juu ya hayo atajua kuwa akiwezacho kujua si kila kitu na kwamba juu ya kila mwenye kujua kuna mjuzi zaidi. Hivyo maana ya uhakiki kuwa ni jitihada ya upataji wa hakika au kweli ya jambo yanazidi kuthibitisha hoja ya wanafalsafa kuwa kuhakiki sharti kukite katika kujua. Uhakiki hauwezekani kufanywa bila ya kuwa kinachohakikiwa kinafahamika ndivyo. Maana haya ndiyo yatakayotawala fikira za makala haya.
Ama kuhusu maana ya pili ya uhakiki kuwa ni “maelezo yanayochambua maandishi kwa kufafanua mambo mbalimbali yaliyomo,” ni dhahiri kuwa ufafanuzi huo sharti ukite pia katika kujua ndaninnje ya hilo jambo linalofafanuliwa, na fani ambayo imelipamba jambo lenyewe. Sharti iwekwe wazi kuwa si kila ufafanuzi ni uhakiki kwani maandishi ya fasihi yana mashiko yake mbali na yale ya maandishi mengine. Na makala haya yanashughulikia uhakiki wa maandishi ya kifasihi ambayo ni kazi zote za kisanaa zitumiazo maneno na viashiria mbalimbali. Na si fasihi yoyote bali Fasihi ya Kiswahili.
Uhakiki ni daraja ya juu ya maelekezo ya kisanii yenye kuwalenga watu wa aina tatu: wasomaji wa kawaida walio majumbani na maskulini, waandishi asilia wa kazi za sanaa, na watu wanaodhaniwa wana macho ya kuona na uwezo wa kutenda na kuyatafakari yasemwayo kwa lengo la kutengeneza. Msomaji hupata mwongozo wa namna bora zaidi za kumuwezesha kuifahamu kazi ya sanaa kutokana na viwango tafauti vya uhakiki tafauti juu ya shairi, ngano, riwaya, tamthiliya, n.k. Mwandishi hupata faraja na hamasa kutokana na uhakiki wa kazi zake, hukua na kukomaa; wachache labda hupata homa na kuingiwa na baridi kazi zao ziwekwapo sawa.
Uhakiki katika jadi za Kiswahili ndicho chuo kikuu cha mafundo makuu. Mathalani, katika maisha ya kila siku, methali huwakumbusha wanajamii: “Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu;” “Mgema ukimsifu tembo hulitia maji,” na “Haambiliki huachwa akaadhirika,” n.k. Hizi ni tahakiki za Idsanaa zinazotawala maisha ya kweli ya mja ya kila siku Uswahilini.
Kama uhaldki ni daraja kuu, ni wazi kwamba manyakanga wa chuo hicho sharti wawe watu wa aina yake. Si kila mfafanuzi wa jambo au mpataji kweli husibu kuwa mhakiki. Ni lazima uhakiki uwe umejikita katika ujuzi wa mtu ambave mzingiro wake wa kimaisha umepanuka na kupevuka na dari lake la akili na fahamu lina kina na kimo kikuu. Na ujuzi huo sharti uwe ujuzi ylio ndiwo kwa namna zote za kuutafutia na kuupatia; sharti uwe ujuzi wa kinadharia; misingi na utendaji kwa upande mmoja, na uwe wa umbuji mkuu kuhusu maisha ya jamii za watu na yao yote kwani fasihi huvielezea vyote vinavyowahusu watu hao na wala haichagui vile vya watu wasio duni wakiwa katika hadhara nyingine. Ama kwa hakika sanaa ya uhakiki ni sanaa kubwa na nzito inayodai umri na ukomavu wa aina yake. Haya hayako tu katika fasihi ya Kiswahili, fasihi ya Tanzania au fasihi ya Afrika tu bali yako katika misingi ya fasihi ya binadamu wowote na popote walipo. Kwa mfano, Thomas Cooke amepata kuandika kuwa “Ukuzaji wa ladha nzuri katika tungo za kishairi ndio ukuzaji pia wa tabia njema.” Kadhalika, “Hapana jingine linaloweza kulishughulisha taifa mbali ya uhimizaji wa waandishi bora.”2 Ni wazi kuwa mawazo haya yanaipa sanaa ya uhakiki nafasi, hadhi na dhima ya namna yake. Kanuni za kitu au jambo zimepewa sifa maalumu hapa ya kwamba zinahusiana sana na ubora wa tabia za watu, jamii na ubora wa yao.
Mhakiki
Mhakild ni msanii aliyekomaa katika nadharia, misingi na utendezi wa taalimu yake. Ni mkomavu wa kuona mengi katika sanaa anayoishughulikia. Tafsiri azitoazo huwa ndizo na zenye kulenga kuwanufaisha wasomaji, msanii wa kazi inayohakikiwa na hadhira kuu, yaani jamii. Ama mhakiki hawi ni “mlimaji” wala “mgongaji” kwani hizo ni ila katika sanaa ya kitaaluma, na si sifa kamwe. “Mlimaji” na “mgongaji” ni mtu atumiaye nguvu za mwili, sana hasira na hisia mfanano. Mhakiki hutumia ufundi, akili na hekima Kamwe mhakiki “halimi” wala “kugonga”.
Kusifu au kulaumu tu si sifa ya mhakiki bali ni haki yake na wajibu pia kuipima kazi kwa vigezo vyake na kusema kweli palipo ndipo. Msanii mstahiki sifa apewe na sababu zitolewe ili sifa hizo ziwe misingi kwa kazi zote nyingine za mithili hiyo.
Ni stahiki ya mhakiki kuitwa mwalimu kwani choyo na inda ya kuwaua wasanii watangulizi au wengine si sifa ya mhakiki kama ilivyo kwa mwalimu azalishaye madaktari, wahandisi na marais. Mhakiki hana gere wala tamaa ya kutaka awe yeye tu na wengine siwo. Na kwa kuwa mwalimu huyu kapevuka vya kutosha, upevu na ukomavu wake humpa hadhi ya mapenzi ya kweli. Ndipo Mtume Muhammad (S.A.W.) alipomfafanua mhakiki kwa maneno yafuatayo: “Ndiye mpenzi pekee yule ambaye atanionyesha udhaifu wangu na kunipa zawadi kwa kufanya hivyo.”3
Hivyo mhakiki ni yule na lazima awe yule ambaye huwa ni mfasiri wa jadi ya jamii anayoiwakilisha. Kazi yake hutegemea athari za muundo wa jamii, hisia, vigezigezi vya vionjo vya mwili, maumbile, wakati, pahala na hali nzima ya kuwepo kwa dunia ya sanaa ya uhakiki. Mwelekeo wake huwa ule wa ndani – nnje na wala si ule wa nnje – ndani. Jadi ya jamii moja huitawala jamii na jamii ikajithaminisha kwayo. Na mhakiki ni mlezi wa jamii yake kwa vile aitakiavyo kheri ya kuendelea zaidi na zaidi katika matengenezo ya vipengele vyote vya maisha ya mja bila ya kuua mlolongo wa jadi ya sanaa wala ya wasanii. Kwa taadhima kubwa, yafaa ikumbukwe kuwa “mhakiki ni mtu na kila mtu ana mipaka yake.”4
Fasihi ya Kiswahili
Kiswahili kwa asili ni lugha ya Waafrika walioishi pwani ya Afrika Mashariki kwa karne na karne. Kiswahili ni Kipwani, ni lugha iliyozaliwa kwa mchanganyiko maalumu wa lugha za Kibantu za jamii za awali ambazo zililazimika kuwasiliana zilipokabiliana baharini au nchi kavu. Kiswahili ni lugha ya muungano wa tamaduni kabla na baada ya majilio ya wageni. Historia hii ya awali iliparaganywa sana na wanasiasa wateule waliojificha katika maziaka ya utaalamu na, au umisionari.
Waarabu walipofika katika upwa wa Afrika Mashariki waliwakuta watu na lugha zao. Kuwaita “watu wa pwani” (sawahil) haikuwa na maana ya kuwa watu hao waliletwa na Waarabu, ama waliwazaa na wanawake weusi wa pwani hiyo. Waliokuja kutoka kwao walibakia kuwa Waarabu, Wamanga, Washihiri, n.k., na vizazi vyao vilivyochanganya damu viliendelea, hadi hivi leo, kuitwa Machotara. Mswahili kabakiza weusi na Uafrika wake.
Hivyo, kanuni za lugha – wiyati na zile za kijamii, zina dalili zenye nguvu kuwa jamii ya Waswahili wa pwani ya Afrika Mashariki isingeishi bila ya lugha kusubiri majilio ya wageni kwa vile ni maumbile ya waja kuwasiliana kwa kutumia lugha. Na kwa fikira za kitumwa ati Kiswahili kilikuwa zao la utumwa, Wazungu waliwatuma Waarabu kushika watumwa Afrika Mashariki, ukanda wa Sudani, Afrika Magharibi na kwingineko. Kwa nini basi Kiswahili kizaliwe na ubwana wa Waarabu waliokuja pwani ya Afrika ya Mashariki tu?
Falsafa nayo inaieleza lugha kuwa ndicho chombo pekee kinachounda na kutumia dhana. Falsafa hii inayoelezea utamaduni wa Kiswahili yaweza pia kuielezea Fasihi ya Kiswahili kwa kuwa ni fasihi iliyojitosheleza na kujikimu kistahiki.
Kwa hiyo, Fasihi ya Kiswahili ni taaluma ya maneno ya kisanii ya Waswahili, ya Wapwani. Makala haya yatakitisha fikira zake katika kweli hii. Hii haina maana kuwa madai ya kisiasa na ya kuhalalisha nafasi za kazi na masilahi ya kimaisha, hayana nafasi. Makala haya yanaheshimu mipaka ya mtumiaji Kiingereza na Mwingereza; mtumiaji Kichina na Mchina; mtumiaji Kinyanyembe na Mnyanyembe; na hali kadhalika Mpogoro aliyejifunza na kukitumia Kiswahili na Mswahili. Hii ni yakini ya kihesabu ambayo haihitaji mizengwe.
Fasihi ya Kiswahili, kwa hali hii ya pili, imekuwa na maana ya kazi za kisanaa zilizowasilishwa kwa Kiswahili. Inawezekana kuwa na fasihi ya Wangoni iliyoandikwa kwa Kiswahili. Sharti ionekane kweli iliyo dhahiri kuwa Ungonini si Uswahilini ingawa miongoni mwa Waswahili, Wangoni nao walikuwemo kama inavyozidi kujidhihirisha kuwa Wangazija wengi wa Visiwa vya Ngazija wana asili ya Umakua, Uyao, Umakonde wa kusini ya Tanganyika na kaskazini ya Msumbiji.
Hali hii ikiwekwa wazi, taaluma hukomaa. Ikionewa kinyaa, taaluma huzorota. Taaluma haitaki kuficha siri. Ndiyo sababu Fasihi ya Kingereza inafahamika kuwa ni Fasihi ya Waingereza na Fasihi kwa Kiingereza ndiyo ile yoyote nyingine iwayo bali hutumia Kingereza ikiwa ndiyo lugha ya mawasiliano. Na wataalamu wasionee haya fasihi zao za Kikwere, Kigogo, Kibondei, Kikerewe, Kipare, Kihehe, n.k., kwani zikipambanishwa na ile ya Kiswahili, kila moja ni fasihi ya hadhi yake na hapana moja iliyo bora kuishinda nyingine katika hali za kawaida.
Wasiwasi wa baadhi ya wanataaluma wa kudhani kuwa Kiswahili kimemeza lugha nyingine hivyo bora nao waiue asili va Kiswahili ili kila mtu awe MswahiB hauna mashiko ya kitaaluma wala ya ukomavu wa kitaalamu. Nao umewafikishia watafiti wa Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kupendekeza kuwa jina la taasisi hapo baadaye liwe Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili na Lugha nyingine za Tanzania na Afrika; ili lugha, tamaduni na fasihi nyingine nazo zifanyiwe kazi za stahiki zao.
Kinachosemwa katika sehemu hii ya makala ni kuwa Fasihi ya Kiswahili ni Fasihi ya Waswahili na Uswahili wao. Kadhalika, kwa sasa, Fasihi ya Kiswahili ina maana ya Fasihi yoyote itumiayo Kiswahili, kwa mfano kazi za waandishi kama Aniceti Kitereza.5
Misingi
Misingi ni vigezo vikuu na muhimu vya kufanyia kazi. Kwa haja ya makala haya, baadhi ya misingi hiyo ni pamoja na nadharia (za fasihi, jadi, utamaduni, n.k.), ukomavu (wa kitaaluma na kiumri), ukweli na haki, uwezo wa kisanii, mwelekeo, na lengo.
Nadharia
Mhakiki wa kazi za sanaa lazima aelimishwe na ahitimu katika taaluma za nadharia. Kuna siri nyingi muhimu katika nadharia za kila fani. Hivyo mhakiki anawajibika kuzimaizi kwa undani sana nadharia za fasihi anayoishughulikia. Ama ajue kuna sanaa za jadi, taalumaratibu ya sanaa nyingine, k.v., hadithisimulizi, thieta ya jadi (sanaa za maonyesho), methali, nyimbo, vitendawili n.k.; na kwamba kila kimoja cha hivi kina nadharia zake. Ajue kuna nadharia za ushairi kwa jumla na nadharia za ushairi wa Kigogo, ushairi wa Kimasai, ushairi wa Kiingereza, kadhalika ushairi wa Kiswahili. Ajue kuna riwaya, tamthiliya, hadithi fupi, na sanaa za muziki; na kwamba kila kimoja cha hivi kina nadharia zake.
Nadharia ni taalumadhahania ambayo inahitaji uwezo mkubwa wa mtu. Nadharia zina sehemu kubwa sana katika utenzi wa kitu au jambo lolote la maana. Mwalimu Kenneth S. Goldstein amepata kuwaambia wanafunzi wake kuwa: “Bila kupata mafunzo katika nadharia, kuna dalili za wazi kabisa kuwa mkusanyaji (mchunguzi) hatakuwa anajua ni matatizo yepi yanahitaji utatuzi.”6 Katika uhakiki wa fasihi bila kuhitimu katika nadharia, matokeo ni kuwa na watu wanaojitia katika sanaa hiyo ili “kulima” au ‘kugonga” wenzao ili nao wapate majina. Mfano mzuri wa “ugongaji” ni ule wa mtu anayemtaka kila mtu mwingine kuwa kama yeye au kuwa yeye kwa fikira na mwelekeo. F.E.M.K. Senkoro7 hafahamiki anadai nini katika misingi iliyowafanya kina Fr. F. Nkwera kusema “sanaa hutoka kwa Mungu”; au ufafanuzi wa kina John Ramadhani na wenziwe walipodai kipengele kimojawapo cha fasihi kuwa ni hisi, hadi kuthubutu kutumia lugha ambayo kabisa haitumiki katika taaluma kwa kuuita kila mtizamo wa watu hawa “mtizamo uliopotoka,” madai ambayo yanakingana na misingi ya kitaaluma. Kwani angeulizwa: “Wewe ni nani hasa katika fasihi hata uone sisi tumepotoka na wewe hujapotoka?” angepata taabu kutoa jawabu. Kama alivyopata kusema Mohamed Bakari kuwa kulithamini shairi, mara nyingine, inampasa mtu kuwa mwizi wa ulimwengu wa faragha wa mshairi,8 ndivyo iwezavyo kusemwa kuhusu mhakiki na ulimwengu wake wa faragha kimalezi, kiitikadi, kimwelekeo na kitaaluma. Mhakiki ni mtu, na watu ni watu na yao. Haimkiniki wahakiki wote wawe mtu mmoja kwa mawazo, itikadi, mwelekeo, n.k.
Hivyo nadharia ndicho kigezo kikuu cha kumwezesha mhakiki kufanya kazi yake ya kujenga jengo la taaluma juu ya matofali ya watangulizl wake. Anayo haki ya kujenga tofali bora zaidi lakini yu mweledi wa adabu za kutothubutu kubomoa msingi. Umbuji wa lugha yake na uwezo wake wa usanii humpa fursa ya kuziba ufa bila ya kujenga ukuta kwa hekima na maarifa.
Ukomavu
Katika falsafa ya elimu, kuna hoja zihusuzo “mzingiro wa maisha” na “dari ya akili”. Mambo haya mawili huenda na umri, elimu na safari za kuiga mazuri. Umri ukizidi, elimu ikipanuka na safari dhahiriya na dhahniya zikiwa nyingi, mtu hupanua mzingiro wake wa uzoefu katika maisha na kupandisha juu zaidi kimo na kina cha dari yake ya akili. Maisha yanapoanza katika umri wa miaka arubaini, kama mtu keshapitishwa katika mfumo bora wa elimu, kapata kisomo na elimu, hususani huwa mpevu na mkomavu wa mengi. Ukomavu wa kitaaluma utamfanya amheshimu kila mtu na kila kifanywacho na wengine. Huwa yu mweledi na mfahamivu wa mbinu na lugha ya kutumia kurekebisha pale ambapo panastahiki. Huwa yu mtu wa kutoa maoni yake na mara nyingi kukiri kuwa hutafautiana na maoni ya fulani ama fulani kwa sababu za kimsingi kadhaa.
Kwa kuwa yu mtu mzima kiumri, magomvi ya kitoto ya kushikana mashati au kumwagiana mchanga si fakhari tena ya mhakiki. Bali huwa mtu mstahiki wa busara itakiwayo na mwandishi au mtunzi wa kazi ya fasihi, msomaji au msikilizaji wa kazi hiyo, kadhalika na athari ya kazi kwa jamii yake, kwake mwenyewe na kwa wahakiki wenziwe.
Ni dhahiri kuwa mhakiki anahitajika awe mpevu katika nadharia na taaluma kwa jumla, katika misingi ya kitaalamu; na kama ana mwelekeo wa kiutamaduni, kisiasa, kiuchumi, kisanii, n.k., awe pia amekomaa katika hayo. Na msingi wa ukomavu ndio mmojawapo’uliolipa taabu sana bara la Afrika kwa kuwa viongozi wake wengi kwa robo karne ya mwanzo wa uhuru hawakuwa nao. Ukomavu wa kisiasa wataka ukomavu wa kiuchumi, kielimu na kiitikadi ili Mwafrika naye ajihisi kapevuka katika kuchangia ukweli na haki.
Nadharia na ukomavu humfanya mtu aandikapo kuhusu fasihi ya Kigogo aanze na Ugogo wenyewe, Wagogo wenyewe, na misingi inayoutawala utamaduni huo. Huu ni mwelekeo wa ndaninnje. Si kweli na si haki kwa mhakiki wa fasihi ya Kiswahili kutumia nadharia au misingi ya fasihi ya Kiarabu, Kijerumani, Kichina au Kihindi kwa kisingizio cha kuwa fasihi ni fasihi. Mja ni yuleyule popote alipo, lakini fasihi yake ni kizaliwa cha utamaduni wa mazingira yake. Si vibaya kuanza na ndani mwa Mswahili kabla ya kumpambanisha na ndugu yake wa “ubantuni” au “ubinadamuni”. Kwa mfano, undani wa mpwani ni pamoja na athari za bahari na itikadi zote zitawalazo maisha yake; dini yake. Mpwani haoni haya kukiri ana Mwenyezi Mungu mwenye uwezo na nguvu, na kwamba mbele yake, yeye Mswahili si lolote si chochote; kwamba maisha mazima ya mja ni upuuzi, hayana maana ila kwa mtu afanyaye ibada na kazi za kuzalisha na kubadilisha hali ya kiuchumi, kisiasa, kijamaa na kuleta amani miongoni mwa watu. Kucha Mwenyezi Mungu ni adili la maisha, halina kusoma ama kutokusoma. Tambiko, jando, unyago, n.k., ni sehemu ya jadi ambayo hubadilika kidogokidogo kwa athari za wakati, maendeleo, n.k. Na kila kimoja katika hivi kina kanuni za mashiko ambazo mhakiki wa mwelekeo wa ndaninnje sharti aziheshimu.
Makala haya yanadai kuwa kweli isemwe na haki ifanywe kuhusu kazi za fasihi. Mwandishi anayeimba nyimbo za kimapinduzi sharti atazamwe yeye mwenyewe alivyo na anavyoishi. Je, yeye mwenyewe ni mwanamapinduzi anayeyajua mapinduzi? Si mnafiki anayetaka labda kuuza maandishi yake katika soko maalumu? Au katili linalotaka kuua watu kwa jaribio lake la siasa? Jamii ya mwandishi itazamwe jinsi inavyompokea na kumthamini mtu huyo. Nayo ipimwe kama kweli inao uwezo wa kumjua mtu aliye ndiye na mtu asiye ndiye. Je, mwandishi huwachezea shere watu wake kiasi gani? Kama yu avaa kindenga, chatosha kumtia katika uwanamapinduzi? Kama yu avaa baraghashiya, yatosha hiyo kumtia katika kundi la waumini? Elimu yake je? Uwezo wake je? Familia yake je?
Hatua hii huenda ikaonekana imechupa mipaka ya kitaaluma na kuingilia mambo ya Idbinafsi. Mwono huo ni wa kitaaluma ambao umetoka nnje ya tamaduni za Kiafrika. Ni mwono wa nnjendani. Uafrikani na Uswahilioi, mtu huthaminiwa kwa vile alivyo mzimamzima. Na mhakiki anapoitathmini kazi ya fasihi sharti aitazame kweli na haki katika ukamilifu wake.
Uwezo
Uwezo wa kisanii katika uhakiki ni jambo la msingi sana. Mhakiki wa riwaya, kwa mfano, si lazima sana awe mwanariwaya yeye mwenyewe, lakini yafaa awe msomaji wa riwaya nyingi sana. Awe ni mpenzi, mtafiti na mtu wa kuzitafakari riwaya. Awe mjuzi wa vigezo na misingi ya riwaya. Ajue riwaya ni nini, miundo na mitindo mbalimbali, wahusika na matukio mbalimbali, tamathali za usemi ambazo ndizo ziko katika uhalisia wa jamii inayohusika. Kadhalika mhakiki wa tamthiliya au wa mashairi, tenzi, ngonjera, nyimbo, n.k. Kanuni za kila fani ya fasihi sharti zipewe nafasi na haki yake. Uwezo hupatikana kwa ari, mafunzo, ukomavu, uzoefu, na kukubali kuoneshwa njia. Nao hukua kadiri ya mhakiki akuavyo. Kwa mfano, kina Kiango9 wa juzi si sawa tena na wa leo. Na kila mhakiki wa kweli hupigania kukuza uwezo wake siku hadi siku.
Mwelekeo
Baadhi ya wapitiaji au wachambuzi hupenda kuwa na “misimamo” katika kazi zao. Kwa daraja ya mhakiki, kuwa na ndoto hiyo ni hasara. Msimamo huwapo katika mijadala ya kishule au labda ya kisiasa. Na mtu sharti asi-mame alipo ili apiganie upande wake. Mhakiki yeye ni mtoa hoja na sababu. Hoja zake na sababu zake zionyeshwapo zinatafautiana na za wengine, mhakiki mkomavu hujifunza haraka iwapo atatosheka na sababu ya kubadili au kuongezea hoja maoni yake. Kigeugeu cha mhakiki si ila: ni sifa mradi tu aseme wazi kuhusu mabadiliko hayo. Ni dalili ya kukua na kuendelea.
Mwelekeo huathiriwa sana na mazingira, malezi, nadharia, na ukomavu wa mtu. Katika Fasihi ya Kiswahili, mhakiki hana nafasi ya kuelekea kwenye dharau au matusi dhidi ya dini kwani utamaduni wa fasihi hiyo umejikita katika imani nzito ya kuwako kwa Mwenyezi Mungu mmoja, mitume, malaika, n.k. Uyakinifu katika fasihi hiyo ni ule wa asilimia kwa mia wa ki-Mungu-mungu; kweli ambayo haishindani wala kulinganishwa na udhanifu wa kisayansi ambao bado binadamu anaufanyia kazi. Mifano ni kanuni za maumbile na kanuni za matokeo ni yakini isiyotoa. Udhanifu wa “atom” iliyosemwa ni chembe ndogo isiyoweza kubabadilika, leo si “atom” tena, ni “neutron”.
Kinyumenyume cha matumizi haya ya uyakinifu na udhanifu kimekusudiwa kuonyesha kwamba kuna haja ya kuzama zaidi katika mambo kabla wahakiki hawajayapamia.
Na viwe viwavyo, mja katika ukamilifu wake haishi kwa mkate tu. Hivyo mielekeo ya uhakiki isiwakanganye wahakiki hadi wakafika kuparaganyika. Mradi washenzi na waungwana wamo maishani pamoja, watake wasitake, sharti wahakiki washirikiane kwani huo ndiwo mtihani waliopewa. Na wahakiki wa Ki-Marx au Ki-Mao sharti wathamini kazi za wahakiki wenzao ambao fikira zao zimekita kwa “Baba Mtakatifu” au kwa “Muhammad (S.A.W.)” au “Mizimuni”, n.k. Vinginevyo wataulizwa: “Nyinyi ni kina nani kudai haki ya kuwa wahakiki bora kutushinda sisi ati kwa kuwa tunatafautiana mielekeo? Marx na Mao wana ubora gani wa kumshinda Yesu na Muhammad?”
Lengo
Lengo la mhakiki ni kujaribu kutumia uwezo wake kusaidia kuifahamisha kazi anayoihakiki kwa mtu aliyeiandika na kwa msomaji. Katika jaribio hili, mhakiki akiwa mwalimu, atakosoa penye kustahili na kuelekeza penye kustahiki. Sifa za wazi atazisema ili wengine wapate kuziiga pindi waonapo zawafaa. Ila nazo zitaonyeshwa ili mwenye nazo aziache na asiye nazo aziepuke. Mradi lengo la mhakiki litabakia kuyatengeneza mambo yawe na yazidi kuwa mazuri. Huu ni wajibu wao kama anavyodai Abdilatif Abdalla kuwa: “Na itakuwa ni wajibu wao kuyasahihishamakosa yaliyokwisha fanywa.na hao waliotangulia.”10 Na watayafanya hayo kitaaluma na kihaki-liliahi, yaani kikwelikweli na kwa uaminifu mkubwa sana.
Nafasi na Kazi ya Mhakiki wa Fasihi ya Kiswahili
Nafasi
Ni jambo la mantiki kwamba mhakiki ni kiungo cha lazima katika fasihi yoyote iwayo. Haingekuwa kinyume cha hivyo kuwa katika fasihi ya Kiswahili mhakiki hana nafasi, haiyumkiniki. Nafasi yake inahitajika zaidi kwa vile taaluma hii haina umri mkubwa baada ya kuwa imeanza katika miaka ya 1970. Mzee John Ramadhani na Farouk Topan ni miongoni mwa waasisi wa uhakiki katika Fasihi ya Kiswahili. Athari ya kazi zao ndiyo iliyowazaa akina Kiango na Sengo wa siku za uchanga wao, na vijukuu akina Mulokozi na Senkoro; na Mbunda Msokile ambaye kawa mchambuzi mkuu wa vitabu redioni na kwenye magazeti, hasa Kiongozi. Ni wazi kuwa mhakiki bado anahitajika sana na ataendelea kuhitajika sana. Kwani yeye ndiye mwalimu na kiungo cha kazi ya fasihi na jamii iliyokusudiwa kinyume na wazo kwamba “sanaa yaweza kujisemea yenyewe”.11Yaweza kweli, lakini sanaa hiyo sharti iwe pamoja na usanii wa mhakiki.
Kazi
Mwanafunzi wangu A.G.N.M. Gibbe, katika makala yake ya “Dhima ya Mhakiki”12 amesema ya kutosha. Kiasi kikubwa kaathirika na nyimbo, mavazi, hamasa na hata fakhari za uwanamapinduzi ambao ulishika sana Afrika Mashariki na Kati katika miaka 1965/80. Katika Tanzania, uwanamapinduzi uliofasiriwa na vijana wasomi ulihusu sana jitihada za kina Mao za kukana uunguungu na kuhimiza uunguwatu. Wachina baada ya Mao wamerudisha imani zao kwa Mwenyezi Mungu na wanamapinduzi wa Tanzania waliendelea kwenda kuabudu siku za Jumapili, na walio wakaidi sana hawakuacha kumtaja Mungu waliposhikwa na gego au malaria. Wengine wengi walibakia na Mwenyezi Mungu wao mmoja na mkweli daima. Hii haina maana kuwa hapajakuweko wanamapinduzi wa kweli ambao tamaa zao, sala zao na juhudi zao ni kuyatendea haki, kweli na kazi maisha ya jamii zao ili mabadiliko ya hali katika elimu, uchumi, siasa (ukweli, upole, uammifu n.k,), na vipengele vyote vya maisha ya kila siku yawe yakidhihirika kwa kila mwananchi, na pasiwe mmoja akawa anadai hadiya za kuwa mbele ya wenziwe. Hivyo basi baadhi ya kazi za mhakiki ni pamoja na:
Quote:
(i) Kuchambua na kuweka wazi funzo ambalo linatolewa na kazi ya asihi.
(ii) Kuchambua na kufafanua picha za kisanii zilizotumika katika kazi ya fasihi.
(iii) Kumshauri mwandishi ili afanye kazi bora zaidi.
(iv) Kumuelekeza msomaji ili apate faida zaidi kuliko yale ambayo angeweza kuyapata bila ya dira ya mhakiki.
(v) Kuhimiza na kushirikisha fikira za kihakiki katika kazi za fasihi.
(vi) Kuweka, kubakiza, na kukuza kiwango cha utunzi na usomaji wa kazi za fasihi.
(vii) Kuonyesha kuwa kwa kila kizuri kuna kizuri zaidi na hapana kizuri kisicho dosari.
(viii) Kutafiti na kuweka sawa nadharia za fasihi teule.
(ix) Kusema kweli ipasayo kuhusu tamaduni na falsafa zinazotawala fasihi.
(x) Kuheshimu na kuthamini kazi za waandishi kwa kuzifanyia haki, n.k.
Maoni
Makala haya kwa jumla yamejaribu kupendekeza mambo kadhaa yanayomhusu mhakiki. Mwandishi wa awali wa kazi za fasihi hakupewa nafasi sana. Kiwango cha mapitio na uchambuzi wa kazi za fasihi, ambacho kimekuwako tangu fani hii ilipoanza katika fasihi ya Kiswahili, kimesemwa hakitoshelezi sifa za kiwango cha uhakiki. Ni maoni ya mwandishi wa makala haya kuwa mhakiki wa fani ya fasihi sharti awe amesoma siyo nadharia na kazi kadhaa za fasihi tu bali pia sharti awe amehitimu katika taaluma za falsafa ya fasihi, falsafa ya sanaa kwa jumla, na katika nadharia za uhakiki na uzoefu wa utendezi wa kazi hiyo.
Kazi, karibu zote zilizochapishwa, zinahusu uchambuzi wa kazi za fasihi ambazo zinasomwa maskulini. Hivyo lengo kuu ni kujaribu kuzieleza na kuzifahamisha kazi hizo kwa wanafunzi na kwa walimu wao. Mwalimu John Ramadhani, Mwalimu Farouk M. Topan, baadaye akina Saifu Kiango, na kufuatiwa na kina Mwalimu Mwarabu Mponda, Mwalimu M. Mulokozi na F. Senkoro – wote hawa wamezielekeza kazi zao kwa wanafunzi na walimu wao, iwe ni shuleni, vyuoni au vyuo vikuu. Kwa mawazo yaliyokusudiwa karatasini humu, wote hao wamekuwa wakifanya kazi za uchambuzi, ufafanuzi, usaili, upitizi, na sanaa za ualimu.
Uhakiki wataka kiwango cha juu zaidi cha uandishi wa kazi za fasihi, k.v., Siku ya Watenzi Wote, Kusadikika, Mashetani, Jogoo Kijijini, na mifano ya hizo; ukomavu wa hali ya juu katika taaluma, nadharia, falsafa, maisha na uwezo wa kupima na kuamua haki. Lengo liwe ni kuzihakiki kazi hizo kwa ajili ya wahakiki wapevu ili nao wazihakiki kwa upevu huo.
Hitimisho
Makala yamejaribu kujadili dhana na misingi ya uhakiki wa fasihi ya Kiswahili. Fasihi hii ni ya upwa wa pwani ya Afrika Mashariki, na ina umri mkubwa na athari nyingi za maingiliano ya jamii. Hivyo mhakiki wa kazi zote za fasihi hii sharti aujue na kwa kiasi kizuri authamini utamaduni wake ambao ni pamoja na dini za jamii, itikadi na imani zao, falsafa na mielekeo yao, kanuni na ada zao, ushenzi na uungwana wao, n.k.
Makala yamehimiza utafiti katika fasihi ya Kiswahili na fasihi za Kimakonde, Kirangi, Kiziguwa, Kikae, Kitumbatu, n.k., ili uhakiki uwe unapiga ndipo.
Fasihi ya Kiswahili, kwa maana ya fasihi ya Kigogo kwa lugha ya Kiswahili, au fasihi ya Kimbulu kwa lugha ya Kiswahili, ina nafasi kubwa katika malezi na elimu ya taifa hili. Muhimu, mhakiki lazima aseme ni fasihi ya watu fulani anayoishughulikia.
Mwisho wa yote, makala yamesema kuwa uhakiki ni usanii mpevu sana unaohitaji kula chumvi nyingi katika mengi. Nao umejikita katika kweli na haki, na usafi wa nia. Na kwa mapendekezo yaliyotolewa, kuna matumaini kuwa taaluma hii itakuzwa na kukomazwa.
Tanbihi
1. TUKI (1981) Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Oxford University Press, Dar es Salaam, uk. 196.
2. Terry Eagleton (1984) The Function of Criticism. London, uk. 14 (tafsiri yangu).
3. Mtume Muhammad (S.A.W.) Katika Kauli zake thabiti za Hadithi za kuaminika.
4. A.G.N.M. Gibbe (1978) “Dhima ya Mhakiki” katika Mulika 12. TUKI, Dar es Salaam, uk. 5.
5. M.M. Mulokozi na D.P.B. Massamba (wh.) (1984) Kiswahili 51/1 & 51/2. TUKI, Dar es Salaam, uk. xi.
6. Kenneth S. Goldstein (1964) A Guide for Field Workers in Folklore. Folklore Associates. Pennesvlvania Inc., uk. 17.
7. F.E.M.K. Senkoro (1982) Fasihi. Press and Publicity Centre, Dar es Salaam, uk. i.
8. Mohamed Bakari (1981) “Swahili Islamic Literature and Westem Literary Critics”. Unpublished paper presented at the Conference of the Nile Valley Countries. IAAS – University of Khartoum, uk. 15.
9. S.D. Kiango na T.S.Y. Sengo (1973) Hisi Zetu, TUKI Dar es Salaam; Ndimi Zetu (1974) Longman, Tanzania Ltd., Dar es Salaam.
10. Abdilatif Abdalla (1975) “Utangulizi” katika T.S.Y. Sengo. Shaaban Robert. Longman Tanzania Ltd., Dar es Salaam, uk. xxv.
11. Eagleton,k.h.j., uk. 42.
12. Gibbe,k.h.j., kur. 2-8.

Print this item

  UHAKIKI: MWANAMKE NI IBILISI?
Posted by: MwlMaeda - 12-28-2021, 04:05 PM - Forum: Uhakiki wa kazi za fasihi - No Replies

Mwanamke ni Ibilisi?
R.D.K. Mekacha
Katika kuchanganua jinsi mwanamke alivyosawiriwa Mbughuni (1982) anaainisha picha mbili za mwanamke zinazojitokeza katika riwaya. Kwanza lu picha ya mwanamke kama kiumbe mharibifu, na pili ni picha ya mwanamke kama kiumbe mwongofu. Katika picha ya uharibifu usawiri wa mwanamke unashabihishwa na wasifu wa Hawaa (au Eva) katika masimulizi ya kibiblia ya dhambi ya asili, na katika picha ya uongofu usawiri wake unashabihishwa na wasifu wa Maryam (au Maria) mama wa Nabii Issa (Yesu Kristu). Katika picha ya mwanzo mwanamke anaiponza jamii kwa kuipoteza pepo (paradiso), na katika picha ya pili mwanamke ni kiumbe wa kufugwa katika ndoa. Matteru (1982) anaainisha picha tatu za mwanamke zinazobainika katika fasihi simulizi: mwanamke kama mzazi, mwanamke kama chombo cha anasa ya mwanamume, na mwanamke kama chombo au mali ya kumilikiwa. Kama mzazi dhima ya mwanamke ni kuzaa watoto, kama chombo cha anasa dhima yake ni kumburudisha mwanamume, na kama mali uamilifu wake ni kumilikiwa na kuwa zana ya kuzalishia mali. Wahakiki wote hawa wanaafikiana kuwa katika picha zote hizo mwanamke anajitokeza akiwa mtu duni akilinganishwa na mwanamume.
Azma ya makala haya mafupi ni kushadidia hoja hiyo kwa kuchanganua mwanamke alivyosawiriwa katika nyimbo za kisasa za muziki wa dansi. Nyimbo za aina hii hutawala sana matangazo ya redio – vyombo vya mawasiliano ambavyo kwa makisio yetu vina nguvu sana katika jamii hii. Mahususi tutajibana katika kuchanganua namna wasanii wa nyimbo hizo wanavyouonyesha udhalili wa mwanamke kwa kumsawiri kama kiumbe mwenye uovu unaozidi ule wa Hawaa hata ukamithilishwa na ule wa ibilisi. Tunatazamia kuonyesha kuwa sambamba na usawiri huo mwanamume anajitokeza akiwa mbabe na mwadilifu. Tumeteua na kutumia nyimbo chache kwa sababu tu ya maudhui yake.
Kama ilivyo katika kazi nyingine za sanaa mwanamke amesawiriwa kwa namna mbalimbali katika nyimbo za kisasa za muziki wa dansi. Mwanamke ni mchapakazi,1 ni mwenye busara na mshauri wa mumewe,2 ni mnyonge na mwenye kumtegemea mume kupata mradi wake wa maisha,3 ni chombo cha anasa cha kumburudisha mwanamume,4ni fasiki na mwovu sawa na ibilisi.
Hakuna mipaka ya wazi na bayana kati ya picha hizo za wasifu wa mwanamke, bali huingiliana kwa namna ya mwendeleo unaoanzia kwenye zile nyimbo zenye mwelekeo chanya hadi zile zenye mwelekeo hasi. Kwa makadirio yetu idadi kubwa ya nyimbo hizi inaegemea kwenye mwelekeo hasi, na hata zile zinazomsawiri mwanamke kwa mwelekeo chanya hatimaye huzishawishi hadhira kuhitimisha kuwa mwanamke ni kiumbe dhalili mbele ya mwanamume hasa kimaadili.
Motifu ya usawiri wa mwanamke kama ibilisi ni utendekaji wa kosa au jambo lolote linalosababisha madhara kwa mtu mmoja au jamii kwa jumla. Ili kuikamilisha motifu ya aina hii watunzi wa nyimbo hizo huumba chanzo kinachosababisha tendo ambalo hatimaye hubainika kuwa kosa, huumba pia mbinu zitumiwazo kukamilisha tendo hilo, malengo ambayo ndiyo huwa tendo limedhamiriwa kuyakidhi na matokeo, taathira au madhara ya tendo hilo.
Mojawapo ya chanzo cha utendekaji wa kosa hilo ni udanganyifu. Katika masimulizi ya kibiblia ya dhambi ya asili ambayo kwa kiasi hushabihiana na picha hii, mwanamke (Hawaa) alishawishiwa na Ibilisi kuchuma na kula tunda lililokuwa limekatazwa.5 Katika idadi kubwa ya nyimbo za kisasa za muziki wa dansi pia mwanamke hushawishiwa. Lakini hapa vishawishi aghalabu huwa tamaa ya maisha ya starehe. Katika kukidhi haja hiyo mwanamke anashawishika ama kuacha masomo, au kumwacha mchumba wake, au kuwatelekeza wazazi wake huko vijijini na kukimbilia mjini.6
Udanganyifu kama chanzo cha kosa hutuelekeza katika kuhitimisha kuwa mwanamke anastahili sehemu tu ya lawama kwa kosa lililotendeka. Sehemu nyingine ya lawama inabebwa na vile vishawishi ikiwa ni shetani (kama ilivyokuwa kwa Hawaa), mali, starehe, au ulaghai wa mwanamume. Lakini pamoja na kugawana lawama hizo, hatimaye nyimbo hizo hutuongoza katika kumwona mwanamke kama kiumbe dhaifu, asiyeweza kuhimili vishawishi, na ambaye kwake yote yang’aayo ni dhahabu. Kwa hiyo madhara yatokeayo hatimaye huwa ni kwa sababu ya udhaifu wake (mwanamke).
Chanzo kingine cha tukio liletalo madhara ni dhiki. Dhiki aliyonayo mwanamke humsukuma kutafuta njia za kukidhi mahitaji yake, na katika kufanya hivyo husababisha madhara au kosa kutendeka.7 Katika chanzo cha namna hii pia inawezekana kuhoji kuwa mwanamke ni mhasirika tu va mahitaji na hivyo lawama anayostahili kubeba ni ndogo. Aidha hapa ile hali ya udhaifu haijitokezi, bali tunamwona mwanamke kama jasiri na mwenye kuthubutu kuchukua hatua za kujiondoa kwenye madhila ya unyonge na umaskini. Lakini si aghalabu hali hiyo kusisitizwa katika nyimbo hizo. Badala yake linalosisitizwa na watunzi ni mbinu aitumiayo (mwanamke) kukidhi haja hiyo na madhara ayasababishayo kwa mwanamume, na hasa kwake mwenyewe.
Katika idadi kubwa ya nyimbo hizo, hata hivyo, chanzo cha matendo au matukio yaletayo madhara si vishawishi vya Ibilisi au tamaa, wala si msukumo wa kukidhi mahitaji ili kukabili dhiki inayomzinga, bali wivu unaochochea nia ya kuharibu “maisha bora” ya ndoa za wenzake. Hapa ubaya wa mwanamke hukiuka ule wa Hawaa katika masimulizi ya dhambi ya asili na kushabihiana na ule wa Ibilisi. Mtunzi wa wimbo uitwao “Mwanameka” anahitimisha kisa cha mwanamke huyo kwa kusema:
Quote:
Hivi sasa nimeshaamini,
Ibilisi wa mtu ni mtu.
Yaani Ibilisi wa Musa (mwanamume) ni Mwanameka (mwanamke). Siyo kwamba kisa hicho kimemfanya atambue hivyo, bali kimethibitisha jambo ambalo alikwishahisi au kudokezwa. Ndiyo maana asema kuwa “sasa nimeshaamini.”
Mbinu zitumiwazo na mwanamke kukidhi malengo yake, ikiwa ni starehe, mali, au uharibifu wa ndoa, ni mbili. Kwanza ni ahadi ya ndoa; ahadi ambayo aghalabu huwa haitimizwi. Msichana aitwaye Mwanaidi katika wimbo wenye jina hilohilo aliahidi kuolewa na mtunzi. Naye mtunzi akatumia mali yake yote ikiwa ni pamoja na kuuza shamba na nyumba ili kumridhisha “mchumba” wake huyo. Lakini hatimaye mtunzi akafilisika na Mwanaidi akamgeuka na kumkataa.
Mbinu ya pili ni mapenzi na uzinzi. Mwanameka katika wimbo tulioutaja ni msichana aliyetumia uzuri wake, vipodozi, na mbwembwe ambazo zilimzuzua Musa hata zikamghilibu akili licha ya kujitahidi kuvumilia. Alipopotea njia na kumtaka mapenzi Mwanameka, basi naye akayatumia hayo mapenzi kumfanya Musa asahau kwake, jambo ambalo lilisababisha ndoa yake kuvunjika. Mtunzi analieleza hilo ifuatavyo:
Quote:
Ukajikuta mrembo
Ukazidisha na mapambo
Kipini wanja kwa poda
Na mwendo wako maringo
Musa macho yake yameona
Na moyo ukaanza sononeka
Ukabadili na njia
Lazima upite kwa Musa
Ukenda sokoni kwa Musa
Musa amevumilia
Mwisho kapotea njia
Kakusimamisha bila kutambua
Akazungumza neno la mapenzi
Ukakubali bila kusita
Uliyotaka yamekuwa
Kazi ikawa ni moja
Ni mapenzi moto moto
Lakini mara tu baada ya ndoa ya Musa kuvunjika Mwanameka pia akavunja mapenzi yake na Musa.
Mbinu hizi mbili, kwa kweli, ni sura mbili za sarafu moja. Zote zinaelekea katika kuhitimisha kuwa mbinu aitumiayo mwanamke kuleta madhara ni ile jinsi yake ya kike. Hii ni jinsi ambayo pia inahusika na dhima muhimu ya kuiendeleza jamii. Kwani mwanamke ni mzazi na mlezi wa kizazi cha kesho, dhima ambayo wasanii hawa huonyesha kuiheshimu sana.8 Lakini hapa inashushwa hadhi na kuonekana kama silaha kuu au ya pekee ya mwanamke kufanyia hila zake za kiovu. Pengine mtazamo huu unaakisi ukweli: (i) kuwa bado jamii yetu inaiona dhima ya msingi ya mwanamke kuwa ni kuzaa watoto (Matteru 1982);9 (ii) kuwa bado jamii yetu inauona wajibu wa kuzaa na kulea kama ni wajibu binafsi hasa kwa mwanamke na wala sio wajibu wa jamii nzima;10 na (iii) kuwa mwanamke katika jamii yetu harithi wala kumiliki chochote isipokuwa uwezo wake wa kuzaa – na kama akizaa – watoto wake.
Mbinu hizi hutumika kukidhi malengo tuliyoyadokeza hapo juu. – Mojawapo ni kupata “maisha bora” hasa katika ndoa. Kwa kweli nyimbo nyingi humwona mwanamke kama “mateka wa saikolojia ya unyonge wake” (Mohammed 1980). Wasanii hudhani kuwa mwanamke mwenyewe huitazama ndoa kama mwokozi. Kwamba anapokuwa ameolewa ndiyo anakuwa amekombolewa kutoka kwenye majanga na madhila ya kilimwengu, na anapokuwa ameachika hujuta kwa kuwa anakuwa ameadhibiwa kwa kutumbukizwa tena katika majanga ya “dunia hadaa ulimwengu shujaa.” Hapa itakumbukwa kuwa wahusika wanawake takriban wote wa nyimbo hizi ni wale walioathiri au kuathiriwa na kuvunjika kwa ndoa, au wale ambao hawajaolewa. Si aghalabu kukutana na mhusika ambaye ndoa yake ni imara au ni wa kijijini.
Hii ni kusema kuwa kuolewa, hasa na mume mwenye mali, ndiyo tamaa ya mwanamke, kwani huko ataishi raha mustarehe. Hata hivyo, kadiri nyimbo nyingi zinavyoonyesha mwanamke anapofanikiwa kuolewa na mume mwenye mali hatimaye hugundua kuwa maisha ya ndoa hiyo siyo raha mustarehe. Ama mume humsahau akamgeuza kuwa pambo au mlinzi wa nyumba akamwacha aghalabu akiteseka na huku yeye (mume) akiendelea kutumbua raha,11 au ndoa huvunjika, au mali kutoweka na mume akafilisika.
Lengo jingine ambalo mbinu hizo hutumika kulikidhi ni tamaa ya mali au utajiri. Mwanamke humlaghai mwanamume, hasa mwenye utajiri, kwa mapenzi “motomoto” au ahadi za kuolewa naye ili aweze kuchuma mali toka kwake. Aghalabu mwanamke huwa hampendi mwanamume huyo, lakini mwanamume anakuwa anampenda mwanamke. Naye mwanamke hutumia hali hiyo kujineemesha, na mara nyingi huwa hata siyo kujitajirisha bali kujisheheneza mavazi na vipodozi tu.12 Anapokuwa amekidhi haja yake, au anapobaini kuwa hawezi tena kuambua chochote kwa mwanamume huyo humpa kisogo akamsahau.
Lengo jingine huwa ni kutibua ndoa au uchumba wa watu wengine. Wasanii hawa wala hawajali kutueleza mwanamke ananufaika vipi kwa kufanya hivyo. Kinyume chake hujaribu kutuaminisha kuwa analolifanya mwanamke amelidhamiria. Tazama maneno haya kutoka wimbo wa “Mwanameka”
Quote:
Uliposikia ee ee
Kwamba Musa ameoa
Kaoa mke wa ndoa
Musa sasa katulia
Uhuni kaacha kando
Ukatumia kila uwezo,
Kuyabadili mawazo ya Musa
Quote:
                                            (Msisitizo umeongezwa)
Tumeelezwa katika beti tulizozidondoa mwanzoni jinsi Musa alivyovumilia. Lakini hatimaye tunaambiwa akapotea njia akamsimamisha Mwanameka “bila kutambua” na kuzungumza neno la mapenzi. Naye Mwanameka kusikia hivyo “akakubali bila kusita” kwani alilolitaka ndiyo hilo nalo likawa.
Matokeo ya matendo hayo ya mwanamke ni madhara. Madhara hayo huathiri mwanamume na mwanamke. Baadhi ya nyimbo huonyesha kuwa mwanamume kahasirika na mwanamke kanufaika. Katika wimbo “Mwanaidi” kwa mfano, mwanamke alinufaika akapata kujineemesha yeye na ukoo wake na mwanamume akahasirika kwani alifilisika na hatimaye hakuwa na la kufanya. Tukichunguza zaidi tunabaini kuwa kilio cha msanii ni kuwa mwanamume ni mwaminifu na mkweli wakati mwanamke ni mwongo na mwenye kujinufaisha kwa hila. Hadhira inashawishiwa imhurumie mwanamume na imbeze mwanamke.
Katika idadi kubwa zaidi ya nyimbo za aina hii wasanii hufanya juhudi ya makusudi kabisa kuonyesha kuwa ingawa mwanamume amehasirika pia, lakini mwanamke ndiye amehasirika zaidi. Mwanamke aitwaye Edita katika wimbo uitwao “Kipenzi Edita”, kwa mfano, anapewa talaka kwa kufanya “mapenzi ya pembeni.”13 Mwanamume anamkosa mke, lakini kinachosisitizwa ni kuwa mwanamke ameadhibiwa kwa kupewa talaka (rejea maelezo hapo juu).
Katika baadhi ya nyimbo wasanii hujitahidi sana kuonyesha kuwa ingawa mwanamume amehasirika, lakini pia amenufaika walau kwa kiasi kidogo. Hivyo ndivyo inavyotubainikia katika wimbo wa “Mwanameka.” Mwanamke alimsababishia mwanamume hasara maradufu: “kakosa mwana” (msingi wa ndoa) na “maji ya moto” (mapenzi). Uteuzi wa maneno katika sehemu ya mwisho ya wimbo huo, hata hivyo, umefanywa makusudi kuonyesha kuwa mwanamume amenufaika au ana liwazo. Nalo ni funzo. Tazama ubeti huu:
Quote:
Bwana Musa hatakusahau mpaka kufa
Tena amekwisha apa
Mambo ya upuuzi hataki tena
Kishaumwa na nyoka
Akiona unyasi anastuka.
Lakini mwanamke hana funzo wala haliwazwi. Badala yake anashutumiwa na kulaaniwa kwa kufanya mkasa, madhambi, na mambo ya kusikitisha. Msanii asema:
Quote:
Kweli Mwanameka
Umefanya madhambi makubwa
Mambo uliyomfanyia Bwana Musa
Yanasikitisha
Mwanameka mkasa uliofanya ni wa mwaka.
Kwa sababu ya mkasa aliofanya, tunaambiwa kuwa watu wanamdharau, wanamkashifu na kumlaani:
Quote:
Mwanameka umetuachia hadithi mtaani
Kila mmoja anashangazwa na vitendo vyako
Kila mtu anasimulia mambo yako
Ati watu wanasema… mgombanishi
Kweli watu wanasema… mhuni
Ati watu wanasema… mdanganyifu
Kwa jumla mwanamke amekuwa mhasirika mkuu wa maovu yake mwenyewe. Kwa hiyo wakati hadhira inashawishiwa imsikitikie mwanamume, inatakiwa pia imlaani na kumshutumu sana mwanamke.
Mambo mawili yanajitokeza katika uchanganuzi huu. Kwanza ni kwamba mwanamke ni mwenye tamaa, mwenye wivu, dhaifu na mwanzilishi wa matatizo katika jamii. Mwanamke hutumia jinsi yake ya kike, tena kwa hila, ili kutenda mambo ambayo huleta madhara. Katika kufanya hivyo mwanamke humshawishi mwanamume na hata hutokea akamshurutisha kwa kumghilibu akili, akamshirikisha katika kutenda maovu. Mwanamke hupania ama kujinufaisha au kutibua maisha bora ya ndoa za wenzie. Madhara yatokanayo na matendo ya mwanamke humdhuru pia mwanamume, lakini mhasirika mkuu wa maovu hayo ni mwanamke mwenyewe.
Pili ni kwamba mwanamume hahusiani na msingi wa matendo hayo maovu. Yeye hushawishiwa tu au wakati mwingine kwa hila akashurutishwa kushiriki katika maovu hayo. Yeye hana hatia. Lakini hudhurika kwa madhara yaletelezwayo na maovu ya mwanamke. Yeye, hata hivyo, aweza kuliwazwa kwa kunufaika walau kidogo, hata kama liwazo lenyewe ni kuhurumiwa tu.
Kwa hiyo hatimaye inabainika kuwa mwanamke ni mwovu, mwanamume ni mwongofu; mwanamke ni fasiki, mwanamume ni mwadilifu; mwanamke ni ibilisi, mwanamume ni malaika!
Ni vigumu kuamini kuwa wasanii wa nyimbo hizi wanaamini kwa dhati kuwa hii ni picha mojawapo ya mwanamke, Nyimbo hizi, kama kazi nyingine za sanaa, hueleza tu jinsi uyakini wa maisha unavyoakisiwa akilini mwa msanii. Lakini pia msanii huwa na uhuru wa kusawiri uakisi huo kisanaa, aweza ama kulitia jambo chuku, au kulidhalilisha ili kukidhi malengo yake ya kisanaa. Licha ya matakwa yake binafsi, msanii pia hudhaminiwa na nguvu mbalimbali za kijamii ambazo zinamzinga. Mojawapo, au zaidi ya moja, ya mambo hayo yaweza kusababisha usawiri wa aina fulani kwa kundi fulani la watu katika jamii.
Usawiri huu wa mwanamke, kwa maoni yetu, unatokana na nia ya wasanii ya kumtaka mwanamke, hasa aishiye mjini na ambaye hajaolewa,14 aendelee kukiri nguvu za mfumo wa mahusiano ya kijamii unaotawala hivi sasa. Asiwe na tamaa ya maisha bora na ya starehe, aepuke au ahimili vishawishi mbalimbali, na aheshimu pingu za maisha katika ndoa yake na zile za wenzake. Au la atasababisha madhara sawa na asababishayo Ibilisi, tena kwake yeye mwenyewe. Wasanii wanajaribu kumwadibu mwanamke kwa kubeza tabia zinazokiuka mahusiano yaliyopo. Hivyo chimbuko la mtazamo huu wa mwanamke ni hofu ya wasanii kuhusu madhara yatakayotokea endapo mwanamke atakiuka mwenendo ambao wasanii hao wanadhani ndiyo murua katika jamii. Ikiwa hofu yao yaweza kutetewa au la ni hoja inayodai mjadala ulio nje ya mipaka finyu ya makala haya.
Tanbihi
1. Kwa mfano katika wimbo uitwao “Kwini Lusi” wa Kimulimuli Jazzband.
2. Katika wimbo uitwao “Mabruki” wa Marquis Orchestra.
3. Kwa mfano katika nyimbo “Ndoa ya Mateso” wa Dar Intemational Orchestra; “Mume Wangu” wa Makassy Orchestra, na nyingine.
4. Hii ndiyo picha inayobainika katika nyimbo nyingi sana ambapo mwanamke kaltwa tausi, tunda, nyota, mwezi, ua, na mengine mengi. Mohammed (1980) ameiita picha ya “sili – sikogi – silali”.
5. Masimulizi haya yamejitokeza vizuri sana Katika Utenzi wa Adamu na Hawa uliotungwa na AbdilatifAbdalla. Rejea pia makala ya Mbughuni
6. Msichana katika wimbo “Mume Wangu”, kwa mfano, anashawishika kupuuza ushauri wa wazazi na kukatisha masomo yake kwa kutamani raha za “nyumba kubwa kama Kilimanjaro, pesa na gari” alizoahidiwa na mwanamume.
7. Mwanamke aitwae Mwanaidi katika wimbo wenye jina hilohilo wa Or- chestra Toma Toma anasukumwa na mahitaji ya kupata mali “ili kuneemesha ukoo wake”, na msukumo huo ndio unaomwingiza katika kutenda kosa.
8. Wahusika takriban wote wa nyimbo hizo huwa ama wasichana wa mjini ambao hawajaolewa au wale ambao ndoa zao zinayumba. Ni nadra sana kusawiriwa mwanamke mzazi isipokuwa pale anapolalamika kuwa kalemewa na mzigo wa kulea watoto. Aidha ni nadra sana kusawiriwa mwanamke anayeheshimu pingu za ndoa yake na za mwenzake.
9. Kwa hiyo mwanamke asiyezaa huonekana kuwa duni zaidi au asiye na thamani. Katika wimbo mmoja wa Juwata Jazz Band, mwanamke anamlalamikia mumewe aliyemfukuza akisema yeye “mwanamke gani asiyezaa”.
10. Katika wimbo uitwao “Ndoa ya Mateso”, kwa mfano, mwanamke analalamika hivi:
Quote:
Niulizieni enyi walimwengu
Huyu mwanamume sijui mume gani
Ananipa mateso huku ugenini
Na mimi nina watoto sijui ni tabu gani
Na mimi nina watoto sijui ni tabu gani.
11. Katika wimbo uitwao “Mume Wangu”, kwa mfano, mwanamke analalamika kuwa hamwoni mume nyumbani, anapika “ubwabwa, chai, chapati” lakini vinachacha. Wenzake wote wametulia na waume zao, naye alitaka mumewe atulie ili wazae, lakini bahati imemtoka. Katika wimbo “Ndoa ya Mateso” inasemekana kuwa mume anakula “makuku ya kukaanga” lakini yeye mwanamke ashindia “mkate mkavu”.
12. Kwa mfano, mtunzi wa wimbo uitwao “Esta” wa Orchestra Marquis du Zaire anadai kuwa msichana Esta “anaponzwa na ujana kwa tamaa ya mavazi” kwani kila wanapokutana hudai fedha za matumizi.
13. Katika wimbo huo ulioimbwa na Mlimani Park Orchestra kitu kinachomfanya mtunzi amtilie mashaka Edita awali ya yote ni kutokumkuta nyumbani arudipo kazini. Kwani mahali pa mwanamke aliyeolewa ni nyumbani. Kuhusu hili rejea Mbunguni (1982).
14. Kwani kama tulivyoeleza juu (tazama maelezo Na. 8) wahusika takriban wote ni wale ambao hawajaolewa na waishio mijini.
Marejeo
Abdalla, A. (1971) Utenzi wa Maisha ya Nabii Adamu na Hawaa. Oxford University Press, Nairobi.
Matteru, M.L.B. (1982) “The Image of the Woman in Tanzania Oral Literature: A Survey” katika Kiswahili, TUKI, Dar es Salaam, Juzuu 49/2.
Mbughuni, P. (1982) “The Image ofWoman in Kiswahili Prose Fiction” katika Kiswahili, TUKI, Dar es Salaam Juzuu 49/1.
Mohamed, S.A. (1980) “Mwanamke katika Ushairi wa Kiswahili” makala yasiyochapishwa, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Print this item

  HISIA KATIKA FASIHI ANDISHI
Posted by: MwlMaeda - 12-28-2021, 03:55 PM - Forum: Fasihi kwa ujumla - No Replies

Hisia Katika Fasihi Andishi
A.J. Saffari
Utangulizi
Makala haya yanazungumzia fasihi andishi ya Kiswahili. Maarubu yake ni kuonyesha kuwa kazi nyingi za fasihi andishi ya Kiswahili zimeshindwa kufikia vipeo vya juu, hususan kisanii, kutokana na utovu wa matumizi ya hisia katika mazingira yanayohusika au kuzungumziwa.
Kwanza, makala yatafafanua maana ya hisia, kuelezea umuhimu na mkabala wake katika riwaya na tungo nyingine, hatimaye kutoa mapendekezo mintaarafu ya suala hili.
Hisia Ni Nini
Kuna aina kuu za hisia zinazotawala na kuongoza maisha ya mwanadamu: kuona, kusikia, kugusa, kuonja na kunusa. Ni vigumu kusema ni hisia gani muhimu kuzidi nyingine ingawa ni dhahiri athari kubwa humuangukia mahuluku asiyeweza kuona. Inasemekana kuwa mishipa ya fahamu inayounga ubongo na macho ni mikubwa zaidi kuliko mishipa ya fahamu inayounga ubongo na viwambo vya masikio. Na katika maisha na nyendo za kila siku kuona hupewa uzito mkubwa minghairi ya kusikia. Pengine basi sio ajabu, kama itakavyobainika punde baadaye, kuwa kazi nyingi za fasihi andishi zimeelemea mno katika hisia hii kana kwamba zile nyingine kuu hazipo kabisa. Hakika hili ni kosa. Maana kusikia, kugusa, kuonja, na kunusa nako ndiko humkamilisha mwanadamu aweze kuyafaidi maisha yake. Na hata mbele ya sheria, ushahidi huweza kutolewa mintaarafu ya kusikia, kugusa, kuonja na kunusa alimradi shahidi awe amesikia, kugusa, kuonja, au kunusa mwenyewe. Ushahidi wa kuambiwa haukubaliwi.1
Kwa hiyo basi kazi ya sanaa ambayo itazituma fikira za msomaji zihisi kuona, kusikia, kuonja, kugusa, na kunusa matendo na mazingira yanayosimuliwa humpeleka msomaji huyo katika mipaka na nyanja za juu za ufahamu na furaha.
Umuhimu wa Hisia
Kila hisia ina umuhimu wake kutokana na mazingira ya tukio linalohusika au kusimuliwa. Maana kazi zote za sanaa hutokana na matendo na maisha ya watu ambao katika matukio, visa na mazingira yao hutumia hisia zao zote tano ama kwa pamoja au kwa nyakati mbalimbali. Ili basi msomaji aweze kupata mandhari kamili, na hata yeye mwenyewe ashiriki katika matukio yenyewe kwa kuchukia, kuonea huruma, n.k., muhimu, kabla ya yote, apate hisia zote hizo tano. Kazi ya sanaa inayojihusisha na hisia moja tu au mbili huwa muflisi kisanii kwa vile inashindwa kuwasilisha mandhari za hali halisi kwa msomaji. Je, mara ngapi nyoyo zetu husononeka au kuripukwa kwa maya kwa sababu ya sauti ndogo tu ya ndege aliaye pekee nyikani, au nyimbo ya zamani? Sauti ya ndege huweza kuleta majonzi ya miaka mingi mno ya utotoni wakati ambapo mtu alifiwa na mzazi, ndugu, jamaa au sahibu wake. Kadhalika nyimbo ya kale huweza kuchimbua ashiki ya zamani baina ya wapenzi, au kutonesha jeraha la masaibu na madhila yaliyopita. Na wala sio nyimbo na sauti ya ndege tu, pengine hata harufu ya maua huwa na nguvu za kumbukumbu kubwa mno.2
Licha ya yote hayo, matumizi ya hisia nyingi yanasaidia kujenga mandhari kamili ya tukio katika akili ya msomaji. Mathalan badala ya kuelezwa tu kuwa paliandaliwa chakula kizuri, msomaji anaelezwa vitu ambavyo vimeandaliwa pamoja na harufu yake. Au badala ya kuambiwa mtu fulani alikuwa na wajihi wa kutisha, huelezwa na kuelewa vyema zaidi kwa kuainishia jinsi pua, macho, rangi, nywele, mdomo na meno ya mtu huyo yalivyo. Na hivyohivyo kwa mifano mingine kadha wa kadha kama vile hasira na ucheshi. Kutokana na maelezo ya kutosha ya hisia msomaji huweza kumuashiki janabi, au akadondokwa na ute kutamani chakula ambacho hakipo mbele yake. Na kadhalika.
Na sio hivyo tu. Hisia zinazotumiwa huweza kumfanya msomaji atafakari zaidi. Ataweza kufikia uamuzi kuhusu picha zinazochorwa kutokana na hisia mbalimbali na wala sio kauli za mkatomkato za mwandishi kama ilivyogusiwa hapo juu. Kauli za mkatomkato sio tu hudumaza sanaa, bali pia hudhalilisha hata akili ya msomaji: kwani umbuji wa mwandishi ni pamoja na kufanya matendo na mazingira anayoyasimulia yawasilishe na kuwakilisha fikira za wahusika wake na hata zake mwenyewe.
Hivyo ni dhahiri kuwa hisia humsaidia msomaji kuzama katika matendo na kuelewa fikra za mwandishi mwenyewe, asili na makazi yake, kuwadadisi na kuwaelewa wahusika wenyewe, n.k.
Kama ambavyo itazingatiwa punde kidogo, ni nadra kuona waandishi wa kazi za sanaa wakitumia hisia japo tatu au zotc kwa pamoja. Vibaya zaidi ni kuwa hata pale hisia moja tuinapotumika haielezwi kwa kimowi. Mathalan katika riwaya’ Ukitoa Siri Utachinjwa3 Bedui, mhusika mkuu, anaelezwa kuwa “alikuwa na umri mkubwa kuliko umri wake.”4Kutokaoa na maelezo hayo ni muhali kuivuta sura ya Bedui na kuimaizi kiasi cha kutosha. Bedui haingii machoni na akilini mwa msomaji bali anapitapita mithili ya kivuli usiku wa manane. Udhaifu huo unajidhihirisha mno kwa kufananisha namna Sembene Ousmane alivyomsawiri Daouda5 katika The Last of the Empire, au Alex la Guma anavyomsawiri Michael Adonis katika A Walk in the Night.6 Mfano mwingine bora ni jinsi Said Mohammed anavyomuelezea Shoka katika Utengano7 sa Fauz katika MtiMkavu.8 Kutokana na undani pamoja na ustadi wa maelezo ya waandishi hao watatu, wahusika wao hudhihirika bayana machoni mwa msomaji kama vile wapo ilihali hawapo. Raha iliyoje hii kwa msomaji kupelekewa mke au mume, mshenzi au muungwana, mnyama au pengine hata maua na harufu yake kwa maneno tu!
Katika mifano yote ya hapo juu hisia iliyotumiwa ni moja tu: kuona. Tena imetumiwa kuelezea vitu vyenye uhai, hususan watu. Lakini hisia ya kuona, hali kadhalika, inaweza kutumiwa vyema au vibaya mintaarafu ya vitu visivyo na uhai kama vile mazingira. Mfano ni namna Alex La Guma anavyoelezea jinsi mawingu yalivyosonga, kuugonga kisha kuuambaa Mlima wa Meza9 au vile anavyoupamba usiku;10 au Willieboy anavyofungwa mikononi mwa askari dhalimu wa Makaburu.11 Katika faala hizohizo Said Mohammed anafuzu mno kuelezea kasi ya upepo12 na chano cha maakuli.13
Hisia Katika Riwaya
Ushahidi unathibitisha riwaya nyingi zinajihusisha na aina moja kuu ya hisia yaani kuona tu, na pengine kusikia.
Kwa kawaida mwandishi huandika anayoyaishi, kuyaona, kuyasikia, kuyaonja, kuyanusa au kuyahisi katika maisha yake ya dunia.14 Hivyo ni dhahiri mwandishi ataathiriwa na mazingira ya alipozaliwa, kukua na hata mastakimu yake. Waandishi waliokulia vijijini aghalabu huwapeleka wahusika wao vijijini, na wale waliokulia mijini huwapeleka mijini.15 Hata William Shakespeare aliathiriwa na mambo kama haya.16
Waandishi wa riwaya za Kiswahili wameshindwa kuelezea mazingira wanayoyajua kwa kutumia hisia zote tano au zaidi. Kitabu Sifi Mara Mbili,17 mathalan, kinazungumzia maisha na mazingira ya kijijini Maneromango kabla ya kuhamia mjini. Lakini hakuna tafauti yoyote ya wazi inayobainisha ushamba na mii katika riwaya hii. Ndivyo ilivyo katika riwaya nyingine nyingi tu kama vile Ukitoa Siri Utachinjwa,18 Mauaji ya Lojingi,19 kwa kutaja chache tu.
Mwandishi anao uhuru wa kuchagua mandhari na wapi kwa kuwapeleka wahusika wake. Iwe mjini au mashambani hakuna udhuru wa kutotumia hisia nyingi au zote tano. Hakika mwandishi wa riwaya ana uwanja mpana zaidi wa kuranda akitumia silaha kali ya kalamu na maneno. Riwaya ina upana na urefu wa kumwezesha mwandishi kujifaragua, hasa katika majitapo ya wahusika, nafasi ya mazingira na urefu wake.20
Kila sehemu ina mazingira yake ambayo kwayo mwandishi anaweza kuranda na kujifaragua. Shamba kuna mashamba, mjini kuna maghorofa; shamba kuna mito, mjini kuna mitaro; shamba kuna harufu ya maua, mijini harufu ya uturi, taka, na kadhalika.
Hisia Katika Tungo
Hapa tungo ina maana ya mashairi na tamthiliya. Kwa bahati mbaya, kama ilivyo katika riwaya, mashairi mengi yanazungumzia hisia ya kusikia zaidi na pengine kuona. Hivyo ndivyo ilivyo hata kwa kazi maarufu kama vile Sauti ya Dhiki21 na Malenga wa Mvita.22 Mathalan hata yale mashairi mwanana “Jana na Leo na Kesho”23 na “Zindukani”25yanaelezea hisia hizo mbili tu: kuona na kusikia. Hakuna haja ya kutoa mifano ya mashairi mengine mengi katika magazeti ya Uhuru au Mzalendo ambayo aghalabu si ya viwango vya chini kisanii tu, bali hata kimaudhui.
Kwa upande mwingine mfano mzuri wa shairi ambalo limesheheni hisia nyingi ni “Kufua Moyo” la Ustadh Hayati Shaaban Robert ambalo lina hisia ya kuona, kugusa, na kunusa.26
Ukiondoa Mashetani27 hali nayo ni hivyohivyo kuhusu tamthiliya. Bali kuna juhudi ambayo inaanza kutoa matunda, ingawa haieleweki kama jitihada hii ni ya kukusudia au ni ajali tu. Isinyago ni tamthiliya ambayo inafungua ukurasa mpya mintaarafu ya suala hili la hisia.28
Hitimisho
Kuna haja kubwa ya waandishi kuzichunguza jamii zao kwa makini, wapenye katika nafsi za wahusika na mazingira yao ambayo ni muhimu mno ili kuwaelewa wahusika wenyewe pamoja na kuleta maana na taswira kamili ya mkasa unaoelezewa.
Maneno ni zana ya pekee inayoweza kumkaribisha au kumtenga mwandishi na wasomaji wake. Kutokana nayo anaweza kuelezea hisia nyingi ambazo zitamfanya awe kipenzi, mcheshi na pengine hata mkomhozi wa wasomaji. Sio lazima hisia zote ziwekwe au kuelezewa pamoja, kwani hivyo ni kushurutisha na ni kinyume cha mambo. Kinachosisitizwa ni kuwa hisia mbalimbali zionekane katika kazi nzima kwa jumla ili kuipa ubora na sura ya juu.
Said Mohammed anasema kwamba uandishi ni kazi ngumu, lakini ni kazi va hiari pia. Ugumu wake ni kama sabaganga, una kazi nyingi ndani ya moja29. La muhimu ni idili na saburi. Chambilecho Abdilatif Abdallah:
Quote:
Mambo yataka busara, kinguvunguvu hayendi,
Yatakatuvu fikira, nyot’u sizo na mapindi,
Fikira za kitwa bora, kitwa bupu hakiundi.30
Tanbihi
1. Fungu la 61, “Sheria ya Ushahidi”, Na. 6, 1967.
2. C.G. Mung’ong’o, Mirathi ya Hatari. TPH., Dar es Salaam, uk. 3.
3. J. Simbamwene, (1987) Ukitoa Siri Utachinjwa. Jomssi Publications, Dar es Salaam.
4. k.h.j., uk. 4.
5. Sembene Ousmane, (1985) The Last ofthe Empire. Heinemann, uk. 50.
6. A. La Guma, (1968) A Walk in the Night, Heinemann Educational Books, London, uk. 2:
Quote:
The young man wore jeans that had been washed several times and which were now left with a paleblue colour flacked with old grease stains and the newer, darker ones of the day’s work going white along the hard seams. The jeans had brass buttons and the legs were too long, so that they had to be turned up six inches at the bottom. He also wore an old khaki shirt and over it a rubbed and scuffed and worn leather coat with slanting pockets and woollen wrists. His shoes were of the moccasin type, with leather thongs stitching the saddle to the rest of the uppers. They had been a bright tan once, but now they were a worn dark brown, beginning to crack in the groves across the insteps. The thongs had broken in two places on one shoe and in one place in the other.
7. Mohamed, S. (1980) Utengano, Longman, Nairobi, uk. 110:
Quote:
Shoka alikuwa barubaru mmoja, fahali wa mtu, kavundumka mwili na kukecha musuli. Mwili wake haukujali suluba au kitisho chochote. Uso wake tinginya. Macho yake ni maboni yaliyojitahidi kutoka kwenye vibofu vyake, lakini hayakufuzu. Meno ya juu yamemng’oka kwa hivyo mdomo wake wa chini umechomoza mbele na ule wa juu umerudi nyuma. Pua yake ni pande la nyama lenye matundu mawili ya ndonya. Nywele zake zimejenga tuta huku na huku, katikati mlima safi unaoteleza. Nyusi nyingi zimetengana na macho. Juu ya urembo huu akapambwa na mbabuko wa mwili, na kwa hivyo rangi yake hapa na pale ilikuwa nyeusi na ya shaba.
8. Mohamed S. (1980) Dunia Mti Mkavu, Longman, Nairobi, uk. 6:
Quote:
Kwisha hivyo alimtazama Fumu kwa ushindi na kejeli. ‘Ha, ha, ha’ alicheka kicheko cha kiburi ambacho kilimwamsha Fumu kutoka jitimai ya kugandwa na jibwa na ule mlio wa bunduki. Alipozindukana, alijikuta amesimama hatua tatu karibu na Fauz. Macho yao yalikutana; ya Fumu yakiwaka moto na Fauz kama pilipili hoho. Fauz alikwaruza meno, ishara ya hamaki. Fumu alimeza fundo la mate; lililoonekana likisukumwa ndani ya umio. Na sasa Fumu alimwona Fauz amesimama kijeuri – miguu yake kaitawanya mmoja huku na mwingine kule bunduki yake imesimamia tako, ameikamatia kwenye mdomo kwa mikono yake miwili aliyoinyoosha. Alipasua kicheko kingine cha jeuri, na Roket, aliyerejea miguuni pake alikuwa akipungapunga mkia.
9. La Guma, m.y., uk. 48:
Quote:
In the dark a swamp of a cloud struggled along the edges of the Table Mountains, clawed at the rocks for a foothold, was torn away by the breeze that came in from the south east and disappeared.
10. La Guma, k.h.j., uk. 71:
Quote:
Night crouched over the city. The glow of street lamps and electric signs formed a yellow haze, giving it a pale underbelly that did not reach far enough upwards to absorb the stars that spotted its purple hide. Under it the city was a patchwork of greys, whites and reds threaded with thick ropes of black where the dark’ness held the scattered pattern together. Along the sea front the tall shadows of masts and spars and cranes towered like tangled bones of prehistoric monsters.
11. La Guma, k.h.j., uk. 93 – 94: Hapa hisia tatu: kugusa, kuona na kusikia, zimetumika kama ifuatavyo:
Quote:
Delirium was an anaesthetic and he no longer felf pain. But his fingers and hands seemed to have thickened and begun to lose all sense of feeling, so that even when he knew that he moved them over his body they did not seem to touch anything. They were like thick, smaller, lifeless things. Also he had difficulty in seeing the darkness inside the van, and there was highpitched ringing sound running through his brain. He tried to look through the darkness but the power of sight had gone from his eyes. They remained open although he could no longer see. Then his mouth was suddenly full of bile and blood and he tasted the sourness and the salt for an infinitesimal instant before he was dead.
12. S.A.M. Khamisi, (1983) “Hatua Mbalimbali za Kubuni na Kutunga Riwaya”, katika                            TUKI, Makala za Semina ya Kimataifa ya Waandishi wa Kiswahili, Juzuu III, Fasihi.Dar es                  Salaam, uk. 242. Hapa hisia tatu zimetumika: kusikia, kugusa na kuona:
Quote:
Upepo upepo ulivuma, ulivuma ukanguruma katika hamsauti wenye kuogofya mithili ya mirindimo ya radi, ulimvaa Sibu ukamkumba, ukataka kumpeperusha, ila alikita kwa uzito, akatia nanga huku akimia kanzu yake iliyokuwa ikipeperushwa isimfedhehi. Mbali kwenye bonde alitupa jicho kwenye uwanda, aliona nyasi zikisukwasukwa.
13. S. Mohamed, (1980) m.y.k., uk. 5.
Quote:
Ilikuwepo treya moja ya vitoweo – kuku wa kupaka wa mbano, katika sahani yake; kuku wa kuchoma, mwekundu kwa pilipili aliyerembwa nayo, kuku wa makshai aliyekaukia, maini kidogo, yamechemshwa kwa malimau na kurashiwa pilipili manga, mnofu wa samaki wa kukaanga, kamba wa kutokosa na zaidi chatne ya kuchachua kinywa.
14. S.A.M. Khamisi, (1983) m.y.k., uk. 241
15. E. Kezilahabi, (1983) “Utunzi wa Riwaya na Hadithi Fupi”, katika TUKI, Makala za Semina ya Kimataifa ya Waandishi wa Kiswahili, Juzuu III, Fasihi, Dar es Salaam, uk. 227
16. F.E. Caroline, (1961) Shakespeare’s Imagery. Cambridge University Press, Cambridge.
17. Nico ye Mbajo (1984) Sifi Mara Mbili. Mcheshi Publications, Dar es Salaam.
18. J. Simbamwene (1987) Ukitoa Siri Utachinjwa. Jomsi Publications, Dar es Salaam.
19. J. Simbamwene (1987) Mauaji ya Lojingi. Jomsi Publications, Dar es Salaam
20. Khamisi, (1983) m.y.k., uk 245.
21. A. Abdalla, (1973) Sauti ya Dhiki. Oxford University Press, Nairobi.
22. A. Nassir, (1974) Malenga wa Mvita. Oxford University Press, Nairobi
23. Abdalla, (1973) m.y.k., uk. 42.
24. k.h.j., uk. 10.
25. k.h.j., uk. 69.
26. S. Robert, (1968) Kielezo cha Fasili. Nelson, Nairobi, uk. 48.
27. E. Hussein, (1969) Mashetani. Oxford University Press, Nairobi.
28. E. Mbogo, Isinyago (Ms), uk. 53; ambapo ametumia hisia nne za kuona, kunusa, kugusa na                     kuonja.
Quote:
Namanduta mwana wa Simbaulanga
Na Singo – mwindaji shujaa
Marafiki wa pete na kidole
Mwayaona maisha haya thakili yaliyokithiri?
Watu hawa wenye uvumilivu uliotendesa
Nchi yao kama ujauzito
Wakulu wao kama watoto wao
Jasho lao kama mbeleko zao
Wakiwabeba migongoni waungwana hao
Kama watoto’ wachanga wenye
Vitovu vibichi matumboni. mwao
Wakiwanyea, wakiwakojolea migongoni mwao
Na huku akina nani kajamba wakifyonza
Wakisafisha kwa ustadi mkubwa
Kamasi za waungwana hao
Kwa kutumia ndimi na midomo yao.
29. Khamisi, (1983) m.y.k., uk. 240.
30. Abdalla., (1973) m.y.k., uk. 56.

Print this item

  UHAKIKI WA RIWAYA YA TUTARUDI NA ROHO ZETU?
Posted by: MwlMaeda - 12-28-2021, 09:56 AM - Forum: Uhakiki wa kazi za fasihi - No Replies

FUNGUA HAPA CHINI KUSOMA KITABU >>>>

.pdf   TUTARUDI-NA-ROHO-ZETU1.pdf (Size: 2.15 MB / Downloads: 1)  
1.0  Utangulizi[/url]
Kazi hii inahusu uchambuzi wa maudhui katika riwaya ya mkondo wa kipelelezi na kiarifu ambayo inaitwa“Tutarudi na Roho Zetu?”iliyoandikwa na Ben Mtobwa. Katika kujadili riwaya hii tutaeleza dhana ya riwaya, dhana ya mkondo wa kipelelezi, usuli wa mwandishi, muhtasari wa kitabuchenyewe, nadharia itakayotumika kuchambua maudhui ya kitabu hiki, uchambuzi wa maudhui na hitimisho.
 
1.1 Dhana ya Riwaya
Kwa mujibu wa Madumulla (2009) akimrejelea Msokile (1992) anafafanua kuwa riwaya ni kazi ya sanaa ya kubuni, ni maandishi ya nathari (ujazo) yanayosimulia hadithi ambayo kwa kawaida ina uzito, upana, urefu wa kutosha, ina wahusika wengi wenye tabia mbalimbali, ina migogoro mingi mikubwa na midogo.
Senkoro (1982) anasema riwaya ni hadithi ndefu ya kubuni yenye visa vingi, wahusika zaidi ya mmoja, na yenye mazungumzo na maelezo yanayozingatia kwa undani na upana maisha ya jamii.
Wamitila (2003), Samwel na wenzake (2013), wanasema kuwa riwaya ni kazi andishi ya fasihi ambayo kwa kawaida ni ndefu zaidi kuliko hadithi fupi. Urefu wa riwaya maana yake ni kwamba msuko simulizi umejengeka vizuri, kuna wahusika wengi, inaenea muda mrefu, na mada zake ni nzito na pana kiasi. Mifano mizuri ya riwaya kwa lugha ya Kiswahili ni “Nagona” au “Mzingile” riwaya za mwandishi Euphrase Kezilahabi.
Kwa ujumla riwaya ni hadithi ndefu za kubuni zenye wahusika wengi au wachache zinazoelezea maisha ya mtu au jamii fulani.
 
1.2 Dhana ya mkondo wa kiarifu na kipelelezi
Kwa mujibu wa Madumulla (katajwa) mkondo wa kiarifu na kipelelezi ni kategoria ya ubunaji kuhusu uhalifu na upelelezi iliyojitokeza katika fasihi ya Kiswahili karibu mwishoni mwa muongo wa hamsini wa karne ya 20.
Mkondo wa kipelelezi; aina hii ya utunzi inahusishahadithi zinazosimulia kuhusu upeleleziwa uhalifu fulani kama vileujambazi, wizi, rushwa, mauaji. Kwakawaida huanza na tukio fulani la uhalifu ambalo limekwisha tendekanaye msimulizi huwaongoza wasomajikatika safari ya kung'amua kiini chauhalifu husika. Sifa kuu ya hadithihizi ni kwamba husheheni taharukinyingi na huiteka hadhira kwa kuchocheahamu ya kugundua au kuteguakitendawili. Kwa mfano riwaya ya'Masaibu ya Ndugu Jero.' (Taifa leo, 2015).
 
Hivyo basi mkondo wa kiarifu na kipelelezi ni mkondo ambao unahusu riwaya zenye uhalifu na upelelezi ndani yake kama vile ujambazi, rushwa na mauaji. Kwa mfano katika riwaya hii ya “Tutarudi na roho zetu?” ni mfano mzuri wa mkondo huu kwani umejaa upelelezi na uhalifu ndani yake.
 
1.3 Usuli wa Mwandishi
Kwa mujibu wa Dr. Mikhail (2008) mwandishi Ben Rashid Mtobwa alizaliwa tarehe 28  mwezi wa nane, mwaka 1958 huko mkoani Kigoma, magharibi ya Tanzania. Maisha yake na kazi yake alijikita katika uandishi kwa lugha ya Kiswahili. Alioa na alikuwa na watoto wanne.
 
Ben Mtobwa alianza uandishi akiwa shule ya sekondari. Baadaye alianza kuandika habari katika magazeti kama “Nchi yangu,” “Bara Afrika” na “Kiongozi”. Pia, uhariri katika magazeti kama “Uhuru na Mfanyakazi”. Akiwa mwandishi alianza kujulikana miaka ya 1980 akiwa miongoni mwa waandishi walioanza kuandika vitabu vya Kiswahili. Vitabu vyake vilivyojulikana sana miaka hiyo ni “Dimbwi la Damu” (1984),“Tutarudi na Roho zetu?”(1984), “Najisikia Kuua Tena” (1985), “Joram Kiango Mikononi mwa Nunda” (1986),Lazima Ufe Joram” (1986),“Pesa Zako Zinanuka” (1986),“Salamu Kutoka Kuzimu” (1987), “Malaika wa Shetani” (1988),Dar es Salaam Usiku” (1990), “Zawadi ya Ushindi” (1992), “Nyuma ya Mapazia” (1996), “Roho ya Paka” (1996)  “Mtambo wa Mauti” (2004). Piaaliandika kitabu cha watoto kilichoitwa “Nitakusubiri” na habari ndogo iliyoitwa“Mwanaharamu”na mwishoni kabla ya kifo aliandika kitabu kilichoitwa “Mikataba ya Kishetani”.
Baada ya kujulikana kama mwandishi miaka ya 1980 Ben Mtobwa alikuwa meneja mwongozaji katika kampuni ya uchapishaji ya Heko iliyopo jijini Dar es Salaam. Baadae kampuni hiyo ilikuwa muhimu sana katika usambazaji wa vitabu vya fasihi, uchapishaji wa magazeti na kuwasaidia waandishi chipukizi.
Ben Mtobwa alifariki tarehe 9/11/2008, akiondoka na mipango mingi mipya na matumaini makubwa katika kuikuza fasihi na maisha ya jamii. Hali hii imezifanya jamii kumkumbuka sana kutokana na mchango wake kiuandishi na kifasihi.
 
1.4 Muhtasari wa kitabu
“Tutarudi na Roho Zetu?” ni riwaya iliyoandikwa na Ben Mtobwa. Riwaya hii inaelezea shughuli zilizofanywa na nchi za mstari wa mbele katika ukombozi kusini mwa Afrika, zimetendwa mengi maovu na utawala dhalimu….hata hivyo haikupatikana kutokea tishio zito la kutisha kama hili, ambalo linakaribia kutokea. Tukio la kutatanisha ambalo linawatoa machozi wananchi wanchi mbalimbali. Wanajitokeza mashujaa kwenda Afrika kusini, lakini kila aendaye huko harudi na roho yake.
Inspecta Kombora nchiniTanzania jasho linamtoka. Anawathamini mashujaa wengi lakini anamtambua shujaa mmoja Joram Kiango. Jambo la kusikitisha ni kwamba sasa hivi Joram ni mtumiaji mzuri ambaye anatembea kutoka jiji hadi jiji akiwa na yule msichana mzuri Nuru. Juhudi za Kombora kumsihi hazikufua dafu. Badala yake Joram anafanya maajabu mengine ambayo yanalichafua jina lake hapa nchini na kote duniani. Wakati huo siku ambayo utawala huo umeweka ili kuachia pigo lao la mwisho inazidi kukaribia. Sasa yamesalia masaa, lakini baadae Joram anaonekana ndiye mkombozi mkuu wa nchi za mstari wa mbele. Mwandishi wa hadithi hii amezungumzia mambo tofauti tofauti kwa zana mbalimbali ambazo ni pamoja na watu wenye bahati na wenye mikosi, wasichana wenye sura nzuri na wale wenye mbaya. Ni hadithi kuhusu mapenzi na chuki, uhai na kifo.
 
1.5 Nadharia ya Uhalisia
TUKI (2004) wanaeleza kuwa nadharia ni mawazo, maelezo na muongozo uliopangwa ili kusaidia kuelezea kutatua au kutekeleza jambo fulani. Nadharia yoyote ile ya kihakiki ni nyezo ya kusaidia kufikisha lengo fulani.
Kwa mujibu wa Ntarangwi (2004) anasema nadharia ya uhalisia ni uwakilishi wa uhalisi wa mambo katika fasihi, nadharia hii ilizuka katika karne ya 19 hususani kwa sababu za kupinga mkondo wa ulimbwende.
 Hivyo basi, nadharia ya uhalisia ni nadharia ambayo hujikita katika mambo yaliyopo, tukio mahususi na matokeo yanayoweza kuthibitika. Tukirejelea katika riwaya ya “Tutarudi na Roho Zetu?”mwandishi amejikita katika uhalisia kwani amezungumzia mambo ambayo yanajitokeza na yapo katika jamii. Hivyo tutatumia nadharia hii kuhakiki maudhui yaliyojitokeza katika kitabu hiki kwa kuwa kitabu hiki kinasawiri mambo ambayo yapo katika jamii zetu.
 
2.0 Maudhui katika Riwaya ya “Tutarudi na Roho Zetu?”
Kwa mujibu wa Madumulla (katajwa) maudhui ni mawazo fikra na ujumbe uliomo katika kazi ya fasihi.Maudhui ina vipengele mbalimbali ambavyo ni pamoja na dhamira, ujumbe, falsafa, migogoro, msimamo na mtazamo wa mwandishi. Katika riwaya ya “Tutarudi na Roho Zetu?” vipengele vya maudhui vinavyojipambanua au kujidhihirisha ni pamoja na:-
 
2.1 Dhamira
Madumulla (katajwa) anasema dhamira ni wazo kuu katika kazi ya fasihi. Dhamira ni sehemu tu ya maudhui. Dhamira ndiyo hujenga kiini cha kazi ya fasihi,yafuatayo ni mawazo au dhamira zilizojitokeza katika riwaya hii ya“Tutarudi na Roho Zetu?”
 
2.1.1 Ukombozi
TUKI (katajwa) wanasema kuwa ukombozi ni uokoaji wa watu kutoka kwenye hali mbaya ya udhalimu au hali duni. Katika riwaya hii kuna aina mbili za ukombozi zilizojitokeza ambazo ni ukombozi wa kisiasa na ukombozi wa kifikra.
 
 2.1.1.1Ukombozi wa Kisiasa
Katika riwaya ya “Tutarudi na Roho Zetu?”miongoni mwa ukombozi uliojitokeza ni ukombozi wa kisiasa. Mwandishi anadhihirisha ukombozi wa kisiasa kwa kumtumia mhusika wakemkuu Joram ambaye ni mpelelezi, analisaidia bara lake kupata ukombozi kutoka katika mikono ya makaburu akishirikiana na mwenzake Nuru. Mwandishi anasema;
“Kwa kila hali inaonyesha dhahiri kuwa Joram Kiango akishirikiana na mwenzi wake, yule msichana mzuri Nuru. Wameshiriki kwa njia moja au nyingine katika kufanya hayo yaliyofanyika huko Afrika Kusini.Na endapo wasingefanya walichokifanya dakika hii hii Afrika nzima ingekuwa katika msiba kwani kulikuwa na mipango ya mtambo huo kuzishambulia nchi zote za mstari wa mbele kwa pamoja”(uk 173).
 
 2.1.1.2 Ukombozi wa Kifikra
 Mwandishi anaonesha ukombozi wa kifikra katikariwaya hii kwa kumtumia mhusika wake Joram.Pale ambapo Joram aliamua kurudi tena na kupigania ukombozi katika bara lake, baada ya kukaa muda mrefu akiwa anastarehe na Nuru katika miji mbalimbali na baadaetunaona jinsi anavyojitoa kusaidia bara lake kwa kutega vigololi vilivyopatikana kwa Chonde na kuvitega katika majengo muhimu ya Makaburu wa Afrika kusini kwa muda wa masaa machache.Mwandishi anasema;
“Wakiwa wameikariri ramani hiyo kikamilifu kazi waliyoifanya mitaani humo ilikuwa ya kufuata yale majengo waliyokusudia na kutega vile vigololi vilivyopatikana kwa chonde na kuvitegesha katika kipindi cha saa tatu kamili”(uk 132).
Katika jamii yetu suala la ukombozi limejitokeza hasa kipindi kilichopita cha uchaguzi, watu wengi wamekombolewa kifikra katika suala zima la siasa, ambapo imepelekea wanajamii (watanzania) wengi kujiingiza katika siasa na kutafuta haki ndani ya siasa.
 
2.1.2 Kujitoa mhanga
Kujitoa mhanga ni kufanya jambo fulani kwa ajili ya kitu, mtu au watu fulani na kuwa tayari kwa lolote ([url=http://www.merriam-webster.com/dictionary/sacrifice]www.merriam-webster.com/dictionary/sacrifice).Katika riwaya ya hii tunaona suala la kujitoa mhanga limejitokeza, kwani tumeona jinsi Joram na Nuru wanavyojitoa ili kuikomboa nchi yao, hadi kufikia hatua ya kuhatarisha uhai wao na hata wao wenyewe kuua ili tu waweze kulikomboa bara lao dhidi ya makaburu. Mwandishi anadhihirisha suala la kujitoa mhanga kwa kumtumia mhusika wake Nuru alivyojitoa mhanga na kumuua Chonde kwa bastola ili kuokoa maisha ya Joram. Mwandishi anasema;
“Risasi mbili tatu zaidi zilisikika kama zilizopigwa bila shabaha yeyote. Kisha kimya kikafuata, kimya ambacho kilitoweka kwa mkoromo wa mtu aliyekuwa akikata roho………….” (Uk 47)
Vile vile mwandishi ameonyesha suala la kujitoa mhanga kwa kumtumia mkaburu aliyetoka Afrika kusini kuja Tanzania kwa lengo la kufanya upelelezi huku akiwa amefanya plastic surgery miaka 10 iliyopita, ambapo tumboni alionekana mweusi, usoni na mikononi alikuwa mweupe ili hali yeye kwa asili ni mtu mweupe,hii inathibitisha jinsi mkaburu huyo alivyojitoa mhanga ili aweze kupata taarifa kutoka katika nchi ya Tanzania. Mwandishi anasema;
“………….Ningependa ieleweke kuwa mimi siyo mzungu…..mimi ni mtu mweusi mzaliwa wa Soweto ….. Ngozi hii nyeupe iliyokaa usoni na mikononi ni matokeo ya plastic surgery ambayo niliifanya miaka kumi iliyopita.” (Uk 95)
Katika jamii tunayoishi suala la kujitoa mhanga limejitokeza kwani tunaona baadhi ya viongozi walivyoamua kujitoa mhanga ili kuleta maendeleo katika jamii.
 
2.1.3 Ujasiri
Kwa mujibu wa TUKI (katajwa) ujasiri ni hali ya kukabili jambo bila ya hofu, uhodari na ushujaa. Katika riwaya hii mwandishi ameonesha suala la ujasiri kwa kuwatumia wahusika wake wakuu Joram na Nuru. Ujasiri umejitokeza kwa kiwango kikubwa kwani tunaona jinsi Joram na Nuru walivyokuwa jasiri katika harakati za kulikomboa bara lao kutoka katika mikono ya makaburu watu ambao waliwafanyia maovu mengi. Mwandishi anasema;
“Lazima tupambane nao, na huu ni wakati pekee wa kuonyesha moyo wetu. Uoga hauwezi kutufanya tukubali kuwa mateka wa utawala haramu kama huu. Lazima tushinde” (Uk 93).
Vilevile tunaona jinsi Joram alivyokuwa jasiri kujibu swali aliloulizwa na Nuru kuhusu wizi alioufanya katika City drive bank. Joram alimjibu kwa ujasiri kuwa ameiba ila ameiba waziwazi tofauti na wenzake wanaoiba kwa siri na kufanya maendeleo ambayo hayaendani na mishahara yao. Mwandishi anasema;
“Huoni watu wenye mishahara ya shilingi elfu mbili wanavyojenga majumba ya mamilioni? Unadhani wanazipata wapi bila wizi? Tofauti yangu na wao ni kwamba mimi nimeiba machomacho, wao wanaiba kusirisiri. Mwizi ni mwizi tu” (uk 65).
 Pia tunaona jinsi Nuru alivyoonesha ujasiri wake kwa kumuua Iron Von baada ya kumteka Nuru kwa nia ya kutimiza haja yake ya mapenzi, na kumwonesha alipo Joram na baada ya hapo amuue. Mwandishi anasema;
“Pokea chako, muuaji mkubwa” Nuru alinong’ona na akiifyatua bastola” (uk 159).
Hivyo, katika jamii yetu suala la ujasiri linajidhihirisha wazi kwani tunaona jinsi baadhi ya wanajamii walivyofanya matendo ya kijasiri katika kufichua ubadhilifu unaofanywa na watu wachache katika jamii ili kuikomboa jamii yao au nchi yao.
 
2.1.4 Uzalendo
Kwa mujibu wa TUKI (katajwa) uzalendo ni hali ya mtu kuwa tayari kuifia nchi yake. Katika kuchambua riwaya hii ya “Tutarudi roho zetu?” Suala la uzalendo limejipambanua vyema, mwandishi anathibitisha suala la uzalendo kwa kuwatumia wahusika wake Joram na Nuru ambao wameonesha uzalendo mkubwa kwa kuipenda nchi yao kwa dhati hadi kuchukua jukumu la kupambana na kuwaua makaburu ambao wamewatesa kwa muda mrefu kwa lengo la kuikomboa nchi yao kutoka katika mikono ya makaburu. Mwandishi anasema;
“Nadhani inatosha. Wanakufa wenye hatia na wasio na hatia sasa iliyobaki ni ile kazi moja ya mwisho kulipua huo mtambo” (Uk 34).
Vilevile, suala la uzalendo linajidhihirisha kwa mhusika inspecta Kombora. Matendo yake yalikuwa ya kizalendo kwa nchi yake kwani alitumia mbinu mbalimbali ya kupambana na kuwaondoa makaburu wa Afrika Kusini. Mwandishi anasema;
“Kombora alikuwa mwenyeji, alikuwa mwenyekiti wa mkutano huo ambao ulifanywa kwa siri kubwa mkutano ambao ulijumuisha watu wenye sura mbalimbali, umri mbali mbali, viwango mbali mbali vya elimu wote wakiwa na dhamira moja” (uk 94).
Pia, Inspecta Kombora amedhihirisha uzalendo pale ambapo aliamua kubaki ofisini baada ya wenzake kuondoka na kwenda kujumuika na familia zao hadi dakika ya mwisho na kushindwa kwenda kujumuika na familia yake ili aweze kuona nini kitatokea. Aliamua kukubaliana na tendo lolote ambalo lingetokea pale. Kwani kutoka muda mfupi uliopita walikuwa tayari wameshapata taarifa kutoka katika kibarua kilichokutwa ikulu kuwa baada ya masaa 3 kungetokea mlipuko katika maeneo hayo. Mwandishi anasema;
“Alikuwa ameamua lolote ambalo lingetukia, limkute katika ofisi yake” (Uk 171).
Katika jamii zetu suala hili la uzalendo linajidhihirisha wazi kwani tunaona jinsi baadhi ya viongozi wanavyojitoa katika nchi hii kwa namna moja au nyingine. Kwa mfano, tunaona baadhi ya viongozi wa kisiasa walivyoonesha uzalendo katika nchi yao kwa kukataa kulipwa hela za ziada au posho za vikao kwa kuona kuwa siyo haki yao bali ni ubadhilifu na kuwanyonya wananchi.
 
2.1.5Ubaguzi wa rangi
Ubaguzi wa rangi ni ile hali au kitendo cha kuwaweka watu katika makundi kutokana na rangi zao kwa ajili ya kutoa huduma tofauti tofauti kulingana na rangi zao. (https://en.wikipedia.org/wiki/Racial_discrimination).Suala la ubaguzi wa rangi limejitokeza katika riwaya hii ambapo inaelezwa kuwa watu wa rangi nyeusi wanatazamwa kuwa ni watu wenye fikra ndogo, wasiokuwa na akili ambao hawawezi kuleta maendeleo yoyote zaidi ya mtu mweupe. Na pia wanathubutu kusema kuwa ngozi nyeusi ni dalili ya laana ambapo mtu huyu mweupe ndiye anaonekana mwenye akili. Mwandishi anasema;
“Ngozi nyeusi ni dalili ya laana. Nywele fupi nidalili ya akili ndogo. Bila hekima uongozi wa mtu mweupe Afrika ingekuwa bado gizani, na endapo ataondoka mtu mweupe giza litarudi”(uk 104).
 
2.2 Migogoro
 Kwa mujibu wa TUKI(katajwa)wanasema kuwa migogoro ni hali ya kutofautiana baina ya pande mbili au zaidi, wanasema migogoro inaweza kuwa ya familia, matabaka ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni. Katika riwaya hii imejitokeza migogoro tofautitofauti kama ifuatavyo:
 
2.2.1 Mgogoro kati ya makaburu (wazungu) na watu weusi
Mgogoro huu ulitokea wakati watu weupe (makaburu) wakiwadharau watu weusi na kuwaona si chochote, watu duni pamoja na kuwafanyia maovu mengi. Mgogoro umesababishwa na tofauti za rangi na kupelekea uadui mkubwa kati ya watu weupe na weusi. Ubaguzi huu wa rangi ambao ulisababishwa na siasa ya magharibi ndio uliopelekea mapigano kati ya watu weupe na weusi na kupelekea vifo hasa kwa watu weusi. Yote haya yamejidhihirisha kwa mawanda mapana katika riwaya hii (uk 104).
 
2.2.2 Mgogoro kati ya Inspecta Kombora na Joram Kiango
Mgogoro huu ulitokea pale ambapo Inspecta alipomfuata Joram na kumsihi arudi katika kazi yake ya upelelezi. Na Joram kukataa ombi hilo. Suluhisho ni pale ambapo Inspecta Kombora aliamua kuondoka (uk 19).
 
2.2.3 Mgogoro kati ya Nuru na Joram
Mgogoro huu ulitokea wakati Nuru akimbembeleza sana Joram arudishe pesa alizoiba kutoka katika Benki ya City Drive. Pamoja na kwenda kuomba msamaha ubalozini na Joram kutokubaliana naye kwa wakati ule. Suluhisho ni pale ambapo baadae alikubali kurudisha pesa zile Benki baada ya kulipua mji wa Soweto uliopo Afrika kusini japokuwa hakupenda kwenda kuomba msamaha ubalozini (uk 66).
 
2.2.4 Mgogoro wa nafsi
Huu ni mgogoro unaojitokeza baina ya mtu mmoja ndani ya nafsi yake. Katika riwaya hii mgogoro wa nafsi umejitokeza kwa Joram pale ambapo alitoka kuongea na Chonde na baadaye akaanza kujiuliza kuwa huyu ni mtu wa aina gani na amelijua vipi jina langu? (uk 25).
 
2.3 Ujumbe
Kwa mujibu wa Madumulla (katajwa)ujumbe ni kitu ambacho mwandishi hudhamiria kumtumia msomaji, kila kazi ya fasihi hubeba ujumbe ambao msanii hutaka umfikie msomaji wake.Katika riwaya ya hii kuna ujumbe wa aina tofauti tofauti uliojitokeza kama ifuatavyo:
2.3.1Kujitoa mhanga ni njia mojawapo ya kupata ukombozi katika harakati za kudai uhuru mwanamke hapaswi kuachwa nyuma kwani ana mchango mkubwa ambao unapelekea ukombozi.
2.3.2 Ujasiri ni muhimu katika harakati zote za ukombozi.
2.3.3Uzalendo ni muhimu katika harakati za kutafuta ukombozi, mwananchi lazima awe mzalendo na nchi yake.
2.3.4Ubaguzi wa rangi ni kikwazo ambacho kinapelekea uadui mkubwa baina ya nchi na nchi. Hivyo hatuna budi kufuatilia mbali ubaguzi wa rangi.
2.3.5 Katika harakati za kudai uhuru mwanamke mwanamke hapaswi kuachwa nyuma kwani ana mchango mkubwa ambao unapelekea ukombozi.
 
2.4Falsafa
 Kwa mujibu wa Madumulla(katajwa)akimrejelea Msokile (2009) falsafa ni wazo ambalo mtu anaamini kuna ukweli fulani unaohusu maisha yake pamoja na maisha ya jamii.Katika riwaya ya hii mwandishi anaamini kuwa ili kufanikiwa katika suala zima la ukombozi ni lazima tujitoe mhanga tuwe na ujasiri pamoja na uzalendo kwa kile tunachotaka kukikomboa.
 
2.5Msimamo
 Kwa mujibu wa Madumulla (katajwa) ni mawazo, mafunzo na falsafa ya msanii. Hubainisha msimamo wake kuhusu masuala mbalimbali ya kijamii na ndiyo huweza kuwatofautisha wasanii wawili au zaidi wanaoandika kuhusu mazingira yanayofanana. Katika riwaya hii mwandishi ana msimamo wa kimapinduzi kwani ameonesha kuwa mtu kuwa na ujasiri, kujitoa mhanga pamoja na uzalendo ni silaha kuu katika kuleta ukombozi.
 
3.0 Hitimisho
Kwa ujumla riwaya hii ya “Tutarudi na Roho Zetu?”inaelezea namna nchi za mstari wa mbele zilivyoshikamana ili kupinga na kupambana na makaburu huko Afrika ya Kusini waliowatenda maovu watu weusi na kuwachukulia kama watu wasio na akili na hatimaye watu weusi kufanikiwa kuwashinda makuburu kutokana na juhudi kubwa zilizoongozwa na Joram Kiango.
 
 
 
 
4.0 Marejeo
Gazeti la Taifa Leo, (15-10-2015),Jumatano.
Kezilahabi, E. (1991), Mzingile,University of Dar es Salaam Press; Dar es Salaam.
Kezirahabi, E. (1990), Nagona, University of Dar es Salaam Press; Dar es Salaam.
Madumulla, S.J (2009), Riwaya ya Kiswahili, Nadharia,Historia na Misingi ya Uchunguzi.                     Mture Educational Puplishers Limited; Dar-es salaam.
Mikhail, G. (2008), Swahili Forum 15. United States International University; Nairobi.
Msokile, M. (1992) Kunga za Fasihi na lugha.Educational Publishers and Distributors, Limited; Dar es Salaam.
Mtobwa, B. (2008), Tutarudi na Roho Zetu?. East Africa Educational Publishers LTD; Dar es Salaam.
Ntarangwi, M. (2004), Uhakiki wa Kazi za Fasihi.
Samwel, M. na Wenzake (2013) Ushairi wa Kiswahili, Nadharia, Mifano na Muongozo kwa Walimu wa Kiswahili.MEVELI Publishers; Dar es Salaam.
Senkoro, E.(1982), Fasihi. Press and Publicity Centre; Dar-es-Salaam.
TUKI (2004), Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Oxford University Press; Dar es Salaam.
Wamitila na Kyallo,W. (2003), Kamusi ya Fasihi Istilahi na Nadharia, Focus Publications; Nairobi.
www.merriam-webster.com/dictionary/sacrifice 17:15 on 22nd Dec. 2015

Print this item

  SHAABAN ROBERT: ASHIKI KITABU HIKI
Posted by: MwlMaeda - 12-28-2021, 09:50 AM - Forum: Uhakiki wa kazi za fasihi - No Replies

Shaaban Robert: Ashiki Kitabu Hiki
SURA YA NANE
Kabla ya kuanza kuyachambua masuala mbalimbali yanayojitokeza katika mashairi ya diwani hii ya Ashiki Kitabu Hiki, tuichunguze kwanza kwa kifupi historia ya Shaaban Robert.
Shaaban Robert alizaliwa tarehe 1 Januari 1909 huko Vibambani, Tanga. Alisoma katika shule mbalimbali Dar es Salaam tangu 1922 hadi 1926, na baada ya hapo alifanya kazi huko Pangani, Longido, na baadaye Tanga. Alifariki tarehe 20 Juni, 1962.
Zaidi ya kuandika riwaya na insha, Shaaban Robert aliandika vitabu vingi sana vya mashairi; na kwa kweli ushairi ndio hasa uliompa umaarufu mwandishi huyu. Kati ya vitabu au tuseme diwani za ushairi za mwandishi buyu zipo za Pambo ta Lugha (1948), Marudi Mema (1952), Uhuru (1967), Ashiki Kitabu Hiki (1968), Mashairi ya Shaaban Rohert(1968), Mwafrika Aimba (1969) na Sanaa ya Ushairi (1972).
Ili kuweza kupata undani wa mashairi ya diwani yoyote ya Shaaban Robert ni vizuri kusoma baadhi kubwa ya diwani hizo zilizotajwa, au hata zote, kwani dhamira mbalimbali alizozishughulikia mshairi huyu katika maisha yake ya uandishi zimejitokeza karibu katika kila diwani.
DHAMIRA KUU
Jambo moja linalojitokeza sana katika mashairi mengi ya diwani hii ni lile la malumbano. Malumbano ni majibizano kati ya washairi kuhusu mambo mbalimbali, na aghalabu malumbano hayo huwa na kujisifu kwirigi kunakotolewa kiushairi. Kujisifu huku kulikuwa kwa kawaida sana kati ya washairi ambao waliandika kuringia na kujigambia ushaha wao katika uwanja wa ushairi.
Katika diwani hii mashairi yafuatayo tunaweza kuyaweka katika kundi hfli la malumbano: “Utangulizi” (uk. xi-xii), “Sichi” (uk. 1), “Wapinzi” (uk. 3), “Ngozi ya Simba” (uk. 3-5), “Bahati” (uk. 10), “Ni Wapuzi” (uk. 27-28), “Tosa Haitatukuka” (uk. 35-36). “Situmii Shoka Ukucha Unapofaa” (uk. 37-39), “Mwezi Hauwi Jua” (uk. 39-40), na “Si Kweli” (uk. 40-41).
Ni wazi kuwa mashairi haya ya malumbano hayaishilii katika kiwango cha kujitapa tu kwani zaidi ya kuringia usanii, hapohapo iliwabidi wanaolumbana kuonyesha ujuzi wao wa mambo waliyokuwa wanayajadili. Kwa mfano katika mashairi ya “Situmii Shoka Ukucha Unapofaa” na “Mwezi Hauwi Jua” suala la umuhimu wa ndoa na ubaya wa ujane linajadiliwa kimalumbano. Mojawapo ya mbinu kubwa zinazotumiwa na washairi wakati wa malumbano ni ile ya kufumba kwa kutumia lugha ya kilinge na sanaa ya hali ya juu. Kwa hiyo katika mashairi haya tunakuta matumizi ya tamathali za usemi, nahau, methali, na mifano mingi ya lugha nzito inayozidisha hali ya shairi kuwa tambo. Nia wakati mwingine ni ya kuwadunisha “maadui” hadi wajione kuwa wao ni chawa wadogo tu ambao hawastahili kuuawa kwa shoka wakati ukucha unatosha.
Katika diwani hii. Shaaban Robert anazungumzia hasa mambo yafuatayo
Quote:
1. Suala la Wanawake
2. Athari za Pesa katika jamii
3. Falsafa kuhusu maisha
4. Hakidhidiyauovu.
Suala la Wanawake
Shaaban Robert ni mmoja wa washairi wa Kiswahili ambao kalamu zao zimelishughulikia sana suala la mwanamke na nafasi yake.katika jamii. Tunaugundua utetezi wake wa mwanamke si katika ushairi tu bali pia katika kazi zake zingine, kwa mfano katika Wasifu wa Siti Binti Saad (1955) na Siku ya Watenzi Wote (1968). Katika kazi hizi anajaribu kuonyesha kuwa haifai mwanamke anyanyaswe au kunyonywa na kugandamizwa na mwanamume. Yafaa – na kwa kweli ni lazima – apate haki na nafasi sawa na ya mwanamume katika nyanja zote za maisha kisiasa, kiutamaduni, na kiuchumi katika jamii. Hata katika Utenzi wa Hati Shaaban Robert anasisitiza kuhusu umuhimu wa kujitegemca na kujiendeleza kwa mwanamke ili asibaki jikoni na kitandani tu.
Katika diwani hii ya Ashiki Kitabu Hiki mashairi yaliyomshughulikia mwanamke ni kama vile “Sijui” (uk. 5), “Nani Atakutendea” (uk. 13). “Kuoa” (uk. 18-22), “Maango” (uk. 22-24) na “Mwanamke” (uk. 32-33).
Katika shairi la “Milango” (uk. 22-24) mshairi anamtetea mwanamke kwa kuonyesha vile ambavyo taasisi ya ndoa inampa nafasi duni. Anasema katika ubeti wa 3.
Quote:
Ndoa mlango wa tatu,
 
Mume humiliki vitu,
 
Ila mke hawi mtu,
 
Huwa baa kwa kupoa
 
Taasisi hii katika jamii yenye maisha ya kimwinyi na kibepari humgeuza mwanamke knwa kitu kimojawapo kinachomilikiwa na mwanamume. Na haya yote hutokca ijapokuwa ni kweli kwamba mwanamke ndiye hasa chanzo kikuu cha uhai wa jamii kwani ndiye abebaye mimba na kuzaa – ndiye aliye na jukumu kubwa la kutimiliza jambo la kwanza kati ya matatu muhimu yaelezwayo na mshairi katika shairi la “Matatu Muhimu” (uk.42).
Katika jamii ambayo imezingwa na utamaduni wa kibepari unaoabudu pesa, kila kitu kinachowezckana kugeuzwa kuwa bidhaa ya kuuzika hufanywa hivyo. Mwanamke hali kadhalika huuzwa ama hulazimika kujiuza kama bidhaa zinginezo. Ndiyo sababu katika shairi la “Sijui” mwandishi anauliza:
Quote:
Bilashi msijivune
Quote:
Quote:
Nanyi ni makurumbesa
Quote:
Hamna jambo jingine
Quote:
Quote:
Ila kudai mapesa!
Quote:
Sijui mwauza nini
Quote:
Quote:
Hata mkataka pesa?
Quote:
Na kuwapasha madeni
Quote:
Quote:
Waume makubwa hasa?
Dhamira hii inajitokeza pia katika shairi “Mwanamke” hasa beti za 2 na 5:
Quote:
Mwanamume kinyozi,
 
Dada mimi simwezi,
 
Heri nipande ngazi,
 
Quote:
Quote:
Nende japo kwa Goa.
Quote:
Sinifanyie kelele,
 
Maneno mapesa mbele
 
Nikanunue mchele,
 
Quote:
Quote:
Huko nitakofikia.
Kwa hiyo mashairi mengi yamhusuyo mwanamke katika diwani hii si ya kumtetea hasa bali yanamwonyesha vile ambavyo katumbukia katika maisha ya kibepari yanayoifanya pesa kuwa kiungo pekee kati ya mtu na mtu. Kwa sababu dhamira hii ya fedha ina uzito wake, tuipe nafasi yake mahsusi katika mjadala wetu.
Athari za Pesa Katika Jamii
Mashairi yote katika diwani hii ambayo yameongelea kuhusu pesa yanatupa taswira ya maisha ya kibepari ya kuabudu fedha na kuzifanya kuwa Mungu pekee wa jamii.
Mashairi tuliyokwishayataja ya “Sijui” pamoja na ya “Nyumba za Ngoma” (uk. 12-13), na “Nani Atakutendea?” (uk. 13-14) yanaonyesha jinsi ambavyo imani hii juu ya pesa imeunda soko la kuuzia kila kitu. Ili kuonyesha kuwa si kwa wanawake tu bali pia kwa wanaume, mshairi kaweka beti mbili za mashairi mawili ambazo zina ushabihiano. Ubeti wa mwisho wa “Nyumba za Ngoma” unasema:
Quote:
Wana wake magunge,
 
Wamezidi pangapunge,
 
Heri tusiwahonge,
 
Wataka kutuibia.
 
Na ubeti wa mwisho wa shairi la “Nani Atakutendea?” nao unasema:
Quote:
Na wanaume magunge
 
Wamezidi pangapunge,
 
Kina dada tujitenge
 
Hasara itatujia.
 
Uhusiano huu wa kibiashara kati ya wanaume na wanawake ndio unaomfanya Shaaban Robert awaite “magunge” na “pangapunge.”
Shairi la “Fedha” (uk. 8 – 9) ni kielelezo dhahiri cha vile ambavyo fedha imeyatawala maisha ya jamii. Ubeti wa 4 unatoa muhtasari wa milki hiyo ya fedha:
Quote:
Fedha imevunja nguu,
 
Milima ikatambaa,
 
Fedha ni kitu kikuu,
 
Aliye nayo shujaa,
 
Hutiiwa na wajuu,
 
Wa chini wakaridhia.
 
Halafu mshairi anaendelea kutueleza jinsi ambavyo fedha zimeua utu wa watu, na kuwafanya watu wabaya walio nazo waheshimiwe:
Quote:
Mtu aliye nafedha,
 
Japo duni ni kubeli,
 
Asemafo lina ladha,
 
Neno lake ikibali,
 
Hazukiwi na bughudha,
 
Uongowe huwa kweli.
 
Hata hivyo baadaye mshairi anatueleza katika ubeti wa 8 kuwa athari za fedha zina ncha mbili: ncha moja huwafikisha watu jehanam, na ya pili huwapeleka peponi.
Shairi la “Simwezi” (uk. 24-25) hali kadhalika linashughulikia suala la athari za fedha na vile ambavyo huumba watu wenye tamaa nyingi, tamaa ishindayo hata ile ya fisi (ubeti wa 5).
Ndoa
Suala la ndoa nalo lilimshughulisha sana Shaaban Robert katika maisha yake ya uandishi. Katika riwaya za Utubora Mkulima na Siku ya Watenzi Wote, na pia katika mashairi yake mengi, Shaaban Robert ameiona ndoa kuwa ni wajibu kwa watu, mradi tu wanaooana wawe watu kufu. Ndiyo sababu hata katika ubeti wa 6 wa shairi la “Kuoa” (uk. 20) mshairi anatuambia:
Quote:
Kuoa mke si kufu,
Quote:
Quote:
Atakuliza machozi,
Quote:
Kwa mambo yake dhaifu,
Quote:
Quote:
Ukonde ubaki ngozi,
Quote:
Huwezi kumsarifu.
Quote:
Quote:
Cheo chako hakiwazi,
Quote:
Kwake kama upuuzi,
Quote:
Quote:
Yafahamu yasemwayo.
Hata hivyo tunagundua kwamba mawazo na falsafa ya mshairi huyu kuhusu ndoa si yale yale daima – uko wakati yanapingana. Kwa mfano, wakati anapopinga ujane na kusisitiza kuhusu umuhimu wa ndoa (tazama mashairi ya “Halali Kitu Akram,” “Situmii Shoka Ukucha Unapofaa” na “Mwezi Hauwi Jua”) bapohapo yapo mashairi ambayo yanaonyesha kuwa ndoa haina maana sana kwani furaha yake ni adimu sana kupatikana. Shairi la “Kuoa” (uk. 18-22) linaonyesha vile ambavyo ni vigumu kupata mke anayefaa ndoani; shairi la “Simwezi” na la “Milango” yanasisitiza jinsi ambavyo ni vigumu kuwa na ndoa yenye furaha. Kwa hiyo tunaelezwa katika ubeti wa kwanza wa “Milango” kwa mfano, kuwa ndoa ina matata na giza. Kwa ujumla mashairi haya yanasisitizajinsi ambavyo taasisi ya ndoa imeharibika. Ila mshairi haingii ndani zaidi kuchambua hasa chanzo na mzizi wa kuharibika huko.
Falsafa Kuhusu Maisha
Mashairi kadhaa katika diwani hii yanajishughulisha na suala la maana ya maisha. Shairi la “Nyuso Mbili” (uk. 1), kwa mfano, linasisitiza wazo kuwa maisha yana nyuso mbili na kwamba maisha lazima yana mwisho kwani “Maisha ni matembezi ya kukoma tasihili.” Kwa hiyo, katika shairi la “Kubadilishana Zamu” (uk. 30) umuhimu wa mabadiliko katika maisha umesisitizwa; na shairi hili linatuasa kuwa hakuna refu lisilo na ncha.
Shairi la “Maswali na Majibu” (uk. 14-18), linatukumbusha shairi lingine maarufu la mshairi huyu huyu liitwalo “Gharika” (linapatikana katika kitabu cha Masomo Yenye Adili).Nalo linaonyesha wasiwasi na machafuko yaliyoenea katika dunia. Katika ubeti wa 3 wa shairi la “Maswali na Majibu” kwa mfano, mshairi anasema:
Quote:
Dunia imetubana,
Quote:
Quote:
Imetuvika masombo.
Quote:
Tulikwenda kwa mapana,
Quote:
Quote:
Tukapiga watu fimbo,
Quote:
Ngoma ikivuma sana,
Quote:
Quote:
Ni kupasuka kiwambo,
Quote:
Roho vmejaa mambo,
Quote:
Quote:
Radha ziko wapi tena?
Malalamiko haya yanarudiwa kwa namna nyingine katika shairi la “Hai” ambamo mshairi anaomboleza kifo cha mwanae, ingawa hapa mshairi anaonyesha pia tumaini jema la faraja ya maisha baada ya kifo. Anasema kuwa japokuwa uhai ni kitu kidogo sana, lakini faraja ipo katika uhai uliopo “huko Ng’ambo hiyo.” Mawazo haya ni sawa na yale ayatoayo mwandishi huyuhuyu katika riwaya yake ya Siku ya Watenzi Wote – faraja yake yote iko juu ya siku ya ufufuo wakati watenzi wote watakapopangwa mbele ya Mola wao kupewa thawabu za matendo yao bora. Kwa Shaaban Robert tofauti baina ya masikini na matajiri zitaondolewa tu na Mwenyezi Murigu siku hiyo ya ufufuo. Utatuzi huu wa “kiutopia” ndio msingi mkubwa wa falsafa ya Shaaban Robert kuhusu maisha.
Hata hivyo, hii haimaanishi kuwa Shaaban Robert kakata tamaa kabisa kuhusu maisha ya hapa duniani. Bado yapo mashairi machache ambayo yanaonyesha kuwa maisha hapa duniani yana uzuri wake. Kwa mfano, shairi la “Dunia Njema” (uk. 28) linaeleza kuhusu uzuri wa maisha. Beti za 2 na 3 zinasisitiza jambo hilo:
Quote:
Dunia nzuri na mambo yake,
 
Yana fahari ya peke yake,
 
Juu sayari ni taa zake,
 
Quote:
Quote:
Chinijohari ardhi yake.
Quote:
Zulia lake nyasi kijani,
 
Na majiyake mvua mbinguni,
 
Kushuka kwake milele shani,
 
Sifa ni zake Mola Manani.
 
Kutetea Haki na Kupinga Uovu
Shaaban Robert alijishughulisha pia na masuala ya kisiasa ya kutetea haki na kupinga unyonyaji, unyanyasaji, na uovu mwingine wote. Katika kitabu chake cha Maisha Yangi na Baada ya Miaka Hamsini tunaona jinsi alivyokuwa anapinga ubaguzi wa rangi uliomfanya Mwafrika kudunishwa, kudharauliwa na kunyanyaswa kutokana na rangi yake. Hate riwaya zake za Kusadikika (1951) na Kufikirika (1951) kimsingi zinatetea haki na kupinga ukoloni.
Katika diwani hii pia yapo mashairi ambayo yanapinga dhuluma na uayonyaji, japokuwa si mengi. Shairi la “Nani Atakutendea” (uk. 13), japokuwa linaeleza mambo mengi mengineyo, hapohapo linapinga unyonyaji wa mtu kufanyishwa kazi bila kupewa malipo:
Quote:
Kazi bila manufaa,
 
Nani atakutendea
 
Sinifanyie hadaa,
 
Kungwi hakuniusia.
 
Sinifanye hamaki,
 
Shetani wangu hataki,
 
Sharti unipe haki,
 
Ndipo ataputulia.
 
Hata hivyo ni shairi la mwisho katika diwani hii, shairi la “Shukrani,” ndilo linaloiongelea dhamira ya vita baina ya uovu na wema kwa kirefu raidi ya mengine. Shairi hili ni la chereko chereko na lelemama za kupatikana kwa uhuru wa Tanganyika. Katika kuupokea uhuru huo mshairi anaturudisha ayuma na kutueleza madhambi ya ukoloni mkongwe. Anatueleza jinsi ambavyo wakulima wanatoka jasho kwa faida ya watu wengine. Anasema katika ubeti wa 2 na wa 3:
Quote:
Kulima na kuchimbua halivunji mapatano,
 
Hasa tukikumbukia mapito mazito mno:
 
Na kulima kwa beluwa hali si yetu mavuno,
 
Wala halikuwa neno kwa wenye kututumia.
 
Kwa wenye kututumia hatukuwa na maneno,
 
Mchana kutwa wa jua katika ngwe ya mbono;
 
Kwa jazila ilikuwa ujira senti tano!
 
Hapakuwa na miguno yote yalivuniliwa.
 
Shairi hili pia linaonyesha jiasi ambavyo hali hiyo iliathiri hata mahusiano baina ya mke na mume (ubeti wa 4) kukawa na kutoelewana na kutotoshelezana kati yao. Twaelezwa vilevile kwamba, wananchi walizidi kukondeana kwa kutumikishwa katika mashamba ya mbono, ngano, katani, miwa, na kadhalika; mazao ambayo yote yalisafirishwa na kuyanufaisha mataifa ya nje.
Shaaban Robert, basi, anashangilia kupatikana kwa huo uhuru ambao anasema umefutilia mbali unyonyaji na unyanyaswaji huo. Kwa hiyo anamshukuru Mungu kwa huo uhuru; na baada ya napo anaishukuru Uingereza kwa kuikirimia Tanzania. Wakati ambapo ni rahisi kuelewa kwa nini Shaaban Robert anamshukuru Mungu hasa tukijua kuhusu maisha na malezi ya kidini aliyoyapata mshairi huyu, inakuwa vigumu kuzikubali shukrani azitoazo kwa Waingereza katika ubeti wa mwisho. Waingereza hawakukaribishwa na Watanganyika waje kututawala. Walitawala kwa nguvu; ndio wao waliowalimisha na kuwanyanyasa wananchi. Badala ya kuwashukuru dhalimu hawa ingefaa walaumiwe kwa ukoloni wao! Hapa basi, msimamo wa mshairi kuhusu suala la uhusiano baina ya mkoloni na mtawaliwa kuwanyenyekea wakoloni unatetereka.
Dhamira Zinginezo
Zaidi ya dhamira kuu tulizokwishachunguza, diwani hu imeshughulikia dhamira nyinginc ndogondogo kama furaha (“Kama Mfaime,” uk. 10), bahati (“Bahati,” uk. 10), kweli (“Nyuso Mbili,” uk. 1), mahaba na mapenzi (“Nasadiki,” uk. 6, “Siwezi,” uk. 24; “Nyakati,” uk. 26); umalaya (“Nyumba za Ngoma,” uk. 12), na mcagineyo.
MATUMIZI YA VIPENGELE VYA FANI
Katika diwani hii, kama ilivyo katika diwani zinginezo za Shaaban Robert, mshairi ameonyesha ustadi wakc wa kutumia mitindo mbalimbali ya ushairi.
Wakati ambapo waumini wa ushairi wa kimapokco wameviita vigezo vya mizani kumi na sita na vina kuwa ndivyo roho ya ushairi wa Kiswahili, Shaaban Robert amepevuka zaidi kwani katuonyesha kuwa si vizuri mshairi atawaliwe na muundo ule ule mmoja daima.
Katika diwani hii mshairi kaandika mashairi ya mizani minne hadi ishirini. Shairi la “Ni Wapuzi”‘ (uk. 27), kwa nafano, ni la mizani minne tu, na la “Nani Atakutendea” (uk. 13-14) ni la mizani 8, wakati ambapo yako ya mizani 12, 16 na kadhalika.
Kuhusu vina, mashairi mengi humu yamefuatia muundo wa vina wa ab/ab/ab/ab, Muundo huu unamaanisha kuwa vina vya kati vya kila mstari vinafanana katika kiia ubeti, na vya mwisho hali kadhalika. Muundo huu wa vina pamoja na ule wa ab/ba/ab/ba mara nyingi huonekana katika mashairi ya tarbia (au ya unne). Hapo hapa upo muundo wa kufuata jozi za vina ambapo mistari miwili ya kwanza ina vina vyake tofauti na vile vya mistari miwili ya mwisho ya ubeti. Hapa tunapata muundo wa ab/ab/cd/cd.
Pamoja na wingi wa miundo ya vina pia upo ule wa jumla ya mistari ya kila ubeti wa mashairi mbalimbali. Hapa pia ni rahisi kwa msomaji kuainisha mashairi tangu ya uwili hadi yale ya mistari ishirini kwa kila ubeti. Ila yatubidi tu tuelewe kuwa wingi au uchache wa naistari iundayo beti hutegemea jambo linaloongelewa. Wazo dogo tu hupewa mistari michache itakayolifanya liweze kunasa akilini mwa msomaji haraka. Jambo linalohitaji maelezo marefu hupewa mistari mingi, tena mirefu, na aghalabu huwa na beti nyingi zaidi ya zile za mawazo madogo madogo.
Matumizi ya taswira na ya misemo mbalimbali iliyoundwa ndani ya methali na nahau yamesaidia sana katika kuleta uzito wa mawazo yatolewayo. Shairi la “Mnyomele” (uk. 5) ni mfano wa fumbo lililofichika vizuri sana kutokana na matumizi yake ya taswira iniayowakilisha kitu kingine kabisa maishani.
Mshairi pia katumia taswira za maumbile kutoa maudhui ya mashairi yake. Kwa mfano tukiangalia shairi la “Dunia Njema” (uk. 28) tunaona vile ambavyo maumbile yamepewa jina la zulia. Twaiona dunia kuwa kama jengo zuri linalowahifadhi watu.
Katika shairi la “Nyakati” (uk. 26) mshairi katumia taswira ihusuyo fuajira na vile ambavyo lazima yanabadilika, halafu akatumia ustadi wa kulinganisha na kulinganua kwa kutumia tabaini kwa kila jambo. L’fundi huu umefaulu kumdanganya msomaji hadi sehemu ya mwisho ya ubeti wa mwisho ambapo ndipo ukweli kuwa shairi linaongelea mapenzi hujitokeza.
Mashairi mengi ya malumbano ama hutumia taswira nzito nzito au lugha ya kimafumbomafumbo ya kimethali. Mfano ni shairi la “Nazi” (uk. 7′) linavyodai kuwa kamwe nazi haiwezi kuvunja jiwe; au lile la “Silumii Shoka Ukucha Unapofaa” (uk. 37-39) ambalo moja kwa moja linafaulu kuwanyamazisha wapinzani kwa kuwafanya wajisikie wadogo wasiofaa mbele ya mshairi huyu. Katika fungu hili tunaweza kuyaweka pia mashairi ya “Wapinzi” (uk. 3), “Ngozi ya Simba” (uk. 3-5), Mwezi Hauwi Jua” (uk. 39-40), na kadhalika.
Shairi la “Halali Kuca” twaweza kulichukua kuwa mfano mzuri wa matumizi ya lugha ya kinahau. Ndoa imeitwa kuwa ni “Nyama ya mafuta.” Ilivyo, nyama ya mafuta ni nono inayotamaniwa na watu wengi. Mfano huu unaifanya ndoa ionekane kitu bora sana ikilinganishwa na ujane.
Matumizi ya aina hii ya lugha, ishara na taswira, pamoja na upana ws miundo ya vina na mizani katika ushairi wa Shaaban Robert, ndivyo vigezo vilivyosaidia sana kuvafanya maudhui ya mashairi yake yaeleweke vizuri, na kuyafanya mashairi yake kwa jumla yapendwe sana na yampe sifa ya shaha wa malenga.
Maswali
1. Zijadili dhamira muhimu ambazo zimeibuka katika Ashiki Kitabu Hiki. Je, mwandishi kafaulu au kashindwa vipi kuzichambua dhamira hizo?
2. Jadili msimamo wa Shaaban Robert kuhusu wanawake kama ujitokezavyo katika Ashiki Kitabu Hiki.
3. Taswira ya athari za maisha ya kibepari inajitokezaje katika Ashiki Kitabu Hiki?
4. Zijadili falsafa za mwandishi kuhusu ndoa na maisha kama zijitokezavyo katika Ashiki Kitabu Hiki.
5. Yajadili matumizi ya vipengee vifuatavyovya fani kama yalivyojitokeza katika Ashiki Kitabu Hiki:
Quote:
a) vina na mizani
b) mistari
c) matumizi ya picha (taswira)
d) lughakwajumla
e) ishara.

Print this item

  MBINU ZA USAWIRI WA WAHUSIKA WA FASIHI
Posted by: MwlMaeda - 12-28-2021, 09:44 AM - Forum: Uhakiki wa kazi za fasihi - No Replies

Mbinu za Ujenzi wa Wahusika na Usawiri wa Sifa Zao: Uhakiki wa Riwaya ya Dunia Uwanja Wa Fujo ya E. Kezilahabi
 Leonard Flavian Ilomo


Ikisiri

Kipengele cha wahusika ni muhimu katika kuunda kazi yoyote ya kifasihi. Kipengele hiki hushirikiana

na vipengele vingine vya kifani katika kutoa maudhui ya kazi yoyote ya kifasihi. Kwa kawaida

wahusika hujengwa kisanaa na mwandishi ili waweze kuwakilisha dhana mbalimbali za maisha katika

jamii (Msokile 1992). Mwandishi huwajenga wahusika wake kwa kutumia mbinu mbalimbali ili

kuwatofautisha na hivyo kuiwezesha hadhira yake kutambua sifa au tabia za mhusika fulani

zinazomtofautisha na mhusika mwingine katika kazi husika. Hata hivyo, ni vema ifahamike kuwa kila

msanii wa kazi ya kifasihi ana mbinu zake za kuwajenga wahusika wake. Hii ina maana kuwa, msanii

wa kazi ya kifasihi anaweza kutumia mbinu moja au zaidi katika kazi fulani kutegemeana na aina ya

utanzu anaoushughulikia. Kwa kutambua hoja hiyo, makala haya yanafafanua mbinu mbalimbali

zilizotumiwa na E. Kezilahabi katika kuwajenga wahusika katika riwaya ya Dunia Uwanja wa Fujo na

mchango wa kila mbinu katika kubaini sifa za wahusika pamoja na dhamira katika kazi hiyo.Makala

hii imegawanyika katika sehemu nne. Sehemu ya kwanza ni utangulizi unaotoa muhtasari kuhusu

riwaya ya Dunia Uwanja wa Fujo; sehemu ya pili inazungumzia dhana ya wahusika katika fasihi;

sehemu ya tatu inajadili mbinu mbalimbali zinazotumika kuwajenga wahusika na jinsi sifa za wahusika

zinavyosawiriwa kupitia mbinu hizo; na sehemu ya nne ni hitimisho la mjadala katika makala hii.

 Utangulizi
Kuna tahakiki na maelezo mbalimbali kuhusu riwaya ya Kezilahabi, Dunia Uwanja
wa Fujo. Tahakiki hizo zimefanywa na wahakiki mbalimbali wa fasihi huku kila
mmoja akiwa na mwelekeo wake kutegemea lengo la mhakiki husika. Suala hili pia
analigusia Mlacha (1991) kuwa, uchunguzi wa riwaya unaweza kufanywa kwa
kuzingatia vipengele tofautitofauti kwa kutegemea kile ambacho mhakiki anakusudia
kukichunguza. Miongoni mwa wahakiki hao ni Senkoro (1982, 2011), Mulokozi
(1983), Wamitila (1997), Wafula (2002) na Diegner (2002).
Senkoro (1982, 2011) na Mulokozi (1983), wanaihakiki riwaya ya Dunia Uwanja wa
Fujo kwa kujikita zaidi katika maudhui yake. Senkoro (keshatajwa) anafafanua kuwa,
riwaya hii inashughulikia migogoro, matatizo na mikinzano ya kijamii, kiuchumi na
kifalsafa katika jamii ya Tanzania baada ya kutangazwa kwa Azimio la Arusha.
Mulokozi (keshatajwa) anaenda mbali kidogo kwa kufafanua viwango ambavyo tatizo
la maisha katika riwaya hii linavyojadiliwa. Anavifafanua viwango hivyo kuwa ni
kiwango cha mtu binafsi na kiwango cha jamii. Wamitila (1997) katika makala yake
“Contemptus Mundi and Carpe Diem Motifs in Kezilahabi’s Works” anaielezea
riwaya ya Dunia Uwanja wa Fujo kuwa ni mfano bora wa motifu ya dunia kama
mahali pabaya pa kuishi na kuwa kuanzia mwanzo mwandishi anachora picha ya
ulimwengu ulio duni na usioaminika: sehemu yenye fujo ambapo utu unafifia katika mateso. Ubaya wa ulimwengu kama inavyooneshwa katika riwaya hii unatokana na
uzinzi, unyonyaji, ukahaba, kushushwa thamani kwa asasi ya ndoa, maamuzi
yasiyozingatia maoni ya wengine, dharau na visasi.
Kwa jumla tunapochunguza tahakiki hizo kuhusu riwaya ya Dunia Uwanja wa Fujo,
tunagundua kuwa zimejikita zaidi katika kuchunguza maudhui. Suala hili linajitokeza
si katika riwaya hii tu, bali linajitokeza pia katika tahakiki nyingi, hususan katika
taaluma ya fasihi ya Kiswahili (Mohochi, 2000). Hivyo, katika makala haya
tunachunguza kipengele cha fani cha riwaya ya Dunia Uwanja wa Fujo, hususan
wahusika kwa kuangalia mbinu zilizotumika kuwasawiri na jinsi mbinu hizo
zinavyosaidia kuyaelewa maudhui.
Dhana ya Wahusika
Wahusika wana umuhimu mkubwa katika kuiunda simulizi ya kifasihi. Hii inatokana
na ukweli kuwa, wahusika huweza kuathiri simulizi inayosimuliwa, yaani wao ndio
hupeleka mbele matukio katika simulizi. Wahusika wanaelezwa kuwa ni sehemu
muhimu ya fani (Msokile, 1992; Njogu & Chimerah, 2008), na kwamba, wahusika ni
viumbe wa kisanaa wanaobuniwa kutokana na mazingira na malengo ya msimulizi.
Bal (1997) anaeleza kuwa, wahusika hushabihiana na watu kwa kuwa fasihi
huandikwa kwa ajili ya watu na kwa hiyo huwahusu watu hao. Kwa kawaida
wahusika si watu halisi, bali ni matokeo ya ubunifu wa msanii ili kuakisi masuala
kadhaa ya kijamii ambayo msanii ameyakusudia. Kuhusu hili Bal (khj: 115) anasema:
“They are fabricated creatures made up from fantasy, imitation, memory: paper
people, without flesh and blood…The character is not a human being, but it
resembles one. It has no real psyche, personality, ideology or competence to act but
it does possess characteristics which make psychological and ideological
description possible”.
 
Wahusika ni viumbe wa kubuni wanaotokana na fantasia, mwigo, na kumbukumbu:
ni watu bandia wasio na damu na nyama…Mhusika si binadamu lakini anafanana
na binadamu. Hana akili, haiba, itikadi wala uwezo wa kutenda bali ana sifa
zinazotuwezesha kumtolea maelezo ya kisaikolojia na kiitikadi (Tafsiri Yetu).
Katika maelezo hayo, kinachojidhihirisha ni kukosekana akili, haiba, itikadi, na
uwezo wa kutenda kwa wahusika hali inayowafanya kuwa viumbe wa kubuni; yaani,
wanaotokana na ubunifu wa msanii ambaye huwaumba kufuatana na malengo yake.
Maelezo haya yanaungwa mkono na Mohamed (1995:72) anayesema, “mwandishi
anapoumba wahusika wake anaumba watu wasioishi katika ulimwengu wetu wa
bayana, bali wenye kuishi katika ulimwengu wao wa hadithi au tamthilia ambamo
wakitolewa watakuwa hawana maisha…”
Madumulla (2009) akiwarejelea Kasper na Wuckel (1982) anaeleza kuwa, mhusika ni
picha ambayo huchorwa na fasihi na ni kiini cha vitu vyote vipya, dhamira na mada
katika fasihi. Anaendelea kueleza kuwa, katika mhusika kuna uwili: mosi, kuna
usawiri wa kisanaa wa mtu kwa upande mmoja; pili kuna sura ya mtu kwa upande
mwingine. Ufafanuzi huu unashadidia hoja tuliyoitoa hapo awali kuwa, wahusika si
watu halisi bali watu wa kubuni. Ubunifu wa msanii humuwezesha msanii kuwaumba
au kuwasawiri wahusika kinafsia, kiakili, na kimwili. Usawiri wa wahusika
unaofanywa na msanii hutegemea mbinu mbalimbali ambazo msanii huyo
amezitumia. Kwa kuzingatia kauli hiyo, katika kipengele kinachofuata tumebainisha
mbinu mbalimbali ambazo msimulizi-mwandishi amezitumia katika kuwajenga
wahusika wa simulizi yake ya Dunia Uwanja wa Fujo. Mbinu hizo ni matendo,
mazingira, matamshi, uzungumzinafsiya, mazungumzo baina ya wahusika, na
uwasilishaji dhahiri.
Mbinu za Ujenzi wa Wahusika
Mbinu ya Kimatendo
Hii ni miongoni mwa mbinu ambazo msimulizi-mwandishi amezitumia katika kuwajenga
wahusika wa simulizi yake. Kwa kawaida matendo ya mhusika yanaweza
kuainishwa katika makundi matatu kama asemavyo Rimmon-Kennan (2002) ambaye
ananukuliwa na Shen (2006). Makundi hayo ni: tendo linalotendwa na mhusika “act
of commission,” tendo ambalo mhusika anapaswa kulitenda lakini halitendi “act of
omission,” na tendo ambalo halijafanikiwa ingawa mhusika amekusudia kulifanya
“contemplated act.” Mbinu hii humfanya msimulizi atumie ufafanuzi kidogo huku
msimuliwaji akipewa nafasi kubwa ya kutafsiri maana na sifa au tabia ya mhusika
kutokana na matendo yake.
Msokile (1992:43) anaeleza kuwa, “msanii huwaunda
wahusika kwa kutoa matendo nusunusu, hatoi maelezo juu ya matendo yote kwa mara
moja.” Katika riwaya ya Dunia Uwanja wa Fujo, mbinu ya matendo imetumika katika
kuwajenga wahusika.
Tumaini ni miongoni mwa wahusika ambao wamejengwa kwa kutumia mbinu hii ya
matendo. Katika riwaya hii tunasimuliwa kuwa Tumaini alimtorosha Anastasia, binti
wa Mulele na mkewe Bukehele ili asiweze kuozwa kwa Tembo, mtu aliyekuwa mume
wa marehemu dada yake Anastasia. Tunasimuliwa kuwa, Tumaini alifanikiwa
kumtorosha na kwenda kuishi naye Shinyanga bila idhini ya wazazi wake Anastasia.
Kutokana na kitendo hiki tunaweza kumuelezea Tumaini kama mtu aliyekuwa hajali
taratibu za jamii yake na pia kitendo hiki kinadokeza mgogoro kati ya vijana na
wazee, mgogoro ambao ni matokeo ya vijana kujitafutia uhuru wao katika masuala
mbalimbali. Kitendo hiki cha Tumaini kumtorosha Anastasia kinaingia katika tendo
linalotendwa na mhusika kama inavyoelezwa na Shen (keshatajwa) ambaye anamnkuu Rimmon-Kenan. Kitendo hiki cha Tumaini kinajidhihirisha katika ukurasa
wa 48 wa riwaya hiyo kama ifuatavyo:
Anastasia alikuta Tumaini anafika kutoka mjini kupeleka vitu vyake. Tumaini
alimbeba Anastasia kwa baiskeli kuelekea Lutare. Njiani Tumaini alimweleza
Anastasia mpango aliokuwa nao. Anastasia alisikiliza kwa makini.
“Anastasia, unafahamu nimekuleta huku ngomani kwa sababu wazazi wako
hawataweza kuvumbua ni nani amekutorosha…”
Zaidi ya kitendo chake cha kumtorosha Anastasia, Tumaini alifanya kitendo cha
mauaji baada ya kumpiga kwa risasi mkuu wa wilaya aliyekuwa akihutubia mkutano
kuhusu ujamaa ambao Tumaini aliupinga. Tumaini alimpiga kwa risasi mkuu wa
wilaya baada ya mashamba yake kutaifishwa na kugeuzwa kuwa mali ya kijiji cha
ujamaa. Hiki ni kitendo ambacho kinamsawiri Tumaini kama muuaji na hivyo kuibua
dhamira ya mauaji. Hili linajitokeza ukurasa wa 128 ambapo tunasimuliwa:
Kelele za watu zilikuwa hazijatulia mlio wa bunduki uliposikika. Hapo hapo Mkuu
wa Wilaya alitotoma chini akaanguka. Mlio wa pili ulisikika pale pale. Tumaini
ambaye alikuwa akijaribu kutoroka alianguka chini. Watu wakasambaa ovyo huko na
huko kwa mbio. Kila mtu akajua roho yake. Uwanja wa mpira ukawa mdogo; mlango
ukawa hauonekani, na ukuta ukawa mfupi.
Katika dondoo hilo tunaona Tumaini akijaribu kutoroka baada ya kumpiga Mkuu wa
Wilaya kwa risasi, kitendo ambacho kinamfanya akamatwe na baadaye kuhukumiwa
kunyongwa. Pia, kitendo cha Tumaini kutozingatia ushauri wa mama yake, ushauri
uliomtaka kutafuta mchumba kwa kuzingatia tabia njema na kisha kuoa kinamsawiri
Tumaini kama mtu mkaidi, na pia kinaibua dhamira ya kiburi na umalaya. Katika
riwaya hii tunasimuliwa kuwa, badala ya kutafuta mchumba na kuoa, Tumaini
alijishughulisha zaidi na kutembea na wasichana tofauti tofauti pale kijijini kama
inavyosimuliwa katika ukurasa wa 17 kuwa:
Wasichana wengi kijijini walimpenda. Siyo kwa sababu alikuwa na pesa lakini kwa
sababu walimwona ni mwenzao: Tumaini hakuwa na kazi ya ofisini. Kwa hiyo
aliweza kuwaoa. Kule tu kutaja jina lake kulimfanya kila msichana kijijini awe na
tumaini la kuolewa naye.
Mama Resi ni mhusika mwingine ambaye amesawiriwa na msimulizi-mwandishi kwa
kutumia mbinu hii ya matendo. Kitendo kimojawapo ambacho alikifanya mhusika
huyu ni kile cha kukataa kushuka kwenye basi, ‘Tanganyika Bus,’ ili abiria wengine
wasukume basi hilo lililokuwa limekwama matopeni. Kitendo hiki cha kukataa
kushuka kwenye basi kinamsawiri mhusika huyu kama mtu mwenye kiburi na dharau.
Katika ukurasa wa 57 msimulizi-mwandishi anatusimulia:
Zilikuwa zimebaki maili arubaini kufika Shinyanga basi lilipokwama matopeni.
Watu wote waliombwa kutoka nje abaki dereva ndani peke yake. Watu wote
walitoka nje lakini yule mama na mtoto wake alikataa kutoka nje.
Kitendo hiki cha Mama Resi kinasawiri sifa ya kiburi aliyokuwa nayo mhusika huyo
na pia kinaibua dhamira ya ukaidi. Aidha, katika ukurasa wa 70 tunaona msimulizimwandishi
anaendelea kutumia mbinu ya kimatendo kumsawiri Mama Resi. Katika
ukurasa huo tunaelezwa matendo ya Mama Resi ya kuwa anaosha vyombo nusu saa
kabla ya kula. Tunasimuliwa kuwa:
Ukifika nyumbani kwa Dennis hukosi kukuta vyombo vimewekwa nje bila
kuoshwa. Kwa Dennis vyombo huoshwa nusu saa kabla ya kula hata vyombo
vilivyotumika usiku.
Kitendo hicho cha kuacha kuosha vyombo kwa muda mrefu, zaidi ya kumsawiri
Mama Resi kama mtu mvivu na mzembe, pia kinasaidia kuibua dhamira ya uvivu na
uzembe miongoni mwa wanajamii. Aidha, kupitia mpango ambao Mama Resi
alishiriki kuuandaa, mpango wa kumuua Tumaini kwa sababu tu ya kutopenda
maendeleo yake, unamsawiri Mama Resi kuwa mtu mwenye wivu, roho mbaya na
mwuaji. Pia, kitendo hicho cha Mama Resi kinaibua dhamira ya wivu na mauaji. Hata
hivyo, tunasimuliwa kuwa mpango wa kumuua Tumaini ulishindikana baada ya
washiriki wa mpango huo kutoelewana. Kitendo hiki kinaingia katika ile aina ya
tendo ambalo mhusika anakusudia kulitekeleza lakini linashindikana kutekelezwa.
“Tukishatenda jambo lazima tulitimize. Hatuwezi kuacha mambo nusu nusu.
Angalieni sasa tumo matatizoni. Huenda tukanyongwa au kufungwa maisha!”
Mama Resi alisema maneno hayo kwa kelele. Alitoa shilingi mia tano na kuzitupa
chini. “Bwana Makoroboi! Chukua hizo pesa. Mimi nataka uniletee kichwa chake!”
(ukurasa wa 88).
Katika maelezo ya dondoo hilo tunaona Mama Resi akinung’unika baada ya mpango
wao wa kumuua Tumaini kushindikana.
Mbinu ya Matamshi
Katika mbinu hii msimulizi huwajenga wahusika kwa kuwafanya wazungumze ili
lafudhi zao ziweze kuwabainisha. Kwa mfano, katika simulizi fulani msimulizimwandishi
anaweza kumjenga mhusika wake kwa kumfanya azungumze kwa lafudhi
ambayo ni tofauti na wahusika wengine ili kumtofautisha na wahusika wengine.
Lafudhi itakayosikika kutoka kwa mhusika huyo huweza kusawiri usuli wake na
kuibua dhamira fulani.
Katika riwaya ya Dunia Uwanja wa Fujo mbinu hii imetumika katika kumjenga
Kasala ambaye anaonekana kuongea Kiswahili ambacho kimeathiriwa na lugha yake
ya asili. Katika ukurasa wa 5 msimulizi-mwandishi anatusimulia:
Polisi walipokuja walimkuta ameinama kichwa, damu ikimtoka puani.
“Mzee! Umekuwaje!” walimwuliza.
“Batoto bamenisondogorasondogora na chichwa! Bengine bamenikorotorakorotora
na kucha!” alijibu kwa Kiswahili alichokuwa anazungumza siku zile.
“Walikupiga kwa hedi labda?”
“Hapana na chichwa!”
“Na ngumi na makofi!”
“Ndiyo balikuwa kumi na kofia!’’
Katika mazungumzo hayo inabainika wazi kuwa matamshi ya Kasala, yaani jinsi
alivyokuwa akitamka maneno yake, na wale polisi yalikuwa tofauti. Kwa mfano,
dondoo hilo linaonesha neno ‘kichwa’ lilitamkwa kama ‘chichwa’, ‘walikuwa’
lilitamka kama ‘balikuwa’ na kadhalika. Zaidi ya matamshi inaonekana Kasala
alishindwa kuelewa maana ya neno ‘ngumi’ kwa kudhani ni ‘kumi’, na ‘makofi’ kwa
kudhani ni ‘kofia’. Kwa hiyo, kutokana na matamshi yake Kasala anasawiriwa kama
mtu aliyekuwa hajui lugha ya Kiswahili vizuri. Zaidi ya kumsawiri kama mtu
aliyekuwa hajui Kiswahili vizuri, mbinu hii ya matamshi inasaidia kubainisha tofauti
za watu kijiografia na kuibua dhamira ya tofauti baina ya miji na vijiji. Matamshi ya
Kasala yanaibua dhamira hii kutokana na ukweli kuwa katika jamii za Kitanzania,
watu waishio vijijini matamshi yao ya lugha ya Kiswahili huwa yameathiriwa sana na
lugha za makabila tofauti na watu waishio katika miji ambako lugha za makabila
hazipewi nafasi kubwa katika mawasiliano ya kila siku.
Mbinu ya Kimazingira
Mbinu hii inajitokeza zaidi tunapozichunguza tabia mbalimbali za Tumaini ambazo ni
matokeo ya mazingira aliyoishi hapo awali. Katika ukurasa wa 11 tunasimuliwa:
Tumaini alikuwa kwa kutengwa. Alinunuliwa vijigari vidogo vingi; kila alicholilia
alipewa. Siku moja Tumaini alimchoma mlezi wake jichoni. Yule mvulana alimpiga
Tumaini kidogo. Tumaini alikimbia kwenda kushitaki kwa mama yake.
Kutokana na maelezo hayo tunapata picha nzima ya mazingira ambayo Tumaini
alilelewa. Tunaelezwa kuwa Tumaini alikulia katika mazingira ya kuengwa sana,
yaliyomfanya awe na tabia zisizokubalika. Ni kutokana na malezi hayo, Tumaini
alijenga dharau kwa watu wengine. Pia, tunasimuliwa kuwa, zaidi ya mazingira ya
kuengwa Tumaini alikulia katika mazingira ya uyatima baada ya wazazi wake
kufariki na ndugu zake kutokuwa tayari kuishi naye. Katika ukurasa wa 16
tunasimuliwa:
Baada ya kifo cha mama yake, Tumaini alikata shauri kuacha shule…Tumaini
alipoacha kusoma aliishi ndani ya nyumba ya baba yake. Marehemu baba yakealikuwa hakai ndani ya nyumba za serikali…Tumaini alirithi shilingi elfu hamsini.
Kwa sababu hii jamaa zake walikataa kuja kuishi naye.
Maelezo hayo yanaendelea kufafanua mazingira aliyokulia Tumaini, mazingira ya
uyatima ambayo yalimsababisha akose mwongozo katika maisha yake. Hali hii
ilimfanya Tumaini aishi kwa kujiongoza mwenyewe. Pamoja na mazingira magumu
aliyoishi, tunaelezwa kuwa Tumaini alipambana na mazingira hayo na hatimaye
alifanikiwa ingawa Azimio la Arusha lilimpotezea matumaini yake. Kwa hiyo,
kutokana na mazingira hayo matendo ya baadaye ya Tumaini yaliathiriwa sana. Kwa
mfano, mazingira ya kuengwa yalisababisha Tumaini aamini kuwa kila alichokifanya
kilikuwa ni sahihi na kwamba ilikuwa ni haki yake. Hali hii ilimfanya Tumaini kuwa
kiumbe aliyetenda kinyume na matarajio ya jamii iliyomzunguka kwa sababu ya
kiburi na dharau. Mbinu hii ya kimazingira, zaidi ya kumsawiri Tumaini kama yatima
pia inaibua dhamira ya malezi na umuhimu wa wazazi.
Mbinu ya Uzungumzinafsiya
Wamitila (2008:379) anaifafanua mbinu hii kuwa ni “mtindo wa kuyawasilisha
mawazo ya mhusika kwa mtindo au njia ya kujizungumzia.” Anaendelea kueleza
kuwa, “katika uchunguzi wa dhana hii tunaweza kubainisha kati ya aina kuu mbili: (a)
uzungumzinafsiya wa moja kwa moja, na (b) uzungumzinafsiya usio wa moja kwa
moja…” Kutokana na maelezo hayo tunaweza kueleza kuwa, uzungumzinafsiya
unahusu monolojia, yaani mhusika anajizungumzia peke yake. Kutokana na
kujizungumzia huko, wasimuliwaji hupata fursa ya kufahamu kile kinachoendelea
katika akili ya mhusika, kwa hivyo wasimuliwaji huweza kubaini sifa au tabia za
mhusika huyo pamoja na maudhui yanayoibuliwa.
Katika riwaya ya Dunia Uwanja wa Fujo mbinu hii imetumiwa na msimulizimwandishi
katika kuwajenga baadhi ya wahusika wake. Miongoni mwa wahusika
wanaojengwa kwa mbinu hii ni Mugala. Huyu alikuwa mama yake Kasala ambaye
alihamishiwa kisiwani kutokana na kuhisiwa kuwa alikuwa mchawi. Msimulizimwandishi
anatumia mbinu hii katika kumsawiri Mugala katika ukurasa wa 19
anasema:
Tumaini alipofika mbali sana, Mugala alianza kucheka hali akizungumza polepole.
Sasa ilikuwa zamu yake kumcheka mwenziwe.
“Samaki amejileta mwenyewe ndani ya chungu. Kenge akikosa chakula huachama;
nzi wakiona mdomo wake mwekundu hufikiri ni nyama na kuingia kwa wingi.
Akiona wamekuwa wengi hufunga mdomo na kuwatafuna. Nimekwishakata shauri
kuumaliza ukoo wao. Na nitaumaliza. Lakini, huyu mtoto ni mzuri vile kwamba
nimemwonea huruma. Oh! Ninakumbuka katika kazi yetu huruma ni kosa kubwa sana. Siku ile niliyoapa msituni, kwa kuuma kidole gumba, kwamba sitamhurumia
mtu yeyote bado naikumbuka. Kwa hiyo nitamchukua mtoto huyu. Lakini hakuna
haraka. Nitamwacha kwa muda afanye mapenzi yake na Leonila.”
Katika dondoo hilo tunamwona Mugala akijizungumzia peke yake baada ya Tumaini
kuondoka. Huu ni uzungumzinafsiya wa moja kwa moja kutokana na mawazo ya
Mugala kuweza kubainika wazi bila kuingiliwa na mtunzi. Kutokana na
kujizungumzia huku, tunabaini kuwa Mugala ni muuaji tena asiye na huruma
kunatokana na kiapo alichokula msituni. Zaidi ya kumsawiri Mugala, mbinu hiyo
inaibua dhamira ya uchawi na ushirikina.
Tumaini ni mhusika mwingine ambaye amesawiriwa kwa kutumia mbinu hii ya
uzungumzinafsiya. Katika ukurasa wa 19 tunasimuliwa kuwa, akiwa njiani kutoka
katika mji wa Kasala kuonana na Mugala, Tumaini alisikia kama sauti ya ndege
akiimba. Hata hivyo, sauti hiyo haikuwa ya ndege bali ilikuwa sauti ya moyo wa
Tumaini. Katika ukurasa huo tunasimuliwa:
Akiwa njiani kurudi nyumbani, Tumaini alisikia sauti kama ya ndege akiimba kwa
huzuni: “Tumaini usidhani kwamba umefanya jambo zuri. Huyo mzee amekwisha
kuwa kama mtoto mdogo. Wewe umemchezea kama picha. Tumaini, hii ndiyo
heshima yako kwa watu kama hawa! Tumaini huna huruma; utakuja kuwa kama yeye
siku moja!”
Hiyo haikuwa sauti ya ndege. Sauti ya moyo wake ndiyo ilikuwa ikisumbua.
Tunapochunguza dondoo hilo tunabaini kuwa, Tumaini alikuwa akijizungumzia
nafsini mwake. Huu ni uzungumzinafsiya usio wa moja kwa moja kwa sababu sauti
inayosikika ni ya msimulizi nafsi ya pili. Uzungumzinafsiya huu unatuwezesha
kubaini sifa ya utovu wa nidhamu aliokuwa nao Tumaini na umuhimu wa kuheshimu
wazee. Ni kutokana na kugundua kuwa alimkosea Mugala, alianza kujuta yeye
mwenyewe.
Tumaini anaendelea kusawiriwa na mbinu hii katika ukurasa wa 32 ambapo
anaonekana akitafakari kitendo cha wanakijiji kumnyanyasa Mugala na hatimaye
kuhamishiwa katika kisiwa cha wachawi. Tukio hili linamfanya Tumaini atafakari
mwenendo mzima wa maisha yake na hatima yake pale kijijini. Katika ukurasa huo
tunasimuliwa:
Alipofika kitandani mawazo mengi yalimwingia kichwani. Alianza kufikiri.
“Nafikiri Mugala alikuwa mtu mwema, hasa kwangu. Alinisaidia kupata chakula
nilipokuwa nina njaa. Lakini kwa muda wa siku moja tu amechukiwa na kila mtu
kwa ajili ya matendo yake mabaya. Mtu ambaye ameshindwa kuishi na raia
amechoka maisha. Huu ni ukweli mtupu. Mugala alipigwa na watoto wadogo, alitemewa mate, lakini hata jamaa zake walimtazama tu. Kumbe raia wakikususa
unakuwa kama mnyama! Mimi je? Huenda labda watu wamekwishaanza
kunikasirikia kwa kuharibu binti zao! Kuna mambo mawili ninayoweza kufanya; au
nirekebishe mwenendo wangu na niendelee kuishi humuhumu kijijini; au nitoroke
niende nchi za mbali kabla mtumbwi haujatoboka…”
Katika dondoo hilo tunaona Tumaini akijizungumzia peke yake. Kujizungumzia huko
kunatokana na matendo aliyofanyiwa Mugala, matendo ambayo yanamfanya Tumaini
ajitathimini mwenendo wake na hatima yake pale kijijini. Kutokana na dondoo hilo
Tumaini anasawiriwa kama mtu aliyekuwa na uwezo wa kugundua hatari inayomnyemelea
na ambaye alikuwa akiujua ukweli lakini alikuwa akiupuuzia. Pia, kutokana
na kujizungumzia huko tunajuzwa umuhimu wa kuishi vizuri na watu. Zaidi ya
dondoo hilo, katika ukurasa wa 120 msimulizi-mwandishi anaendelea kumsawiri
Tumaini kwa kutumia mbinu hii. Katika ukurasa huo tunasimuliwa kuwa:
Alipokuwa akiosha vyombo, Tumaini alikuwa ameshindwa kupata usingizi. Alikuwa
sasa akizungukazunguka humo chumbani. Mawazo haya yalikuwa yakimzunguka
kichwani
“Siwezi kutukanwa na mwanasiasa anayetegemea kura yangu! Haiwezekani! Mimi
sikumkataza kunenepa! Na hata hivyo ninakula jasho langu. Tabu niliyoipata zamani
imenifunza kutafuta pesa. Nilikata shauri kufanya kazi; nikawa nashinda shambani
asubuhi na jioni. Na sasa nimepata mali. Halafu huyu mwanasiasa ananiita
mnyonyaji! Mali niliyosumbukia mwenyewe wakati watu wengine walikuwa
wakishinda kwenye kangara! Haiwezekani! Potelea mbali vijiji vyao vya ujamaa
ambavyo vimerudisha nyuma maendeleo ya watu wengi. Haiwezekani!”
Katika dondoo hii msimulizi-mwandishi anamchora Tumaini akijizungumzia. Katika
kujizungumzia huko, Tumaini anatuwezesha kutambua msimamo wake kuhusu sera
ya vijiji vya ujamaa ambavyo vilikuwa ni matokeo ya Azimio la Arusha. Hivyo,
mbinu hii inamjenga au kumsawiri Tumaini kama mtu aliyekuwa akipinga sera ya
vijiji vya ujamaa kwa sababu aliamini kuwa vijiji hivyo vilikuwa vikirudisha nyuma
maendeleo. Zaidi ya kumsawiri Tumaini, mbinu hii inaibua dhamira ya suala la
upokezi wa Azimio la Arusha miongoni mwa Watanzania. Katika dondoo hilo
inaonekana kuwa Azimio la Arusha lilikumbana na upinzani wa wanajamii kama
anavyofafanua Senkoro (2011:88), “kwa wakulima, kwa vile hawa ni tabaka lililo
gumu sana katika kubadili wenendo wake na kaida zake za maisha; ilikuwa vigumu
kwao kulipokea Azimio kwa urahisi.”
Mbinu ya Mazungumzo baina ya Wahusika
Mbinu hii imetumika kwa kiasi kikubwa katika riwaya ya Dunia Uwanja wa Fujo,
ambapo msimulizi-mwandishi amewapambanisha wahusika ili wazungumze wao kwa wao. Msokile (keshatajwa:44) anaeleza, “kadiri wanavyoendelea, wazo la mhusika
pamoja na tabia yake hujulikana taratibu katika kazi hiyo.” Katika riwaya hiyo,
wahusika mbalimbali wamejengwa au wamesawiriwa kwa kutumia mbinu hii.
Miongoni mwa wahusika hao ni Mama Resi na Tumaini. Katika riwaya hiyo,
msimulizi-mwandishi amewapambanisha wahusika hawa katika sehemu mbalimbali
za simulizi yake. Kwa mfano, katika ukurasa wa 71 Tumaini anaoneka akizungumza
na Mama Resi kama ifuatavyo:
“Imekwendaje hata ukaoa msichana ambaye hakusoma?”
“Ni mapenzi tu, Mama Resi.”
“Mapenzi gani hayo! Mimi ninafahamu kwa nini umemwoa. Umemwoa ili uweze
kumwonea. Unataka mwanamke ambaye unaweza kumwamrisha kama mtoto mdogo,
karibu kama mtumwa.”
“Wewe na Dennis mko sawa?”
“Mimi na bwana wangu tunaamini katika jambo hili usawa. Hata mimi ninaweza
kutoa maoni yangu mbele ya bwana wangu…”
“Mama Resi, jambo la usawa linakuharibu mawazo yako bure. Jambo la maana katika
jamii yoyote ni heshima. Bwana na mke, hata kama wanajidai kwamba wao ni sawa,
wasipopeana heshima jamii yao haitakuwa thabiti kamwe.”
Katika dondoo hilo tunaona Tumaini akipambanishwa na Mama Resi katika
mazungumzo. Ni katika mazungumzo hayo ndipo tunapogundua mitazamo ya
wahusika hawa kuhusu usawa kati ya mwanamume na mwanamke. Kupitia mazungumzo
hayo msimulizi-mwandishi anawasawiri wahusika hawa kuwa ni watu
waliokuwa wakitofautiana kimtazamo na kifikra. Wakati Tumaini anasawiriwa kama
mtu aliyekuwa akiamini katika heshima; Mama Resi anasawiriwa kama mtu
aliyekuwa akiamini katika haki na usawa wa kijinsia. Usawa huo anaouamini Mama
Resi, kwa Tumaini ulikuwa ni usawa uliojikita katika mtazamo wa Kizungu wakati
kwa mtazamo wa Kiafrika usawa ni wa kuheshimiana (ukurasa wa 72). Kutokana na
mazungumzo hayo, pia inaibuliwa dhamira ya Uafrika dhidi ya Umagharibi. Katika
dhamira hii tunaelezwa kuwa kwa mtazamo wa Kiafrika heshima ni jambo la msingi
wakati kwa mtazamo wa Kimagharibi usawa wa kijinsia ndio jambo la msingi bila
kujali iwapo usawa huo unazingatia utu.
Pia, mbinu hii imetumika kuwapambanisha Tumaini na Dennis katika mazungumzo
yao. Kupitia mazungumzo yao (ukurasa wa 63-64) tunabaini mtazamo wa kila
mhusika kuhusu maisha. Katika ukurasa wa 63 Tumaini anasawiriwa kama mtu
aliyeamini kuwa, ulimwengu hauwezi kuwa na taabu kama mtu ana pesa, nyumba, na
gari. Wakati Tumaini akisawiriwa hivyo, Dennis anasawiriwa kama mtu aliyeamini
kuwa furaha ya mwanadamu haiwezi kuletwa na vitu kama nyumba hasa ukizingatia
kuwa “nyumba za binadamu zinaonesha upungufu wa uhuru alionao” (ukurasa wa
64). Kutoka na mbinu hii ya mazungumzo tunaweza kubaini ujumbe ambaomsimulizi-mwandishi anataka tuupate. Mathalani, katika ukurasa wa 64 tunaelezwa
kupitia Dennis kuwa furaha katika maisha hailetwi na wingi wa vitu ambavyo mtu
anavimiliki.
Aidha, Leonila na Anastasia wamepambanishwa ili kubainisha uhusiano wao. Katika
riwaya hiyo inaonekana Leonila na Anastasia walikuwa marafiki kabla ya
kuhitilafiana kutokana na wote kumuhitaji Tumaini. Kuhitilafiana huko kunasawiriwa
kwa kutumia mazungumzo yao katika ukurasa wa 25-26:
“Vipi dada; mbona hivi!”
 “Mimi sikuelewi,” Anastasia alijibu.
 “Mbona umenipindulia serikali yangu!”
 “Nani amekwambia!”
 “Nimesikia kwamba kitanda cha bwana wangu siku hizi kimekuwa chako!”
 “Sikufahamu kama alikuwa amekwisha toa mahari! Tangu lini dada yangu, huyu
akawa bwana wako?”
“Hufahamu kwamba ninamtunzia mtoto wake!”
 “Samahani dada yangu, yeye mwenyewe aliniambia kwamba amekwisha kupiga
chaki.”
 “Umesema nini? Sema tena nisikie!”
Katika dondoo hilo Leonila na Anastasia wanachorwa wakiwa wanazungumza.
Wahusika hawa wanasawiriwa kama watu waliokuwa marafiki lakini baadaye walihitilafiana
kwa sababu ya kugombea mwanamume, Tumaini. Kupitia dondoo hilo,
uhusiano kati ya wahusika hawa unaonekana kubadilika kutoka ule wa kirafiki na
kuwa wa kiuadui. Hivyo, zaidi ya kusawiriwa kwa uhusiano baina ya Leonila na
Anastasia, pia unasawiriwa mgogoro wa kimapenzi uliopo baina ya wahusika hao.
Mbinu ya Uwasilishaji Dhahiri
 Mbinu hii inahusisha kutaja moja kwa moja na kwa uwazi sifa za mhusika fulani
katika matini husika. Hii ina maana kwamba sifa na matendo ya mhusika yanaelezwa
waziwazi na msimulizi. Mbinu hii ya kuwaumba wahusika husaidia kumfanya
msomaji asipate taabu katika kutambua wasifu wa ndani na wasifu wa nje wa
mhusika. Pia, mbinu hii humsaidia msomaji kutambua kiini cha kisa, wazo au
dhamira (Msokile, 1992:43).
Katika riwaya hii, mbinu ya uwasilishaji dhahiri imetumiwa na msimulizi-mwandishi
katika kuwajenga wahusika wake. Miongoni mwa wahusika waliojengwa kwa
kutumia mbinu hii ni Dennis. Katika riwaya hii tunaelezwa kwa uwazi kuwa, “Dennis
alikuwa kifungua mimba” (uk. 5), na “aliishi kwenye nyumba kubwa” (ukurasa wa
60). Maelezo haya kuhusu Dennis yanaonesha wazi kuwa mtu huyo alikuwa ni nani na aliishi maisha ya namna gani. Kwa mfano, tunaelezwa wazi kuwa Dennis aliishi
kwenye nyumba kubwa ya serikali; hali hii inamjenga Dennis kama mtu aliyekuwa na
unafuu wa maisha kuliko watu wengine.
Mhusika mwingine aliyejengwa kwa kutumia mbinu hii ni Mulele. Mhusika huyu
anaelezwa kama mtu ambaye “alikuwa akijishughulisha na kilimo” na ambaye
“alikuwa akiupinga ujamaa” (ukurasa wa 33). Zaidi anajengwa kama “mtu mkarimu”
(ukurasa wa 38) na ukarimu wake unaelezwa wazi kuwa alikuwa akitengeneza pombe
na kuwakaribisha jirani zake kunywa bila malipo. Kutokana na maelezo hayo,
tunaweza kumuelezea Mulele kama kiwakilishi cha watu ambao hawakuwa tayari
kuupokea ujamaa kwa sababu tayari wao walikuwa wakiishi kijamaa katika vijiji vyao
kwani walikuwa wakishirikiana katika masuala mbalimbali. Kutokana na kusawiriwa
huko, tunabaini dhamira ya ukarimu, na zaidi tunajuzwa kuwa ujamaa ni jadi ya
Waafrika.
Mhusika mwingine aliyesawiriwa kwa kutumia mbinu hii ni John, rafikiye Tumaini.
Katika ukurasa wa 47, msimulizi-mwandishi anamsawiri John kwa uwazi kuwa,
“aliacha shule alipofukuzwa baada ya kuwagomesha wenzake kula chakula,” na
“aliishi kama mhuni.” Kutokana kusawiriwa huko, kadiri simulizi inavyoendelea
tunaelezwa John akifanya matendo ambayo hayakubaliki kama vile, kufanya tendo la
ndoa na wake wa rafiki zake, ulevi, na kadhalika. Matendo haya hayana budi
kufanywa na mhusika huyu kutokana na namna alivyosawiriwa tangu mwanzo.
Mbinu hii, zaidi ya kumsawiri John, inaibua dhamira mbalimbali kama vile uhuni,
umuhimu wa elimu, na kadhalika.
Hitimisho
Tunapochunguza kuhusu mbinu zilizotumika kuwajenga wahusika, zaidi ya kusawiri
sifa za wahusika na kudokeza dhamira, zimefanikisha kufafanua falsafa
iliyofumbatwa katika jina la riwaya: Dunia Uwanja wa Fujo. Falsafa hii inayaona
maisha kuwa ni fujo tupu (Senkoro, 2011). Fujo hizi zinaonekana kila mahali, vijijini
mpaka mijini. Aidha, fujo hizi zinaokana katika maeneo mbalimbali kama vile; katika
siasa, lugha, ndoa, na kadhalika. Kwa mfano, katika mbinu ya matendo tumeeleza
matendo kadhaa kama ya Tumaini kumtorosha Anastasia; Mama Resi kukataa
kushuka kwenye basi na kadhalika. Matendo haya yanasawiri fujo zinazoendelea
ulimwenguni. Kitendo cha Tumaini kumtorosha Anastasia ni fujo kwa jamii kwa
sababu misingi ya ndoa inakiukwa. Aidha, kitendo cha Mama Resi kutoshuka kwenye
basi ni fujo. Kimsingi matendo hayo yanadokeza falsafa iliyofumbatwa katika jina la
kitabu. Kwa hivyo, mbinu zilizobaishwa katika makala haya zina mchango mkubwa
katika kuelewa mawazo ya riwaya au falsafa inayohusika.
Marejeleo
Bal, M. (1997). Narratology: Introduction to the Theory of Narrative (2nd edition). Toronto:
University of Toronto Press.
Diegner, L. (2002). “Allegories in Euphrase Kezilahabi’s Early Novels,” katika Swahili
Forum IX, uk. 43-74.
Kezilahabi, E. (2007). Dunia Uwanja wa Fujo. Nairobi: Vide-Muwa Publishers Limited.
Madumulla, J. S. (2009). Riwaya ya Kiswahili. Dar es Salaam: Mture Educational Publishers.
Mlacha, S. A. K. (1991). “Point of View as Stylistic Device in Kiswahili Novels,” katika
Kiswahili: Jarida la Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, Juz. 58, kur. 54-61. Dar es
Salaam: TUKI.
Mohamed, S. A. (1995). Kunga za Nathari ya Kiswahili: Tamthilia, Riwaya na Hadithi Fupi.
Nairobi: East African Educational Publishers.
Mohochi, E. S. (2000). “Usimulizi wa Riwaya ya Nyongo Mkalia Ini” katika Nordic Journal
of African Studies 9 (2), uk. 49-59.
Msokile, M. (1999). Misingi ya Hadithi Fupi. Dar es Salaam: Dar es Salaam University Press.
 Mulokozi, M. M. (1983). “Dunia Uwanja wa Fujo (Mapitio ya Kitabu),” katika Kiswahili:
Jarida la Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, Juz. 50/1, kur. 1-12. Dar es Salaam:
TUKI.
Njogu, K. & Chimerah, R. (2008). Ufundishaji wa Fasihi: Nadharia na Mbinu (Chapa ya
Pili). Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.
Senkoro, F. E. M. K. (1982). Fasihi. Dar es Salaam: Press and Publicity Centre.
Senkoro, F. E. M. K. (2011). Fasihi. Dar es Salaam: KAUTTU.
Shen, F. (2006), “Narrative Strategies in Robert Cormier’s Young Adult Novels.” PhD
Dissertation, Ohio State University.
Wafula, R. (2002). “Language and Politics in East African Swahili Prose: Intertextuality in
Kezilahabi’s Dunia Uwanja wa Fujo ‘The World a Playground of Chaos,’” katika
Obeng, S. G. & Hartford, B. (wah.), Surviving Through Obliqueness: Language of
Politics in Emerging Democracies, uk. 19-29. New York: Nova Science Publishers
Inc.
Wamitila, K. W. (1997). “Contemptus Mundi and Carpe Diem Motifs in Kezilahabi’s Works”
katika Kiswahili: Jarida la Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, Juz. 60, kur. 15-24.
Dar es Salaam: TUKI.
Wamitila, K. W. (2008). Kanzi ya Fasihi: Misingi ya Uchanganuzi wa Fasihi. Nairobi: VideMuwa
Publishers Ltd.

Print this item

  AINA ZA TASWIRA
Posted by: MwlMaeda - 12-28-2021, 09:35 AM - Forum: Uhakiki wa kazi za fasihi - No Replies

Taswira ni picha inayojengeka akilini mwa msomaji. Kuna aina tofauti tofauti za taswira. Kama vile
Taswira uoni –inajitokeza unapopewa picha ya mtu (umbile)
Taswira sikivu- unapewa picha akilini lakini inayopitia masikio
-(Kana kwamba unaskia sauti masikioni)
Mfano katika wimbo aliomtungia mamake Kongowea kuhusu kifo chake
Taswira mwonjo – mfano Musa na Maksuudi wameandaliwa chakula na Kazija – (unasikia      kana kwamba kuna harufu na wanakula chakula kwa maelezo)
Taswira mnuso – ni pale ambapo mwandishi anakupa maelezo
yanayokufanya unuse harufu. Mfano: Kongowea anapoinusa harufu ya Kazi-Kwisha alipofika kwake siku ya mwisho kutambua ni
babake
Taswira hisi  – wakati msomaji anaelezewa kuhusu kitendo kinachotoa hisia mfano wakati mhusika katika Utengano (Tamima) anachapwa na Maksuudi.
Taswira Mguso  – msomaji anapohisi yuaguswa anaposoma wakati Vumilia anamshika   Kongowea Mswahili akimsihi aende kulala.

Print this item

  UHAKIKI WA TAMTHILIYA YA ORODHA
Posted by: MwlMaeda - 12-28-2021, 09:24 AM - Forum: Uhakiki wa kazi za fasihi - No Replies


.pdf   UHAKIKI WA TAMTHILIYA YA ORODHA.pdf (Size: 193.83 KB / Downloads: 12)

Print this item

  UHAKIKI WA TAMTHILIYA YA NGOSWE – PENZI KITOVU CHA UZEMBE
Posted by: MwlMaeda - 12-28-2021, 09:22 AM - Forum: Uhakiki wa kazi za fasihi - No Replies


.pdf   UHAKIKI WA TAMTHILIYA YA NGOSWE.pdf (Size: 133.48 KB / Downloads: 12)

Print this item

  UHAKIKI RIWAYA YA WATOTO WA MAMAN’TILIE
Posted by: MwlMaeda - 12-28-2021, 09:06 AM - Forum: Uhakiki wa kazi za fasihi - No Replies

UCHAMBUZI WA RIWAYA WATOTO WA MAMA NTILIE
MWANDISHI: EMMANUEL MBOGO
WACHAPISHAJI: HEKO PUBLISHERS
MWAKA: 2002
WASIFU WA MWANDISHI
Emmanuel Mbogo ni Profesa wa drama na fasihi na amehudumu katika vyuo vikuu mbalimbali ikiwemo, Chuo Kikuu cha Kenyatta Kenya na Chuo Kikuu Huria. Mbogo ni mwanafasihi mahiri sana katika Afrika ya Mashariki.
MUHTASARI WA RIWAYA
Maman’tilie, mama mwenye watoto wawili lakini wote wamefukuzwa shule kwa kukosa ada na sare. Anajitahidi hapa na pale ili apate, lakini wapi? Pesa imegeuka nyoka inateleza kwenye nyasi. Mumewe Mzee Lomolomo hana muda, yeye kila kukuchapo huelekea bunge la walevi kunywa pombe tani yake. Akiwa huko hunywa na kurudi nyumbani akiwa mbwii! Mwisho mwandishi anauliza swali gumu, ‘Nani anajali?’
UCHAMBUZI WA FANI NA MAUDHUI
MAUDHUI KATIKA RIWAYA YA WATOTO WA MAMAN’TILIE
Maudhui hujumuisha mawazo na pengine mafunzo mbalimbali yaliyomsukuma mtunzi ama mwandishi wa kazi ya fasihi akaandika kazi yake.
DHAMIRA
Dhamira ni lile wazo linalomfanya mwandishi wa kazi ya fasihi aandike kazi yake. Katika riwaya hii, dhamira nyingi zimejadiliwa kama:
UMASIKINI
Dhamira hii imetawala katika riwaya. Asilimia kubwa ya wahusika ni watu wenye maisha ya dhiki na kazi za kijungujiko. Umasikini wao unadhihirishwa na mitaa wanayoishi kama: Manzese, Msufini, Tabata, Kisutu na Temeke. Maeneo haya ndiyo yaitwayo uswahilini leo hii.
Zita na Pita wanafukuzwa shule kwa sababu ya kukosa ada na sare (uk 1). Mamant’ilie naye anatumia maji ya mwarobaini kutibu homa yake kwa sababu hana pesa ya kununulia dawa za hospitali.
ULEVI
Unywaji wa pombe kupitiliza huweza kusababisha madhara makubwa kwa mtumiaji. Mzee Lomolomo ni mlevi mzoefu, kutokana na ulevi wake, anashindwa hata kuwalipia ada wanae ili waendelee na shule. Ni ulevi huohuo unamfanya aishi maisha ya dhiki huku akishindwa kutoa mchango kwa familia yake na taifa linalomtegemea. Mwisho Lomolomo anakufa kwa sababu ya pombe.
Mwandishi anasema, “… Lomolomo alikuwa lofa, mtu wa kazi za kijungujiko na vipesa vyake viliishia kwenye pombe…” (uk 7).
MALEZI YA WATOTO
Watoto wasipopata malezi yanayostahili kutoka kwa wazazi wote wawili huwa ni rahisi kwao kujiingiza katika mambo yasiyofaa.
Mwandishi anaonyesha aina tatu za watoto. Kwanza kuna Zita na Pita. Hawa wana wazazi wote wawili lakini baba hajishughulishi na malezi yao. Pia mama naye ametingwa na shughuli nyingi katika genge lake la uuzaji wa chakula. Zita na Pita hawana malezi ya kueleweka. Hali hii inamfanya Pita ajiingize katika biashara ya madawa ya kulevya.
Pili, kuna Dan na Musa hawa hawana baba, wanaishi na mama zao tu. Mama zao hawawajali wala kuwakemea kwa chochote kibaya wanachofanya. Dan anajiingiza katika ujambazi na kupoteza maisha. Musa anajiingiza katika biashara ya madawa ya kulevya na kuishia jela.
Tatu kuna Kurwa na Doto. Hawa hawana wazazi kabisa. mwandishi anasema, “… walikuwa chokoraa namba moja, kupigana kulala na njaa, kukamatwa na polisi… yalikuwa sehemu ya maisha yao…”
Doto anajiingiza katika ujambazi, huko anauawa na mlinzi Simango.
RUSHWA
Rushwa imeota mizizi katika jamii. Kila uendako, kila upitako na kila utokako utaambiwa toa rushwa ili upate kitu fulani.
Mamant’ilie alishindwa kuyamudu maisha ya mjini kwa sababu ya rushwa aliyokuwa akiwapa askari wa jiji. Kwa kalamu yake isiyoisha wino, Mbogo anaandika, “Kodi na hongo kwa askari wa jiji, ziliikamua faida yake.” (uk 32).
MMOMONYOKO WA MAADILI NA KUKOSEKANA KWA UTU
Maadili ya siku hizi si yale ya zamani. Miaka inabadilika na vizazi navyo vinabadilika. Watu ni watu tu lakini hawana utu. Watoto wadogo sasa wanavuta sigara na kutafuna mirungi kama tumuonavyo Dan na Musa. Watu hawana moyo wa kusaidiana tena, wao wanaamini kuwa kila mwenye janga atalila peke yake. Zita anazidiwa na maradhi yaliyosababishwa na kuumwa na mbwa mwenye kichaa. Watu hawakumsaidia, badala yake walivishangilia vioja alivyovifanya. Mwandishi anatuonesha Zenabu akiwaomba msaada na kuwakalipia, “Nisaidieni, mnacheka nini? Wendawazimu wakubwa.” (uk 82).
NAFASI YA MWANAMKE KATIKA JAMII
Nafasi ya mwanamke ni jumla ya matendo yote yafanywayo na mwanamke katika jamii yake. Mara nyingi huwa mabaya na yenye mtazamo hasi, lakini mara chache huwa mazuri yenye mtazamo chanya. Mwandishi wa riwaya hii, amemchora na kumjadili mwanamke kwa mawanda mapana kama inavyoelezwa:
  • Mama mlezi na mwangalizi mkuu wa familia. Maman’tilie ndiye aliyejua familia yake ile nini, ifanye nini na iishi vipi. Mumewe mzee Lomolomo hakuwa na mchango wowote. Yeye kila kukuchapo alikwenda kilingeni kufakamia mataputapu na pombe haramu.
  • Mwenye huruma na moyo  wa kutoa msaada. Zenabu anawakilisha tabia hii. Alimsaidia Pita alipokuwa na njaa. Ni yeye akishirikiana na Mama sara walimpeleka Zita hospitali.
  • Mwenye mapenzi na kazi. Kurwa anapenda kazi, alifuatana na Maman’tilie kwenda gengeni, huko alimsaidia kuuza chakula. Hata siku moja kurwa hakuchoka kufanya kazi.
  • Aliyenyimwa elimu. Zita ni mwanamke aliyenyimwa elimu. Anafukuzwa shule kwa kukosa ada na sare.
  • Mzembe na asiyejali malezi ya watoto. Mama Musa ni mzembe na hajali malezi ya mwanae. Yeye ameshika themanini zake na Musa kashika hamsini zake.
  • Dhamira nyingine zilizojitokeza ni:
  • Hatari ya ugonjwa wa Malaria
  • Elimu
  • Athari ya sayansi na teknolojia
  • Adha ya usafiri
  • Wizi na ujambazi
UJUMBE
Ujumbe ni funzo litolewalo na kazi ya fasihi. Mafunzo mengi yametolewa katika riwaya hii:
  • Watoto wasifukuzwe shule kwa sababu ya kukosa ada, kwani kufanya hivyo kunawanyima haki yao ya kupata elimu.
  • Majalala ya kuchoma takataka yajengwe mbali na makazi ya watu. Mwandishi anasema, “Mapafu ya wakazi yaliendelea kuteketea kwa moshi siku hadi siku… watu wale walikuwa wanakufa taratibu.” (uk 27).
  • Pombe si suluhisho la matatizo.
  • Mzaha mzaha hutumbua usaha. Zita alikwaruzwa na mbwa mwenye kichaa, lakini wakapuuzia, mwishi ni kifo cha Zita.
MIGOGORO
Migogoro ni kukosekana kwa maelewano baina ya watu binafsi, jamii, taifa au mataifa. Migogoro iliyojitokeza ni:
Migogoro ya wahusika
  • Mwalimu Chikoya na wanafunzi wasiokuwa na ada wala sare za shule. Huu unasababishwa na wanafunzi wasiokuwa na ada wala sare. Suluhisho lake ni wanafunzi hao kufukuzwa shule.
  • Maman’tilie na mzee Lomolomo. Huu unasababishwa na ulevi wa Lomolomo. Suluhisho ni kifo cha mzee Lomolomo.
  • Peter na Doto. Huu unasababishwa na Doto kumfukuza Pita jaani. Suluhisho la mgogoro huu ni Kurwa kumsaidia Peter.
Mgogoro wa nafsi
  • Huu unampata Peter, yeye anamawazo ya kurudi shule lakini hajui ni kipi afanye ili apate pesa za kumrudisha.
Migogoro mingine ni: migogoro ya kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni na kijamii.
FALSAFA
Falsafa ni imani ya mwandishi. Emmanuel Mbogo anaamini kuwasaidia watoto kupata elimu yao kutaondoa matatizo yanayozuia ujenzi wa jamii mpya.
MTAZAMO/MSIMAMO
Mwandishi anamsimamo wa kimapinduzi. Anaamini kuwapatia watoto elimu na kusimamia malezi yao kutaliokoa taifa.
UCHAMBUZI WA FANI NA VIPENGELE VYAKE
Fani ni ule ufundi wa kisanaa anaoutumia msanii katika kazi yake. Fani ndiyo hutupatia kile kiitwacho maudhui. Katia riwaya hii, fani imechambuliwa kama ifuatavyo:
WAHUSIKA
Wahusika ni watu au viumbe waliokusudiwa uwakilisha tabia za watu katika kazi ya fasihi. Wahusika waliopo katika riwaya hii ni:
  • Maman’tilie. Ni mke wa mzee Lomolomo. Ni mchapakazi. Ni mama yao Zita na Peter na anafaa kuigwa na jamii.
  • Lomolomo. Ni mume wa Maman’tilie. Ni mlevi wa pombe haramu. Hawajibiki katika malezi ya watoto wake na hafai kuigwa na jamii.
  • Zita. Mtoto wa Maman’tilie na mzee Lomolomo. Alifukuzwa shule kwa kukosa ada na sare akiwa darasa la sita. Pia, alikwaruzwa na mbwa mwenye kichaa. Mwisho anakufa kwa kupuuzia ule mkwaruzo wa mbwa.
  • Peter. Mtoto wa Mzee Lomolomo na Maman’tilie. Anafukuzwa shule akiwa darasa la tano. Anatafuta ridhiki dampo. Baadaye anajiingiza katika biashara ya madawa ya kulevya.
  • Chikoya. Ni mwalimu mkuu wa shule ya msingi Makurumla. Anawafukuza wanafunzi wasiokuwa na sare wala ada.
  • Musa. Anafukuzwa shule kwa kukosa ada na sare. Hamheshimu mama yake. Anajiingiza katika biashara ya madawa ya kulevya.
  • Sara. Mwanafunzi wa Makurumla na ni jirani yao Zita.
  • Mama Sara. Mama yake Sara. Alimsaidia Zita alipopatwa na kichaa.
  • Zenabu. Anafanya kazi Kikale Bar. Ana huruma. Anafaa kuigwa.
  • Kurwa. Ni yatima. Anaishi vichochoroni. Anategemea chakula cha dampo. Anasingiziwa kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya.
  • Doto. Ni yatima. Anauawa kwa kujihusisha na ujambazi.
  • Rhemtulah. Ni mfanyabiashara wa kihindi.
  • Simango. Ni mlinzi wa Rhemtulah. Anawaua Doto na Dan.
  • Dani. Ni mtoto ambaye hamjui baba yake. Anauawa kwa kujihusisha na ujambazi.
  • Jane. Aliwalea Doto na Kurwa baada ya kufiwa na mama yao. Naye pia anakufa.
  • Master Baroni. Anawatumia watoto katika biashara yake ya madawa ya kulevya. Si mfano wa kuigwa na jamii.
MATUMIZI YA LUGHA
Fasihi ni sanaa itoayo maudhui kwa kutumia lugha ya maneno ambayo hutamkwa au kuandiwa. Kipengele cha lugha ni muhimu kwani ndicho kinachotofautisha fasihi na sanaa zingine.
Lugha iliyotumika katika riwaya hii ni nyepesi na yenye kueleweka. Mwandishi ametumia vipengele vingi vipatikanavyo katika matumizi ya lugha kama: ucheshi na lugha ya picha, misemo na tamathali za semi.
TAMATHALI ZA SEMI
Tamathali za semi ni maneno au sentensi ambazo hutumiwa na wasanii wa fasihi ili kutia nguvu katika maana, mtindo na hata sauti katika maandishi ama kusema. Wakati mwingine hutumiwa ili kupamba na kuongeza utamu wa kazi za fasihi. Mwandishi ametumia tamathali nyingi za semi kama:
  • Tanakali sauti (onomatopoeia). Tanakali sauti ni maneno au nomino ziundwazo katika sentensi kutokana na sauti zinazofanana.
            “Bwee!”
           “Paah!” (uk. 5)
  • Tashibiha. Katika tamathali hii, watu ama vitu viwili au zaidi hulinganishwa na watu au vitu vingine kwa kutumia maneno, ‘kama’, ‘mithili’…
        “Masikio yamesimama wima kama anasisitiza kitu.” (uk. 2)
         “Mdomo wake uliokaa kama bakuli la pombe.” (uk. 10)
  • Tafsida. Hii hutumika kupunguza ukali wa maneno.
         “Akaenda haja ndogo.” (uk. 2)
        “Akakitibu kidonda chake kwa maji ya chumvichumvi.” (uk 55)
  • Takriri. Katika tamathali hii, maneno hurudiwarudiwa ili kuonyesha msisitizo.
         “Yalaa! Yalaa!” (uk 2)
          “Mjomba! Mjomba!”
  • Mdokezo. Hapa msemaji husema kitu bila kukimalizia kukitaja.
       “Shikamoo mama…” (uk 6)
        “Una… una…” (uk 11)
  •  Tashihisi. Hapa vitu hupewa sifa alizonazo binadamu.
         “Maman’tilie alimtupia jicho bintie.”
         “Mabega yameangalia juu.” (uk 10).
  • Mjalizo. Katika tamathali hii maneno hufuatana pasipo kiunganishi.
         “Walikaa, wakala, wakanywa maji, wakamshukuru Mungu.”
  • Kejeli. Hii ni tamathali ya semi ambayo maneno yake huwa kinyume na maana yanayotoa.
          “Naye pita aliitikia salamu hizo za ukarimu kwa kupiga chafya             mbili au tatu.” (uk 19).
          “Lomolomo uso wake uliopendeza kwa chang’aa…” (uk 70).
  • Sitiari. Tamathali hii hulinganisha vitu bila kutumia viunganishi.
“Wakatembea mwendo wa farasi.” (uk 86).
  • Ritifaa. Katika tamathali hii, mtu huongea na kitu ambacho husikika kwa fikra tu.
“Kumbe wewe na mwanao mna hila kiasi hiki? Mmepatana kuondoka na kusafiri katika dau moja.” (uk 94).
  • Misemo.
“Ukienda Tabata utapata.”
“Waswahili hawana dogo.”
  • Matumizi ya lugha za kigeni.
“Nikukonekti.” (uk 78).
  • Methali.
“Kamba hukatikia pembamba.”
  • Ucheshi na lugha ya picha.
“Alikunywa funda moja, akajisikilizia kabla ya kulimeza. Alisikia pombe ikisafiri kufuata barabara ya lami hadi tumboni.” (uk 87).
MTINDO
Mtindo ni ule upekee wa mtunzi wakazi ya fasihi na mtunzi mwingine. Mfano, mwandishi anaweza kutumia, nyimbo, mashairi, nafsi zote, dayolojia, monolojia n.k. mwandishi amefanikisha mtindo wake kwa kutumia,
  • Matumizi ya nyimbo. Mfano katika ukurasa wa 10 Lomolomo aliimba,
“Kuleni nae,
Hata bangi vuteni nae,
Lakini ni bure,
Mwenzenu nimezaa naye…”
  • Mwandishi katumia monolojia (masimulizi) na dayolojia (majibishano).
  • Mwandishi katumia nafsi zote tatu.
MUUNDO
Muundo ni mpango na mtiririko wa kazi hiyo kwa upande wa visa na matukio.
Riwaya hii imetumia muundo wa kurukia. Mwandishi amemuonyesha Lomolomo akiwa katika hali ya ulevi, baadaye anatukumbusha alipokuwa anafanya kazi bandarini. Vilevile anawaonyesha Kurwa na Doto wakiishi peke yao. Lakini baadaye anatukumbusha kipindi walipokuwa wanalelewa na mama yao ambaye hata hivyo alifariki kisha wakalelewa na Jane ambaye naye anafariki.
MANDHARI
Mandhari ni sehemu ambayo kazi ya fasihi hutendeka. Riwaya hii imetumia mandhari ya jiji la Dar es Salaam na mitaa yake kama, Manzese, Msufini, Tabata, Kisutu, Urafiki na mtaa wa Ajentina.
JINA LA KITABU
Jina la kitabu, Watoto wa Maman’tilie, linasadifu yaliyomo, kwani ndani ya riwaya hii kuna mhusika mkuu ambaye ndiye Maman’tilie.
Riwaya hii inamwonesha mama huyu akijaribu kujinasua yeye na watoto wake katika wimbi la umasikini, lakini wapi? Jitihada zote anazofanya zinagonga mwamba na matatizo yake yanazidi kuongezeka.
KUFAULU NA KUTOFAULU KWA MWANDISHI
KUFAULU KIMAUDHUI
–      Mwandishi amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuonyesha shida wazipatazo watoto wa mitaani.
–      Mwandishi amefanikiwa kuonyesha madhara ya umasikini.
–      Mwandishi ameonyesha madhara ya unywaji wa pombe kupita kiasi na ulevi.
KUFAULU KIFANI
–      Amekitendea haki kipengele cha mtindo, kwani humo ametumia vipengele vingi kama nyimbo n.k.
–      Kazi yake imeshibishwa kwa tamathali nyingi za semi.
–      Ametumia lugha ya picha inayomwelewesha zaidi msomaji.
KUTOFAULU KWA MWANDISHI
–      Kimaudhui. Mtazamo wa mwandishi katika suala la umasikini hauko sawa. Yeye anaamini hata ukifanya kazi kwa bidii kama ni masikini utaendelea kuwa masikini kama tumuonavyo Maman’tilie.
–      Kifani wahusika wa mwandishi hawana uwiano. Wengi wao ni watu masikini.
–      Pia, mandhari yote yaliyotumiwa na mwandishi ni ya mjini. Mwandishi ameutenga upande wa kijijini ambao nao kama ungetazamwa, jamii ingejifunza mengi.

Print this item