KEJELI KATIKA FASIHI YA KISWAHILI – TANZANIA (7) - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Uhakiki wa kazi za fasihi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=78) +--- Thread: KEJELI KATIKA FASIHI YA KISWAHILI – TANZANIA (7) (/showthread.php?tid=1867) |
KEJELI KATIKA FASIHI YA KISWAHILI – TANZANIA (7) - MwlMaeda - 12-28-2021 4. Hitimisho
Tumeona
kwamba kejeli haitumiki tu katika kuukosoa uongozi katika jamii, ni mzaha wenye kuweza kuwasema, kuwasengenya, kuwakebehi wanajamii wote kwa lengo la kuwarekebisha, kuwaonya na kuwaelimisha ili waende sambamba na wanajamii wengine. Kejeli haitumiki kwa lengo la kuwakosoa viongozi na watu wa tabaka la chini tu, bali hutumika kuwakosoa hata wanazuoni wenye kwenda kinyume na taaluma. Kejeli
ni mojawapo ya mbinu ambazo hutumiwa na wasanii na waandishi katika muktadha wa kuelimisha, kukosoa na kuburudisha jamii. Aidha, kejeli hutumika kwa malengo ya kuyaweka wazi mambo yaliyopo katika jamii, kulingana na mabadiliko na matukio yaliyopo na yanayotokea. Kejeli
hutoa uhuru wa waandishi na wasanii. Kwa hakika hii ni njia ya pekee sana ambazo inawapa wanajamii nafasi ya kushiriki kwa katika kuwakosoa walioko madarakani na kuifanya kazi yao kuwa nyepesi kueleweka. Katika
kipindi cha ukoloni, kipindi cha baada ya ukoloni na kipindi tulichonacho hivi sasa cha utandawazi, mbinu za kejeli zimekuwa zikibadilika badilika. Hii inawezekana kwamba ni kwa sababu kadri ya mfumo wa maisha na mbinu mbalimbali za kupambana na mabadiliko hayo ya maisha zinavyobadilika, ndivyo na mbinu za kejeli zinavyobadilika. Kwa mfano hivi asa vijana wamebuni michezo ya kuchekesha inayorushwa katika baadhi ya vituo vya televisheni vya Tanzania kama vile Ze Komedi iliyokuwa ikionyeshwa kwenye EATV chaneli 5, The Original Komedi inayoonyeshwa na TBC Mizengwe inayooneshwa kwenye kituo cha ITV; na baadhi ya vituo vya televisheni vya Kenya kama Vitimbi au Vioja Mahakamani vinavyooneshwa na kituo cha KBC wanaitumia kejeli kuusema uozo, ufisadi, unyama, udhalilishwaji, unyanyapaa na ukandamizwaji ulioshika kasi katika jamii. Aidha vikundi hivi hutumia kejeli kuwasema wafanyakazi, wala-rushwa na wanajamii vigeugeu walioko na wanaoziongoza nchi na jumuiya mbalimbali. Kufanya hivyo kunaisaidia jamii iliyoko mbali na miji mikuu kufahamu kinachotokea ndani na nje ya nchi yao. Vikundi
vya vichekesho na dhana yao ya kejeli husaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza uchovu wa wanajamii baada ya shughuli nyingi na nzito za mchana kutwa. Hii ina maana kwamba jamii inapokusanyika pamoja na kuburudishwa kwa kuviangalia vikundi hivi vya vichekesho, inapunguza uchovu kwa kucheka na kufurahi. Hii pia ni kwa sababu, maigizo yanayo manufaa kwani yanabeba ujumbe muhimu ambao kwa hali ya kawaida hauwezi kubebwa na sanaa nyingine. Kwa mfano, suala la UKIMWI ni vigumu kuliongelea kwa urahisi bila kuigiza au kwa kuonyesha picha. Kwa kupitia vichekesho vyenye kejeli wana- jamii hujikuta wakiwa na shughuli za kufanya baada ya kazi na kujiepusha na mambo mengi yenye kusababisha maambukizo na usambazaji wa Virusi vya UKIMWI. Ifahamike
wazi kwamba, kejeli katika fasihi ya Kiswahili na kumbo zake hubeba ujumbe mzima wa kazi ya msanii au mwandishi kisaikolojia, kifani na kimaudhui katika kujikamilisha kwake. Kwa
mfano, wanamuziki wetu wa kizazi kipya, wana taarabu, wacheza maigizo, wachekeshaji, wanakomedia, wanakomiki na vikundi vingine vingi vya kisanii. hutumia kejeli kuielimisha jamii juu ya janga la madawa ya kulevya. Wasanii wetu hawa wamefanikiwa kwa kuiangazia misuguano iliyopo katika serikali, jitihada za kuinua uchumi, maisha bora, n.k.. Hivyo
ni wajibu wa wasanii, waandishi na wanazuoni wengine kuhakikisha kuwa wanaitumia mbinu hii na kuiendeleza ili kufichua uozo, ubadhirifu, ufisadi, ufidhuli uliopo, unaojitokeza na unaozidi kujikita katika jamii na taifa zima kwa ujumla. MAREJELEO
Balisidya,
M. L. 1982. Uchunguzi katika fasihi simulizivizingiti na mkabala. Katika makala za semina
za TUKI na makala mbalimbali. Dar es Salaam. TUKI. Gibbs,
R. W. 1994. The Poetics of Mind. Figurative thought, Language & Understanding. Cambridge:
Cambridge University Press. Honero,
L. N. na wenzake. 1980. Matunda ya Azimio la Arusha, Mashairi ya Mwamko wa Siasa.
Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili: Dar es Salaam. Kezilahabi,
E. 1988. Karibu Ndani. Dar es Salaam: Dar es Salaam University Press. Kezilahabi,
E. 1999. Kaputula la Marx. Dar es Salaam: Dar es Salaam University Press. Khatibu,
M. S. 1988. Fungate ya uhuru. Dar es Salaam: Dar es Salaam University Press. Mbatiah,
M. 2001. Kamusi ya Fasihi. Nairobi: Fotoform Ltd. Mbogo,
E. 1981. Morani. Dar es Salaam: Dar es Salaam University Press. Mtesigwa,
P. C. K. 1989. Methali ni nini? Katika Mulika juzuu Na. 56 Dar es Salaam: TUKI. Muhando,
P. 1984. Lina Ubani. Dar es Salaam: Dar es Salaam University Press. Mvungi,
T. A. 1985. Chungu Tamu. Dar es Salaam: Tanzania Publishing House. Mvungi,
T. A. 1978. Raha Karaha. Dar es Salaam: Continental Publishers. Mvungi,
T. A. 1995. Chekacheka. Dar es Salaam: Continental Publishers. Mwakyembe,
H. 1980. Pepo ya Mabwege. Dar es Salaam: Longman. Mulokozi,
M. M. 1989. Tanzu za fasihi simulizi. Katika Mulika juzuu Na. 21 Dar es Salaam: TUKI. Ngahyoma,
N. 1975. Kijiji Chetu. Dar es Salaam: Tanzania Publishing House. Penina,
M. M. 1984. Lina Ubani. Dar es Salaam: Dar es Salaam University Press. Ruhumbika,
G. 1995. Miradi Bubu ya Wazalendo. Dar es Salaam: Tanzania Publishing House. Rutashobya,
M. G. R. 1980. Nuru Mpya. Dar es Salaam: Tanzania Publishing House. Kandoro,
S. 1971 Mashairi ya Saadani. Dar es Salaam: Mwananchi Publishing Ltd Shaaban,
R. 1951. Kusadikika. Nairobi: Nelson & Sons. Shaaban,
R. 1968. Kufikirika. Nairobi: OUP. Short,
M. 1980. Style in Fiction. London: Longman Wales,
Katie 2001. A Dictionary of Stylistics. Harlow: Personal Education. Wamitila,
K. W. 2008. Kanzi za Fasihi. Misingi ya Uchanganuzi wa Fasihi: Nairobi Vide Muwa Publishers Ltd. SHUKRANI
ZA PEKEE KWA: STEVEN
E. MRIKARIA[url=http://www.qucosa.de/fileadmin/data/qucosa/documents/9089/17_09_Mrikaria.pdf][/url]
|