KEJELI KATIKA FASIHI YA KISWAHILI - TANZANIA (6) - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Uhakiki wa kazi za fasihi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=78) +--- Thread: KEJELI KATIKA FASIHI YA KISWAHILI - TANZANIA (6) (/showthread.php?tid=1868) |
KEJELI KATIKA FASIHI YA KISWAHILI - TANZANIA (6) - MwlMaeda - 12-28-2021 3.3. Kejeli wakati wa utandawazi
Karne ya ishirini na moja kwa hakika imeshuhudia kuingia kwa teknolojia mpya katika nyimbo za Kiswahili. Teknolojia hii ilijiimarisha kwa kiwango cha juu na kupata
mashiko na mwelekeo wa utandawazi. Utandawazi si mfumo mpya katika ulimwengu wa sayansi ya habari na teknolojia mpya. Mfumo huu umekuwepo kwa karne nyingi japo kwa viwango tofauti kutoka karne moja hadi nyingine. Kuingia
kwa dhana ya utandawazi katika fasihi simulizi kumeleta maingiliano na mabadiliko mengi Kitaifa na hata Kimataifa katika tanzu zake nyingi. Kwa upande wa mashairi na nyimbo maingiliano haya yanaonekana dhahiri na kuleta mabadiliko makubwa katika jamii. Vijana wengi hususan wale wa Afrika ya Mashariki walizitumia mashairi yao kuielezea jamii juu ya matatizo wanayopambana nayo kila siku. Mathalani ukosefu wa ajira, umaskini waliokuwa nao, athari za ukosefu wa ajira kwa vijana, uongozi, polisi, mahakama, n.k.. Kutungwa,
kuimbwa na kuonekana majukwaani kwa wasanii na mashairi haya kumewezesha vijana kuwa wabunifu, wajasiriamali na weledi wa kueleza kero zao na matatizo wanayopambana nayo katika maisha ya kila siku. Kwa mfano, mashairi ya msanii Ras Lion katika wimbo Umasikini Huu: Umaskini
huu (x 3) Utaisha lini Umaskini
huu (x 3) Utaisha lini Umasikini
huu (x 3) Utaisha lini Msanii
analalamikia kwa masikitiko makubwa umasikini uliokithiri tanzania bila ya kupata jibu ya kuwa mwisho wake ni lini. Kwa upande mwingine anaikejeli nchi za Tanzania pamoja na viongozi wake ambapo kila siku wanaulalamikia huku nchi ni inao utajiri mkubwa wa raslimali. Hii inatuonyesha wazi kuwa msanii anaona uchungu sana juu ya umasikini unaozikumba nchi zetu ilhali viongozi wake ni matajiri. Msanii
Jaffer Rhyme yaliyopo wimbo wake wa Niko Bize yaani nina shughuli nyingi, anasema: (…)
ndiyo pekee inayonifanya nipate ninachotaka Umenipata
(brother) kaka ofisini hatujaliwi Ndio
sababu hasa tunasafa, Kwenye muziki cash tunapata Niko
Bize naandika rhyme kila time nnayopata Sio
bize tu for nothing, Bize nageti something Kwenye
life time hivi sasa kazi ni kazi afisa Ili
mradi tu inalipa ukiifanya kiuhakika Ni
mfano mwingine wa kejeli inayowasema viongozi wa siku hizi. Kiongozi kila siku anakuwa safarini bila kujali nchi yake na wananchi wa eneo lake wanaishi namna gani. Kila siku kiongozi anapoulizwa jambo fulani yeye anajibu kuwa hana nafasi kwa kuwa ana kazi nyingi (Niko Bize). Kuwa bize huko hakumsaidii yeye wala wananchi wake bali hutumika kama fimbo ya kukwepea majukumu yake. Kwa
upande mwingine, msanii Jaffer Rhyme anaongeza kwamba wapo viongozi wengine ambao wako bize kwelikweli. Hawa ni wale waliomeza au walikunywa damu ya bendera. Viongozi hawa ni wale wenye kuona uchungu kwa wananchi wake. Hawa ni wale wenye kujitoa mhanga kwa ajili ya kuitetea jamii nzima bila kujali uwezo walionao wanajamii. Pia hawa ni wale viongozi wanaokosa muda wa kuzurura ovyo na kupata nafasi ya kuwasikiliza wananchi waliowachagua. Maudhui ya mashairi haya ndio msingi mkuu wenye kujengwa na utandawazi. Kwa
upande mwingine tunauona mashairi ya Mr Ebbo katika wimbo wa Mi Mmasai Bana: Mi
Mmasai bwana nasema mi Mmasai, Nadumisha
mila zile wengine walishashindwa, Mi
Mmasai bwana nasema mi Mmasai. Naruhusu
kushangaa kwa wageni na wenyeji, Mi
Mmasai bwana nasema mi Mmasai. Tamaduni
asilia ilobaki Afirika… Msanii
anatamba kwa kulisifia kabila lake la Kimasai, mila na desturi za Kimasai zilizomzunguka na ambazo zinazomshangaza kila mtu. Anasema kuwa hata utandawazi utandawae namna gani yeye hawezi kuuacha utamaduni wake huo. Mmasai huyu kwa namna moja au nyingine anawasema wale wote wenye tabia ya kuukana utaifa wao na kuufurahia utaifa wa wengine kuwa hawatafaidika lolote. Aidha mashairi haya yanazisema nchi na makabila mengi kuwa yameshindwa kudumisha tamaduni zao na kuiga tamaduni za kigeni. Mashairi
ya wasanii wengi yamegubikwa na kasumba waliokuwa nayo wanajamii wengi ya kuwa Kiingereza ni lugha ya wasomi. Kwa kasumba hiyo wasanii wanachanganya na lugha za Kiingereza na Kiswahili/Kabila jingine kama mbinu za kuwapata wapenzi wengi na wasomi. Kwa mfano mashairi ya msanii Lady JayDee katika wimbo wake What I need from you is understanding: Ninachotaka
kutoka kwako maelewano What
I need from you is understanding nakupenda,
nakutaka nakuhitajiii I
love you, I need you … Nakupenda,
Nakutaka … Msanii
huyu pamoja na wengine wamesahau kwamba lugha ni kitu cha kujivunia kwa sababu ndio
kielelezo cha utamaduni wa taifa. Aidha utamaduni ndio msingi na roho ya taifa
lolote. Nchi ambayo haina Utamaduni wake yenyewe ni sawa na mkusanyiko wa watu
wasio na roho ya kuwawezesha kujiita taifa.
|