Welcome, Guest |
You have to register before you can post on our site.
|
Online Users |
There are currently 50 online users. » 0 Member(s) | 49 Guest(s) Bing
|
Latest Threads |
Buy Vilitra 60 Mg |【Get E...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-24-2023, 11:45 AM
» Replies: 0
» Views: 0
|
How to take Cenforce50?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-19-2023, 12:59 PM
» Replies: 0
» Views: 0
|
About the Vidalista 60 Mg...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-04-2023, 04:07 PM
» Replies: 0
» Views: 0
|
What Is Vidalista 60?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-03-2023, 10:49 AM
» Replies: 0
» Views: 0
|
How to take Cenforce 100 ...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
03-29-2023, 02:37 PM
» Replies: 0
» Views: 66
|
How is Vidalista 10 Mg us...
Forum: Watunzi wa Kiswahili
Last Post: Kieth_winsett
03-27-2023, 01:26 PM
» Replies: 0
» Views: 117
|
Obtain Thesis Paper Assis...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Minny02
03-24-2023, 03:01 PM
» Replies: 0
» Views: 200
|
SEO services for sports f...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Maria Poland
03-17-2023, 01:51 PM
» Replies: 1
» Views: 223
|
NUKUU ZA KISWAHILI DARASA...
Forum: Nukuu
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:31 PM
» Replies: 0
» Views: 788
|
NECTA K4 2022
Forum: Mitihani
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:25 PM
» Replies: 0
» Views: 403
|
|
|
TASWIRA YA MWANAMKE KATIKA RIWAYA YA ROSA MISTIKA |
Posted by: MwlMaeda - 08-27-2021, 03:03 PM - Forum: Riwaya
- No Replies
|
|
Taswira ya Mwanamke katika Riwaya ya Kezilahabi (1971) Rosa Mistika
Mwandishi Kezilahabi katika riwaya yake ya Rosa Mistika anamtumia Rosa kama mhusika mkuu wa riwaya yake. Ukuu wake umezawadiwa kwa kubeba jina la riwaya husika. Rosa katika riwaya hiyo anaoneshwa kuwa alizaliwa na kukulia kwenye mazingira ya kunyanyaswa na baba yake, mzee Zakaria. Aidha, mwandishi anasawiri maisha ya Rosa alipokuwa anasomo shule ya sekondari na pia alipokuwa katika Chuo cha Ualimu. Mwandishi ametuonesha katika kazi yake hii, jinsi Rosa alivyobahatika kwa mafanikio makubwa kuhitimu mafunzo yake ya ualimu na kuajiriwa kama mwalimu. Mwisho mwandishi anamsawiri Rosa katika picha ya kusikitisha. Kwa ujumla, kwa kumpitia Kezilahabi, tunamwona mwanamke akisawiriwa katika taswira zifuatazo:
Taswira ya Unyanyaswaji wa Wanawake
Tunaposema taswira ya unyanyaswaji, tunamaanisha kwamba, mwanamke anafanyiwa vitendo au mambo ya dharau na dhuluma kwa kunyimwa haki zake za msingi. Taswira hii inajitokeza kwa kiasi kikubwa kwenye riwaya hii, ambapo tumemwona Rosa akinyanyaswa na baba yake mzazi mzee Zakaria. Mzee huyu alimnyanyasa binti huyu kwa kumpiga kila mara. Manyanyaso haya ya binti kuitwa na kupigwa yanaoneshwa na mwandishi:
…..Zakaria alichafuka, Rosa aliitwa mara moja, Rosa alikuja hali shuka ikiteremka chini. Kabla hajasema lolote alipigwa na kuanguka chini makofi yalikwenda mfululizo hata damu ikamtoka puani na mdomoni (uk. 6).
Nukuu hii inaonesha na kuthibitisha ukatili wa wazazi wa kiume kwa mabinti zao. Wazazi mithili ya mzee Zakaria huhofia kuwa mabinti zao wataharibika endapo watapewa uhuru usiokuwa na mipaka. Kisa kilichomfanya Zakaria aonekane akimpiga Rosa ni kile kitendo cha kupewa na kupokea fedha na barua toka kwa kijana wa
kiume aitwaye Charles.
Mwandishi anatuonyesha jinsi unyanyasaji huu unavyoweza kuleta athari kubwa katika malezi na makuzi ya vijana hususan wale wa jinsia ya kike. Hii inampelekea Rosa kujijengea tabia ya kumwogopa baba yake tangu alipokuwa mdogo. Woga huo umeonekana kudumu hadi kuleta mfarakano katika familia ya mzee Zakaria. Ikafikia hatua kwamba, Rosa anaamua kumuasi kabisa baba yake, kama mwandishi anavyothibitisha kwa kuandika:
Kila wakati Unatuchunga. Unafikiri utatuoa wewe. Rosa mwishowe aliyasema haya maneno. Maneno aliyopaswa kusema siku ile aliyopigwa angali msichana. Zakaria aliyapata yote. Zakaria kutunza heshima yake, alifunua mdomo. Maneno fulani yalitoka mdomoni mwake “Rosa, tangu leo wewe si mtoto wangu Tangu leo wewe si baba yangu”Rosa alidakia…. (uk. 58).
Kwa hakika katika nukuu yake hiyo, Rosa anachorwa katika taswira hii ili kuakisi hali halisi ya maisha ya jamii nyingi za Kiafrika, ambapo wazazi wanaamini kwamba, wasichana wanastahili kuchungwa ili kuwaepusha na mitego ya wavulana.
Wazazi wengi kama Zakaria, huwaadhibu kwa kuwapiga na hata kuwanyima uhuru mabinti zao kwa kisingizio kuwa eti wataharibika au kuwa na tabia mbaya. Wazazi hawa wamesahau kuwa malezi haya ni uasi na mfarakano mkubwa miongoni mwao na watoto wao. Wamesahau pia kuwa, malezi yao hayo yatarithiwa na watoto wao wa kiume kutokana na ukweli wa usemi usemao kwamba, mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
Mwanamke kama Chombo cha Starehe na Biashara
Katika riwaya ya Rosa Mistika, taswira hii inatufungamanisha na ile hali ya umalaya kwa wanawake. Mwandishi amemsawiri mwanamke kuwa ni mpenda starehe na umalaya. Hata hivyo tukiangalia kwa undani suala hili la starehe na umalaya halitendwi na mwanamke peke yake, bali linawashirikisha wanawake na wanaume. Tendo hili linaloshirikisha jinsia zote mbili, zinazopata starehe ya pamoja ingawa linaonekana kwa makusudi kabisa kusukumiwa kwa jinsia ya kike. Kwa hakika hapa panazuka suala la unyanyaswaji wa kijinsia, ya kuwa mwanamke ndiye anayeonwa kumwingia mwanamume. Pia lipo swali la kujiuliza kuwa, ni kwa nini Rosa aliitwa malaya na kupachikwa jina la Laboratory na wanachuo wenzake huko Morogoro ilhali walishiriki tendo hilo na wanaume? Jibu na ufafanuzi wa swali hili ni yale tunayoyaita katika utafiti huu unyanyaswaji wa kijinsia, ambapo mwanamume ndiye anaonekana kuwa mtakatifu siku zote.
Katika riwaya ya Rosa Mistika, Rosa amesawiriwa na mwandishi akiendesha umalaya kuanzia alipokuwa kwenye shule ya sekondari ya Rosary. Rosa alibadilika tabia alipofika kidato cha tatu baada ya
kushawishiwa na rafiki yake Thereza. Hapa mwandishi anatueleza kuwa, mwanzoni Rosa alikataa ushawishi huo wa picha za wavulana toka kwa Thereza. Hata alidiriki kukataa kuongea na wavulana kwa kudhihirisha kuwa alikuwa akiziogopa tabia za wanaume.
Hata hivyo alipokuwa kidato cha tatu, ndipo tabia ya Rosa ilipobadilika ghafla, akawa ni wa kwenda kwenye madansi, hata akakutana na mwanamume Deogratias, ambaye alileta mabadiliko makubwa katika tabia ya Rosa. Baada ya hapo, Rosa aliyavamia mapenzi kwa nguvu zote na kwa kipindi kifupi alijipatia wapenzi watano. Rosa anamweleza rafiki yake Theresa kuwa:
Unafahamu, Thereza, siku hizi ninawachezea wavulana kama mtu aendeshaye punda…
(uk. 33).
Taswira hii ya umalaya haikuishia katika ngazi ya sekondari, bali iliendelea hadi Rosa alipojiunga na Chuo cha Ualimu. Rosa anaoneshwa akibadilisha wavulana apendavyo ili mradi anapata fedha. Ndipo vijana walipoamua kumpachika jina la Laboratory kwa maana ya majaribio, kwani kijana yeyote aliweza kufanya jaribio lake la kukutana naye kimwili. Haya yalithibitishwa na mwandishi anapowachora vijana wakiangalia gazetini na Rosa akawasikia wakihojiana kuwa:
……staili hii bado sijaitumiaKwa nini bwana usiende Lab Lab kwenyewe ni wapi? (uk.5). Aidha mwandishi anabainisha kuwa Rosa aligundua kuwa alibandikwa jina la Laboratory yaani nyumba ya kufanyia majaribio. Katika kuthibitisha umalaya wa Rosa, mwandishi anamchora Rosa akivuruga ndoa ya mkuu wa Chuo cha Ualimu, Bwana Thomas. Haya yanaonekana wakati Rosa apoalikwa na mwalimu Thomas amtembelee nyumbani ilihali akijua yule ni mkuu wake wa Chuo. Matokeo ya mwaliko huo ni majuto na kupotea kwa kiungo cha mwili wa Rosa. Mwandishi anatuonyesha jinsi ukahaba huu unavyoleta madhara Rosa asemapo:
…..Rosa alipofika shuleni aliingia upesi chumbani mwake. Alipojiangalia ndani ya kioo hakuweza kuamini! Alilia kwa sauti. Alililia sikio lake. Yule mwanamke alimuuma sikio na kutoa sikio lote la nje (uk 55). Hapa taswira ya umalaya wa Rosa inahusishwa tabia za baadhi wa wanawake, wenye kuvuruga asasi ya ndoa, kwa kuwa kumekuwepo na mifarakano mingi katika ndoa nyingi. Lakini, umalaya huu umesawiriwa upande mmoja tu wa Rosa kuvuruga ndoa ya mwalimu. Upande wa mwalimu kuuvuruga ujana, kumvurugia Rosa elimu na kuuharibu mwili wa Rosa haukuongelewa, kisa ni mwanamke kutumika kama chombo cha kumstarehesha mwanamume. Hii inatuonesha taswira ya uonewaji wa jinsia ya kike na utukuzwaji wa jinsia ya kiume. Mtazamo huu unaenda kinyume na nadharia ya ufeministi inayozingatia usawa baina ya jinsia ya kike na kiume.
Mwanamke katika Taswira ya Ulaghai
Taswira nyingine tunayoipata katika riwaya ya Rosa Mistika ni ile ya Rosa kuonekana mlaghai. Mhusika huyu anachorwa akiwalaghai vijana wengi akiwemo Charles na kujipatia fedha nyingi. Vilevile Rosa ameoneshwa akiwadanganya wazazi wake juu ya matukio kama yale ya kupoteza sikio lake.
Kama vile haitoshi, Rosa anaendelea kumlaghai Charles kuwa yeye ni bikira (hajafanya ngono na mwanamume yeyote) ili waweze kuoana. Ulaghai huu unathibitishwa katika majibizano kati ya Rosa na Charles wakati wakiwa chumbani kama ifuatavyo:
Charles siyo leo, Mpaka siku tutakayooana. Afadhali tungoje siku yenyeweHaiwezekani…. Vumilia kidogo muda umekaribia. Ninakuomba usiniharibu kabla ya muda. Charles — mimi ni bikira (uk. 78).
Ulaghai huu unaofanywa na Rosa una athari kubwa mara inapogundulika kuwa msichana si bikira kama alivyotegemewa na mchumba wake. Kwa tabia kama hii ya ulaghai unaweza kutuletea maswali ambayo yanahitaji maelezo ya kina, Je ni kwa nini mwanamume haonekani mlaghai anapomdanganya mwanamke kuwa atamuoa na asimuoe? Je, ubikira wa mwanamke ndicho kipimo cha yeye kuolewa? Je, kuna uhalali gani kwa mwanamume kukutana kimwili na mwanamke kabla ya kufunga ndoa? Je, ni kwa
nini mwanamume asipimwe na mwanamke kwa kutumia kigezo cha ubikra? Maswali haya na mengine mengi yatapatiwa ufumbuzi katika sura ya tano.
|
|
|
TASWIRA YA MWANAMKE KATIKA RIWAYA YA NYOTA YA REHEMA |
Posted by: MwlMaeda - 08-27-2021, 02:47 PM - Forum: Riwaya
- No Replies
|
|
Taswira ya Mwanamke katika Riwaya ya Mohamed (1976) Nyota ya Rehema
Nyota ya Rehema ni riwaya iliyoandikwa na Mohamed (1976). Riwaya hii inamsawiri
na kumjadili Rehema ambaye ndiye mhusika mkuu. Riwaya inatuonesha jinsi Rehema
alivyozaliwa na kukulia kwenye unyanyaswaji mkubwa wa mama yake mzazi kwa
sababu alizaliwa mweusi tititi, wakati ambapo wazazi wake wote wawili ni wa
asili ya Kiarabu. Mwandishi anaelezea maisha ya jadi katika visiwa vya Zanzibar
kabla ya mapinduzi ya mwaka 1964 yaliyomng’oa Sultani. Kuzaliwa kwa Rehema
kulisababisha mfarakano baina ya wazazi wake wawili, ambapo mama yake Rehema,
bi. Aziza alipewa talaka na kuhamishiwa nyumba nyingine. Akapewa kisogo na
Fuad: ambaye alioa mke mwingine aliyeitwa bi. Adila. Baada ya kifo cha mama
yake, Rehema alirejea na kuishi kwa baba yake pamoja na mama yake wa kambo.
Maisha ya malezi ya mama wa kambo yalikuwa magumu mno kwa Rehema. Rehema
aliamua kuyatoroka maisha haya, hatimaye alijikuta akiokolewa na Sulubu huko
msituni. Baada ya kukaa na Sulubu kwa muda, Rehema aliamua kukimbilia mjini ambako aliona raha na taabu
za dunia. Kwa kifupi Riwaya ya Nyota ya
Rehema imemsawiri Rehema katika taswira mbalimbali zinazomfanya mwanamke
awe kiumbe duni na dhalili.
Taswira ya Mwanamke kama Chombo cha
Starehe
Taswira
mojawapo ni ile mwandishi aliyomchora mwanamke kama chombo cha kumliwaza na
kumstarehesha mwanamume. Mwandishi anatuchorea tabia dhalimu walizokuwa nazo
baadhi ya wanaume, ikiwa ni pamoja na kuwabaka mabinti wanaokataa kufanya ngono
nao. Haya yanathibitishwa na mwandishi wakati Rehema aliposikika akisema:
….Ngojea
kwanza bwana Mansuri; Rehema alisema, huku akishindana kuuzuia mwili mzito
uliokuwa ukimwelemea, Unataka kufanya nini? Usijifanye mtoto, Rehema unajua
mimi nakupenda, alisema Mansuri sauti yake ikiwa imebadilika. Rehema akijibu,
mimi si… sitaki … (uk. 65).
Mansuri
alitumia nguvu na uwezo wake aliokuwanao alipokuwa juu ya Rehema, ingawa Rehema
alijitahidi kujizuia asifanyiwe tendo kama hili. Lakini hatimaye Rehema
anabakwa na Mansuri.
Aidha,
mwandishi anatuonyesha jinsi Rehema alivyotumiwa na Mansuri ili kumfurahisha;
ingawa alikuwa ni mfanyakazi wa ndani wa Mansuri. Mansuri alipomletea Rehema
zawadi ya nguo, alimbusu kwa shauku kuu ikiwa ni ishara ya kumtaka kimapenzi.
Hapa mwandishi anatuonyesha Mansuri akimwambia Rehema:
…Ah,
hiyo ndiyo iliyokuchukua kuliko zote; huku akinyanyuka na kumsogelea Rehema.
Alimshika mikono yote miwili na kwa ghafula, bila ya Rehema kutarajia, Mansuri
aligusisha midomo yake juu ya shavu la Rehema, na kuondoa. Akisema umeonaje
Rehema, ugumu upo katika mara ya kwanza na ya pili tu. Sasa nenda kajitazame
kiooni….(uk. 63).
Hayo
ni baadhi ya matukio yanayochora hali ya matendo machafu na ya kudhalilisha
anayotendewa mwanamke katika fasihi ya Kiswahili. Mwanamke anachorwa kama
chombo cha starehe na kiburudisho kwa mwanamume. Hapa mara moja tunaoneshwa
kuwa mwanamke hapati starehe yoyote ile mbali na kupata karaha kutoka kwa
mwanamume huyo. Hapa yanajitokeza maswali kwa mtafiti katika suala zima la
mapenzi na kumwona mwanamke kama chombo cha starehe. Hii ni kutokana na ukweli
kwamba, kitendo hiki kinachowashirikisha jinsia zote mbili zinatumia tendo hili
liitwalo tendo la ndoa kufurahishana, kustareheshana na kuoneshana mapendo.
Hivyo waandishi hawana budi kuandika ukweli juu ya suala hili kwani jinsia zote
zinastareheshana na sio mwanamke pekee.
Taswira ya Umalaya
Taswira
hii ya umalaya unaofanywa na wanawake kujiuza miili yao ili kujipatia riziki
zao za kila siku ndiyo tunayoiongelea hapa. Kwa mfano mwandishi amewachora
Rehema, Kidawa na Ruzuna wakiwa katika harakati za kufanya umalaya ili waweze
kukidhi haja zao.
Mwandishi
anamsawiri Rehema akiendesha ukahaba wa hali ya juu mara alipoacha kazi kwa
Mansuri. Hapa mwandishi anathibitisha umalaya wa Rehema asemapo:
….Palikuwa
na vijana kemkem wa kitajiri waliomwomba aishi naye… Alitembea nao na kufanya
nao Ukahaba na baadhi yao alikaribia kuwapenda. Walimchukua hotelini, Vilabuni
na michezoni ambako wenzake walikuwa wakikulilia. Walimwambia wanampenda,
akaona ladha na maneno yao walimridhi aliyoyataka, akadeka na upole wao…..(uk.
78).
Hivyo
taswira ya umalaya inasababisha ugomvi kati ya wanaume, ambapo mhusika Chiku aliwagonganisha
wanaume hao na kuwafanya wagombane. Mwandishi anatueleza tukio hili kama
ifuatavyo:
…muda
si muda, wanaume wawili waliingiana maungoni. Mishindo ya ngumi ilisikika
waziwazi…. Yule bwana aliyeachwa uchi alipokimbilia kuficha sehemu ya siri,
adui yake alimpiga mweleka akamtupa chini (uk. 56-57).
Hapa
wahusika wanawake wanasawiriwa kuwa malaya na chanzo cha ugomvi kati ya
wanaume. Hili linasababishwa na kuyageuza mapenzi na tendo la kujamiana liwe na
sura ya kibiashara. Taswira hii inamsukuma mtafiti kujiuliza kuwa, Je wale
wanawake wanaowahonga wanaume fedha kwa ajili ya kufanya nao ngono watawekwa
katika kundi gani? Je wakati wa biashara hizo za ngono, jinsia zote hazifaidiki
kwa namna yoyote ile katika kujamiana huko? Maswali haya yatafumbuliwa katika
sura ifuatayo.
Taswira ya Wanawake kupenda Starehe
na Raha
Taswira
hii imejitokeza katika riwaya Nyota ya Rehema, Rehema amesawiriwa kuwa mhusika
asiyethamini kazi kuwa ndio msingi wa uhai na utu wa binadamu. Rehema anaamua
kuacha kazi kwa Mansuri na Rozi baada ya kuona kuwa anajitesa, mwandishi
anatueleza:
….Rehema
hakuona taabu ya kukosa kazi kwa Mansuri na Rozi na kusema kweli alishukuru
mapenzi aliyoonyeshwa yaliuviza unyonge wake; alitanabahi kuwa umbo lake ni
rasilimali yenye kutumainika. Maadam mwanamume yeyote aliyepishana naye, akiwa
topasi na ufagio wake au mtaalam wa kalamu yake wote hawakuweza kujizuia
wasigeuke kumtazama (uk. 78).
Kuwepo
kwa wanawake wanaoishi pasipo kufanya kazi halali kunadhihirisha dhana kwamba
jinsia ya kike ni mali mbele ya jamii inayohusudu kuuza utu kwa fedha.
Halikadhalika jinsia ya kiume nao wapo wanaotumia utu wao ilimradi kupata
mahitaji yao muhimu hawa ni wale wanaolelewa na wamama wenye pesa wanaojiita shuga mami. Hivyo sio wanawake tu
wanaopenda starehe na anasa kama anavyobainisha mwandishi. Hata hivyo, tofauti
za kimaumbile kati ya mwanamke na mwanamume zinaifanya jinsia ya kike ijione ni
bora na yenye thamani katika jamii hasa katika mfumo wa uchumi wa soko huria.
Taswira ya Mapenzi na Pesa kwa
Wanawake
Wapo
watu ambao wakipata fedha wanaweza kununua kitu chochote hapa duniani. Wanaweza
kununua mapenzi ya mtu, raha ya kila aina na hata ya kuupata utu wa mtu. Watu hawa
hawana imani ya kuwa hakuna uhusiano wowote ule kati ya fedha na mapenzi. Kwa
mfano, Fuad alikuwa tajiri aliyeamini kuwa Aziza atapata kila alichotaka, yaani
mambo yatakuwa sawa. Mwanamume huyu alikosea! Ilionekana kuwa fedha zilimfanya
Fuad asahau kwamba Aziza alimtaka yeye na sio fedha zake. Pia mwandishi
amemchora mwanamke akijiuza ili kupata pesa za kujikimu kimaisha. Kwa mfano,
wahusika kama wale akina Kidawa, Ruzuna na Chiku walimwingiza Rehema kwenye
maisha ya tamaa ya fedha na kujiuza pasipo binti huyu kujua hali halisi ya
dunia hasa kwenye upande wa mapenzi. Haya tunayaona mwandishi alipoandika:
Mwandishi
anasema, “Palikuwa na vijana kemkem wa kitajiri walimwomba Rehema waishi naye,
tayari kukidhi haja zao zote. Alitembea nao na kufanya nao mahaba, na baadhi
yao alikaribia kuwapenda (uk. 78).
Hali
hii aliendelea nayo akiamini kuwa fedha na mahaba vinakwenda pamoja, kwamba utu
na penzi halisi si vitu vya haja. Hadi alipochukuliwa na Bikiza ndipo
alizikumbuka zile siku nne alizoishi kwenye kibanda cha Sulubu. Ndipo
alipogundua kuwa kutembea kote huko na wanaume wote hao hakukutana na mwanamume
aliyemtosheleza na kumridhisha kama Sulubu.
Mapenzi
ya pesa yanaonekana kwa mhusika Karimu hakuwa na mapenzi ya dhati kwa Salama
bali alipenda pesa zake tu. Mapenzi ya Karimu na Salama hayawezi kulinganishwa
na yale ya Sulubu na Rehema, ambao walipendana kwa wema na sio fedha. Sulubu
alimsaidia Rehema bila tamaa isipokuwa kwa wema. Aidha, hakumpata hata mmoja
aliyekaa naye faraghani muda mfupi tu asidhihirishe uchu wake wa mapenzi
isipokuwa Sulubu.
Katika
sehemu hii, Rehema na Ruzuna wanawakilisha pande zote mbili za mapenzi
yanayomsibu mwanamke, yaani mapenzi ya dhati na mapenzi ya ulaghai ambayo ni ya
uongo. Rehema alichanganya mapenzi na tamaa ya fedha. Ndipo baadaye alizinduka
na kufahamu mapenzi ya kweli na hapo ndipo alipoamua kuishi na Sulubu. Kwa
upande mwingine Ruzuna alianza na mapenzi ya ukweli kati yake na Karimu lakini
baada ya kudanganywa na wanaume, akaamua kulipiza kisasi na kuingia kwenye
mapenzi ya uongo ili afurahi kuwaona waanaume wanavyopigana, ambapo tunaweza
kusema kuwa alifanya makosa makubwa.
|
|
|
TASWIRA YA MWANAMKE KATIKA RIWAYA YA SHIDA |
Posted by: MwlMaeda - 08-27-2021, 10:47 AM - Forum: Riwaya
- No Replies
|
|
Taswira ya Mwanamke katika Riwaya ya Balisidya (1981) Shida
Riwaya ya Shida imeandikwa na mwandishi wa kike aitwaye Balisidya N. kilichochapishwa mwaka 1981. Riwaya hii inayasawiri
maisha ya jamii za Watanzania na inaonyesha matatizo jamii hizi zinavyokumbana nayo. Katika riwaya hii, mhusika mkuu Matika anapambana na madhila ya mfumo dume ambayo yanamfanya awaasi wazazi wake. Aidha, riwaya hii inamsawiri mhusika mkuu katika taswira mbalimbali kama vile mwanamke kama pambo la mwanamume, mwanamke kama chombo cha kumfurahisha mwanamume, mwanamke kama malaya na mwanamke kama mtu wa kunyanyaswa. Katika riwaya hii mwandishi ametuonesha tabia
ya pekee kwa baadhi ya wanawake kuwa na moyo wa huruma kwa vijana wa jinsia zote mbili.
Kama tukiliangalia jina la riwaya Shida tunaona picha ya riwaya nzima. Shida hapa sio jina la mhusika au mtu wa kawaida tu, bila shaka ni taswira inayoimulika dhamira ya Balisidya tofauti na ile ya binadamu wa kawaida. Ni mtu anayepambana na matatizo kuanzia utotoni hadi utu uzima. Shida ni msimbo wa Kihemenitiki wenye kuwaashiria wanawake kuwa kuna ukandamizwaji na uonewaji wa kijinsia miongoni mwao, kwa masilahi wanaume.
Mwanamke kama Pambo na Chombo cha Starehe
Mwandishi wa riwaya hii kwa kiasi fulani anatuonyesha kuwa bado mwanamke amebaki katika nafasi ya chini katika ujenzi wa jamii mpya. Mwanamke bado anaonekana kama pambo na chombo cha kumfurahisha mwanamume. Mwanamke katika riwaya ya hii bado
hajapewa uhuru wa kuchagua mwanamume anayempenda kwa dhati. Mwanamke hususan mabinti bado wangali wamefungwa na mila potofu za kuchaguliwa wenzi wao wa kuwaoa. Matokea ya kulazimishwa huko tunayaona pale Matika analazimika kutoroka nyumbani kwao, kwa sababu baba yake kumlazimisha aolewe na kijana wa familia ambayo mzazi wake ameichagua bila hata kumshirikisha kwa kumuuliza kama anampenda.
Picha ya mwanamke kuonekana kama pambo na chombo cha kumstarehesha mwanamume tunaiona pale tunapoelezwa kuhusu maisha ya Shaibu. Mwandishi anasema:
…Shaibu alikuwa akifanya kazi katika kiwanda cha kamba hapa mjini. Alikuwa amepanga katika nyumba moja iliyopo Manzese, Alikuwa na vitu maridhawa pamoja na uhuru wake. Wasichana wengi walimtembelea wakabadilishana nafasi kama alivyopenda yeye. Wasichana hawa waliijaza nyumba ya Shaibu kila leo, kila saa alipokuwa hayupo kazini, wakamstarehesha usiku na mchana (uk. 29).
Lakini uhusiano huu baina ya wanawake na wanaume haukuzuka hivihivi. Wenyewe umeshikamana na mfumo wa kijamii, kiuchumi pia kuzuka kwa miji na utamaduni wake mpya pamoja na maisha ya kibiashara yanayowaunganisha watu kwa kiungo cha pesa, upanikanaji wa pesa umekuwa mgumu sana tena umechangiwa na hali ngumu ya maisha. Pesa imekuwa ndio kitambulicho cha kila kitu, kama huna pesa ni wazi kuwa utopata chakula, mavazi, malazi na mahitaji mengine muhimu, hivyo wasichana katika riwaya hii wako radhi kujiuza miili yao ili kupata chakula kama tuelezwavyo:
…kwa kawaida wasichana hawa hufuata kipato kama huna basi mpige bia moja, mpe
semadarina starehe yote ni yako….. (uk. 30).
Mwandishi anatuambia kuwa wasichana wa siku hizi wako radhi kujiuza ili mradi wapate chakula na vinywaji, wako tayari hata kama una kipato kidogo kuwapata si kazi ngumu.
Taswira ya Unyanyaswaji wa Mwanamke
Hii ni taswira iliyotamalaki sana katika riwaya ya Shida. Shida ni msichana mdogo aliyemaliza darasa la saba. Ana sifa za ziada ukilinganishwa na wasichana wengine wa rika lake. Jina lake ni la kiishara na la picha zinazompata Shida ni ishara ya matatizo ya vijana kama Shida. Pia ni picha ya matatizo yanayotokana na harakati za vijana kutaka kuyabadili maisha yao. Kazi hii inatueleza maisha kuwa maisha mazuri yapo mjini suala ambalo hata Shida mwenyewe alitamka waziwazi pindi aliposema:
……nimezoea maisha ya fedha na starehe ….( uk. 9).
Mwandishi Balisidya anaonyesha unyanyasaji katika ngazi mbalimbali kama ulivyojitokeza katika riwaya ya Shida. Unyanyasaji huo unafanywa na wanaume ambao wanadhani wanayo mamlaka juu ya wanawake. Dhana hii imepewa nguvu zaidi na mila na
desturi zinazomfanya mwanamke asiwe na haki ya kutoa hoja zao hata katika mambo yanayomhusu.
Mhusika Shida analazimishwa na baba yake aolewe na kijana ambaye si chaguo lake. Shida alitakiwa kukubali bila kutoa hoja au ushauri wowote, kama baba yake anavyotuthibitishia anapomwambia Shida kuwa:
Wanaleta mahari ukoo wa Mbukwasemwali, nasi tumeamua kupokea mahari hiyo. Sipendi ubishi utaolewa na Njasulu. Tunafanya hivi kukuokoa na janga, maadamu sasa huna kazi wala chochote, usije ukaingia uhuni ….. (uk. 3).
Baba Shida alidhani kuwa Shida atakubaliana naye, lakini Shida hakuwa tayari kuolewa. Kutokana na shurutisho hilo aliamua kuondoka huku akiazimia kufanya safari ya kuusaka uhuru wa kujiamulia mambo yanayohusu maisha yake. Shida hakukubali kunyanyaswa na mfumo dume ingawa baba yake aliona ni njia ya kumwepusha na janga la kupotea. Hapa mwandishi amempa mwanamke uwezo wa kuyakimbia matatizo sio kuitikia tu kila kitu unachoambiwa na mwanamume. Mtafiti anazua maswali kwamba: Je, tatizo hili la wanawake kulazimishwa kuolewa na mwanamume asiyemtaka limetatuliwa vipi? Je, suala la kukimbia matatizo na kuanza maisha mapya ni suluhisho? Je kuyakabili matatizo yanapokukabili sio suluhisho la kweli? Kwa hakika maswali haya na mengine yanahitaji suluhisho la utafiti huu.
Unyanyaswaji mwingine unaosawiriwa na Balisidya katika riwaya yake hiyo ni kuwa wanawake hawashirikishwi katika maamuzi mbalimbali ya kifamilia. Mathalani, mama Shida hakushirikishwa kabisa katika suala la ndoa ya binti yake. Aidha, mama Shida
alipata kipigo toka kwa mumewe baada ya binti yake kutoroka. Sababu ya mwanamke huyu kupigwa kwa upande mmoja ni kwamba, inasemekana kuwa alionekana kushiriki katika kumtorosha binti yake na kwa upande mwingine ni unyanywaswali wa kuwa mwanamke hana uwezo wa kuhimili miguvu ya mwanamume. Mwandishi anathibitisha haya asimuliapo:
Huku nyumbani baba yake alipata habari, Alilaani na kugombana na mkewe hata Akampiga Sana (uk. 6).
Unyanyasaji wa wanawake unasawiriwa na mwandishi kwa kuwachora wanawake kama viumbe wanaozalishwa au kuzaa watoto kisha kutelekezwa na waume zao. Katika riwaya ya Shida, mke wa Machupa anatelekezwa kijijini ambapo Machupa anaenda jijini
kutafuta kazi. Hata baada ya kupata kazi, Machupa haijali familia yake, anamnyanyasa mke wake hatimaye anampatia talaka ati amezaa watoto wengi. Machupa anathibitisha azma yake kama inavyojitokeza asemapo:
Tatizo langu……ni matoto a-a tatizo lilikuwa matoto mengi mno nikamtupilia mbali yule mama na mizigo yake ya kila siku. Angekuwa pekee yake, loo (uk. 62).
Mwanamke bado yungali ananyanyaswa, tena kwa makosa ambayo si yake. Mfano wa Machupa hapo juu anamfukuza mtoto wake kisa amezaa watoto wengi ambao hawezi kumudu kuwalea. Machupa anadai wingi wa watoto ni kosa la mkewe, naye akidhani
hakushiriki katika kuwaumba hao watoto. Huu ni uonevu mkubwa unaofanywa na wanaume kumgandamiza mwanamke. Hali hii imeshamiri hadi hii leo kwamba, mwanamke anapozaa watoto wa kike watupu, mumewe haridhiki ilhali ndiye mwenye
kumwezesha mkewe kuzaa mtoto/watoto wa kiume. Vilevile mwanamke anapokosa uzazi mwanamume humwacha na kutafuta mwanamke mwingine ili afanikiwe kupata mtoto.
Dhuluma hii huwadhalilisha wanawake kila iitwapo leo na bila kikomo. Kwa upande mwingine, huku kutokuwa na uhuru kwa mwanamke, na kuwafanya kuonekana kwao kama mapambo na vyombo vya starehe kunawarudisha wanawake nyuma na vilevile kunarudisha nyuma juhudi za ujenzi wa jamii. Hivyo kama mwanamke na mwanamume wote wangetumika sawa na wangekuwa bega kwa bega katika kujenga uchumi wa nchi.
Vitendo kama vya Machupa vinamnyanyasa na kudhalilisha mwanamke kwa kiasi kikubwa. Wanawake wamekuwa wakiachiwa majukumu ya kuwalea na kuwatunza watoto katika familia zetu. Hii dhna inakwenda sambamba na ufeministi wa kiafrika unaotenga
majukumu kati ya mwanamume na mwanamke katika jamii. Wazazi wenzao wa kiume hudiriki kutumia kipato chao cha ziada kwenye masuala yasiyo ya msingi kama vile ulevi, ukahaba, uasherati, na kadhalika na kuziacha familia zao zikiwa na hali duni ya kiuchumi. Suala hili litashadidiwa kwa undani katika sura ifuatayo.
Taswira ya Umalaya kwa Mwanamke
Taswira ya umalaya tunaipata katika Riwaya ya Shida. Mwanamke anasawiriwa akiendesha umalaya huko jijini. Matika alipofika jijini Dar es Salaam aliamua kutafuta njia muafaka za kukidhi mahitaji yake, ingawa alikuwa akifanya kazi katika baa, hakuweza kupata pesa inayokidhi mahitaji yake na ndipo alipoamua kufanya umalaya na kujikuta ana mimba bila kumtambua aliyempatia ujauzito huo. Umalaya huu unathibitishwa na maelezo ya wafanyakazi wenzake walipohojiwa na Chonya, wao walimjibu:
….kazi yetu ilivyo, mtu hawezi kujua ni nani amemnasa. Kwa kuwa Mwarabu, Mzungu, Mbantu wote huwa tunakubali ….(uk. 63).
Maelezo haya yanatushawishi tukubaliane na usawiri huu kwani unaakisi hali halisi iliyopo katika jamii yetu. Hali hii imemfanya mwandishi wa riwaya hii amsawiri mhusika wa kike katika hali ya umalaya wa kutisha ilhali ni mwandishi wa kike tulitegemea kuwa angepinga taswira hii ya kumdhalilisha mwanamke mwenzake lakini kumbe nao wapo mstari wa mbele katika kumdunisha mwanamke.
Taswira ya Wanawake ya Upendo na Huruma
Taswira ya kumchora mwanamke mtu mwenye upendo na huruma inaonekana kukubalika katika jamii. Taswira hii inajitokeza katika riwaya ya Shida, ambapo mama Upendo anachorwa kuwa na upendo na huruma kwa Chonya. Mama Upendo anamshauri Chonya juu ya maisha mema; anamshauri ajiwekee fedha benki na ajinunulie vitu vitakavyomsaidia katika maisha yake. Mwandishi anathibitisha upendo huo anapomchora mama Upendo akimweleza Chonya kuwa:
Mshahara wako hautakutosha kwa mahitaji yote ya mji huu. Ndiyo maana tumekupa chumba, chakula maji na umeme bure…. (uk. 29). Katika maelezo haya, mama Upendo anatekeleza wajibu wake wa malezi kwa vijana. Mama Upendo amesawiriwa kuwa mwenye huruma na hekima kwa sababu anamlea Chonya, pia anamwasa juu ya maisha ya jijini wakati Chonya alipoamua kuacha kazi. Mama
Upendo alimuasa Chonya akisema:
….Mji huu una anasa nyingi tena zisizo na faida. Mimi nakuonya Chonya jiwekee akiba kidogo, endelea kama ulivyoanza, usipoteze pesa yako bure ….umri wa kuoa ufikapo chagua binti asiyependa mambo ya mji usiyoyaweza mkaanze maisha pamoja….. (uk. 30).
Hapa inathibitika wazi kuwa wanawake wana jukumu kubwa la kuilea jamii yetu, hivyo Chonya anaasa katika uchaguzi wake asikosee kwani kima chake ni kidogo hivyo awe mwangalivu katika kumpata mwenza atakayempenda kama alivyo na sio kufuata pesa. Jamii ya leo mapenzi ya pesa yameshamiri sana, kuna baadhi ya wanawake wanaopenda hela kuliko utu.
|
|
|
SHAIRI: NAMTAKA BABA YANGU |
Posted by: MwlMaeda - 08-27-2021, 10:36 AM - Forum: Ushairi
- No Replies
|
|
NAMTAKA BABA YANGU
Wenzangu nikiwaona, na baba zao nyumbani,
Moyo unanisonona, Kama wao natamani,
Natafuta kila kona, nikamtia machoni,
Mama, baba yuko wapi? Namtaka baba yangu.
Wenzangu hupewa pipi, akirejea nyumbani,
Nilichokosa ni kipi, nimkose duniani?
Baba alienda wapi, na hayumo kaburini,
Mama, baba yuko wapi? Namtaka baba yangu.
Yananifika madhila, kubakia ukiwani,
Tazama ninapolala, mithili ya jalalani,
Ninakosa hata ndala, nisitiri miguuni,
Mama, baba yuko wapi? Namtaka baba yangu.
Lakini Sina makosa, sema Nina kosa gani?
Ikiwa alikukosa, na mie kanitendani,
Mbona wanitia visa, viso vyangu duniani?
Mama, baba yuko wapi? Namtaka baba yangu.
Vilaka najibandika, vinisitiri mwilini,
Kiatu kinanicheka, ati mie masikini,
Ee mama fanya haraka, niondoke ukiwani,
Mama, baba yuko wapi? namtaka baba yangu.
Kaditama nimefika, baba ninamtamani,
Yaniondoke mashaka, nifurahi maishani,
Kuishi nae nataka, nikae mbali kwa nini?
Mama,baba yuko wapi, namtaka baba yangu.
Mtunzi Filieda Sanga
Mama B
Mabibo Dsm
0753738704
|
|
|
USAWIRI WA MWANAMKE KATIKA RIWAYA YA HIBA YA WIVU |
Posted by: MwlMaeda - 08-27-2021, 08:00 AM - Forum: Riwaya
- No Replies
|
|
Usawiri wa Mwanamke katika Riwaya ya Mwanga (1984) Hiba ya Wivu
Riwaya ya Hiba ya Wivu imeandikwa na mwandishi wa jinsia ya kike bi. Mwanga. Riwaya hii imejikita katika kuonesha mapenzi aliyonayo mhusika mkuu Farida kwa mumewe. Aidha, mapenzi haya yanaegemezwa kwenye wivu mkali aliokuwa nao Farida. Penzi limesababisha mchomo mkali wa wivu moyoni mwa Farida Kimambo. Wivu huo ulimfanya Farida atoke nyumbani kwake mbio kwenda kumsaka mumewe usiku mzima. Kitendo hicho kikazaa janga lililotia dosari ndoa yake, akajikuta mikononi kwa kijana Ray kimapenzi lakini bila ridhaa yake Farida. Kumnasua Ray ikawa kazi kwani alishampenda na akatamani awe mke wake. Ray akawa mwiba 68 mguuni mwa Farida. Vioja alivyofanya Farida ili kuokoa ndoa yake na kutoa mwiba uliomchoma (Ray) kwa upande mmoja, vinasikitisha lakini kwa upande mwingine vinachekesha na kufurahisha. Vioja hivyo ni pamoja na jitihada za kutaka kurudi kwa mumewe akiwa kama mtu aliyetekwa nyara kitu ambacho hakikufanikiwa na hatimaye ukweli ukajulikana.
Mwanamke kama Kiumbe Mwenye Wivu
TUKI (1981) wivu ni hali au tabia ya mtu kusononeka au kukasirika muda mtu amuonapo mpenzi au rafiki yake ana uhusiano wa mapenzi na mtu mwingine. Wivu katika Hiba ya Wivu unafanywa na mhusika Farida mara anapoona mumewe kachelewa kurudi nyumbani na kuamua kumfuata ili akamfumanie. Mwandishi anamwonesha Farida akisema:
Leo nitamfuata hukohuko nikamfume. Hoteli zote anazopendelea kwenda nazifahamu, haitakuwa kazi kumpata. Tena saa hizi bila shaka kaishalewa; na kaanza upuuzi wake. Atashaa! (uk. 3).
Hali kama hii inaoneshwa na mwandishi kwamba mwanamke ni mtu mwenye wivu uliopita kiasi. Wivu huu unaonekana ukimnyima Farida usingizi kama mwandishi alivyosema:
Farida binti Kimambo akiwa kitandani kwake kajilaza kifudifudi, mikono yake miwili usoni huku akibubujika na machozi, aliyaona maisha machungu mfano wa shubiri.
Kila alipojaribu kutuliza mawazo ili apate usingizi, ilishindikana. Machozi yalizidi kutiririka na kulowesha mto (uk. 2).
Mwandishi anaendelea kuonesha hali hiyo kwa kuandika kuwa:
….Mwanamume huyu; biashara ya saa sasa ndio imekuwa nongwa” aliendelea kuwaza. “Miezi sita sasa Ihucha hatulii, kutwa nzima kwenye biashara mpaka usiku, biashara, biashara, biashara tu. Biashara gani hiyo… (uk. 5).
Kitendo hiki kinazua janga lililoleta mashaka katika familia ya Ihucha. Panatokea hekaheka zenye kusababisha dosari zenye kuitia kasoro ndoa yao changa. Farida anajikuta akinaswa katika mtego wa mapenzi na kijana Ray, ambapo inakuwa kazi kubwa kwake kujinasua. Ndipo inambidi Farida atumie ulaghai ili asijepewa talaka na mume wake wa ndoa. Hali hii ya wivu inatuunganisha na hali ya ulaghai ambayo tutaiangalia kama tabia inayomtawala mwanamke kila iitwapo leo.
Mwandishi wa riwaya hii amejitahidi kukwepa kumsawiri mwanamke katika hali ya kudhalilika akilinganishwa na yule wa riwaya ya Shida.
Pamoja na ukwepaji huo, bado kuna taswira kadhaa zilizojitokeza katika riwaya hii. Taswira hizi ni zile mwandishi alizozichora kama utegemezi wa mwanamke kwa mwanamume na pia mwanamke kuwa kiumbe adhimu na laghai.
Taswira ya Mwanamke kama Tegemezi Taswira ya utegemezi wa mwanamke kwa mwanamume imedhihirishwa na mhusika Farida. Farida
alitegemea sana ushauri wa Ray katika kutafuta suluhisho la matatizo yake. Alimtegemea Ray amsaidie kujinasua kutokujulikana kwa mumewe juu ya hila na matendo yake maovu. Hata hivyo, mwandishi anatuambia:
Lakini angewezaje kumtegemea Ray kwa kila jibu wakati aliyeulizwa ni yeye? Ray angeweza kubuni maswali yote ya Ihucha? Isitoshe Ray Alimwambia ‘akili kichwani mwako’ wakati anamuaga… (uk 63).
Mwandishi anatuonyesha kuwa jamii yetu bado inamwona mwanamke kama kiumbe kisichofikiri na chenye kumtegemea mwanamume katika kila jambo.
Kwa upande mwingine Mwanga anatuonesha taswira ya mwanamume iliyo tofauti kabisa ya kwamba wanaume wanawathamini sana wanawake, na kutokana na thamani hiyo, wako tayari kuwasaidia kuliko ilivyo kwa wanaume wenzao. Mwandishi anaonyesha haya aandikapo:
Lakini kumbe jamaa hakuwa na ugonjwa wala hakukatazwa kunywa bia. Alikuwa kachacha kama mchuzi wa juzi, Fedha aliyokuwa nayo ilitosha kumshibisha na kumywesha Fatuma tu…(uk1).
Usawiri huu unamfanya mwanamke ajione ana haki ya kutendewa fadhila na mwanamume, hata mwanamume kuamua kijinyima ili mradi aweze kumfurahisha mwanamke. Hii hupelekea wanawake kubweteka na kubaki kuwa tegemezi kwa wanaume. Hali hii wanaume wanaichukua kama silaha kwao ya kuwanyanyasa wanawake.
Mwanamke Kama Mlaghai Mwanamke kama laghai katika riwaya hii imebainika pale Farida alipomlaghai mumewe kuwa ametekwa nyara, wakati sio kweli. Pia pale Ray anapomwambia Farida kuwa amepata wazo zuri la kujifanya kuwa ametekwa nyara, Ray anaongea maneno yafuatayo:
Bwana Ihucha: Mkeo tumemteka nyara jana usiku. Kwa usalama wa maisha ya mke wako, unatakiwa utoe shilingi elfu hamsini kabla ya saa tano kesho asubuhi. Hizo fedha zifunge vizuri, uzipeleke bonde la mkwajuni chini ya mbuyu. Kumbuka tupo wengi usijidanganye kijificha na kutuwinda… (uk. 19).
Tunaoneshwa Farida akiafikiana na wazo la Ray ili aweze kuinusuru ndoa yake, na hivyo alikuwa yuko tayari kwa lolote litakalotokea. Mwandishi anaandika: Farida hakuwa na njia nyingine isipokuwa kukubali. Aliamini kuwa Ihucha hatoshindwa kutoa hizo pesa. Lakini hakuwa na uhakika wa kurudishiwa pesa hizo na Ray. (uk. 21).
Mwanamke kama chombo cha starehe Farida anaonekana akiwa nyumbani kwa Ray na akijifanya ametekwa kwa siku kadhaa huku
wakipeana starehe akimwacha mumewe Ihucha katika dimbwi la mawazo na mahangaiko ya usiku na mchana. Taswira hii imejitokeza pale Ray alimposema:
Hallo Darling, bado unasononeka tu? Ray alijitapa kwa lugha za kizungu kwa uchangamfu huku anamshika Farida begani….. Kesho ukifika yule Mnyaturu atakufanyia pati ya kukupa pole kwa kutekwa nyara. Atakufaidi! Farida alijibu “Basi bwana yamekwisha! Usikasirike bure” Farida alikuwa ametambua kosa alilofanya. Alizungumza kwa sauti ya kubembeleza ili mpango isivurugike….. (uk. 22). Hapa mwandishi anamchora mwanamke kama chombo cha starehe ingawa Farida alifanya hivyo ili kutimiza azima yake ya kurudi kwa mumewe. Kitendo cha Farida kumbembeleza Ray na kumpa kila alichohitaji kinaonesha udhaifu wa mwanamke kwani angeweza kutumia fikra na mawazo yake binafsi kutatua shida yake.
Hitimisho Malengo yetu katika sura hii ni kuwakilisha data kama zilivyoonekana katika vitabu teule vya riwaya vilivyotumika katika utafiti huu. Katika uchambuzi wa riwaya hizi mtafiti ameweza kubaini taswira mbalimbali katika kumchora mwanamke katika kazi zao. Mojawapo ya taswira hizo ni mwanamke kama chombo cha starehe, mwanamke kama tegemezi, mwanamke kama malaya na mwanamke kama mtu mwenye wivu. Taswira hizi zimebainishwa na waandishi wa jinsia zote mbili. Katika sura ya Tano tunachambua data na kutoa matokeo ya utafiti huu ili kuona ni kwa kiasi gani waandishi 72 hawa wameweza kufanana na kutofautiana katika kumchora mwanamke katika kazi zao.
Hapa msomaji ama mhakiki atajiuliza ni kwa nini mwanamke anakuwa dhaifu na kusawiriwa namna hii? Je, mwanamke afanye nini katika kujinasua na kujitoa katika wimbi hili lililomsibu na kusawiriwa na mwandishi? Tunapojaribu kutoa majibu kwa maswali haya katika tasnifu hii, ndipo tutakapopata suluhisho na hitimisho la tasnifu hii.
Aidha tafiti nyingine zinapendekezwa zifanyike kama mwendelezo wa nini kifanyike ili kumchora mwanamke katika mwanga angavu. Tafiti hizo pia zitatakiwa kuchunguza vipengele ama mbinu nyingine na kuzichambua kwa kina ili kuona namna zinavyojenga na kuibua dhamira mbalimbali katika riwaya za Kiswahili.
|
|
|
MGOGORO WA KIJINSIA KATIKA RIWAYA YA UTENGANO YA SAID MOHAMED |
Posted by: MwlMaeda - 08-26-2021, 05:22 PM - Forum: Riwaya
- No Replies
|
|
Utengano
Mgogoro wa kijinsia katika riwaya ya Utengano ya Said Ahmed Mohamed
Muhtasari
Kutokuwepo kwa usawa wa kijinsia ni mojawapo ya mada kuu za majadiliano ya kimataifa juu ya maendeleo ya nchi za bara la Afrika. Kuna msimamo maarufu kwamba maendeleo ya wanawake ni maendeleo ya jamii nzima. Kwa hiyo, insha hii inalenga kujadili moja kati ya matokeo ya kutokuwepo kwa usawa huo, yaani mgogoro wa kijinsia katika nchi nyingi za kiafrika unaosawiriwa kwa kina na mtunzi Said Ahmed Mohamed katika riwaya yake ya Utengano. Insha hii inazungumzia kwa kina sababu, maendeleo na suluhisho za mgogoro huo katika riwaya ya Utengano. Inahitimishwa kwamba sababu kuu za mgogoro wa kijinsia uliomo katika jamii husika ya riwaya ya Said Ahmed Mohamed ni siasa za ubaguzi, mwelekeo wa wanaume wa kuwadharau wanawake na kutokuwepo kwa wanawake wengi wanao ari ya kuyaleta mabadiliko. Aidha, kuondolewa kwa sababu hizo kunaweza kueleweka kama suluhisho kuu ya mgogoro wa kijinsia.
Utangulizi
Katika matumizi ya kawaida neno mgogoro hutumiwa katika maana ya ‘hali ya watu kutoelewana ambayo huweza kusababisha ugomvi’ na kila siku tunakabiliana na migogoro ya aina fulani. Katika matumizi ya kifasihi mgogoro ni kipengele kikuu cha uhahiki wa dhamira kuu ya mwandishi katika kazi yake ya fasihi na unaweza kuwa wa (1) mtu na nafsi yake, (2) mtu na mtu mwengine, (3) kikundi cha watu na kikundi kingine na pia, (4) kikundi cha watu na mtu mmoja. Dhamira ya mwandishi, ambayo ni kipengele muhimu cha maudhui, ‘inachukuana na azma, lengo au kusudi la mtunzi katika kuitunga kazi yake’ na hakuna mwandishi anayetunga bila dhamira. Kwa hiyo, katika kazi nyingi za fasihi wandishi wanasawiri mgogoro fulani ambao, aghalabu, unadhihirisha maoni yao juu ya jambo maalum na, vilevile, uhalisi wa kimaisha wa jamii yao. Katika riwaya ya Utengano (1980) mtunzi Said Ahmed Mohamed anaisawiri migogoro kadhaa mathalan migogoro ya kitabaka, kisiasa au kiutamaduni lakini mgogoro wa kijinsia ndio mgogoro unaojitokea mwanzoni mwa sura ya kwanza na kuendelezwa mpaka mwisho wa ploti. Mgogoro wa kijinsia umejikita sana katika fasihi ya Kiswahili na mifano miwili ya wandishi wengine wanaohusisha kazi zao na dhamira hiyo ni Eurphrase Kezilahabi katika riwaya yake ya Rosa Mistika au Mohamed Said Mohamed katika riwaya yake ya Kiu. Lengo la insha hii ni kuueleza mgogoro huo katika riwaya ya Utengano kwa kuvifuata vipengele vikuu vitano, yaani: (1) sababu za mgogoro wa kijinsia, (2) jinsi mgogoro huo unavyotokea, (3) jinsi unavyoendelezwa na mwandishi, (4) nani anashiriki katika maendeleo ya mgogoro huo na mwishowe – (5) jinsi mgogoro wa kijinsia unavyosuluhishwa na mwandishi. Mwishoni, insha hiyo inafikia hitimisho (a) kwamba mgogoro wa kijinsia katika riwaya ya Utengano (unaoweza kugawika kwenye mgogoro mkuu na migogoro midogo inayochangia katika maendeleo ya mgogoro mkuu) hauwezi kusuluhishwa kamili mpaka jitihada za wanawake, wanaume na pia, serikali, ziunganishwe pamoja, na (b) kuwa kuwepo kwake ni hatua ya kwanza ya kuuleta usawa kati ya wananchi wote katika jamii husika bila kujali jinsia.
Migogoro midogo ya kijinsia katika riwaya ya Utengano
Insha hii inapendekeza kwamba katika riwaya ya Utengano kuna mgogoro wa kijinsia mkuu unaozungushwa na kukuzwa na migogoro midogo ya kijinsia iliyomo, vilevile, ndani ya ploti. Said Ahmed Mohamed anautambulisha mgogoro wa kijinsia mkuu katika sura ya kwanza ya riwaya na anauendeleza mpaka mwisho wa ploti, yaani anayazungumzia matokeo yake na anayapendekeza maarifa ya kuusuluhisha. Mwanzoni, migogoro midogo inazungumziwa.
Kwanza, insha hii inajadili kwamba katika riwaya ya Said Ahmed Mohamed, kuna mgogoro wa kijinsia ndani ya fikra na hisi za mhusika wa kike unaotokea wazi mhusika huyo anapomkabili kiumbe wa kiume. Kazija ni mhusika wa kwanza msomaji anayekutana naye katika riwaya ya Utengano na jambo la kwanza tunalopata kujua kuhusu yeye ni chuki anayohisi dhidi ya wanaume wote. Mwandishi anatuelezea kwamba sababu ya msimamo wake huo wenye chuki ni kutokuwepo kwa usawa kati ya wanaume na wanawake (‘Anamchukia mwanamme kwa sababu dhahiri, nayo ni kuwa amewekwa mbele, ingawa Kazija hajui na nani.. Pamoja na hayo, Kazija anajichukia kwa kiasi anavyomchukia mwanaume kwa sababu ya nafsi yake ‘iliyolemaa na kuridhi siku zote kumpembejea mwanamme ambaye ni kiumbe kama yeye’. Upevu wa mgogoro wa kijinsia unaokuzwa ndani ya fikra za Kazija unatokea katika sehemu chache za riwaya ya Utengano. Katika sura ya kwanza Kazjia anapokutana na mvulana anayeitwa Mussa tunashahidi jinsi mwanamke huyo alivyopevuka katika kuyatetea maslahi yake na yale ya wanawake wengine. Ingawa Mussa ni mvulana wa umri mdogo, tayari ameingia katika mambo ya ulevi na anamwandamana Kazija ambaye ni mtu mzima. Kazija anapomkabili anajizungumzia akilini mwake kuhusu unyonyaji unaopokewa na wanawake wengi kutoka kwa wanaume (‘Mwanamke, mtumwa […] Viumbe vya kupika na kupakua, kufua na kupiga pasi, kushika mimba na kuzaa…’). Zaidi ya hayo, Kazija hasiti kuzungumza kwa sauti ya ushujaa anapomwonyeshea Mussa ufahamu wake mzuri juu ya sababu ya kutokuwepo kwa elimu miongoni mwa wanawake, Mussa anapojaribu kuzungumza katika lugha ya Kiingereza (‘Usiniseme Kizungu miye. Si ndivyo mlivyotuweka? Tusisome. Tuwe wajinga. Mtutawale na kutuparamia maisha, au sivyo?’). Hali kadhalika, Kazija anapomkabili Makusudi (mwanasiasa na baba yake Mussa), anajawa na hisia zile zile za chuki na ghadhabu (‘Alimtazama Makusudi kama vile alikuwa kakabiliana na chatu’). Anamwambia kwa maneno ya ujasiri kwamba anawadhulumu wanawake na, vilevile, kuwa ni mwanasiasa anayetawala kwa njia ya vitendo vilivyopotoka. Kwa sababu ya msimamo wake wenye chuki dhidi ya wanaume na ari ya kuanza vita vya ukombozi wa wanawake, Kazija anakubali kumsaidia rafiki yake wa kike, Farashuu, kwenye kumlipiza kisasi Makusudi aliyesababisha kifo cha mwanawe, Mwanasururu – hatua ya kwanza ya maendeleo ya mgogoro mkuu wa kijinsia katika riwaya ya Utengano. Yaani, Kazija anaamua kuwa mwanamke wa kando wa Makusudi na, sawia, kuzikubali posa za kimapenzi za Mussa ili kuusababisha ugomvi wa kifamilia hadi nyumba ya Makusudi itenganishwe na ishindwe na kisirani. Mwishoni, Kazija ndiye mshindi katika mgogoro baina yake na mwanaume – alitekeleza lengo lake na alipata jina la ‘mwanamke aliyekuwa na ujasiri kuliko wanaume’. Biti Kocho (mtumishi katika nyumba ya Bwana Makusudi) ni mhusika anayefanana kimsimamo na Kazija. Kama Kazija, Biti Kocho anasumbuliwa na mgogoro wa kijinsia uliomo akilini mwake na unaotokeza anapokabiliwa na mwanaume au matokeo ya dhuluma zake. Anapotambua jinsi Makusudi anawatendea Tamima (mkewe) na Maimuna (mwanawe) na, vilevile, anavyowalaghai wananchi, Biti Kocho anajaribu kuwatetea na kumkabili Makusudi kwa kupaza sauti yake ya ujasiri (‘Kumbe bwana wewe mjinga een. Yupo mtu asiyejua siasa dunia hii? Wadanganye hao wasiokujua, mimi nakujua vilivyo’). Anakata shauri kuwashawishi Maimuna apate uhuru wake kwa kutoka nyumbani (‘Wewe ni wa kufungwa ndani kama kuku? Huyo kuku ana afadhali’) na Tamima amwite mkunga wa kienyeji akamzalishe pasi na idhini ya Makusudi. Biti Kocho anamwita mkunga wa kienyeji anayeitwa Farashuu, yanni mwanamke anayepanga kumlipiza kisasi Bwana Makusudi. Ingawa katika mgogoro baina Biti Kocho na Makusudi hakuna mshindi wala mshindwa wazi, kwa minajili ya mwamko wake, Biti Kocho anatoa uamuzi wa kuchangia kwenye kuitekeleza mipango ya Farashuu na kwa maneno mengine – kwenye maendeleo ya mgogoro mkuu wa kijinsia katika riwaya ya Utengano.
Pamoja na hayo yote, kabla ya kujadili juu ya mgogoro mkuu wa kijinsia, maelezo mafupi kuhusu mgogoro wa kijinsia katika ndoa yangefaa ambao, katika riwaya ya Utengano, unawahusu hususan wahusika wawili – Selume na mumewe, Shoka. Ingawa mgogoro baina yao hauchangii katika maendeleo ya mgogoro mkuu wa kijinsia, unasisitiza kadiri kubwa ya upevu wa mgogoro wa kijinsia wa kijumla uliojikita katika jamii husika. Selume anayafahamu manyanyaso ya wanaume na anajaribu kupingana na Shoka ambaye ni mlevi asiyejali kuhusu wema wa aila yake. Bali, anapendelea kulała nje kumlaghai mkewe na kumwachia watoto wao ili awatunze pekee yake. Selume anaonekana kuwa mshindwa katika mgogogro baina yao kwa sababu walau anasema ‘tumo taabuni wanawake na huu utumwa kamili’, haelewi namna gani wanawake ni watumwa na anafikiri kuwa kuwafuata wanaume ni sharti zilizo ngumu kubadilika.
Mgogoro mkuu wa kijinsia katika riwaya ya Utengano
Kama ilivyotanguliwa kusemwa hapo awali, wanawake watatu wanahusika katika mgogoro mkuu wa kijinsia (Farashuu, Biti Kocho na Kazija) wanaopingana na mwanaume mmoja – Bwana Makusudi. Chanzo cha mgogoro huo ni matendo mabaya ya Bwana Makusudi ambaye alikisababisha kifo cha mke wake wa kwanza, Mwanasururu (binti yake Farashuu). Makusudi aliponyima mali Mwanasururu aliyorithi, akamwacha na Mwanasururu akawa mlevi, mwendawazimu na mwishoni akafa. Katika sura ya kwanza tayari tunapata kujua kwamba Farashuu aliamua kumlipiza kisasi kwa yote aliyomtendea binti yake na kuyasababisha madhara katika aila yake (‘Mimi nitalipa kisasi […] Bado nalia na kilio changu bado hakijanyamaza’). Pamoja na wenzake wawili, Kazija na Biti Kocho, walitoa uamuzi wa kuziunganisha sababu zote za chuki wote watatu waliyosikia dhidi ya Makusudi ili kuitenganisha familia yake. Kama ilivyoelezewa hapo awali, Kazija alisababisha utengano baina Makusudi na mwanawe wa kiume, Mussa. Farashuu pamoja na Biti Kocho waliwatenganisha Makusudi na Maimuna na mkewe, Tamima, aliyepewa talaka na kufukuzwa kutoka nyumbani. Aidha, Makusudi alipojaribu kuwahutubia wananchi wakati wa kampeni ya kugombea uchaguzi, Kazija aliwadhihirishia wasikilizaji ubaya Makusudi alionia na unyama ambao aliifanyia aila yake (‘Huyu Makusudi ambaye ameshindwa kuiendesha nyumba yake ataweza kuangalia maslahi yetu?’). Kwa hiyo, Makusudi alifungwa gerezani kwa muda wa miezi kadhaa na baada ya kutoka na kujaribu kumwona bintiye, Maimuna, akalazwa hospitalini kwa minajili ya kupigwa. Maimuna akaamua kumsahau baba yake na kubaki kutenganishwa na yeye kwa sababu ya yote mabaya aliyomtendea. Walau Said Ahmed Mohamed hauendelezi mgogoro mkuu wa kijinsia moja kwa moja mpaka mwisho wa ploti, anayazungumzia matukio yanayozuka kwa minajili ya mgogoro huo yaani momonyoko wa maisha ya Maimuna na Makusudi. Aidha, mgogoro wowote hauwezi kuanzishwa bila ya sababu, iwe ya maana kubwa au ndogo. Insha hii inajadili kwamba kuna sababu kadhaa za mgogoro wa kijinsia katika riwaya ya Utengano, zinazoimarishana na kupishana.
Sababu za mgogoro wa kijinsia katika riwaya ya Utengano
Kuna mshabihiano mkuu baina ya migogoro ya kijinsia iliyomo ndani ya ploti ya riwaya ya Utengano – yote inazuka kwa minajili ya matendo mabaya ya wanaume wanaowabagua wanawake na, sawia, kwa sababu ya ufahamu wa wanawake kuhusu ubaguzi unaotendwa dhidi yao na shauku yao ya kuukoma. Hata hivyo, mizizi ya mgogoro huo inafichwa ndani zaidi. Insha hii inajadili kuwa kuna sababu zinazokuwa na uhusiano wa moja kwa moja na mgogoro wa kijinsia (utengano baina wanawake na wanaume) na zile ambazo haziuna (siasa na dini). Aidha, zote tatu zinapishana na zinaimarishana. Utengano baina wanawake na wanaume unatajwa kama sababu ya mgogoro wa kijinsia na mwandishi mwenyewe tayari katika sura ya kwanza anapomsawiri mhusika anayeitwa Kazija. Kazija anatambua kuwa mwanamke ni ‘pambo la mwanaume ambalo alitazame apumbae nalo’ na kwa sababu hiyo anawachukia wanaume na anaamua kuwashinda. Utengano huo unawasababisha wanawake wawe wanyonge wakati wanaume wanafaidika kutoka kwa cheo chao cha juu. Insha hii inajadili kuwa utengano kati ya wanawake na wanaume una mizizi miwili mikuu, yaani siasa za ubaguzi na dini inayowatenganisha wafuasi wake (wanaume na wanawake). Said Ahmed Mohamed anazungumzia mada ya siasa na dini ili kuonyesha jinsi zote mbili zinavyoathiri maisha ya jamii husika. Mwandishi anatuelezea matendo ya wanasiasa wanaojali kuhusu maslahi yao tu kuwabagua wanawake na wanyonge wengine. Vilevile, anatudhihirishia kwamba siasa ni eneo la wanaume pekee yao ambapo mwanamke haruhusiwi kuingia, kwa hivyo – haruhusiwi kujitawala na kuyatawala maisha yake ambayo yanamtegemea mwanaume, kiumbe mwenye kuamua juu ya kila jambo. Hii inaonekana wazi Makusudi anapomwambia Biti Kocho ‘katafute kifuu na mchanga uchezee, usijitie kwenye mambo usiyoyajua’. Aidha, dini ya Kiislamu inachangia sana katika kuwepo kwa mgogoro wa kijinsia katika jamii husika, ingawa jambo hilo halipendekezwi na mwandishi moja kwa moja. Kwanza, dini ya Kiislamu inawaruhusu wafuasi wake kulipiza kisasi na inakubali ulipizaji kisasi uwe njia bora zaidi ya kutia adhabu (kanuni ya ‘jino kwa jino, jicho kwa jicho’). Ulipizaji kisasi ni silahi inayochaguliwa na Farashuu anapotoa uamuzi kwamba atapingana na mwanaume, Makusudi. Pili, Korani yenyewe inakubali wanawake lazima wawe chini ya wanaume na daima wakae watiifu (‘na uvumilie kwa kimya nyumbani kwako…’). Kwa muujibu wa Korani, mwanamke lazima apate idhini ya mwanaume ya kutoka nje au kumkaribisha mgeni nyumbani kwao – jambo linaloonekana wazi nyumbani kwa Makusudi anayemkataza mkewe, Tamima atoke bila ya maarifa yake (‘babako hataki tutoke nje ila kwa ruhusa yake, na humu asiingie mtu ila kwa ruhusa yake’). Bila shaka yoyote kanuni hizo zilizaa ghadhabu ya Biti Kocho aliyekata shauri kutozitii, kinyume cha Tamima aliyetaka kubaki mtumwa wa mumewe. Aidha, wakati wa kujadili kuhusu mgogoro katika kazi ya fasihi ni lazima kujiuliza, je mwandishi anaipendekeza suluhisho yoyote?; na aya inayofuata italichambua swali hilo.
Suluhisho za mgogoro wa kijinsia katika riwaya ya Utengano
Mwanzoni, ni muhimu kukubali nani ni mshindwa na mshindi wa kijumla katika mgogoro huo: mwanamke au mwanaume? Makusudi anaonekana kuwa mshindwa kwa sababu anateseka – anatenganishwa na familia yake, anafungwa gerezani, analazwa hospitalini, mwishoni anakufa na hapati nafasi ya kuwaona wote katika familia yake waliojikusanya kwa ajili ya arusi ya Maimuna. Licha ya hayo yote, mwanamke bado hawezi kuitwa mshindi kwenye mgogoro wa kijinsia katika riwaya ya Utengano kwa sababu kadhaa zilizo, vilevile, suluhisho za mgogoro wa kijinsia. Insha hii inajadili kuwa mgogoro wa kijinsia unaachwa na mwandishi bila kusuluhishwa lakini mtunzi anapendekeza kwamba mgogoro huo unaweza kusuluhishwa mwanamke anapomshinda mwanaume na mwanaume anapokubali ushinde wake na kujibadilisha kitabia. Kwa hivyo, kwanza, Said Ahmed Mohamed analenga kutuambia kwamba wanawake wanaweza kuwa washindi katika siku za mbele ikiwa wote wataziunganisha bidii zao kuwakabili wanaume na unyonyaji unaofanyiwa nao. Katika riwaya ya Utengano, wanawake, badala ya kuziunganisha nguvu zao zote ili kuyapambana na maudhui ya wanaume, wana mwelekeo wa kuwadhuru wanawake wengine jinsi Farashuu and Biti Kocho walivyosababisha unyonge wa Maimuna. Pili, wanawake wengi (kama Selume au Tamima) wanaamini kwamba mila au dini yao inawashurutisha daima wawafuate wanaume na kuwa hawaruhusiwi kupambana na kiumbe wa kiume (‘alijiona anafuata kawaida na kanuni iliyotoka mbali ambayo imekuwa ngumu kugeuka’). Said Ahmed Mohamed anania kuwadhihirishia wasomaji kwamba moja kati ya suluhisho za mgogoro wa kijinsia ni kuwepo kwa wanawake kama Biti Kocho, yaani ufahamu mzuri wa umuhimu wa uhuru miongoni mwa wanawake ambao bado wanaogopa kusimama na kuzitetea haki zao. Tatu, mwandishi anayapendekeza mabadiliko ya mfumo wa kisiasa ambao ni mmoja wenye ubaguzi na ufisadi. Wanasiasa wana nguvu kuliko wananchi wengine na mgogoro wa kijinsia utaendelea kujikita katika jamii husika ikiwa wao hawatazibadilisha sera zao kwenye zile za kidemokrasia (yaani, kama zile za mwanasisasa Siwa). Mwishoni mwa riwaya, Maimuna anasoma katika gazeti kwamba serikali inapanga kufanya kampeni ya maendeleo ya wanawake kwa sababu ‘maendeleo ya wanawake ni maendeleo ya jamii nzima, na ukombozi wa wanawake ni ukombozi wa jamii nzima’. Mwisho lakini si uchache, mwandishi anasisitiza umuhimu wa kuwepo kwa wanaume kama Kabi (mume wake Maimuna) na geuko la mtazamo wa wengi wa wanaume ambao bado wana mwelekeo wa kuyadharau maneno ya wanawake (‘inahitajia wanaume waelimishwe kuhusu maslahi ya wanawake’).
Hitimisho
Mwenda Ntarangwi alivyosema na kinachoonekana wazi katika riwaya ya Utengano ya Said Ahmed Mohamed ni kwamba ‘uhusiano kati ya mwanaume na mwanamke ni mambo ya kati kabisa katika fasihi’. Hakuna mwandishi anayetunga kutokana na ombwe bali tajriba yake (mambo aliyoshuhudia) iliyomtilia moyo wa kuwawasilishia watu ujumbe fulani, uwe mzito au mwepesi. Said Ahmed Mohamed aliamua kuandika kuhusu mgogoro wa kijinsia kwa sababu dhahiri – mgogoro huo umejikita sana katika jamii nyingi za Waswahili bila kusuluhishwa na hicho ndicho mojawapo ya vizuizi vikuu vya maendeleo yao ya kijumla. Insha hii inajadili kwamba mgogoro wa kijinsia katika riwaya ya Utengano unaweza kugawika kwenye mgogoro mkuu na migogoro midogo inayochangia kwenye maendeleo na kadiri ya mgogoro mkuu unaoendelezwa kutoka mwanzo mpaka mwisho wa ploti ya riwaya. Insha hii inahitimisha kwamba kuwepo kwa mgogoro wa kijinsia ni hatua ya kwanza ya kuyaleta mabadiliko yanayohitajika ili kuboresha hali ya maisha ya jamii husika. Hata hivyo, mtunzi anapendekeza kwamba mgogoro huo uko katika Afrika kwa sababu kadhaa, yaani: siasa za ubaguzi, mwelekeo wa wanaume wa kuwadharau wanawake na kutokuwepo kwa wanawake wengi wanao ari ya kuyaleta mabadiliko, ambazo ni vizuizi vikuu vya kuusuluhisha mgogoro wa kijinsia.
Bibliografia
Kamusi ya Kiingereza-Kiswahili, Institute of Kiswahili Research, Tanzania (Dar es Salaam), 1996
Kamusi ya Kiswahili ya Karne ya 21, Longhorn Publishers, Kenya (Nairobi), 2011,
Mwenda Ntarangwi, Uhakiki wa kazi za fasihi, Augustana College, Rock Island, 2004
Said Ahmed Mohamed, Utengano, Longhorn Publishers, Tanzania (Dar es Salaam), 1980
//www.thereligionofpeace.com
Kamusi ya Kiswahili ya Karne ya 21, Longhorn Publishers, Kenya (Nairobi), 2011, ukurasa 313
Mwenda Ntarangwi, Uhakiki wa kazi za fasihi, Augustana College, Rock Island, 2004, ukurasa 80
Said Ahmed Mohamed, Utengano, Longhorn Publishers, Tanzania (Dar es Salaam), 1980, ukurasa 1[url=https://mwalimuwakiswahili.co.tz/mgogoro-wa-kijinsia-katika-riwaya-ya-utengano-ya-said-mohamed/#_ftnref4][/url]
Qur’an(33:33), tafsiri yangu (//www.thereligionofpeace.com/Quran)
Said Ahmed Mohamed, Utengano, Longhorn Publishers, Tanzania (Dar es Salaam), 1980, ukurasa 20
Mwenda Ntarangwi, Uhakiki wa kazi za fasihi, Augustana College, Rock Island, 2004, ukurasa 80
|
|
|
UCHAMBUZI: RIWAYA YA MUNGU HAKOPESHWI |
Posted by: MwlMaeda - 08-26-2021, 04:34 PM - Forum: Riwaya
- No Replies
|
|
UCHAMBUZI: RIWAYA YA MUNGU HAKOPESHWI
UTANGULIZI
Riwaya ya Mungu Hakopeshwi inaelezea maisha ya familia moja inayoishi sehemu ya mtaa wa Malindi kisiwani Unguja ambapo familia hiyo ya Bwana Ahmed Said mwenye hasira yake kali, asoambilika na asokubali kushindwa wala kutetereka katika maamuzi yake ambapo kiundani anaonekana ana siri fulani ambaye kaihifadhi katika kifua chake na hata mkewe Bi Khadija binti Najash anapomshauri hamsikilizi anaona mwanamke ni mtu wa ndani tu hana lolote la kuchangia katika familia na jamii.
MAUDHUI
Maudhui ya kitabu hiki kwa ujumla yanaelezea maisha ya Bwana Ahmed na mkewe Bi Khadija ambao ni baba na mama wa watoto wane nao ni Said, Layla, Zahra na Salah ambapo wanaishi katika maisha mazuri lakini uzuri wake ni wa kibatari ambapo unawamurikia mwanga watu wegine lakini chenyewe ni giza tupu ndani kwani maisha ya familia hii ni ya mtafaruku, mikwazano, kejeli, dharau na yaliyojaa kunyimwa uhuru wa mtoto wa kike na hata mke katika hata yale maamuzi mazito yanayohusu maisha yao.
LENGO
Lengo la muandishi ni kuonesha kua bado katika Zanzibar au Tanzania kwa jumla kuna hizi familia ambazo zina mfumo dume ambapo mwanamke hawezi kupaza sauti kudai haki yake na wala hana uhuru wa kuamua kama Bi Khadija katika uk 32 anaposema “Ahmed unakosea unaposema hivyo mtoto wa kike nae ana haki yake”.
Haki yake? Haki ya nini? Usitake kunitibua sasa! Migogoro ya utumwa anotumishwa mwanamke haina kifani na kufikia kushushwa hadhi yake kama ukurasa 33 bwana Ahmed anamwambia mkewe “ unakistaajabia kitu gani hapo kilichokua kipya kwako kachukue tambara uje ufute hapo hizo ndio kazi zenu wanawake.”
Katika kukamilisha kusudio lake mwandishi kajitahidi kuzielezea falsafa za maisha vizuri sana pamoja na changamoto zinazokabiliana nazo, kama katika ukurasa wa 11 anasema “dunia mviringo kwa kupanda na kushuka”.
Umuhimu wa kuwepo kodi za serikali pia umezungumzwa uk 9 “Muhimu kulipa kodi za serikali kwa wakati”.
Tabaka tawala anavyoamini muandishi haliwakubali sana na watu wenye asili ya kiarabu ukurasa wa 10 “Wanatudhulumu kwa maneno yao ya shutuma na chuki”.
Falsafa ya mabadiliko ya maisha imezungumziwa vyema muandishi akizungumza kuhusu baadhi za familia namna zilivyoporomoka mdomoni kwa bwana Ahmed “Iangalie familia ya Bw Salim Mahfudh Mungu amrehemu ……wamebakiwa na nini watoto maskini uk 13.
Mwandishi pia anazungumzia suala la ugumu wa ajira “wote ni wasomi wa elimu ya juu, lakini zimewafaa nini? Yule mmoja ni Mwanasheria na Yule mwengine ni mkemia lakini wote hawana ajira mpaka sasa”.
Falsafa juu ya ndoa gani inafaa imezungumzwa na mwandishi kama inavojieleza uk 29 Bi khadija anaposema “Sijakusudia kumjua kwa sura wala anafanya nini nakusudia tabia yake ikoje”?…… sura ya mtu na mali zake hazisaidii kitu katika maisha ya ndoa ikiwa tabia yake mbaya .
Falsafa juu ya umuhimu wa elimu imeelezwa vyema kuwa elimu inamfata popote anapokwenda na kumuangazia nuru ya maisha yake .Haya anadhihirisha mwandishi wa riwaya hii katika ukurasa 83 Bwana Ahmed anapoaambiwa na mkewe: “Khah! Sikufikiria kama una dhana potovu kama hizo kuwa na elimu yenye manufaa ni utajiri bora kuliko kumiliki mali, elimu ni nuru na vazi bora na heshima kwa mwenye nayo, elimu haiishi, humfata mtu kila aendapo na humsaidia kila inapohitajika. Basi vipi mali inaweza kushika nafasi ya elimu?
Falsafa ya ukweli kama nyenzo za kutetea mtu haki yake imejadiliwa na mwandishi tangu mwanzo mpaka mwisho kama ukurasa 88 Zahra anapomuambia dada yake “Ukikosa kumchagua mume sahihi ndio ushaharibu maisha yako yote”. “Hakuna njia nyengine ila useme ukweli tu”. “Layla ndugu yangu ,usitake kuukwepa ukweli ukitaka usitake ukweli unabaki pale pale kuwa bado una hisia kwa Hassan”.
Falsafa ya tabaka la kitajiri ambalo inaliona tabaka la kimaskini halina hadhi ya kuingiliana nao ubia wala change zozote zile za kuoana wala kusuhubiana .Mwandishi kalizungumzia uk 12 bwana Ahmed aliposema oh! Eti mtoto wa Ahmed bin Said aolewe na mwenye daladala. Mwenyewe nimekufa ama? Kuonesha dharau za pesa na kujitukuza.
MIGOGORO ILIYOJITOKEZA
- Mfumo dume ni miongoni mwa migogoro iliyojitokeza tangu mwanzo mpaka karibu na mwisho wa kitabu husasan kumkandamiza mtoto wakike na mke kumnyima haki kama vile bi Khadija anavyojaribu kumnasihi mumewe uk 113 akubali posa za Hassan na kukataa kata kata kua yeye diye mwenye maamuzi ya pekee na anasema; “Usianze somo lako, nimechoka kubishana na wewe mwenye maamuzi ya mwisho ndani ya nyumba hii ni mimi na siku zote itabaki kua hivyo, name nimeshaamua Layla atolewa na Hafidh tu sitaki kusikia tena mada hii hapa ndipo imeshafika kikomo.
- Mfumo dume unaomfanya Said pia awanyime ndugu zake wa kike haki na Zahra anapojaribu kujielezea anawakaripia kwa kejeli,dharau na ukali uk 108 sio kama tunatafuta mabwana…… “Nyamaza kenge we! Mnaleta mambo ya kipuuzi humu ndani kisha unajitia kidomodomo juu bado? Katika umri wenu wote mliwahi kumuona nani kafanya ujinga huo mlioufanya nyinyi”?
- Mgogoro kati ya mtoto wa kiume wa bwana Ahmed Said na baba yake . Mgogoro uliojitokeza baada bwana Ahmed kutaka kumuozesha Said mke na kufika kwenda kumposea na kutoa mahari bila hata kumuarifu uk 131 Said anasikika akimueleza baba yake “Ina maana umefanya yote hayo bila kuniambia chochote hata hukujali kujua ninahitaji kitu gani”? “Wewe ni mwanangu najua nini bora kwako ndio maana nikakutafutia “ “Na nikikwambia kuwa simtaki Sifati”? “Eti ? Na usimtake ana kasoro gani”? “Hana kasoro yeyote ila simuhitaji kwenye maisha yangu”
- Mgogoro kati ya bwana Ahmed na wazee wa Sifati kaka zake Awadh na Yahya, uk 135 “Ami Ahmed kuna habari zimetapakaa mji mzima kua Said ameondoka nyumbani na hajulikani alipo. Eti habari hizi zina ukweli wowote”? Yahya alimuuliza suali bwana Ahmed “Aaa ni kweli, lakini….musiwe na wasiwasi, kila kitu kitakua sawa…….. ni mambo ya kitoto tu. “Kwani basi hakukutaarifu”? Awadh aliuuliza huku uso kaukunja…. uk 140 “Umefanya yote haya kwa ajili ya kutudhalilisha tu kwa sababu umetuona sasa sisi ni maskini”.
Tukizungumzia migogoro yote iliyozungumzwa hatuimalizi kwani kuna migogoro kati ya Bi Maimuna na mumewe bwana Mahfudh kuna migogoro kati Hafidh mume wa Layla kuhusiana na ndoa bubu, yote imegubika katika kumkandamiza mwanamke na kumnyima haki yake.
FANI
Katika maandishi yake kijumla mwandishi amejitahidi kutumia kiswahili fasaha kinachozungumzwa “kisiwani Zanzibar na kwa jumla tukitazama kazi yake kilugha, fani imeweza kuyaibua maudhui yaliyokusudiwa na kuibeba vyema dhamira aizungumzayo katika muktadha wa kile akizungumziacho na kutoa mwanga kwa jamii iliyokusudiwa kuifahamu vyema riwaya yake.
JINA LA KITABU
Tukianza na jina la kitabu kwamba gamba la nje lina mchoro wa mwanamme jasiri lakini na ujasiri wake kazongwa na senyenge za damu na jicho moja linachiriza machozi na ujumbe uliopo “MUNGU HAKOPESHWI”.Unapoisoma riwaya hii tangu mwanzo hadi mwisho utajua kwa kweli mwandishi kajitahidi kusibu katika kitabu chake kwani kama bwana Ahmed alipompuuza baba yake na kumkimbia nayeye alikimbiwa na mwanawe Said na hakutokea hadi kumkuta maiti,kama bwana Ahmed alivyomtupa Lulu na mkungu wa mimba na yeye kulipwa, na kuja kujishtukia na aibu.Aibu ambayo imempeleka akhera mosi,lakini pili imesababisha kuoana Zahra na Ahmed ambao ni ndugu wa damu ya baba mmoja. Hafidh ,kama alivyomtoa Layla roho kajikuta na yeye anaishi na virusi vya ukimwi kwa vitimbi alivyokuwa akimfanyia mkewe huenda ikawa ni malipo na kama hilo halitoshi baba yake alikuwa ni mhimili wake wa kumuunga mkono anahangaika na maradhi ya kiharusi hana mkono wala mguu, na anatapia nafsi yake.
“MUNGU HAKOPESHWI”ni kweli Said aliwakimbia wazee wake na majukumu ya familia kuyakwepa, na mdogo wake Layla hakumjali wakati alipokuwa anahitaji sana msaaada kamkuta keshafariki hakushuhudia hata maziko yake na huyo mwanamke aliyemzuzua Farhat, alipoanguka tu kimaisha amemkimbia akafika kufanya kazi ya kupara samaki.
LUGHA ILIYOTUMIWA
Mwandishi wa riwaya katumia lugha ya Kiswahili chepesi kinachotumiwa mjini Unguja lakini hakuacha kuirashia tauria, stiari,tamathali za semi, tashbiha ambazo zimetawala tangu mwanzo wa riwaya yake mpaka mwisho hata nyengine zikawa zinajirejea.
Mathalani hazikuchusha na pengine zilimsaidia msomaji awe na hamu zaidi ya kuimaliza haraka riwaya yake.
• LUGHA ZA PICHA
Mwandishi kila sura anaivuta vyema lugha ya picha na msomaji hujihisi kile kitu kipo mbele yake. Katika ukurasa wa 5 mwandishi akiuelezea wasifu wa Bi Khadija anaeleza
“Bi Khadija alishapindukia miaka arubaini na tano lakini uzuri wake bado haujafifia uso wake ulikua na umbo la yai wenye weupe wa wekundu pua yake ndefu iliyosimama sawa sawa baina ya mashavu yenye rangi ya waridi , chini ya macho makubwa yenye kope ndefu zilizozidisha uzuri wa macho yake. Nyusi ndefu nyembamba zilizozipinda juu ya macho zilikamilisha urembo wa mwanamke huyu. Midomo membamba iliyoficha meno nadhifu yaliyopangika vyema yalizidisha urembo wake kama vile alijua ladha ya tabasamu. Mara nyingi kama si zote uso huu ulikuwa umechanua kwa tabasamu murua na kuzidisha haiba ya uzuri wake. Mwanamke huyu alikua maridhia kwa kila jambo.
Lugha za tashbiha ambazo zimetawala riwaya hii zimeshonana tangu mwanzo hadi mwisho wa riwaya na baadhi yake akurasa ” Mkasa mzima unamp
itia kwenye kichwa chake kama vile mkanda wa filamu ” uk 1
“Bwana Ahmed alijitupa kitandani kama gunia la mbatata”
“Bwana Ahmed alikua mkali kama samba jike mwenye watoto uk 4
“ Sauti kama ya punda” uk 18
“Akichagua wanaume kama anavyochagua chuya kwenye mchele “uk 21
“Zinamiminika mkononi kama maji yanavyotiririka baharini” uk 21
“Akinua miguu juu kama mtu anaetaka kupaka hina”uk 30
METHALI
“Maji yakimwagika hayazoleki” uk 3
“Kidole kimoja hakivunji chawa” uk 4
“Mganga hajigangi” uk 4
“Riziki ya mtu hailiki” uk 10
“Mungu si athumani” uk 10
“Majuto ni mjukuu” uk 12
“Hakuna siri ya watu wawili” uk 20
“Kidole kimoja hakivunji chawa” uk 101
TAURIA NA STIARI
Miongoni mwa vipengele vya lugha vilivonogesha riwaya hii ni stiari na tauria kama zinavojionesha katika kurasa tofauti
“Said mawazo yalimzidi kichwa” uk 8
“Dola inatutia kitanzi shingoni” uk 72
“Maneno yalikua yameingia kwenye moyo” uk 16
“Uchumi unakuja kuangusha stuli” uk 3
“Jicho likafanya kazi yake “ uk 21
“Kioo kimemcheza” uk 24
“Mapenzi yao…….. ikatoa mche, mche nao ukatoa mti mkubwa” uk 24
“Ukimya ulitawala ukumbini hapo” uk 26
“Heshima imekwenda likizo” uk 32
ATHARI ZA LUGHA ZA KISLAM
Kwa vile mazingira ayazungumziayo ni mjini Unguja , hivyo muandishi wa riwaya hii hakuacha kuonyesha athari za lugha za kislam kama zilivyojionesha kwa baadhi kurasa
“Usomaji wa Qur-ani uk 26
“Lailaha illa Allah “ uk 53
“Hii riziki ninavyokunywa hapa iwe sumu mwilini mwangu” uk 52
MAWAZO YA KIUJUMLA
Kwa kuhitimisha mwandishi Zainab Alwi Baharoon kwa vile hii ni kazi yake ya mwanzo amejitahidi sana kuitumia vizuri fani katika kuelezea maudhui yaliyokusudia na jamii aizungumziayo yaani mjini Unguja katika mtaa wa Malindi (na iwe popote Zanzibar) ilimradi kaweza kuzikonga roho za wasomaji wake na mimi binafsi kitabu chake kimenivutia na leo naelezea kimuhtasari tu lakini nachukua ahadi ya kukifanyia uhakiki wa kina na nina kila sababu ya kufanya hivyo kwanza ni muislamu mwenzangu,mwanamke mwenzangu na ikiwa hilo halitoshi ni msanii kama mie, hivyo nachukua fursa hii kumwambia bado mapambano yanaendelea kuzinduliwa kwa kitabu hiki leo iwe chachu ya kutoa chengine na chengine.
Ahsanteni kwa kunisikiliza.
Muhtasari huu umetayarishwa na
Khadija Said Suleiman AL- Battashy
Kwahajitumbo ,Zanzibar
JINA LA KITABU: Mungu Hakopeshwi
MTUNZI: Zainab Alwi Baharoon
MCHAPISHAJI: Z.A. Baharoon, 2012
|
|
|
UCHAMBUZI WA FANI NA MAUDHUI KATIKA RIWAYA YA ADILI NA NDUGUZE |
Posted by: MwlMaeda - 08-26-2021, 03:31 PM - Forum: Riwaya
- No Replies
|
|
UCHAMBUZI WA FANI NA MAUDHUI KATIKA RIWAYA YA “ADILI NA NDUGUZE” ILIYOANDIKWA NA SHAABAN ROBERT
1.0 Utangulizi
Kazi hii inahusu uchambuzi wa fani na maudhui katika riwaya ya “Adili na Nduguze” iliyoandikwa na Shaban Robert mwaka 1952. Katika kujadili riwaya hii tutaeleza dhana ya riwaya, usuli wa mwandishi, muhtasari wa kitabu chenyewe, nadharia zitakazotumika kuchambua fani na maudhui ya kitabu hiki, uchambuzi wa fani na maudhui na hitimisho.
1.1 Dhana ya Riwaya
Kwa mujibu wa Madumulla (2009) akimrejelea Msokile (1992) anafafanua kuwa riwaya ni kazi ya sanaa ya kubuni, ni maandishi ya nathari (ujazo) yanayosimulia hadithi ambayo kwa kawaida ina uzito, upana, urefu wa kutosha, ina wahusika wengi wenye tabia mbalimbali, ina migogoro mingi mikubwa na midogo.
Senkoro (1982) anasema riwaya ni hadithi ndefu ya kubuni yenye visa vingi, wahusika zaidi ya mmoja, na yenye mazungumzo na maelezo yanayozingatia kwa undani na upana maisha ya jamii.
Wamitila (2003), Samwel na wenzake (2013), wanasema kuwa riwaya ni kazi andishi ya fasihi ambayo kwa kawaida ni ndefu zaidi kuliko hadithi fupi. Urefu wa riwaya maana yake ni kwamba msuko simulizi umejengeka vizuri, kuna wahusika wengi, inaenea muda mrefu, na mada zake ni nzito na pana kiasi. Mifano mizuri ya riwaya kwa lugha ya Kiswahili ni “Nagona” au “Mzingile” riwaya za mwandishi Euphrase Kezilahabi.
Kwa ujumla riwaya ni hadithi ndefu za kubuni zenye wahusika wengi au wachache zinazoelezea maisha ya mtu au jamii fulani.
1.2 Usuli wa Mwandishi
Sheikh Shaaban Bin Robert alizaliwa tarehe mosi January mwaka wa 1901 katika kijiji cha Vibambani, mahali paitwapo Machui, maili sita kusini ya Tanga. Yakisiwa kuwa jina hili la ‘Robert’ lilitokana na matamshi mabaya ya Jina lake alilopewa akiwa skuli, Msimbazi, kwa kuwa baba yake hakuitwa Robert. Mara nyingi aliandika jina lake kama “Roberts”
Baba yake alifanya kazi kama karani katika Shamba la makonge la Amboni. Mama yake alikuwa Mdigo. Yasemekana kuwa wazazi hawa wawili walikuwa wa ukoo wa Mganga wa kabila la Kiyao. Lakini, Sheikh Shaaban alikataa kuitwa Myao akawa mmoja wa watu wachache waliojiita Waswahili.
Shaaban alitafuta mke wake wa kwanza kwa utulivu na makini kwa miaka kumi. Alitaka mke mzuri, mwaminifu na mwenye tabia ya kuigwa katika nyumba. Alifanikiwa hata akaoa mke wake Amina. Baada ya miaka kumi mke wake alifariki dunia. Shaabani aliomboleza kifo cha mke wake hata akatunga shairi la msiba huo. Yasemekana kuwa mke wake aliacha watoto watano, dada yake mwana Saumu na mama yake. Alivumilia maisha ya ugane kwa miaka mitano. Kisha akaposa mke wake wa pili na kuoa tena. Alioa mara tatu.
Kuanzia mwaka wa 1926 hata1944, Shaaban alifanya kazi na Idara ya Forodha, Pangani. Alikuwa mtu mwenye kufanya kazi yake kwa uangalifu na uvumilivu hata alipandishwa vyeo viwili katika kazi hii: “Grade III Higher Division” na “Grade II Local Service Council”. Alihamishiwa Mpwapwa mwaka wa 1944 akafanya kazi na Idara ya wanyama hadi 1946. Kutoka 1946 hadi 1952, alifanya kazi ofisi ya mkuu wa Jimbo la Tanga. Kabla ya kustaafu mwaka wa 1959 alifanya kazi na ofisi ya kupima nchi Tanga. Alikuwa mtu mwaminifu, mwenye kupenda urafiki, mvumilivu na mwenye bidii sana. Alipostaafu, akiba ndogo aliyokuwa nayo aliitumbukiza kwa upigishaji chapa uandishi wake. Hii ilikuwa ni kazi ngumu na ya kugharimu fedha nyingi sana. Lakini hakufa moyo kwa maana ilikuwa ni kazi ya hiari na mpenda hiari si mtumwa kama alivyopenda kusema.
Sheik Shaaban alikuwa hodari kwa kazi yake ya uandishi na uendelezaji wa lugha ya Kiswahili. Uandishi wake ulikuwa kazi ya hiyari na matokeo ya mazoezi ya ujana wake. Aliandika hadithi za mawazo yake kama Kusadikika na Kufikirika, Historia kama vile utenzi wa vita vya pili vya dunia, Insha, Magazeti, Tawasifu na vitabu vya wasifu kwa mjazo na ushairi. Lugha aliyoitumia ilikuwa bara bara na uandishi wake ulihusu mambo yanayotokana na wahenga. Alitilia maanani desturi iliyoenea na ile inayoelekea kusahauliwa kwa sababu ilitumiwa na washairi waliotangulia. Uandishi wake ulikuwa na maneno ya hekima tupu na mafundisho yanayowafaa wake na waume katika ndoa, wajane, watoto na hata wazee. Hivyo basi, aliweza kutunzwa kwa zawadi ya waandishi inayoitwa “Margaret Wrong Memorial prize”. Alikuwa mwandishi wa kwanza wa Kiwahili kutuzwa nishani ya “Member of British Empire, (M.B.E.)” kutoka kwa Malkia wa Uingereza. Tuzo nyingine aliyopata ilikuwa nafasi ya kwanza kwa kuandika insha juu ya maisha yake katika shindani lililofanywa Afrika Mashariki. Katika Shindano lingine la uandishi wa insha juu ya utaifa na uzalendo, insha ya Shaaban ilipata zawadi ya kwanza. Shindano hili lilitolewa na serekali ya Bara la Hindi.
Katika uendelezaji wa lugha, Shaaban alijiunga na vyama kama vile, “East African Swahili Committee, East African Literature Bureau, Tanganyika Language Board, Tanga Township Authority”. Aliheshimiwa Dar es Salaam akawa mtu wa pili kati ya watu kumi na mmoja kupewa shahada ya kutoka chuoni. Waziri wa Elimu Dar es Salaam mwaka wa 1966, alimsifu Shaaban na kusema kuwa jina lake limeota mwamba usiobomoka mioyoni mwa waafrika wengi wa Afrika Mashariki.
Shaaban alifungua duka lake la vitabu Julai 1960. Alisaidiwa na rafiki yake Mzungu kupigisha chapa katika kiwanda kingine Kenya. Biashara hii ilikuwa ngumu kwa maana watu wengi walikuwa hawajui kusoma na kuandika. Wachache waliojua kusoma na kuandika, hawakuwa na fahamu kwamba katika vitabu ndimo ghala za utamaduni na elimu hupatikana. Alifurahia kuwapa hawa watu wachache vitabu vyake wasome bure. Hodari huyu wa lugha ya Kiswahili ameandika zaidi ya vitabu ishirini vya Mashairi. Katika vitabu vyake, amewashawishi wasomaji wasome mara kwa mara kuendeleza lugha. Ingawa hayuko sifa zake bado zaenea na vitabu vyake vyatumika kwa ufundishaji wa lugha katika vyuo vya Tanzania, Kenya na kwingineko ulimwenguni wanakofundisha lugha ya Kiswahili.
Alifariki tarehe 22 Juni mwaka 1962. Mpaka anafariki kwa maradhi ya moyo na upungufu wa damu, Shaaban Robert alifanikiwa kuandika vitabu 24 kwa lugha adhimu ya Kiswahili, na mpaka sasa kazi zake zinazidi kukusanywa na taasisi ya uchunguzi na kukuza Kiswahili (TUKI) ya chuo kikuu cha Dar es Salaam. Kipo kitabu cha 25 ambacho kilitolewa miaka ya karibuni ambacho kina barua alizokuwa akiandikiana na jamaa zake.
Katika kitabu hicho kumeonekana uwezo mkubwa aliokuwa nao Shaaban Robert katika kuchagua maneno na ufasaha wa lugha ya Kiswahili na Kiingereza. Kwani watu wengi walidhani Shaaban Robert hakuwa mjuzi wa lugha ya Kiingereza lakini katika barua zake zipo ambazo aliziandika kwa lugha hiyo ya kigeni kwa ufasaha wa hali ya juu.
1.3 Muhtasari wa kitabu
Adili na Nduguze ni riwaya iliyotungwa na Shaaban Robert; mwandishi mashuhuri (maarufu) kutoka Tanzania. Riwaya hii ilitungwa mnamo 1952. Katika riwaya yake anashughulika na mambo mengi kuhusu tabia mbalimbali za watu. Mtunzi anatueleza kuwa tushinde uovu kwa kutenda mema yaani “Wema hauozi”. Adili alimwokoa Huria wakati alipokaribia kuuwawa na Hunde. Kutokana na wema huo, Huria naye alimwokoa Adili wakati alipotoswa baharini na ndugu zake. Haya yanazingatiwa na msemo wa Kiswahili “kinifaa huangua, nitakufaa kwa mvua” au methali isemayo “Mwosha huoshwa”. Katika kufikisha ujumbe mwandishi ameijenga kazi yake kwa kuwahusisha wahusika mbalimbali. Amemchora Mfalme Rai kuwa ni kiongozi mzuri na mfuatilizi bora wa kazi ambayo humwezesha kuistawisha nchi yake ya Ughaibu katika mifugo. Mshauri wake Ikibali alikuwa bingwa wa uchunguzi wa kodi za wanyama ila alielemewa na siri ya kiongozi wa Janibu, Adili kuwaadhibu vikali manyani waliokuwa kwake. Alishangaa kuona jinsi ukatili huo ulivyohitilafiana sana na tabia ya wema na huruma ya Adili akaamua siri hiyo ifichuliwe mbele ya Mfalme Rai. Alipoletwa mbele ya Mfalme Rai, Adili alijitetea akieleza kuwa wanyama hao walikuwa zamani nduguze kwani walizaliwa na baba mmoja, Faraja. Alijulisha kuwa alilazimika kuwagawia urithi wake wakati walipofilisika ugenini na kurejea nyumbani kwao Janibu. Alisimulia jinsi ndugu wote watatu walivutwa na faida za biashara na kusafiri mpaka walipoufikia mji wa mawe, Adili alipokutana na mchumba, Mwelekevu. Hapo hapo, Adili alieleza kuwa uovu waliomfanyia nduguze ndio uliwafanya wageuzwe kuwa manyani. Kwanza kutokana na mali aliyoleta jahazini na mwanamke huyo mrembo kutoka mji wa mawe, nduguze walimwonea wivu na kumlia njama za kumtosa baharini. Wakati huo huo, aliokolewa na jini, Huria binti Kisasi, ambaye aliwahi kulisaidia liliposhambuliwa na nyoka, ama jini jingine Hunde. Adili aliporejea katika chombo akiwa na Huria, jini hilo ndipo liliamua kuwafanya manyani ikiwa ni adhabu na kutoa amri ya kuwa watapigwa kila siku kutokana na maovu yao. Adili aliporudi nchini mwake, Ughaibu, ndiye aliadhibiwa wa kwanza kwa kusahau kuwapiga manyani. Tokea hapo ilikuwa mazoea yake kuwapa chakula na kuwapiga vikali hadi siku Ikibali alipogundua siri hiyo. Baada ya kisa hicho, Mfalme Rai almsihi Adili asiwapige tena manyani ila awatunze vizuri na kula nao. Alijitahidi kuwaombea msamaha kwa Mfalme wa majini Kisasi na bibiye Huria. Ombi lake lilisikilizwa na nduguze Adili waligeuzwa kutoka uhawayani na kuwa watu tena. Siku hiyo ilikuwa ya furaha, na nduguze wote watatu walifunga ndoa pamoja.
1.4 Nadharia / mkabala wa Ki-akisiko/kifumano
Nadharia hii inaelezea fasihi kama inayoakisi uhalisia uliopo nje yake. Mawazo ya aina hii yanahusishwa na Lenin. Mtaalamu huyu aliziona kazi za Leo Tolstoy kama zilizoakisi mikinzano ya kijamii iliyoishia kuyasababisha mapinduzi ya Urusi. Kwa njia hiyo ni kazi za kifanisi. Mkabala huu unategemezwa kwenye itikadi ya kiujumi iliyokuzwa na Myunani Aristotle katika dhana yake ya ‘muhakati’ au ‘mimesia’ pamoja na msimamo wa Marx kuwa uhalisia ulio wazi au dhahiri unachukua nafasi ya kwanza kabla ya mawazo akilini. Mhakiki wa Ki-hungary, George Lukacs anayehusishwa na mkabala huu anaichukulia fasihi kama maarifa ya uhalisi. Hii haina maana kuwa lazima pawepo na mfanano wa moja kwa moja na uhalisi. Uhalisi huo lazima ushughulikiwe na ubunifu wa mwandishi, na kazi yake inayoupa muundo maalum. Katika msingi huu panakuwapo na jinsi mbalimbali za kuwasilisha uhalisi fulani. Njia hizi hutofautiana katika mkazo wa masuala fulani yanayoshughulikiwa. Mkabala huu unakuwa msingi mzuri wa kuzitathimini kazi fulani katika msingi wa uhalisia au utohalisia (Wamitila 2002).
Hivyo basi, nadharia ya ki-akisiko/kifumano ni nadharia ambayo hujikita katika mambo yaliyopo yaani uhalisia wenye matukio mahususi na matokeo yanayoweza kuthibitika na mambo yasiyokuwepo yaani utohalisia ambao matukio yake ni vigumu kuyathibitisha kama sehemu ya uhalisia. Tukirejelea katika riwaya ya “Adili na Nduguze”mwandishi amejikita katika uhalisia na utohalisia kwani amezungumzia mambo ambayo yanajitokeza na yapo katika jamii na yale ambayo ni sehemu ya utohalisia kwani yanasikika yakisemwa lakini kuyathibitisha kama sehemu ya uhalisia ni vigumu. Hivyo tutatumia nadharia hii kuhakiki maudhui yaliyojitokeza katika kitabu hiki kwa kuwa kitabu hiki kinasawiri mambo ambayo yapo katika jamii zetu na yale ambayo ni utohalisia.
1.5 Nadharia ya Umuundo
TUKI (2004) wanaeleza nadharia kuwa ni mawazo, maelezo na muongozo uliopangwa ili kusaidia kueleza kutatua au kutekeleza jambo fulani. Nadharia yoyote ile ya kihakiki ni nyenzo ya kusaidia kufikisha lengo fulani.
Ntarangwi (2004) anasema kuwa umuundo waweza kuelezwa kama mtizamo wa kitathimini ambao huzingatia zaidi miundo inayojenga kazi binafsi. Mwasisi anayetajwa sana katika nadharia hii ni Ferdinard De saussure aliyependekeza mtizamo mpya kuhusu lugha. Kinyume na wataalamu wengine walioshughulikia historia na sura maalum za lugha fulani, Saussure alivutiwa na miundo inayohimili lugha zote, huku akijaribu kuonyesha kwamba lugha zote za ulimwengu zaweza kutathiminiwa kwa kaida maalum za umuundo. Alizua istilahi `parole’ na `langue’ kueleza maoni yake: `Parole’ au uzungumzi ni lugha katika matumizi na hiki ndicho walichokizingatia wanaisimu wa awali, lakini Saussure alivutiwa na mfumo wa kinadharia unaounda lugha zote au `Langue’ – yaani masharti au kaida zinazoiwezesha lugha kuwepo na kuweza kufanya kazi. Hata hivyo, kazi ya Saussure ilikuwa imetengewa wanaisimu peke yao. Katika miaka ya 1950, mtizamo huo wa Saussure ulianza kusambaa katika masomo mengine hasa wakati mawazo yake yalipozingatiwa na Mwanaanthropolojia Claude Levi-strauss. Kwa kuchukua maoni ya isimu ya Saussure na kuyaingiza katika sayansi ya kijamii. Hasa alichotaka kuendeleza kidhana ni kwamba pana viwango viwili katika kuelewa maisha ya jamii, isimu, lugha na chochote kingine kile. Viwango hivi ni cha juu juu (surface) na cha ndani (deep).
Mkondo huu wa mawazo ya umuundo kuhusu sayansi za jamii ulianzia ulaya na kuathiri mtazamo wa elimu mbalimbali (duniani) kama vile: Falsafa, Anthropolojia, Historia, Uhakiki wa kifasihi na Sosiolojia. Kwa hivyo twaweza kuangalia jamii katika muundo wake wa kijuu juu na kuielewa lakini tukitaka kupata maana mwafaka lazima tuchunguze muundo wake wa ndani ambao hupatikana katika kila jamii ya wanadamu. Kwa hiyo hata katika kuielewa fasihi lazima tuifahamu lugha yake. Katika kupata maana lazima kuwe na uhusiano wa kipembetatu yaani kuna dhana, alama na kitajwa.
Kama vile muundo wa lugha ulivyo mfumo, muundo wa fasihi pia una vipengele vinavyotegemeana na vinavyoelezwa katika muktadha wa vipengele vingine. Katika kazi ya fasihi kuna kitengo cha kisanaa kama vile maudhui, ploti, wahusika, muktadha na lugha. Hakuna kipengele cha fasihi kati ya hivi kitakachoelezwa katika upekee wake. Lazima kielezwe kwa kuzingatia kuwepo kwa jukumu la vipengele vingine. Kwa mfano katika kueleza au kuzungumzia ploti, wahusika watashirikishwa na lugha yao kuzingatiwa. Kwa hiyo nadharia ya umuundo husisitiza vipengele vya kazi ya sanaa jinsi vinavyohusiana hadi kuikamilisha kazi hiyo. Huangalia namna sehemu mbalimbali za kazi za sanaa zilivyofungamana. Yaani Neno halihitaji urejelezi ili lipate maana, na kazi yenyewe ilivyoundwa ndivyo hutoa maana. Yaani maana inavyoumbwa ina dhima kubwa kuliko maana yenyewe.
Hivyo nadharia hii tutaitumia katika kuchambua sehemu ya fani katika riwaya ya “Adili na Nduguze” kwani nadharia hii itatusaidia kuibua vipengele vilivyoijenga fani na kuifungamanisha katika kutoa kusudio la Msanii kwa jmii husika.
2.0 Maudhui katika Riwaya ya “Adili na Nduguze”
Kwa mujibu wa Madumulla (katajwa) maudhui ni mawazo fikra na ujumbe uliomo katika kazi ya fasihi. Maudhui ina vipengele mbalimbali ambavyo ni pamoja na dhamira, ujumbe, falsafa, migogoro, msimamo na mtazamo wa mwandishi. Katika riwaya ya “Adili na Nduguze” vipengele vya maudhui vinavyojipambanua au kujidhihirisha ni pamoja na:-
2.1 Dhamira
Madumulla (katajwa) anasema dhamira ni wazo kuu katika kazi ya fasihi. Dhamira ni sehemu tu ya maudhui. Dhamira ndiyo hujenga kiini cha kazi ya fasihi, yafuatayo ni mawazo au dhamira zilizojitokeza katika riwaya hii ya“Adili na Nduguze”
2.1.1 Uongozi mzuri.
Uongozi ni dhana, taaluma inayompa muhusika madaraka na uwezo wa kuwawezesha wale wanaoongozwa naye kuunganisha nguvu, stadi na vipaji vyao na kuvitumia ili kufikia malengo yao. Kuongoza ni kujua lengo la wale wanaoongozwa na njia ya kufikia lengo lao (www. Sw.wikipedia. org/wiki/uongozi)
Katika riwaya hii ya Adili na Nduguze suala la uongozi mzuri limejitokeza. Tunamwona jinsi Rai alivyokuwa kiongozi muadilifu na mfalme mwema sana katika jamii yake. Hakuwa na tabia ya kumlazimisha mtu kufanya kazi bali aliwashawishi watu kufanya kazi. Alijituma katika kufanya kazi kwa bidii zake zote, hakusita kufanya kazi iwe kubwa au ndogo. Mwandishi anasema;
“Kwa bidii zake kubwa aliweza kushiriki katika mambo mengi ya maisha, akasaidia maendeleo makubwa ya nchi yake. Hakulazimisha mtu yeyote kutenda tendo Fulani, lakini alishawishi kila moyo wa mtu kuiga alivyotenda kwa hiyari yake mwenyewe, alikuwa na mvuto mkubwa juu ya mioyo ya watu. Alitumia mvuto huu juu ya watu mpaka nchi yake ilikuwa haina mvivu, goigoi wala mwoga” (uk 2).
Tukilejea katika jamii ya sasa suala la uongozi mzuri linasisitizwa ili kufikia malengo ya kimaendeleo. Wapo viongozi ambao ni wazuri na uongozi wao ni bora wakiwa wanawajibika katika kuangalia maendeleo ya jamii zao.
2.1.2 Matabaka
Kwa mujibu wa
Katika riwaya hiii ya Adili na Nduguze suala la matabaka limejitokeza kwani tunaona kuna matabaka kati ya mtawala na mtawaliwa. Kwa mfano kuna Rai ambaye ndiyo mfalme wa Ughaibuni na Watawaliwa ambao ndio raia wa ughaibuni. Mwandishi anasema;
Rai, mfalme wa Ughaibu, alikuwa mfalme wa namna ya peke yake duniani.
“……Kutawala suluhu na mapenzi ya wanadamu, utunzaji wa wanyama, na utii juu ya viumbe wasioonekana kama majini hutaka uwezo mkubwa sana. Kmama hivi, fikiri wewe mwenyewe jinsi Rai alivyojipambanua mwenyewe na wafalme wengine”.
Tukilejea katika jamii zetu pia suala la matabaka halipingiki kutokana na kuwepo kwa mgawanyo wa kazi. Yapo matabaka katika nyanja za uongozi, elimu, siasa na hata nyanja za kiuchumi na kidini.
2.1.3 Mapenzi ya kweli
Katika riwaya hii suala la mapenzi ya kweli limejidhihirisha kwani tunamwona muhusika Adili jinsi alivyokuwa na mapenzi ya kweli na ndugu zake. Kwani hakuwa mbinafsi kwa kuwa alikuwa tayari kugawana na yeyote chochote alichokuwa nacho. Mwandishi anasema;
Adili alikuwa tayari siku zote kugawana na mtu yeyote tonge moja la chakula lililokuwa mikononi mwake” (uk. 12).
2.1.4 Ukaidi na Dharau
Katika riwaya hii ya “Adili na Nduguze” watawala wa mji wa mawe ambao ni mfalme Tukufu na Malkia Enzi na raia wao walikuwa waabudu mizimu. Walionywa kuachana na tabia hiyo na Mrefu ambaye alikuwa ametumwa kuja kuwaonya juu ya kuabudu mizimu ambayo ilikuwa ni miti na matokeo ya kaidi hiyo, mji na watu wote waligeuzwa mawe isipokuwa Mwelekevu ambaye alikuwa Binti mfalme kutokana na utii wake kiimani. Mwandishi anasema
“Tukufu hakujali onyo hili akahamrisha kushikwa kwa Mrefu aliyekuwa hasogeleki wala hashikiki……………, kwa laana iliyotamkwa na Mrefu……………kila kiumbe kilichokuwa na maisha katika
fahari kiligeuka jiwe” (uk 29)
2.1.5. Suala la Imani
Imani lina maana mbalimbali (mfano. “huruma”), na maa kuu inahusiana na kitenzi kuamini, kinachofanana nakusadiki. Hapo ni kukubali ukweli wa jambo lisiloweza kuthibitishwa. Katika dini msingi wake ni mamlaka ya Mungu aliyeshirikishwa ukweli huo kwa njia ya ufunuo maalumu ili kumsaidia binadamu amjue yeye, ajifahamu pamoja na maisha yake duniani na ahera. Kwa msingi huo, au wa namna hiyo, mtu anaweza kushikilia jambo bila ya uthibitisho mwingine, ingawa pengine Ukristo unatia maanani pia akili katika ujuzi wa ukweli.
Katika riwaya hii ya ‘Adili na Nduguze’ suala la Imani limejitokeza kwani tunaona kuwa mfalme Tukufu na malkia Enzi na raia ambao waliishi katika mji wa Mawe walikuwa wanaamini katika mizimu, Mizimu hiyo ilikuwa ni miti ambapo baadae miti hiyo iligeuka na kuwa mawe ukutani. Mwandishi anasema;
“Walakini, juu ya sifa hizo, malkia, mfalme na raia walikuwa waabudu mizimu. Mizimu yao ilikuwa miti. Miti yenyewe ni ile iliyogeuka kuwa mawe ukutani. Kawere, mganga na imamu wa mizimu hiyo alivuta mioyo ya watu wote”(uk. 27).
2.1.6 Suala la ukatili
Suala la ukatili limejidhihirisha wazi katika riwaya hii. Tunaona jinsi Ndugu zake Adili (waliitwa Mwivu na Hasidi) walivyomtosa Adili baharini wakati wakiwa katika jahazi kuelekea Janibu, huku lengo lao likiwa ni kumuuwa ndugu yao ili waweze kumuoa kiushirika Mwelekevu ambaye alikuwa ni mchumba wake Adili, kutokana na uzuri aliokuwa nao yule msichana. Mwandishi anasema;
“Alitoswa baharini kama kitu kilichokuwa hakifai.”
Vilevile katika jamii zetu suala la ukatili lipo. Kuna watu ambao wamejeruhiwa na hata kuuawa na ndugu au rafiki zao kwa sababu ya migogoro inayosababishwa na mapenzi.
2.2 Migogoro
Kwa mujibu wa TUKI (2004) wanasema kuwa migogoro ni hali ya kutofautiana baina ya pande mbili au zaidi, wanasema migogoro inaweza kuwa ya familia, matabaka ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni. Katika riwaya hii imejitokeza migogoro tofautitofauti kama ifuatavyo:
Mgogoro kati ya Mrefu na Tukufu. Mgogoro huu ulitokea baada ya Mrefu kumshauri Tukufu kuachana na kuabudu mizimu, lakini Tukufu alikaidi. Suluhisho la mgogoro huu ni kuwa mtu akikaidi mambo ya kiimani hudhurika.
Mgogoro kati ya Adili na Ndugu zake. Mgogoro huu unatokea pale ambapo Adili aligawa sawia mali zake kwa nahodha,na ndugu zake alizozipata kutoka katika mji wa mawe, lakini ndugu zake hawakuridhika kwani walitaka wapate zaidi. Vivyo hivyo, mgogoro unajitokeza pale ambapo walimtosa Adili baharini kwa lengo la kutaka kumuoa mchumba wake (Mwelekevu). Suluhisho la mgogoro huu ni kuadhibiwa kisheria, kutokana na kufanya matendo ya kihalifu na unyama kwa binadamu.
Mgogoro kati ya Hunde na Huria. Mgogoro huu unajitokeza pale ambapo Hunde ambaye ni jini, anamwitaji Huria kimapenzi, ambaye ni mtoto wa mfalme wa majini lakini Huria anamkataa Hunde. Suluhisho la mgogoro huu ni kuwa Hunde anaemlazimisa Huria kumkubali kimapenzi ni kushtakiwa kisheria na sheria kuchukuwa mkondo wake.
2.3 Ujumbe
Kwa mujibu wa Madumulla (katajwa) ujumbe ni kitu ambacho mwandishi hudhamiria kumtumia msomaji, kila kazi ya fasihi hubeba ujumbe ambao msanii hutaka umfikie msomaji wake. Katika riwaya ya hii kuna ujumbe wa aina tofauti tofauti uliojitokeza kama ifuatavyo: - Uongozi mzuri na uadilifu ndiyo chanzo cha maendeleo.
- Majuto ni mjukuu
- Ukaidi na dharau ni chanzo cha madhara
- Bidii katika kazi ni chanzo cha maendeleo
- Imani ni ukombozi
2.4 Falsafa
Kwa mujibu wa Madumulla (katajwa) akimrejelea Msokile (2009) falsafa ni wazo ambalo mtu anaamini kuna ukweli fulani unaohusu maisha yake pamoja na maisha ya jamii. Katika riwaya hii ya ‘Adili na Nduguze’ mwandishi anaamini kuwa uadilifu katika uongozi ni nguzo ya maendeleo katika jamii.
2.5 Msimamo
Kwa mujibu wa Madumulla (katajwa) ni mawazo, mafunzo na falsafa ya msanii. Hubainisha msimamo wake kuhusu masuala mbalimbali ya kijamii na ndiyo huweza kuwatofautisha wasanii wawili au zaidi wanaoandika kuhusu mazingira yanayofanana. Msimamo wa riwaya ya Adili na Nduguze ni wa kiimani kwani amesisitiza kuachana na masuala maovu yasiyompendeza Mungu ikiwa ni pamoja na kuabudu mizimu na badala yake kutenda yale yanayompendeza Mungu na binadamu ikiwa ni pamoja na kumwabudu Mungu.
Fani katika riwaya ya “Adili na Nduguze”
Fani ni jumla ya mbinu, ufundi na mtindo wa vipengele vingine vinavyotumika kuwasilisha maudhui (Mhilu na wenzake 2008). Huu ni ufundi wa kisanaa autumiao msanii katika kutoa ujumbe wake kwa hadhira iliyokusudiwa. Fani imegawanyika katika vipengele vikuu viwili ambavyo ni muundo na mtindo
3.1. Mtindo
Kwa mujibu wa Senkoro (1982) anasema mtindo katika kazi ya fasihi ni ile namna ambayo msanii hutunga kazi hiyo na kuipa sura ambayo kifani na kimaudhui huainisha kanuni au kawaida zilizofuatwa (za kimapokeo ama za pekee). Pia Wamitila (2003) anasema mtindo ni jumla ya mbinu au sifa zinazomwezesha mwandishi kuwasilisha ujumbe wake, huelezea mwandishi alivyounda kazi yake.
Hivyo tunaweza kusema mtindo ni ule upekee alionao mtunzi wa kazi ya fasihi katika kuipa kazi yake sura fulani kifani na kimaudhui ambao mtunzi mwingine hawezi kufanya hivyo hata kama kinachozungumziwa ni kilekile. Mtindo ndiyo jinsi msanii alivyotumia ufundi, umahiri na hisia zake katika kutenda au kueleza jambo fulani. Mtindo huu ndio hutofautisha kati ya msanii mmoja na mwingine.
Katika riwaya hii ya ‘Adili na Nduguze’ msanii ametumia mtindo wa masimulizi katika kueleza visa na matukio, kwani tunaona msanii anaeleza kisa kinachomhusu Adili na nduguze, Hasidi na Mwivu. Mwandishi anaeleza jinsi vituko vilivyotiririka tokea mwanzo, ndugu hawa watatu waliokuwa wakitoka familia moja, ndugu wawili, (waovu) Hasidi na Mwivu, waliomfanyia Adili na malipo ya uovu huo (kama upeo wa kugeuzwa manyani na kupata adhabu ya kupigwa kila siku). Mwishoni kabisa anaujadili msamaha waliopewa ndugu hao. Kutokana na majuto na ahadi ya kutorudia tena uovu huo.
Pia msanii ametumia mtindo wa nyimbo ili kufikisha ujumbe. Mfano katika uk. 26, msanii ametumia nyimbo katika kutoa sifa ya msichana mrembo aliyekutana na Adili katika mji wa mawe. Vilevile katika uk. 42, msanii ametumia nyimbo akionyesha jinsi Adili alivyokuwa akijutia kuwaadhibu ndugu wa damu yake. Pia msanii ametumia nyimbo katika uk. 48 ambapo uliwakilisha kusherekea baada ya kupata msamaha kutoka kwa mfalme wa majini.
Aidha, msanii ametumia mtindo wa barua katika uk. 44, ambapo amemchora mfalme Rai akiandika barua kwa mfalme wa majini inayohusu kuomba msamaha kwa ajili ya ndugu zake Adili waliogeuzwa manyani kusamehewa. Na matokeo yake msamaha wanaupata na kurudi katika hali yao ya kawaida.
3.2 Muundo
. Hapa tunachunguza jinsi msanii wa kazi ya fasihi anavyofuma, unda na kuunganisha matukio moja baada ya jingine, wazo na wazo, ubeti na ubeti, hata mstari wa ubeti. Baadhi ya vipengele vya kimuundo vinavyotumika zaidi ni mistari, beti, mizani na vina. Hivyo, katika muundo tunaangalia umbo la kazi ya fasihi mfano, yaweza kugawanywa katika sura mbalimbali, sura hizi ndizo hujenga muundo
Mtindo wa riwaya hii ni mtindo wa rejea. Mwandishi huanza kuisimulia riwaya yake wakati Adili anapofanya ukatili wa kuwaadhibu manyani (ambao walikuwa nduguze). Kugundulika kwa uovu huu ndiko kulifuatiliwa na maelezo ya kisa na sababu ya nduguze kuwa manyani na hatimaye kuwa watu tena baada ya ombi la Mfalme Rai kukubaliwa na majini.
Muktadha
Muktadha ni jumla ya mazingira ambamo kazi ya fasihi inafanyikia. Muktadha wa riwaya hii ni ya nchi ya Ughaibu, yaani nchi ya mbali. Nchi hiyo ni ya kufikirika kwa kuwa haipo katika mazingira ya kawaida. Kuna vituko vichache vilivyotokea katika nchi za kigeni zisizotajwa kwa majina na vingine vilitokea katika nchi ya majini.
3.5. Wahusika
Wahusika katika riwaya ya “Adili na Nduguze”, wana majina yanayowiana na tabia zao. Wale ambao hawakubadilika kitabia kama Adili, Mfalme Rai ni wahusika bapa. Wahusika Huria, Hasidi na Mwivu ambao walibadilika kitabia ni wahusika duara. Wahusika hao na sifa zao ni kama ifuatavyo:
3.5.1 Adili
Huyu ni mhusika mkuu wa riwaya hii. Alikuwa mwema, mwenye huruma, msamehevu, mvumilivu na mwenye mapenzi ya kweli, jasiri na mfanyabiashara hodari. Tabia yake ile haikubadilika toka mwanzo hadi mwisho wa hadithi. Kwa hiyo, tabia yake ni mhusika bapa kielelezo.
3.5.2 Hasidi na Mwivu
Hawa ni ndugu zake Adili. Walikuwa watu wakatili, wenye tamaa, choyo kubwa na wabadhilifu kitabia, kwa hiyo ni wahusika duara.
3.5.3 Mfalme Rai
Huyu alikuwa mtawala wa nchi ya Ughaibu ambaye aliiletea nchi yake ustawi wa kiuchumi kutokana na uongozi mzuri, ufuatilizi bora wa kazi na ushauri wa kuwahimiza raia kuwa wachapakazi.
3.5.4 Ikibali
Huyu ni mshauri wa Mfalme Rai na halmashauri yake. Alikuwa mcheshi na mtu aliyechukuana na watu kutokana na kuwatunzia haki zao.
3.5.5 Mwelekevu
Huyu ni msichana mwenye upendo wa kweli, mrembo na mwaminifu kidini na kindoa.
3.5.6 Huria
Huyu ni jini aliyekuwa na uwezo mkubwa wa kutenda kila jambo alilotaka na kujigeuza sura kwa utashi wake (mhusika duara)
3.5.7 Mfalme Tukufu na Malkia Enzi
Hawa ni watawala ambao walipuuzi/walidharau ujumbe wa Mola, wakaadhibiwa kugeuzwa mawe, mji wao na raia wao.
3.5.8 Mfalme Kisasi
Huyu ni mfalme wa majini aliyewaelekeza raia wake majini kutii uongozi wa binadamu.
3.3 Matumizi ya lugha
Williady (2015) anaeleza kuwa matumizi ya lugha ni ustadi wa msanii katika kutumia lugha itakayoleta mvuto kwa wasomaji au wasikilizaji wa kazi ya fasihi.
Lugha ya Shaaban Robert katika riwaya ya Adili na nduguze ni rahisi na inayoeleweka. Ni lugha yenye msamiati wa kawaida, misemo ya kawaida, nahau na methali nyingi. Pia ametumia lugha ya ushairi, lugha ya picha na tamathali za usemi za kipekee. Kuna wakati mwandishi huyu alipotumia lugha ya kisheria katika barua, na hayo yote ni kuonyesha jinsi ana ustadi wa kuimudu lugha ya Kiswahili katika nyanja zake zote.
3.3.1 b) Matumizi ya methali, nahau, mashairi na misemo
2.2.1.1 Misemo
Misemo ni maneno yanayotumiwa na makundi maalumu ya watu katika jamaii yaliyo jitenga kwa kufuatana na mambo yanayo pendelea, mazoea, kazi au shughuli yao, nafasi yao katika jamii. Ni semi fupi amabazo hutumiwa mara kwa mara kwa lengo la kuleta maana maalumu. (Mwansoko 1994) Misemo iliyotumika katika riwaya ya Adili na Nduguze ni;
(i) Atakaye makaa ya mgomba hapati kitu ila jivu tupu (uk. 39.)
(ii) Damu nzito kuliko maji (uk. 40)
(iii) Mwenye saburi hukidhiwa haja zake (uk. 45)
(iv) Busara kubwa kichwani haina faida kama moyoni hamna chembe ya wema (uk. 10).
- i)Methali
Ni usemi mfupi w matokeo unaodokeza kwa muhtasari fikra au mafunzo mazito yatokanayo na uzoefu wa maisha ya jamii husika. Kauli fupi zenye pande mbili za fikra(www. Wikipedia.org)
Methali zilizojitokeza katika riwaya ya Adili na Nduguze ni;
(i) Mtu huchuma juani akala kivulini (uk. 14).
(ii) Mali bila daftari hupotea bila habari (uk. 12).
- c) Matumizi ya nyimbo
Katika riwaya ya Adili na Nduguze, mwandishi ametumia nyimbo ili kuwasilisha ujumbe alioukusudia kwa hadhira. Nyimbo zimetumika katika (uk.26, 42, 48)
Mfano katika uk. 26 mwandishi anasema;
“ Miguu ya msichana,
Na mwendo aliokwenda,
Adili alipoona,
Moyowe ulimshinda.
- Alikuwa na miguu,
Mfano wa cherahani,
Wala ulimwengu huu,
Hajatokea kifani.
Msanii alitumia ushairi kueleza kwa usanii uzuri wa Mwelekevu”
Tamthali za usemi
Senkoro (1984) anasema tamathali za semi ni maneno, nahau au sentensi ambazo hutumiwa na wasanii ili kutia nguvu katika maana, mtindo na hata sauti katika maandishi ama kusema. Pia Msokile (1992) anasema tamathali za semi ni fungu la maneno lilogeuzwa maana yake kamili ili kuiwakilisha maana nyingine.
Hivyo basi, tamathali za semi ni matumizi ya maneno kwa namna fulani ili kuifanya lugha iwe ya kuvutia na kuifanya kazi ya sanaa iwe ya kupendeza. Vipengele vya tamathali za semi ambavyo mwandishi amevitumia katika riwaya ya ‘Adili na Nduguze’ ni pamoja na tashibiha, sitiari, taswira, tashihisi na tafsida. Vipengele kama hivyo ni muhimu sana katika kuunda au kutoa msisitizo wa maana pamoja na kuunda maana mpya katika kazi ya fasihi.
– Tashbiha:
Hii ni mojawapo ya tamathali za semi ambayo inafanya kazi ya kulinganisha vitu viwili visivyo na hadhi sawa kwa kutumia viunganishi kama vile mithili ya, kama. Tamathali hii ya semi huweza kufanya kazi endapo kuna vitu vinavyolinganishwa wakati kimoja hutumiwa katika kukirejelea kingine. Katika riwaya hii ya ‘Adili na Nduguze’tashibiha zilizotumika ni pamoja na;
(i) Moyo wake ulifumwa na msiba akalia kama motto mdogo (uk.41).
(ii) Tabia yake ijigawa katika theluthi tatu mbalimbali kama rangi ya ngozi ya pundamiliya (uk. 1)
(iii) Alitoswa baharini kama kitu kilichokuwa hakifai (uk. 3)
Tashihisi
Mhilu na wenzake (2008) anasema tashihisi ni tamathali ambayo vitu visivyo na sifa walizonazo watu hupewa sifa hizo. Hivyo, tashihisi ni vitu kama vile jiwe, mti na hata kichaka hupewa sifa ya kutenda kama binadamu afanyavyo. Katika riwaya hii, Tashihisi zilizotumika ni pamoja na;
(i)Wakati umefika wa mawe kusema, miti kujibu na wanyama kuwa watu (uk. 9).
(ii) Mimea hii ilieneza neema ya vyakula kwa watu na malisho ya wanyama (uk. 3).
(iii)Mazizi yote katika miliki yake amekwishalipa kodi zake, ila mazizi ya Janibu (uk.3).
(iv)Atasema kweli, na manyani yatakuwa mashahidi (uk. 9)
Mjalizo
Hii ni aina ya tamathali za semi ambazo msanii/mwandishi huitumia kutaja vitu au mambo yaliyo katika orodha bila kutumia viunganishi
(i) Zilipatikana pacha katika mbuzi, kondoo, ng’ombe, farasi na wanyama wengine (UK. 1)
(ii) Sebule hiyo ilikuwa imesakifiwa kwa marmar za rangi tatu, yaani, nyeupe, nyekundu na samawati (uk. 5).
MAREJEO
Senkoro, F.E.M.K (1982) Fasihi. Dar es salaam: Press and Publicity Centre.
Wamitila, K.W. (2003) Kichocheo cha Fasihi Simulizi na Andishi. Naiobi: Focus Publishers.
26
Mhilu, G. G na Masebo, J. A (2008) Kiswahili kwa Shule za Sekondari Kidato cha Tatu. Nyambarinyangwine Publishers: Dar es salaam.
Mulokozi, M. M. (1996). Fasili ya Kiswahili. Chuo kikuu huria cha Tanzania: Dar es Salaam
TUKI (2004) Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Oxford University Press: Dar es saam.
|
|
|
|