MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI

Welcome, Guest
You have to register before you can post on our site.

Username
  

Password
  





Search Forums

(Advanced Search)

Forum Statistics
» Members: 5,481
» Latest member: Kundlimatching
» Forum threads: 2,178
» Forum posts: 2,256

Full Statistics

Online Users
There are currently 32 online users.
» 0 Member(s) | 31 Guest(s)
Bing

Latest Threads
Buy Vilitra 60 Mg |【Get E...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-24-2023, 11:45 AM
» Replies: 0
» Views: 0
How to take Cenforce50?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-19-2023, 12:59 PM
» Replies: 0
» Views: 0
About the Vidalista 60 Mg...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-04-2023, 04:07 PM
» Replies: 0
» Views: 0
What Is Vidalista 60?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-03-2023, 10:49 AM
» Replies: 0
» Views: 0
How to take Cenforce 100 ...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
03-29-2023, 02:37 PM
» Replies: 0
» Views: 66
How is Vidalista 10 Mg us...
Forum: Watunzi wa Kiswahili
Last Post: Kieth_winsett
03-27-2023, 01:26 PM
» Replies: 0
» Views: 117
Obtain Thesis Paper Assis...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Minny02
03-24-2023, 03:01 PM
» Replies: 0
» Views: 200
SEO services for sports f...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Maria Poland
03-17-2023, 01:51 PM
» Replies: 1
» Views: 223
NUKUU ZA KISWAHILI DARASA...
Forum: Nukuu
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:31 PM
» Replies: 0
» Views: 788
NECTA K4 2022
Forum: Mitihani
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:25 PM
» Replies: 0
» Views: 403

 
  MWANDISHI WA RIWAYA YA KISWAHILI NA SUALA LA UKWELI WA MAISHA
Posted by: MwlMaeda - 08-27-2021, 06:00 PM - Forum: Riwaya - No Replies

Mwandishi wa Riwaya ya Kiswahili na Suala la Ukweli wa Maisha
 

J.S. Madumulla
Dokezo
Makala haya yanaanza kwa kutazama kwa ufupi maana ya dhana ya “ukweli wa maisha” kinadharia. Kisha yanaangalia jinsi baadhi ya waandishi wa fasihi ya Kiswahili (hususan riwaya) walivyouakisi ukweli huo wa maisha katika kuyaeleza kisanii matukio ya mazingira yao ya karibu na ya mbali. Suala moja linalozingatiwa ni kujaribu kuona jinsi mwandishi alivyofaulu au kushindwa katika kutoa maudhui aliyokusudia kuyatoa kwa msomaji wake kwa njia ya “ukweli wa maisha” anaousimamia au aliousimamia. Na hatimaye, swali muhimu linalojitokeza ili kujadiliwa ni lile linalohusu “ukweli wa maisha” ambao ungefaa kuzingatiwa na waandishi wetu wa wakati huu. Makala haya yanajiduru katika uwanja wa riwaya tu; kama kuna tanzu nyingine zinazotajwa humu, inakuwa ni kwa kugusia tu. Kisha, mada ya “ukweli wa maisha” ni pana sana. Ingehitaji kurasa nyingi na muda mrefu ili kuijadili kwa utoshelevu. Kwa jinsi hiyo, makala haya yachukuliwe kama ni mchango mdogo katika mada hii, na papo hapo ni kichokozi cha mjadala.
Aristippos: Kwa hiyo, na kapu la takataka nalo ni zuri?
Socrates: Bila shaka; na pia ngao ya dhahabu ina ubaya wake; hasa pale ambapo kapu linafaa kwa kazi yake na ngao haifai kwa kazi yake.
Aristippos: Kwa hiyo basi, unadhani kwamba uzuri na ubaya ni kitu kilekile?
Socrates: Ndiyo, hata wema na uovu ni sawa. Aghalabu ni kwamba kile kitu kifaacho kwa njaa, hakifai kwa homa; na kile kifaacho kwa homa hakifai kwa njaa. Kitu kinachosaidia katika upigaji mbio aghalabu hakifai katika ulingo wa ngumi; na kinachofaa ulingoni huweza kuharibu upigaji mbio. Kila kitu ni chema na kinafaa kutegemea matumizi yake; lakini ni kiovu na kisicho na faida katika uwanja ule ambamo kinaleta uharibifu.1
Xenophon
Kinjeketile: Wao wanataka niseme kuwa maji yalikuwa uwongo. Kwani la uwongo nini hapo?
Kitunda: Maji, yalikuwa kweli? Wewe unaamini? (Kinjcketile anacheka)
Kinjeketile: Unajua kesho watasema nini? Bwana afisa atawaambia watoto – watoto wetu, Kitunda – atawaambia kuwa tuliyofanya sisi makosa. Kupigana ni makosa? Kupigania nchi itakuwa makosa? Anataka na mimi nimsaidie niseme kweli tulikosa. Hapana… Hapana! Sitasema neno hilo. Neno limezaliwa. Watoto wetu watawaambia watoto wao neno hilo. Wajukuu wetu watalisikia. Siku moja neno hilo halitakuwa ndoto, bali ukweli.2
E. Hussein
Kweli hunipa maisha, ya mwangaza wa kandili
Kweli huniadibisha, utu huletwa na kweli
Kweli hunielimisha jinsi ya kuwa kamili
……………………………………………..
Kweli ni sawa na radi, inapotoa kauli
……………………………………………..
Kweli ikifutu neno, haliji mara ya pili.3
 
Sheikh S. Robert
 
Kutokana na madondoo hayo maswali yanayojitokeza haraka ni: je, ukweli wa maisha ni nini? Je, ni ule wa kiujumi unaojadili masuala ya ubaya na uzuri, wema na uovu kama Xenophon anavyoonyesha? Au ni ule ukweli wa kisiasa unaojadili masuala ya haki za binadamu, uzalendo na amani kama anavyoonyesha Ebrahim Hussein? Au pengine ni ule ukweli wa kiadilifu (au wa kifalsafa) kama aonyeshavyo Sheikh Shaaban Robert? Ni lengo la makala haya kuijadili mada ya ukweli wa maisha yakitumia mifano kutoka katika riwaya ya Kiswahili. Tunapenda kutazama nafasi ya ukweli wa maisha kama istilahi muhimu ya kiujumi na kinadharia katika fasihi, na umuhimu wake katika historia ya maendeleo ya mwanadamu. Kwa jinsi hiyo tunaweza kubaini wajibu wa mwandishi katika kuusawiri ukweli wa maisha wa mahali alipo na wakati aliomo.
Katika nadharia ya talsafa ya ufahamu (Erkenntnistheorie) sheria ya msmgi ya ukweli iko katika matendo. Matendo (au uzoefu) ni msingi’na lengo la ufahamu (maarifa), na pia ni kigezo cha ukweli. Ndiyo maana wataalamu wengine wamepata kusema kuwa maisha ndiyo huzindua ufahamu,4 na wala si kinyume chake, ijapokuwa ufahamu unaweza kustawisha maisha.
Tunaweza kuugawa ukweli katika mafungu mawili makubwa ambayo yanahusiana sana, kwa sababu fungu la pili hulitegemea lile la kwanza katika kuwako kwake. Fungu la kwanza ni lile tuwezalo kuliita la “ukweli katika hali halisi” – yaani jinsi ukweli unavyojitokeza katika vipengele mbalimbali vya maisha, k.m. dini, siasa, utamaduni, itikadi, sheria, falsafa, n.k. Ukweli huu unafafanuliwa na wanafalsafa kuwa ni ile hali ya (au sifa za) kauli kukubaliana na maudhui ambayo yanaakisiwa na kauli. Fungu la pili la ukweli ni lile la ukweli wa kisanaa. Katika fungu hili ukweli wa maisha wa kisanaa ni istilahi muhimu katika ujumi na nadharia ya fasihi. Husawiri uswanifu wa ubunaji na matukio halisi ambavyo huwasilishwa kwa hadhira (msomaji au msikilizaji) kwa njia ya kisanaa. Aghalabu jambo au tukio linalosawiriwa halipati maana yake halisi kutoka kwa msanii, bali hupata kutoka katika matamanio, malengo, na vipimo maalumu vya jamii ambamo jambo hilo limetokea. Kauli ya kisanaa ina upekee wake; haifuati kanuni za kisayansi za kauli. Katika sanaa ‘ukweli’ katika kauli huweza kuvuka mipaka ya uhalisi. Kwa jinsi hiyo ili kuweza kugundua ukweli uliomo ni sharti kuisoma kazi ya sanaa kwa uangalifu na kuuelewa mfumo wa usawiri wa matukio.
Kiini cha picha au taswira ya kisanaa ni ule uhusiano wa kitu na msanii ambapo kitu kinasimama badala ya tukio na msanii anawakilisha uakisi wa kisanaa wa tukio hilo.
[Image: p143.gif]
Taswira
 
“A” huumba ‘ukweli’ wa ‘B’ kutokana na maisha ya watu kwa njia ya kauli za kisanaa. Na kauli ya kisanaa inasemekana kuwa ni kweli ikiwa imeakisi vizuri uhusiano wa mtu na ukweli wa asili na wa kijamii.5 Uakisi sahihi hupata msingi wake katika jumuiko la mambo mawili: ufahamu wa kisanaa wa ukweli, na ubora wa kiujumi wa ukweli. Katika maelezo ya kisanaa, msanii hujihusisha zaidi na jinsi ambavyo jambo lingewezekana kutokea au jinsi ambavyo jambo lingefaa litokee lakini katika hali halisi halikutokea au halijatokea hivyo. Nguvu ya usanii (uakisi wa jambo) hutokana na uzoefu wa mwandishi katika mazingira yake na kiwango cha ufahamu wake. Na umuhimu wa kazi ya sanaa unatokana na jinsi mwandishi alivyohusisha kazi yake na matukio muhimu ya wakati wake.
Hapo juu tumesema kwamba ukweli wa kisanaa na ukweli wa kiujumi kwa pamoja hujenga msingi wa uakisi mzuri. Wajibu wa ujumi katika kazi ya sanaa ni kubainisha masuala muhimu ya kiutu, sifa za utu, masuala ya kuujenga wakati ujao (k.m. amani, njaa, ukame, n.k.) kwa kutumia vigezo vya ujumi vya wakati huo. Ijapokuwa ukweli wa kisanaa huweza kuvuka mipaka ya kauli, lakini mara nyingi maana ya taswira za kisanaa inapaswa ilingane na maana ya matukio katika maisha halisi.
Katika kuchunguza maendeleo ya riwaya za Kiswahili tangu enzi za Shaaban Robert hadi sasa tutabaini kuwa tunajishughulisha na utanzu wa fasihi ambao ni hai, tena uliofungamana imara na nguvu au sheria zinazoidhibiti jamii katika vipengele mbalimbali vya maisha. Hii inadhihirisha kuwa asili yenyewe ya fasihi pamoja na tanzu zake ni tukio la kihistoria, ambamo vipengele vyake vyote vya kazi za kisanaa pamoja na mwenendo wenyewe wa kisanaa na sifa zote za fasihi hubadilika daima. Hii ina maana kuwa fasihi ni mfumo wa kisanaa wenye uhai na ambao unaguswa sana na mabadiliko ya maisha.
Katika majaribio ya awali ya uandishi wa riwaya za Kiswahili tunaweza kuona kuwa ijapokuwa mada inayahusu mazingira ya wakati wa sasa, na hivyo kuonyesha usasa wa wakati na mahali, msanii anatumia mbinu za zamani za kisanaa katika kuusawiri ukweli wa maisha. Majaribio haya ya awali yanajitokeza katika mkondo wa riwaya ya kimaadil – Bildungserzaehlungambayo lengo lake la msingi ni kufundisha maadili ya jamii. Namna msanii anavyofundisha maadili ya jamii tunaipata katika jinsi alivyowachora wahusika wake ambao kwao anausawiri ukweli wa maisha. Na ni mhusika mkuu ndiye anayetumiwa kuufafanua, kuhubiri na kuutetea ukweli huo wa maisha. Mhusika huyu, kwa kiasi kikubwa, ana sifa za kitendi, yaani ana nguvu za ajabu na ujasiri usio wa kawaida; ana sifa za uadilifu na akili zisizo na mpaka; tena ana hamu isiyolegea ya kutimiza lengo alilodhamiria kulitekeleza. Mhusika huyu amechorwa na msanii kwa makusudi mazima ya kuumba mfano bora wa kuigwa na kumfanya awe kielelezo cha ukweli na ukamilifu wa maisha. Hebu tuipitie mifano michache ya riwaya zenye wahusika hawa.
Adili na Nduguze (1952) na Kusadikika (1951) ni mifano mizuri ya riwaya za Shaaban Robert za mkondo wa kimaadili. Adili anayapata majaribu magumu, akishindana na watu na majini, na hatimaye anashinda. Vivyo hivyo katika riwaya ya Kusadikika wale wajumbe sita ambao ni mashahidi wa mhusika mkuu, yaani Karama, wanapita katika majaribu magumu na ya kusikitisha kwa ajili ya uzalendo wao, ijapokuwa wenye mamlaka juu yao hawathamini uzalendo wa wajumbe hawa. Hata hivyo hatimaye wanashinda kwa msaada wa Karama. Je, Shaaban Robert anatumia kigezo gani katika kueleza ukweli wa maisha?
Mhakiki mmoja, E. Bertoncini (1977: 85) aliandika kuwa kazi za sanaa za Shaaban Robert ziliathiriwa na ushairi wa kimaadili wa kame ya kumi na tisa na masimulizi ya jadi. Tukiuchunguza huo ushairi wa karne ya kumi na tisa tutagundua kwamba sehemu yake kubwa ilikuwa ni tenzi ambazo zilikuwa na uhusiano wa karibu sana, au wa moja kwa moja na dini.6 Kigezo cha ukweli wa maisha kilikuwa ni dini. Hivyo ndivyo ilivyo hata katika maandishi ya Shaaban Robert. Wahusika wake wamegawika kati ya wazuri na wabaya. Wazuri ni wazuri (wema) wasio na dosari, na wabaya ni wabaya moja kwa moja; na katika migogoro na mikinzano wazuri wanawashinda wabaya. Ndiyo maana Shaaban Robert alijulikana na baadhi ya wahakiki kama ni “mhubiri mimbarini”. Kwa maneno mengine, ukweli wa maisha katika Shaaban Robert au katika kazi za mkondo wa kimaadili umo katika mhusika adili. Katika kuusawiri ukweli huu, msomaji anashuhudia jinsi Shaaban Robert anavyotumia kwa ufundi ujumi wa uzuri na ubaya na lugha ya busara ili kuziteka hisia za msomaji wake.
Mifano mingine ya riwaya zinazoangukia katika mkondo wa kimaadili ni Mtu ni Utu (G. Mhina, 1971) na riwaya za M.S. Abdulla zenye mhusika mkuu Bwana M(u)sa. Wahusika wa Mtu ni Utu ni wa kiShaaban Robert, yaani ni bapa. Pia wamegawanywa katika uzuri unaoshindana na ubaya, na hatimaye uzuri unashinda. Kwa G. Mhina ukweli wa maisha kwa jamii mpya uko katika mhusika adili anayepigania utu – kwa njia ya kuheshimiana, kupendana, kushirikiana, kusameheana, na kufanya kazi kwa bidii. Mhusika mkuu, Sozi, anajaribu kuishi katika maadili haya na kupingana na uovu. Jinsi uovu unavyosamehewa unadhihirisha falsafa ya kibiblia ya kumsamehe aliyekukosea hata mara saba au sabini. Na katika riwaya za M’.S. Abdulla, ijapokuwa tunashuhudia maendeleo makubwa katika mbinu za uandishi wake kama vile lugha na wahusika (kwamba vimekaribiana sana na maisha ya kila siku), bado wahusika wake (hasa mhusika mkuu) wana dalili ya wahusika wa mkondo wa kimaadili. Bwana (M(u)sa ameumbwa juu ya wahusika wengine kwa kuwa na sifa za ukamilifu katika uneni na utenzi wake, na hivyo kuwa mhusika adili. Kisha karibu wahusika wote wa M.S. Abdulla hawakui; mwenendo wao ni wa mlalo.
Tukiichunguza zaidi riwaya ya mkondo huu wa kimaadili ambayo inauchora ukweli wa maisha kwa kumtumia mhusika adili tunayaona masuala mawili ambayo yanaweza kuitwa ni upungufu wa msingi wa riwaya hii. Kwanza, mhusika huyu adili, ijapokuwa anajitokeza kuwa ni shujaa na mtenzi mkubwa, hana saikolojia wala hisia; na kwa jinsi hiyo kwa kiasi fulani anaonekana kama ni kipaza sauti tu cha matukio ya wakati wake.7 Pili, ni suala la uhusiano kati ya mhusika huyu na wakati. Mhusika huyu – kama alivyo mhusika wa kwenye hadithi ya kifasihisimulizi – ni mhusika wa wakati wote. Kwa msanii wa namna hii ya mhusika, yaarii mhusika adili ambaye ameainishwa kama mhusika mkwezwa, dhana za wakati na ukweli uliokamilika zinaonekana kuwa ni vitu visivyobadilikabadilika. Kwa hiyo mhusika huyu adili anauwakilisha ukweli uliokamilika wa wakati wote.
Kwa upande wa Shaaban Robert ambaye anajitokeza zaidi katika uchoraji wa mhusika wa namna hii, anawapa wahusika wake lugha teule tena sanifu, ambapo waandishi wa baadaye ambao wameandika riwaya ya mkondo huu, hususan waandishi wa riwaya – pendwa,8 wamewapa wahusika wao lugha ya kila siku, ikiwa ni pamoja na ya mitaani. Hii inatokana na kuathiriwa kwa waandisni na mazingira ya wakati wao. Ukweli wa maisha wa Shaaban Robert ulikuwa na mizizi yake katika dini, na hii ndiyo iliyolazimisha utumiaji wa lugha teule. Hali kadhalika usanifu wa lugha inawezekana ulitokana na Shaaban Robert kuwa mmoja katika kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki ambayo, kwa kipindi fulani, alipata kuwa Mwenyekiti wake. Kama kiongozi wa chombo hicho cha lugha, tena lugha changa, wakati wa ukoloni Shaaban Robert alijiona kuwa ni mtetezi na mdhamini wa lugha hiyo katika kuwaonyesha wengine uwezo na mvuto wake kama chombo cha kitaaluma na cha kisanii.
Kwa ufupi, waandishi wa riwaya ya mkondo wa kimaadili pamoja na kuwa wameyagusia au kuyazungumzia masuala mbalimbali ambayo yameikabili jamii yao na hata kuifunza juu ya maadili yanayotakiwa (yaani ukweli wa maisha unaofaa), lakini wanaonyesha bado upungufu wa namna ya kuyachunguzamasuala ya kijamii na kiasili. Mtazamo wao wa matukio unajikita mno katika mkabala wa kijadi wa ujumi na wa kuangalia ukweli wa maisha.
Mwanzoni mwa miaka ya sabini kuliendelezwa namna nyingine ya kuutazama ukweli wa maisha, hatua fulani ilipigwa, hasa kwa upande wa fani. Hapa tutamchukua E. Kezilahabi na riwaya yake ya Rosa Mistika. Mhakiki mmoja, E. Bertoncini, aliandika kuwa E. Kezilahabi huandika kwa kuguswa juu ya matatizo nyeti ya kisiasa na kijamii yanayotukia kila siku katika Tanzania na katika Afrika ya leo.9 Na kuhusu riwaya ya Rosa Mistika mhakiki huyo anaeleza kuwa ni riwaya iliyopokelewa kwa mchanganyiko wa furaha, mshangao na chuki ambayo ilielekea kwenye fedheha kwa sababu mtunzi aliichagua kama mada yake moja ya maovu ya msingi yanayoishambulia jamii ya wakati huu ya Afrika Mashariki, akaishughulikia waziwazi bila kujizuia.10
Katika nadharia hapo nyuma tumeona kuwa jambo au tukio linalosawiriwa halipati maana na umuhimu wake kutoka kwa msanii bali hutokana na matamanio, malengo na vipimo maalumu (hususa vya kiujumi) vya jamii. Lakini ‘jamii’ hapa ina maana gani? Lini jamii hukutana na kuweza kuyafanyia uamuzi maandishi fulani, licha ya kuwa si jamii nzima yenye uwezo wa kuyasoma maandishi hayo na kuyaelewa? Hata sehemu ya jamii yenye uwezo wa kuyasoma maandishi hayo, si yote inayopendelea kuyasoma. Hatimaye itabainika kuwa ‘jamii’ izungumziwayo hapa ni kijiidadi kidogo tu cha watu kinachopitisha maamuzi juu ya maandishi fulani kwa niabaya jamii. Aghalabu matamanio, malengo na vipimo maalumu vya jamii huamuliwa na kijiidadi kidogo hiki kwa niaba ya jamii. Hivyo basi katika Rosa Mistika vipimo vya kiujumi vilivyotumika kuusawiri ukweli wa maisha havikuafikiana na vile vya ‘kijamii’.
Kezilahabi ndiye aliyeleta mapinduzi ya kwanza ya mhusika katika riwaya ya Kiswahili kwa kumuumba mhusika mwenye saikolojia na hisia. Mhusika huyu, ijapokuwa hakuchorwa vizuri kama yule wa M.S. Abdulla, lakini alionyesha dhahiri mambo mawili juu ya ukweli wa maisha. Kwanza, alibainisha utatu (multiplicity) wa maisha katika mtu ambao ulimwondosha mhusika mkwezwa. Pili, ukweli na wakati havikutulia pamoja. Rosa Mistika aliasi kutii vigezo vya jadi vya ukweli mkamilifu. Na mwishoni mwa riwaya kigezo cha jadi ambacho ni muhimu kupita vyote katika kupima ukweli wa maisha (yaani Mungu) kinapaswa kirudi katika hali halisi ili kiutafute ukweli halisi. Riwaya hii tunaiweka katika hatua za mwanzo za tapo la uhalisia wa kihakiki. Pamoja na kuleta mchango uliotajwa hapo juu na kuibua masuala kadhaa ya kijamii kama vile ya urithi, mimba mashuleni, n.k., bado kiwango cha riwaya hii cha kujadili bado ni cha chini, na matatizo ya jamii hayatafutiwi suluhu.
Katika Rosa Mislika linajitokeza suala moja ambalo linachukuliwa kama ni upungufu mmojawapo wa kisanii kwa Kezilahabi. Hili ni kuhusu jinsi wahusika wake wanavyoamua kuyakwepa matatizo kwa kujiua. Upungufu huu unajitokeza pia katika baadhi ya kazi zake nyingine, k.m., Kichwamaji, Gamba la Nyoka, “Cha Mnyonge Utakitapika Hadharani” na “Mayai Waziri wa Maradhi”. Kujiua hakumalizi matatizo ya jamii, bali pengine humaliza kwa kiasi fulani tu matatizo ya aliyejiua. Baadaye, katika kazi zake nyingine za sanaa, hususan Dunia Uwanja wa Fujo (1974) na Nagona (1987) Kezilahabi analizamia kwa tafakuri suala la ukweli wa maisha. Katika Dunia Uwanja wa Fujo kwa njia ya mhusika Dennis, mwandishi anayaona maisha hivi:
Quote:
Zamani niliamini kwamba kila mwanadamu ameumbwa kuja hapa duniani ili apate kufurahia ulimwengu kiasi awezavyo kabla hajafa. Laki ni sasa ninaamini kwamba ‘Dunia Uwanja wa Fujo’. Kila mwanadamu ameumbwa kuja kufanya fujo yake halafu anajiondokea na kupotea. Kuna fujo za aina nyingi. Watu wengine wamefanya fujo kuliko watu wengine. Hao ndio wamejulikana kwa sababu walitumia nguvu. Watu kama kina Napoleon, Juliasi Kaizari, Alekizander, Hitler; wengine wamefanya fujo kwa jina la amani: nao pia wamejulikana, watu kama kina Bwana Yesu, Lincoln, Livingstone, Gaodhi; wengine wamefanya fujo kwa maandishi; fujo waliyoanzisha watu hawa haitakwisha mpaka ulimwengu utakapofutika; watu kama akina Karl Marx, Shakespeare, Plato, Mao; na halafu kuna watu wengine wanaofanya fujo kidogo na kutapakaa kama viwimbi vya maji baada ya kutupa jiwe dogo majini; ni wale tu walio karibu wasikiao mshindo wao, lakini wanatisha zaidi; watu kama kina Mkwawa, Mutesa, Marais mbalimbali ambao hawajatenda makuu, Wakuu wa Mikoa na Wilaya; halafu mwisho kuna watu kama sisi na wengine, hasa wakulima; sisi tunafanya fujo ambayo haipati kujulikana. Tunafanana na mtu mwehu anayelala chini na kupigapiga miguu juu mpaka atakapojifia mikono yake mapajani… Kwa mfano mwalimu atafanya fujo yake darasani halafu atajifia na kikohozi cha chaki; polisi atapiga kelele ‘hoi! hoi’ halafu atajifia na mishipa yake miguuni; mwanamke anayefanya kazi bar atafanya fujo humo kwa kueneza magonjwa na kuvunja nyumba za watu, halafu atajifia.” uk. 92).
Dennis anapoulizwa kwamba mambo haya yote ameyapata wapi anakionyesha kichwa chake kwanza! Lakini waumini wa uyakinifu wa kihistoria wanaoona kuwa maisha ndiyo huzindua ufahamu (being determines consciousness) – kama ilivyodokezwa katika sehemu ya nadharia wangeliona jibu la Dennis kuwa ni kinyume cha mambo. Ndiyo maana mhakiki mwingine wa Kezilahabi, M. Mulokozi (1976:11) alipata kusema juu ya falsafa ya kazi za sanaa za Kezilahabi katika maisha kwamba: “Kwa kuwa mahitimisho yake yanabuniwa kichwani zaidi kuliko kutoka katika mambo ya ukweli wa kijamii, mahitimisho hayo, kwa vyovyote vile, hayaleti matumaini bali yanamwelekeza mtu kwenye kukata tamaa na hali ya upweke”.
Katika kiwango hiki riwaya za Kezilahabi hazikuwa na kazi za tapo la uhakiki wa kihalisia tu, bali zilijipatia sifa nyingine iliyobainisha upekee wa msanii huyu akilinganishwa na waandishi wengine wengi wanaoangukia katika tapo hili ambao wengi wao waliinukia katika miaka ya sabini. Sifa hiyo ni ile inayoziweka kazi za Kezilahabi katika mkondo wa kidhanaishi (existentialism) kutokana na mkabala wake wa ukweli wa maisha ambao msingi wake ni “Cogito ergo sum” (m.y. ‘Nafikiri, kwa hiyo nipo!’)12 Katika sehemu ya nadharia tumeona kuwa matendo (au uzoefu) ni msingi wa ufahamu, tena ni lengo la ufahamu, na hali kadhalika ndicho kigezo cha ukweli. Kwa kukitumia kipengele hiki cha nadharia tutaona kuwa msingi wa kidhanaishi wa kuutazama ukweli wa maisha unawekwa juu chini, chini juu, unakuwa “Nipo’ Kwa hiyo nafikiri.”
Jinsi Kezilahabi alivypendelea na uandishi ndivyo ambavyo ameelekea kujikita zaidi katika mkondo huo wa kidhanaishi akiudadisi ukweli wa maisha kwa namna ya kufikirisha zaidi kuliko hapo awali. Hii inajidhihirisha katika Nagona (1987). Akitumia mtindo wa kihemetiki13 wa kuuangalia ukweli wa maisha, anaona maisha yako katika namna ya duara, na ukweli upo katikati. Katika duara hii watu wanatumia njia (‘fujo’) mbalimbali ili kuufikia ukweli pale katikati. Maisha yanaendelea katika mzunguko huu daima pasipo kuifikia kweli ya katikati, kwani kuifikia kweli pale katikati na kuishika mkononi ndio mwisho wa kufikiri. Mduara wa kihakiki wa kihemetiki wa M. Heidegger14 ndio unaochangia vikubwa katika mtazamo huu wa maisha wa Kezilahabi katika Nagona.
Kwa kifupi, Kezilahabi ni mwandishi aliyejitokeza kuliko waandishi wote katika mkondo huu wa kidhanaishi katika riwaya ya Kiswahili, na kwa kutumia mkondo huo ameyajadili masuala ya kisiasa na ya kijamii yanayoisibu jamii ya wakati huu ya Kitanzania ijapokuwa, kama ilivyodokezwa, suluhu ya matatizo hayo si ya msingi. Kifani na kiujumi katika riwaya zake zilizotangulia alionyesha matukio bila kujali mipaka ya vionjo vya ‘jamii’ akajikuta akigongana na ‘jamii’. Lakini katika Nagona huenda atakwepa mgongano mwingine kutokana na uwezekano wa riwaya hiyo kutokueleweka na ‘jamii’, hasa kwa namna alivyoijenga riwaya yake akitumia visasili vya asili mbalimbali duniani.
Waandishi kadhaa walioandika riwaya zao katika miaka ya sabini wanaangukia katika tapo la uhakiki wa kihalisia, na miaka ya sabim inaweza kuitwa kama ni kipindi cha riwayadhati (serious novel) ya Kiswahili. Baadhi ya waandishi hao ni M.S. Mohammed, Sh. A. Shafi, N. Balisidya, S. Komba, H. Mwakyembe, J. Ngomoi, W. Seme, M. Mvungi, C. Chachage, C. Mung’ong’o, A. Banzi, F. Senkoro, C. Liwenga, n.k. Idadi kubwa ya maandishi haya inajihusisha na ujenzi wa jamii mpya baada ya Azimio la Arusha na siasa ya ujamaa na kujitegemea, pamoja na mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964; na pia kulitazama suala la mkinzano wa kipembuzi kati ya kijiji na mji, kati ya jadi na mamboleo.
Hata hivyo, katika miaka hiyohiyo ya sabini kuna riwaya iliyojitokeza ikiwa imeguswa kiasi kikubwa na itikadi ya kiMarx. Riwaya hii inaona kuwa ukweli wa maisha uko katika usawa na haki, na mambo haya yatapatikana pale ambapo watu wote watakuwa huru na sawa, na pasipokuwepo matabaka wala ukoloni. Kwa hiyo riwaya hiyo imejihusisha na masuala ya ukombozi au kuwapa wananchi mwamko wa kisiasa. Mifano ya riwaya hizo ni Ubeberu Utashindwa (J.K. Kiimbila, 1971), Mzalendo (F. Senkoro, 1975), Kuli (Sh. A. Shafi, 1979), Kabwela (A.J. Saffari, 1978) na Dunia Mti Mkavu (S. A. Mohamed, 1980). Riwaya hii imeainishwa kama ni ya ‘kimapinduzi’. (Neno ‘mapinduzi’ katika muktadha wa kifasihi nimelitumia hapa kwa maana ya mabadiliko ya haraka ya kisiasa, kiuchumi na kifikra katika jamii kwa lengo la kuyaleta mahusiano mapya ya kijamii yanayoleta uhuru, usawa, amani na maendeleo).
Riwaya ya mwisho, yaani Dunia Mti Mkavu, ikijitokeza kwa ubora katika kundi hili, na hasa inavyoyajadili maudhui katika mazingira ya wakati wake kwa jicho la ufahamu wa sheria zinazoyatawala maendeleo na mahusiano ya jamii. Wakati ambapo riwaya kadhaa hazijaonyesha wazi kuwepo kwa matabaka ya kijamii na ukinzani uliopo baina yao, Dunia Mti Mkavu imelishughulikia suala hili vizuri. Sifa nyingine ya kisanii ni jinsi msanii anavyoutazama ukweli wa maisha. Katika jadi ya riwaya nyingi wahusika muhimu wanatokana na umuhimu wa nafasi zao katika jamii tangu mwanzo, au baadaye katika maisha yao. Katika riwaya ya kimapinduzi maendeleo yanamlenga mtu (mfanyakazi) wa kawaida. Mtu huyo anatakiwa azinduliwe na kuendelezwa kwa kufahamishwa nafasi muhimu aliyo nayo katika kuleta maendeleo na mapinduzi ya kijamii. Katika Dunia Mti Mkavu watu wa kawaida wamepewa nafasi ya kuwa na hali ya udadisi katika harakati za kujielewa wenyewe, kuielewa jamii yao, mazingira yao, na mahusiano ya hayo yote. Mtazamo wa ukweli wa maisha wa riwaya hii ni ule wa upembuzi wa kiyakinifu.
Upungufu wa riwaya hii uko hasa katika upande wa fani. Wasanii wake aghalabu wameondokea kuunda risala za kisiasa. S.A. Mohammed katika Dunia Mti Mkavu amejaribu kulikwepa tatizo hili kwa kutumia sana mifano.
Hatimaye kuna hadithi nyingi zilizoandikwa katika miaka ya themanini ambazo tumeziweka chini ya fungu la riwayapendwa kutokana na ukweli kuwa zinasomwa na idadi kubwa ya watu, hasa vijana.15 Maandishi ya namna hii kwa bahati mbaya yamezungumziwa kidogo sana na wahakiki wa fasihi ya Kiswahili kwa sababu yanadhaniwa kuwa hayana umuhimu kama vile riwayadhati. Lakini kwa sababu maandishi haya yanasomwa na wengi, hasa vijana – ambao ni taifa la kesho – hayakosi yawe na jambo fulani linalowavutia na pengine hata kuwaathiri. Je, riwaya hii au maandishi haya yana nafasi gani katika kuakisi ukweli wa maisha? Riwaya hii imejitokeza katika mikondo ya mapenzi na mazingira, uhalifu na upelelezi. Riwaya hii imelaumiwa na wahakiki kuwa ni ya utoro wa ukweli wa maisha kwa sababu inauakisi ‘ukweli’ ambao hauchukuani na mazingira yetu; pia imedhaniwa kuwa inafundisha majangili na wahalifu mbinu mpya katika shughuli zao za kufanya uhalifu.16
Ijapokuwa katika sehemu ya nadharia tumeona kuwa katika ukweli wa kisanaa, ‘ukweli’ wa kauli huweza kuvuka mipaka ya hali halisi, lakini ukweli huo unatakiwa usipingane na matamanio na malengo ya jamii. Katika kazi nyingi za riwayapendwa kiasi cha mwigo kutokana na fasihipendwa ya kigeni pamoja na filamu kimezidi hadi kuweza kumnyima msanii nafasi ya kubuni kazi zenye utajiri wa mawazo yake mwenyewe na ujumi wa jamii yake. Hata hivyo, kuna waandishi wa kutoka katika kundi hili, kama vile Mbunda Msokile, ambao kazi zao hazina budi kutazamwa kwa jicho tofauti kidogo kutokana na jinsi wanavyolishughulikia suala kuu la wakati wetu ambalo ni m’gongano wa kitabaka, wakionyesha mtu wa kawaida anavyoonewa.17 Kwa kuwa riwayapendwa itaendelea kuwa baina yetu kwa muda mrefu ujao kutokana na kupendwa na wengi, pengine wasanii wangenasihiwa wajaribu kuiandika riwayapendwa inayozibomoa kuta zinazouhifadhi utoro wa ukweli wa maisha. Pia wahakiki wangejihusisha nayo zaidi ili kuifahamu vizuri zaidi, na kuona jinsi ya kuisaidia iyafae mazingira yake, kuliko kuishambulia tu au kuisoza pembeni.
Baada ya kuipitia mifano hii michache ya waandishi wa Kiswahili na jinsi wanavyolitazama suala la ukweli wa maisha katika wakati wao, bado swali la msingi linabaki: Je, ni mtazamo upi wa ukweli wa maisha ungefaa kutumiwa na wasanii wetu? Swali hili linastahili kujibiwa na wakati. kwa maana, kadiri wakati unavyozidi kusonga mbele ndivyo uga wa uelekeobinafsi (subjectivism) unavyozidi kupungua, na ule wa uhalisi (objectivism) kuzidi kupanuka kutokana na mabadiliko ya mahusiano ya kijamii na kiasili. Na ikiwa kauli hii ni sahihi maana yake ni kwamba mitazamo ya ukweli wa maisha itazidi kujichuja kufuatana na wakati wa historia hadi hapo mtazamo bora zaidi utakapofikiwa (huenda kwa waumini wa dini mbalimbali ni siku ya kiama, na kwa waMarx ni siku ukomunisti utakapopatikana). Kwa wakati huu mahusiano ya kijamii yanadhihirisha ongezeko la mapambano ya kitabaka kati ya walionacho na wasionacho, kati ya watawala na watawaliwa wanaokandamizwa na kuonewa; kuna ongezeko la harakati za kupigania ustawi wa jamii kwa njia ya mapinduzi ya kisayansi na kiteknolojia, harakati za kupiga vita njaa, umaskini na ujinga, na pia kusisitiza suala la amani na maendeleo ya binadamu. Riwaya inayostahili ya wakati huu ni ile inayousawiri na kuupigania ukweli huu wa maisha.
Hata hivyo, pamoja na kuwa waandishi wa Kiswahili hawajaziandikia mada hizi kwa upana wa kutosha, lakini ni suala la wakati tu, kwani wanazidi kuandika. Lakini vile vile si lengo la waandishi kujiandikia wenyewe au kuwaandikia wahakiki ili kazi zao zihakikiwe, bali lengo lao kuu ni kuwaandikia wasomaji ili kuwasiliana nao juu ya maisha kwa njia maalumu ya kiujumi: kwa kufurahisha, kusikitisha au yote mawili kwa pamoja. Bila msomaji, waandishi na hata wahakiki wanafanya kazi bure; na majadiliano haya juu ya ukweli wa maisha katika riwaya au fasihi yanakuwa ni kupoteza muda tu. Kwa bahati mbaya hutokea kwamba wale ambao wangetakiwa kusoma kazi hizi zaidi ili wajifunze zaidi juu yao wenyewe na shughuli zao na uhusiano wao na jamii, n.k., hawajajenga bado hamu na tabia ya kuzisoma kazi za fasihi. Hivyo uandishi unakuwa kama ni shughuli ya wasanii kwa ajili ya mashule na vyuo tu. Na kwa jinsi hiyo nafasi ya msanii na umuhimu wake bado havijapata uzito unaostahili katika jamii yetu.
Kumbe riwaya nzuri au kazi nzuri ya fasihi ni mfano wa ‘nadharia’ zinazosubiri kutekelezwa; nadharia ambazo zimetayarishwa na waandishi baada ya kuyachunguza mazingira yao kwa makini, wakayasawiri matukio kwa kuyakosoa au kupendekeza njia ambazo zingeyafanya maisha ya jamii yawe bora zaidi, na pia kuifanya dunia isiwe ni ‘uwanja wa fujo’, bali uwanja wa mapatano, furaha, amani na maendeleo. Huenda upana huu wa mada utamfanya mtu ajiulize ni kwa vipi riwaya ya Kitanzania inayotumia Kiswahili itajitanua namna hiyo katika majukumu yake. Jibu ni kwamba siku hadi siku Kiswahili kinazidi kupata nyanja mpya na hadhi mpya za utumishi wake. Watu wengi walioko nje ya dunia ya Kiswahili wanazidi kujifunza Kiswahili na kuweza kusoma kazi za wasanii wetu. Kwa njia hii kazi zinazowavutia zinaweza kufasiriwa katika lugha zao kama baadhi ya kazi zilivyoanza au kwisha kufasiriwa tayari.18
Marejeo na Maelezo
1. Dondoo kutoka katika kitabu kilichohaririwa na J. Krueger (1983) Aesthetik der Antike. Aufbau-Verlag, Berlin und Weimar, uk. 28.
2. E. Hussein (1969) Kinjeketile. OUP, Nairobi, uk. 49.
3. Shaaban Robert (1968) Kielelezo cha Fasili. Nelson, Nairobi uk. 93 – 4.
4. Buhr, M. na Kosing, A (1982) Kleines Woerterbuch der Marxistisch – Leninistischen Philosophie. Dietz Verlag, Berlin, uk. 203 – 5.
5. KulturPolitisches Woerterbuch (1978) Dietz-Verlag, Berlin, uk. 751 – 6. Rejea “Kuenstlerisher Wahrheit”.
6. E. Bertoncini (1977) “Two Contemporary Swahili Writers…” katika The East African Experience, Frankfurt a.m. uk. 88.
7. J. Madumulla (1982) “Maendeleo ya Wahusika katika Riwaya ya Kiswahili,” Makala hayajachapishwa. Chuo Kikuu Dar es Salaam.
8. Riwayapendwa imejadiliwa kwa kirefu katika makala yaitwayo “Riwaya ya Kiswahili (Tanzania) katika miaka ya Themanini” yaliyoandikwa na J. Madumulla (1987) na huenda yakatoka katika Lugha Yetu.
9. E. Bertoncini, m.y.k., uk. 87.
10. k.h.j., uk. 87.
11. M. Mulokozi (1976) “Development of Kiswahili Literature,” katika: Daily News Supplement, DSM, 21.7.1976, uk. 6, 11 & 18.
12. Wanadhanaisni wana namna kadhaa za kuieleza falsafa yao, hii ikiwa ni namna yao mojawapo, wakiwa na lengo la kusisitiza kwamba wazo ndilo huja kwanza kuliko uzoefu (au tendo). Soma Kleines Woerterbuch der Philosophie chini ya “Materialismus.”
13. Neno hili “hemetiki” hnatokana na neno la Kiingereza hermeneutics linalosimamia mbinu mojawapo ya kisanaa ya kuelewa maana na kutambua mpango wa maandishi ambapo vipimo muhimu vya kiitikadi vya wakati ‘fulani’ vimetumika. Mbinu hii ilianza kupata nguvu katika dini, hasa namna ya kufafanua Biblia, tangu karne ya 16 hivi.
14. Kwa habari zaidi soma Senkoro, F.E.M.K. (1987) “Nadhana ya Fasihi na Fasihi ya Kiswahili ya Majaribio” (Makala hayajachapishwa), au D.C.
Hov (1978) The Critical Circle, UCP. London. 15. J. Madumulla (1987) “Riwaya ya Kiswahili (Tanzania) katika Miaka ya themanini,” m.y.k.
16. P. Mhando na N. Balisidya (1976) Fasihi na Sanaa za Maonyesho, TPH, uk. 70. Pia Madumulla (1987) k.h.j. uk. 7.
17. Soma M. Msokile (1981) Nitakuja kwa Siri, DUP, Dar es Salaam.
18. Mifano ya vitabu vinavyofasiriwa au viliyyofasiriwa ni Myombekere na Bugonoka, Kusadikika, Gamba la Nyoka, Dunia Uwanja wa Fujo, na baadhi ya vitabu vya S.A. Mohamed.

Print this item

  UCHAWI KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI
Posted by: MwlMaeda - 08-27-2021, 05:50 PM - Forum: Riwaya - No Replies

Uchawi katika Riwaya za Kiswahili

A.J. Saffari
Utangulizi
Makala haya yanazungumzia nafasi ya uchawi katika riwaya za Kiswahili. Lakini kwa vile riwaya zote, japo ziwe za kubuni, zinakita mizizi na kupata uhai wake kutoka maisha halisi, suala linakuwa: Je, uchawi wenyewe ni kitu dhahiri au dhana tupu?
Waama nadharia na suala zima la uchawi limezungumziwa na kujadiliwa mwahala mwingi na watu wa kawaida tu mitaam, viongozi wa nchi pamoja na wanazuoni wa vipeo vya juu masomoni. Vitabu vya dini mbili kubwa duniani Kuruani2, yaani Msahafu, na Biblia3, vinazungumzia uchawi katika sehemu mbalimbali kadiri itakavyoonyeshwa baadaye. Nao Geofrey Parrinder4, Middleton5, Murray6, Michael7, Harwood8, Alastair Scobie9, Amold,10, Mary Douglas11 , kwa kutaja baadhi tu, wamejitoma katika mjadala kuhusu uchawi.
Makala baya yataanza na tafsiri ya uchawi, baadaye kujadili ushahidi mintaarafu ya uchawi, sababu zake, uchawi na utamaduni, pamoja na maendeleo.
Tafsiri ya Uchawi
Maana au tafsiri ya uchawi imezua utatanishi kama suala lenyewe la uchawi. Hivyo George Parrinder hajakosea anapodai kwamba ni masomo machache tu yamewakanganya watu kuliko uchawi.12 Kamusi, Encyclopaedia, na vitabu vya waandishi mbalimbali vimezidi kutatanisha maana ya uchawi. Vingi vinachanganya uchawi, wanga na uganga.
Kamusi ya Oxford inaanza kwa kudai kuwa mchawi (witch) ni mwanamke anayetumia madawa kwa madhumuni mabaya hasa miongoni mwa washenzi.13 Kwa upande mwingine Kamusi ya Kiswahili Sanifu inaeleza kuwa uchawi ni ufundi wa kutumia dawa, aghalabu mitishamba na vitabu maalum vya uganga, ili kuleta madhara kwa viumbe, yaani sihiri. Baadaye kamusi hiyo inamwelezea mwanga kama mtu afanyaye mazingaombwe ya uchawi usiku, mtu achezaye ngoma ya mahepe.14
Ni dhahiri matatizo kadha yanajitokeza kutokana na maana au tafsiri zilizoelezwa hapo juu. Kwanza, ni kutoainishwa baina ya uchawi, wanga na madawa. Pili, madai kuwa mchawi ni mwanamke. Madai hayo yameungwa mkono na waandishi wengine kadhaa, bila ya ushahidi wowote. Na tatu, dai kuwa uchawi ni suala linalowahusu washenzi tu”. Maana yenyewe ya ushenzi haikuelezwa hapa, iwapo ni mtu ambaye hakustaarabika, yaani yuko nyuma kimaendeleo, au habithi wa matendo.
Katika mkanganyiko huo wa maana nastahabu ile inayodai kuwa uchawi ni ufundi, yaani utaalamu wa kutumia sio dawa tu, bali mbinu nyingine mbalimbali pamoja na vitabu maalum vya uganga ili kuleta madhara kwa viumbe. Bora kufafanua hapa kuwa hii ndiyo maana inayolingana na matumizi ya neno uchawi miongoni mwa watu wa Afrika. Lakini basi, kwamba taaluma au ufundi huu (uitwao uchawi) aghalabu huaminika na kutumika kuhasiri viumbe, haina maana kuwa hauwezi kutumiwa kwa manufaa.
Ushabidi Mintaarafu ya Uchawi
Leo hii watu wengi, hata wasomi, hawaelewi namna bomu la Neutron la Wamarekani linavyoweza kuua viumbe vyenye uhai na kuviacha visivyo na uhai bila ya athari yoyote. Hata hivyo kweli ni kuwa jambo kama hilo hutokea ingawa wanaojua kwa nini inakuwa hivyo ni wale wachache wenye taaluma hiyo. Wataalamu hao huishi chini ya ulinzi mkali kuliko marais wao na kuficha siri za utaalamu wao kama wafichavyo sehemu zao za siri. Basi ndivyo hivyo kwa elimu nyingi pamoja na uchawi wenyewe.
Baadhi ya waandishi, akiwemo George Parrinder, wanashikilia kuwa msingi wa uchawi ni imani tu. Ya kwamba imani hiyo ilianzia na kuzagaa Ulaya katika karae za kati. Hadi leo hii imani ya uchawi imelikumba Bara la Afrika na kusambaza hofu na vifo. Mwandishi huyo anaendelea kusema kuwa imani hiyo ya uchawi ilisababishwa na dhiki ya maisha. Kutokana na maradhi ya kuambukiza, uchafu na vifo vingi binadamu walitafuta sababu za maafa hayo. Walipozikosa au kutozijua, wakaanza kusingizia uchawi.15 Kama ambavyo itaelezwa baadaye, naafiki kuwa taaluma ya uchawi kwa maana ya kudhuru viumbe, imeshamiri zaidi katika jamii ambazo ziko nyuma kimaendeleo. Lakini wachawi sio masikini tu. Hata Mary Douglas anathibitisha kwamba matajiri wakubwa huko Uingereza na Ujerumani walitumia uchawi kuwaroga wenzao.16 La maana zaidi ni kuwa siafikiani na George Parrinder kuwa uchawi ni imani tu. Uchawi ni jambo la hakika wala sio dhanatupu.
Hapa sitathubutu kujinadi kujua kunga za uchawi kama vile ambavyo sijui namna bomu la atomiki linavyoua, japo linaua. Ila nitajitahidi kuthibitisha kuwa uchawi sio dhana wala imani tupu ya washenzi kama ambavyo George Parrinder na wenzake wanavyotaka tukubali.17
Je, ushahidi gani unadhihirisha kuwepo kwa taaluma ya uchawi?
Kwanza vitabu vya dini mbili kubwa duniani, yaani Korani na Biblia, vinazungumzia kwa ufasaha jambo hili. Aya ya 102, Surat l’Baqara18, inaeleza kuwepo kwa taaluma ya uchawi. Na katika tanbihi ya 105 ya Sura hiyohiyo Mungu anaelezea namna taaluma hiyo inavyoweza kutumiwa vizuri mikononi mwa watu ashrafu kama vile Hart na Marut, stadi wa taaluma hiyo walioishi Babylon awali hizo.19 Ikumbukwe kwamba katika siku hizo ayani Babylon ilivuma kuwa kitovu cha sayansi, hususan elimu ya nyota. Hata hivyo, hapohapo Mungu anaonya nanma ambavyo taaluma hiyo ya uchawi inavyoweza kutumiwa vibaya mikononi mwa mahabithi wenye ghera, choyo na tadi. Pamoja na yote hayo Mungu anasisitiza kuwa uwezo au taaluma hii ya uchawi ina ukomo; kwamba mchawi hawezi kutenda akafanikiwa kama Mungu hapendi. Yaani mchawi, japo awe fundi mangungu kiasi gani, hawezi akatumia uchawi kuroga au kuopoa akafanikiwa pasi Mungu kupenda. Kwa wale waumini wanaelewa fika kuwa kila kheri na shari humuelea Mungu.
Kuna hadithi moja iliyopokelewa enzi na enzi inayosimulia kwamba aliishi stadi mmoja wa taaluma ya uchawi kwa jina Maalim Kisisina. Hadithi inaeleza kuwa Maalim Kisisina alikuwa anabuni mipango ya kuzuia kudura za Mungu. Basi Mungu akamtuma malaika wake Jibrili kumfuata Maalim Kisisina na kumtaka undani wake. Jibrili alimwasilia Maalim Kisisina kwa umbo la mwanadamu. Kufika akamuomba amueleze aliko Jibrili kwa wakati ule. Basi Maalim Kisisina akapekua buku kubwa na taaluma ya uchawi na kumjibu kuwa kama Jibrili siye yeye mwenyewe Maalim Kisisina, basi Jibrili ni yule mtu aliye mbele yake, yaani Jibrili mwenyewe. Hadithi inasimulia kuwa mara hiyohiyo Jibrili akatumia wahyi ya Mungu kumpokonya Maalim Kisisina buku hilo la uchawi. Kufumba na kufumbua Jibrili alimpora Maalim Kisisina, naye kwa kutumia taaluma yake ya uchawi, akaapa kumuandama Jibrili. Kwa pamoja wakapaa juu na juu mbinguni hadi Mungu akamtumia tena wahyi Jibril kuwa achane karatasi moja la buku lile la taaluma na uchawi amtupie Maalim Kisisina. Jibrili alitii amri hiyo. Kuona kataa linaanguka kutoka mikononi mwa Jibrili, Maalim Kisisina akalidaka kataa hilo akiamini kuwa ni buku lake lote kumbe sivyo. Inadaiwa na hadithi hiyo kuwa taaluma yote ya uchawi duniani imo kwenye kataa lile moja alilotupiwa na kuachiwa Maalim Kisisina.
Hadithi ya Maalim Kisisina inasadikiwa na baadhi kuwa ya kweli. Lakini kama itazua ubishi bado kuwa ushahidi mwingine mwingi unaothibitisha taaluma ya uchawi. Tumeona maelezo ya Korani, sasa tuangalie Biblia.
Agano la Kale linaelezea miujiza baina ya Musa na wachawi wa Farao, namna ambavyo wachawi wa Farao walivyoweza kugeuza fimbo kuwa nyoka.20 Lakini hata hapa tunaelezwa kuwa Musa, kutokana na kubuli ya Mungu, aliweza kuitupa chini fimbo yake ikageuka joka kubwa lililowameza nyoka wote wa wale wachawi wa Farao.
Mnamo mwaka 1958 aliishi mpigania uhuru mmoja huko Tanga akiitwa Osale Otango kwa jina la utani. Waingereza waliamua kufanya msako mkubwa dhidi yake; na hatimaye kumkamata na kumpeleka Gereza la Maweni. Gereza hilo lilikuwa maarufu na humo ndani Osale aliwekwa kwenye chumba cha pekee akiwa ametatikwa pingu na minyororo ya mikono na miguu. Asubuhi iliyofuatia Mkuu wa Gereza, Mwingereza, alifika ofisini kwake mapema akakuta karatasi imeachwa juu ya meza yake imeandikwa: “Kwa heri, tutaonana. Osale Otango.” Upesi alikimbilia kule rumande na kukuta chumba salama lakini Osale Otango hayumo. Hakuna mtu aliyeiba funguo za rumande na wala hapakuweko sehemu iliyovunjwa katika rumande hiyo.
Tukio jingine lilitokea Mwanza mnamo miaka ya sabini. Tukio hili lilielezewa sana na magazeti yote ya Uhuru na Daily News. Mvulana mmoja alifariki ghafla, akazikwa. Siku nyingi kupita akapatikana hai, ingawa hakuwa na fahamu nzuri wala kuweza kuzungumza. Mvulana huyo alipelekwa Hospitali ya Bugando kwa uchunguzi zaidi.
Aidha kuna ikirari na maungamoya wachawi wenyewe. Kwa kawaida, na hata kwa mujibu wa sheria, ikirari 21 na maungamo22 ni ushahidi muhimu sana dhidi ya mtuhumiwa; madhali tu uwe umetolewa kwa hiari, bila vitisho wala ahadi za uongo. Waandishi wa vitabu kadhaa wanaelezea ikirari na maungamo haya ya wachawi. Geofrey Pamnder, kwa mfano, anaelezea kuwa wachawi huungama kukutana usiku kujadili masuala yao na kula nyama za watu ambao wamewaua kwa njia za uchawi.23 Wachawi hao hufanya mashindano kuonyeshana ujuzi na maajabu yao. Anazidi kuelezea kuwa wachawi wa Basuto hukiri kukutana usiku wakiwa uchi, hutumia madawa kuwafanya watu walale kisha huiba ng’ombe zao.24 Yafaa ikumbukwe hapa kuwa matendo hayo ya wizi wa ng’ombe kwa njia za uchawi yanafanyika mno Mwanza na Shinyanga. Wakati fulani yalifikia kiwango kikubwa cha kutisha, hata watu binafsi wenye mifugo yao wakaanza kuwasaka na kuwaua watu waliowadhania ni wachawi waliofanya madawa ya kuwaibia ng’ombe wao. Kesi maarufu ya Elias Kigandye25 ni ithibati ya kutosha. Itakumbukwa kuwa mauaji yaliyotokana na upelelezi wake si hiyo yalisababisha Mheshuniwa Ali Hassan Mwinyi, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wakati huo, ajiuzulu.
Mary Douglas naye anatoa mifano kadhaa ya maungamo ya wachawi Uingereza na Ujerumani. Anaelezea namna Malkia mmoja alivyokufa kwa miujiza huko Uingereza,26 na jinsi ambavyo watu mbalunbali, waume kwa wake, walivyokiri na kuungama mauaji katika miji mbalimbali ya Ujerumani ya Magharibi. Mmoja kati ya wachawi hao, Paul Camperle, mwenye umri wa miaka thelathini na tano, aliungama kuwa alianza uchawi tangia utoto wake alipofunzwa na nyanya yake. Tangu hapo alijinadi kuwa aliwaroga na kuwaua watoto mia moJa, na kuwalemaza au kuwafanya viwete matajiri kadhaa wajiji la Munich.27 Mkewe, Anne Camperle, naye aliungama kuua watoto mia na watu wazima kumi na tisa. Aidha alijitapa kumshakizia mke wa mtu mmoja kujichoma ndani ya jiko hadi kuiva. Mumewe naye akamfuatia. Akajitapa zaidi kuua idai kubwa ya ng’ombe wa watu.28 Mwanae Simon Camperle naye aliungama kuuwa watoto kumi na sita, watu wazima sita, pamoja na kuwalemaza wengine au kuwafanya viwete.29
Mtu mwingine Olrich Schelltibann, umri miaka themanini, alijifaragua kuua watoto arobaini, watu wazima thelathini, na kuwalemaza au kuwafanya wengine viwete.30 George Smeltes naye aliungama kuua watoto thelathini na sita, watu wazima kumi na tano, na kuwalemaza au kuwafanya wengine viwete.31 Maungamo hayo yanasemekana yalifanywa kwa hiari mbele ya Gavana wa Jiji la Munich. Baadaye wachawi hao walichomwa moto hadi kufa.32
Wachilia mbali maungamo hayo ya vitabuni, ushahidi uko katika sehemu mbalimbali hapa Tanzania wa wachawi kuungama kuwaua watu kwa kutumia uchawi. Wachawi hao, mathalan, wamewahi kuungama mbele ya Tekelo, Dar es Salaam; Kabwere, Tanga; na Mandondo, Korogwe. Tekelo, Kabwere na Mandondo ni waganga maarufu ambao waliweza kuwafichua wachawi katika sehemu hizo. Licha ya kuungama tu, baadhi ya wachawi hao walijitokeza na mafuvu ya vichwa, mifupa ya wafu na hata makoba yao ya uchawi na vyungu vya kupikia nyama za wafu. Wengine walidiriki hata kuelezea namna walivyogawana na kufaidi nyama ya mtu fulani.
Sababu za Uchawi
Kila kitu kina nia na madhumuni yake. Uchawi nao, kwa maana hii yake mbaya ya madhara, una sababu zake kuu zifuatazo. Kwanza ni sababu ya kiuchumi. Katika jitihada ya kupata, mathalani mifugo, kama ambavyo imeelezwa awali wachawi hutumia uchawi kuswaga ng’ombe wa wenzao. Au, ili kupata mavuno mengi, wachawi huhitaji huduma ya watu wengi mithili ya watumwa. Hivyo hutumia mbinu za kuwafanya watu waonekane wafu, kumbe wazima, kisha huwatumikisha kulima mashamba na kuyahudumia. Aina hii ya uchawi ni maarufu kote Afrika, na hapa Tanzania hujulikana kwa majina mbalimbali. Mathalan huko sehemu za Kusini, kama vile za Lindi, huitwa ndondocha. Sehemu za Mwanza na Shinyanga huitwa mitumba. Tanga huitwa msukure. Na kwajumla neno kizuu lina maana ya mtu ambaye anafungwa na kutumikishwa baada ya watu kumzika wakidhani amefariki.33
Alistaire Scobie anaelezea mauaji ya kutisha huko Basuto, yaani Botswana, kwa minajili ya kupata mali.34 Mtu mzima hukamatwa usiku na kukatwa viungo mbalimbali huku yu hai. Viungo hivyo kama vile macho, maini, huchanganywa na vitu vingine na kutumiwa kama dawa ya mavuno makubwa. Ayi Kweyi Annah pia anaelezea mauaji ya aina hiyo katika Nigeria.35
Mauaji kama hayo pia yako sehemu nyingi hapa Tanzania kwa nia ileile ya kutafuta mali. Kwa mfano, mara nyingi watu hukutwa wameuawa na kukatwa sehemu za siri. Baadhi ya wakazi wa Nyanda za Juu huamini kuwa sehemu hizo zinavutia utajiri wa biashara.36
Sababu nyingine mbili hukaribiana mno na hii ya kwanza, nazo ni sifa na uwezo. Kwa mfano, baadhi ya viungo vya mwanadamu vikikatwa yungali hai, kama vile maini na moyo, hutumiwa kumpa mchawi au yeyote anayekusudia uwezo, sifa na ujasiri. Vijiji vingi Afrika vina baadhi ya watu, waganga ambao hutisha na kuogopesha kutokana na sifa, uwezo na utajiri wao utokanao na uchawi.
Sababu ya mwisho ni kustarehe. Wachawi wanatumia taaluma hiyo kufanya ufidhuli wa kuchezea watu usiku, kama vile kuwapanda, kuonyeshana miujiza, kucheza uchi, kula nyama za watu waliowaua, n.k. Zaidi ya yote wachawi hutumia taaluma hiyo kuwapora watu wake zao, ikibidi hata kwa kuwaua waume zao kwanza.
Uchawi na Utamaduni
Matendo yote ya mwanadamu hutokana na mfumo wa kuzalisha mali na mahusiano ya uzalishaji mali yenyewe katika jamii inayohusika. Taaluma mbalimbali hubuniwa kwanza kwa kukidhi haja ya jamii inayohusika. Uchawi nao ni hivyohivyo.
Awali niliafikiana na hoja ya Parrinder kuwa mara nyingi uchawi hustawi kwenye umaskini kwa sababu aghalabu umaskini hutokana na zana duni za kuzalisha mali. (Sitazungumzia mahusiano ya uzalishaji mali.) Badala ya kutumia matrekta au majembe ya ng’ombe watu wa sehemu nyingi za dunia, hasa Afrika, hutumia viserema. Ukulima wa kiserema ni wa tonge domoni tu, basi. Anayetaka kupata mazao mengi hana budi apate watu wengi wamlimie. Na watu hao wataka kulipwa. Kulipa nako kunapunguza faida. Jambo moja la kufanya ni kupata watumwa. Lakini utumwa mkongwe hauko siku hizi. Na utumwa mamboleo nao unahitaji kiasi fulani cha ijara, sio bure. Hivyo la kufanya ni kuweza kupata watumwa kwa namna nyingine. Hapa ndipo taaluma ya uchawi kama vile ndondocha, mizuka, msukure, na kadhalika hutumika. Vizuu ni watumwa bora zaidi maana hawawezi kugoma’wala kujadili vitu vizuri. Kama asemavyo Dk. Emmanuel Mbogo, wao hulishwa kinyeke na kuridhika.37
Riwaya ya Mirathi ya Hatari inaelezea mkasa uliokitikisa kijiji cha Kitelevadzi na kuashiria mfarakano mkubwa.38 Kisa ni kuwa Mzee Kasembe alikuwa anagombania shamba la watu wengine wawili, yaani Kipedzile na Malipula.39 Ili kujipatia shamba hilo kulihali, Malipula, kwa kutumia radi, aliteketeza familia yote ya Mzee Kasembe isipokuwa Gusto ambaye hakuwa nyumbani.
Kadiri nyenzo za uzalishaji mali zinavyoimarika ndivyo taaluma ya uchawi kwa minajili ya kudhuru kwanza ili kujinufaisha inavyopotea.
Uchawi na Maendeleo
Baada ya mjadala wote uliotangulia suala linabakia: nini nafasi ya uchawi katika maendeleo ya Watanzania na riwaya zao za Kiswahili.
Kwa bahati mbaya, kwa mujibu wa ushahidi uliopo – kama ilivyoonyeshwa katika makala haya – taaluma ya uchawi imetumika zaidi kuibananga badala ya kuiendeleza jamii. Kutokana na taaluma ya uchawi inabidi kwanza mchawi adhuru ili ajinufaishe binafsi. Zaidi ya yote elimu hiyo yote ni kunga inayohifadhiwa kwa misingi ya ubinafsi dhidi ya maendeleo ya jamii kwa jumla.
Kwa kuwa, basi, kazi za sanaa kama vile riwaya hupata taswira yake kutokana na jamii inayohusika, riwaya za Kiswahili mintaarafu ya taaluma hii ya uchawi nazo zimeelezea uovu wa uchawi na hata kulaani kwamba inapasa utokomelee mbali.40
Riwaya Fadhili Msiri wa Naugua inaelezea uadui unaozuka baina ya nchi ya Naugua na Ramali. Katika hadithi hii kijana Kadi alitoka kwao Ramali nchi ya Wachawi, kwenda Naugua. Huko alimpenda mwali mmoja Mwanagele na kutaka kumuoa. Lakini kutokana na mila ya Naugua ilibidi kwanza amgombanie na kijana mwingine Fadhili, ili kupata ushindi wa kumuoa. Katika mashindano hayo Kadi alipigwa na kuumia. Watu wa Ramali wakaja juu na kutaka kuiangamiza Naugua kwa sihiri. Kwa bahati nzuri waganga – Mzee Jala na Bi Kizee Mkunyambi kutoka nchi ya Tiba – walizuia azma ya Waramali kumuua Fadhili, Mwanagele na kuteketeza familia nyingi za Wanaugua.
Mirathi ya Hatari42 nayo inaonyesha namna taaluma ya uchawi ilivyotumiwa kuteketeza watu kwa minajili ya ubinafsi wa mtu au watu wachache.
Lakini, kama ilivyodaiwa awali matumizi mabaya ya taaluma hayafanyi taaluma hiyo nayo kuwa mbaya. Hivyo katika Mirathi ya Hatari Mzee Kazembe aliukumbatia mkono wa mwanawe Gusto na kumuusia:
“Mwanangu, nakuachia kazi kubwa. Ni urithi mkubwa ukiutumia vyema; bali pia ni mirathi ya hatari usipojihadhari nayo.”43 Na hata baadaye wakati Gusto alipokuwa anatawazwa kuwa mchawi usiku kule pangoni, Mzee Mavenge, mmojawapo wa wachawi, alimsisitizia Gusto: “Kama nilivyokueleza yote hii ni elimu ya pekee. Ukufahamu na kuitumia vizuri unaweza kuumiliki ulimwengu. Ni siku hizi tu Wazungu wamekuja na elimu yao ya uongo na kweli wakawapotosha vijana wetu”.44 Kama hoja ni matumizi mabaya Mzee Mavenge alisema: “Hebu sikiliza jinsi wanavyouana! Hebu angalia mavyombo yao ya kivita! Nayo vile utasema yanasaidia kuinua hali ya binadamu!”45
Mijadala hiyo michache katika Mirathiya Hatari inapanua mawazo kuwa hakika taaluma ya uchawi ina sura mbili: ya wema, na ya uovu. Wengi wetu tunaiona ile sura ya uovu tu. Na kwa hivyo waandishi nao wameangukia katika upofu huo. Hili ni kosa kubwa kwa vile linapingana na kweli. Je, sio kweli kwamba kweli itashinda namna tunavyoishi!46
Sifa moja adhimu kwa mwandishi, na hasa msanii wa riwaya na tungo nyingine, ni kuheshimu kweli. Wakati mwingine hana budi kuitafiti na kujua kweli imesimamia wapi maana daima kuna watu ambao kazi yao ni kuipotosha na kuificha kweli.
Taaluma ya uchawi imejificha, dhahiri, lakini imepotoshwa ama kutokana na ukufi wa elimu au kwa kusudi. Kazi ya waandishi ni kutandua utandabui huu hasidi.
Hitimisho
Hoja inatolewa hapa kuiangalia vizuri sura ya pili ya taaluma ya uchawi ili kuutumia kwa maendeleo na hata ulinzi. Kwa mfano, wachawi wanaweza kuruka na kusafiri mbali kwa muda mfupi tena bila ya kuonekana. Wanaweza wakapenya ndani ya nyumba bila ya kuibomoa na kuwataa watu usingiri mzito kwa muda mrefu.47 Wanaweza wakafanya mengi mengine ya manufaa.
Basi nini wajibu wa waandishi wa riwaya katika suala hili la kuitumia taaluma ya uchawi kwa maendeleo?
Kwanza kabisa narejea katika hoja yangu ya awali kuwa moja ya sababu kubwa ya taaluma ya uchawi kutumika vibaya au kwa ubinafsi ni kutokana na kuwa na zana duni za uzalishaji mali, yaani umaskini. Kadiri maendeleo yatakavyoongezeka ndivyo matumizi ya madhara ya uchawi yatakavyopungua. Hata hivyo uchawi unaweza ukaendelea kutumika kwa madhara kwa muda mrefu kutokana na udhaifu wa wanadamu kutapia mali, uwezo, hata anasa tu, pamoja na wivu. Mchawi anaweza kuwa tajiri lakini akaamua kumuua tajiri mwenzake ili aondoe upinzani naye katika biashara.
Iwapo ni hivyo, nini wajibu wa waandishi wa riwaya katika kipindi hiki cha mapito? Ni vigumu kutoa jibu la mkato kwa sababu ileile niliyoigusia awali: kuwa kazi yoyote ya sanaa hupata taswira yake kutokana na jamii inayohusika. Hivyo kadiri uchawi unavyotumika zaidi kwa uovu ndivyo itakuwa muhali kwa waandishi kuuenzi kwa njia ya maendeleo.
Hata hivyo badala ya kuulaani tu uchawi utokomezwe kulihali, waandishi wanaweza kufanya mambo mawili makubwa: kwanza, kuwahamasisha wenye taaluma ya uchawi waifundishe pasi na kificho. Pili, waitumie kwa nia ya maendeleo kama anayoonyesha Ibrahim Hussein katika Kinjeketile48 ambapo wazalendo wa Tanganyika waliazimia kuitumia taaluma ya uchaw kupigana na wakoloni wa Kijerumani.
Tanhihi
1. Hivi karibuni viongozi wa ngazi za juu kabisa hapa nchini wamedai kuwa uchawi ni imani isiyo na msingi.
2. Yusuf, A.A. (1983) The Holy Quran. Translation and Commentary. Al Rajhi Co., Maryland.
3. Agano la Kale, (1980) T.M.P., Tabora.
4. G. Parrinder, Witchcraft, European and African. Faber and Faber, London.
5. J. Middleton, (1963) Witchcraft and Sorcery in East Africa. Praegar, New York.
6. A. Murray, (1963) The Witchcraft ni West Europe, Clarendon Press, Oxford.
7. G. Michael, (1967) The African Witch. London.
8. A. Harwood, (1970) Witchcraft, Sorcery and Social Categories Among the Wasafwa, Orford.
9. A. Scobie, (1965) Murderfor Magic. Cassel, London.
10. E. Arnold, Witchcraft. London, 1969.
11. M. Douglas, (1970) Witchcraft: Confessions and Accusations, Tavistock Publications, London.
12. Parrinder, (m.y.k.) uk. 10
13. A.S. Homby, (1924) Oxford Advanced Learners Dictionary of Current English. Oxford University Press, Oxford, uk. 131.
14. TUKI (1981) Kamusiya Kiswahili Sanifu. Oxford, Dar es Salaam.
15. Parrinder, (m.y.k.) uk. 9. Makabila ya nchi mbalimbali za Afrika yanatajwa kuhusiana na imani hiyo ya uchawi, nayo ni pamoja na Basuto wa Basutoland, siku hizi Botswana, Lorendu wa Afrika Kusini, Yombo na Ibo wa Nigeria, na Azande wa Sudan.
16. k.h.j., 114.
17. Douglas, (m.y.k.) uk. 35. Mfano unaotolewa hapa ni wa tajiri mmoja aliyeitwa Nutters aliyeishi Lancashire, Uingereza, mnamo 1622.
18. Parrinder, (m.y.k.) uk. 9.
19. A.A. Yusuf, (m.y.k.).
20. k.h.j. uk. 45.
21. Agano la Kale, (m.y.k.) uk. 803.
22. Tanzania (1962) Fungu la 19, Sheria ya Ushahidi, Na. 6.
23. Fungu la 27 k.h.j.
24. Pamnder, (m.y.k.), uk. 143.
25. k.h.j., uk. 145.
26. Tanzania (1981) Elias Kigadye na Wenzake, Shauri la Jinai la Rufani Na. 41,1981, Mahakama ya Rufani ya Tanzania, Dar es Salaam.
27. Douglas, (m.y.k.) uk. 305.
28. k.h.j. uk. 318.
29. k.h.i. uk. 318.
30. k.h.j. uk. 319.
31. k.h.i. uk. 320.
32. k.hJ. uk. 320.
33. TUKI (m.y.k.), uk. 131. Kizuu ni mtu aliyefunikwa kwa mazingaombwe ili kutumika nyumbani kwa uchawi; kijumbe cha uchawi.
34. A. Scobie, (1965) Murder for Magic. Cassel, London, uk. 96.
35. A.K. Armah, (1984) The Healers. Heinemann, Logos.
36. Wakati mwingine watu hutumwa kutafuta sehemu hizo za siri au viungo vya mwanadamu na kuviuza kwa anayevihitaji.
37. E. Mbogo, (1986) “Ngoma ya Mwanamalundi” (Muswada), Dar es Salaam.
38. C.G.M. Mung’ong’o (1977) Mirathi ya Hatari. TPH., Dar es Salaam, uk. 2.
39. k.h.j., uk. 2.
40. k.h.j., uk. 26.
41. A. Kondo, (1975) Fadhili Msiri wa Naugua. TPH, Dar es Salaam.
42. Mung’ong’o, (m.y.k.).
43. k.h.j., uk. 16.
44. k.h.j., uk. 25.
45. k.h.j., uk. 26.
46. S. Robert, (19/65) Masomo Yenye Adili. Nelson, Nairobi.
47. Watu kadha wa kadha, pamoja na viongozi wengine wa nchi hii, wamewahi kujikuta wametolewa nje wakati wa usiku bila ya kujijua, wengine wakiwa uchi wa nyama.
48. E. Hussein, (1969) Kinjeketile. Oxford University Press, Dar es Salaam.

Print this item

  MCHANGO WA WAANDISHI WA RIWAYA
Posted by: MwlMaeda - 08-27-2021, 05:44 PM - Forum: Riwaya - No Replies

Mchango wa Waandishi wa Riwaya

R.S. Mabala
Quote:
Quote:
Kila mwandishi ni mwandishi mwanasiasa.
Swali la pekee la kujiuliza ni: siasa gani na ni siasa ya nani.
Ngugi wa Thiong’o
 
Lugha na Fasihi
Mjadala kuhusu lugha na fasihi hapa Tanzania una sura tofauti sana tukilinganisha na nchi nyingine za Afrika kwa sababu ambazo sote tunazifahamu. Ijapokuwa wapo bado waandishi wachache ambao wanapendelea kutumia Kiingereza, kwa waandishi walio wengi hakuna mjadala tena kuhusu suala hili kama linavyowatatiza waandishi wengi kama kina Ngugi wa Thiong’o.
Hali hii ni ya kimaendeleo kwa sababu waandishi na wahakiki Watanzania wanaweza kuzama moja kwa moja katika uandishi wenyewe bila kupoteza nguvu nyingi katika mijadala mirefu kuhusu lugha ipi itumike. Vilevile waandishi hawana tatizo kuhusu wasomaji, maana lugha wanayoitumia ni ile ambayo wasomaji wote wanaijua. Kwa hiyo wana nafasi nzuri ya kuweza kuifikia jamii nzima, tofauti na Ngugi ambaye, bila kuwa na wafasiri, analazimika kuchagua ama Kiingereza, ili aweze kuongea na watu wa kila taifa ndani ya Kenya, japo wasomi wachache tu; ama Kikikuyu ili awafikie wakulima na wafanyakazi kama anavyodhamiria, Japo Wakikuyu tu. Ndiyo maana Ngugi anasisitiza umuhimu wa kuwa na wafasiri wawezao kufasiri kazi zake katika kila lugha ya Kenya.
Hata hivyo, nafasi hii ya kipekee aliyo nayo mwandishi Mtanzania lazima itafakariwe vizuri maana ni rahisi kwa mwandishi kujiona yu mwandishi wa umma kwa sababu tu anatumia lugha ya umma bila kutafakari yaokanayo na matumizi ya lugha hiyo. Iko hatari ya mwandishi kuridhika kwamba iugha ndiyo kigezo pekee cha mwandishi wa kimapinduzi. Hali hii hasa yahusu kizazi kipya cha waandishi ambacho kimerithi mafanikio yanayotokana na mapambano ya ‘vaandishi wakongwe kukipa Kiswahili nafasi na hadhi yake kama lugha ya Watanzania. Katika mapambano kama hayo mtu huelewa zaidi umuhimu wa lugha, pia matumizi na maudhui yanayobebwa na kuwasilishwa na lugha hii. Kwa mfano, msimamo thabiti wa Ngugi umetokana na mapambano hayo. Katika kitabu chake Decolonising the Mind anasisitiza mambo mawili muhimu:
Quote:
(a) Mwandishi Mwafrika anayedai kwamba hawezi kuandika bila kutumia lugha ya kigeni ni sawasawa na mwanasiasa ambaye anasema kwamba Afrika haiwezi kuendelea bila ubeberu. Tena mwandishi huyu yuko nyuma zaidi kuliko wamisionari na tabaka la vibepariuchwara ambao wote, kutokana na masilahi yao, wanatambua umuhimu wa kutumia lugha za watu ili waweze kufikisha ujumbe wao hata kama ujumbe wenyewe si wa kimaendeleo.
Quote:
(b) Kutumia lugha za Afrika ni hatua ya kwanza ya lazima, lakini ni hatua ya kwanza tu. Kutumia lugha hii hakutachochea mabadiliko wala maendeleo ya maana iwapo haitatumika kuendeleza mapambano ya wafanyakazi na wakulima dhidi ya ubeberu.
Na anaendelea; “Kwa maneno mengine, waandishi wanaotumia lugha za Kiafrika wanapaswa kujihusisha upya na mila za kimapinduzi za wakulima na wafanyakazi wakijitayatisha katika mapambano yao ili washinde ubeberu na kujenga mfumo madhubuti zaidi wa kidemokrasia na kijamaa.”1
Hoja hii ya Ngugi ni nzito sana na sitegemei kwamba kila mwandishi anaweza kulenga hivyo katika kila analoliandika. Lakini hoja hii, katika muktadha wa dondoo letu la kwanza – kwamba kila mwandishi, akubali asikubali, anahusika na siasa – ni msingi mzuri sana katika kuangalia na kupima mafanikio ya waandishi wetu.
Mwandishi na Jwnii
Kutokana na maneno ya Ngugi hapo juu, yafaa vilevile kukumbuka maneno ya wananadharia wawili wengine ambao waliandika katika mazingira tofauti. Kwanza, Lenin alimwandikia Maxim Gorky baada ya Mapinduzi ya mwezi Oktoba 1917:
Quote:
Ukitaka kuchunguza, sharti uchunguze kutoka chini, ambapo yawezekana kuangalia vizuri kazi ya kujenga maisha mapya katika makazi ya wafanyakazi, mikoani au vijijini.2
Hii inafanana na usemi wa Bertolt Brecht aliyesema kwamba mwandishi sharti “atazame mdomo wa umma.”3
Hapa tunaona kwamba Lenin na Brecht, kama wananadharia wote wa kijamaa, waliona hatari ya mwandishi kujitenga na jamii. Lenin alimwandikia Gorky kwa sababu wakati ule Gorky, ambaye daima huko nyuma alikuwa akiakisi maisha ya wafanyakazi, alikuwa ameanza kulowea makao makuu akishirikiana na waandishi na wasomi wenzake tu kiasi kwamba alianza kujitenga na umma. Brecht kadhalika aliona umuhimu wa kuwakumbusha waandishi na waigizaji hatari hiihii. Na hapa Tanzania hatari hii ipo vilevile kwa baadhi yetu. Uwezo wetu wa kuona, kuelewa na kuakisi jamii barabara umeanza kufifia kutokana na kujitenga kwetu na jamii au kushirikiana na aina au tabaka fulani tu ya watu, au kuchunguza kutoka juu.
Lengo la Makala
Lengo la makala haya basi, ni kuangalia baadhi ya waandishi ambao wameamua kuandika kuhusu matatizo, migongano, mapambano na maendeleo ya Tanzania baada ya kupata uhuru. Hivyo sitaweza kuangalia wale ambao lengo lao ni kustarehesha, wakiendeleza, kudekeza na kukuza fikra potofu katika jamii kama anavyotahadharisha Ernest Fischer:
Quote:
Kuigeuza sanaa kuwa biashara tu ili kuburudisha na kuridhisha nafsi ni hatari sana kwa sababu wakati vitabu vya aina hii vinajifanya kuwa vinamkomboa binadamu kumbe vinamdhalilisha.4
Hata baada ya kufinya uwanja wa makala haya, bado hatuwezi kusema kwamba kutalii huku katika mada kunatosheleza, ila tu katika riwaya ambazo napenda kuzingatia mielekeo fulanifulani inajitokeza. Unaweza kuzigawanya riwaya hizi katika mafungu matatu:
Quote:
(a) Riwaya zinazohusu Tanzania na suala la ukombozi kwa jumla nje na ndani ya Tanzania.
Quote:
(b) Riwaya zinazoangalia hasa tabia ya watawala wa nchi.
Quote:
© Zile zinazoangalia matatizo ya jamii ya tabaka la nchini, hususan katika vijiji.
Nimeamua kuangalia riwaya hizi kwa misingi mitatu mikubwa:
Quote:
1. Haitoshi kusema kwamba fasihi inaakisi jamii. Kama anavyosema Ngugi:
Quote:
Quote:
Fasihi haiakisi hali halisi tu bali hujaribu kumshawishi msomaji kujenga msimamo fulani kuhusu hali halisi hii. Kwa hiyo suala siyo je, ameakisi Jamii? Bali je, ameakisi kutoka wapi na ana shabaha gani katika uakisi wake?5
Quote:
Quote:
Nikinukuu shairi moja fupi kabisa la mwandishi mashuhuri wa Afrika ya Kusini, Dennis Brutus, anasema:
Quote:
Quote:
Quote:
Kioo kinahudumia
Mtazamaji anakielekeza.6
Quote:
2. Yawezekana na yatokea mara kwa mara kwamba mwandishi anaweza, bila kujitambua mwenyewe,
Quote:
Quote:
(i) kuonyesha mambo ambayo hakudhamiria
(ii) kuonyesha mambo ambayo yanapingana na yale aliyodhamiria kuonyesha.
Quote:
Kwa hiyo yawezekana kutokea mgongano kati ya ujumbe wa wazi aliodhamiria na ule uliofichika ambao pengine hakudhamiria au aliutambua kwa mbali.
3. Ijapokuwa makala haya yanaangalia hasa maudhui ya riwaya hizi, ni wazi kwamba suala hili haliwezi kutengwa na fani anayoitumia mwandishi.
Mafanikio ya Riwaya
Mafanikio yanaonekana katika ule ujumbe wa wazi. Waandishi wameongelea dhamira nyingi zenye maana na umuhimu sana hapa Tanzania.
Kwanza riwaya zimechochea na kuendeleza fikra za ukombozi wa Tanzania na Afrika kwa ujumla. Kwa mfano, Pepo ya Mabwege na Njama vimesaidia kuwapa Watanzania mwamko na urazini mkubwa zaidi. Katika Njama mwandishi ametumia fani ya kina James Hadley Chase ambazo huhusu uhalifu na upelelezi kupanua mawazo kuhusu ukombozi wa Afrika ya Kusini, uonevu wa makaburu na mbinu zao.
Pili, zimefichua na kukosoa wapinga maendeleo ambao wamejivisha ngozi ya kondoo na wanatumia nafasi zao kama viongozi kujinufaisha wenyewe na kuihujumu Tanzania. Dhamira hii inaonekana katika riwaya karibu zote, k.m. Pepo ya Mabwege, Sudiya Yohana, Nguzo Uhondo, Nyota ya Huzuni, na kadhalika. Bila kuogopa, wameonyesha uozo mbalimbali ndani ya jamii, jinsi viongozi walivyo na vyeo vingi, k.m., Sir Henry Mwapeker na Mzee James Katika Pepo ya Mabwege; na mbinu wanazotumia ili kujijenga na kujiimarisha mpaka wote wanawaogopa. Hata polisi wanaogopa kufungua kesi ya Kalenga dhidi ya Waziri. Hali hii yaonekana hadi uongozi wa kijijini. Kwa mfano, katika Njozi Iliyopotea wanakijiji wote wanaogopa mwanzoni kumpinga Jumbe Mpwite kwa kuwa ni Mwenyekiti na anaye mganga wake.
Vilevile waandishi wamekazana kuonyesha ulaghai wa watu kama hao. Mzee James anagombea ubunge kama mjamaa. Joseph katika Sudi ya Yohana anahubiri kuhusu ukombozi wa Mwafrika na anapenda kusaidia ndugu zake huku akiwa mstari wa mbele katika kuhujumu kijiji chake na kuharibu maisha ya nduguze. Katika Njozi IliyopoteaLupituko anatumia nguvu kujenga siasa ya ujamaa ili kuridhisha silika yake ya ukatili na kuonyesha uwezo alio nao. Kadhalika itikadi ya Mambosasa katika Gamba la Nyokaimejaa kujitetea kwingi na visingizio vya kuridhisha nafsi yake.
Tatu, riwaya hizi zimeweza kuangalia kwa undani na kufundisha juu ya matatizo yanayolikabili tabaka la wanyonge.
Mojawapo ni kuhusu uongozi mbaya. Viongozi wengi ni vidikteta vidogo kama Lupituko au Katibu Tarafa Kagunda ambao wanaonea wananchi. Lupituko anahamisha familia kikatili kwa sababu mtoto wa kike alimkataa na baadaye anaua msichana mwingine katika kujaribu kumnajisi. Katika Sudi ya Yohana Kagunda kadhalika alimfunga mwanamke aliyemkataa. Katika Gamba la Nyoka Mambosasa anapokea hongo kutoka kwa wafanyabiashara.
Uongozi huu ulionekana hasa katika kipindi cha kuanzisha vijiji. Mara nyingi vijiji vilijengwa mahali pabaya kwa sababu ya wivu wa pimapima au hongo wanazopewa na makabaila au matajiri. Vilevile nguvu zimetumika kuhamisha watu bila sababu yoyote.
Athari za udhanifu katika jamii, ukiwa uchawi au Ukristo, unaonyeshwa pia. Katika Mirathi ya Hatari tunaona jinsi uchawi unavyotishia jamii nzima hadi hapo wachawi wote wanapoteketea. Hali kadhalika katika Gamba la Nyoka tunaona jinsi imani za wanakijiji zilivyoruhusu Mmarekani asiye hata Padre kupenya, kuchokoza vita kati ya wanakijiji na serikali, na kusababisha vifo vingi na baadaye kuua wengine kwa kutia sumu kisimani.
Katika Sudi ya Yohana, Amina anamsifu na kumshukuru Yohana kwa kusema:
Quote:
Mwenyezi Bwana ndiye kakutuma uje uniokoe, hakunitupa mimi mja wake. Si haki kumlaumu bali kuomba kujaziwa mema zaidi.7
Nne, riwaya zimeonyesha vijana wengi wanavyokimbilia mjini, kwa mfano, Matika na Chonya katika kitabu cha Shida. Hii yaweza kutokana na mila (kwa mfano Matika alikimbia kuozwa kwa nguvu); au fikra finyu kuhusu maisha ya mjini na nafasi za kupata kazi na kuishi kwa raha.
Tano, riwaya hizi zimefaulu kuonyesha matatizo ya wanawake katika jamii. Mara kwa mara wanawake wanaonyeshwa kuwa chombo cha uchu na ulafi wa wanaume. Familia ya Nyalindele inahamishwa kwa nguvu kwa sababu Nyalindele anamkataa Katibu Kata. Tulilumwi anakufa kwa sababu hiyohiyo; Losia analeweshwa na kudanganywa na kuachwa na mimba hadi anaamua kujiua. Agnes, mke wa Yohana, ananajisiwa kwa nguvu na shemeji yake. Matika anapokimbilia mjini analazimika kuwa malaya; Josina naye ananajisiwa baada ya kupewa dawa za kulevya. Mkewe Zautwa nave anafungwa kwa sababu ya kumkataa Katibu. Wanawake wanaonyeshwa wakidharauliwa kupita kiasi. Anavyosema Lukova katika Njozi Ilivopotea:
Quote:
Mke ni kama ngalawa. Matumizi yake makubwa na faida yake kidogo daima imaji mkukuu; hufaa lakini haiaminiki.8
Hata wanapojitahidi kujitetea au kubaki na msimamo wao wanaadhirika vibaya. Mara nyingi mwisho wanahesabiwa kuwa vyombo vya starehe tu.
Sita, waandishi nao wametoa ufumbuzi wa aina mbalimbali wa matatizo wanayoyaonyesha. Kwa mfano, mwishoni mwa Njozi Iliyopotea wanavijiji wameshagundua ubaya wa Jumbe Mpwite, na wanasimama imara kwa pamoja dhidi yake na wenzake. Katika Gamba la Nyoka mwandishi anaonyesha vizuri sana kwamba watakaoendeleza maisha ya wakulima ni wakulima wenyewe, si wahubiri kutoka nje, wawe wa siasa au dini:
Quote:
Wana mapinduzi halisi ni wale waishio vijijini wanaoathiriwa na upepo wa wakati unaowasukuma mbele kutoka walipokuwa. Kwao maisha ni maisha. Wanatazama kwa uangalifu kila badiliko linalohusu maisha yao kama watazamavyo kwa uangalifu na matumaini makubwa mimea yao ikikua9
Mara nyingi pia waandishi wanapenda kuonyesha maadui wakifichuliwa au kuteketezwa kama katika Pepo ya Mabwege.
Kwa kweli maelezo haya ya mafanikio yamekuwa mafupi mno na ya jumla, maana lengo la makala haya halikuwa kuangalia mafanikio haya ya wazi kwa undani sana. Lakini isingefaa kuzama kwenye matatizo tu bila kutambua kwamba waandishi hawa wamekwisha kutoa mchango mkubwa.
Matatizo ya Riwaya
Mafanikio ya dhamira za waandishi yameathiriwa mara nyingi na mambo makuu manne:
Quote:
(a) Kushindwa kuonyesha uhalisia kamili.
Quote:
(b) Kuzama katika nadharia ya ubinafsi bila hata kujitambua.
Quote:
© Falsafa na mtazamo wa kukata tamaa katika maisha – mtazamo kwamba maisha ni matatizo tu; mfululizo wa mateso usio na mantiki wala utatuzi.
Quote:
(d) Waandishi kupenda kusisitiza hoja zao kwa kuhubiria watu.
Uhalisia
Katika riwaya zao waandishi kwa ujumla wamefuata mtindo wa uhalisia, yaani wamedhamiria kuakisi jamii jinsi ilivyo, mara nyingi wakiwa na lengo la kuikosoa jamii ili ijirekebishe. Katika hali hii, lazima matukio na wahusika viwe vya kuaminiwa. Iwapo msomaji husita kupokea yanayotokea, riwaya huanza kuchechemea.
Mtiririko wa Vituko
Udhaifu huu unaonekana mara a kwa mara katika riwaya. Kwanza kuna matukio mengi ambayo yanapunguza uzito wa dhamira. Kwa mfano katika Pepo ya Mabwege, Josina, Kalenga na Hamisi ambao walikuwa wameachana siku nyingi wanakutana kwa bahati tu wakati mambo yameiva. Kalenga anapokwenda kumshitaki Mzee James, asingefika popote bila kufika ghafla kwa Hamisi ambaye hajaonanana Kalenga miaka kumi na nne lakini sasa amerudi na bahati nzuri amepandishwa cheo sana kiasi cha kuweza kumsaidia Kalenga moja kwa moja. Vilevile katibu wa Mzee James ni Blandina ambaye ndiye alikuwa mchumba wa Hamisi walipokutana Urusi, na ni huyuhuyu ambaye mbele ya Josina na Kalenga “anaponda” mvulana wake kwenye kituo cha basi kwa sababu ya kupewa lifti na mkwasi. Matukio kama haya labda yaweza kukubalika lakini utatuzi wa matatizo yote katika riwaya unakuwa kana kwamba ni wa juujuu tu na wa kulazimisha. Kalenga ameshachukiwa na wakubwa, wakiwemo Mhariri Mkuu wa gazeti analofanyia kazi. Msimamo wake wakati huu umekwishakua, na hata kufukuzwa amefukuzwa kazi, lakini katika siku chache zilizobaki anaachiwa gazeti awe mhariri mkuu. Anatumia nafasi hii vizuri kufichua njama kadha wa kadha na maadui wa taifa wanakamatwa. Basi ufumbuzi mzima wa riwaya. wategemea kitu ambacho kiko nje ya uhalisia.
Kadhalika katika Njama, mtiririko wa vituko wategemea Willy Gamba au wenzake wa Sierra Leone kuwepo, kwa bahati tu, mahali na wakati unaofaa kila mara. Mfano ni Willy anavyomwokoa Zabibu nukta chache kabla ya kuchinjwa. Kadhalika Willy anapokwenda Sierra Leone anatokea kukutana na mtu atakayemfaa katika mapambano ya baadaye.
Mtiririko mzima wa Njama unamtaka msomaji afumbe macho ili asione mambo yasiyoaminika. Kwa mfano, mauaji makubwa yanafanywa na kundi la majasusi wasaliti lakini kila mara wanapomkaribia Willy wanamwonya tu na hivyo kumpa nafasi ya kuwamaliza wote mwishoni. Vilevile shabaha yao ghafla inageuka kuwa mbaya kila wakimlenga yeye. Hivyo umaarufu wote wa Willy Gamba unatokana na mwandishi kwenda nje ya uhalisia.
Mtiririko wa Gamba laNyoka nao haufuati uhalisia katika sehemu muhimu. Kwa mfano, maisha ya Mambosasa na Mamboleo hayaeleweki. Wamerudishwa kijijini kwa sababu ya tabia zao mbaya na upinzani wao dhidi ya serikali. Sasa yashangaza kwamba japo hawajaonyesha kuwa wamejirekebisha wanaruhusiwa kugombea uongozi wa kijijini. Halafu baadaye ingawa bado matendo yao hayakubaliki kwa watawala (k.m., wanampiga Padre Madevu, wanakula fedha za kijiji, na wanahongwa na watu binafsi hadi kijiji chenyewe kinawakataa), Mamboleo anachaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Maendeleo wa Wilaya. Kwa hiyo matukio yanaonekana yanatukia tu kwa amri ya mwandishi ambaye yeye, kama Mungu, anaweza kuamua afanye lolote lile na dunia aliyoiumba. Hata mwanzoni mwa riwaya watu wa Kisole, katika kuamua kukataa kuhamia kijiji kipya wanaua wanamgambo karibu mia moja lakini zaidi ya kukalishwa juani kwa muda wa saa chache na kuhamishwa kwa nguvu siku inayofuata, hakuna hatua yoyote inayochukuliwa dhidi yao, au viongozi wao. Hivyohivyo, Madevu anapoua watu ishirini kwa sumu hatuoni hatua yoyote ya maana inayochukuliwa. Mikasa hii ya hatari katika jamii inapita sawasawa na mkasa wowote mwingine kama vile mtu anavyowatembelea wakwe zake! Uzito wa mikasa na vipi jamii inalichukulia jambo hili zito hatuonyeshwi. Badala yake tunaona tu kwamba Tina anajuta kumwua Madevu bila hata kukumbuka wanakijiji wenzake waliokufa.
Upande wa Njozi Iliyopotea yaelekea kwamba mwandishi anataka kutuonyesha kwamba viongozi wanatumia vibaya madaraka yao lakini uzito wa hoja hii unapungua kutokana na kwenda nje ya uhalisia. Hii inaonekana hasa katika kesi ya Lukova baada ya kumpiga Katibu Lupituko.
Lupituko, akiwa ni kiongozi wa serikali, alikuwa na nafasi ya kutosha kummaliza Lukova kwa kuonyesha jinsi Lukova, kama ‘mpinga mapinduzi’, alivyomwingilia katika kazi yake na kumpiga akiwa kazini. Lupituko angeweza kula njama na hakimu na kumwadhiri Lukova sawasawa. Mashtaka dhidi ya Lukova ni makubwa: wizi wa kutumia nguvu, kuwa na meno ya tembo kumi na moja na ngozi tatu za chui bila kibali, kuwa na bangi masanduku mawili, na kuwa na bunduki ya serikali iliyoibiwa. Mashtaka kama hayo yanahitaji ushahidi wa kutosha na yanaweza kubatilishwa kabisa na wakili mahakamani, lakini utetezi wake tu ni kwamba ndugu na marafiki wanasema kwamba Lukova hana tabia ya namna hii. Hivyo:
Quote:
(a) Mashtaka yenyewe yameongezwa kupita kiasi
Quote:
(b) Utetezi upande wa mshtakiwa ni mdogo mno. Iwapo wakili kweli alimwonea huruma na kuamua kumtetea ipasavyo, anastahili kufukuzwa kazi kwa kushindwa kubatilisha mashtaka yasiyo na ushahidi.
Quote:
© Ushahidi wa Kiligilo usingekuwa na maana yoyote hata kama angeweza kusema bila kuondoka kwa ghadhabu. Kwa hiyo dhana ya kwamba rafiki yake alihukumiwa kwa sababu Kiligilo alishindwa kumtetea haipo kabisa. Kutokana na hayo, uzito wa hoja ya mwandishi unapunguzwa.
Mifano kama hii inaonekana katika karibu kila riwaya. Katika Sudiya Yohana Joseph anazidi kumdhulumu ndugu yake kuanzia kumwingilia mke wake kwa nguvu, hadi kumkatalia nafasi yake ya kusoma ng’ambo, na mwisho kumfukuzisha kazi. Licha ya yote haya bado anategemea kwamba Yohana atakubali kumwendeshea kampuni yake. Vilevile migomo ya wafanyakazi inapachikwa tu kwa kuwa mwandishi anataka kuonyesha mwamko wa wafanyakazi.
Uchoraji wa Wausika
Kukosa uhalisia upande wa wahusika nako kunaathiri sana dhamira ya mwandishi. Tukianzia kwa Mambosasa na Mamboleo katika Gamba la Nyoka, ni kweli kwamba hawa ndugu wawili wana migongano mikubwa ndani yao kutokana na kulewa itikadi na ukatili wao, lakini mwandishi ameshindwa kuoanisha vipengele mbalimbali katika tabia zao. Mara twaambiwa wamefanya mema mengi katika jamii, kwa mfano, kufichua wenye maduka wanyonyaji na wapimaji wa pamba walaghai; kujenga visima vizuri kwa kushirikiana bega kwa bega na serikali katika operesheni vijiji, n.k.; mara twaambiwa kwamba ni wapinzani wakubwa ambao walimpiga mwalimu wa siasa J.K.T. na kusambaza karatasi ya uchochezi kambini. Upande wa mapenzi, Mambosasa anajiambia:
Quote:
“Sina muda wa mapenzi. Mapenzi ni mojawapo kati ya mambo ambayo hayapasi kuambatana na tabia njema ya mwanamapinduzi halisi.”10 Lakini hapohapo tunafahamishwa kwamba sababu nyingine ya kurudishwa kwao kijijini ni kwamba walimnajisi msichana. Hivyohivyo katikati ya mjadala mzito juu ya matatizo ya ujamaa Mambosasa anauliza: “Mamboleo umekwishashika maziwa ya msichana mdogo?”11
Ni kweli kwamba binadamu amejaa mikinzano ya kila aina, lakini lazima kuwepo na uhusiano na mfungamano kamili wa wahusika hao ambao utafanya tuyaamini mabadiliko haya ya tabia ya mara kwa mara. Hali hii inaathiri hata wahusika wengine. Mara nyingi pia tabia za wahusika hazionekani kwa vitendo kiasi kwamba kunakuwepo na mgongano. Kwa mfano, katika Njozi Iliyopolea mwandishi anataka kujenga dhana ya kwamba Kiligilo ni mcbapakazi na mpenda haki anayewafunulia wanakijiji haki zao na kujenga umoja thabiti katika kuendeleza kijiji. Hayo yote tunaambiwa moja kwa moja na mwandishi mwenyewe, hatuyaoni sana katika vitendo vya Kiligilo. Kinyume chake mara nyingi anachelewa kuamka na kwenda kazini; mara tu baada ya kufika kijijini na kuanza kazi, anapata matatizo na anapotea mwezi mzima. Hajaonyesha tabia yoyote inayotudhihirishia kwamba maneno ya mwandishi ni kweli. Hivyo inaonekana kwamba mwandishi analazimisha hoja zake.
Hata hivyo Kiligilo angalau ni binadamu, kinyume na Willy Gamba ambaye kwa uwezo wake anafanana na miungu, na kama miungu walivyo anaabudiwa, hasa na wanawake. Anatamba mwenyewe, “mimi huwa sielewi kwa nini binadamu hawa hutokea kunipenda mara tu nionyeshapo uso wangu.13
Na kweli. Kwa mfano, Zabibu anaambiwa kwamba mpenzi wake ameuawa. Wakati huohuo mara amekwishampenda Willy:
Quote:
Niko tayari kukusaidia kwanza kwa sababu umeniokoa pia kwa sababu unapeleleza kifo cha mpenzi wangu na tatu nafikiri wewe ni kijana mwenye kupendeka.13
Ikifika usiku anakwenda kulala na Willy.
Mfano huu unaonyesha uhalisia hafifu katika uchoraji wa wanawake. Nisingependa kusema mengi maana mada hii ina siku yake, lakini kwa ujumla wanaonekana binadamu dhaifu kupita kiasi. Katika Njama, mapenzi yao hubadilika mara moja. Mfano mwingine ni Margret. Mara atokeapo mwanamume shujaa basi tunaona mara moja msichana huyo “ameshakwisha” japo wakati huo anaomboleza kifo cha mpenzi wake. Hata kama wako wasichana ambao nao wana nguvu, kama vile Veronica, bado haifuti wazo kwamba wanawake ni chombo cha starehe, hasa kwa mtu kama Willy ambaye mwandishi anatuambia kwamba anastahili warembo hao kwa sababu ya kazi ngumu anayoifanya.
Hata katika riwaya nyingine, wanawake huonyeshwa wadhaifu kupita kiasi na rahisi kudanganywa au kulazimishwa. Hata jitihada za baadhi yao kusimama imara zinaishia ukingoni tu. Josina anapewa dawa za kulevya na kunajisiwa. Losia, msichana mwenye tabia nzuri ajabu, ambaye wakati wote akiwa shuleni hakuteteleka hata kidogo, anadanganyika kirahisi na pombe ya siku moja na kuamka kesho yake kitandani mwa mwanamume bila hata kujitambua alifikaje pale. Tena hapohapo anabeba mimba na mwisho kuona njia ya pekee ni kujiua. Ameshindwa. Mama Liganga naye anasimama imara kujitetea lakini matokeo yake anafungwa miaka mitatu na kugeuka malaya anapofunguliwa. Mkewe Yohana naye analazimishwa na Joseph. Kuna mifano mingine mingi. Ni kweli kwamba waandishi wanataka kuonyeshajinsi wanawake wanavyoonewa, lakini mwishoni inaonekana kwamba hata wale wanaotaka kusimama imara wanashindwa wote. Kwa hiyo watabald dhaifu tu.
Mwisho, upande wa wanawake, mara nyingine tunalazimishwa kujiuliza kama wanawake wasio na uzuri kupita kiasi wana nafasi kalika jamii. Hali hii yajitokeza hasa katika Njama. Kila msichana ni mrembo kupita kiasi, ambaye hajawahi kuonekana, na ni haohao wenye uwezo. Hii ni kurahisisha mambo kupita kiasi na inadhalilisha uwezo na tabia za wanawake. Katika riwaya nyingine hali hii siyo mbaya sana lakini hujitokeza hapa na pale.
Mauaji
Riwaya nyingi zimejaa mauaji. Katika Njama Willy anaua karibu watu mia moja peke yake. Katika Pepo ya Mabwege, Josina na Master Peter wanakufa. Katika Njozi IliyopoteaLosia Lukova, Tulilumwi, na Lupituko wanafariki; na katika Mirathi ya Hatari wanakufa watu wengi sana. Huenda hali hii inatokana na:
Quote:
(a) kutaka kumshawishi msomaji kwa kutumia vituko visivyo vya kawaida
Quote:
(b) haja ya kuipatia riwaya tamati yenye kuridhisha. Hata hivyo mauaji nayo yakizidi uhalisia hupungua.
Kutia Chumvi Nyingi
Mauaji ni mfano mmoja tu wa jinsi waandishi wanavyotia chumvi kupita kiasi. Njama inatupa mfano halisi mwingine:
Quote:
“Nilijiviringisha hewani namna ambayo wote walishangaa; risasi zao zote zikanikosa. Wakati uleule nikaachia za kwangu nikawapata wote nao wakaanguka chini.14Au kwingine tunaambiwa kwamba Willy anaweza kuruka futi nane, ambayo ni zaidi ya rekodi ya dunia. Kutokana na chuku za namna hii, mhusika haaminiki.
Hali hii inaonekana mara nyingine mwandishi anapotaka kusisitiza hoja yake. Kwa mfano hadithi nzima ya Amina anavyoachwa pale kwenye kituo cha basi huku akitaka kujifungua. Mwandishi anataka kutuonyesha jinsi jamii ilivyoharibika lakini lengo na msisimko wa sehemu hii unapotea.
Mwisho waandishi wengi wanapenda kutuinia tashititi, ucheshi, n.k., ili kuwasilisha ujumbe wao. Kwa mfano, katika Pepo ya Mabwege mwandishi anaonyesha jinsi watumishi wa hoteli wanavyowakimbilia Wazungu hadi wanagonganisha vichwa na mmoja anapoteza jino. Vivyohivyo kanisani Josina anapomkataa Peter, matendo ya watu kuhusu jambo hili yanatiwa chumvi sana. Tashititi kwa kawaida hutegemea utiaji wa chumvi lakini ili ifanikiwe inapaswa iwe sehemu kamili ya muundo na mtiririko wa hadithi kwa jumla.
Udhanifu
Udhanifu huonekana hasa katika tamati za riwaya. Mwandishi anapenda kuonyesha hali ya maendeleo au kuondoa waovu, kwa hiyo anapachika tamati nzuri ambayo mara nyingine inakwenda kinyume na yaliyotokea awali. Pepo ya Mabwege ni mfano mzuri. Tumeshaonyesha kwamba kufichuliwa na kuondolewa kwa uovu ndani ya jamii kunategemea Kalenga kuwa Mhariri Mkuu kinyume cha hali halisi. Matokeo yake ni kwamba wema unashinda, jamii inasafishwa, na Kalenga anapandishwa cheo kuwa Mhariri Mkuu. Kwa hiyo inavyoonekana uozo haukutokana na mfumo hata kidogo, bali umetokana na watu wachache tu wenye nia mbaya ambao wametumia nafasi zao kwa faida yao. Sasa kizazi kipya kimeshika hatamu, kwa hiyo hakuna matatizo yoyote wala haja ya kufanya mabadiliko katika jamii.
Katika Shida, Chonya na Matika wanarudi katika kijiji cha Paradiso. Mapambano yamekwisha. Katika Gamba la Nyoka mwandishi anakwepa udhanifu huu. Anaonyesha matatizo kadha wa kadha yanayokabili uanzishaji wa vijiji vya ujamaa, lakini mwishoni mapambano yanakwisha hivyohivyo. Viongozi wabaya vijijini na wilayani wanaondoka, trekta inafika, na mabomba ya maji – mpaka tunaelezwa hata kazi za kila kamati kijijini. Kwa hiyo baada ya dhiki, faraja yapatikana moja kwa moja. Katika Mirathi ya Hatari wachawi wote wanateketea. Si kwamba tamati nzuri ya matatizo haiwezi kupatikana, ila tamati hizi zinaishia katika ndoto kwa sababu:
Quote:
(a) mara nyingine hazitokani na yaliyotangulia; na
(b) zinakuwa nje ya maisha ya kila siku ya jamii. Harakati zinatoweka.
Kwa kifupi, lengo la sehemu hii ya “udhanifu” ni kuonyesha jinsi udhaifu wa uhalisia unavyoathiri sana dhamira za waandishi, maana mahali ambapo msomaji anashindwa kukubali uakisi wa wahusika na hali halisi basi na dhamira ya mwandishi nayo haitakubalika.
Ubinafsi
Ijapokuwa waandishi wanaonyesha jamii ikipambana na waovu, mapambano haya daima hutegemea nguvu ya watu wachache sana. Umma haupo. Mfano halisi ni Njama.Ijapokuwa mwandishi anasema kwamba riwaya ni: “Kwa ajili ya wale wote ambao wamejitoa mhanga katika kupigania uhuru wa bara hili la Afrika,”16 dhamira inayojitokeza ni kwamba bila Willy Gamba na uwezo wake wa kujiviringisha kwa namna ya ajabu, ukombozi wote ungekwama. Wapigania uhuru wenyewe wamepigwa butwaa pamoja na kamati ya ukombozi na polisi. Hawana nguvu yoyote. Hata mwishoni mahali ambapo imeeleweka wazi mahaini wako wapi na ni kiasi tu cha kuwazingira na kuwakamata bado ni Willy tu na Sherriff, Eddy na Isaac ambao wanakwenda peke yao kuteketeza kundi zima la wahalifu. Hivyo dhana inayopatikana hapa ni kwamba ukombozi wategemea nguvu ya binadamu wachache wenye vipawa vya ajabu. Kazi ya umma ni kukaa na kushangilia na kushukuru hawa wachache kwa kuwaokoa wao wasio na akili na uwezo wowote.
Huu ni mfano mmoja wa dhamira zilizojificha, dhamira zenye kuhitilafiana na zile zilizo wazi. Mapema katika riwaya mwandishi anaeleza kwa ufasaha umuhimu wa mapambano ya umma na jinsi vyama vya kupigania uhuru vinavyojitahidi, lakini hadithi yenyewe inaonyesha kwamba mbele ya mbinu za hali ya juu ya makaburu, umma hauwezi kitu.
Dhana nyingine inayotokana na hiyo ni kwamba hawa binadamu wachache wa ajabu wanastahili maisha ya ukwasi wa hali ya juu kutokana na mchango wao. Hivyo Wasichana warembo “wanawaangukia” kila dakika, wanaweza kusafiri dunia nzima kupumzika kama Willy alivyokwenda Sierra Leone, maisha yao ni.kula katika hoteli za kitalii na kunywa pegi nyingi za wiske. Hapo vilevile twaambiwa kwamba lipo tabaka la juu linalostahili maisha haya mazuri lakini siyo tabaka la umma.
Katika Pepo ya Mabwege hali hii haijitokezi kiasi hicho lakini ipo. Mwapeker na James ni watu wakubwa katika jamii na nyadhifa zao ni nyingi lakini wanaangushwa na jitihada za Kalenga peke yake akisaidiwa na Hamisi na watu wengine wachache. Kwa hiyo hapa vilevile mapambano ni kati ya wale waovu wakubwa na watu wachache wanaowaona. Ni vita vya mafahali, sisi wengine twabaki ni watazamaji tu.
Kwa ujumla nguvu ya wafanyakazi haionekani kabisa. Hata wale wasaidizi wa Kalenga waliosoma naye wana kazi nzuri katika jamii, k.m. mwandishi wa habari, inspekta wa polisi, mwalimu – wote wamepata nafasi ya kusafiri nje. Kwa hiyo karibu ni wa tabaka lilelile la kina Mwapeker. Labda tofauti ni kwamba hiki ni kizazi kipya lakini nafsi zao ndani ya mfumo ni zilezile, na mfumo unabaki palepale. Mwapeker na James wanajenga himaya yao kwa kutumia watu binafsi wanaowafahamu, na Kalenga na wenzake wanawaangusha kwa kufanya hivyohivyo. Tunaweza kujiuliza kama Hamisi angemsaidia Kalenga iwapo hawakusoma pamoja. Vilevile ni jambo la ajabu kwamba wote wenye msimamo imara wanatoka nje ya Tanzania au wamekwenda ng’ambo. Katika Njama Willy anasaidiwa hasa na watu wa Sierra Leone. Ni vizuri sana kuonyesha umoja wa Afrika lakini Watanzania nao hawana uwezo huu isipokuwa Willy na wenzake katika upelelezi? Katika Pepo ya Mabwege kadhalika, Kalenga amesoma Nairobi na kufanya kazi Msumbiji, Josina kasoma Cuba, na Hamisi Urusi. Waliosoma Tanzania wanaonekana hawawezi kupata urazini huo mkubwa.
Ubinafsi unaonekana vilevile katika dhamira ya wahusika wengi ya kulipiza kisasi. Willy anamfuata Shuta kumlipizia kisasi Veronica. Kalenga naye anasukumwa na nia ya kumlipizia kisasi Josina. Vilevile katika Sudi ya Yohana mwandishi anaona kwamba njia pekee ya kutatua matatizo yanayojitokeza katika jamii ni Yohana kwenda kumchoma kisu Joseph. Zautwa alikuwa hoi kwa sababu alishindwa kulipiza kjsasi. Mdogo wake Wakili Mwakipusi naye aliishia kulipiza kisasi. Kwa hiyo, kwa kufanya hivyo waandishi wanaleta dhana ya kwamba kila mtu binafsi akiamka namna hiyo basi hata kama jamii haibadiliki angalau haki fulani itakuwa imetendeka; kilio cha wanyonge kitakuwa kimesikika na mwovu atakuwa ameadhirika hata kama mfumo ulioruhusu uovu huu umebaki palepale.
Kusema yote hayo hakuna maana kwamba mwandishi wa makala haya anataka kuona wafanyakazi wakiamka na kupigana moja kwa moja wakiwa na urazini mkubwa na mikakati ya hali ya juu. Hii itakuwa kinyume cha uhalisia tena. Lakini yawezekana kwamba waandishi hao wameathiriwa na elimu yao na nafasi zao katika jamii kiasi cha kuona mapambano upande wa tabaka la kati tu, na mapambano ya mtu binafsi kutetea haki zake kazini, shuleni, na kadhalika, bila kuona na kushiriki katika mapambano ya walio wengi ambayo yanaendelea siku hadi siku. Tukitumia mfano mmoja wa tamthiliya, tunaona kuwa katika mchezo wa mafuta wafanyakazi wanagoma lakini mara tu wanapofukuzwa kazi na kuona njaa ya siku mbili wanarudi na kulamba miguu ya tajiri wao. Hii ni tofauti na waandishi wengine mashuhuri wa Afrika, k.v., Sembene Ousmane, Ngugi wa Thiong’o na Alex la Guma ambao daima wanatambua kwamba umma upo na nguvu unazo hata kama hawaamki wote kwa pamoja na kupambana kila wakati. Kwa hiyo mapambano ya mtu binafsi yanapewa nafasi yake katika mapambano mapana na mazito zaidi ya jamii nzima.
Kukata Tamaa
Waandishi wengine wanaonyesha vizuri sana matatizo ndani ya jamii lakini yaelekea kwamba matatizo haya hayatokani na mfumo wa jamii uliojengeka bali hulka za binadamu. Mambo yakiwa hivi, basi hakuna matumaini ya kuleta mabadiliko ndani ya jamii. Dunia ni tambara bovu. Labda tungoje ya mbinguni. Kwa mfano katika Gamba la Nyoka,maisha ya Mambosasa na Mamboleo yanabadilika siku hadi siku bila kueleweka. Inavyoonekana maisha hayana mantiki kabisa: Mamboleo ghafla anapandishwa kuwa Mkurugenzi bila kufanya lolote la maana. Mwenzake anarudishwa kuwa Mwalimu vilevile bila sababu yoyote ya kuonekana tofauti na mwenzake. Mkuu wa Wilaya anakalia barua ya Mambosasa tu bila sababu wakati Mamboleo anapewa ya kwake.
Katika Njozi Iliyopotea kadhalika tunaona jamii na wema katika jamii wakizidi kudidimizwa na mwandishi. Si kwamba tunatakiwa kuona kwamba wema wanashinda kila mara, la hasha, lakini ni kama mwandishi amedhamiria kutuonyesha kwamba maisha ya binadamu ni kuwa mpweke tu. Kiligilo na Mzee Malongo wanaelewana mara moja kwa sababu ya upweke wao, lakini kila Kiligilo akiwa na tegemeo la kuondoa upweke, tegemeo hili linavunjiliwa mbali. Mpenzi wake Losia anadanganywa na mwisho anajiua. Lukova anaonewa kwa mashitaka ya ajabu na baadaye anakufa ghafla kutokana na ugonjwa unaozuka jela. Matumaini ya Kiligilo kwa Tulilumwi yanakatishwa na ukatili wa Katibu Lupituko mpaka Kiligilo anaishia kupata kichaa. Mwandishi anatuonyesha kwamba kweli njozi imepotea kabisa.
Mahubiri
Mara nyingi mwandishi anaamua kufikisha ujumbe wake kwa njia ya mahubiri, ambayo mara nyingine yanapingana na uhalisia. Kwa mfano, katika Mirathi ya Hatari mhusika mkuu anaamua kuwahubiria wachawi palepale ndani ya pango lao. Katika Njama mwandishi anafikisha ujumbe wake sehemu ya mwanzo ya kitabu kwa kutueleza historia yote ya nyuma ya Afrika ya Kusini na sababu ya mapambano – Vero, Sherriff na Willy ambao wote wanajua mambo hayo fika inabidi wahutubiane ili sisi wasomaji tupate ujumbe sawasawa. Hali hii inatokea vilevile katika Pepo ya Mabwege kati ya Josina na Kalenga. Katika Gamba la Nyoka mwishoni, mwandishi anaamua kuingilia kati kuhakikisha kwamba kweli tunaelewa sawasawa. Hatari za hali hii ni kwamba:
Quote:
(a) riwaya hugeuka hotuba na kupoteza nguvu yake ya kutufanya sisi kuona na kusikia kwa namna ya pekee yale yanayojitokeza katika jamii.
Quote:
(b) Huu ujumbe wa hotuba huhitilafiana na ujumbe unaotokana na vitendo vilivyoelezwa awali.
Tamati
Kazi ya msanii, kwa kuwa inagusa hisia zetu zote, ina uwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko makubwa katika urazini na msimamo wa wasomaji. Hivyo wajibu wa mwandishi ni mkubwa. Inafurahisha kuona jinsi baadhi ya waandishi wa riwaya walivyobeba wajibu huu; wamekazana kuakisi na kuelimisha jamii, na kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa.
Hata hivyo, mara nyingi ujumbe na dhamira zao vinaonekana zaidi katika maelezo yao ya wazi mwandishi anapoingilia mwenyewe au kwa kupitia kwa mhusika mmojawapo. Lengo la makala haya limekuwa ni kuonyesha kwamba ili aweze kufanikisha zaidi dhamira anayoikusudia, mwandishi wa riwaya anapaswa kuzingatia zaidi jinsi muundo mzima wa riwaya unavyochangia kutoa ujumbe wake; na iwapo ana nia ya kuwakilisha umma katika maandishi yake yafaa ajichunguze zaidi anaiandikia jamii kwa mtazamo gani na wa nani ili pasiwe na mgongano kati ya ujumbe ulio wazi na ule uliofichika.
Tanbihi
1. Ngugi wa Thiong’o, (1986) Decolonising the Mind. Currey, London, uk. 29 – 30, tafsiri yangu.
2. V. Lenin, (1981) On Literature and Art. Progress Publishers, Moscow, uk. 226, tafsiri yangu.
3. D. Craig (ed) (1975) Marxists on Literature. Penguin, Harmondsworth, uk. 14, tafsiri yangu.
4. E. Fischer, (1969) Art Against Ideology. Braziller, New York, tafsiri yangu.
5. Ngugi, (1981) m.y.k. uk. 6 – 7, tafsiri yangu.
6. D. Brutus, (1978) Stubborn Hope. Heinemann, London, uk. 79, tafsiri yangu.
7. C.S.L. Chachage, (1981) Sudiya Yohana. DUP, Dar es Salaam, uk. 18.
8. C.G. Mung’ong’o (1980) Njozi Iliyopotea. TPH, Dar es Salaam, uk. 28.
9. E. Kezilahabi (1979) Gamba la Nyoka. Eastern African Publications, Arusha, uk. 150.
10. Kezilahabi, (1979) uk. 46.
11. Kezilahabi, (1979) uk. 58.
12. A.E. Musiba, (1981) Njama Continental Publishers, Dar es Salaam, uk.
13. Musiba, k.h.j., uk. 129.
14. Musiba, k.h.j. uk. 170.
15. Musiba, k.h.j. Kwenye jalada la nyuma.
Bibliografia
Balisidya, N. (1981) Shida. DUP, Dar es Salaam.
Brutus, D. (1978) Stubborn Hope. Heinemann, London.
Craig, D., ed. (1978) Marxists on Literature. Penguin, Harmonds worth.
Femia, J.V., (1981) Gramsci’s Political Thought. O.U.R, Oxford.
Fischer, E., (1969) Art Against Ideology. Braziller, New York.
Gugelberger, G., (Mh.) (1985) Marxism and African Literature. Currey, London.
Kavanagh, R.M., (1985) Theatre and Cultural Struggle in South Africa. Zed, London.
Kezilahabi, E., (1979) Gamba laNyoka. Eastern African Publications, Arusha.
Lenin V., (1982) On Literature and Art. Progress, Moscow.
Mung’ong’o, C.G., (1977) Mirathi ya Hatari, TPH, Dar es Salaam.
Quote:
(1980) Njozi Iliyopotea. TPH, Dar es Salaam.
Musiba, A.E. (1981 Njama. Continental, Dar es Salaam.
Mruma I., (1980) Nguzo ya Uhondo. TPH, Dar es Salaam.
Mwakyembe, H., (1981) Pepo ya Mabwege. Longmans, London.
Ngugi wa Thiong’o (1981) Writers in Politics. Heinemann, London.
Quote:
(1986) Decolonising the Mind. Currey. London.

Print this item

  MATATIZO YA UCHAPISHAJI WA RIWAYA
Posted by: MwlMaeda - 08-27-2021, 05:25 PM - Forum: Riwaya - No Replies

Matatizo ya Uchapishaji wa Riwaya

Cleveland Nkata
Nataraji kuchunguza kwa ufupi upeo wa matatizo yanayoambatana na uchapishaji wa vitabu vya riwaya. Makala haya hayawanii kutoa tiba bali kuyakinisha maradhi. Kwa sababu, kwa maana moja shughuli za uchapishaji zina namna ya ubinafsi ndani yake. Kutokana na ubinafsi huo, basi, kila kampuni ya uchapishaji, baada ya muda, huzua namna ya utendaji kazi wake ulioathirika kwa namna fulani na ujuzi, uwezo na tabia ya watendaji wa kampuni hiyo. Hivyo wakati wa matatizo kila kampuni huwa na ufumbuzi unaoonyesha athira hizo za kibinafsi.
Hata hivyo, yapo matatizo yanayoikabili shughuli ya uchapishaji katika ujumla wake. Na kulingana na kuathirika kuliko sawa kunakotokana na matatizo hayo, unakuwepo uelewano, kwa kiwango fulani, kwa wengi miongoni mwa wanaohusika na shughuli za uchapishaji kuhusu namna ya kuyashughulikia baadhi ya matatizo hayo. Nimejaribu kudokeza kwa muhtasari’tu njia ya ufumbuzi wa matatizo haya.
Ili kutoa mwangaza zaidi wa upeo na kina cha matatizo yanayoambatana na uchapishaji wa vitabu vya riwaya, nimeona yafaa kutenganisha matatizo hayo katika mafungu mawili.
Kutokana na asili ya matatizo yanayohusika nimeyaita mafungu hayo matatizo ya kiufundikiutamaduni, na matatizo ya kibiashara. Mafungu haya huingiliana. Masuala ya fedha yanayohusu uchapishaji kama biashara, huathiri sana maamuzi ya awali ambayo mchapishaji hufanya katika ngazi ya kiufundikiutamaduni kuhusu kuchapisha au kutochapisha muswada, maamuzi ambayo hatimaye huihusisha kampuni yake katika majukumu ya kifedha kwa maelfu ya shilingi. Matatizo ya kiufundikiutamaduni yanachukuliwa katika makala haya kama mkusanyiko wa matatizo yote yanayoihusu kazi ya riwaya kutoka mwanzo kabisa wa mawazo ya kuandika mpaka wakati mchapishaji anapomiusisha kampuni yake na uchapisluui wa riwaya hiyo kwa kutia sahihi yake katika fomu ya makubaliano ya mrabaha wa mwandishi.
Katika kuyatizama matatizo ya kiufundikiutamaduni, inalazimu kugusia masuala ambayo awali yanaonekana kana kwamba hayahusiani moja kwa moja na shughuli ya uchapishaji kama inavyoeleweka kikawaida (japokuwa kwa makosa). Mathalani, kwa mchapishaji kuchukulia matatizo ya kutojua kusoma kwa jamii kubwa ya Watanzania yanayotokana na kiwango kidogo cha maendeleo ya utamaduni wa jamii hiyo kama sehemu ya matatizo ya uchapishaji hakuhalisi. Walakini uchunguzi zaidi utadhihirisha kuwa matayarisho ya kielimu kwa jamii yana uhusiano mkubwa sana na masuala ya mawasiliano baina ya mwandishi na msomaji, ambayo bila ya shaka yoyote ndiyo shughuli ya mchapishaji. Kwa upande wa matatizo ya uchapishaji yanayohusiana na biashara, nitayashughulikia zaidi masuala ya mahitaji na utoaji wa vitabu.
Matatizo ya Kiufundi-Kiutamaduni
Kwa muhtasari, mwandishi anapoandika riwaya, uandishi wake huathiriwa kwa kiwango kikubwa na nguvu za kiasili zinazotawala maisha yake kama binadamu, pamoja na namna yeye mwenyewe anavyoyaelewa mazingira yake. Ni namna mwandishi anavyoitikia kisanii miito inayotokana na mazingira yake pamoja na uwezo na kiwango cha ustadi wake kuhusu ufundi na miiko ya sanaa inayohusika ndivyo hatimaye vinavyoathiri sifa za kipekee zilizomo katika muswada anaomkabidhi mchapishaji. Mgongano uliopo katika ngazi hii ni mfano wa mvutano mkubwa unaojitokeza katika ngazi ya uchapishaji unapochukuliwa katika ujumla wake. Mgongano huu upo katika fani ya mvutano kati ya mwonjo wa kisanaa wa mwandishi na mtazamo wake kwa upande mmoja; na kwa upande mwingine, jukumu la mchapishaji kuhusu sifa za muswada aliokabidhiwa na masuala ya fedha yanayohusu uchapishaji, uchapaji na uuzaji wa vitabu, pamoja na matakwa maalumu ya kampuni ambayo mchapisbaji anaiwakilisha.
Yapo maswali kadhaa ambayo mchapishaji hujiuliza kuhusu muswada anaoushughulikia. Mathalani, atapendelea kuwa na uhakika jinsi kazi yenyewe ilivyo kulingana na sifa za kisanaa, hususan, kutokana na maudhui na uwezo wa mwandishi kuwasiliana na hadhira anayoikusudia.
Atapenda kujiridhisha na namna maandishi yanavyoonyesha migongano mbalimbali katika jamii na jinsi migongano hiyo ilivyowasilishwa ikitiliwa maanani matumizi ya lugha, ufundi wa uchoraji wa wahusika na mazingira, mtiririko wa matukio, mtindo na muundo wa riwaya yenyewe. Mchapishaji atataka kuwa na uhakika kuhusu namna muswada unavyotofautiana na vitabu vingine vilivyokwisha kuchapishwa na ambavyo tayari vimo katika maduka ya vitabu, kutokana na uasili na ubora wa mawazo yanayowasilishwa kulingana na dhima ya fasihi katika jamii yetu.
Hatima ya riwaya Bwana Myombekere na Bibi Bugonoka na Ntulanalwo na Bulihwali iliyoandikwa na marehemu Aniceti Kitereza na kuchapishwa na Tanzania Publishing House ni mfano mzuri wa baadhi ya masuala yaliyotajwa hapo juu. Bwana Myombekere na Bibi Bugonoka ni riwaya iliyoathir»wa kwa kiwango kikubwa na hisia za kikulima, si kimaudhui tu bali hata kutokana na mtazamo wa mwandishi.
Riwaya ya marehemu Kitereza ina sifa tele za sanaa zinazotakiwa. Kwa upande wa maendeleo ya historia ya uandishi wa riwaya nchini Tanzania, Bwana Myombekere na Bibi Bugonoka na Ntulanwalo na Bulihwalini hatua muhimu katika historia ya fasihi. Walakini hadithi inayojitokeza juu ya mahesabu ya mauzo ya riwaya hii ni ile ya wasiwasi unaoweza kumpata mchapishaji endapo ataamua kuchapisha kazi ambayo kutokana na umuhimu wa mvuto wake hailingani na hisia ya wale katika jamii wenye uwezo wa kufurahia kazi za fasihi andishi na uwezo wa kununua vitabu. Mauzo ya riwaya ya Mzee Kitereza yanadokeza masuala mengine. Riwaya hii inadhihirisha kutokuwepo kwa tabia ya kusoma miongoni mwa jamii ya wakulima, na kutokuwepo vilevile kwa tabia ya kununua vitabu hasa kwa sehemu za nchi yetu nje ya miji.
Inaelekea kwangu mimi kuwa leo hii mnunuzi wa vitabu vya Tanzania hupatikana sana mijini. Lau kama aghalabu yeye ni kizazi cha mkulima, mtazamo wake wa vitu na mambo huhitilafiana na ule wa wazazi wake. Atbari za mji mimi naziona kuwa zinasaidia kumfanya awe mpokevu wa fasihi andishi. Ni mijini ambako ubinafsi na maisha unapokuwa zaidi. Ubinafsi huu unalingana na ubinafsi katika utamaduni uliozaa riwaya. Sasa kwa mchapishaji tatizo ni namna ya kuitikia hamu ya mwandishi ya kuwasiliana katika fani ambayo kwa sehemu kubwa ya umma wa wakttlima ni utamaduni mpya!
Matatizo ya Biashara
Ili kuelewa asili ya matatizo yanayoambatana na uchapishaji wa riwaya kama biashara, inapasa mtu aelewe japo kidogo tu namna ‘viwanda’ vya utamaduni vinavyofanya kazi yake. Tunazungumzia uchapishaji kuwa mfano wa viwanda vya utamaduni kutokana na shughuli zake muhimu, yaani uchapaji na usambazaji wa vitabu kufanyika kibiashara. Misingi ya maamuzi mengi muhimu huzingatia zaidi fedha kuliko utamaduni.
Sasa kwa Tanzania tatizo kubwa ni lile lililodokezwa hapo awali kuhusu mvutano kati ya sanaa na biashara. Mvutano huu ndiyo sifa kubwa ya viwanda vya utamaduni. Viwanda vingi vya kawaida vinatengeneza na kuuza bidhaa zinazoweza kuwekewa thamani katika masoko bila matatizo yoyote. Viwanda vya utamaduni hufanya kazi yake, kwa kweli katika hali ambayo mahitaji ya bidhaa zake hayaeleweki vizuri. Mwandishi wa riwaya, mathalani, kwanza kabisa huamua kuchukua kalamu yake na karatasi si kutokana na mategemeo ya pesa atakazozipata pindi kitabu chake kitakapouzwa, bali kutokana na msukumo ndani ya nafsi yake unaompa hamu kubwa ya kutaka kuwasihana na wenzake. Lakini hata hivyo shughuli za uchapishaji na kwa hivyo biashara inayotokana na shughuli hizo zinaendeshwa kana kwamba tayari kuna soko lenye nia na uwezo wa kulipia gharama ya vitabu. Madhara makubwa ya uvutano uliopo baina ya uchapishaji kama sanaa na uchapishaji kama biashara ni kwamba kile kinachofikishwa kwenye duka la vitabu si lazima kiwe cha kuridhisha kisanaa.
Kwa hivyo, basi, matokeo ya uchapishaji usio na msaada wa kifedha na ambao unatarajiwa kutii sheria za biashara yanapingana sana na mategemeo ya waandishi wa maana wa riwaya. Kwa msomaji wa kawaida matumizi ya vitabu, hasa vya riwaya, hayana sifa ya kurudiwarudiwa kama vile bidhaa za sukari, mavazi na mafuta ya taa, ambayo huhitajiwa mara kwa mara mpaka mtumiaji anapofariki. Aidha tofauti kidogo tu ikitokea katika kipato cha mnunuzi basi hata ukubwa ama wingi wa manunuzi yenyewe, hususan bid haa kama vitabu vya riwaya, hupungua kwa kiasi kikubwa.
Profesa Breton amelihusisha tatizo la wasiwasi wa biashara unaoambatana na uzalishaji na uuzaji wa bidhaa za kitamaduni na kutorudiwarudiwa kwa matumizi ya bidhaa hizo na athari za mabadiliko ya kipato juu ya wingi wa manunuzi. Mtu anapata picha nzuri zaidi ya tatizo la mchapishaji ukiongeza matatizo mengine kama vile uhaba wa mtaji na urefu wa muda kabla gharama ya kuchapishia haijarejeshwa na kampuni kuanza kupata kijifaida kidogo.
Matatizo ya usambazaji vitaou nayo huwa kipingamizi kikubwa sana kati ya mwandishi na msomaji. Maduka ya rejareja ya kuuzia vitabu ni haba. Na pale yanapopatitcana hayapati vitabu vya kutosha vya kuuza kutokana na uhaba wa mtaji wa kufanyia biashara. Njia za mawasiliano ni mbovu na gharama za kusafirishia vitabu kwa njia ya posta zinakatisha tamaa.
Matarajio ya Uchapishaji
Sharti la msingi kabisa ambalo lazima litiliwe maanani tunapofikiria maendeleo ya shughuli za uchapishaji ni maendeleo ya uchumi wa taifa zima. Muungano wa uchumi na utengenezaji na matumizi ya bidhaa za kitamaduni hauhitaji kuimbiwa nyimbo. Jamii shurti iwe na uwezo wa kujitimizia manitaji yake ya msingi ndipo inaweza kuanza kufikiria masuala ya bidhaa za kitamaduni.
Kuna baadhi ya watu wanaodai kuwa kampuni za uchapishaji sasa hazina uwezo wa kutosheleza mahitaji ya waandishi na wasomaji. Watu hawa wanapendekeza kubadili miundo’ ya kampuni za uchapishaji. Wengine wamependekeza uchapishaji kwa misingi ya ushirika wa waandishi.
Madai hayo ni ya kweli kabisa. Walakini kasoro ipp katika kuzingatia chanzo na asili ya matatizo yanayokabili kampuni za uchapishaji. Ndiyo maana ufumbuzi unaonekana kana kwamba upo katika kubadilisha miundo ya kampuni za uchapishaji.
Ingefaa ieleweke kwamba chanzo na asili ya matatizo yanayokabili shughuli za uchapishaji ni ya kifedha. Nguvu ya matatizo hayo inaongezwa na serikali yetu wenyewe ambayo mpaka sasa haijaona umuhimu wa kuwa na sera madhubuti ya kitaifa katika uwanja wa utamaduni inayoweza kuongoza shughuli za upatikanaji na matumizi ya bidhaa za kitamaduni.
Serikali inawajibika kujihusisha kikamilifu, kuandaa sera maalumu itakayoleta mwamko wa kkamaduni. Tayari serikali imekwishafanya mambo mengi, hasa katika kampeni za kufuta ujinga. Hata hivyo kampeni hizo shurti ziende sambamba na hatua madhubuti za kuendeleza tabia ya kusoma, ambayo bado haipo nchini. Tayari inadhihirika kuwa mafanikio yaliyokwishapatikana katika kampeni za kufuta ujinga yamo katika hatari ya kutoweka kadri idadi ya watu wanaosahau kusoma inavyoongezeka.
Ni mawazo yangu kwamba kinachotakiwa kufanywa ni kwa serikali kuunda sera yenye uhakika ya utamaduni, sera itakayoleta mwafaka baina ya utoaji na matumizi ambavyo kwa sasa vina ukinzani mkubwa katika mahusiano yao. Vilevile serikali itabidi iandae sera hii katika namna itakayosuluhisha mvutano uliopo baina ya thamani ya bidhaa zinazotolewa na ukubwa wa hadhira inayokusudiwa. Kwa maana nyingine serikali iongozwe na madhumuni mawili yaliyofungamana – kupanua uwezo wa janui kupata vitabu, na kuongeza uwezekano wa kitaifa wa kutoa vitabu kwa nyenzo mbalimbali na misaada.
Misaada inaweza kuwa ya moja kwa moja mathalani kwa njia ya misaada ya fedha ama ruzuku. Ama inaweza ikawa ya namna ya kusaidia kununua vitabu vinavyochapishwa. Tunaweza kuiga mipango mizuri ya nchi nyingine, kama vile Norway ambako serikali yao huhakikisha kuwa inanunua idadi maalum ya kila kitabu kilichoandikwa na Wanorway na kuchapishwa na kampuni za Norway. Mpango kama huo upaweza kusaidia kuhakikisha kipato cha mwandishi na kupunguza wasiwasi wa biashara kwa wachapishaji. Zaidi ya hapo mpango kama huo utawezesha kukuza tabia ya kusoma nchini.
Serikali ingeweza vilevile kusaidia kuongeza mitaji ya kufanyia kazi ya wachapishaji kwa kuwa na mpango maalumu ambapo kampuni za ucbapishaji zinashirikishwa kikamilifu, kutokana na uwezo wa kampuni hizo, katika mpango wa kuchapisha vitabu vya kiada kwa shule za msingi na za sekondari, kinyume na ule uliopo hivi sasa ambao kwa kweli ni chanzo cha matatizo zaidi badala ya kuwa ufumbuzi.
Tuzo ni njia nyingine ambayo inaweza kusaidia uchapishaji wa vitabu murua zaidi. Chama cha wachapishaji cha Tanzania (PATA) kilichoanzishwa nchini hivi karibuni kina mpango wa kuanzisha mfuko maalumu utakaotumika kwa ajili ya tuzo za tasihi ili kuleta msisimko kwa waandishi na kuwapa motisha wa kuandika vitahu vya hali ya juu.
Kinyume

Fasihi, Uandishi na Uchapishaji ni matokeo ya Semina ya Umoja wa Waandishi wa Vitabu Tanzania (UWAVITA) iliyofanyika Dar es Salaam tarehe 26 – 29 Oktoba, 1989.
Makala yaliyomo yanahusu maeneo matatu mahsusi ambayo ni, Uandishi, Uhakiki, na Uchapishaji.
Makala juu ya uandishi hayajadili mbinu za uandishi tu, bali yanajadili pia matatizo yanayowapata waandishi wanaoanza, na pia suala la uhusiano baina ya fasihi na jamii, hususan mipaka ya uhuru alio nao mwandishi katikajamii yetu, najinsi gani uhuru huo unaweza kulindwa na kuendelezwa.
Makala kuhusu uhakiki yanagusia mbinu na misingi ya uhakiki, dhima ya uhakiki na vipengele kadhaa vya historia, fani na maudhui ya t’asihi ya Kiswahili.
Mwisho, kuhusu uchapishaji. mvutano mkuhwa kati ya waandishi na wachapishaji unachambuliwa. Mvutano huu unasahahishwa na kushindwa kwa haadhi ya wachapishaji kuwahudumia waandishi ipasavyo. Tatizo hili imedhihirika limekuzwa zaidi na hali ngumu ya uchumi amhayo imeathiri vihaya shughuli za uchapishaji.
Kitahu hiki cha kipekee ni tunu kwa waandishi, wachapishaj! na wote wale wapendao kupata elimu ya vitahuni.
DAR ES SALAAM UNIVERSITY PRESS
ISBN 9976 60 081 x
COVER DESIGN: R.A. MTAWAZI

Print this item

  RIWAYA PENDWA KATIKA FASIHI YA KISWAHILI
Posted by: MwlMaeda - 08-27-2021, 05:17 PM - Forum: Riwaya - No Replies

Riwaya Pendwa Katika Fasihi ya Kiswahili

J.S. Madumulla
Katika miaka ya themanini makini ya mhakiki wa fasihi yameelekezwa au kwa usahihi zaidi, yameanza kuelekezwa kwenye aina ya riwaya ambayo hapo nyuma haikupata kushughulikiwa kwa upana kwa sababu ilikuwa haijajitokeza kwa nguvu. Ijapokuwa dalili za aina hii ya riwaya zimekuwako katika fasihi ya Kiswahili tangu miaka ya hamsini, lakini katika miaka ya themanini riwaya hii imejitokeza zaidi. Hata hivyo, kwa kuwa riwaya hii ni ‘ngeni’ katika Fasihi ya Kiswahili, imekuwa na matatizo kadhaa ya msingi ambayo pindi yakitaaliwa vizuri yanaweza kusaidia kuiainisha na kuibainisha vizuri zaidi. Matatizo hayo ni ya kihistoria, kiistilahi, kifafanuzi, kimawanda, n.k.
Kiistilahi
Mpaka sasa hapajawa na istilahi muafaka ya Kiswahili ya kuliwakilisha neno la Kiingereza la ‘popular literature’ au ‘popular novel.’ Pamekuwa na majina kadhaa kwa ajili ya riwaya hii, kama vile riwaya ya mitaani, riwaya maarufu, riwaya ya taharuki, riwaya ya vijana, n.k. Ijapokuwajina la ‘riwaya pendwa’ ndilo linaelekea kujitokeza zaidi, na ndilo litakalotumiwa katika sura hii, na hata kupendekezwa lipokelewe kuwa istilahi ya aina hii ya riwaya, lakini hapanajina mpaka sasa ambalo limekuwa na mashiko zaidi. Kwa kuiita riwaya hii ‘riwaya ya mitaani’ kutokana na kukosa maduka maalum ya kuiuzia, ni sawa na kuidunisha kama kitu kisichofaa, kitu cha mitaani tu. Hivyojina hilo lisingeisadifu aina hii ya riwaya.
Ingewezekana kabisa kuiita riwaya hii ‘riwaya ya taharuki’ kwani, kama tutakavyoona mbele, sifa moja kuu na ya msingi ya riwaya hii ni hiyo ya taharuki. Lakini tungesita kupendekeza iitwe hivyo kwa sababu si aina hii tu ya riwaya inayotumia kipengele cha taharuki kama mbinu muhimu ya kifasihi na kiujumi. Hivyo jina hilo pia lisingefaa sana. Kisha kuna jina la ‘riwaya ya vijana.’ Ni kweli ikitazamwa kwa haraka inaonekana kuwa riwaya hii ni uwanja wa vijana, hususan katika mashule, miji na vyuo. Lakini uchunguzi wa makini ungeonyesha kuwa, iwe kwa waandishi au kwa wasomaji, riwaya hii imeziteka pia hisia za wasio vijana, licha ya udogo wa idadi yao kwa sasa hivi. Kwa hiyo linabaki jina la ‘riwaya-pendwa.’ Hili linatokana na ukweli kwamba aina hii ya riwaya inapendwa na idadi kubwa ya watu, bila kujali umri wao wala matabaka yao. Huko Ulaya, tayari mwishoni mwa karne ya 18 aina hii ya uandishi ilikwishaingia katika hatua mpya kwa kupata wasomaji wengi waliotoka katika matabaka mbalimbali (H. Foerster na W. Foerster, 1986). Aina hii ya riwaya katika Tanzania inazidi kuziteka hisia za wasomaji wengine, bila kujali umri wala tabaka, na hivyo kulifanya jina la riwaya-pendwa kuwa muafaka kama istilahi yake.
Tatizo hili la istilahi kwa aina hii ya riwaya haliko katika fasihi ya Kiswahili tu, bali hata kwa mataifa mengine. Kwa Wajerumani kuna maneno kama vile “Trivialroman,’ ‘Unterhaltungsroman,’ ‘Kitschroman,’ ‘Abenteuerroman,’ ‘Schundroman,’ n.k. (Woerterbush der literaturwissenshaft, 1986) ambayo yanaelezea vijikondo vya riwaya hii vinavyoingiliana mno kiasi kwamba ni vigumu ama kuona mipaka yao ama kuona ni istilahi ipi ingekuwa bora kuliko zingine, ijapokuwa ‘Kitschroman’ na ‘Schundroman’ tungeziweka katika ngazi ya chini kabisa.
Historia yake
Huko Ulaya aina hii ya riwaya inasemekana kuwa na mizizi yake katika riwaya ya kilimbwende ya kikabaila (romance of chivalry) na riwaya ya unyang’anyi, na vilevile riwaya ya baadaye, yaani karne ya 18, ya kisaikolojia (k.v. Pamela iliyoandikwa na S. Richardson, 1740). Kama ilivyogusiwa hapo nyuma, mwishoni mwa karne ya 18 aina hii ya riwaya ilijitanua zaidi kwa kuwapata wasomaji wengi zaidi na hata wasanii wake kuongezeka.
Katika Tanzania aina hii ya riwaya ililetwa kwa mara ya kwanza katika Fasihi ya Kiswahili na Mohammed Said Abdulla alipoiandika riwaya ya Mzimu wa Watu wa Kale(1957/8). Msanh huyu, yaani Abdulla, inaelekea aliathiriwa na Doyle katika uandishi wa riwaya, na hususan katika mjengo wake. Baadaye katika miaka ya sitini Katalambulla alijitokeza kuendelea na riwaya ya aina hii. Katika miaka ya themanini uandishi wa aina hii ya riwaya uliongezeka maradufu. Madumulla (1988) alidai kuwa ongezeko la riwaya hii katika miaka ya themanini limelazimishwa na kukua kwa mahusiano ya kiuchumi na kijamii ya kibepari ambayo yameilazimishajamii kuyakabili maisha kwa mbinu zinazosadifiana nayo. Mabala (1989) alisema kuwa kuzuka kwa wingi kwa riwaya hii kulionyesha kuzuka kwa namna ya fasihi iliyoendana na mafcakwa ya wakati huo. Tutakipitia tena kipengele hiki huko mbele.
Katika Tanzania na hasa katika miaka ya themanini, riwaya hii ilikuja na sifa moja ya aina yake: haikupitia tena milango ya kawaida ya riwaya iliyozikuta, hasa milango ya kiuchapishaji na kisoko. Milango hiyo ilikuwa imefungwa dhidi yake kwa muda mrefu mno, hivyo waandishi wake wakaanzisha taasisi zao za uchapishaji, baadhi yao zikiwa na uhai wa muda mfupi tu, na walianzisha masoko ya mtaani, waandishi wenyewe wakiwa ni ‘duka la vitabu lijongealo’ na pia wahazini na wahasibu wake wakuu. Sababu ni kwamba vyombo vya udhibiti wa fasihi vilichelea kwamba aina hii ya fasihi iliichupa mipaka ya ujumi wajadi wa mazingira yake, na badala yake iliukaribisha pasi na simile ujumi wa kigeni. Suala la mapenzi, mathalani, katika jadi za Kitanzania, kwa kiasi fulani, na kwa muda mrefu lilikuwa ni suala la faragha. Mambo yanayohusu sehernu za siri, matusi madogo na makubwa, miiko, n.k. ni baadhi ya masuala nyeti ambayo ujumi wa Kitanzania una mkabala wake maalum nayo. Katika riwaya-pendwa mambo hayo yalijitokeza kama ndivyo vikolezo na vivutio vyake.
Kifafanuzi
Arnold (1980) akiifafanua fasihipendwa (popular literature) aliandika:
Quote:
is in the final analysis applied to what people need and often want, and not to what they read because nothing else is available, or what they read because forces opposed to their true prosperity claim they want it.
(hatimaye inahusu kile ambacho watu wanakihitaji na aghalabu wanakitaka, na siyo kile wakisomacho kwa sababu ya kutokuwepo kitu kingine, au kile wakisomacho kwa sababu nguvu ambazo zinapingana na kile ambacho wanakitaka zinadai kuwa wanaldtaka…)
Arnold alikuwa akiizungumzia hali ya fasihi-andishi yenye kulenga umma katika Tanzania ya miaka ya 1970. Hali hiyo aliiona katika vijitabu vya Mazungumzo ya Mchana na vingine vihusianavyo na Mpango wa Elimu ya Ujamaa na Kujitegemea vilivyoandikwa na Msuya katika miaka ya sabini. Ni katika kuangalia uwezekano wa kuenea kwa urahisi kwa vijitabu hivyo miongoni mwa umma, na hasa wale waliojishirikisha kusoma kwa njia ya Elimu ya Watu Wazima na kuuhusisha mpango mzima na itikadi na nadharia za Kijamaa (bila kujali suala la kupokeleka), ndipo tunaweza kuuona uzito wa ufafanuzi na hoja ya Arnold. Vinginevyo kuna maswali ya kujiuliza kuhusu usadifu wa ufafanuzi huo: Je, fasihi ya Msuya ilikuwa na ukubalifu kiasi kikubwa hata kuitwa ‘popular’ (pendwa)? Fasihi ya Msuya inawapa vijana nafasi gani? Aidha inazima kiu ya kifasihi kwa vijana waliomaliza shule za msingi na sekondari kwa kiasi gani? n.k. Zaidi ya hayo fasihi-pendwa iliyopendekezwa na Arnold inazidi kupoteza uzito wake tukitilia maanani kuwa mipango ya Elimu ya Watu Wazima ilizidi kufifia katika miaka ya themanini. Tena fasihi ya Msuya ni vigumu kusemekana kuwa ilisomwa kwa ‘kupendwa,’ ila ni rahisikusemekana kuwa ilisomwa kwa sababu ndiyo iliyokuwepo kama vitabu vya kiada na ziada katika mpango wa Elimu ya Watu Wazima. Kwa jinsi hiyo, fasihi hiyo ina matatizo ya kuitwa ‘fasihi-pendwa’ ya wakati huo au hata baadaye.
Hata hivyo, kama tulivyogusia, ‘upendwa’ aliouzungumzia Arnold wakati huo ulikuwa ni wa kisiasa na kiitikadi ambao unahusiana na ufafanuzi wa Brecht wa ‘kitu-pendwa’ ambacho hakina budi kiwe:
Quote:
Intelligible to the broad masses, adopting and enriching their forms of expression; assuming their standpoint, confirming and correcting it, representing the most progressive section of the people so that it can assume leadership.
(ni chombo kinachoeleweka kwa umma; kikizipokea na kuzitajirisha namna zao za kujieleza; kikiuchukua, kuuthibitisha na kuusahihisha msimamo wao; kikiiwakilisha sehemu ya kimaendeleo (zaidi) ya watu, ili hatimaye iweze kuuchukua uongozi).
Arnold alifikiria hivi kutokana najinsi fasihi hiyo ilivyoanzishwa na kusambazwa, ijapokuwa ilikuwa bado kuzitimiza sifa za ufafanuzi huu. Muda wake wa kuitwa ‘fasihi-pendwa’ ulikuwa bado sana.
Mabala (1989) baada ya kuitalii aina hii ya riwaya pamoja na tahakiki zake chache ambazo zilikuwa zimejitokeza hadi hapo, aliona kwamba aina hii ya riwaya ilibainishwa na wahakiki kwa namna isiyokubalika vizuri kama ifuatavyo:
Quote:
Popular literature is that which has been produced by the non-literate who do not belong to the academic establishment and therefore are unsophisticated. By the same token, serious novels are written by members of academic establishment who are colleagues of the critics thus making it easy for their seriousness to be recognized. Thus ‘popular’ carries a pejorative meaning which explains the resentment of the writers branded as popular…
(Fasihi-pendwa ni ile ambayo imeandikwa na wasio wasomi ambao hawamo katika taasisi za kitaalam na kwa hiyo si weledi. Hali kadhalika, riwaya-dhati zimeandikwa na watu wasomi ambao ni wenzao na wahakiki. Uhusiano huu unafanya udhati wa kazi zao ujulikane. Hivyo neno ‘pendwa’ lina maana hasi ambayo inachukiwa na waandishi wa aina hiyo ya fasihi…)
Kwa mtazamo huo, Mabala anadhani kuwa kuiona aina hii ya fasihi kwa namna hiyo kuna kasoro, kwani vigezo vyake haviko katika maudhui na fani za fasihi hiyo bali katika ‘utu’ wa waandishi.
Aidha Mabala anaendelea kusema kuwa waandishi wa aina hii ya fasihi, hasahasa ni vijana ambao bado wangali wakijifunza sanaa hii huku wakiwa wameathiriwa na jamii ambamo wanaishi, na ambao wamejaribu kulitafutia jibu tatizo kubwa la uhaba wa vitabu vya kusoma kwa wakazi wa mijini. Wameonyesha mwamko unaogusa wa kushughulika na masuala muhimu ya kijamii na wanayatetea maandishi yao hata dhidi ya uhakiki wa kirasimu wa miaka ya themanini. Aidha Mabala anaona ni vigumu kuitenganisha riwaya-pendwa kutoka kwenye riwaya-dhati. Ndiyo maana anahitimisha kuwa riwaya-pendwa ni aina mpya ya fasihi ya mjini ambayo inasomwa kwa upana na vilevile inavibainisha vipengele vya kimaendeleo vya utamaduni wa umma.
Kwa kuwa ni vigumu kuitenganisha riwaya-pendwa na riwaya-dhati, Mabala hakujaribu kueleza tofauti zao kimaudhui au kifani. Hii inawezekana kuwa mhakiki huyu alielemea zaidi katika kuitetea nafasi ya mwandishi wa riwaya-pendwa ili ainuliwe kufikia kiwango cha mwandishi wa riwaya-dhati katika hadhi ya usanii. Suala hili ni la msingi kisanii:na limeanza kusemewa tayari (Madumulla, 1988). Pamoja na ugumu wa… kutenganisha riwaya-pendwa na riwaya-dhati, ingefaa hata hivyo tuone ni vipi ufafanuzi na sifa zake vinaweza kuangaliwa, na vipi makundi haya mawili tunaweza kuyatenganisha.
Katika lugha ya Kijerumani kuna aina ya fasihi/riwaya inayoitwa Unterhaltungsliteratur (inayoweza kufasiriwa kisisisi kama fasihi ya kuburudisha). Hii inakaribiana sana na fasihi-pendwa. Foerster na Foerster (1986) wanaifafanua kama:
Quote:
zusammenfassende Bezeichnung fuer massenwirksame, vor allem erzaehlende Literatur mit ausgepraegter Unterhaltungsfunktion und entsprechenden eigentuemlichen Strukturen und Themen….
(Ni ufafanuzi unaokusanya pamoja fasihi, hususan za kinathari, anibazo zinapendwa kwa mapana sana, zikiwa na dhima hayana ya kuburudisha, na ambazo muundo na dhamira zake ni vya pekee…)
Wanatahadharisha kuwa katika ufafanuzi huu, lazima kutofautisha kati ya kuburudisha kwajumla kunakoweza kujitokeza katika fasihi yoyote ya kisanaa na ile dhima maalum ya kuburudisha ambayo imo katika kazi na tanzu za fasihi ya kuburudisha yenyewe (au fasihi-pendwa) ambamo hali ile ya kufurahisha imepewa nafasi ya mbele katika mahusiano ya ujumi na muundo wa hadithi. Mambo muhimu yanayojitokeza katika fasihi ya namna hiyo ni pamoja na:
Quote:
– kiasi kikubwa cha taharuki na utendaji
– mtiririko unaofuatika wa wahusikana matukio
– Mhusika mkuu ni mhusika-mkwezwa
– dhamira zakezinapendwa na wengi
– mandhari yameundwa kwa namna ya pekee
– mtindo ni rahisi uliotumia lugha ya kila siku
– kuenzi jinsi ya kike kama chombo cha anasa, na uhalifu.
Zaidi ya hayo, katika aina hii ya fasihi kuna uwezekano wa kubeba dhima nyingine za kimawasiliano, kimaadili, kisiasa, licha ya dhima kuu ya kuburudisha. Aidha fasihi hii, kama ilivyo fasihi-dhati, ina viwango mbalimbali vya usanii, na wasomaji wake wanatoka katika matabaka mbalimbali.
Zilizoonyeshwa hapo juu ni sifa za fasihi-pendwa kwa jumla. Riwaya-pendwa ya Kiswahili ina sifa hizo pamoja na nyingine chache ambazo ni:
Quote:
– uigaji wa mawazo na, mara nyingine hata matendo kutoka kwenye fasihipendwa za nchi zilizoendelea
– upangaji wa haraka wa mtiririko wa matukio kiasi kwamba sehemu zingine zinakosa upatanifu na mantiki
Katika sifa hizo zote zilizotajwa na zisizotajwa za riwaya-pendwa sifa za taharuki na utendaji ndizo zinachukua nafasi muhimu zaidi. Waandishi wamejitahidi kutumia mbinu ya misukumo-pofu kadhaa ili kuvichelewesha vilele katika masimulizi yao. Katika ucheleweshaji huu ndimo ambamo ufundi wa mwandishi unajibainisha katika kuvisuka visa visivyomchosha msomaji, ufundi wa kuwaokoa wahusika wanaokandamizwa na sheria kwa knonewa na kuwaonyesha walikojificha wahalifu. Mifano iko kadhaa. Vitabu karibu vyote vya Mohammed Said Abdulla vinaonyesha jinsi Inspekta Seif anavyotuongozea kwenye misukumo-pofu. Anatupeleka kwa wahusika wasio na hatia ambao, kwa mantiki yake yeye inspekta, wanaonekana kuwa wahalifu. Lakini misukumo-pofu hii inakuja kuwekwa sawa na Bwana Musa ambaye anaonyesha dosari za Inspekta Seif. Katika kufanya hivyo anaturejesha kwenye msukumo mkuu. Pale tunapofika tu kwenye msukumo mkuu tunapambana na kilele ambacho kinatuongozea kwenye suluhisho, au ‘peripetie’. Vitabu vya Katalambulla na Musiba vinaelemea kwenye mkabala huu. Au kwa kifupi, masimulizi yote ya kipelelezi yametumia mbinu ya misukumo-pofu katika ujenzi wa taharuki ndani ya mtiririko wa matukio yao.
Ijapokuwa dhima muhimu ya riwaya-pendwa ni kuburudisha, lakini kazi hizo haziko katika kiwango kimoja tu cha usanii. Kutofautiana huku kwa viwango vya usanii ndiko kunazifanya kazi hizi ziweze kupangika katika aina kadhaa.
Aina za riwaya-pendwa
Mapema tumeona kuwa Mabala anaelekea kudai kuwa waandishi wa riwaya-pendwa wameelezwa na wahakiki wa fasihi kuwa si wasomi, na maandishi yao hayana weledi. Hali kadhalika, waandishi wa riwaya-dhati ni wasomi na wametetewa na wahakiki kwa sababu ni wasomi wenzao. Vingincvyo, aonavyo Mabala, hakuna tofauti kati ya riwaya pendwa na dhati.
Lakini ukweli ni kwamba wengi wa waandishi wa riwaya-pendwa ni wale waliosoma kufikia Sekondari; na katika waandishi wa riwaya-dhati baadhi yao wana elimu ya Chuo Kikuu. Wengi wa waandishi wa riwaya-pendwa hawana kazi maalum isipokuwa uandishi. Na huenda wamefanikiwa kuanzisha miradi fulani baada ya kupata mtaji kutoka kwenye maandishi yao. Suala hili ni la msingi. Hili ndilo linaloonyesha kwanmi riwaya-pendwa imefurika. Kwa sababu inawaruzuku na kuwakimu waandishi wake. Tena imekuwa muhimu zaidi katika miaka ya themanini ambayo matatizo ya kiuchumi yamezidi. Hili linaeleza vile vile sababu ya kuwepo kwa sifa za nyongeza zilizogusiwa awali katika riwaya-pendwa ya Kiswahili. Kwa upande mwingine, wengi wa waandishi wa riwaya-dhati ni watu wenye kazi zao tayari. Hivyo uandishi ni kazi ya ziada kwao. Hapa haina maana kwamba waandishi wa riwaya-dhati hawapendi fedha. Tunaangalia suala la jinsi maudhui na fani vinavyomudiwa. Inawezekana kwamba katika uandishi wa kazi zao wanajipatia muda wa kutosha wa kuyapanga mawazo yao, na elimu yao pia inawasaidia katika ufuaji na uchanganyaji wa sanaa, maudhui, lugha, uhalisia, falsafa, n.k. Waandishi wengi wa riwaya-pendwa wameanzisha taasisi za uchapishaji na namna yao ya masoko wakilazimishwa na hali halisi ya maisha. Hali hiyo ya maisha ndiyo inayoyalazimisha na kuyadhibiti hata maudhui ya kazi zao. Hata hivyo, mtazamo huu hauhalalishi au kuweka sheria kuwa kila kazi inayoandikwa na ‘msomi’ ni ya dhati, na nzuri, na zile zinazoandikwa na wengine ni ‘fasihi-pendwa’ na chapwa. Mtazamo huo hauna mantiki, ni mtazamo wa kimhemuko. Badala yake, pawepo na bidii za kuitalii na kuifahamu zaidi riwaya-pendwa. Kazi hii ni kichocheo cha utafiti huo.
Kwa ujumla, riwaya-pendwa ya Kiswahili inaweza kuangukia katika aina tatu. Ya kwanza ni aina ya Abdulla. Aina hii sifa yake kubwa ni ya upepelezi na uchanganuzi wa kadhia kwa kutumia mantiki au fomula maalum. Kunaweza kuwa na uhalifu au dhuluma katika mtiririko wa matukio. Polisi wanajitahidi kulitatua tatizo lakini wakati mwingine wanashindwa. Hivyo katika visa vingine msaada wa mpelelezi binafsi unatakiwa. Aina ya pili ni ya Musiba. Sifa kuu ni ya upelelezi na kupambana na majambazi na majasusi kwa kutumia nguvu. Hapa kunahitajika mhusika mkuu anayeweza kufikiri haraka haraka, kutumia silaha na viungo vya mwili kwa ustadi katika vipindi vya dhiki na raha. Mhusika mkuu ni bingwa wa kufikiri na kutenda na mara nyingine anafanya makosa madogo madogo yanayomwingiza katika majaribu ambayo hatimaye atayashinda. Hapa upelelezi na mapenzi vinakwenda pamoja. Inaelekea kama wapelelezi wakubwa ni wajuzi au ‘wachezeaji’ wakubwa wa mapenzi pia. Kipengele hiki kinachangia sana katika kuidhalilisha aina hii ijapokuwa inaweza kuwa imebeba dhamira nzito zinazoigusa sana jamii ya wakati huu. Aina hizi mbili zina uigaji wa hali ya juu wa riwaya-pendwa za nchi zilizoendelea, k.v. kivazi, vifaa, vijitabia fulani, namna ya lugha, n.k. Hii inathibitisha tu jinsi waandishi wetu walivyo wachunguzi wepesi kuhusu mambo yanayofanyika katika sehemu nyingine za dunia. Na jinsi gani wanayachambua na kuyapokea na kuyatumia mambo hayo kwa manufaa ya mazingiria yao ni jambo ambalo tayari limo katika majadiliano baina ya wanafasihi.
Aina nyingine ya riwaya-pendwa ni ile ya Mbunda Msokile. Riwaya hii imesukwa kwa namna ambayo imeelemea kwenye riwaya-dhati, hususan kwa maadili yake na, kwa kiasi fulani, uwiano kati ya wahusika na uhalisia. Hata hivyo kazi za aina hii zinaingizwa kwenye riwaya-pendwa kutokana na kuitilia mkazo mno dhima ya kuburudisha na kuzishughulisha zaidi hisia za huruma au chuki za msomaji badala ya mchangamano wenye kuwiana wa hisia, tafakari na mantiki. Katika aina hii kwa kawaida upelelezi haumo. Pindi uhalifu unapotokea polisi na njia nyingine za kisheria zinatumika.
Mawanda ya riwaya-pendwa
Mawanda makuu ya riwaya-pendwa ni uhalifu (wizi, uuaji, ujambazi, dhuluma, unyang’anyi, uporaji, n.k.), mapenzi, ujasusi na upelelezi. Kwa riwaya-pendwa za zamani kipengele cha jasira (adventure) kilikuwa ni muhimu pia. Migogoro mikubwa na midogo, misukumo-pofu na mikuu imejengwa kwa kujiduru katika mawanda haya. Masimulizi mengi ya Muhammed Said Abdulla yanahusu uhalifu (dhuluma na mauaji) na upelelezi. Yale ya Musiba yanahusu ujasusi, upelelezi na mapenzi. Ya Simbamwene ni uhalifu wa aina nyingi kidogo, mapenzi na upelelezi, n.k. Ijapokuwa tunajaribu kuyatenganisha hivi, lakini katika kusoma riwaya mbalimbali za aina hii inajibainisha kuwa kuna mwingiliano mkubwa baina ya aina hizi.
Fani: Namna ya jumla ya uandishi wa riwaya-pendwa:
Msomaji makini wa riwaya-pendwa atagundua kuwa waandishi wake wameweza kuchapisha sanjari ya vitabu kadhaa kwa kipindi kifupi tu, na bado wanakuwa na uwezo wa kuendelea kutoa sanjari nyingine. Hii inatokana na namna fulani ya kanuni ambayo inafuatwa katika uandishi wao. Kanuni hii tutaiita ‘topo’. Kuna topo la kimaudhui ambalo linayachunga mawanda ya dhamira wanazoziandikia waandishi. Mathalani, Abdulla akichungwa na topo la kimaudhui, ameendelea kuandika sanjari za vitabu kuhusu uhalifu na upelelezi. Kisha kuna topo la kifani ambalo linazichunga mbinu za kuyaandikia maudhui. Msuko wa malukio, matumizi ya misukumo-pofu, ujenzi wa peripetie, suluhu, ni vipengele ambavyo, kimsingi, havibadiliki sana. Hii inathibitishwa na matumizi ya wahusika wakuu walewale katika sanjari nzima ya vitabu. Vilevile mwandishi anajitahidi kujenga uhusiano kati ya kitabu chake kipya na kile cha nyuma kwa kumrejesha msomaji kwenye matukio fulani katika vitabu vilivyopita (Abdulla, Simbamwene, Musiba, n.k.). Waandishi wamefanya hivyo ili kuonyesha mwendelezo wa matukio kwamba wanafanya hivyo si kwa bahati nasibu tu, bali kwa makusudi mazima.
Katika kuandika riwaya kisanjari kwa mbinu za wahusika wakuu walewale na urejeshi wa matukio fulani, waandishi wameifanya kila riwaya katika sanjari ionekane kama tuko (episode) moja linalojitegemea katika mfululizo wa matuko. Hii imemwezesha mwandishi mmoja kutoa matuko (episodes) mengi katika kipindi kifupi. Hata hivyo aghalabu matuko hayo yamekuwa ni mafupi mno, tena yaliyosanwa kwa kuharakishwa kiasi kwamba upatanifu wa matukio umekuwa na uchapwa fulani, hususan katika ujenzi wa msuko wa matukio na wahusika.
Athari za riwaya-pendwa kwa jamii
Riwaya-pendwa, kwa vyovyote vile, ina nafasi yake katika jamii. Ikiwa ina nafasi yake ina wajibu pia, ijapokuwa kupokeleka kwa wajibu huo ni suala la kujadiliana. Mabala anaandika.
Quote:
..Just as people’s culture is a mixture of progressive elements and ruling class mystifications, ignorance and obscurantism, the popular novels reflect the mixture as a whole both in the characters and settings and in the philosophy of the authors writing them. Almost without exception, the novels expound lumpen bourgeois and proletarian values which have’ so influenced urban dwellers throughout Tanzania.
(Jinsi utamaduni ulivyo mchanganyiko wa mawazo ya kimaendeleo na ya tabakatawala ambayo yanakanganya na kupotosha, ndivyo riwaya-pendwa zinavyoaldsi mchanganyiko (huo) mzima katika wahusika na mandhari na katika falsafa za waandishi wake. Karibu riwaya- (pendwa) zote zinaelezea amali za kibepari na kijamaa ambazo zimewaathiri wakazi wa mijini wa Tanzania nzima).
Hivi ndivyo riwaya-pendwa inavyoonekana kwa mhakiki mmojawapo. Je, wasomaji wengi wanaiona hivyo? Hata hivyo, linalosisitizwa ni lile lililogusiwa tayari hapo nyuma, kwamba dhima ya msingi ya riwaya-pendwa imekuwa ni ile ya kuburudisha. Kuna baadhi ya dhima ambazo zinaweza kujitokeza bila makusudio wala matazamio ya mwandishi. Huenda hoja ambayo inachukuana kwa namna fulani na dondoo la hapo juu ni ile ya Madumulla (1988) kwamba:
Quote:
– riwaya-pendwa imejitokeza katika miaka ya themanini kutokana na kustawi kwa mahusiano ya kibepari. Ni fasihi ambayo haifumbati tu uozo wa kibepari, bali pia ni zao halisi la uozo huo.
– riwaya-pendwa imejitokeza kwa wingi si kwa lengo la awali la kuziba pengo la upungufu wa maandishi ya kifasihi, bali kwa lengo la awali la kujikwamua kiuchumi.
– riwaya-pendwa inadhihirisha kiasi gani fasihi-pendwa ya kigeni ilivyoathiri mawazo ya kisanii ya waandishi wetu.
– riwaya-pendwa ni matokeo ya mwigo ambayo yameathiri uasili wa waandishi wetu katika ubunaji kimaudhui na kifani.
Baadhi ya wahakiki wamedhani kuwa fasihi-pendwa ni mwendelezo wa maandishi na filamu za magharibi za uhalifu, mapenzi, ugaidi, ujasusi na upepelezi. Wasomaji wengi wameifanya riwaya-pendwa kama kibadala au kijalizo cha filamu. Katika Hofu, kwa mfano, Musiba tayari amempeleka mhusika wake mkuu, Willy Gamba, Japani ambako amesomea mbinu za kupigana za kininja. Katika mapambano dhidi ya majasusi, Willy Gamba anakutana na maninja wenziwe ambao walikuwa pamoja kwenye mafunzo huko Japani. Wanapopigana, wanafuata sheria za kininja. Katika Hofu mada kuu inahusu ukombozi kusini mwa Afrika, na riwaya za Musiba zingesaidia sana kuwaamsha watu na kuwajuvya kuhusu suala hilo. Lakini lililowekwa mbele ni uhodari wa wahusika wakuu katika kutenda: Katika kuwindana, kupikuana kwa maarifa, kupigana kwa silaha na mikono mitupu na kufanya mapenzi. Mada ya ukombozi inafuatia nyuma ikinyemelea kwa mbali. Watu wanaosoma mikasa wanafikiria zaidi vipi Willy Gamba atawamudu maadui zake kuliko vipi na lini ukombozi utakamilishwa. Kwa sababu ukombozi ‘hauonekani’, kwani umefichwa na utendaji, kwa hiyo mada hiyo nzito inakuwa ni ‘kiziba macho’ tu cha vyombo vya udhibiti na wala hakina athari au uzito wowote, ila kidogo mno ndani ya kichwa cha msomaji. Aidha kiujumi na utendaji unaojitokeza humo unaziteka nafsi za wasomaji wengi; na wanalitazamia kwa hamu andiko lijalo la mwandishi kama Musiba.
Hitimisho
Katika mahusiano ya miaka ya themanini ya kijamii, ingekuwa vigumu kwa Tanzania kutokuwa na fasihi-pendwa, kwa sababu ya kuwepo kwa mazingira maridhawa kwa ajili ya fasihi ya namna hiyo. Je, iendelee hivyohivyo? Mpaka lini? Maswali ni magumu. Hata hivyo, kiwango ilichonacho riwaya-pendwa ya Kiswahili kinalilia kuboreshwa. Ingawa ni mwigo wa akina Doyle, Christie, Flemming, Robbins, Chase, n.k. lakini ukomavu wa waigwa haujafikiwa, hususan katika msuko wa matukio, ujenzi wa wahusika na mandhari, n.k.
Licha ya dhima kuu ya kuburudisha, riwaya-pendwa inaakisi, bila kukusudia, hali halisi ya Tanzania ya wakati wa riwaya hiyo hususan katika mahusiano ya kijamii na kiuchumi. Riwaya-pendwa ingeweza kujipatia dhima kubwa zaidi kwa kuyaweka makusudi yake makuu si, katika kuburudisha bali katika kuchochea fikra za kimaendeleo, za usawa wajinsi, za ustawi wajamii, n.k. kwa wasomaji wake. Dhima ya kuburudisha iende sambamba na masuala hayo.

Print this item

  UCHAMBUZI WA KIFANI KATIKA RIWAYA
Posted by: MwlMaeda - 08-27-2021, 05:10 PM - Forum: Riwaya - No Replies

Uchambuzi wa Kifani Katika Riwaya

S.A.K. Mlacha
Uchambuzi wa kifani katika kazi ya fasihi ni njia moja ya kuielewa kazi ya fasihi. Fani ni aina ya uchambuzi ambao hujumuisha sehemu zote zinazoiunda kazi ya fasihi na kutokea kuwa mkusanyiko ambao unaweza kuonyesha upekee wa maandishi ya mwandishi mmoja. Kujua fani husaidia kujifunza na kuifahamu kazi moja ikihusiana au kufananishwa na nyingine hasa kwa vile huzingatia lugha, dhamira, wahusika, umbo la kazi hiyo na sehemu nyingine. Kwa sababu hii pia, fani husaidia kuielewa kazi moja kwa undani zaidi. Sehemu hizo tofauti za kazi ya fasihi huchunguzwa kwa mwingiliano unaokubaliana kulingana na kazi hiyo ilivyoundwa.
Sura hii itazingatia uchambuzi wa kifani wa riwaya na tutajikita hasa katika riwaya ya Bwana Myomhekere na Bibi Bugonoka. Tutazingatia fani ya kifasihi, ambayo kwa kiasi kikubwa ni upanuzi wa uchambuzi na uhakiki wa kazi yote ukizingatia dhamira, wahusika na muundo. Aidha hapa tutaangalia fani ya lugha ambayo itazingatia miundo ya lugha na uhusiano wa maneno yaliyounda lugha ya mwandishi, jinsi maneno hayo na lugha iliyotumika inavyokidhi haja za fani ya kifasihi na sehemu zake.
Katika uchambuzi wa fani kifasihi ni muhimu tuelewe kwamba fasihi huvuka mipaka ya wakati na mahalt ili kutoa kauli zinazohusu binadamu na matendo yake, tabia na maisha yake. Riwaya ya Bwana Myombekere na Bibi Bugonoka (kuanzia sasa BMBB), kama kazi ya fasihi, inatupatia ujuzi mpana unaohusu watu wengine, utamaduhi mwingine na pia kutupatia uwezekano wa kufikiria kuhusu sisi wenyewe na shughuli zetu. Kama kazi nyingine ya fasihi, riwaya hii inatupa nafasi ya kuweza kuwa mahali pamoja kimawazo na binadamu wengine. Kwa hali hiyo basi, uchambuzi wa kifani wa riwaya hii utazingatia wakati uliopita, uliopo na hata ujao na vilevile kuangalia riwaya hiyo ndani na nje ya mipaka ya utamaduni au jamii iliyozingatiwa. Ili kwenda nje ya mipaka hiyo miwili tunaweza kuiangalia dhamira kuu inayojitokeza kwenye riwaya ya BMBB kuona ni vipi uchambuzi wa kifani wa dhamira unaweza kutupatia mwanga zaidi.
Dhamira, ikiwa ndilo wazo kuu linalotenda au kujitokeza katika riwaya nzima, huashiriwa na mfululizo wa vijiwazo vinavyoweza kuoanishwa na kuunganishwa kutoa wazo moja. Vijiwazo hivyo hujitokeza katika kila sehemu inayoikamilisha riwaya; iwe ni wahusika, muktadha, maneno au hata mazingira. Ni uhusiano baina ya dhamira na sehemu zingine ambao huashiria fani iliyotumika na pia nafasi ya fani hiyo katika kuikamilisha kazi hiyo. Kama asemavyo Geoffrey Leech (1970:125) kunakuwa na “uhusiano wa kimshikamano unaotoa kidokezo cha ufafanuzi wa kazi hiyo.” Kwa maneno mengine ni kama wavu uliojengwa kwa sehemu tofauti za kazi ya fasihi (kwa mfano riwaya). Katika riwaya ya BMBB dhamira kuu inayojitokeza ni unyumba. Riwaya hii imeliangalia swala la unyumba kwa kutumia mila na desturi za Wakerewe (Mlacha:1988). Riwaya nyingi za Kiswahili zimeligusia swala la unyumba kwa namna tofauti lakini tofauti kubwa baina ya riwaya hizo na hii ya BMBB ni ile ya kifani kuliko kimaudhui au muktadha. Hata hivyo, tofauti kubwa zaidi ambayo imejumuisha fani, maudhui na muundo ni ile aliyoitumia mwandishi wa riwaya hii kwa kuitumia familia moja (ya mke na mume) ambayo imo ndani ya jamii. Familia hii, katika ufinyu na upana wake imezingwa na jamii ambayo imehusishwa kikamilifu katika maisha ya Myombekere na Bugonoka na swala hilo la unyumba. Ni kutokana na muundo huu ambapo tunaiona riwaya ikiwa katika mshikamano wa kimkufu. Hii ina maana ya kwamba tukio moja linahusiana na jingine na kutegemea tukio jingine ili kukamilika. Wahusika vile vile wapo kwenye uhusiano wa kutegemeana na kukamilishana kulingana na dhamira kuu ya hadithi hii.
Katika uchambuzi wa kifani lugha huchukua nafasi kubwa. Hii inatokana na kufahamu kuwa lugha ndiyo inayotumika kuiunda kazi hiyo na kuwajenga wahusika ambao ndio wabebaji wakuu wa mawazo ya mwandishi. Nafasi ya lugha katika uchambuzi wa kifani inaweza kuonekana katika pande mbili. Upande wa kwanza ni ule ambapo lugha hutumiwa ili kuifanya kazi ya fasihi ivutie zaidi na iwe ndio chombo cha kuifanya kazi hiyo iwe nzuri. Upande wa pili ni pale ambapo fasihi nayo huchangia kuikuza lugha ingawa fasihi hiyo imetokana na lugha. Uhusiano huu wa kutegemeana tutauangalia kwa makini katika uchambuzi wetu hapo baadaye.
Lugha hutumiwa ili kuifanya kazi ya fasihi ivutie, ikiwa ni pamoja na kuifanya kazi hiyo iweze kueleweka, kwa msomaji. Malengo haya huandamana na lengo la kuburudisha, kigezo ambacho kimeonekana ni muhimu pia kwa wasomaji. Malengo haya yote yanaweza kufikiwa kutokana na mpangilio wa maneno na uundaji wa sentensi. Aidha uteuzi wa maneno na kauli na pia namna wazo lilivyojengwa ni njia nyingine. Katika riwaya hii Aniceti Kitereza ameweza kutunga hadithi ndefu ambayo imejengwa kutokana na lugha inayoweza kuchambuliwa chini ya misingi hiyo. Kazi hii inaweza kueleweka vizuri iwapo msomaji anaweza kuzingatia maisha ya Bwana Myombekcre yanavyokwenda siku baada ya siku na matukio yote yanayotokea. Lugha iliyotumika m nyepesi na inayoeleweka. Paleambapo anatumia maneno ambayo siyo ya Kiswahili amejitahidi kuyaelezea kwa Kiswahili sanifu ili kumpa msomaji picha karnili ya wazo lililofumbatwa katika neno hilo. Kwa mfano:
Quote:
Kwa kuwa yeye alikuwa Omugimba, yaani mletamvua na alikuwa anataka mbuzi mweusi yule wa kutoa sadaka kwa sababu ya mvua …. (uk. 417)
Hapa mwandishi amefafanuamaana ya neno omugimba na kumfanya msomaji asiyejua lugha hiyo aipate picha kamili. Kwa wale wanaolifahamu neno hilo kifungu hiki kinawapeleka kwenye picha kamili zaidi na hivyo kuyakaribia mazmgiraya hadithi. Maneno mengine mwandishi ameyaacha kwenye mabano au bila kuyafafanua ndani ya hadithi. Badala yake ameyachukua maneno haya na kuyapa ufafanuzi mwishoni mwa kitabu kwa mfano:
Quote:
lakini huyu ni mnyama mkali (ekikaka) haliwi kamwe na Abakerebe (uk. 487)
Nerio ekikaka limetafsiriwa mwishoni (uk. 597) kama dude, mnyama mkali anayetisha; nduli nk. Matumizi ya maneno ya Kikerewe katika hadithi hii yamekuwa na umuhimu sana katika kuielewa hadithi. Ni maneno ambayo yanaelezea vitu ambavyo vinaelezea utamaduni wa Wakerewe na ambavyo vinaweza kueleweka na kuvutia wasomaji wa jamii hiyo na pia kuwaelimisha waleambao wanatoka kwenye jamii zingine. Huu ni uandishi Pekee kifani katika uandishi wa Kiswahili lakini si uandishi mgeni katika fasihi. Waandishi mashuhuri kutoka Afrika Magharibi kama vile Chinua Achebe, Wole Soyinka na wengine wameutumia vile vile na kufanikiwa kuufikisha ujumbe kwa undani zaidi.
Matumizi ya fani ya aina hii katika uandishi wa riwaya yanaweza kurahisisha kufuatilia wazo na kuona namna lilivyojengwa. Hatari yake ni kuwa na maneno au kauli zinazojenga wazo hilo lakini zinaonekana kama zinapingana. Nitafafanua zaidi hapa. Maneno hayo ambayo sio ya Kiswahili yanaweza kuchukuliwa kama yalivyo na kueleweka hasa kama yamerudiwarudiwa baada ya kufafanuliwa, kwa mfano:
Quote:
Pale tena ndipo pakawa kivumbi, wale walaji wa nyama mbichi, iitwayo obubisi, wakafuata wakiwa na uchu mwingi, hata watu wazima na wazee pia wakajongea karibu wapate kula obubisi (uk. 37.)
Katika ukurasa huo wa 37 neno obubisi limerudiwa sana (mara nane) licha ya kuwa limetumiwa tena baadaye. Hata hivyo, maana yake hasa sio nyama rnbichi tu ba1i ni nyama inayoliwa ikiwa mbichi. Kwa hali hii mtunzi ametumia neno obubisi kuweza kumfanya msomaji aweze kufuatilia wazo kirahisi hata pale ambapo sentensi yenye neno hilo imeundwa visivyo kama vile:
Quote:
Mke wa pili aliwaletea majt ya kuoshea utumbo, na vingine villvyobaki, yaani visivyoliwa obubisi katika nchi ya Bukerebe. (uk. 38.)
Hali iliyokuwa inasisitizwa hapa ni ya nyama za aina fulani ambazo haziliwi zikiwa mbichi na sio kila kitu. Hata hivyo, jambo muhimu hapa ni kwamba uteuzi wa neno hilo na mpangilio wa sentensi zake ambazo zina neno hilo kifani huashiria msisitizo wa kile anachokizungumzia. Wakati mwingine, kama ilivyoonyeshwa awali, uteuzi na mpangilio huo wa maneno unaweza kuachana na miundo na hata matumizi ya kawaida katika lugha. Mtindo huo huwa na umuhimu sana katika kuichambua fani ya kazi ya fasihi au kazi za mwandishi mmoja.
Jambo moja la kusisitiza hapa ni kwamba mara nyingi maneno yote ambayo si ya Kiswahili yamepewa nafasi maalum katika sentensi. Mara nyingi maneno hayo hujitokeza kabla ya kituo kikubwa au kidogo au karibu sana na vituo hivyo. Hii kifani inaweza kuangaliwa kama sehemu ya ‘mapumziko’, baada ya wazo kuu kujengwa na kumaliziwa na neno hili na hivyo kurahisisha kueleweka neno hilo. Kwa mfano:
Quote:
Munegera akarudi kule kwa Kalibata pamoja na vipande vya miti ya migazu alivyoviweka kwa wakati ule walipokuwa maarusi wanafukiziwa manukato ya Omugazu, … (uk. 519)
Pamoja na hayo itaonekana kwamba maneno yote yaliyotumiwa arnbayo sio ya Kiswahili yanaweza kuepukika na wala yasiathiri kuielewa hadithi. Ni wazi picha kamili haitapatikana bila kuipata picha inayowakilishwa na neno hilo lililobeba utamaduni huo. Kifani haya ni mafanikio makubwa hasa kwa vile maneno haya yanachukua nafasi ya msisitizo pamoja na malengo ya msingi aliyotaja Mulokozi (1985:213) ya
Quote:
Kuhifadhi lugha, desturi, practices na utamaduni wa Bakerebe.
Kwa kuangalia lugha aliyoitumia Kitcreza tunaona kwamba lengo la kuelekeza limejitokeza sana. Ufundi wa kifani aliotumia mwandishi kukidhi lengo hili umejitokeza kwenye kutumia maneno fulani fulani na vile vile maneno hayo kurudiwarudiwa. Maneno haya ni maneno ambayo yanalumika sana kwenye lugha ya mazungumzo. Luglia ya mazungumzo imeweza kuifanikisha riwaya hii kwa kuwaangalia wasomaji kama wasikilizaji wa hadithi na hivyo kuwahusisha kikamilifu kufuata matendo yanayoelezewa.
Quote:
1. Pite pite Kahwagizi mweleka mmoja chini; Puu! mgnu wake ukavunjika, loo? Masalale. (uk. 408.)
2. Myombekere akayadaka maneno hayo akamjibu mke wa Kanwakefa hivi, “kumbe, kweli! ndivyo hivyo! Kazi zenu zinawapa wasiwasi nyingi hivyo, shemeji. (uk. 368.)
Wakati mwingine mwandishi anatumia lugha isiyo sanifu na hali ya msisitizo inajitokeza.
Quote:
1. Mimi huwa ninakwambia kila siku hivi: litoto hili ni lyehu, wewe unakataa, sasa vipi? (uk. 157)
2. Ee! hili ni litu la ovyo kama mama yake (uk. 158)
Hapa katika lugha ya mazungumzo badala ya litoto ingekuwa toto, litu ingekuwa jitu na lyehu ingekuwa jehu. Mabadiliko hayo yangeweza kuifanya lugha ikawa ya mazungumzo na pia sanifu ukilinganisha na hiyo aliyoitumia mwandishi. Kitereza ametumia muundo huo kwa kuathiriwa na lugha yake ya asili na hivyo kuongezea msisitizo wa mhemuko na hasira iliyosababishwa na matendo ya mtoto huyo.
Muundo wa sentensi za mwandishi wa BMBB ni wa pekee katika sehemu kubwa ya hadithi hh. Ni muundo ambao haukubaliki katika Kiswahili sanifu lakini unatoa picha kamili ya kile mwandishi anachotaka kukielezea. Uandishi wa aina hii umeweza kuwapa sifa waandishi kadhaa Afrika ambao wameivunja lugha ya Kiingereza ili kukamilisha mawazo yao kulingana na jamii wanamoishi. Waandishi kama Ken Sora-Wiwa (1985) aliyeandika Sozaboy: A Novel in Rotten English aliweza kutajwa kwa heshima kwenye zawadi ya Noma mwaka 1987. Mifano michache itatuonyeshajinsi Kitereza alivyotumia Kiswahili kibaya ili kufikisha ujumbe muhimu kwa wasomaji wake:
Quote:
Akakaa penye mchana wa asubuhi pamoja na wengine aliwakuta wamekwisha fikapo. (uk. 158)
Hapa yaelekea mwandishi, alikuwa anataka kuelezea muda maalum bila kutumiasaa. ‘Mchana wa asubuhi’ inaweza kuwa mnamo saa tano hivi kwani sio alfajiri au asubuhi na mapema. Ni asubuhi ambayo inaelekea mchana. Muda umechukuliwa kama mahali – akakaa penye -. Hata hivyo inaelezwa kwamba wote walikuwa wamekaa nje ya nyumba. Hii inaonyesha kuwa mwandishi alitaka kuweka msisitizo wa hali katika wakati huo. Namna yake ya kuandika ni tofauti na waandishi wengine kwani anatumia Kiswahili ambacho katika undani wake kina mantiki ingawa kwa juu juu kinaonekana kama Kiswahili kibovu. Mfano uliopo hapo chini unadhihirisha haya:
Quote:
Akose leo na kesho, keshokutwa aende kumleta mwanamke atakayesindikiza binti wao kwa maarusi hayo; tena siku ile atakapolala amekwisha kutoka kumleta mwanamke msindikizaji yule apumzike miguu, tena atakapokucha ndipo atume mtu wa kwenda kujulishwa wakati gani wa kwenda kuoa. (uk. 494)
Aidha kipengele hiki ni mfano mzuri wa hadithi nzima inavyokwenda. Kuna mfululizo wa vitendo ambavyo viko huru lakini vile vile vimeunganishwa kimantiki. Hadithi yenyewe imejengwa na mfululizo wa visa ambavyo ingawa vipo huru vina uhusiano wa kutegemeana na visa vingine. Mtindo wa kimkufu (Mlacha: 1988) unajitokeza sana. Huu ni mtindo unaotumika sana kwenye simulizi. Aghalabu mtindo huu huifanya hadithi ieleweke zaidi pale unapozingatiwa na msomaji.
Muundo wa riwaya ni sehemu mojawapo katika kujadili fani ya sanaa. Katika riwaya hii itaonekana kwamba familia ya Bwana Myombekere na Bibi Bugonoka ndiyo inayofungua hadithi. Mwandishi anaanza kwa kuyahadithia matatizo ya familia hii na kisha hadithi inaanza kukua na kuwaingiza ndugu za mume na mke. Hapa ndipo tatizo walilokuwa nalo watu hawa wawili linaonekana kwamba ni kubwa na linaihusisha jamii nzima ya Wakerebe. Kwamba kutokuwa na mtoto sio kitu kidogo kwani kinahusu hata vizazi vinavyofuata. Myombekere anajitahidi amrudishe mkewe ili aweze kuimarisha farnilia yake. Pamoja na matatizo mengine ya maisha hadithi inakwisha baada ya kuonyesha mafanikio ya Myombekere na Bugonoka kupata watoto.
Wahusika wote wamehusishwa na mhusika mkuu, Bwana Myombekere. Mtindo huu wa uandishi unaonyesha upevu kisanii. Kwa vile wahusika wameshikamana na wamejengwa katika hali ya uhalisi wameweza kuchangia sana katika kukuza dhamira kuu. Myombekere na Bugonoka ndio wahusika wakuu katika kulikuza swala la unyumba na kulitoa kwa uwazi katika kazi hii. Wazazi wa Myombekere ndio wachochezi wakuu ambao wanasababisha watu hawa waachane wakati wazazi wa Bugonoka wamehusishwa zaidi kwenye masikitiko ya Bugonoka. Vivyo hivyo wahusika wote vvamekuwa na michango tofauti katika kuyakamilisha maisha ya kina Myombekere kwenye raha na matatizo. Nafasi walizopewa wahusika zinalingana na nafasi yao katika kuikamilisha hadithi. Kwa mfano Myombekere anaonekana ni mtu mwenye shida baada ya kuachana na mkewe. Akiwa katika hali hiyo anaonekana akiitegemeajamii nzima ili kumpata mkewe na kuweza kupata watoto.
Riwaya ya BMBB ni riwaya ambayo ina methali nyingi. Methali zilizotumika ni za Kikerewe ambazo zmaweza kupata rnethali za Kiswahili zinazoelezea falsafa ya aina hiyo hiyo. Kwa mfano methali ya ‘Mgongo hauna macho’ (uk. 5) imelinganishwa kwa kiasi fulani na methali isemayo ‘mshika mbili moja humponyoka! Mlinganisho huo unafafanuliwa zaidi na maelezo yafuatayo: Walipozidi kuzungumza na baba mkwe wake, Bwana Myombekere akageuka asikie vizuri maneno kumtazama asikilize kwa makini’ (uk. 5.) Kitereza hutumia methali kuhitimisha maelezo yake na kuyapa maelezo hayo nguvu zaidi pia huwatumia wahenga. Kwa mfano Myombekere anapokwenda kwa baba mkwe wake kuomba arudishiwe mkewe anahitimisha maombi yake kwa methali; anasema: Sababu wahenga walisema: ‘Mzazi hatapiki ila huchukizwa tu’ (uk. 49.)
Pamoja na mbinu zote hizo kifani, Aniceti Kitereza ametumia fani mbali mbali kuijenga riwaya yake. Ametumia nyimbo (uk. 101, 115, 116, nk.,) lugha ya mazungumzo, misemo tofauti na kurudia maneno ili kuweka msisitizo. Hata hivyo, lugha ya Kikerewe imejitokeza sana katika riwaya hii kiasi ambacho mara nyingi inabidi msomaji aende kwenye maelezo ya maneno ya Kikerewe ili kuielewa hadithi kikamilifu.
Hitimisho
Kitabu hiki kimeiangalia riwaya ya Kiswahili kwa ujumla na wala hakikunuia kuichambua kazi moja au nyingine. Lengo lake ni kumpa mwalimu na mwanafunzi ujuzi zaidi kuhusu uhakiki wa riwaya na pia kumpa nyenzo za kuweza kuielewa riwaya ya Kiswahili. Kama ilivyoonekana katika sura zote zilizotangulia uhakiki wa kijadi ulikuwa finyu mno na uliwafanya wanafunzi wasiwe na ustadi wa kuitambua riwaya wanayoijadili darasani na badala yake kuishughulikia juu juu tu. Ni wazi baada ya kuzingatia tuliyoyajadili hapo juu itaonekana kuwa riwaya ni ngumu zaidi kuliko wengi wetu tulivyodhani hapo awali, lakini ni katika ugumu huo ambapo tunaweza kuielewa. Ugumu wa riwaya ni kweli unatokana na kuiangalia riwaya kwa jicho la uhakiki.
Kwa mhakiki na msbmaji makini wa riwaya jambo la muhimu zaidi ni kuelewa ni wakati gani riwaya fulani ilipotokea na ilikuwa inazungukwa na vitu gani katika maisha halisi. Inabidi kuangalia siasa za wakati huo, elimu ya wanajamii na ya kijamii, hali ya kiuchumi na kadhalika; kwani vyote hivi huhusika sana katika kuiunda riwaya. Kadhalika inahitajika kuwaangalia waandishi wenyewe wanavyohusiana na wakati pamoja na hayo yote tuliyogusia awali. Kwa hali hii sura ya pili imekuwa ni muhimu sana kutangulia sura zingine ili kuitoa picha kamili ya kihistoria kuhusu riwaya ya Kiswahili. Wakati ni muhimu sana katika uundaji wa riwaya. Waandishi wa wakati mmoja wanaweza kuwa na uandishi unaofananafanana au wenye kutofautiana. La muhimu hapa ni kwamba kunaweza kuwa na mikondo tofauti ambayo inaweza kujitokeza katika nyakati tofauti. Mikondo hiyo inaweza kutambulika baada ya kuisoma riwaya na kuangalia wahusika, dhamira na hata maudhui na lugha iliyotumika. Kwa kuangalia inaendeleo na mabadiliko ya wahusika tumeweza kuonyesha jinsi historia na mikondo tofauti iliyojitokeza vilivyoweza kuathiri wahusika na uundaji wao. Muundo wa riwaya ni nadharia mpya ambayo imetumiwa hapa kuonyesha mabadiliko katika uhakikl. Mtindo uliokuwa ukitumiwa sana, ule wa kijadi kama ilivyoelezwa katika sura hii, ni mtindo ambao hauipi riwaya na uhakiki wake nafasi ya kutosha. Unafanya riwaya iwe inaelezwa upya badala ya kuonekana na kuweza kujengwa, kubomolewa na kujengwa upya. Hapa tumewaelewesha wanafasihi namna mpya ya kuichambua riwaya ambayo tunadhani itawasaidia zaidi na kuwapa nafasi pana zaidi ya kujibu maswali ya fasihi na hasa riwaya. Sura ya riwaya pendwa imetoa mwangaza kuhusu upande mwingine wa riwaya ambao haujapewa nafasi na kupata mashiko katika uhakiki wa riwaya. Hata hivyo, tumedokezea sababu zilizosababisha hali hiyo kwa kuonyesha tofauti ya riwaya pendwa na riwaya dhati. Hivyo kitabu hiki kinaweza kuwa cha manufaa sana kwa kumtambulisha mwanafasihi riwaya ya Kiswahili, kumwelimisha kuhusu uchambuzi wake na hali ya hivi sasa.
Kitabu hiki hakidai kuwa ndicho chenyewe tu ambacho kimekidhi malengo muhimu ya uhakiki wa riwaya au kuitoa picha nzima ya riwaya hiyo bila kasoro. Hata hivyo ni kitabu ambacho ni msaada mkubwa kwa wanafunzi, waalimu, wasomaji wa riwaya kwa jumla na hata waandishi. Ni kitabu ambacho kinatoa vidokezo maridhawa na wala sio sheria za kuweza kufurahia na/au kuielewa riwaya ya Kiswahili.
Ni vema pia kugusia kuwa pamoja na uhakiki wa kijadi, kumekuwa na ule wa Kisosholojia ambao ulikuja Afrika pamoja na kuko la Umarx. Uhakiki huo umekuwa na mkabala wa upembuzi na uyakinifu wa kihistoria, na kilele chake katika Fasihi ya Kiswahili kilikuwa katikati ya miaka ya sabini. Kati ya wafuasi wake wenye makini na walioumudu vizuri ni Mulokozi na, kwa kiasi fulani, Senkoro. Mkabala huu uliondokewa kusemwa kuwa ama ulielekea kutia uzito mkubwa upande wa maudhui na kuisahau fani, ama ulielekea kuingiza siasa (kidogo au sana) katika Fasihi, iwe katika kazi za sanaa au za uhakiki. Hata hivyo, ni uhakiki uliochangia kwa kiasi kikubwa katika kuipigisha hatua mbele Fasihi ya Kiswahili. Umuhimu wa uhakiki huu kifasihi na kijamii ni suala linalohusu majadiliano kama vile tu namna nyingine za uhakiki zinavyohitaji majadiliano juu ya usadifu wao na mafao yao.
Hali kadhalika, katika uhakiki ‘mpya’ uliojitokeza katika Fasihi ya Kiswahili sambamba na ule wa kimuundo ni ule wa kihemetiki na, kwa namna fulani, kukawa na dalili za ule tunaouita wa kimjenguo. Uhakiki wa kihemetiki umeletwa katika Fasihi ya Kiswahili na Kezilahabi katika joho la falsafa ya kidhanaishi.
Riwaya fupi ya Nagona ya mhakiki huyu, pindi ikichunguzwa kwa makini, inajitokeza kama ni jaribio la kuuthibitisha mkabala huo wa kihemetiki unaoonyesha mahusiano kati ya msanii, maudhui ya kazi yake na msomaji, na hatimaye kudai kuwa mwandishi ndiyo mdhibiti, ndiye kitovu, cha hayo yote. Na kwa nmi iwe hivyo? Kwa sababu inadaiwa kuwa maana halisi ya kazi ya fasihi (au sanaa) imo ndani ya msanii mwenyewe. Msimamo huu usingekubaliwa na Wanauyakinifu wa Ki-Marx.
Kuhusu uhakiki wa kiudadisi dalili zake zimejionyesha vizuri hadi sasa katika kazi mbili ndogo za J. Mbele (1988) (1989). Aina ya uhakiki huu ambao misingi yake imejengwa na wataalam kama vile Nietzsche na, baadaye, Jacques Derrida, kwa kiasi fulani inadhani, na hata kudai kuwa jadi au mikabala inayofuatwa na wengi katika jamii au taaluma si lazima iwe ndiyo sahihi. Ndiyo maana katika mifano miwili ya tahakiki za mkabala huo, Mbele anajaribu kuidadisi na kuisaili mikabala mitangulizi iliyozitazama hizo mada; anajitokeza na fikra zake mwenyewe zinazojaribu kuchochea udadisi ambao ama unathibitisha kinyume cha mikabala mitangulizi ama inaibua hoja zilizokuwa zimejificha hapo awali. Upungufu unaojitokeza haraka katika uhakiki huu ni ule wa mhakiki kuweza kupinga kwa ajili ya kupinga tu au kwa ajili ya kutaka kuchokoza hoja zaidi. Huku kupinga kunaweza kuwa kumewekwa kwa namna ambayo inaweza kupotosha. Mfano mzuri ni ule wa ‘Mhakiki, Uandishi na Jamii’, makala ambayo yanadai, kwa lugha nzuri tena inayoshawishi, kuwa mhakiki si muhimu katikajamii, ni mtu aliyejipachika tu. Lakini katika hali halisi hii si kweli, na mwandishi wa makala haya anajua kuwa anachokoza tu mawazo ya wasomaji ili waweze kumchunguza mhakiki kwa undani zaidi. Je matokeo yatakuwaje kwa wale wasiopenda kujifikirisha zaidi?
Fasihi ya Kiswahili, hususan kipehgele cha riwaya, kingali kikijitanua na kuzidi kulidhoofisha dai la Ortega Y. Gasset (1948) kwamba ni makosa kufikiri kuwa riwaya ni uwanja utakaoendelea kutoa namna mpya za riwaya pasipo kukoma. Riwaya ya Kiswahili inazidi kustawi kimaudhui, kifani na kinadharia; inazidi kubainisha kuwa waandishi wake wanazidi kuyapanua mawanda yao kwa njia ya kusoma riwaya zingine pamoja na tahakiki na, hali kadhalika, wahakiki wanazidi kutononoka katika uwanja wao kwa kusoma tahakiki na riwaya mbalimbali. Kwa jinsi hiyo riwaya ya Kiswahili inaendelea kwa kasi kubwa katika mbinu za uandishi na uhakiki wake.

Print this item

  FANI NA MAUDHUI KATIKA RIWAYA YA DUNIA UWANJA WA FUJO
Posted by: MwlMaeda - 08-27-2021, 04:32 PM - Forum: Riwaya - No Replies

Dunia Uwanja wa Fujo
Dunia Uwanja wa Fujo ni riwaya iliyoandikwa na Euphrase Kezilahabi mwaka wa 1975. Ni riwaya ambayo inasawili maisha ya wanadamu hususani waishio Afrika Mashariki, hasa hasa katika nchi ya Tanzania.
“Dunia Uwanja wa Fujo” inaelezea jinsi maisha yaliyopo duniani ni sawasawa na fujo, kwani kila mtu anayekuja duniani huleta fujo zake na baadaye kutoweka. Mwandishi anaelezea kwamba kila mtu anafanya fujo zake na kusababisha matatizo mbalimbali katika jamii yake kama vile mauajiukabilaumalayauchawiubakajiulevi wa kupindukia n.k. Hivyo basi mwandishi anaamini kwamba katika dunia kila mtu anakuja na fujo zake na kutoweka. Kwa mfano, mhusika Tumaini katika riwaya hii ameleta fujo zake kama vile umalaya, mauaji na mengine mengi na baadaye kutoweka.
Mbinu za kifani katika riwaya hii
Fani za kijadi ndizo zilizosababisha riwaya izalike. “Dunia ni Uwanja wa Fujo” ni mojawapo ya riwaya zilizotokana na fani ya kijadi ambayo ni sira. Sira ni fani ya kijadi ambayo hujumuisha wasifu na tawasifu, yaani habari za maisha ya watu; kwa mfano mwandishi E. Kezilahabi katika riwaya yake hii amejaribu kumuonyesha mhusika Tumaini maisha aliyokuwa akiishi.
Mfano uk. 11, “Alibatizwa, alikuwa mtoto wa mwalimu Kapinga……”. Vile vile Tumaini alikuwa mlevi, malaya, mfano uk. 73 “mwenyewe kaingiaaaa, tajiri wetuuu”. Hivyo basi riwaya hii inasadifu kuwa ni mojawapo ya riwaya za fani za kijadi ambayo hujumuisha wasifu wa mhusika Tumaini toka mwanzo hadi mwisho wa maisha yake.
Muundo
Muundo ni namna visa na matukio hufuatana kwa mtiririko. Hivyo tunaweza kusema pia muundo ni mfuatano wa masimulizi katika kazi ya fasihi. Katika riwaya hii mwandishi ametumia muundo wa rejea pamoja na changamano.
Katika muundo wa rejea mwandishi anaanza kwa kuonyesha maisha ya Dennis pale alipowapokea wageni akina Tumaini na pia kurejelea kwa kuonyesha maisha ya Dennis pale tangu utoto wake (uk.66).
Pia mwandishi ametumia muundo changamano au rukia ambapo visa vinakuwa vinarukiana: hii inajidhihirisha sehemu ya kwanza ambapo anatuonyesha nyumbani kwa Kasala ambaye anaishi kijijini Bugolola; kisa hakijaisha tunaona pia kisa cha Tumaini (uk.11) ambapo mwandishi anaonyesha alivyozaliwa na kubatizwa.
Mwandishi pia ameigawa kazi yake katika sehemu kuu tatu na kila sehemu ameipa namba ili kusadifu yaliyomo katika kazi yake ya riwaya.
Katika sehemu ya kwanza E. Kezilahabi amewachora wahusika kwa kuonyesha adha na matatizo mbalimbali yanayoikabili jamii ya Bugolola, kwa mfano ushirikina, umalaya na ulevi: mambo hayo yote ameyaonyesha katika namba 1, 2, 3, 4, 5.
Pia katika sehemu ya pili tunamuona Tumaini akiwashawishi akina John na Anastasia kwenda nao mjini Dar es Salaam, lakini inakomea Shinyanga baada ya kukutana na dada ya Dennis, kitu kilichompelekea Tumaini na wenziwe kuanza maisha mapya mjini Shinyanga. Lakini katika maisha hayo Tumaini na John wanakuwa wenye kupenda pombe na ansa, kitu kilichopelekea kufilisika kwa Tumaini.
Sehemu ya tatu inaonyesha baada ya Tumaini kuamua kufanya kazi alivyopata mafanikio makubwa, lakini mafanikio hayo yanaingia doa baada ya serikali kuingiza mfumo wa ujamaa, kitu kilichopelekea mali zote za Tumaini. Mwisho kabisa tunamuona akichukua jukumu la kumuua mkuu wa wilaya ya Shinyanga ambaye ndiye alikuwa msimamizi mkuu wa shughuli za ujamaa; kitendo hicho kinapelekea hukumu ya kifo kwa Tumaini (namba 12, 13, 14).
Msuko
Mbunda Msokile (1992:206) anasema kuwa msuko ni mtiririko au mfuatano wa matukio yanayosimuliwa kuanzia mwanzo mpaka mwisho. Hali hii huandamana na uchaguzi au mpangilio na ufundi wa kusimulia matukio yaliyoungwa vyema katika kazi ya sanaa ya kubuni itumiayo lugha. Lakini si tofauti na ule ufafanuzi huu si tofauti na ule unaofafanua muundo, kwani nao ni mtiririko wa matukio jinsi jinsi yanavyopangwa kiufundi kutoka mwanzo wa simulizi hadi mwisho.
Pesa za urithi alizoachiwa Tuamini pamoja na malezi mabaya kutoka kwa wazazi wake ndio zinakuwa usababishi wa utonvu wa nidhamu wa Tumaini katika kijiji chao cha Bugolola, mambo hayo ya uonvu wa nidhamu ni kama vile;- mlevi, Malaya, kutofanya kazi, pia alitumia ovyo mali alizoachiwa. Mfano katika (uk.15) “tunamuona mama yake Tumaini akimkabithi Tumaini funguo ya kufungua sanduku la marehemu baba yake ammbalo lilikuwa limebeba urithi wake.
Tumaini baada ya kupewa pesa za urithi hapa ndio tunaona mshitikizo kwani kwani pesa za urihi zilimsababisha kuamua kuacha shule na kuanza kuzitumia pea hizo ovyo kama vile ukahaba umalaya, ulevi, na mengineyo (uk. 16, 17).
Pia katika riwaya hii msuko unaendea kuonekana pale ambapo Tumaini, John, na Anastazia walipofika Mwanza na kufanya maamuzi ya kuelekea Daes saalam baada ya kuona eneo la Mwanza haitawafaa kwa kuanza maisha mapya kwani palikuwa karibu mno na kijini kwao, sababu nyingine ilikuwa Akina Tumaini hawahuondoka kijijini kwao kwa wema. Safari yao ya kuelekea Dar es saalam inafikia kikomo pale ambapo walipofika Shinyanga na kukutana na Dennis ambaye aliwasihi wasitishe safali yao ili aambatane nao wakapajue kwake na kumpasha habari juu ya mambo yaliyokuwa yakiendelea kijijini kwao Mugele (uk. 55-72).
Hali ya kuahilisha safari ya kuelekea Shinyanga ilisababisha akina Tumaini kuanza maisha mapya mjini Shinyanga na kwa vile Tumaini alikuwa na pesa nyingi za urithi alianza maisha ya anasa hali hiyo ilipelekea kuishiwa Tumaini kipato na kumpelekea Tumaini kutafuta kazi ya ulinzi ambayo alisaidiwa na Dennis katika kuipata ajija hiyo(uk.114). Lakini pindi alipoanza kazi hiyo alijikuta akichukiawa na watu mbalimbali kutokana na kazi yake ya kuchunguza watu sili zao na kuzilipotisha serikarini. Kazi hiyo ilisababisha hata baadhi ya watu kumkimbia Tumaini mahali alipotia mguu wake. Mfano pindi alipofika baa wateteja walikunjwa haraka haraka na kukimbia hali hiyo ilisababisha wenye biashara zao kumchukia Tumaini na ikafikia hatua ya kumtafutia Tumaini wajambazi wa kumuadabisha Tumaini.
Baada ya Tumaini kutafutiwa majambazi na kuwa ameadabishwa hali hiyo inatumika kama usababishi wa Tumaini kuichukia kazi yake na kuamua kutafuta kazi nyingine ya kujiajili yeye mwenyewe, kazi yenyewe ilikuwa ni kazi ya ukulima japo alianza kama mkulima mdogo lakini baadae akajikuta akipata maendeleo makubwa katika kazi yake mfano alinunua shamba kubwa na alitumia Trekta katika shuguli zake za kilimo. lakini ngombe wa maskini hazai serikali ikapitisha mfumo wa ujamaa ambapo ilidai hakuna umiliki binafsi na mali zote ni za ni za umma hali hiyo ilisababisha kumuingiza tumaini matatani kwa hakukubaliana na hali hiyo na kupelekea kufanya tukio la mauaji ambapo alimuua mkuu wa wilaya ambaye ndiye alikuwa ni kiongozi wa ujamaa (uk. 114). Kitendo hicho kilitumika kama usababishi kwa Tumaini kuwekwa chini ulinzi wa polisi na hatimaye kuhukumiwa kunyongwa (uk. 131).
Mtindo
Mtindo ni jinsi msanii anavyotumia ufundi, umahiri na hisia zake katika kutenda au kueleza jambo fulani. Katika riyawa hii kuna mitindo mbalimbali ambayo mwandishi ameitumia; ni kama vile:
  • Monolojia: Masimulizi kwa kiasi kikubwa mwandishi ametumia lugha ya masimulizi katika kuelezea visa/matukio, sifa na tabia za wahusika katika kuikamilisha kazi yake.
  • Barua: Mwandishi pia ametumia mtindo wa barua, m kwa mfano katika uk. 68 mwandishi ametumia mtindo wa barua tunaona Vera akimwandikia Denis barua, pia uk. 105 mwandishi ametumia mtindo huu wa barua, Tunamuona Tumaini akimuandikia Joku barua vilevile katika uk 110 “tunamuona Denis akipokea barua kutoka kwa Vera”, uk. 123 “bibi Kimalio alimuandikia barua Denis”.
  • Hotuba: Mwandishi katika kazi yake hii ya riwaya ya “Dunia ni uwanja wa fujo” ametumia mtindo wa hotuba. Kwa mfano katika uk. 115 – 117 mtindo wa hotuba umetumika na hotuba ilikuwa ya kusisitiza Azimio la Arusha ambalo lililenga hatua ya siasa ya ujamaa na kujitegemea ambayo ilitaka watu wote wamiliki mali na uchumi kwa pamoja bila kujali mwenye nacho na asiye ncho.
  • Nyimbo: Ni mtindo mmoja wapo aliotumia mwandishi aliotumia mwandishi wa riwa hii. Kwa mfano uk. 10 mwandishi ametumia wimbo ulioimbwa na mpiga zeze.
  • “Wanaume Bugolola
  • Mchana hawajambo
  • Usiku hawana tendo”
Mwandishi pia ametumia wimbo kwa mtindo wa shairi katika kazi yake hii kwa mfano katika uk. 13 tunona Tumaini akiandika shairi ambalo lilisomwa na mwalimu darasani kama ifuatavyo.
  • “Yeh,
  • Nitaoa msichana
  • Msichana mwenye shingo
  • Shingo shingo kama la mbuni..”
Mwandishi ametumia wimbo wa maungunzo, mwandishi katika mtindo wa mazungumzo ametumia nafsi zote tatu yaani nafsi ya nafsi ya kwanza, nafsi ya pili, nafsi ya tatu katika kazi yake hii, kwa mfano. – Uk. 13 tuaona nafsi ya kwanza umoja “nitaoa msichana” na – uk. 27 tunaona nafsi ya kwanza wingi. “hata sisi,” pia – Pia nafsi ya pili katika riwaya hii imetumika kwa mfano uk. 36 “…wewe kasala Pia nafsi ya tatu katika riwaya hii tunaona katika uk. 35 “….yeye alisema kwa machozi
Matumizi ya lugha
Lugha ni muhimu katika kazi ya fasihi. Pasipo lugha hakuna riwaya. Mwandishi wa riwaya hii ametumia lugha sanifu iliyosheheni taswira, mkoto, misemo, methali, tamathali za semi, nahau, lugha za kigeni, na mbinu zingine za kisanaa kama ifuatavyo:
Lugha sanifu ni mojawapo ya lugha ambayo mwandishi ametumia toka mwanzo hadi mwisho. Lugha iliyotumika ni Kiswahili sanifu.
Pia mwandishi ametumia lugha isiyo sanifu kwa kiasi kidogo. Kwa mfano katika uk. 5, Mwandishi anasema “…. Batoto bamenisosondogorasondogola na chichwa, bengine bamenikorokorakorokora na kucha”. Uk. 30 “…. Vizuri walilia kwa sauti za kutisha, yuhuu. Huba, huba, huba. Wotha ,wotha”
Lugha ya kigeni imetumiwa na E. Kezilahabi katika riwaya yake hii. Lugha ya kigeni aliyotumia ni Kiingereza kwa mfano: – “Africans royal bar” (uk. 62). – “Snow cap” (uk. 62) – “You are too optimistic about life and you are too pessimistic” (uk. 65, 66). – “Welcome back” (uk. 88). – “Security (uk. 89 na 90).
Mchanganyo ndimi: Ni matumizi ya lugha ambayo mwandishi ametumia katika riwaya hii. Mchanganyo ndimu ni ile hali mtu kuongea kwa kutumia lugha zaidi ya mbili. – Mfano: “mimi …naturalist” (uk. 41).
Lugha za matusi: Ni mbinu nyingine zilizotumiwa na mwandishi katika riwaya hii ni lugha za matusi kwa mfano. – “Washenzini ninyi”. (uk. 12). – “Kumbe bado washenzi” (uk. 50). – “Yule mshenzi amekwenda” (uk. 93) – “Nimemfukuza mbwa tumaini (uk. 109). – “Kwanza wewe bwege. (uk. 121). – “…. Alidakia na kusema unyokonyoko (uk. 122).
Tamathali za semi: Ni maneno yanayotumiwa yanayotumiwa na wasanii ili kutia nguvu katika kazi hiyo. Hivyo tamathali za semi zinazotumika katika riwaya hii ni pamoja na:
Tasbihiha/Mshabaha: Ni maneno ambayo hutumia kulinganisha kitu na kitu kingine kwa kutumia maneno kama vile “mithili, sawa, kama” mfano: – “Miaka ni kama kunguni” (uk. 6). – “Baba yako atakuwa mkali kama samba” (uk. 6). – “Mapenzi ni kama mpunga mototo wangu” (uk. 14). – “Lakini mimi ninaumwa ninaumwa kama panya.” (uk. 17). – “Si tutakufa kama mbwa” (uk. 19). – “Kukaa kama watakatifu” (uk. 19). – “Aliyekunyata nyumbani kwake kwa uoga kama panya aliyesikia mlio wa paka”. (uk. 130).
Sitiari: Ni tamathali za semi ambazo ulinganisha vitu vizuri kwa kutumia viunganishi au linganishi. Mfano “ni”: – “Watoto wote yatima ni watoto wangu” (uk. 15). – “Huyo ni baba yako” (uk. 12). – “Ujamaa ni mzuri” (uk. 112).
Takriri: Ni tamathali za semi ambayo neno hujirudiarudia kwa lengo la kusisitiza jambo fulani. Takriri ni matumizi ya lugha ambayo msanii ametumia katika riwaya hii, mfano wa takriri: – “Mauti, mauti”. (uk. 17). – “He! Hee! Hee!” (uk. 18) – “Kasala, kasala, ngoja nije!”(uk. 22) – “Yuhu! Yuhu!” (uk. 27) – “Haa! Haa! Haa! (uk. 42) – “Msiue, msiue!” (uk. 44)
Tashihisi: Ni tamathali za semi ambazo vitu ambavyo si viumbe hai hupewa hadhi ya kutenda kama binadamu. Mfano: – “Mwezi uliona nyota ziliona hata jua liliona.” (uk. 12) – “Tumaini alisikia sauti kama ya ndege akiimba kwa huzuni.” (uk. 19) – “kila jiwe walilokalia liliwaambia “samahani umekalia bega langu”. (uk. 32)
Tanakali sauti: Ni tamathali ya semi ambayo uigaji wa sauti za asili. Mfano Katika riwaya hii tanakari sauti alizotumia msanii ni kama ifuatavyo: “boooouuu! (uk. 130)
Tafsida: Ni tamathali za semi ambazo kwazo matumizi zake ni za adabu. Mfano: “Kazi kutembeza kengele zako kwenye mabaa.” Uk. 121. – “Tumaini alikuwa akishika mahali pabaya”. Uk. 53.
Methali: Usemi wa kisanii wa kimapokeo unaofikiriwa na jamii kuwa kweli na unaotumiwa kufumbia au kutolea mifano na huwa unabeba maana pana kuliko maneno yenyewe yanayotumiwa. Kwa mfano: – “Wema wa mtu hujulikana siku ya mazishi yake.” (Uk. 13) – “Ugonjwa haufichwi. Afichae ugonjwa ndio hufa.” (Uk. 29) – “Kweli wajinga ndio waalimu wa kuwafunza welevu. (uk. 78) – “Ukishikwa shikamana.” (Uk. 102)
Misemo: Ni mafungu ya maneno yanayotumiwa na jamii ya watu wa lugha hiyo kwa namna maalumu ili kutoa mafunzo, maadili na kuihadharisha jamii. Misemo ni maneno ambayo jamii huyatumia kutokana na uzoefu katika maisha. Kwa mfano: – “Ponda mali kifo chaja.” (Uk. 10) – “Ulimwengu hauna mwema.” (Uk. 103) – “Mapenzi yao sasa yalikuwa yamekwisha pata kovu”. (Uk. 108) – “Nilitaka uniondoe kwenye mdomo wa samba.” (Uk. 24)
Nahau: Haya ni mafungu ya maneno yenye maana maalumu ambayo haitokani na maneno ya kawaida yaliyopo kwenye maneno hayo. Nahau za lugha yoyote hutumiwa zaidi na jamii yenye asili ya lugha hiyo. Kwa mfano: – “Amezunguka mbuyu – amekula rushwa”. (uk. 25) – “Unamvika kilemba cha ukoko”. (Uk. 71) Tanakali sauti: – “Booouuu!”
Mjalizo: Katika tamathali hii sentensi huwa ni mfuatano tu wa maneno yasiyo na viungo vyovyote. Mfano: – “Wenye mashoka ! wenye mikuki na miundu! Wenye pinde na wenye mapanga walianza kulifyeka lile chaka”. (Uk. 27)
Wahusika
Wahusika ni watu au viumbe waliokusudiwa wawakilishe tabia za watu katika kazi za fasihi. Wahusika wa fasihi ni wa aina kuu tatu,wahusika kazi ya fasihi wanaweza kuwa wahusika wakuu, wahusika wadigo, na ewahusika wajenzi. Wahusika huonyesha dhana mbili muhimu katika maisha ya watu yaani wema na mabaya pia wahusika humaanisha tabia maalumu iliyokusudiwa na jamii.
Katika riwaya ya “Dunia uwanja Fujo” wahusika wake ni mhusika mkuu, whusika wadogo, na wahusika wajenzi kama alivyoainisha Catherine Ndugo (1991) na Wangali Mwai (1991). Katika riwaya hii mwandishi ametumia wahusika wa aina tatu kwa kutumia kigezo cha Catherine na Wangeri Mwai(1991) Kama wahusika wakuu, wadogo, na wajenzi kama ifuatavyo:
Mhusika mkuu: huyu ni yule anayejitokeza kila mara katika kazi za fasihi tangu mwanzo hadi mwisho. Maudhui ya kazi ya fasihi huwa yanamzungukia na hata kutolewa na mhusika mkuu zaidi ya wahusika wengine.
Tumaini: Huyu ndiye mhusika mkuu katika riwaya hii kwani maudhui na dhamira zimejengwa juu yake. Pia tunaona wahusika wajenzi akina John, Anastazia, Dc, na mgeni kutoka Dar es saalam dhamira wanazozitenda zinamgusia mhusika mkuu ambaye ni Tumaini. Jina Tumaini ni jina ambalo amepewa na mzazi wake mzee Kapinga ambaye alikuwa mwalimu. Jina Tumaini linasadifu matumaini ya wazazi wake, pia alikuwa ni mototo pekee wa kiume katika familia ya mwalimu Kapinga pia walikuwa na matumaini pindi atakapomaliza shule ndio atakuwa msaada wao katika familia na pindi watakapokuwa wazeeka. Mambo hayo yanapatikana katika (uk.11). Inasema “… Naam Tumaini alikuwa mtoto wa watu hawa. Tumaini kama jina lenyewe lionyeshavyo alikukuwa peke yake katika tumbo la mama yake…..”
Wasifu wake: – Alikuwa ni mtoto wa Kapinga. (uk. 9) – Alikuwa Malaya (uk. 8, 24) – Alikuwa mlevi (uk. 94) – Mchapa kazi (uk. 114) – Mtumia Pesa vibaya (uk. 55) – Alikuwa muuaji. (uk. 128) – Alikuwa na mapenzi ya dhati kwa mkewe (uk. 128) – Alikuwa na matusi (uk. 12)
Wahusika wadogowadogo: Hawa ni wahusika ambao hawajitokezi mara kwa mara katika kazi ya fasihi ndio ambao husimamia dhamira ndogo ndogo. Katika riwaya hii ya “Dunia uwanja wa fujo” wahusika wadogo wadogo waliojitokeza ni kama ifuatavyo:
1. Kapinga. Wasifu wake: – Baba yake na Tumaini. (uk. 9) – Alikuwa mwalimu. (uk. 9) – Alikuwa na malezi mabaya kwa mwanae. (uk. 12) – Alikuwa ni Mume wa miango. (uk. 9) – Alikuwa ni mbinafsi. (uk. 15) – Alikuwa hapendi kushilikiana katika jamii. (uk. 12).
2. Kasala. Wasifu wake: – Ni mwanakijiji wa Bugolola. (uk. 1). – Mtoto wa Mugala. (uk. 2). – Baba yake na Misana. (uk. 2). – Mume wake na Mugele. (uk. 2). – Mtu mwema. (uk. 4). – Kiasi fulani alikuwa ni mvivu. (uk. 6)
3. Mungere. Wasifu wake: – Mke wa Kasala (uk. 2). – Mama yake na Misana (uk. 2). – Mwanakijiji wa Bugolola (uk. 2). – Mtu mwema na mchapa kazi. (uk. 4).
4. Misana. Wasifu wake: – Mtoto wa Kasala (uk. 2). – Alikuwa mtundu. (uk. 3). – Mtoto wa Mungere (uk. 2). – Mdogo wao na akina Dennis, Leonila, Aulelia. (Uk. 5).
5. Mugala. Wasifu wake: – mwananchi wa Bugolola. (Uk. 3) – Mchawi. (Uk. 3 na 7). – Ni mama yake na Kasala. (uk. 2) – Ni mjane (uk. 4). – Mtu mwenye hasira (uk. 22) – Alikuwa na malezi mabaya kwa wajukuu zake (uk. 19).
6. Leonila. Wasifu wake: – Alikuwa dada yake Dennis na Misana. – Alikuwa mtoto wa Kasala Mungere. – Alikuwa mpenzi wa Tumaini (uk. 8 na 24).
6. Benadeta. Wasifu wake: – Mke wa pili wa Dennis (uk. 121) – Mtu mwenye chuki (uk. 120) – Alikuwa na dharau na mwenye matusi. (uk. 121)
7. Christina. Wasifu wake: – Alikuwa kahaba. (Uk.96) – Alikuwa mlevi (uk.94) – Alikuwa mlaghai (uk.95) – Hana mapenzi ya dhati (uk.96) – Alikuwa anapenda sana pesa. (Uk. 94)
8. Makoroboi. Wasifu wake: – Alikuwa jambazi (uk.96) – Alikuwa mkatili na mwenye kisasi (uk.96) – Anapenda pesa. (Uk.96)
Wahusika wajenzi
Ni wahusika ambao maudhui yao na dhamira wanazozitenda zinamsaidia mhusika mkuu katika dhamira azitendazo. Mara nyingi wahusika wajenzi wanakazi ya kunjenga au kumsaidia mhusika mkuu katika dhamira zake. Katika riwaya hii wahusika wajenzi ni kama ifuatavyo:
1. John. Ni mhusika mjenzi kwani dhamira alizobeba na nafasi alizotumiwa na mwandishi ni kwa lengo la kumjenga mhusika mkuu tumaini. Pia tunaona John na Tumaini walikuwa na mahusiano na ushirikiano tangu wakiwa kijijini Bugolola mpaka waliposafiri kuelekea mjini Shinyanga.
Wasifu wake: -Alikuwa mlevi (uk. 62) -Alikuwa Malaya (uk. 62 na 66). -Alikuwa mvivu (uk. ) -Ana mapenzi ya dhati (uk. 97)
2. Anastazia. Pia huyu ni mhusika mjenzi kwani alikubali kuambatana na Tumaini kijijini kwenda Mwanza halafu mjini Arusha. Pia uhusiano wao ulidumu na kupelekea kuoana na Tumaini.
Wasifu wake: – Alikuwa na mapenzi ya dhati. (Uk. 57, 97, & 99). – Alikuwa mke wa Tumaini. (Uk. 61) – Mtu mwenye huruma (uk. 99) – Mtu mvumilivu. (Uk. 89)
3. Dennis. Ni mmojawapo wa wahusika wajenzi kwani ndio anaemjenga mhusika Tumaini kwa kiasi kikubwa akiwa mjini Shinyanga.
Wasifu wake: – Ni mtu mwenye mapenzi ya dhati. (Uk. 59) – Alikuwa mtoto wa Kasala. (Uk. 3) – Alikuwa mtumishi wa serikalini
Maudhui
Katika kazi ya fasihi ni jumla ya mawazo yote yanayozungumzwa pamoja na mtazamo wa mwandishi juu ya mawazo hayo. Maudhui hujumuisha mawazo pamoja na mafunzo mbalimbali yaliyomsukuma msanii hadi akatunga na kusanii kazi fulani ya kifasihi. Vipengele vya maudhui ni pamoja na dhamira, migogoro, falsafa ujumbe na msimamo.
Katika riwaya hii mwandishi amejitahidi kwa kiasi kikubwa kuonyesha maudhi mbalimbali katika kazi yake kupitia vipengele mbalimbali kama vile Dhamira, migogoro, ujumbe, falsafa, mtazamo itikadi hii yote ni kwa lengo kuu la la kuelimisha jamii kuhusu mambo mbalimbali yanayotukia katika jamii hiyo.
Dhamira ni wazo kuu au mawazo mbalimbali yanayojitokeza katika kazi ya fasihi. Senkoro anataadharisha maana hii isichanganywe na maudhui kwani dhamira ni sehemu tu ya maudhui na aghalabu dhamira kuu ndio hujenga kiini cha kazi ya fasihi. Dhamira zimegawanyika katika makundi mawili, kuna dhamira kuu na dhamira ndogondogo.
Dhamira kuu ni wazo kuu linalojitokeza katika kazi ya fasihi, dhamira kuu katika riwaya hii ni matatizo na mikinzano ya kijamii, kiuchumi, na kisiasa, sasa tuangalie ni kwa jinsi gani mwandishi ameijadili dhamira hii.
Matatizo na mikinzano ya kijamii, kiuchumi, na kisiasa, Katika riwaya hii “Dunia uwanja wa fujo” kwa kiasi kikubwa riwaya hii imejikita katika dhamira hii ambapo ameonyesha matatizo na mikinzano kiuchumi na kijamii ambayo jamii ya Kitanzania iliyoandikiwa hukabiliwa nayo. Ili kuijenga dhamira hii mwandishi amewatumia wahusika kama vile Tumaini, John ,Anastazia, Kapinga, Dennis ili kuiunda dhamira yake kuu katika riwaya hii. Tukianza na Tumaini mwandishi amemuonyesha kuwa ni mhusika ambaye anapinga sera za kijamaa ya siasa ya ujamaa iliyoanzishwa na serikari nchi nzima hali hiyo inaleta ukinzani kwa tabaka lenye mali kwani hawakuwa tayari kuachia mali zao kwa umma. Hali hii inadhihilisha pale Tumaini alipoamua kupingana na hali hiyo ya kunyanganywa mali zake na kupelekea kumuua mkuu wa wilaya, ambaye alikuwa ndio kiongozi mkuu katika mkoa wa Shinyanga katika shughuli za kusimamia sera hiyo ya ujamaa. (uk. 127) Hali hiyo ni mfano tosha kudhihirisha kuwa dhamira kuu katika riwaya hii ni Matatizo na mikinzano ya kijamii, kiuchumi, na kisiasa.
Dhamira ndogo ndogo. Haya ni mawazo yanayojitokeza ili kujenga dhamira kuu. Dhamira ndogondogo zinazojitokeza katika riwaya hii ni:
Mapenzi na ndoa. Mwandishi E. Kezilahabi amejadili suala la mapenzi na ndoa katika pande mbili tofauti, kwanza ameonesha mapenzi ya dhati na mapenzi ya ulaghai lakini pia ameonesha ndoa za dhati na ndoa za ulaghai. tukianza na mapenzi ya dhati, mapenzi ya dhati yanajitokeza kwa:
a) Mapenzi ya dhati kwa Tumaini na mkewe Anastazia Mwandishi ameonesha mapenzi ya dhati aliyokuwa nayo Tumaini kwa mke wake, Mwandishi anathibisha hili pale anapoamua kutoroka na Anstazia na kuelekea mjini Shinyanga ambako walianza maisha mapya pia tunaona jinsi gani wawili hawa walivyojaliana hata katika kipindi cha matatizo. Mfano Anastazia alionyesha mapenzi ya kweli pale alipompelekea Tumaini chakula na kumfaliji kuwa atapona, pindi Tumaini alipopigwa na akina makoloboi. (Uk. 97)
Mapenzi ya dhati aliyokuwa nayo kwa mke wake pia yanajidhihirisha pindi mke wake huyo alipokubali kuishi na Tumaini japo alikuwa ni mhuni na mlevi pia ha baada ya Tumaini kupigwa na kualibiwa sura Anastazia alindelea kuafiki kuishi na mumewe Tumini, hii ni kwa kuwa alikuwa akimpenda. Mwandishi anathibitisha hili katika uk. 64.
2. Ulevi Mwandishi E, Kezilahabi hakuwa nyuma kujadili suala la ulevi na athari zake kwa binadamu na jamii kwa ujumla, katika riwaya yake hii amemtumia muhusika Tumaini pamoja na John kuelezea dhamira hii. Tukianza na Tumaini, mwandishi anamwonesha Tumaini akianza tabia ya ulevi wa pombe kali baada ya kufiwa na wazazi wake kijijini Bugololola hata alipoamia mkoani Shinyanga aliendelea na tabia hiyo ya ulevi wa pombe, Mwandishi hakuishia hapo tu bali ameonesha na athari za tabia hiyo ya ulevi kama vile kupelekea kufilisika kwa tumaini kama mwandishi anavyothibitisha (Uk. 94 & 95).
3. Malezi kwa watoto Hii ni dhamira nyingine inayojitokeza katika riwaya hii, Mwandishi amemtumia muhusika Tumaini kuilezea dhamira hii, tunamwona Tumaini akipata malezi mabaya kutoka kwa wazazi wake kitu kilichopelekea kuyahalibu maisha ya Tumaini na kumfanya aache shule, awe mlevi, pamoja na mengine mengi.
Mfano: Siku moja Tumaini alimchoma mlezi wake jichoni. Yule kijana alimpiga Tumaini kidogo, Tumaini alikimbia kwenda kushtaki kwa mama yake. “Mama Mpishi amenipiga!” Kwa nini umempiga mtoto wangu!” Mugaya alifoka.” Hali hii inaeleza jinsi Tumaini alivyo lelewa vibaya na kudekezwa na wazazi wake (uk. 11).
Ushirikina na uchawi Ni hali ya kuamini nguvu za giza, ni jambo ambalo lina sababisha jamii nyingi kugawanyika na kukosa amani. Kwani mwandishi anadhihirisha hili anaposema:
“Vizuu walilia kwa sauti ya kutisha: yuhu!yuu! huba!” (uk. 30).
“Tena alikuwa akilala ndani ya nyumba yako! Ndio maana mama yako alikuwa mchawi” (uk. 36).
Suala la ushirikina katika jamii inayotuzunguka ni janga ambalo kila siku linahatarisha maisha ya watu hususani wazee wenye macho mekundu wako hatiani kupoteza maisha yao katika baadhi ya maeneo mfano mkoa wa Shinyanga na Simiyu, hivyo dhamira hii haijapitwa na wakati.
Unafiki Hii ni dhamira pia inayojitokeza katika riwaya hii, katika kuijadili dhamira hii Mwandishi amemtumia mke wa Dennis kama mtu mnafiki kwani alijifanya anampenda mmewe kumbe alikuwa na uhusia mwamume mwingine ambaye ni John rafiki yake na Dennis. Mwandishi anadhihilisha hali hiyo akionyesha katika kitabu chake kwamba:
“Heshima yangu imekwishapotea John ukiniacha hivihivi nitaona aibu sana!” (uk. 72).
Tukigeukia katika uhalisia, tabia hii ya unafiki imeshamiri katika jamii zetu, unaweza ukawa na rafiki au ndugu ambaye akawa mnafiki kwako. Jamii inatakiwa kuondokana na tabia hii kwa haifai kabisa.
Nafasi ya mwanamke Katika riwaya hii mwanamke amechorwa katika pande mbili, amechorwa katika upande hasi lakini pia mwanamke amechorwa katika upande chanya, upande hasi mwanamke amechorwa kama kiumbe duni na dhaifu wakati katika upande chanya amechorwa kama mtu jasiri, mchapa kazi, mwenye upendo. n.k. Sasa hebu tuangalie nafasi ya mwanamke katika jamii kama alivyochorwa katika riwaya hii tukianza na upande hasi.
Katika riwaya hii mwanamke amechorwa kama kiumbe duni, dhaifu, katika nafasi mwanamke amechorwa kama:
A) Chombo cha starehe. Mwandishi amemchora mwanamke kama chombo cha starehe anayeweza kutumiwa kuwastarehesha wanaume ili mradi kufurahisha nafsi zao, hili linathibitishwa na Mwandishi katika riwaya hii akimtumia muhusika Christina kama chombo cha starehe, ambaye alionekana kujirahisishwa kwa wanaume ili mladi apate fedha. Mfano uk. 95 & 96.
“Sijaona mwanaume mwoga kama wewe! Kristina alisema.
Tumaini alilala kitandani. Kristina alizima taa” (uk. 96)
Hata katika jamii yetu inayotuzunguka wanawake kwa kujijua au kutojua wamekuwa wakifanywa kama chombo cha starehe kuwastarehesha wanaume, jamii inatakiwa kubadilika na kuondokana na dhana hii kwani mwanamke pia anastahiri heshima katika jamii.
B) Mtu asiye na maamuzi katika jamii. Mwandishi amemchora mwanamke kama mtu asiye na maamuzi katika jamii yake, kwa mfano anamtumia muhusika ambaye alikuwa nini mama yake Tumaini kushindwa kufanya maamuzi juu mali alizoziacha kama urithi wa Tumaini japo hakupenda kumuachia mtoto wao fedha nyingi(alijua zitamuangamiza mwanae) lakini alishindwa kubatilisha kutokana na maamuzi yaliyoachwa na mumewe.mfano anaonyesha;
“Ni vizuri zaidi mtoto kurithi vitu kama hivyo, licha ya hekima na kumrithisha mototo pesa ni ni kunvisha taji la uovu.” Baba yako alikataa kabisa; na kwa kuwa nilishindwa mawazo ya baba yako alipokuwa bado mzima, siwezi sasa kugeuza tamshi lake.” (uk. 15)
Hata katika jamii yetu, inawachukulia wanawake kama watu wasio na maamuzi katika familia na pindi inapotokea kufiwa na waume zao huwa wanapata shida na manyanyaso kutoka kwa ndugu wa mwanaume kama vile kufukuzwa kwenye nyumba, kunyang’anywa watoto na mali nyingine alizoshirikiana kuzichuma na mumewe. Jamii inatakiwa kumpa nafasi mwanamke na itambue kuwa ana haki sawa kama mwanamume.
C. Msaliti. Hii ni nafasi nyingine ambayo mwandishi amemchora mwanamke, kwa mfano tunaona mke wa Dennis kama mtu mnafiki kwani alijifanya anampenda mmewe kumbe alikuwa na uhusia mwamume mwingine ambaye ni John rafiki y yake na Dennis. Mwandishi anadhihilisha hali hiyo akionyesha katika kitabu chake kwamba:
“Heshima yangu imekwishapotea John ukiniacha hivihivi nitaona aibu sana!” (uk. 72).
Migogoro ni mivutano na misuguano mbalimbali katika kazi za fasihi. Migogoro inaweza kuwa kati ya wahusika, familia zao, matabaka yao, au hata katika nyadhifa mbalimbali.
Vilevile migogoro yaweza kuwa ya kiuchumi, kijamii, mogogoro ya nafsi, na migogoro ya kisiasa ambayo hujitokeza katika mitazamo tofauti kulingana na mtiririko wa visa na matukio yanavyopangwa na mwandishi. Kwa kuanza
Mgogoro wa nafsi tunamuona Tumaini akipatwa mgogoro nafsi pindi alipofiwa na wazazi wake na baadae kug unduli kuwa walikuwa wamechuliwa ka vizuu na bibi ake na Leonila pia mgogoro nafsi wa pili ni pale ambapo leonila ankataliwa kuolewa na Tumaini anajikuta akiingia katika lindi la mgogoro nafsi. Pia Leonila anjikuta akiingia katika mgogo wa nafsi pindi pindi wazazi wake walipomwandalia mazingila ya kuolewa na tembo (uk. 15 & 39).
Mgogoro kati ya mtu na mtu Hapa tunaona mgogoro kati ya Anastazia pamoja na wazazi wake, Dennis na John, Dennis na Benadeta, Tumaini na Serikali,Kasala na mama yake.mfano. (uk. 22, 23 & 128).
-“Kumtunza mzee ni mzigo lakini inabibi uuchukue kwa fulaha” (uk. 23)
-“Baba nihurumie! Lakini Kasala aliendelea kumpiga.
Bibi wameniua kwa sababu yako!” (uk. 22).
Ujumbe/Mafunzo
Ujumbe: mwandishi anapoandika kazi yake huwa na ujumbe ambao hutaka uifikie jamii aliyoikusudia. Ujumbe katika kazi fasihi ni mafunzo mbalimbali ambayo hupatikana baada ya kusoma kazi ya fasihi. Katika kazi ya fasihi dhamira kuu hubeba ujumbe wa msingi na dhamira ndogondogo hubeba ujumbe ambao husaidia kuujenga au kuupa uzito zaidi ujumbe wa msingi. Baadhi ya ujumbe unaopatikana katika riwaya hii ni pamoja na:
Kikulacho kinguoni mwako: Huu ni ujumbe ama funzo tunalolipata baada ya kusoma riwaya hii, ujumbe huu tunaupata kupitia muhusika mama Resi pindi kwani alijifanya anampenda mmewe kumbe alikuwa na uhusia mwamume mwingine ambaye ni John rafiki yake na Dennis. (uk. 72)
Majuto ni mjukuu: Ujumbe huu unajitokeza pia katika riwaya hii, mwandishi anamtumia mhusika Tumaini pale alipoendekeza starehe zilimsababisha aingie kwenye mtego wa majambazi wa kupigwa na kuhalibiwa sura yake. (uk. 98)
Elimu ni ufunguo wa maisha: Mwandishi anatupa ujumbe mwingine kuwa, ili mtu aweze kufanikiwa hana budi kushikiria na kuizingatia elimu kwani elimu ni ufunguo wa maisha, ujumbe huu katika riwaya hii unajitokeza kwa muhusika Dennis ambaye alipata kazi nzuri sababu alikuwa amekwenda shule na kupata elimu ya kutosha.
“Nyumba ya Dennis ilikuwa ni kubwa sana. Ilikuwa na vyumba saba bila kuhesabu jiko lililokuwa mumo humo ndani” (uk. 60)
Mpende akupendaye asiyekupenda achana nae, ‘katika riwaya hii anaipa ujumbe jamii yake kuwa penda pale unapopendwa na si kumng’ang’ania tu mtu kwa kuwa moyo wako unataka tu kuwa naye, ujumbe huu tunaupata kupitia kwa muhusika Dennis alipogundua kuwa mke wake alikuwa na mapenzi ya uongo aliamua kuachana nae.
“Dennis alipofika nyumbani alipiga kerere nimemfukuza mbwa,Tumaini” (uk. 109)
Msimamo
Msimamo katika kazi ya fasihi, mawazo, mafunzo na falsafa ya msanii hubainisha msimamo wake kuhusu masuala mbalimbali ya kijamii. Msimamo ni ile hali ya mwandishi kuamua kufuata na kushikilia jambo fulani. Jambo hili huweza kukataliwa na wengi lakini akalishikilia tu. Msimamo ndio huweza kuwatofautisha wasanii wawili au zaidi wanaoandika kuhusu mazingira yanayofanana. Hivyo basi mwandishi anamsimamo kwamba mambo yote yanayotendeka katika ulingu huu ni sasawa na fujo tupu, kwani hata kama utajitahidi vipi kupambana na shida za ulimwengu huu matatizo yataendelea kukukabili mpaka umauti utakapokufikia.
Jina na jalada la kitabu
Tukianza na jina la kitabu, jina ni “Dunia uwanja wa fujo” linasadifu yale yaliyomo ndani ya kitabu kwani tangu mwanzo wa riwaya hii kuna matukio au fujo mbalimbali ambazo zimejitokeza fujo hizo ni kama vile umalaya, ulevi, uchawi pamoja na mengineyo mengi. Mfano suala la uchawi lidhihilika pale katika uk. 36 unasema “Tena alikuwa akilala ndani ya nyumba yako! Ndio maana mama yako alikuwa mchawi” (uk. 36).
Falsafa ya mwandishi
Kulingana na Mbunda Msokile yeye anasema kuwa Falsafa ni wazo ambalo mtu anaamimini lina ukweli Fulani unaotawala maisha yake pamoja na maisha ya jamii. Hivyo basi katika riwaya hii anaamini kuwa katika riwaya yake ya “Dunia ni uwanja wa fujo” Kwamba maisha hayana raha wala maana isipokuwa dunia ni uwanja wa fuzo.
Kufaulu kwa mwandishi
Mwandishi wa riwaya hii amefaulu kwa kiasi kikubwa kuibua dhamira dhamira mbalimbali katika jamii. Kwani dhamira hizo zimeonekana kuwa ni kikingamizi kikubwa cha katika maendeleo ya jamii. Mfano suala la uchawi na ushirikina , malezi mabaya, ukale na usasa. Pia mwandishi amefaulu katika suala zima la lugha kwani ametumia lugha rahisi na inayoeleweka kwa msomaji yeyote hata kama si msomi mkubwa.

Print this item

  BAADHI YA RIWAYA ZA KISWAHILI ZILIZOVUMA SANA TANZANIA (1)
Posted by: MwlMaeda - 08-27-2021, 04:17 PM - Forum: Riwaya - No Replies

Leo tujikumbushe baadhi ya Riwaya za Kiswahili zilizovuma sana Tanzania.

1.Siku ya Watenzi wote (1968) Shaaban Robert
2.Nyota ya Rehema (1978) M.S Mohamed
3.Dunia Mti Mkavu (1980) Said A.Mohamed
4.Rosa Mistika (1971) E.Kezilahabi
5.Alipanda Upepo Akavuna Tufani (1969) John N.Somba
6.Titi la Mkwe (1972) Alex Banzi
7.Kasri ya Mwinyi Fuad (1979) Shafi Adam Shafi
8.Kichwa Maji (1974)E.Kezilahabi
9.Kiu (1972)M.S.Mohamed
10.Tata za Asumini (1990)Said Ahmed Mohamed
11.Kifo cha Ugenini (1977)Olaf Msewa
12.Kaburi bila Msalaba (1971)M.Kareithi
13.Kuli (1976)Shafi Adam Shafi
14.Kwa Heri Iselamagazi (1992)B.Mapalala
15.Wimbo wa Sokomoko (1990)A.Lihamba
16.Ngome ya Mianzi (1991)M.M.Mulokozi
17.Ngoma ya Mianzi (1992)M.M.Mulokozi
18.Miradi Bubu ya Wazalendo (1992)G.Ruhumbika
19.Dunia Uwanja wa Fujo (1975)E.Kezilahabi
20.Adili na Nduguze (1952)Shabaan Robert
21.Kusadikika (1951)Shabaan Robert
22.Lila na Fila (1966)J.K.Kiimbila
23.Mbojo Simba-Mtu (1971)N.J.Kuboja
24.Mirathi ya Hatari (1977)C.Mung’ong’o
25.Nagona (1987)E.Kezilahabi
26.Mzingile (1991)E.Kezilahabi
27.Mafuta (1984)K.G.C.Mkangi
28.Mwisho wa Mapenzi (1972)Simbamwene J.
29.Kweli Unanipenda? (1978)Simbamwene J.
30.Jeraha la Moyo (1974)Kiango,S.D
31.Pete (1978)Komba,S.M
32.Kwa Sababu ya Pesa (1972)Simbamwene J.
33.Buriani (1975)F.Katalambula
34.Mtu Mwenye Miwani Meusi (1970)L.O.Omolo
35.Kifo Changu ni Fedheha (1972)S.J.Chadhoro
36.Tabu (1977)A.Komanya
37.Ufunguo wa Bandia (1979)Hmmie Rajab
38.Kikomo (1980)E.Musiba
39.Mzimu wa Watu wa Kale (1960)M.S.Abdulla
40.Kisima cha Giningi (1968)M.S.Abdulla
41.Duniani kuna Watu (1973)M.S.Abdulla
42.Siri ya Sifuri (1974)M.S.Abdulla
43.Mwana wa Yungi Hulewa (1976)M.S.Abdulla
44.Kosa la Bwana Msa (1984)M.S.Abdulla
45.Simu ya Kifo (1965)F.Katalambula
46.Muuaji ni nani? (1987)Simbamwene J.
47.Dimbwi la Damu (1984)Ben Mtobwa
48.Kijasho Chembamba (1980)Ganzel
49.Kikosi Cha Kisasi (1979)E.Musiba
50.Njama (1981)E.Musiba
51.Mpango (1982)K.M.Kassam
52.Tutarudi na roho Zetu? (1987)B.Mtobwa
53.Roho Mkononi (1984)Hammie Rajab

Print this item

  MAKUWADI WA SOKO HURIA (CHACHAGE S. CHACHAGE) KATIKA MUKTADHA WA RIWAYA YA KIHISTORIA
Posted by: MwlMaeda - 08-27-2021, 03:41 PM - Forum: Riwaya - No Replies

MAKUWADI WA SOKO HURIA (CHACHAGE S. CHACHAGE) KATIKA MUKTADHA WA RIWAYA YA KIHISTORIA KATIKA FASIHI YA KISWAHILI


Makuwadi wa Soko Huria (Chachage S. Chachage) katika Muktadha wa Riwaya ya Kihistoria katika Fasihi ya Kiswahili

Mugyabuso M. Mulokozi
Ikisiri
Miongoni mwa kazi bora za fasihi duniani ni zile zilizojikita katika matukio na/au mashujaa halisi wa kihistoria. Mifano mizuri ni tendi za Homer za Kiyunani, baadhi ya tamthilia za W. Shakespeare (k.m. Julius Kaisari), na riwaya mashuhuri za Kirusi za Pushkin na Leo Tolstoi. Katika fasihi ya Kiswahili, riwaya ya kihistoria haijaendelezwa sana. Miongoni mwa kazi zilizoinua kiwango cha riwaya ya kihistoria katika Kiswahili ni Makuwadi wa Soko Huria. Makala haya yataichambua riwaya hiyo katika muktadha wa riwaya ya kihistoria katika Kiswahili ili kuona mchango wa riwaya hiyo, na wa Chachage mwenyewe, katika kuuendeleza na kuukomaza mkondo huo wa uandishi wa kubuni.
_______________________________________
“Mtu huandika kitabu kimoja tu katika maisha yake.” Chachage S.Chachage
_______________________________________
“…katika kuandika historia isiyokuza ushujaa wa mtu au watu binafsi, Chachage amemkaribia mwandishi mashuhuri wa kimapinduzi, Maxim Gorky. Kwangu mimi, hili tu linatosha kumweka Chachage katika orodha ya wasanii stadi wa Tanzania, na wa Bara la Afrika” (Issa Shivji ,2002).
                        _________________________________________
1.0 Utangulizi Riwaya ya Makuwadi wa Soko Huria iliandikwa mwaka 1999-2000, na kuchapishwa mwaka 2002 na kampuni ya E & D. Katika mahojiano aliyoyafanya na Diegner (2004: 228), mwandishi anasema alitumia miaka mitatu (1996-1999) kufanya utafiti wa masuala yaliyomo katika riwaya hiyo. Muda huo mrefu wa utafiti ni ushahidi kuwa C.S. Chachage alikusudia kuandika kazi changamani na yenye mawanda mapana na kina cha kutosha. Makuwadi wa Soko Huria inazo sifa hizo na zaidi. Riwaya ya Makuwadi wa Soko Huria (baadaye Makuwadi) ilihakikiwa kwanza na Shivji (2000/2002) na baadaye Mbonde (2004). Tutazipitia kidogo tahakiki zao kabla hatujajikita katika uchambuzi wetu wa riwaya hiyo katika muktadha wa bunilizi za kihistoria katika Kiswahili.
Makala ya Shivji ni mapitio na utambulisho wa riwaya hiyo na inafanya mambo kadha muhimu: Inatupa mtazamo na mwelekeo wa kitabaka wa kisiasa-kiitikadi wa kuitazama riwaya hiyo, na hivyo kuonesha dhima na mchango wake katika kufafanua na kuendeleza harakati za wanyonge wa Tanzania na Afrika za kupambana na mifumo inayowakandamiza. Pili, tahakiki hiyo inabainisha vizuri mtanziko wa kimawazo na kivitendo wa tabaka la vibwanyenye wa Tanzania linalowakilishwa na wahusika Mjuba na Sifuni. Hili ni tabaka linaloyumba kati ya kukubali kuukumbatia ubepari na raha zake, au kujiunga upande wa mapambano na mawanio ya umma na karaha zake. Mtanziko huu, aliouelezea vizuri Amilcar Cabral mwaka 1966, bado haujasuluhika. Mchango muhimu wa makala ya Shivji ni kutupatia kiunzi cha kinadharia na kiitikadi cha kuitazama riwaya hiyo ya Chachage, maana haingii sana katika uchambuzi wa riwaya yenyewe.
Mbonde anafanya uchambuzi wa
kijadi wa riwaya ya Makuwadi kwa
kuzingatia vipengele vya dhamira, muundo na mtindo. Anabainisha dhamira muhimu
zinazojitokeza katika riwaya hiyo. Kwa upande wa muundo na mtindo, Mbonde
anaonesha kuwa Chachage anatumia kwa ufanisi mbinu-rejeshi; anachanganya
usimulizi na uandishi ili kuileta hadhira karibu na msimuliaji. Aidha, anatumia
lugha fasaha iliyosheheni tamathali, na anaonesha migogoro (labda hiki ni
kipengele cha maudhui kuliko mtindo). Mbonde anadhihirisha kuwa riwaya hiyo
inatumia historia kuakisi mapambano ya leo, na kwamba inashabihiana na ile ya
Alex Haley ya Roots (siyo The Roots) katika kupekua nasaba na
mahusiano ya kiukoo ya makabila mbalimbali ya kusini mwa Tanzania (suala la Roots kuwa riwaya nalo lina mjadala;
wengine huweza kudhani kuwa ni historia).
Kwa hakika wahakiki hawa wawili
wametupatia mahali pazuri pa kuanzia katika kuiangalia riwaya ya Makuwadi.  Makala haya hayakusudiwi kurudia yale
waliyokwishasema vizuri zaidi, bali tutajikita katika suala la Makuwadi wa Soko Huria kama bunilizi ya
kihistoria, jambo ambalo Shivji na Mbonde hawakulizungumzia sana kwa kuwa
halikuwa lengo lao. Chachage mwenyewe, katika mahojiano na Diegner
(tumekwishayataja hapo juu), analipa suala la historia uzito mkubwa kuhusiana
na riwaya yake. Lengo letu si kujadili sifa za riwaya ya kihistoria kidhahania,
bali kuonesha nafasi na umuhimu wa riwaya ya kihistoria katika kuibua riwaya
bora ya Kiswahili ya kimaendeleo, tukitumia Makuwadi
kama kielezo chetu.
2.0
Riwaya ya Kihistoria katika Fasihi ya Kiswahili
Riwaya ya kihistoria ni hadithi
ndefu ya kubuni iliyojikita katika matukio ya kweli ya historia, hasa yaliyo
muhimu kwa taifa au jamii inayohusika, kuyachanganya na matukio ya kubuni, na
kuyapangilia upya kisanii ili kutoa ujumbe fulani kwa jamii inayoandikiwa.  Riwaya ya kihistoria huwa ni jaribio la
kuoanisha mgogoro wa kihistoria na mgogoro wa kisanaa (k.m. wa kibinafsi),
ukweli wa kihistoria na ukweli wa kisanaa, na viumbe wa historia na viumbe wa
sanaa, ili kujenga simulizi yenye maana, ujumbe maridhawa na kumbukumbu ya
kudumu kwa walengwa (Lukacs, 1962; Mulokozi, 1990).
Masimulizi ya kihistoria si jambo
geni katika utamaduni wa Waswahili na Waafrika kwa jumla. Kila jamii
huwasimulia watoto wao juu ya matukio ya zamani yanayowahusu, hususani yale
yanayohusu chimbuko lao, namna walivyofika mahali walipo sasa, harakati
walizozipitia, mahusiano yao na majirani zao, na mapambano yao na maadui zao.
Masimulizi hayo huweza kuwa ni historia ya moja kwa moja, hasa kuhusiana na
matukio ya siku za karibuni, au historia iliyochanganyika na visakale
(kuhusiana na matukio ya zamani zaidi) au visakale vilivyochanganyika na
visasili (kuhusiana na matukio ya kale sana). Historia halisi husahaulika na
kuingia katika kumbo la visakale na visasili kwa kadiri muda unavyopita.  Hiyo ni tabia ya kawaida ya simulizi za
mdomo.
Katika fasihi ya Kiswahili,
simulizi za kihistoria zimekuwapo tangu kale. Vitabu vya Tarihi vinatupa simulizi zilizoandikwa kutokana na mapokeo ya
mdomo, hususani zile zinazowahusu watawala. Ni vitabu vyenye historia finyu
kulingana na malengo yake ya kuhifadhi habari za nasaba za watawala. Masimulizi
ya kihistoria yenye mapana na taarifa zaidi ni yale ya kishairi – hasa yale
yanayopatikana katika tendi. Ya zamani zaidi yanamhusu shujaa Liyongo, na
yalitolewa kwa njia ya nyimbo na mashairi, na pia tendi-simulizi ambazo sasa
zimepotea (Steere, 1870). Zipo pia tendi mashuhuri za miaka ya karibuni, kwa
mfano Utenzi wa  Vita
vya Wadachi Kutamalaki Mrima (Hemed Abdallah, 1895) na Vita vya Maji Maji (Abdulkarim Jamaliddini, 1910; TUKI, 2006),
zinazohusu mapambano ya wananchi kupinga uvamizi na utawala wa Wadachi, na Utenzi wa Vita vya Uhuru (Robert, 1961)
unaosimulia matukio na mwenendo wa Vita vya Pili vya Dunia. Sambamba na tenzi,
zimechapishwa tamthilia kadha za kihistoria tangu miaka ya 1960. Baadhi yake
ni: Kinjeketile (Hussein, 1969) na Mashetani (Hussein, 1971); Mkwawa Mahinya (Nkwera, 1968), Mukwava wa Uhehe (Mulokozi, 1979) na Harakati za Ukombozi (1982).
Ubunilizi wa kihistoria katika
umbo la riwaya hauna historia ndefu kama ulivyo katika ushairi. Kitabu cha Habari za Wakilindi (Ajjemy, 1895)
kinafikiriwa na baadhi ya watu kuwa ndicho riwaya ya kwanza ya Kiswahili. Hata
hivyo, dai hili lina walakini, kwani mtunzi wa masimulizi hayo hakuyakusudia
yawe riwaya, bali aliamini kuwa alikuwa akiandika historia ya Wakilindi,
hususani utawala wa nasaba ya kina Kimweri huko Usambara. Visasili na visakale
vinavyojipenyeza katika masimulizi hayo haviondoi ukweli kuwa yale ni
masimulizi ya kihistoria yanayotokana na simulizi za mdomo na matukio ya
kushuhudiwa na mwandishi mwenyewe, na kwamba mtindo uliotumika ni wa taaluma ya
kijadi ya usimulizi wa historia isiyopambanua visakale na historia halisi.
Hivyo tunaweza kusema kuwa riwaya
halisi ya kwanza ya historia ni ile ya James Mbotela ya Uhuru wa Watumwa (1934). Riwaya hiyo inasimulia juu ya masaibu ya
mateka waliochukuliwa utumwani na baadaye kukombolewa na meli ya Wazungu katika
miongo ya mwisho ya karne ya 19. Mengi yanayosimuliwa ni matukio ya kweli ya
kihistoria, japo bila shaka hapa na pale mtunzi katia chumvi kwa malengo ya
kisanaa. Baada ya hapo hapakutokea riwaya ya kihistoria tena hadi miaka ya 1970.
Baada ya mwaka 1970 riwaya ya
kihistoria katika fasihi ya Kiswahili imejitokeza kwa dhati zaidi. Riwaya ya
Msewe ya Kifo cha Ugenini
iliyochapishwa mwaka 1977 ilihusu kipindi cha uvamizi wa Wadachi  – kipindi ambacho kwa hakika ndicho
kilichohamasisha  kazi nyingi zaidi za
simulizi za kihistoria. Baadaye zilichapishwa riwaya mbili za.Shafi; Kuli (1979) na Kasri ya Mwinyi Fuad (1978). Riwaya hizo zilizohusu migogoro ya
kijamii-kitabaka huko Zanzibar kabla ya mapinduzi ziliisogeza mbele riwaya ya
kihistoria. Riwaya za Kezilahabi za Dunia
Uwanja wa Fujo (EALB, 1975) na Gamba
la Nyoka (EAPL, 1979) vilevile zina sifa fulani za uhistoria, hasa zile
zihusuzo mchakato wa ujenzi wa Ujamaa katika Tanzania katika miaka ya
1967-1977, japo haziingii moja kwa moja katika mkondo huo.
Riwaya za Kezilahabi zilifuatiwa
na riwaya za Said Ahmed Mohamed na M.S. Mohamed za Nyota ya Rehema (Mohamed 1978), na Dunia Mti Mkavu (Ahmed, 1980).
Hizo nazo zina sifa kadha za uhistoria, maana zinaonesha migogoro ya
kijamii-kitabaka ya kipindi cha kabla ya Mapinduzi nchini Zanzibar. Na ingawa
riwaya hizo zilitoa mchango mkubwa katika kuitajirisha na kuikomaza riwaya ya
Kiswahili, bado fani ya riwaya ya kihistoria, hadi mwaka 1990, ilikuwa bado
haijaenea sana.
Kutokana na hali hii, mwishoni mwa
miaka ya 1980 jopo dogo la wapenda fasihi, likiratibiwa na Bi. Elieshi Lema,
ambaye wakati huo alikuwa mhairiri katika Shirika la Uchapishaji Vitabu la
Tanzania (TPH), lilianza kukutana nyumbani kwa Bi. Lema mara mbili kwa wiki saa
za jioni kujadili na kupanga namna ya kustawisha riwaya ya kihistoria kwa
Kiswahili, hususani kwa ajili ya wasomaji vijana. Wanajopo walikubaliana wao
wenyewe waandike riwaya kama tano za kihistoria zenye kuzingatia matukio
yafuatayo: 1. Biashara ya Watumwa (mwandishi A. Lihamba); 2. Vita vya Wahehe
dhidi ya Wadachi (mwandishi M.M. Mulokozi); 3. Vita vya Wachagga dhidi ya
Wadachi – Mangi Meli – (mwandishi: R. Mabala), na Vita vya Maji Maji (Mwandishi
E. Kezilahabi). Wanajopo waligawiana kazi na kuanza kuandika. Walipata msaada
mdogo kutoka shirika la Kanada la Misaada ya Maendeleo kupitia Elimu (CODE)
ambalo wakati huo kiongozi wake wa ofisi ya Afrika ya Mashariki alikuwa Scott
Walter. Afisa huyo alitoa msukumo mkubwa uliowawezesha wahusika kufanya utafiti
mdogo wa uwandani kuhusiana na mada hizo. Kutokana na mchakato huo, kufikia
mwaka 1991 miswada viwili ya hadithi za historia kwa picha na maelezo
mafupimafupi ilipatikana: Miswada hiyo ni Wimbo
wa Sokomoko (A. Lihamba) kuhusu biashara ya watumwa; na Ngoma ya Mianzi (M.M. Mulokozi) kuhusu
uvamizi wa Wadachi huko Kilosa, uliofuatiwa na vita vya Lugalo vya 1891.
Punde ilionekana kuwa shughuli ya
kuandika vitabu kwa ajili ya watoto na vijana ilikuwa nzito, na huenda
isingewezekana kuratibiwa na Bi. Lema na shirika la CODE, kwa ufanisi bila kuwa
na chombo mahsusi cha kudumu. Ikapendekezwa na kukubaliwa kuwa uanzishwe Mradi
wa kuratibu shughuli hiyo ambao awali ungegharimiwa na CODE. Huo ukawa ndio
mwanzo wa kuzaliwa kwa Mradi wa Vitabu vya Watoto Tanzania (Children’s Book Project – CBP) mwaka
1991. Vitabu viwili vya jopo hili vikawa miongoni mwa machapisho ya mwanzo ya
Mradi huo. Hivi leo jopo hilo halipo tena, na riwaya kuhusu Mangi Meli na Vita
vya Maji Maji hazijaandikwa, lakini Mradi umekua na kuzaa vitabu vingi zaidi
(kama 300) na shughuli nyingi zaidi, zikiwamo za kuratbu usomaji shuleni.
Juhudi za CBP
ziliwezesha kuchapishwa kwa riwaya tatu za kihistoria kwa Kiswahili kwa ajili
ya vijana zilizoandikwa na M.M. Mulokozi. Riwaya hizo ni: Ngome ya Mianzi (1990), Ngoma
ya Mianzi (1991) na Moto wa Mianzi
(1996). Lengo lake  lilikuwa ni kuwapa
vijana mwamko wa kupenda kusoma na kutafiti historia ya jamii zao kama njia
mojawapo ya kujenga mapenzi kwa nchi (uzalendo) na chuki kwa adui, kujiamini na
kujithamini. Bahati mbaya si waandishi wengi katika Mradi waliojitokeza
kuendeleza mkondo huu wa uandishi, isipokuwa Dumea aliyeandika novela ya Usiku wa Balaa (E&D, 2009).
.
Nje ya Mradi, uandishi wa riwaya
ya kihistoria ulifikia hatua ya juu ilipochapishwa riwaya ya Bernard Mapalala
ya Kwa Heri Iselamagazi (TPH 1992).
Riwaya hiyo ilitupeleka katika historia ya Mtemi Mirambo na warugaruga wake
katika muktadha wa ujenzi wa himaya ya Kinyamwezi kwenye karne ya 19. Ni riwaya
nzuri ambayo haijapata kutendewa haki (kwa kuchunguzwa kitaaluma na kutumika
kwa mapana) na wahakiki, watafiti na wakuza mitaala. Iselamagazi ilifuatiwa na riwaya mbili za Shafi: Vuta N’kuvute (1999) na Haini (2003). Zote mbili zinahusu
matukio yenye maana kubwa kwa majaaliwa ya Zanzibar na Wazanzibari, na
zinatuingiza katika undani wa matatizo ya mapinduzi ya Zanzibar ambayo
yaliwageuka wale waliojitoa muhanga kuyatengeneza.  Suala la utawala wa chuma (ambao dola
inajaribu kuuhalalisha kwa kurejelea historia ya mapinduzi) dhidi ya haki za
binadamu linachanganuliwa vilivyo katika riwaya ya Haini. Riwaya nyingine ya kipindi hiki iliyojaribu kusawiri
historia ya Tanzania kisanaa ni ile ya Miradi
Bubu ya Wazalendo. (1995). Riwaya hiyo, kama ile ya Kiingereza ya M.
Vassanji The Gunny Sack (1989),
ilijaribu kusimulia kisanaa historia ya Tanganyika/Tanzania tangu enzi za
ukoloni hadi kudai uhuru na ujenzi wa ujamaa, hadi kushindwa kwa ujamaa na
kustaafu kwa Mwalimu J.K. Nyerere. Kama riwaya ya Vassanji, riwaya hii inatumia
wahusika wa kutoka makundi mbalimbali ya kijamii-kitabaka ili kuonesha
majaaliwa ya makundi hayo katika Tanzania “huru”. Tunaoneshwa kuwa wafanyakazi
wa kawaida na wakulima hawakunufaika na sera za Ujamaa; walionufaika zadii ni
tabaka jipya la vibwanyenye wa dola (kina Nzoka) na wafanya biashara. Kama
anavyoeleza Mbonde (2004) kwa usahihi, ni vizuri kuisoma riwaya hii sambamba na
riwaya ya Makuwadi wa Soko Huria,
maana maudhui yake yanakamilishana.
Kwa jumla tunaweza kusema kuwa
miaka ya 1990 utanzu wa riwaya ya kihistoria katika fasihi ya Kiswahili umekua
na kujipatia nafasi muhimu katika historia ya fasihi hiyo. Riwaya ya Makuwadi wa Soko Huria imetokea katika
muktadha huu wa kifasihi. Lakini, tofauti na riwaya zilizotangulia, Makuwadi imepanua mawanda na kutazama
hata nje ya Tanzania katika kujaribu kulifafanua tatizo kuu la kitaifa la enzi
zetu.
Kama wanafasihi waliomtangulia,
Chachage alifahamu umuhimu wa historia katika harakati za maendeleo na ukombozi
wetu. Alijua kuwa kosa kubwa mojawapo linalofanywa na matabaka tawala ya sasa
ya Afrika ni kudharau au kupuuza historia. Baadhi yamediriki hata kufuta somo
la historia katika mitaala ya shule (mfano: Tanzania wakati wa Awamu ya Tatu),
na mengi bado yanafundisha historia iliyoasisiwa na mkoloni – ile ya ustaarabu
wa mzungu na jusura zake katika bara la Afrika. Riwaya hii inatuonesha kuwa
kudharau historia ni hatari, kwa kuwa ni kukinyima kizazi kipya haki ya
kujitambua na kujua tulikotoka, tulipo na tuendako. Bila kujua matatizo yetu ya
kihistoria ya nyuma na ya leo, ni vigumu kubuni njia sahihi ya kufuata kwa siku
zijazo.  Maana adui wetu wa zamani, wa
sasa, na wa kesho bado ni yuleyule, na mbinu zake hazijabadilika sana.
Tunaposahau historia tunaishia kumkumbatia adui huyo tukidhani ni rafiki, na
madhara tunayoyapata katika uhusiano wetu naye yanazidi kuongezeka.
Riwaya ya Makuwadi wa Soko Huria inajaribu kuturudisha nyuma katika mizizi ya
kihistoria ya matatizo yetu ya leo ili historia hiyo iwe ni mwega wa
kutuwezesha kusonga mbele katika mapambano yetu ya kudumu ya kutafuta ukombozi
kamili na maisha bora kwa ajili ya jamii zetu. Katika kufanya hivyo, Chachage
anaturudisha katika jadi bora ya wahenga wetu ya kuhifadhi historia na
kuipokeza kwa vizazi vyao; jadi ambayo ilipigwa vita na ikakaribia kuuliwa na
tawala za kikoloni na asasi zake kwa kuwa zilitambua fika hatari za mwamko wa
kihistoria wa wenyeji kwa utamalaki wao.
Kwa ufupi, huu ndio muktadha wa
kifasihi uliochipuza riwaya ya Chachage ya Makuwadi
wa Soko Huria.  Sasa tuiangalie
riwaya yenyewe.
3.0 Makuwadi
wa Soko Huria
Riwaya ya Makuwadi wa Soko Huria iliandikwa na hayati Chachage S. Chachage
mwaka 1999-2000 na kuchapishwa na E &
D Publishers mwaka 2002. Hii ndiyo riwaya ya mwisho inayofahamika
aliyoiandika Hayati Chachage kabla hajafariki mwaka 2006, ingawa katika
mahojiano yake na Diegner anasema wakati huo (2004) alikuwa amemaliza kuandika
sura kama mbili za riwaya nyingine. Riwaya hii iliandikwa wakati wa kipindi cha
ukomavu wa utandawazi wa Kimagharibi na Kimashariki katika Tanzania na Afrika,
kuvamiwa kwa uchumi wa Tanzania na “wawekezaji”, pamoja na mawakala wao wa
kidini na kitamaduni kutoka Magharibi na Mashariki, kuundwa kwa utatu usio
mtakatifu wa mabepari wenyeji, mabepari wa kigeni, na viongozi wa serikali ili
kushirikiana kupora rasilimali za nchi,
na hivyo kujigeuza kwa tabaka la watawala kuwa mafisadi wakubwa na mawakala
wa ubepari wa kigeni dhidi ya wananchi. Mchakato huu uliambatana na
kufukarishwa kwa wananchi walio wengi kutokana na kufungwa kwa viwanda,
kufukuzwa kwa wakulima, wafugaji na wavuvi katika maeneo yao ya jadi ili
kupisha “wawekezaji”,  kutelekezwa kwa
watoto wa maskini katika mfumo wa elimu (kuwapa baadhi yao mikopo ya elimu
badala ya ruzuku), na kuvurugika kwa vyama vya ushirika na bei za mazao ya
wakulima wadogowadogo. Mwenendo huu ulimwudhi sana Chachage, ambaye aghalabu
alikuwa akiandika makala na kuhutubia kuhusu utandawazi, ambao aliuita
“utandawizi.” Riwaya yake ya Makuwadi wa
Soko Huria ilikuwa ni mwendelezo wa mapambano yake dhidi ya ubepari na
utandawazi katika medani ya kifasihi.
3.1 Muhtasari wa Riwaya
Hadithi inaanza na “kifungua
pazia” ambacho kinaelezea kuhusu kutekwa kwa Mjuba na Sifuni (ambao ni
waandishi wa habari) na kundi la Kaboko kutokana na kuandika habari zenye
kufichua njama za kukwepa kulipa kodi. Inamalizika na “kifunga-pazia” ambapo
kesi ya kutekwa kwa Mjuba na Sifuni imepanuka na kuwa kesi ya mauaji yenye
kuhusisha masuala mengi na watu wengi, wakiwamo watu wakubwa katika uchumi na
utawala. Baina ya “kifungua-pazia” na “kifunga pazia” kuna sura 12 zenye
masimulizi kuhusu maisha, masaibu na mahusiano ya wahusika wakuu wa hadithi:
Fidelis, Mjuba, Sifuni na Binti Wenga; na wahusika muhimu wengine –  kina Amina,
Japhet Lupocho,  Joshua Lupocho,
Mooney, Alibhai, Chaurembo, Sorrenson, Sadiki Mazengo, Hakimu Mazengo, Mzee
Mrisho, Mzee Miraji, na Mzee Abdurahaman. Maisha na masaibu yao yanapambanishwa
na yale ya wananchi wa vijijini (Delta ya Rufiji na Ruhimba) kwa upande mmoja,
na mizengwe na vitendo vya mabepari wa kimataifa na mawakala wao wa ndani kwa
upande mwingine. Waandishi wa habari wanakuwa ndio kiungo na kioo cha kumulikia
uhusiano wa kihasama uliopo kati ya pande kuu mbili: upande wa wananchi
(wakulima, wavuvi, wafugaji) na upande wa mabepari wa dunia au watandawazaji
(wawekezaji, wahisani, “wataalamu”) na “Makuwadi” wao wa ndani.
Waandishi wa habari za mazingira
wenye mwelekeo wa kimaendeleo: Fidelis, Mjuba, Sifuni na Saada wanaamua kwenda
Rufiji kufuatilia suala la “Mradi wa Kamba” Rufiji, hususani baada ya
kuhudhuria Mkutano wa Wanarufiji uliofanyika Dar es Salaam kujadili Mradi
huo.  Wanaahidiwa msaada wa fedha na
wahisani kupitia kwa Sorrenson, afisa wa Kiswidi mwenye kazi ya kuratibu suala
hilo.
Safari ya Mjuba na wenzake
inawekewa vikwazo na Wizara ya Misitu na wawekezaji ambao hawataki habari za
mipango yao na mapambano yao na wananchi huko Rufiji zifahamike. Hata hivyo,
waandishi wa habari wanafanikiwa kufika Rufiji katika kijiji cha Nyamisati na
kupokewa kwa uhasama na viongozi wa kijiji hadi wanapodhihirisha kuwa wao wako
upande wa wananchi na wala hawakutumwa na wawekezaji au serikali. Wanaelezwa
masuala yote yanayohusu Mradi wa Kamba na uchumi wa delta wa mikoko na uvuvi,
na wanatembezwa katika visiwa mbalimbali kujionea wenyewe hali ilivyo.
Wanaelezwa pia historia kuhusu maisha na mapambano ya wananchi wa delta na
Tanzania nzima kupinga uvamizi na unyonyaji wa wageni.
Safari hii inatokea pia kuwa ni ya
ugunduzi kwa Fidelis, ambaye anakutana na ndugu zake waishio Rufiji ambao
alikuwa hawafahamu. Ni safari ya utakaso pia kwa wale walioikosea jamii – ama
kwa usaliti ama kwa kuvunja miiko. Wanarejea Dar es Salaam huku Fidelis akiwa
ameufahamu ukoo wake na akiwa ameandamana na baadhi ya ndugu zake wa Rufiji.
Safari hii ya Rufiji ya kusaka
habari na ufahamu kutoka kwa wananchi kuhusu matatizo yao ndiyo mkondo mkuu wa
hadithi. Mikondo mingine inahusu hadithi binafsi za wahusika wakuu, hasa
Fidelis, Mjuba, Sifuni, Amina, Binti Wenga, Japhet Lupocho,  Joshua Lupocho, Paul Mooney, Alibhai,
Chaurembo, Sorrenson, Sadiki Mzengo, na wengine. Masimulizi kuwahusu watu hawa
na wasifu wao na matazamio yao yanatuingiza katika undani wa mahusiano na hisia
zao za mapenzi na za chuki, za upevukaji wao kwa kadiri hadithi inavyoendelea,
hadi kufikia hatua ya baadhi yao kujitambua wao ni nani  (Japhet, Fidelis, Joshua, Amina), baadhi
kubadilika kimtazamo (Sorrenson, Japhet, Salama – mkewe Mjuba, na Oscar Mayowe
– mzinzi anayegeuka mlokole), na baadhi kuathirika kisaikolojia kutokana na
aibu ya usaliti na uvunjaji miiko hadi kufikia hatua ya kujaribu kujiua
(Japhet).
Hatimaye tunaona mabadiliko
mwishoni mwa hadithi: baadhi ya waovu wanaadhibiwa, wema wanatunukiwa, na
mshikamano wa wananchi na “wasomi” wapenda maendeleo unakuwa umejengeka na
kuimarika. Tunabaki na hisia kuwa msingi wa mapambano yajayo tayari umejengeka,
na kwamba “Makuwadi” na mabwana zao watakuwa na kazi ngumu sana katika
kuendeleza ajenda yao yenye madhara kwa wanyonge.
3.2 Mawazo Makuu
Muhtasari huu unaonesha kwamba
mgogoro wa riwaya hii una pande tatu: Upande wa wananchi wa Rufiji na Ruhimba
ambao ndio waathirika wa mfumo wa ubinafsishaji na uhuria unaosimikwa; upande
wa wawekezaji na mabepari wa kigeni na mawakala wao wenyeji (wa kisiasa na wa
kibiashara), ambao ndio wanaopambana na wananchi kwa sera na vitendo vyao; na
upande wa waandishi wa habari, ambao wako katikati na wamegawanyika kati ya
wale wanaowatetea wananchi (Mjuba, Sifuni, Fidelis) na wale wanaowatumikia
maadui wa wananchi (Mwenerumango, Jonathan Massawe, na Alhaji Seif Said). Kundi
hili la waandishi linawakilisha kundi au tabaka dogo la wasomi na vibwanyenye
uchwara kwa ujumla, na mgawanyiko wao unaakisi mgawanyiko halisi ndani ya
tabaka hilo miongoni mwa Watanzania. Hata hivyo, tabaka hili ndilo lenye jukumu
la kuuchunguza na kuuelezea mwenendo wa kijamii na mivuvumko iliyomo,
kutuonesha mahusiano ya kihasama ya makundi ya kijamii,  kiini chake na mustakabali wake. Hivyo
tunaiona jamii ya Watanzania na migogoro yake kupitia katika macho, mawazo,
uwezo na udhaifu wa kundi hili. Mipaka ya muono wa kundi hili la waandishi wa
habari ndio unaojenga mipaka ya muono wa riwaya hii. Je, kwa nini Chachage
kalichagua tabaka hili, ambalo aghalabu hulegalega kimsimamo na bila shaka lina
ufinyu wa kimawazo, liwe jicho letu la kuiangalia jamii yetu? Hatujui; labda
kwa kuwa yeye mwenyewe, akiwa ni msomi na mtafiti, alikuwa katika kundi hili,
au uhusiano wake na wale aliowatafiti (wakulima na wavuvi) haukuwa tofauti na
wa wahusika hawa na wananchi wanaoandika habari zao.
Mwandishi anatuonesha kuwa
ubinafsishaji na uhuria si sera zilizobuniwa na watawala wetu hivi karibuni,
bali zina mizizi yake katika historia ya kutawaliwa kwetu, ya ubeberu, ambao
kwa sasa ndio unaoitwa utandawazi. Hivyo, kupitia kwa mhusika Fidelis
Msakapanofu anatushauri turejee huko kwenye mizizi iwapo tunataka kuielewa
vyema tanzia ya Mwafrika wa leo:
“Kwa nini usianzie mwanzo wa hayo mambo, kule
yalikoanzia? Lakini, akili inaniuliza, mwanzo huo ndio upi?” (uk. 50)
Binti Wenga, na wazee wengine,
kina Mzee Mrisho, Mzee Abdurahaman na Mzee Miraji, na Bi. Khadija, wanaletwa
katika masimulizi haya wakiwa na jukumu la kuturejesha huko tulikotoka, kutupa
historia ya mababu na mabibi zetu, ya namna tulivyovamiwa na kuporwa tangu enzi
za biashara ya watumwa na ukoloni wa Wadachi na Waingereza, na mwitiko wa hao
wahenga  wetu kwa ubeberu wa wakati wao.
Riwaya, kupitia masimulizi ya
wazee hao, inatuonesha kuwa uporaji wa ardhi na maliasili za nchi hii ulianza
mapema kabisa, na ulifanywa na Wazungu na wengineo kwa zaidi ya miaka mia, na
kwamba wananchi, ambao kabla ya hapo walikuwa na maingiliano na uhusiano mzuri
wa kibiashara na kijamii, walivurugwa na ukoloni na kutenganishwa na kugeuzwa tribes. (Neno la Kiingereza “tribe”, kwa
namna walivyolitumia, halimo katika lugha ya Kiswahili, na si tafsiri ya neno
“kabila.” Tribe linabeba dhana ya
dharau na matusi ambayo haimo katika neno “kabila”). Hata hivyo, wananchi
wenyewe waligundua njama hizo za kuwagawa mapema na wakaamua kuungana ili
kupambana na adui yao.  Matokeo ya
mchakato huo yalikuwa ni Vita vya Maji Maji.
Mto wa Rufiji na matawi yake,
ambao sasa unaporwa na wageni, kina Mooney na Vangalatus, ukawa ndio kiungo
kikuu cha wananchi na barabara kuu iliyopeleka ujumbe wa ukombozi hadi pembe
zote za kusini mwa Tanzania:
Tulikuwa tunasafiri katika mto ambao maji yake
yalikuwa yamesafiri zaidi ya maili mia nne, mto mkubwa kuliko yote nchini ambao
sehemu kubwa ya maji yake yalitokea mto Ruaha ulioanzia Mbeya, mto Kilombero
ambao ulianzia sehemu za Njombe kama mto Ruhuji na mto Luwengu ulioanzia sehemu
za Ruvuma. Mto huu uliwaunganisha watu wa sehemu mbalimbali, nao wakajihisi
kwamba ni wamoja, na labda ilikuwa ni kwa sababu hii, watu wote wa sehemu hizi
waliungana pamoja wakati wa vita vya Maji Maji (uk. 219).
Hadithi hii ni kielezo cha picha
hii ya muungano wa watu kufuata Mto Rufiji: inahuisha, kupitia kwa wahusika
wakuu wa familia za kina Lupocho Msakapanofu, Wenga, na Nguvumali, muungano huo
wa Maji Maji wa jamii za kutoka Uzaramo hadi Rufiji hadi Ubena (Njombe), Songea
mpaka Mbamba Bay. Huu ni mtandao unaounganisha jamii za Wazaramo na nyinginezo
za upwa wa Mzizima kama vile Wandengereko, Wamatumbi, Wangindo, Waluguru,
Wamakonde, Wamakua, Wangoni, Wabena, Wapangwa, Wandendeule, Wamatengo, Wakinga,
n.k. Ni muungano unaojumuisha watu wa imani mbalimbali – za jadi na Uislamu.
Familia ya kina Lupocho ni kielezo cha muungano huu:  mababu na mabibi zao kutoka Mbamba Bay
(Msakapanofu na Wenga Mhalule) walikutana katika harakati za mapambano na wazee
wa Rufiji (Nguvumali na Samadi) na baadaye watoto wao wakaoana na kuzaa wana na
wajukuu ambao walisambaa kwenda kuishi Rufiji, Songea, Njombe, Tabora na Dar es
Salaam, na wakawa hawafahamiani. Hatimaye ndugu hao wanakutanishwa tena na
harakati za kupinga ufugaji wa kamba Rufiji na uuzaji wa ardhi Ruhemba. Baadhi
yao (Japhet na Amina) wanataka kuoana bila kujua kuwa ni ndugu, na wanapogundua
udugu wao inabidi lifanyike tambiko la utakaso). Hivyo historia ya familia hii
imebeba historia ya nchi na misukosuko yake.
Hivyo basi tunaweza kusema kuwa
riwaya hii ni istiara ya vuguvugu la ukombozi la Maji Maji katika mazingira ya
leo: kutoka Rufiji hadi Ungoni hadi Mbamba Bay. Ni kama mwandishi anataka
kutuambia kuwa kama ambavyo babu zetu waliungana bila kujali mipaka, lugha au
kabila ili kupambana na ukoloni, sisi wajukuu zao pia tunawajibika kufuata
mfano wao na kuungana ili kupambana na utandawazi unaokuja katika umbo la
uhuria, uwekezaji wa kigeni, ubinafsishaji na ukuwadi.  Mto wa Rufiji uwe ni kiungo chetu kama
ulivyokuwa enzi za Maji Maji.
Ukombozi huu, kwa mujibu wa riwaya
hii, sharti ujengwe katika utaifa mpana ambao unavuka mipaka ya kabila, na hata
taifa, na kuwa Upanafrika (Umajumui wa Afika). Maana Afrika ni moja na Waafrika
ni watu walewale popote pale walipo. Mawazo ya Mjuba huenda yanawakilisha
mawazo ya mwandishi: Wakombozi wa kweli wa nchi yetu hawakuipigania Tanganyika
tu, bali mama Afrika:
Hao walikuwa watu kama akina Dennis Phombeah, akina
Austin Shaba, akina Oscar Kambona, na wengine – watu waliomjua mama mmoja tu
bila kujali kama walizaliwa wapi. Naye alikuwa mama Afrika (uk. 213).
Sentensi ya mwisho inakuwa na
maana zaidi tunapokumbuka (kwa wale wenye kufahamu) kuwa baadhi ya mashujaa
walioipigania Tanganyika anaowataja Chachage, kwa mfano Eric Fiah na Osare
Otango, hawakuwa Watanganyika. Osare Otango, ambaye aliendesha mapambano huko
Tanga dhidi ya walowezi, alikuwa Mmaragoli wa Kenya.
Hivyo riwaya hii inatusogeza mbele
na kutupeleka kwenye dhana ya umoja wa Afrika iliyohubiriwa na kina William du
Bois, George Padmore, Kwame Nkrumah na Julius Nyerere.
Uhuria ni zao la utandawazi, na
unakuja na sura mbalimbali. Kuna sura ya uchumi – ubinafsishaji na uwekezaji wa
kigeni. Wananchi wananyang’anywa ardhi na maeneo yao, wanapewa wawekezaji
kutoka nje. Kuna utalii – mbuga za wanyama zinabinafsishwa, wanyama wanauliwa
kwa ajili ya starehe za wawindaji matajiri kutoka Magharibi (Rais Roosevelt),
na kuna udini – makanisa ya kilokole (bila shaka kutokea Marekani) yanaenezwa
nchi nzima na kuwateka na kuwapumbaza watu. Ndoa ya Mjuba na Salama inavunjika
kutokana na kuokoka kwa Salama. Na haya yote yanawezekana kwa kuwa wapo watu –
wenyeji, wafanyabiashara na wanasiasa, ambao wako tayari kununuliwa na wageni
na kuiuza nchi kwa manufaa yao binafsi. Kina Japhet Lupocho, Chaurembo,  Jonathan Massawe, Moddy Mwenerumango,
Alibhai, Njovu Luhala – Mbunge, wako katika mkumbo huo. Hao ndio wanaoitwa Makuwadi,
yaani “washenga-nuksi” wanaosaidia kufanikisha mipango ya waporaji wa kigeni
hapa nchini.
Mh. Luhala anawakilisha wanasiasa,
na tunaona namna anavyoshiriki katika kuuza/kubinafsisha ardhi ya wananchi huko
Ruhimba, na anavyokataa kukutana nao wanapokuja kumwona Dodoma. Hatimaye,
wabunge wanapokubali kukutana na wananchi, wanadai posho, na wanapoona hakuna
posho, wanataka mkutano uishe haraka ili wawahi nyama choma mnadani!
Uhuria unaambatana na ufisadi.
Rushwa, ukwepaji kodi, magendo, uuzaji wa madawa ya kulevya, usaliti na
upotoshaji wa habari vimetawala. Mtandao wa ufisadi unawahusisha kina Alfred
Chaurembo (kupitia mashirika yasiyo ya kiserikali-NGOs), Roshan Alibhai, A.
Kongoro, K. Kongoro, Maua Mutabingwa na Sadiki Mazengo. Pia, Wazungu wa
mashirika ya “hisani” wanaishi kwa anasa kwa kutumia misaada ya wakimbizi (uk.
185).
Kuna uharibifu mkubwa wa
mazingira; wawindaji wanateketeza wanyama wa pori (Roosevelt, Pretorius na
Louis); mikoko katika delta inakatwa bila mipangilio; samaki wanavuliwa na
kuuliwa ovyo.
Kuna unyanyasaji wa wanawake, na
mwenendo wa kuwanyima haki yao ya ardhi. Wanawake wa Ruhimba wananyang’anywa
ardhi yao na uongozi wa wilaya bila malipo wakati wanaume wanalipwa (uk. 45).
Kwa wananchi, uhuria huu
unaonekana kuwa wa bandia kwa kuwa unawanyang’anya wananchi haki yao na
kuwakabidhi wageni badala ya kuruhusu ushindani halali ambao unapaswa kutoa
nafasi kwa ushirikiano pia miongoni mwa umma (uk. 199). Mzawa wa Rufiji
anayeleta mitambo yake kuwekeza pale Rufiji anakataliwa na serikali wakati
mgeni (Mgiriki) anakubaliwa.
Kwa jumla, tunaweza kusema kwamba
riwaya hii inasawiri dhana ya uhuria na madhara yake kwa wananchi wa kawaida
(wakulima/wavuvi/wafugaji/ wachimba madini). Mfumo mzima wa uhuria unasailiwa
kwa mtazamo wa umma – wa walio wengi, kuonesha nani ananufaika, na nani
anadhurika. Riwaya inadhihirisha kuwa uhuria ni mkono wa utandawazi ambao nao
ni mwendelezo wa ubeberu wa tangu karne ya kumi na tisa na hata kabla.
Jina lenyewe la riwaya linabeba
ujumbe mzito: “Makuwadi (makuwadi) wa soko huria” ni usemi unaowasawiri waasisi
na waendelezaji wa mfumo wa soko huria kama watu waovu wanaohudumia mfumo
uliokosa uadilifu. “Makuwadi” ni watu wafanyao kazi ya kuwatafutia watu wengine
wenzi wa kufanya nao umalaya au uzinzi kwa ujira maalumu. Ni mawakala wa
ukahaba. Katika riwaya hii Chachage anawalinganisha mawakala wa soko huria na
mawakala hao wa uzinifu kwa lengo la kuonesha kwamba hawatofautiani katika kazi
zao na madhara yao kwa jamii. Na tunaoneshwa wazi kwamba mawakala wa soko
huria, kama walivyo makuwadi halisi, wanafanya biashara ya kuuza watu kwa mabepari wa kigeni.  Hivyo jina la riwaya hii ni kauli thabiti na
hasi ya mwandishi kuhusu mfumo mzima wa ubepari huria anaouchambua. Ili
kujinusuru kutokana na hali hii, mwandishi anatuasa turejee nyuma katika
historia yetu, tujue kwa nini haya yametokea, na tujifunze kutoka kwa wahenga
wetu namna ya kupambana na mfumo huu wakati huo huo tukibuni mbinu mpya
zinazolingana na hali na enzi zetu.
Udhaifu wa usawiri wa mgogoro mkuu
wa riwaya hii unatokana na ufinyu wa mtazamo na uwezo wa tabaka linalotumika
kuendeleza na kufafanua mapambano haya kwa msomaji – tabaka la vibwanyenye
wasomi (waandishi wa habari). Hili ni tabaka tegemezi ambalo takriban shughuli
zake za kimaendeleo zinategemea misaada ya wahisani. Fidelis, Mjuba na wenzao
wanakwenda Rufiji na kwingineko na kuchunguza madhara ya uhuria kwa msaada wa
shirika la Kiswidi la Sorrenson. Bila shirika hilo hawawezi kufanya kitu. Huu
ndio udhaifu na unyonge wa tabaka hili na asasi zake.  Hivyo ni kejeli na ni njozi kwamba chombo cha
utandawazi–mashirika ya hisani–ndicho kinachotumika kuuchambua na kuupiga vita
utandawazi huo. Je, kitafanikiwa?
Mbali na kiwango hiki cha
kijamii-kisiasa cha masimulizi ya riwaya hii, kuna kiwango cha binafsi cha
mahaba kati ya jozi mbili za wahusika, ambao wote bado ni vijana: Mjuba+Sifuni;
Makoba+Amina. Safari yao ya kutafuta maarifa na taarifa inakuwa pia ni safari
ya kujigundua kuwa wanapendana na kukomaza mapenzi yao hadi kufikia hatua ya
kuoana. Ni hitimisho murua la uhusiano wao unaojengwa katika mapambano.
Chachage S. Chachage anatumia
mbinu nyingi za kisanaa na kimasimulizi ili kutimiza malengo yake. Mbinu kuu
anayoitumia ni uchanganyaji wa ubunifu na uhistoria, yaani uchanganyaji wa
historia halisi na mambo ya kubuni, wakiwemo watu halisi na wa kubuni.  Mbinu hii inafanikiwa kuileta hadithi karibu
zaidi na msomaji, hasa wa Tanzania, kiwakati na kihisia. Tunahisi kuwa
tunachokisoma ni habari za kweli kama zile za magazetini au katika vitabu vya
historia. Watu halisi waliopata kuishi, kama Kinjikitile, Pretorius, Nguvumali
na Nyerere, na hata ambao bado wanaishi (wakati kitabu kinaandikwa), kama Issa
Shivji na Edward Barongo, wanapambanishwa na kuingiliana na wahusika wa kubuni
kama Binti Wenga, Japhet Lupocho, Mazengo na wengineo. Mchanganyiko huu
unakolezwa na mbinu ya udokezi (allusion)
ambayo inaifinya historia katika maelezo au madokezo mafupi mafupi. Hii ina
maana kwamba msomaji wa riwaya hii sharti awe na welewa mpana kiasi wa historia
na habari nyinginezo za nchi hii, vinginevyo anaweza asiupate vilivyo undani wa
baadhi ya maelezo na masimulizi. Kwa mfano, madokezo kuhusu Mganga Nguvumali,
Osare Otango, madawa na mizimu ya Maji Maji, na wapigania uhuru kama Phombeah
na Abduwahid Sykes yana maana zaidi kwa mtu mwenye fununu ya kutosha kuhusu
watu hao.
Mafanikio haya ya kimaudhui
yanaungana pia na mafanikio katika kujenga taharuki na mvuto. Riwaya hii
inasomeka vizuri na haraka, angalau kwa msomaji aliyepevuka kiasi. Aidha, mara
kwa mara mwandishi anaingiza ucheshi, lakini wenye maana, ili msomaji asichoke.
Mfano ni ile michapo ya “Padri wa Musoma” (Sura ya 6: 136-7) na “Mzungu Kala
Fenesi” (Sura ya 7: 145-7).
Matumizi ya kejeli hapa na pale
pia yanaongeza ucheshi. Kwa mfano, uk. 287 tunaambiwa: “nani asiyejua mchango
wa wawekezaji hawa katika kuinua uchumi wa nchi?” Lakini kusudi la riwaya ni
kinyume chake: ni kutuonesha mchango wa wawekezaji katika kuudidimiza uchumi wa nchi!
Riwaya hii inazo dosari kadha za
lugha na mtindo. Mathalan, neno “ibura” linatumika sehemu nyingi kama kivumishi
ilihali halipaswi kutumika hivyo. (Mfano: hali ngeni ibura ilimwingia moyoni” –
uk. 203). Kadhalika, kuna makosa mengi kiasi ya tahjia na matumizi ya lugha
ambayo yangeweza kusahihishwa na mhariri makini. Mifano ni mingi, hapa tutatoa
michache tu:
·
“Makuwadi”
badala ya “makuwadi” (mahali pengi)
·
“maaluni” badala ya “maluuni” (uk. 13)
·
“ngombe” badala ya “ng’ombe” (uk. 14)
·
“karatasi zingine” badala ya “karatasi nyingine” (uk.
19)
·
“mmojawao” badala ya “mmoja wao” (uk. 23)
·
“Al-Bussaidy na na ukoo”  badala ya “Al-Bussaidy na ukoo” (uk. 53)
·
“asili ya Kidachi” badala ya “asili ya Kiholanzi”
(uk. 53)
·
“askari wa kijerumani” badala ya “askari wa
Kijerumani” (uk. 54)
·
“mume wa baba yangu mkubwa” badala ya…?, n.k.
Hata hivyo, haya ni matatizo
madogo. Tatizo kubwa zaidi ni la usimuliaji. Mwandishi kaamua kutumia nafsi ya
kwanza ya usimulizi kupitia mhusika mmoja: Fidelis Mvumi. Usimulizi wa nafsi ya
kwanza unaitwa usimulizi-tinde, kwa kuwa una mipaka yake ambayo inamnyima uhuru
mwandishi. Mathalan, haiwezekani kuelezea mambo ambayo msimulizi hakuyashuhudia
au kuyashiriki, na wala haiwezekani kueleza, kama afanyavyo Fidelis, mambo
yaliyomo moyoni au katika fikra za wahusika wengine. Hayo yanaweza kufanywa tu
katika usimulizi maizi (omniscient)
ambao unawezekana tu katika nafsi ya tatu. Lakini  katika riwaya hii tunamwona Fidelis
akisimulia habari za mawazoni mwa wahusika wengine bila wasiwasi – yaani akiwa
msimulizi maizi ambaye kihalisi ni tinde! (Mifano; Sura ya 4.III – fikira za
Japhet. Pia kur. 212-216 – mawazo ya Mjuba na Sifuni). Hii ni dosari.
Dosari nyingine ni ile ya kutumia
wahusika kama Binti Wenga kuelezea historia na kufanya uchambuzi wa matatizo ya
maeneo yanayohusika kwa namna ambayo haielekei kusadifu uzoevu wao wa
kitaaluma. Masimulizi ya watu wa kijijini kwa kawaida huwa na umbile tofauti na
yale ya wasomi au waandishi wa vitabu (ambao hutumia marejeleo, huelezea miaka
ya matukio n.k.). Wasimuliaji wa mdomo hutumia mbinu simulizi, ambazo mara
nyingi huepuka kutaja miaka na tarehe, na si rahisi kwao kuzungumzia mambo ya
mbali kama Ulaya. Katika riwaya hii, sifa hizi zimechanganywa katika mtu mmoja,
na kumfanya msomaji aamini kwamba anayeongea si Binti Wenga bali ni Chachage
mwenyewe kupitia kwa mhusika huyo (kur. 67-8).
4.0  Hitimisho
Mbali na dosari chache hizi,
riwaya hii ni mchango wa pekee kabisa katika fasihi ya Kiswahili. Kwa hakika,
riwaya hii ni majumuisho ya kazi, fikra, mawazo, mtazamo, mawanio na harakati
za maisha za Chachage S Chachage. Ni kana kwamba alikuwa akituaga kwa
kutuandikia “wosia” au ushuhuda wa yote aliyokuwa nayo moyoni kuhusu matatizo
na mustakabali wa Tanzania na Afrika.
Marejeo
Abdallah,
H (1960), (uliandikwa kama 1895) Utenzi
wa Vita vya Wadachi Kutamalaki Mrima. (Mh. J.W.T. Allen). Dar es Salaam:
East African Literature Bureau (EALB)
Ajjemy,
A.H (1972); (1895), Habari
za Wakilindi (Mh. J.W.T. Allen). Nairobi: EALB, Allen, J.W.T 1971 Tendi. London: Heinemann
Cabral,
A (1966),  “The Weapon of Theory” (Silaha ya Nadharia). Address delivered to the first Tricontinetal Conference of the Peoples
of Asia, Africa and Latin America  held
in Havana in Janury 1966. Hotuba inapatikana katika Revolution in Guinea: Selected Texts (Mfasiri R.Handyside). New York:
Monthly review Press
Diegner,
L (2002), “Mahojiano na Chachage Seithy L. Chachage Juu ya Riwaya Yake Makuwadi
wa Soko Huria (2002)” katika  Swahili Forum 11 (2004): 227-234
Heepe,
M (1928), “Suaheli-Chronik von Pate.” M.S.O.S. XXXI: 145-92
Hichens, W (1938) “Khabar al Lamu — A Chronicle of
Lamu.” Bantu Studies 12(1):1-33
Hussein,
E (1969), Kinjeketile. Nairobi:
Oxford University Press (OUP)
Hussein,
E (1971), Mashetani. Nairobi: OUP
Kezilahabi,
E (1975), Dunia Uwanja wa Fujo. Nairobi: EALB
Kezilahabi,
E (1979), Gamba la Nyoka. Arusha: EAPL
Knappert,
J (1979), Four Centuries of Swahili
Verse. London: Heinemann
Lihamba,
A (1990), Wimbo wa Sokomoko. Dar es
Salaam: Tanzania Publishing House (TPH)
Lukacs,
G (1962), The Historical Novel. ,
Harmondsworth: Penguin Books
Mapalala,
B (1992), Kwa Heri Iselamagazi. Dar
es Salaam:TPH
Mbonde,
J.P (2004), “Chachage Seithy L.Chachage: Makuwadi
wa Soko Huria (2002)Uchambuzi na Uhakiki” Katika Swahili Forum11 (
2004): 214-226
Mohamed,
M.S (1978)  Nyota ya Rehema. Nairobi: OUP
Muhando, P Balisidya, N na Lihamba, A  (1982) Harakati
za Ukombozi. Dar es Salaam: TPH
Mulokozi, M.M (1990)
“Utunzi wa Riwaya ya Historia.” Mulika
Na.22: 1-12
________
(1990)  Ngome ya Mianzi. Dar es Salaam: MPB Press,
________ (1991)  Ngoma
ya Mianzi. Dar es Salaam: TPH
________ (1996)  Moto wa
Mianzi. Morogoro: ECOL, Morogoro
________
(1997) Utenzi wa Nyakiiru Kibi. Morogoro: ECOL
Mohamed,
S.A (1980) Dunia Mti Mkavu. Nairobi: Longman
Robert, S (1967) Utenzi
wa Vita vya Uhuru. Nairobi: OUP
Ruhumbika, G (1995)
Miradi Bubu ya Wazalendo. Dar es
Salaam: TPH
Shafi, A (1978) Kasri
ya Mwinyi Fuad. Dar es Salaam: TPH
Shafi, A (1979) Kuli.
Dar es Salaam: TPH
Shafi, A (1999) Vuta
N’kuvute. Dar es Salaam: Mkuki na Nyota
Shafi, A (2003) Haini.
Nairobi: Longhorn Publishers
Shivji, I (2000) (2002) “Makuwadi wa Soko Huria.” Mulika
Na. 26 (2000): 93-97
Tolmacheva,
M (1993) The Pate Chronicle. East Lansing: Michigan State University Steere, E (1870)
Swahili Tales, as Told by the Natives of Zanzibar . London: Bell and Daldy
Vassanji, M (1989) The Gunny Sack. Oxford: Heinemann International

Print this item

  TASWIRA YA MWANAMKE KATIKA RIWAYA
Posted by: MwlMaeda - 08-27-2021, 03:26 PM - Forum: Riwaya - No Replies

Taswira ya Mwanamke

Tunaposema taswira ya
mwanamke, tunamaanisha picha ya mwanamke inayojitokeza baada ya matumizi
mbalimbali ya semi na ishara katika kazi ya fasihi. Waandishi wa riwaya za
Kiswahili wamewachora wahusika wa kike katika taswira mbalimbali. Katika
utafiti huu, mtafiti amechunguza uchorwaji wa taswira hizo katika kazi chache
ziitwazo Rosa Mistika, Nyota ya Rehema, Shida na Hiba ya Wivu ambazo ni riwaya
za Kiswahili. Waandishi wa riwaya hizi ambao ni wa jinsia tofauti, wamewapanga
wahusika wanawake wa riwaya hizo katika taswira za uzinifu, ubidhaishaji
(mali), vyombo vya kuwastarehesha mwanamume na wapenda fedha. Aidha baadhi ya
waandishi wamediriki kuwatenga wanawake wasifanye shughuli nyingine muhimu za
kuzalisha mali katika jamii zao kwa kuwapangia kazi za malezi ya watoto na
kuwatumikia wanaume. Mwanamume ndiye anayeonekana kuwa mwuamuzi, msimamizi na
mpiganaji wa majukumu muhimu katika jamii ilhali mwanamke akiwa mzalishaji.
Wakati mwingine, mwanamke amechorwa katika riwaya kama mtekelezaji wa yale
yanayoamuliwa na kuamuriwa na mwanamume. Mahali pengine mwanamke ameonekana
akiwa na uwakilishi finyu au hakuna kabisa katika uongozi wa juu ndani ya
jamii. Uwasilishwaji wa kina wa taswira ya mwanamke katika sura hii umerejelea
riwaya hizo nne teule, zilizotajwa hapo juu.

Print this item