MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI

Welcome, Guest
You have to register before you can post on our site.

Username
  

Password
  





Search Forums

(Advanced Search)

Forum Statistics
» Members: 5,481
» Latest member: Kundlimatching
» Forum threads: 2,178
» Forum posts: 2,256

Full Statistics

Online Users
There are currently 48 online users.
» 0 Member(s) | 47 Guest(s)
Bing

Latest Threads
Buy Vilitra 60 Mg |【Get E...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-24-2023, 11:45 AM
» Replies: 0
» Views: 0
How to take Cenforce50?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-19-2023, 12:59 PM
» Replies: 0
» Views: 0
About the Vidalista 60 Mg...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-04-2023, 04:07 PM
» Replies: 0
» Views: 0
What Is Vidalista 60?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-03-2023, 10:49 AM
» Replies: 0
» Views: 0
How to take Cenforce 100 ...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
03-29-2023, 02:37 PM
» Replies: 0
» Views: 66
How is Vidalista 10 Mg us...
Forum: Watunzi wa Kiswahili
Last Post: Kieth_winsett
03-27-2023, 01:26 PM
» Replies: 0
» Views: 117
Obtain Thesis Paper Assis...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Minny02
03-24-2023, 03:01 PM
» Replies: 0
» Views: 200
SEO services for sports f...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Maria Poland
03-17-2023, 01:51 PM
» Replies: 1
» Views: 223
NUKUU ZA KISWAHILI DARASA...
Forum: Nukuu
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:31 PM
» Replies: 0
» Views: 788
NECTA K4 2022
Forum: Mitihani
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:25 PM
» Replies: 0
» Views: 403

 
  VUTA N’KUVUTE YA SHAFI ADAM SHAFI
Posted by: MwlMaeda - 08-28-2021, 07:58 AM - Forum: Riwaya - No Replies

Vuta N’Kuvute ya Shafi Adam Shafi

Kwa miongo mingi sasa, wahakiki wa kazi za fasihi wamezisifu kazi za waandishi wa Kizanzibari kwa sifa tele. Kwa mfano, akirejea riwaya za Mohamed Suleiman Mohamed, Said Ahmed Mohamed na Shafi Adam Shafi, M. M. Mulokozi aliandika mwaka 1985: “Maendeleo muhimu kabisa, na pengine ya kufurahisha sana, katika kazi za fasihi za Kiswahili katika miaka ya 1970 na 1980, ni kuibuka kwa Zanzibar kama mtoaji bora kabisa wa kazi za Kiswahili kuwahi kutokea hadi sasa, na kiongozi wa wazi wa riwaya za Kiswahili katika siku zijazo.”
Hisia kama hizi zinaelezewa pia na R. Ohly ambaye, baada ya kukumbana na riwaya zilizoandikwa na waandishi wa Kizanzibari na wale wa Kitanzania na Kikenya baina ya mwaka 1975 na 1981, amezielezea riwaya za Kizanzibari kama changamoto kubwa kwa uwezo wa kisanaa kwa waandishi wengine wa Kiswahili.
Ingawa mnasaba uliotumiwa na Ohly unaweza kujadilika kwa kujikita kwake na kazi zilizotolewa Bara hasa hadithi fupi fupi na kuwaacha waandishi wenye vipaji kama vile Euphrase Kezilahabi au Claude Mung’ong’o, uhakiki wake bado umezungumzia sifa kuu za riwaya za Kizanzibari, yaani kujikita sana kwenye masuala ya kihistoria na kijamii, pamoja na utajiri wa lugha mwanana na kutokufanya mzaha kwenye masuala ya fani.
Sifa hizi za fani zinashabihiana sana na riwaya ya ‘Vuta N’kuvute’ iliyoandikwa na Shafi Adam Shafi na kuchapishwa mwaka 1999, ambayo ndiyo shughuliko la uhakiki huu.
Waandishi wa Kizanzibari mara kadhaa wameandika riwaya za kihistoria, wakizikita simulizi zao katika zama za ukoloni ama za kabla ya Mapinduzi visiwani humo. Kufuatia hali hiyo, matukio kwenye ‘Vuta N’kuvute’ nayo yanazungumzia siku za mwisho mwisho za ukoloni visiwani Zanzibar.
Mandhari ya riwaya hii ni changamano sana, maisha ya dhiki ya wahusika wakuu yanachorwa kupitia matukio kadhaa, wahusika wadogo, matendo ya kuchangamsha, yote yanaunganishwa na mapenzi ya uhuru na kujitawala katika viwango tafauti vya maisha ya kibinafsi, kijamii na kisiasa, na hivyo kuusafirisha ule moyo wa Ujamaa katika muonekano wa kilimwengu zaidi.
Hadithi yenyewe inaanza kwa kumtambulisha msomaji kwa msichana wa Kihindi, Yasmin, ambaye kutokana na mila ya ndoa za kupangwa na wazazi, anakwenda Mombasa na mume wake, mfanyabiashara mzee, Bwana Raza. Lakini Yasmin anaoneshwa kuwa mtu asiye na furaha na mpweke na hatimaye anaasi na kurudi nyumbani, Zanzibar.
Kutabiri matokeo ya makuzi mabaya ni jambo maarufu kwenye riwaya za Kiswahili, ambapo kawaida waandishi huchora mashaka yale yale yanayoathiri maisha ya vijana, hasa wa kike, ama kushindwa hadi kufikia mauti yao au mateso ya kiakili na kimwili kama vile Rosa Mistika au Asumini, au kukimbia mazingira kandamizi kama vile Maimuna na Yasmin, ambapo mote hupelekea maisha mapya kabisa.
Mara tu baada ya kurudi Zanzibar, Yasmin anakataliwa na mjomba wake na anaomba msaada wa shoga yake wa pekee, Mwajumba, msichana wa Kiswahili anayeishi kwenye mitaa ya masikini ya Ng’ambo, ambaye anampokea kwa moyo wote.
Licha ya ukarimu wa Mwajuma, mama yake Yasmin anakataa kumsamehe bintiye sio tu kwa kuiabisha familia kwa kumuasi mumewe, bali pia kwa kujichanganya na Waswahili na hivyo kuvunja khulka ya jamii yake na tafauti za kijamii na kitamaduni zilizojikita sana kwenye unyanyapaa wa sera za kikoloni linapohusika suala la mahusiano kati ya makabila yanayounda jamii kubwa ya Kizanzibari.
Baada ya kukandamizwa kwenye misuguano na ubaguzi wa kijamii huko alikokulia, Yasmin anapata ladha ya maisha mapya wakati akiishi kwa Mwajuma, ambako anagundua maisha yenye wasaa zaidi, mukiwemo ulevi, klabu za usiku na, zaidi ya yote, anapendana na kijana aitwaye Denge.
Denge ni kijana msomi aliyerejea nyumbani akitokea Ulaya akiwa hana chochote zaidi ya digrii yake ya Kirusi na dhamira madhubuti ya kuikomboa nchi yake kutoka kwenye Himaya ya Mwingereza. Yeye na marafiki zake wanaandamwa na polisi kwa kufanya propaganda ya kisiasa na kuingiza kwenye nchi vitabu na magazeti yaliyopigwa marufuku na wakoloni.
Yasmin anajikuta akihusika moja kwa moja katika mapambano kati ya kundi la Denge na polisi, ambao wanajaribu kumlazimisha amsaliti mpenzi wake “mkomunisti” na “kafiri”, lakini anaamua kuwasaidia wanaharakati hao, akiamini wanaandamwa kwa sababu tu wanapigania uhuru.
Kama inavyoelezwa na Denge katika ukurasa wa 68 wa riwaya hii, serikali ya Kiingereza ilijaribu kuwatenganisha wapigania uhuru na wafuasi wao kwa kutumia sera ya wagawe uwatawale:
“Sikiliza Sista, hawa wakoloni na vijibwa vyao ni watu wapumbavu kabisa, kwao kila mtu ni koministi Ukidai haki yako wewe koministi Ukisema kweli wewe koministi Ukipinga kutawaliwa wewe koministi. Kila anayedai haki kwao ni koministi, na sumu yao kubwa wanayoitumia ya kutaka kutenganisha watu kama hao na wananchi wenziwao ni kusema kwamba watu hao wanaowaita makoministl hawaamini Mungu.”
Mapambano ya daima kati ya maafisa wa kikoloni na wapigania uhuru yanaipeleka riwaya hii kwenye upeo wa hadithi ya kusisimua, kurusha roho na hekaya za kijasusi, mtindo ambao uliletwa kwa mara ya kwanza kwenye riwaya za Kiswahili na Mohamed Said Abdulla (Bwana MSA), ingawa kwenye riwaya hii polisi wamekuwa wahusika wabaya, wanaotumikia maslahi ya kikoloni kibubusa.
Kama inavyoelezewa na Pazi katika ukurasa wa 113, katika mapambano ya kuwania uhuru, ni muhimu kutumia hata njia zisizo za halali kisheria:
“Wakati tunapambana na adui lazima tutumie mbinu zote tunazoweza kuzitumia. Pale inapoyumkinika kutumia mbinu za dhahiri basi tuzitumie kwa kadiri ya uwezo wetu.. Pale ambapo hapana budi ila kutumia njia ya siri kwani mapambano yetu ni ya vuta n’kuvute. Wao wanavutia kule na sisi tunavutia huku na katika mvutano huo hapana suluhisho linaloweza kupatikana isipokuwa kuwa huru. Uhuru ndiyo suluhisho, kwa hivyo lazima tutumie mbinu mbalimbali katika kutafuta suluhisho hilo.”
Jambo la kufurahisha ni kuwa upinzani na mapambano kwenye riwaya hii hayajumuishi vitendo vya kutumia nguvu dhidi ya binaadamu wengine, bali maandamano na mashambulizi dhidi ya alama ya nguvu za kikoloni (kama vile mikahawa iliyotengewa watu wa matabaka fulani tu), kusambaza kazi ambazo zinachukuliwa na serikali kuwa ni haramu na uanzishaji wa gazeti liitwalo Kimbunga.
Mambo yote haya yanaelezewa kwenye Vuta n’kuvute kama kipimo cha majaribu ya mapambano ya kusaka uhuru.
Hapa pia, kama ilivyo kwenye kazi nyingi za Kizanzibari, tunaona uhusiano wa wazi baina ya jina na maudhi, ambao ishara yake inajidhihirisha wazi  kwenye mtiririko wa visa unaomsaidia msomaji kuitafsiri riwaya katika muktadha wa kihistoria.
Katika Vuta n’kuvute, uhuru wa mawazo na kujieleza ni sehemu muhimu ya mapambano ya jumla, lakini baadhi ya wakati pande hizo mbili hukinzana. Kwa mfano, wakati mwengine mtu kusimamia haki yake kwenye mapenzi ni jambo la anasa linapolinganishwa na suala la ulinzi wa nchi, kama anavyoungama Denge katika ukurasa wa 145:
“Yasmin mimi najua kama unanipenda, na mimi nakupenda vile vile, lakini kuna kitu kimoja napenda uelewe. Kuna mapenzi na wajibu wa mtu katika jamii. Kila mtu ana wajibu fulani katika jamii na mimi wajibu wangu mkubwa ni kufanya kila niwezalo kwa kushirikiana na wenzangu ambao wengine unawajua na wengine huwajui ili kuona kwamba nchi hii inakuwa huru. Hii ni kazi ngumu, ina matatizo mengi na inahitaji kujitolea muhanga na mimi ni miongoni mwa hao waliojitolea muhanga kufa, kupona, potelea mbali. Tupo wengi tuliojitolea namna hiyo, tena wengi sana, maelfu.”
Maisha ya Denge yametolewa muhanga kwa kile akiaminicho, ikiwemo kutengwa au kuishi uhamishoni, na Yasmin anapaswa kukubali majaaliwa yake ya upweke, na kushika njia akaenda zake.
Kwa mara nyengine, Yasmin anakabiliwa na upotoshaji wa kikabila. Makutano yake na Bukheti, aliyewahi kuwa jirani yake Mombasa, yanapingwa na familia zote mbili, zikionesha khofu na dharau zao kwake kama mkando.
Anadhalilishwa kwa kila aina ya maneno machafu, kama anavyoibuka na kutoa kauli kwenye ukurasa wa 254:
“Iko wapi heshima ya binadamu, ikiwa Muhindi anamwita Mswahili golo na Mswahili naye anamwita Muhindi ponjoro?”
Upatanishi uliofanywa na marafiki wa zamani wa kifamilia na ambao ni watu wenye mwamko, unasaidia kuzitenga kando dharau hizo; na riwaya hiyo inamalizia kwenye muunganiko wa furaha, unaofunikwa na ghamu ya Yasmin.
Tukio la mwisho lenye kumuacha msomaji na athari kubwa kutoka riwaya hiyo linaelezewa kwa nyimbo ya Kihindi ambayo Yasmin aliisikiliza Mombasa, na kudimka peke yake kutuliza roho yake na pia kuiimba kwenye kundi la taarab kisiwani Unguja.
Daima Yasmin anauchukulia muziki kama kimbilio binafsi na beti za nyimbo hizo zinamkumbusha utamu na ukali wa uhuru.
Fani
Sasa natuangalie baadhi ya vipengele vya usimulizi wa riwaya hii ya Vuta n’kuvute, tukichunguza zaidi muundo wa hadithi yenyewe, mitindo na matumizi ya lugha.
Kama zilivyo kazi nyingi za Kizanzibari, kazi hii ina kiwango kikubwa cha kisanii, ikiwa imejengwa kwa sura fupifupi kumi na nane, zinazokwendana na mjengeko wa matukio, mikasa, na mapigo yanayomfanya msomaji azidi kupata hamu ya kuisoma.
Kipengele cha wakati kwenye riwaya hii kwa jumla kimetumika vyema – ni nadra kukuta matukio yanayoelezewa kwa kurudi nyuma, kama lile la maisha ya Denge barani Ulaya.
Mtiririko wa visa unasimulia hadithi mbalimbali za maisha ya wahusika wakuu, wakati mwengine zinazopishana na wakati mwengine kuoana. Matukio mengi ni muhimu sana kwa mjengeko mzima wa riwaya.
Ufundi huu wa uandishi unaipa riwaya sifa ya kuwa “riwaya ya masimulizi” bila ya kuondosha mantiki ya matukio kama lile la mazingira ya Roger na Salum kumtembelea Mwajuma na ugomvi uliozuka baina ya wanaume hao wawili.
Mwandishi amefanikiwa kwa ustadi mkubwa kuweka mizani baina ya mbinu za kuonesha (ambapo matukio huwa yanasimuliwa na wahusika) na ile ya kuelezea (ambapo matukio yanasimuliwa na msimulizi, yaani mwandishi mwenyewe).
Uwasilishaji wa msimulizi aliye wazi na aliyejificha ni miongoni mwa vipengele vya ubora kwenye kazi za fasihi, na katika riwaya hii tangu awali kabisa msimulizi huyo huonekana kwa sura zote mbili na katika viwango tafauti.
Kwa mfano, riwaya hii imejengwa kwa majibizano – ambapo msimulizi anakuwa haonekani kabisa – sio tu kwenye mazungumzo mafupi mafupi, lakini zaidi kwenye mistari mirefu ya kujenga hoja, lakini wakati mwengine majibizano haya huchukua nafasi muhimu sana katika kutoa taarifa kuhusu wahusika na au ujumbe muhimu, ambao mwandishi anauwasilisha kwa hadhira yake, kama dondoo za Denge na Pazi zilizotajwa hapo juu.
Ndani ya riwaya hii, msomaji anagundua pia matumizi ya kauli zisizo za moja kwa moja, ambako maneno au mawazo yanasimuliwa na msimulizi lakini yakinasibishwa kwa ukaribu sana na mhusika, kama vile kwenye ukurasa wa 49 pale mwandishi anapoelezea namna Yasmin alivyomuona Denge kwa mara ya kwanza:
“Kwa Yasmin huyo alikuwa n’do Mwafrika wa kwanza kuambiwa ametoka Ulaya. Shilingi mbili za kununua ukanda wa kufungia suruali yake zinamshinda, na ile suruali isiyokuwa na pasi aliyovaa imezuiliwa kiunoni kwa tai labda aliyorudi nayo kutoka huko Ulaya, na hivyo viatu alivyovaa, karibu vidole vingine vinataka kuchungulia nje.”

Print this item

  UDHANAISHI KATIKA RIWAYA YA KICHWAMAJI
Posted by: MwlMaeda - 08-28-2021, 07:53 AM - Forum: Riwaya - No Replies


.pdf   MUKHTASARI NA UCHAMBUZI WA FASIHI.pdf (Size: 157.86 KB / Downloads: 3)

Print this item

  FALSAFA YA KIAFRIKA NA RIWAYA YA KISWAHILI
Posted by: MwlMaeda - 08-28-2021, 07:36 AM - Forum: Riwaya - No Replies

John mbiti

Huyu ni mwanafalsafa maarufu aliyezaliwa nchini Kenya, alitumikia waasifu wa uparoko katika kanisa la Roman Catholic (RC). Aliandika maandiko mawili yaliyotalii falsafa ya kiafrika “Africa Religious Philosophy (1966) and African concept of God (1970). Alizungumzia yafuatayo kuhusu falsafa ya kiafrika.
Dhana ya wakati; kwa waafrika hawaangalii wakati na hawana haraka na wakati, mwafrika katika kuangalia wakati, namba za saa ni kitu dhahania, kwa mwafrika wakati hauamui matendo kama ilivyo kwa mzungu, dhana hii imedhihirika katika riwaya ya “ Nagona” kwa muhusika babu alipokuwa akimweleza mjukuu mwaka wake wa kuzaliwa kwa kuyarejea matukio kama matukio ya “utupu” ajali gharika kupatwa kwa jua kama asemavyo mwandishi.
“……nataka kujua habari za kuzaliwa kwangu wazazi wangu hajapata kunieleza kikamilifu….. natakueleza. Hivi ndivyo ilivyokuwa…….hapakuwa na ujuzi wa jema na baya. Hapakuwa na fikra. Palikuwa na utupu katika kitovu cha undani na hapakuwa na nguvu zilizoweza kutoa uongozi…….. ajali hii ilitokea katika bonde la hisia……. Katika ukweli huu palitokea gharika katika mto wa bonde…..(uk 11)”.
Vilevile katika kitabu cha riwaya ya “Mirathi ya hatari”  wazo limethibitishwa na familia ya Mzee Kazembe alivyokuwa akijilimisha usiku na mchana bila hata ya kuangalia wakati.      “……si yule wa mji wa Kazembe ajilimishaye usiku na mchana..(uk 5)”.
Hata katika mazingira halisi ya waafrika mambo haya yanahalisika.
Dhana ya kifo, Mwafrika anapokaribia kufa huwa anatoa urithi mfano mali, uchawi, jina au maelekezo fulani kuhusu baraka au laana katika “Mirathi ya hatari”, Gusto, kijana wa Mzee Kazembe aliachiwa urithi wa pesa, Mirathi ya hatari (uchawi), mashamba pamoja na baraka anasema.
“….mwanangu nakuachia kazi kubwa. Ni urithi mkubwa ukitumia vema; bali pia ni mirathi ya hatari usipojihadhari nayo. Nakuachia dawa zote na milki yangu katika mizungu ya sihiri…(uk 15-16)”.
vile vile, Dina alimuachia maagizo Gusto alisema
 “mali yangu yote isipokuwa kitabu kilicho sandukuni mwangu, uwape maskini” (uk 90).
Pia katika kitabu cha “Nagona” Babu anatoa maagizo au maelezo kwa mjukuu wake baada ya kukaribia kufa alisema
“…. Mjukuu jihadhari siku ya ngoma kuu usikanyagwe daima fuata duara na macho yako wakati wote watazame hapo katikati hicho kitovu kitakapo pasuka mengi yaliyofichika kwa karne nyingi yataonekana harafu kwa shida alisema Nag…..Nag….” (uk 45).
Dini, kwa mwafrika , dini ni chimbuko la mambo yote na kwa asili mwafrika alizaliwa na dini yake, si suala la kujifunza na kusilimishwa; katika “Mirathi ya hatari” ametumia familia ya Mzee  Kazembe, Madoda na Mavengi waliokuwa na dini yao ya asili ilivyokuwa ikifanyika mapangoni usiku pamoja na baadhi yao kuamini dini ya kujifunza na kusilimishwa lakini hawakuiacha kamwe, kama asemavyo mwandishi;
                        “enyi mahoka wa mababu;
                                Enyi wazee mliotangulia
                                Enyi wenzangu,
                                Sikiliza kiapo changu!
                                Sitasema wala kuwaza lolote,
                                La ndani ni la ndani!
                                Nishindwe mara tatu,
                                Pembe hili linichome moto…!(uk 22)
Haya ni maneno yanayoonesha utii wa dini za asili zenye kuamini miungu, mahoka, wazee na binadamu.
Pia katika riwaya ya “Nagona” mwandishi amemtumia mhusika Padri ambaye alikuwa anaamini dini ya kujifunza na kubatizwa (Ukristo) na Wazee walishikiria dini ya kipagani kama dini ya asili kama asemavyo;
“…Padri alikaa kimya, wazee wote walimtazama, Padri alitabasamu aliwatazama wazee halafu akafungua kinywa chake, hakuna mkristo miongoni mwenu?” wazee walitazamana “ Hakuna” babu alijibu. (uk 10).
Hii inadhibitisha kuwa waafrika wanaozithamini dini zao za asili na kuzitupilia mbali dini za wageni kama ukristo hii hata katika mazingira halisi ya kiafrika imetawala sana hususani maeneo ya vijijini.
Kuhusu ufahamu wa ulimwengu na uwapo, waafrika wanaamini kuwa ulimwengu uliumbwa na Mungu na Mungu ndiye muumba wa vyote. Mfano katika riwaya ya “Nagona” imejidhihirisha katika majibizano ya Padri na Mtubu dhambi kama asemayo mwandishi;
                        “…Mmh! Baba unazo dhambi zingine”
                                “kubwa moja na ndogo nyingi”
                                 Lakini unajibebesha mzingo mzito! Dhambi za karne mbili!”
                                “Mungu aliumba ulimwengu na vyote vilivyomo…….” (uk 51)
Pia katika kitabu “Mirathi ya hatari” mwandishi amemtumia Gusto kama mhusika aliyekabiliwa na changamoto nyingi kutoka kwa wanafunzi wenzake katika safari yake ya masomo ila kwa kuwa alimwamini Mungu ndiyo chanzo cha yote hapa duniani alijipa moyo atayashinda kama asemavyo;
“…. Kwani yaliyopita si ndwele tugange yajayo kwa uwezo wa mbingu natumaini nitafanikiwa, sijui nianzie wapi” (uk 4).
Hivyo basi nukuu hii inaonesha jinsi waafrika wanavyotumaini Mungu kuwa hata mambo yawe magumu ama mepesi kuwa ndiyo yeye pekee anayeyajua kwani ndiye aliyeyafanya yawepo hapa dunia au ulimwenguni.
Kwa ujumla John Mbiti anaona kuwa falsafa ya kiafrika ipo na inaendelea kuwepo, na uwepo huo unajidhihirisha katika mambo ya kiutamaduni, japo athari za kiutamaduni wa kigeni unaokweza na sababu za maendeleo ya sayansi na teknolojia na zile za kiutandawazi.
Kwasi Wiredu
Ni miongoni mwa wanafalsafa wa kiafrika, alizaliwa mwaka 1931 katika nchi ya Ghana yeye aliangalia dhana ya Ngano na hadithi. Na jinsi gani zinavyojidhihirisha katika falsafa ya kiafrika. Kwasi Wiredu alidai kuwa waafrika hawana falsafa yao wenyewe bali mawazo yao hujiegemeza katika mapokeo ya watu wa magharibi. Hivyo Kwasi Wiredu katika kulinda mtazamo wake ametoa baadhi ya hoja madhubuti kuhusu kutokuwepo kwa falsafa ya kiafrika.
Hoja zake zinaweza kuwa na ukweli fulani na zisiwe na ukweli fulani kulingana na uchunguzi uliofanyika kwa kutumia riwaya ya “Nagona” na ile ya “Mirathi ya Hatari” kama ifuatavyo:
Mawazo ya kiafrika ya kiutamaduni na kijamii huwa hayabadiliki kulingana na wakati. Suala hili la kutobadilika kwa utamaduni sio tu kwa Afrika bali ni duniani kote. Hii hutokana na waafrika kushikilia baadhi ya misimamo yao kiutamaduni bila kujali mabadiliko ya wakati kutokan na waafrika wenyewe kutoruhusu fikra mpya. Haya yanadhirishwa kwenye riwaya ya “Nagona” japokuwa utamaduni unabadilika lakini mawazo ya kiafrika yanabaki vilevile. Mfano suala la ndoa katika riwaya hii mhusika Mimi alipotaka kumkumbatia msichana ambaye alilkuwa bado hajaolewa ilikuwa ni kinyume na tamaduni za kiafrika mwandishi anasema;
“….nilipomkaribia niliinua tena mikono yangu kuukumbatia mwanga. Lakini aliishika mikono akaishusha tena mahali pake akisema.
“Mila”
“mila gani?”
Myeleka lazima kwanza tupige myeleka ukifanikiwa kunishika na kunitupa kitandani basi umeshinda. Sitakuwa na la kusema. Utaruhusiwa kucheza ngoma kati kati ya duara” (uk 67).
Hii inaonyesha kuwa pamoja na mabadiliko ya wakati lakini bado waafrika wana mawazo yao juu ya utamaduni kwani hata katika jamii zetu mawazo kama haya bado yapo. Mfano, wamasai na wasukuma ili uweze kuoa binti wa kimasai lazima ufuate utamaduni. Pia katika riwaya ya “Mirathi ya Hatari” mtunzi anaonyesha hayo pale mtunzi anaposema;
“majira ya wakati yanabadilika mzee wangu…..ukweli ni kwamba sisi wenyewe wazee ni wa kulaumiwa tumeshindwa kutambua kuwa dunia ya leo si dunia yetu….tumeshindwa kutambua kwamba ulimwengu wa leo ni ulimwengu unaobadilika kwa kasi tusiyoweza kuimudu…. Nani kati yenu angetegemea kufika hospitalini na kupimwa huku na mwanamke mwafrika ambaye pia huendesha gari lake mwenyewe (uk 56)”
Hii inaonyesha dhahiri kuwa mawazo ya waafrika hayabadiliki kwani wazee wanashangaa jinsi wanawake wanavyoweza kufanya kazi ambazo hapo awali zilikuwa zikifanywa na wanaume katika jamii zetu pia tuanona kuna wazee ambao bado wanalalamika kwa jinsi waonavyo ulimwengu ulivyobadilika. Kwani kuna mawaziri, wabunge na wakuu wa mikoa.
Afrika hakukuwa na falsafa kwa kuwa mawazo yao yanahusisha wahenga na haina uthibitisho tofauti na ile ya kimagharibi. Kwasi anaamini kuwa Afrika hakuna falsafa kwa kuwa haikuandikwa bali mawazo yao yalihusisha Wahenga tu. Haya yanadhirika kwa kutumia riwaya ya “Nagona” pale mtunzi anaposema;
“…sauti ya kiwiliwili ilisikika kutoka katika mwanga, kwa sasa mazungumzo na roho yako yanatosha utakapo jua kuzungumza na roho yako vizuri mambo yataenda kwa haraka kidogo…..huu si mwanzo mbaya meza roho  yako….”(sura ya tatu (3).
Hii inaonyesha kuwa waafrika wakipata matatizo hukimbilia kuwaomba wahenga ili waweze kuwasaidia katika matatizo hayo. Katika jamii yetu pia kukiwa na matatizo wazee wa jamii huenda kuzungumza na wahenga ili waweze kuwasaidia, mfano katika jamii ya Wangindo wakipata  matatizo huenda “Ngende”. Pia katika riwaya ya “Mirathi ya Hatari” kuna mawazo yanayohusishwa na wahenga pale watu wapatapo matatizo;
                        “enyi mahoka wa mababu;
                                Enyi wazee mliotangulia
                                Enyi wenzangu,
                                Sikiliza kiapo changu!
                                Sitasema wala kuwaza lolote,
                                La ndani ni la ndani!
                                Nishindwe mara tatu,
                                Pembe hili linichome moto…!(uk 22)
Lakini kutokana na Kwasi anadai kuwa mawazo hayo ya Wahenga hayawezi kuthibitishwa kwa sababu hayakuweza kuandikwa katika andiko lolote bali yalikuwa ya kurithishwa tu. Hivyo hakuna falsafa ya Kiafrika.
Kinachoitwa falsafa ya Kiafrika kinajumuisha hekima, elimu, mila na desturi ambapo kwa Kwasi Wiredu anasema; vitu hivi haviitwi falsafa lakini matendo au vitu hivyo vyote vilikuwa vikifanywa na waafrika, kwani vinajidhihirisha kama ifuatavyo; Kuhusu hekima, huangalia matendo mema na maneno ya busara yaliyokuwa yakifanywa na waafrika hasa wazee wa zamani na hivyo huweza kurithisha hekima hizi kwa vijana au vizazi vya sasa. Katika riwaya ya “Mirathi ya Hatari” Mzee Mavengi alimshangaa Gusto alivyokuwa akitoa maneno ya hekima kwa wenzie kuliko vile alivyokuwa akidhania.
            “…hivyo nadhani kuna chembe fulani ya ukweli na hekima fulani katika maneno yako…” (uk 26- 27)
Hii ni dhahiri kuwa Gusto alikuwa kijana mwenye hekima ambaye ni moja kati ya viashiria vya mawazo ya kifalsafa.
Kuhusu elimu, huangalia elimu ya awali kwa waafrika ambayo ni jando na unyago ambayo humuandaa kijana katika kupambana na mazingira yake na jamii kwa ujumla katika kudhihirisha hili katika riwaya ya “Nagona” mwandishi nanaonyesha kuwa waafrika walikuwa na njia/ chombo chao cha kutolea elimu ambacho ni jando;
            “….hatutaki ajali nyingine. Bado hujaenda jandoni, ukivalishwa ushanga…”(uk 20)
Elimu hii pia bado inatolewa katika jamii tafautitofauti za kiafrika mfano kimakonde.
Kuhusu mila na desturi, waafrika wanamila na desturi zao kama vile namna ya kusalimia, maisha yao na kurithisha mali ni desturi ya waafrika. Mawazo haya ambayo yalisemwa na Kwasi Wiredu yanadhihirishwa katika riwaya ya “Mirathi ya Hatari” .
            “….mwanangu nakuachia kazi kubwa, ni urithi mkubwa ukiutumia vema…..” (uk 15)
Hapa baba Gusto anamrithisha mwanae mirathi ya hatari kama desturi ya waafrika wengi pale mzazi anapokaribia kuaga dunia anaendelea kusema;
            “….nakuachia dawa zote na milki yangu katika mizungu na sihiri…(uk 16).
Hayo pia yanadhihilishwa katika riwaya ya “Nagona” ambayo wazazi wanadesturi ya kuachia urithi wanao. Mfano, babu alipokuwa anakaribia kufa lakini mimi nimeacha mali gani nyuma? Hakuna isiyopokuwa wewe, baba yako na mama yako. Hii inaonyesha hata kama mzazi hana mali basi hupenda hata kuacha wosia kwa wale wanaobaki.
Mawazo mengi na tamaduni za kiafrika ni za kishenzi, ushirikina, uchawi na kupitwa na wakati. Hata wasomi wa kiafrika wanaamini mawe, mizimwi, miti, mapepo, mahoka na Miungu Kwasi anadai, kuwa hata kama mwafrika akisoma lazima atakuwa na tamaduni za kishenzi, kichawi na kushirikina hayo yanadhihilishwa katika riwaya kama zifuatavyo;  kuhusu uchawi, mwandishi wa riwaya ya “Mirathi ya Hatari” imejishughulisha sana na suala hili la uchawi kuwa mawazo waliyonayo waafrika kwa kiasi kikubwa. Gusto kijana mdogo tu wa shule alirithishwa tunguli (uchawi) na baba yake baada ya baba yake kufa, waafrika wengi huamini mazingaombwe kwa kila kitu hayo yanaonekana pale baba Gusto anasema;
          “….ukipatwa na adha
                Sihiri hii ikutulize
                Ukiona na hasidi
                Fingo hii impumbaze
utende mambo kwa idhaa
Kago hii ikuongoze…” (uk 23)
Pia katika riwaya ya “Nagona” mawazo ya kiafrika yamejikita katika suala hili la uchawikwa mfano anaposema;
            “….ndege wa mawio walipoanza kuwaimbia wachawi….(uk 23).
 Inaonesha waafrika huamini kiasi cha kushindwa kulala; “….hata wachawi hubisha  hodi…(uk 16).
 Hii inajidhihirisha kuwa mawazo ya waafrika yapo kwenye utamaduni wa kichawi. Pia kuhusu ushirikina, mwandishi anajaribu kuonyesha imani ya kishirikina kwa jamii za kiafrika, katika riwaya ya “Nagona” yanadhihishwa hayo kama ifuatavyo;
            “…na huyo paka! Yeye ndiye mlinzi wa kifo..(uk 9)”,
Wanajamii hii huamini kuwa paka anaweza kuwalinda dhidi ya kifo. Pia katika riwaya ya “Mirathi ya Hatari” Mzee malipula na wenzake wanajadili juu ya suala la safari ya kwenda Malawi kumpeleka Gusto wakajue nani aliyehusika na kifo cha Mzee kapedzile;
“…njia iliyobora ni kwenda Malawi kwa Chikanga yeye amejaaliwa na kipawa cha kujua yupi mcahwi yupi si mchawi…nilichanjwa kifuani nilichanjwa magotini na usoni na vidoleni chale zilipotoka damu nikapakazwa madawa ya aina aina….(uk 59).
Pia anaendelea kusema juu ya imani ya kishirikina;
 “…nilivishwa kitu kama hirizi…(uk 23)
hii imekuwa imani ya waafrika wakiamini kuwa hirizi inaweza kuwalinda dhidi ya magonjwa au wachawi. Hivyo Wiredu anashauri kuwa waafrika hawana budi kuachana na Mila hizi pamoja na imani hizi ambazo kwa sasa hazina nafasi tena.
Waafrika wanaamini uchawi miungu, uhalali wa utumwa na ukandamizaji wa mwanamke Kwasi Wiredu anashauri waafrika waachane na mambo hayo kwani hayana tija kwa maisha yao. Kuhusu Miungu, waafrika huamini katika miungu wanapopatwa na shida, shida hizo zilitatuliwa kutokana na imani hiyo ya Miungu. Haya yanadhihilishwa katika riwaya ya “Mirathi ya Hatari”
“…shida ya mvua, homa, ukame na mengineyo mengi…. Mahoka ya mababu, …enyi wazee mliotangulia.., …pembe hili linichome moto…”(uk 22)
Pia katika Miungu wanasema
 “….Mahoka wamempokea vyema kwao…(uk 52)”.
Hii inaonyesha kuwa Miungu wamepokea maombi yao. Vilevile katika riwaya ya “Nagona” kuna Padri aliyekuwa akihubiri habari za Kristo.
“..mimi nahubiri habari za kristo wewe unahubiri upagani…”(uk 19).
Hii ni kwamba waafrika walikuwa wakiamini kwenye upagani. Hali kadharika kuhusu uhalali wa utumwa hupenda kutumikiwa utemi, kuwa juu ya wengine yaani kunyenyekewa na watu wa chini yao. Mfano katika “Mirathi ya Hatari”, Mzee mavengi, Mzee malipula na wengine  walikuwa ni watu wenye mamlaka katika kijiji chao. Mzee malipula alikuwa Balozi wa nyumba kumi alitumia madaraka yake kuwanyanyasa wengine;
            “…hivi unafahamu kuwa mimi ni Balozi wa nyumba kumi kumi hapa…” (uk 60).
Kuhusu ukandamizaji wa mwanamke, waafrika wengi waamini kuwa mwanamke si chochote ni mtu asiye na umuhimu mkubwa sana kuliko mwanaume katika jamii. Hapa ndipo mfumo dume hujidhihilisha, falsafa hii inapendelea mwanamke kunyimwa uhuru hasa katika elimu, kuchagua mume ampendae. Mfano katika riwaya ya “Mirathi ya Hatari” pale msanii anapobainisha haya yafuatavyo;
            “…kumsomesha mtoto wa kike ni kama kumpa bangi imvuruge akili….?(uk 56)
Inaonekana kuwa wanawake wa kiafrika hawaaminiki kabisa katika kufanya lolote huu ni mfumo dume kuonekana kuwa mwanaume ndiye kila kitu. Hivyo Wiredu anashauri kuwa waafrika hawana budi kuachana na fikra hizo kwani ni potofu badala ya kuendeleza kuwalinda kwa madai kuwa ni falsafa yao.
Kwasi Wiredu anaonekana kuamini sana falsafa ya kimagharibi na kupuuza falsafa ya kiafrika, lakini katika mitazamo yake inazua maswali yafuatayo; je ni kweli hakuna falsafa ya kiafrika? Kama haipo kuna nini? Kama ipo ipoje? Je uchawi na ushirikina ni falsafa ya kiafrika? Kama ndio kwa nini? Kwa vipi? Na kama sio kwa nini? Hivyo hayo ni maswali kadhaa ambayo amewaacha wasomaji wakiwa bado wanajiuliza na kutokupata jibu kwani hajaweka wazi mambo hayo yote.
Placide, J.W. Temples
Huyu pia ni mwanafalsafa ambaye alikuwa padri aliyeishi nchini Kongo mwenye asili ya ufaransa na aliishi 1906 hadi 1977 alifanya uchunguzi juu ya sayansi ya makabila. Hivyo aliangalia falsafa ya kiafrika na kutoa baadhi ya mambo aliyoyachunguza kama ifuatavyo;
Maisha na kifo, mwanadamu katika fikra zake zimetawaliwa na vitu viwili yaani uhai na kifo, hivyo kwa waafrika mtu anayeweza kupunguza maisha ni mchawi na anayeweza kuongeza maisha ya mwanadamu ni mganga, hivyo waafrika wakipata matatizo huzirudia imani zao za jadi na Wahenga au mizimu huachiwa suluhisho la matatizo na wahenga wananguvu kuliko waliohai na hakuna kifo kisicho na sababu na kinatokana na uchawi. Hivyo haya yote yanajidhihilisha katika Riwaya ya “Mirathi ya Hatari” hivyo mwanafasihi anasema;
            “.. waaidha nilipewa kisu nikaonyeshwa sehemu za kukata…..”(uk 43)
Kutokana na kifo cha Mzee kapedzile sababu zilitolewa na Mzee malipula na Mzee mavengi kuwa aliyehusika ni Gusto.
“…..unasemaje nini, Dina? Mlifanya nini jana usiku?” ..usinidanganye sasa Gusto nafahamu yote, jana mmekutana na wale wazee mkamuua Kapedzile…..(uk 51).
Ukweli ni kwamba hata katika jamii zetu yapo mfano katika kabila la wabena kama mtu amefariki kwa ajali, au kufa ghafla ama kwa homa bado huwa inasadikika kuwa anaweza akawa ameuawa na miongoni mwa ndugu zake ili wapate kufanikiwa, na hii haipo katika jamii ya kusini tu mwa Tanzani bali ni viwakilishi tu kwamba jamii yote ya kiafrika mambo haya yapo.
Dhana ya kuhusu Mungu, Mwafrika anaamini kwamba kuna ngazi tofauti tofauti za kumfikia Mungu mkuu ambaye ndiyo nguvu kuu, Mizimu, Wahenga (walio kufa), Wazee waliohai, binadamu (mtu wa kawaida). Hivyo dhana hii inajidhihirisha katika riwaya ya “Nagona” ambapo mizimu imeonyeshwa kupitia Jogoo ambaye ni mzimu wa kulinda kisima, Paka Mzimu wa kulinda nyumba na kisima hicho cha damu. Pia Wahenga wazee waliokuwa wawili waliobakia pale kijijini walikuwa na uwezo wa kuwasiliana na mizimu, ambapo mizimu hiyo hufikisha taarifa kwa Mungu Mkuu. Kwa mfano Mzee aliyekuwa akilinda kisimani pale alikuwa anapata taarifa kupitia kuongezeka kwa damu kuwa kuna mtu atakuja.
Pia dhana hii ya imejidhihirisha katika riwaya ya “Mirathi ya Hatari” ambapo Gusto alikuwa na nguvu za sihiri bado aliamini kuwa Mungu bado yupo alichukuliwa na Madoda kwa ajili ya kuapishwa kuwa ndiye mrithi wa cheo kile alichokuwa nacho baba yake, lakini baada ya kuamka siku ya jumapili bado alijiandaa kwa kwenda kanisani, mfano;
“….niliporudi niliingia chumbani nikavaa nguo zangu rasmi tayari kwa kwenda kanisani… (uk 29).
Hivyo hii inaonesha jinsi waafrika wanavyoamini Mungu kuwa hata mambo yawe magumu au mepesi kuwa yeye pekee anayeweza kuwafanikishia mambo yao. Japokuwa waafrika tangia awali tulikuwa na dini zetu.
Mwafrika anaamini kuwa kuna watu wenye nguvu ya kubariki na kutoa laana pamoja na viongozi au wazee au watu mashuhuri. Hivyo wazo hili ni mojawapo ya mawazo ya Temples amejaribu kuwaainisha waafrika na kuona kuwa waafrika wanaamini hivyo katika maisha yao hasa pale mtu anapokuwa anaishi ama anakaribia kufa. Hivyo basi wazo hili linajitokeza katika riwaya ya “Mirathi ya Hatari” mwandishi amemtumia Mzee kazembe alimwita Gusto ili ambariki ampe mirathi. Lakini vilevile Mzee kazembe hakutaka kusogeleana na Rafael aliyekuwa amejitenga na kupewa laana na wazazi wake.
“….mwanangu nakuachia kazi kubwa. Ni urithi mkubwa ukitumia vema; bali pia ni mirathi ya hatari usipojihadhari nayo. Nakuachia dawa zote na milki yangu katika mizungu ya sihiri …(uk 15)”.
Pia Mzee malipula alimlaani binti yake Dina kuwa hawezi kufanikiwa baada ya kuonekana anataka kuolewa na Gusto ambaye alidaiwa kuwa mchawi hivyo Mzee Malipula hakupenda.
Hivyo jambo hili katika jamii zetu linajidhihirisha wazi pale wazazi waonapo mtoto anafanya vema, wanatumia fursa hii kuwabariki na kuwatakia mema katika maisha yao na siyo tu watoto hata jamii kwa ujumla ionapo mtu fulani anafanya vizuri basi humbariki.
Mwaafrika anaamini kuwa mchawi ana nafsi mbili yaani nafsi iliyotulia na nafsi inayotembea ambapo ipo katika makundi mawili kundi la ndoto (nafsi iliyotulia) na nafsi inayotembea ndiyo inayoweza kudhuru. Temples katika uchunguzi wa falsafa ya kiafrika amebaini hilo ambalo pia linajidhihirisha katika riwaya ya “Mirathi ya Hatari” Gusto alipoguswa mikono akiwa usingizini na mtu asiyeonekana ambaye ni Madoda;
“..usiogope Gusto ndimi Madoda mtumishi wa baba yako katika milki yake nimetumwa nije nikuchukue na nikuongoze huko wenzangu waliko……” (uk 18).
“…. Kweli hakuwa mwingine bali Madoda sura yake ilikuwa haijanitoka bado tangu tulipochunga ng’ombe pamoja…” (uk 19).
 Hivyo Madoda ni nafsi inayotembea na ndiyo yenye kumchukua Gusto wakati akiwa nyumbani kwao. Pia jambo hili hili linajitokeza katika riwaya ya “Nagona” ambapo tunakutana na nafsi inayotembea ambayo hudhuru na inajidhihilisha kama ifuatavyo;
“….nilishitukia napigwa viboko matakoni na mgongoni …nilipigwa viboko mfululizo lakini sikuweza kujitingisha…..”(uk 1).
Hapa ni nafsi inayotembea ambapo mtu anapigwa kiboko kichawi bila mtu kumwona. Hali kadharika katika jamii zetu jambo hili lipo mfano katika kabila la wabena (Njombe) mtu anayedhaniwa kuwa ni mchawi ukienda kumuuangalia usiku wa manane hata ukimshitua kwa nguvu mtu yule huwa haamuki lakini baada ya muda mtu yule akiamka husema nilikuwa nimesafiri, hivyo hii wazi kuwa ipo nafsi inayotembea na nafsi tuli.
Mwaafrika anatawaliwa sana na suala la ukarimu na ushirikiano katika shida na raha, Temples anaamini kuwa waafrika wamekuwa na ukarimu na ushirikiano hasa pale jirani ama ndugu yake anapopatwa na tatizo kama vile (msiba, ajali) na mengine yamfanyayo mtu kuwa na huzuni au kama kuna tukio la furaha kama vile kufanikiwa kitu fulani, arusi, jando na unyago, sherehe za kuhitimu shule na sherehe nyinginezo ambazo bado zinamfanya mtu awe mwenye furaha. Katika mambo hayo yote waafrika wanakuwa wakarimu pia hata kushirikiana ili kuhakiki jambo lile linafanikiwa, hivyo jambo hili limejidhihilisha katika riwaya ya “Mirathi ya Hatari” kama ifuatavyo;
“…..msichana mdogo aliyekuwa anazungumza na mama “kamwene binti yangu… habari gani zikuletazo asubuhi hivi?….(uk 49).
                “…mimi nakwenda huko kwenye kilio labda nitarudi tu jioni kuchukua matandiko..” (uk 50).
Bado wazo hili linajidhihirisha katika riwaya ya “Nagona” ambapo Mzee wakati anamkaribisha msanii na hii ndiyo inayoendelea kuthibitisha kuwa waafrika wanaukarimu.
“….karibu karibu karibu uketi. Tumekuwa tukikusubiri,” sauti ilitoka katikati ya mwanaga wewe mwenyewe” ahsante…(uk 14)”.
Hivyo kama ambavyo yamedhihirishwa katika riwaya zote mbili yaani Mirathi ya hatari na Nagona inasawili katika jamii zetu za kiafrika kwani waafrika hushirikiana na kuwa wakarimu katika shida na raha pale litokeapo tukio la furaha ama la huzuni kwa ndugu au jirani.
Mwaafrika hasahau jadi au asili hata kama ana elimu ya kimagharibi na kimashariki. Utafiti huu wa Temples katika suala hili ni kweli kwani licha ya kuwa mtu ana elimu ya juu kabisa ya kimagharibi yaani katika shahada ya kwanza, shahada ya uzamili pia shahada ya uzamivu bado akilejea kule alikozaliwa hufuata mila na taratibu zilizopo katika jamii husika bila kwenda kinyume, mfano katika makabila kama ni msukuma akirudi alikozaliwa huongea kisukuma na kama mnyakyusa hali kadharika. Na pia licha ya mtu kuwa na elimu hiyo bado anaamini nguvu za sihiri na hii imejidhihirisha katika riwaya ya “Mirathi ya hatari” ambapo mwandishi amemtumia mhusika Gusto ambaye alikuwa ana elimu hiyo lakini bado anaamini kuwa hirizi ndiyo yenye kumfanikisha kufaulu mitihani;
            “…baba yako ni mchawi na hiyo hirizi uliyoivaa ni ya madawa ya kufaulu mitihani…(uk 6).”
Pia jambo hili linajitokeza katika riwaya ya “Nagona” ambapo mwandishi amemtumia mhusika Mkombozi wa pili pamoja na kuwa msomi lakini aliwafuata wazee wa mila ili kuleta ukombozi mbali na elimu aliyokuwa nayo ya kimagharibi;
“…nilipomkaribia niliinua tena mikono yangu…(uk 37)”
Kwahiyo basi ni hili lipo hata kwa sisi japo tuna elimu ya kimagharibi lakini hatuzipuuzi mila na desturi za kule tulikotoka.
Kila mtu ana chembe za nguvu hai yaani inayomwezesha kutenda mambo yake na chembe hai ya kike ni kubwa zaidi kuliko ya kiume. Uchawi ni nguvu hai watu hutumia kupatia vyeo, ushindi na hata vita, lakini nguvu hai inaweza kuboresha au kufifiza katika utendaji wa mambo. Mfano, matumizi ya hirizi na kupiga lamri ni kuongeza nguvu hai. Hivyo jambo hili limejitokeza katika riwaya ya “Mirathi ya Hatari” ambapo Gusto amekuwa akitumia hirizi aliyopewa na mama yake ili kujikinga na maovu kijijini na hata wakati mwingine kuitumia ili kuweza kufanikisha kuyafanya masomo yake kwa ustadi wa hali ya juu, kwani utumiaji wa hirizi ndio umemfanya Gusto asidhurike na maovu ya kijijini;
“…ni kweli kwamba nilikuwa navaa hirizi; hirizi niliyopewa na mama kama kinga ya maovu kijijini.(uk 6).
“….wengine tulipochoka yeye alikuwa kama vile ndiyo kwanza anaanza. Hata leo bado nashangaa nguvu zile alizipata wapi….” (.Uk 5)
Pia katika riwaya ya “Nagona” ambapo mhusika Mimi anaonekana ana chembe nguvu hai zilizomwezesha kuyashinda mambo makubwa kama ya kishirikina na kichawi yaliyomkabili katika safari yake (uk 1-3).
 
Hivyo basi nukuu hizi inaonesha namna waafrika wanavyoamini nguvu za sihiri katika kuyashinda mambo hata yawe magumu ama mepesi hirizi na lamri ndiyo mshindi wao katika kuyatatua kwani ndio aliyeyafanya mambo hayo yawepo hapa dunia.

Print this item

  Ufafanuzi wa shairi la Jiwe si Mchi toka diwani ya Wasakatonge ya M.S. Khatibu
Posted by: MwlMaeda - 08-28-2021, 07:30 AM - Forum: Ushairi - No Replies

BOFYA HAPA KUTAZAMA >>>>

Print this item

  LULU YA USHAIRI NA Abdilatif Abdalla
Posted by: MwlMaeda - 08-28-2021, 07:10 AM - Forum: Ushairi - No Replies

BOFYA HAOA KUTAZAMA >>>>

Print this item

  LULU YA USHAIRI NA Abdilatif Abdalla
Posted by: MwlMaeda - 08-28-2021, 06:56 AM - Forum: Ushairi - No Replies

BOFYA HAPA KUFUNGUA >>>

Print this item

  SHAIRI: NAKUPENDA VIOLETH
Posted by: MwlMaeda - 08-27-2021, 07:47 PM - Forum: Ushairi - No Replies

NAKUPENDA VIOLETH
Kwangu naona bahati, kukupata mke wangu,
Nikwonapo Violeth, moyo walia ngungungu,
Nimepewa Stiwart, zawadi toka kwa Mungu,
Nakupenda Violeth!

Hata nikienda mbali, bado nakufikiria,
Mapenzi Kama awali, moyoni yalivyomea,
Na tupendane wawili, achana nao wambea,
Nakupenda Violeth!

Mfano wako maua, ona ulivyojitenga,
Umbo umejichorea, hasa ukivaa kanga,
Mie chali nahemea, mpenzi umenifunga,
Nakupenda Violeth.

Na hivi unanilea, kwa chakula na mavazi,
Kitambi wakifumua, Violeth yako kazi,
Hakika nakuambia, wewe ni mke mjuzi,
Nakupenda Violeth!

Macho nilishapofuka, wenginewe siwaoni,
Najua wananitaka, naona wakazi gani,
Mrembo umeumbika, mwenye shepu kama mbuni,
Nakupenda Violeth.

Idara umetimia, jikoni na kitandani,
Nazidi kukuzimia, vile unanithamini,
Nani anakufikia, naona haufanani,
Nakupenda Violeth.

Mpenzi nipo njiani, sana nimekukumbuka,
Niandalie maini, chumba ukishatandika,
Ndo wangu nambari wani, mumeo sasa nafika,
Nakupenda Violeth.

Print this item

  (MTAGUSANO) NA MBINU ZA KIFANI KATIKA RIWAYA YA BINA – ADAMU
Posted by: MwlMaeda - 08-27-2021, 06:35 PM - Forum: Riwaya - No Replies

Mtagusano
Ni athari au mwingiliano wa vipengele mbalimbali katika kazi za fasihi, kwa kawaida hii inahusishwa na mwigo au uathiriano wa kazi moja na nyingine.

SWALI: Jadili kipengele cha fani katika riwaya ya Bina-Adamu kwa kuzingatia mielekeo chomozi ya kifani katika riwaya ya Kiswahili ambayo ni:

 
Mwendo wa riwaya.
Naratolojia.
Msuko wa vitushi.
Uhusika na wahusika.
Mtagusano.
Kipengele cha lugha.
Mbinu za kibunilizi.
Mtindo.

 
[url=http://mwalimumkindi.blogspot.com/2016/08/vipengele-vya-kifani-katika-riwaya.html][/url]Bina-Adamu ni riwaya iliyoandikwa na Wamitila KyalloWadi na kuchapishwa na Phoenix Publishers mwaka 2002, Nairobi, Kenya.
Wamitila KyalloWadializaliwa mwaka 1966 katika nchiya Kenya. Ni mwandishi mwenyeshahada ya Ph. D katika somo la fasihi. Mwandishi huyuamebobea katika fani za fasihi ambazo nitamthiliya, hadithi fupi, riwaya na mashairi.Pia ni mhakiki wa fasihi ambayeamechapishamakala mbalimbali katika majarida ya kisomi Afrika, Ulaya na Marekani:
Baadhi ya kazi zake ni kama zifuatazo:
-Bina-Adamu-2002
-Jumba la Huzuni-2006
-Kamusi ya Ushairi-2006
-Kuku na Mwewe-2006
-Harufu ya Mapera-2012
-Nguvu ya Sala (Riwaya)
-Shingo ya MbungenaHadithi Nyingine-2007
-Uncle’s Jokes-2007
-Wingu la Kupita
Bina-Adamuni riwaya inayotumiasitiari ya kijijikuangalia hali ya mataifa ya ulimwengu katika kipindi hiki ambapo hali za kijamii, kisiasa na kiuchumi zinadhibitiwa na ubepari wa mataifayaliyoendelea. Hii ni riwaya changamano yenye ufundi wa lugha na kimtindo, inayomfanya msomaji awaziesiotu yanayozungumzwa bali pia muundo wa riwaya ya Kiswahili.Hii ni riwaya dhati ambayo ipo katika kigezo cha fani upande wa riwaya changamano ambazo hutumia lugha fiche, mandhari fiche, majina na mtiririko wa matukio huwa changamano.
Kwa mujibu wa Wamitila katika kamusi yake ya fasihi, isimu na nadharia, (2003) anaonyesha aina tofautitofauti za riwaya kama vile riwaya changamano, riwaya sahili, riwaya kiambo na nyinginezo. Katika uainishaji huu, riwaya huweza kuainishwa kwa kutumia vigezo vya kifani, kimaudhui, upeo wa kijiografia na kigezo cha usimulizi. Pamoja na vigezo vyote hivyo, riwaya huweza kugawanywa katika makundi makuu mawili yaani riwaya dhati na riwaya pendwa.
Katika kuainisha riwaya hii ya Bina-Adamu, tunaiainisha kwa kujigeza katika kigezo cha fani ambapo tunaona kuwa hii ni riwaya changamani kwa sababu mwandishi ametumia lugha ya mafumbo, hivyo msomaji anahitajika kuwa na ufahamu wa kutosha ili aweze kuielewa riwaya hii. Kwa mfano katika ukurasa wa 100, mwandishi anasema:
“Nilikumbuka vituko kadhaa nilivyopitia huko nyuma kuanzia Zakongwe wazee walinieleza matatizo mengi waliyokabiliana nayo zamani walipokuwa wakipambana na mazimwi yaliyovamia nyumba miaka mingi iliyopita.”
Hapa mwandishi ametumia mazimwi kuelezea jinsi gani nchi za kiafrika zilitawaliwa na wakoloni na ndipo wakaamua kupambana nao kuwaondoa. Hapa tunaona kuwa ili msomaji aweze kuelewa maudhui yaliyomo katika riwaya hii anapaswa kutumia tafakuri ya hali ya juu sana. Mara nyingi waandishi hutumika mbinu hii ya ufumbaji ili kukwepa mkono wa dola na kuepuka udhibiti wa kazi zao za fasihi.
Mwandishi wa riwaya hii amefanikiwa kwa kiwango cha juu katika utunzi wake katika kipengele cha fani na maudhui pia. Kwa kujikita katika kipengele cha fani, mwandishi amefanikiwa kutumia mielekeo chomozi ya kifani kwa kiasi kikubwa. Mielekeo chomozi ya kifani ambayo imejidhihirisha katika riwaya hii ni kama ifuatavyo:
Naratolojia; hikini kipengele ambacho huelezea namna ambavyo usimulizi umefanyika katika kazi ya fasihi. Dhana ya usimulizi kwa mujibu wa Madumulla (2009:110), ni dhana katika fasihi inayobainisha sehemu alipo anayesimulia hadithi au tukio, kwa jinsi hiyo, msomaji anapata picha ya jinsi matukio yanavyohusiana, yanavyosababishana na yanavyo endelea mwanzo hadi mwisho.Msimuliaji anaweza kutumia usimulizi shahidi au usimulizi maizi. Naratolojia husaidia kuelewa maudhui kutokana na jinsi mtunzi alivyoipangilia kazi yake. Ili usimulizi uweze kueleweka kwa hadhira, mtunzi hana budi kuwa na taaluma hiyo ya usimulizi na uzingativu wa lugha anayoitumia kulingana na jamii aliyoikusudia kuifikishia ujumbe.
 Katika kitabu hiki cha riwaya ya Bina-Adamu, usimulizi shahidi umetumika kwa kiasi kikubwa. Usimulizi shahidi kwa mujibu wa Wamitila (2006:41),ni usimulizi ambao hutofautiana na usimulizi wa nafsi ya tatu kutokana na sifa yake ya kutoweza kuyaona yote isipokuwa, kama tulivyoona, usimulizi wa tendi. Anaendelea kusema kuwa msimulizi anayepatikana katika kazi iliyosimuliwa hivi huwa ana mkabala mmoja tu maalum. Mawazo anayoyatoa kuhusu tukio mtu au hali huwa yake tu. Mwandishi wa riwaya hii amejikita kwa kiasi kikubwa katika aina hii ya usimulizi kwani tunaona matumizi ya nafsi ya kwanza yametumika kwa kiasi kikubwa sana kuanzia mwanzo wa riwaya hii hadi mwisho japo ametumia aina nyingine ya usimulizi. Kwa mfano katika ukurasa wa 7 mwandishi anasema:
“Nilipozaliwa niliwakuta watu wakikiogopa kiini cha kijiji chetu na mpaka leo unapoisoma hadithi hii bado wanakiogopa.”
Pia ametumia usimulizi shahidi katika ukurasa wa 32 ambapo anasema:
 “Nilishindwa kuelewa. Lakini ili kuuficha mshangao wangu niliamua kumuuliza maswali.” Katika ukurasa wa 79 mwandisi anasema:
“Nilianza kujilaumu kwa kutomwelewa nyanya yangu.”
Pia usimulizi maizi umetumika kwa kiasi fulani katika riwaya hii. Wamitila (2006:40) anasema kuwa usimulizi maizi ni usimulizi ambao hufuata mkondo unaodhihirisha ufahamu wa siri na mambo yote. Katika usimulizi maizi, msimulizi huwa na sifa za ki-ungu na humaizi na kuelewa kila kitu kinachowahusu wahusika, mandhari, hadithi, mwelekeo, saikolojia ya viumbe wa hadithini, na kadhalika. Kwa mfano ukurasa wa 7 mwandishi anasimulia kwa kuwaelezea watu watatu ambao waliishi kijijini kwao hapo zamani. Mwandishi anasema:
 “Mmoja alikuwa mhubiri aliyeishi upande wa pili unaoelekeana na machweo ya jua. Nyumba yake siku hizi imebakia kuwa banda kuu baada ya mkewe kuondoka kwa kulalamika chakula kimepotea na wamebakia kula vyakula vinavyotolewa kama sadaka na waumini.”
Katika   ukurasa wa 8 mwandishi anasema:
“Mkazi wa tatu hakujulikana kwa jina na watuwengi kijijini. Lakini alikuwa na watoto watatu; huntha waliondoka zamani na haijulikani walikozamia.”
Msuko wa vitushi, kwa mujibu wa Mbunda Msokile (1992:206) ni mtiririko au mfuatano wa matukio yanayo simuliwa kuanzia mwanzo hadi mwisho. Mbinu hii ya Msuko wa vitushi husaidia katika kufikisha maudhui kwa hadhira na humrahisishia msomaji katika usomaji.
Pia Wamitila (2006:6) anatoa maana ya msuko kuwa ni mfuatano wa matukio yanayopatikana katika kazi ya kifasihi kwa kutegemea uhusiano wake kiusababishi. Yaani tukio fulani linasababishwa na nini? Hivyo basi kipengele hiki huangalia motifu mbalimbali alizotumia mwandishi pamoja na mjongeo wa vitushi.
Motifu kwa mujibu wa kamusi ya Kiswahili sanifu (2010:963) ni sababu, matilaba au malengo, msukumo wa kufanya jambo fulani. Zipo aina nyingi za motifu ambazo zinaweza kutumika katika kazi ya fasihi. Baadhi ya motifu zilizo tumika katika riwaya hii ni motifu ya safari ambayo huonyesha mhusika au wahusika wakiwa katika safari.Motifu hii ya safari inajidhihirisha kuanzia sura ya kwanza hadi sura ya mwisho ya riwaya hii ya Bina-Adamu. Kwa mfano katika ukurasa wa 12 anasema:
 “Nilikuwa bado nimesimama niliposhituka nimepigwa teke la nyuma na kuambiwa haya anza safari yako ya ufumbuzi.” 
Pia motifu hii ya safari imejidhihirisha katika ukurasa wa 27 ambapo mwandishi anasema:
“Baada ya safari ndefu tulitokeza sehemu iliyokuwa na miti mingi ajabu”
Vilevile katika ukurasa wa 76, mwandishi anasema:
“Badala ya kuifuata ile njia niliyokuwa nimependekezewa na yule kijana, nilishika njia tofauti iliyoishia baharini.”
Vilevile katika ukurasa wa 33 mwandishi anasema:
“Baada ya kutembea mita kama mia moja hivi, nilitokea mahali palipokuwa na majengo yaliyoonekana kama ya miaka mingi.”
Pia ukurasa wa 89, mwandishi anasema:
“Nilianaza safari yangu tena. Nilikuwa sijaenda mbali niliposikia mmoja wao akiniita kutoka nyuma.”
Motifu ya safari imejidhihirisha tena katika ukurasa wa 88 ambapo mwandishi anasema:
“Wewe ni Msafiri,” aliniambia, inamaana bado hujaimaliza safari yako. Jikaze. Ufikapo mwisho wake utajua maana ya wimbo huu.”
Aina nyingine ya motifu ambayo imejitokeza katika riwaya hii ni motifu za majini au baharini. Aina hii ya motifu huhusisha safari ndani ya maji. Katika ukurasa wa 15 mwandishi anasema:
“Niliamua kuufuata ushauri wake. Hatukuenda sana kabla ya kutumbukia kwenye mto uliokuwa na maji mengi ajabu lakini hatukuzama, badala yake tulielea juu juu……….”
Pia katika ukurasa wa 21, mwandishi anasema:
 “Nilipozinduka nilikuwa kwenye mto wa ajabu. Maji yake yalikuwa yakienda kwa kasi ya ajabulakini mara hii hayakuwa yakienda nyumanyuma bali yalienda mbele”.
Vilevile mwandishi wa riwaya hii ya Bina-Adamu ametumia motifu ya mambo ya ajabu ajabu, majini na mazimwi kwa kiasi kikubwa sana. Motifu hii hujumuisha vitu ambavyo havionekani katika mazingira halisi lakini huwasilisha dhana fulani kwa hadhira, ambayo ikiletwa katika uhalisia inaeleweka. Motifu hii imejitokeza sehemu nyingi katika riwaya hii. Kwa mfano katika ukurasa wa 10, mwandishi anasema:
 “Nilijaribu kushikashika hapa na pale kama mtu asiyekuwa na uwezo wa kuona. Nilishitukia nimepigwa kofi kali “huyu ni nani anayewakanyaga wanangu? Mjinga gani? Mnatufuatia nini mpaka huku nyie? Wajinga wakubwa, kwanini hamtosheki na dunia yenu?” ilisema sauti ya kike kwa uchungu.”
Pia katika ukurasa wa 78, mwandishi anasema:
 “Nilipozinduka lile gogo lilikuwa karibu sana na nilipokuwa nimelala. Nilipigwa na butwaa kubwa. Nililiangalia tena. Lilichukua sura ya nyanya kisha baada ya muda nikaona likichukua sura ya mke wangu halafu Hanna.”
Vilevile mwandishi ametumia motifu hii katika ukurasa wa 14 ambapo anasema:
“Nilipotua nilishitukia nimesimama na jitu refu, nilijitahidi kusimama ili niweze kuliona jitu hilo vizuri. Ilikuwa shida kuliona sawasawa. Miguu yake ilikuwa mikubwa ajabu. Nilirudi nyuma kuweza kuliona vizuri lakini likarefuka nikashindwa kuliona vizuri.”
Pia mwandishi anaendelea kuonyesha motifu hii katika ukurasa wa 137, ambapo anasema:
“Niliguswa bega la kulia na kugeuka kwa wepesi wa ajabu lakini sikumwona yeyote. Niliangalia mbele kisha nikaguswa bega la kushoto,usishangae, sauti hapa zinaingiliana, ndio uhalisia mpya huu.”
Pia katika Ukurasa wa 156, mwandishi anasema:
“Majini ya pale yamemshika! Jinsia yake itabadilika!”
Vilevile katika ukurasa wa 144, mwandishi anaonyesha motifu hii kwa kusema:
 “Nilikuwa na nia ya kusogea karibu na kuangalia vizuri nilipopigwa ngoto kali na kuambiwa kwa sauti ya juu, huna muda wa kumangamanga hapa kama mmanga. Huntha umewaona au hata kuwatambua? Je, na Peter P….?”
Aina nyingine ya motifu ni motifu ya ndoto. Motifu ya ndoto hutumiwa na msanii wa kazi ya fasihi kwa lengo la kuwasilisha dhamira nzito katika jamii au hutumika motifu hii kwakukwepa mkono wa dola katika kuwasilishakatikakile alichokusudia kwa jamii. Wakati mwingine, mwandishi anapotumia ndoto huwa ni mbinu ya kuipa kazi yake upekee au kuepuka kuwasilisha dhamira kwa njia ya kawaida pasipo kuonyesha athari ya mhusika moja kwa moja. Katika kuthibitisha hili, mwandishi anaonyesha ukurasa wa 77 ambapo anasema:
“Ghafla nilisikia sauti iliyofanana na iliyonijia katika ndoto.”
Kwa upande wa mjongeo wa vitushi katika riwaya hii ni sahili kwa sababu visa na matukio yamepangiliwa moja kwa moja kuanzia mwanzo hadi mwisho. Tunaona kuwa mwandishi anamuonyesha Bina-Adamu jinsi anavyoanza safari yake, vikwazo anavyokutana navyo katika safari yake hadi anapofika mwisho wa safari yake. Mbinu hii humsaidia katika kuumba matukio na kuyaendeleza katika kazi za fasihi,
Mwendo wa riwaya ni ule mtiririko na mshindilio wa vitushi katika riwaya kwa kuzingatia vigezo vya Msuko, mandhari, masafa ya kiwakati na kijiografia. Katika riwaya hii ya Bina-Adamu, mwandishi ametumia Mwendo wa polepole. Tumebaini kuwa ni Mwendo wa polepole  kwa sababu zifuatazo:
Kwanza mwandishi anasimulia kila tukio hatua kwa hatua ambapo harushi matukio ya riwaya hii. Usimulizi shahidi uliotumika katika riwaya hii unadhihirisha hili kwani kila kile anachokisimulia, amekishuhudia. Kwa mfano katika ukurasa wa 54, mwandishi anasema:
“Nilitokeza mbele ya wazee waliokaa na vijana kwenye kikundi. Wote walikuwa wakifanya kazi huku wakiongea. Waliponiona walinijia na kunialika kujiunga nao. Wawili waliondoka na kurudi na sahani lililokuwa na chakula. Niliwaangalia.”
Pili, maudhui yaliyotumika katika riwaya hii, kwa kiasi kikubwa ni ya kitanzia kitu ambacho kinatudhihirishia kuwa Mwendo wa riwaya hii ni wa polepole. Kwa mfano, katika ukurasa wa 144-145 mwandishi anasema:
“Nakumbuka kijijini kulikuwa na barabara iliyokuwa na daraja dhaifu. Mwaka mmoja palitumbukia gari dogo wakafa watu wawili. Viongozi walisema watafikiria la kufanya. Kimya. Miaka miwili baadaye hali hiyo ikajirudia, mara hii wakasema tumejifunza. Kimya. Mara ya tatu lilitumbukia basi la abiria wakafa watu mia, ikawa mara hii lazima tutajenga daraja upya kuzuia tanzia ya kitaifa kama hii. Mpaka leo bado, wanangojea kukumbushwa.”
Pia katika ukurasa wa 133, mwandishi anasema:
“Mwenzetu amepigwa risasi nyingi ajabu, kwa kudhaniwa mwizi, kudhaniwa tu unasikia?”Utanzia mwingine unaojitokeza katika ukurasa wa 137 na ukurasa wa 148.
Tatu, Mwendo wa riwaya hii ni wa polepole kwa sababu za kijiografia ambapo mwandishi anaonyesha mandharia ya kiafrika na mandhari ya kimagharibi kwa kuonyesha kipindi kirefu ambacho Bina-Adamu alikuwa katika safari yake. Kama mwandishi angeonyesha maramoja kuwa amefika huko alipokuwa akienda ambako ni nje ya bara la Afrika pasipo kuonyesha matukio aliyoyafanya njiani, ungekuwa ni mwendo wa haraka.Kwa mfano katika ukurasa wa 130-131 anaonyesha majengo ya Mefu na jengo la Pembetano ambako Bina-Adamu alikuwa amefika huko.Pia mwandishi anaonyesha mandhari ya nchi za kimagharibi katika ukurasa wa 119 anaposema:
“Darling, huyu anatoka jana. Hawa ndio wanaojua furaha. Nilitamani kuwaeleza kuwa maisha yetu yalikosa furaha kwa sababu ya umasikini na uongozi mbaya.”
Katika maneno hayo hapo juu, ni ya watu wawili ambapo awalimmoja alikuwa Afrika lakini kwa wakati huualikuwa nje ya Afrika na kukutana na mwenzake huko ughaibuni.
Mwendo wa riwaya husaidia katika kubaini masafa ya wakati na masafa kijiografia katika kazi za fasihi.
Mtindo kwa mujibu wa Wamitila (2006: 28),ni upangaji wa fani na maudhui katika kazi ya fasihi kwa njia ambayo hatimaye hutokeza au huonyesha nafsi na au labda upekee wamtunzi huyu. Kwa ujumla, mtindo hurejelea mbinu aitumiayo msanii wa kazi ya fasihi katika kufikisha ujumbe wake.Mwandishi wa riwaya ya Bina-Adamu ametumia monolojia kwa kiasi kikubwa katika kazi yake kwanzia sura ya kwanza hadi sura ya mwisho. Katika ukurasa wa 7, mwandishi anasema kuwa:
“Nilipozaliwa niliwakuta watu wakikiogopa kiini cha kijij chetu na mpaka leo hii unapoisoma hadithi hii bado wanakiogopa. Kijiji chenyewe kimezungukwa na mito isiyokaukwa na maji pande zote na kimejitenga na vijiji vingine vinavyohusiana nacho kama Utaridi na Kausi. Katikati pana mti mkubwa ulioota na unaoonekana na mtu akiwa mbali na kilipo kijiji chenyewe”.
Pia ametumia dayolojia ili kuipa uhai kazi yake. Katika ukurasa wa 15,mazungumzo kati ya Hanna na Bina-Adamu mwandishi anasema:
“Mimi naitwa Hanna, unaweza ukasema Anna ukitaka’’,aliniambia. Anaongea kama yeye kabisa, nilijiambia.”
“Hapa ni wapi?”
 “Umeuliza swali hilo mapema mno! Ulipotoka hukufunzwaharakaharaka hainaBaraka?”
Hayo ni mazungumzo kati ya Bina-Adamu na Hanna,alipokuwa nataka kujua ni wapi aliko na anaelekea wapi. Majibizano pia yametokea uk 34-35, piauk. 47 mazungumzo baina ya Bina-Adamu na mzee mmoja aliyekuwa anamwambia Bana-Adamu asimshangae:
 “Usishangae Bina-Adamu Msafiri!” alisema Yule mzee kwa sauti dhaifu lakini imara.
 “Kulifanyika nini huku?” niliuliza.
“Matokeo ya mchezo!”                          
“Wa nani?……..”
Majibizano pia yametokea uk 68-69,uk 70-71, uk 95-97,uk 108,uk 119,uk 124,uk 127-128,uk 130,uk 141-142,uk147,uk 150-151,uk 152-153,uk 154-156.
Matumizi ya nafsi katika riwaya  hii yaBina-Adamunafsi  zote  tatu zimetumika lakini nafsi  ya kwanza na ya  tatu ndizo zilizotumika kwa kiasi  kikubwa  zaidi kuliko nafsi ya pili.
Kwa kuanza na nafsi ya kwanza  umoja  hii ndiyo imetawala kwa kiasi kikubwa  takribani riwaya yote  kwa  mfano  nafsi  ya kwanza  umoja   imetumika  ukurasa wa  7 mwandishi anasema:
“Nilipozaliwa niliwakuta watu wakikiogopa kiini cha kijiji chetu na mpaka leo hii unapoisoma hadithi hii bado wanakiogopa”
Pia matumizi ya nafsi ya kwanza yanajitokeza katika ukurasa wa 11, 12, 15, 27, 52, 59, 67.87, 119, 121, 129 na kadhalika.
Vilevile nafsi yakwanza wingi imeonekana katika ukurasa   wa 74 mtunzi anasema:
 “Tulizunguka kuangalia nyumbanyingine lakinitukashindwa kuzimaliza kwa siku moja”
Matumizi yanafsi ya pili umoja na uwingi pia yamejitokeza kwa kiasi kidogo. Mfano nafsi ya pili umoja  katika ukurasa wa  16, 88, 124,125 na 154  na  nafsi   ya pili uwingi inajidhihirisha katika ukurasa  wa 112 mwandishi  anasema:
“Tatizo lenu kuu, hamtaki kuukabili uhalisia wenu na kujitahidi   kuubadilisha……………”
Pia kwa kiasi fulani nafsi ya tatu imetumika katika umoja na uwingi .kwa  kuanza na nafsi  ya tatu umoja  nafsi  hii  imetumika  katika   kurasa zifuatazo  18, 19, 50,  55,  58,  86,  87, 97, 103, 108,  117,  124,  126, 128, 132, na sehemu nyinginezo. Mfano katika ukurasa wa 132 mtunzi anasema:
 “ Alinizungusha  nyumbani  akinieleza ,  “ Hii ni friji ambayo  ina uwezo  wa kumfanyia  mtu mambo mengi.”
Kwa upande wa nafsi   ya tatu uwingi imejitokeza katika ukurasa wa 17, 19, 38, 50, 57, 99, 100, 101, 102, 113 na kadhalika. Mfano katika ukurasa wa 100 mwandishi anasema:
 “Walielezea matatizo waliyoyapata siku hizi: karo ya watoto, upungufu wa chakula, magonjwa, matatizo ya kazi, hospitali kukosa dawa, wizi wa nguvu; tuseme shida za kila aina.”
Pia katika kipengele cha mtindo, mwandishi hutumika lugha kwa namna ya kipekee sana na kibunifu sana.

Kipengele cha matumizi lugha kitajadiliwa kwa undani katika mbinu za kibunilizi na katika mtagusano ambapo kuna matumizi ya lugha mbalimbali.
Umuhimu wa matumizi ya nafsi ya kwanza ni kuonesha ushahidi wa matukio anayoyasimulia kwa hadhira yake kwa ukina.  Na matumizi ya nafsi ya pili humufanya msomaji kujiona kuwa yeye ndiye mlengwa mkuu wa kazi husika. Matumizi ya nafsi ya tatu humweka karibu msomaji wa kazi husika.Mbinu hii ya mtindo, hutumika kwa lengo la kuipa uhai kazi ya fasihi, kuwachora wahusika wake, kuonyesha upekee wa kazi ya mtunzi na kufikisha ujumbe kwa hadhira.
Uhusika na wahusika. Wahusika kwa mujibu wa Senkoro, (2011:7) ni watu ama viumbe waliokusudiwa wawakilishe dhana, mawazo au tabia za watu katika kazi ya fasihi. Uhusika wa wahusika katika riwaya ya Bina-Adamu unajitokeza pale wanapopewa sifa na tabia fulani na kuweza kuwa wawakilishi wa watu wema au wabaya.  Katika riwaya hii mwandishi ameonyesha wahusika wanaojipambanuawaziwazi na wahusika ambao hawajipambanui waziwazi.
Wahusika ambao wanajipambanua waziwazi ni kama vile, Mhubiri, Mwanasayansi, Kichaa na Bina-Adamu Msafiri. Kila mhusika, uhusika wake unaonekana katika riwaya hii kulingana na mwandishi wa riwaya hii alivyompa uhusika huo. Kwa mfano uhusika wa Bina-Adamu unajidhihirisha kuanzia mwanzo wa riwaya hii hadi mwisho. Uhusika wake unaonyesha matendo na tabia ambazo zinastahili kuigwa katika jamii kwani anaonyesha juhudi ya kufanya uvumbuzi ambao unaibua dhamira ya upelelezi na kufanya mapinduzi.
Pia mwandishi ameonyesha wahusika ambao hawastahili kuigwa katika jamii kutokana na jinsi walivyochorwa na mwandishi. Kwa mfano P.P ambaye ni Peter Pan hastahili kuigwa katika jamii kwa mfano, Ukurasa wa 71 mwandishi anasema:
“Sasa huyu P.P ni nani anayeelekea kuhusika na kila kitu? Nilijiuliza. Niliyakumbuka maafa niliyoyaona huko nyuma nilikoelezwa yalitokana na bomu lake.”
Pia mwandishi ametumia wahusika ambao uhusika wao ni wa ajabuajabu kwa sababu wana sifa kama mizimu. Kwa mfano. Mwanishi anamchora mhusika Hanna kama mhusika ambaye anabadilikabadilika na wakati mwingine anatokea na kupotea. Mwandishi anathibitisha hili katika ukurasa wa 32 kwa kusema:
“Hanna alikuwa ametoweka sasa lakini wale viumbe wa ajabu walikuwa wakiongoza njia,”
Licha ya mwandishi kutumia wahusika wanaobadilikabadilika wamefanikiwa kuonyesha uhusika wao kwa kutoa msaada mkubwa wa kumwongoza Bina-Adamu.
 Kwa upande wa wahusika wasiojipambanua waziwazi, mwandishi anamwonyesha mhusika X katika ukurasa wa117 ambapo mwandishi anasema:
“Jina langu ni X. Basi karibu leo na kesho. Karibu utafika kwenye Bustani ya Eden ya pili!”
Mianzo na miishoni mbinu ambayo hutumiwa na wasanii wa kazi za fasihi katika kazi zao kwa kusudi la kuiandaa hadhira katika kazi husika, kuonyesha mwazo wa hadithi na uhitimishwaji wa hadithi. Mbinu hii mara nyingi hutumika katika kazi za fasihi simulizi na katika fasihi andishi kwa kiasi kidogo. Kazi za kifasihi za zamani zinautofauti mkubwa sana kwa na kazi za siku hizi. Kazi nyingi za kifasihi za zamani zilikuwa zikifuata mianzo na miisho ya kifomula kwa sehemu kubwa tofauti na kazi za siku hizi ambazo mara zinakuwa na mianzo ya kawaida. Mwandishi wa riwaya hii ya Bina-Adamuametumia mianzo ya kawaida ambayo siyo ya kifomula. Kwa mfano katika ukurasa wa 7, anaanza kwa kusimulia visa vyake moja kwa moja pasipo kufuata mianzo ya kifomula ambavyo huanza kwa namna ya kipekee kama vile, “hadithi hadithi…..”, “puakwa…..pakawa”, na mianzo mingineyo. Mwandishi anaanza kwakusema:
“Nilipozaliwa niliwakuta watu wakiogopa kiini cha kijiji chetu na mpaka leo unapoisoma hadithi hii bado wanakiogopa. Kijiji chenyewe kimezungukwa na mito isiyokaukwa na maji pande zote.”
Pia katika kuhitimisha riwaya hii, mwandishi hajaonyesha miisho ya kifomula ambayo mara nyingi huishia na maneno kama vile, “hadithi yangu ikaishia hapo”, na “wakaishi kwa raha mstarehe”. Mwandishi amemalizia kazi yake kwa kawaida sana ambapo anaiacha hadhira yake bila kuridhika kwani haonyeshi dhahiri nini kiliendelea baada ya Bina-Adamu kufika alipokuwa amekwenda kuwatafuta huntha watatu jambo ambalo ni tofauti na kazi nyingi za kifasihi ambazo huwa na miisho ya kifomula.
Mtagusano ni kipengele kinachohusiana na muingiliano wa vipengele mbalimbali katika kazi ya fasihi kutokana na athari za utamaduni na sayansi na teknolojia. Mtagusano umejitokeza kama dhamira, madhari na lugha.
Mtagusano unajidhihirisha katika riwaya hiikwa kusadifu dhamira za kimagharibi kama vile uonevu ambapo waafrika wanateswa na kuonewa pindi waendapo nchi za magharibi. Kwa mfano katika ukurasa wa 133, mwandishi anasema:
“Mwenzetu amepigwa risasi nyingi ajabu kwa kudhaniwa mwizi; kudhaniwa tu, unasikia? Tunajua tu ni kwa sababu ya rangi tu, unasikia rangi tu!”
Pia mtagusano kama dhamira, unajidhihirisha katika ukurasa wa 128 ambapo tunaona watu wakiufanyia uchunguzi ubongo wa Alberty Einstean ili kuweza kutambua akili alizokuwa nazo kabla ya kifo chake. Mwandishi anaonyesha dhamira hii ambayo inafungamana na dhamira za kimagharibi wa kuonyesha namna watu wenye upeo mkubwa wa akili wanavyofanyiwa katika nchi zilizo endelea. Mwandishi anasema:
“Kwanini Albert Einstein alikuwa na akili za ajabu. Tunauchunguza ubongo wake sasa!”
“Ubongo wake?”
“Ehh, tuliufukua baada ya kifo chake!”
“Huku hakuna miiko?”
“Baada ya kifo aliipoteza haki ya mwili wake. Tunachunguza kiini ili kuiendeleza jamii ya kesho.”
Kwa upande wa mandhari kama mtagusano, mwandishi anatumia madhari ya kimagharibi kwa sehemu kubwa na hivyo kutumika kama mtagusao. Mwandishi anathibitisha hili kwa kusema:
“Kwanza kuna jengo la Mefu” (ukurasa wa 130)
“Jengo la pili ni Pembetano” (ukurasa wa 131)
 Pia mwandishi ametumia lugha za kigeni katika kazi hii. Kwa mfano katika ukurasa wa 20 ametumia neno la kilatini Vitaslenye maana ya maisha. Pia ukurasa wa 38 ametumia neno la kijerumani Fyuraa ambalo kwa Kiswahili linamaanisha kiongozi. Vilevile mwandishi ametumia maneno ya kiingereza kwa kiasi kikubwa. Kwa mfano; International water(ukurasa wa 50), Reconditioned car (ukurasa wa 50), Global village (ukurasa wa 87), Global pillage (ukurasa wa 87),Darling (ukurasa wa 119), the soul  of Black folk, (ukurasa wa 126), Balance of power (ukurasa wa 142), Dollar (ukurasa wa 142), Rhythm (ukurasa wa 143), na Global villain (ukurasa wa 155).
Matumizi ya lugha, mwandishi ametumia lugha nyepesi na ya kawaida iliyojaa Methali, nahau, vitendawili, tamathali za semi na mbinu nyingine ya kisanaa ili kufikisha ujumbe kwa hadhira kwa mujibu wa Senkoro (2011) fasihi ni sanaa itowayo maudhui yake kwa kutumia lugha ya maneno ambayo hutamkwa ama kuandikwa. Kipengele hiki ni muhimu sana kwani ndicho kinachotofautisha fasihi na sanaa nyingine. Kwa kiasi kikubwa mwandishi wa riwaya hii ametumia lugha ya kawaida iliyojaa misemo, methali, tamathali za sina mbinu nyingine za kisanaa kama ifuatayo.
Misemo na nahau, katika riwaya hii misemo na nahau vimeonekana katika kurasa mbalimbali kwa lengo la kuijulisha hadhira wakati unaohusika katika kazi ya fasihi husika, misemo hiyo imesawiriwa na mwandishi kama ifuatavyo:
Usiwe yule fisi wa masimulizi (uk.54)
Kichwa cha nyoka hakistahimili kilemba (uk13)
Msahau jana kesho humkumbusha (uk125)
Kila ukombozi unahitaji shujaa (uk128)
Usipende mwanga kabla hujalijua giza (uk106)
Kuaga dunia (uk47)
Methali, hizi ni semi fupi fupi zenye kueleza kwa muhtasari fikra au mafunzo mazito yaliyotokana na uzoefu wa jamii (Mlokozi 1989). Katika riwaya hii mtunzi ametumia methali mbalimbali kamavile;
“Msahau jana kesho humkumbusha” (uk.125)
“Mgeni njoo mwenyeji apone” (uk.139)
“Haraka haraka haina Baraka” (uk.23)
“Kidole kimoja hakivunji chawa” (uk.88)
“Hasira hasara” (uk.15)
“Mwenye pupa hadiliki kula tamu” (uk.140).
“Kigumba kwa nguruwe kwa binadamu kichungu” (uk143)
“Kichwa cha nyoka hakistahimili kilemba” (uk13)
“Msahau jana kesho humkumbusha” (uk125)
“Kila ukombozi unahitaji shujaa” (uk128)          
“Usipende mwanga kabla hujalijua giza” (uk106).
Mwandishi katumia methali, misemo, vitendawili na nahau kwa lengo la kumfanya msomaji asichoke,kuonyesha ufundi wake katika lugha anayoitumia, kuweka msisitizo juu ya jambo fulani, pia matumizi ya misemo kama methali husaidia kuonya jamii juu ya jambo fulani.
Tamathali za semi ni maneno au sentensi ambazo hutumiwa na wasanii wa fasihi ili kuvitia nguvu katika maana, mtindo na hata sauti katika maandishi ama kusema. Katika riwaya hii mwandishi ametumia tamathali za semi mbalimbali kama zilivyoainishwa hapo chini.
Tashibiha, hii ni hali ya kulinganisha vitu viwili au zaidi kwa kutumia maneno kama vile; “kama”, “mithili” na “mfano wa”. (Senkoro 2011).
Tamathali hii imetumika katika riwaya ya Bina Adam! Mfano:
“Umati wenyewe umekodoa macho pima huko juu kama kuku anayemwangalia mwewe” (uk.69)
“Nilivuta tabasamu na kutoa pumzi kama kiboko kasha nikaogelea hadi ukingoni na kutoka” (uk.77)
“Lakini niliweza kuziona pia zake za miguu zilizokuwa kubwa kama masahani” (uk.63)
“Anaendelea kung’ang’ania mlingotini tu kama kima”(uk.91)
Tashihisi, hii ni tamathali ambayo vitu visivyokuwa na sifa za binadamu hupewa sifa za kutenda kama binadamu. Mfano katika riwaya hii tamathali hii imejitokeza kama ifuatavyo,
“Uwongo umechukua kiti na kuketi kijijini”(uk.75)
“Huko mbele kulikuwa na msululu mkubwa wa milima”(uk.32)
“Niliamua kuifuata ile njia pana iliyoishia kunitokomeza”(uk.144)
Mbinu nyingine ya lugha iliyojitokeza katika riwaya hii ya Bina-Adamu ni:
Tanakali sauti, haya ni maneno yaundwayo kutokana na sauti zinazofanana nayo. Mfano katika (uk.125) mwandishi ameandika:
“Kutokwa na machozi yaliyoanguka nde! Nde! Nde!”
Mdokezo, hii ni hali ya kutamka maneno bila kuyamalizia ili kuleta maana halisi. Mfano katika (uk.122)
Mwandishi ameandika:
“Hi..i.ndiyo…njia…a a ya..peke..e..e. kuhakiki..isha kuwa hukw..amizwi…pia katika” (uk.21)
Pia mwandishi ameandika:
“Nyoka…Nyoka…..”
Takiriri, hii ni tamathali ya semi ambapo sehemu ya neno hurudiwa rudiwa au neno zima. Mwandishi hutumia mbinu hii kwa ajili ya kusisitiza juu ya jambo fulani. Katika riwaya hii mwandishi ametumia takriri kuonyesha msisitizo wa mambo anayoyazungumzia katika kazi yake, takriri zilizo tiumika ni kama vile:
“Beberu …….!Beberu……!Beberu……….!Nilijiambia akilini nikiliangalia, beberu, beberu, beberu, linanuka beberu” (uk14)
“Kwanini? Kwanini? Kwanini?” (uk 22)
“Hatimaye nilianza kutapika. Nikatapika, nikatapika, nikatapika”. (uk83)
“Nyoka …….! Nyoka………!” (uk21)   
Pia riwaya hii imeshehenezwa na taswira kwa kiasi kikubwa. Madumulla J. S (2009: 153) akimnukuu Senkoro F. M. E. K,anasema,taswira ni mkusanyiko wa picha mbali mbali ziundwazo kwa maelezo ya wasanii katika kazi ya fasihi. Anaendelea kusema kuwa ni lugha inayochora picha ya vitu au mahali kwa kutumia ishara.
Hivyo, taswira ni lugha ya picha ambayo hutumiwa na mtunzi kufikisha ujumbe mzito kwa hadhira. kuna aina mbili ya taswira yaani ya wazi ambayo huwa na mkusanyiko wa picha mbali mbali zinazotoa ujumbe wa moja kwa moja bila kuficha na zisizowazi ni zile ambazo hazitoi ujumbe wa moja kwa moja ambayo humhitaji msomaji afikiri sana.
Katika riwaya ya Bina-Adamu mwandishi ametumia taswira mbali mbali katika kufikisha ujumbe, taswira hizo ni kama zifuatazo:
“Kijiji”- mataifa ya ulimwengu katika kipindi hiki hali za kijamii, kisiaa na kiuchumi zinadhibitiwa na ubepari wa mataifa yaliyoendelea (juu ya jarada)
“Paani”- madarakani (uk. 67)
“Maganda, makokwa na makaka”- kile kidogo wanacho kipata watu
“Ngazi”-dhamana ya kuingia madarakani
“Matunda”-utajiri.
“Kitambara”-bendera (uk. 68)
Taswira zingine ni mawe, beberu, mkoba na nyingine nyingi.
Umuhimu wa kutumia mbinu hiii, ni kukwepa mkono wa dora, kufikisha ujumbe kwa hadhira na kumfakarisha msomaji wa kazi ya fasihi.
Kipengele kingine cha mwelekeo chomozi wa kifani uliotumika katika riwaya hii ya Bina-Adamu ni mbinu za kibunilizi.Mbinu za kibunilizi ni mbinu mbalimbali za kiubunifu ambazo huzipa kazi za fasihi upekee. Mbinu hizi za kibunilizi ambazo zimejitokeza katika riwaya hii ni kama zifuatazo:
Taharuki kwa mujibu wa Wamitila (2006:8) ni ile hali ya matarajio ambapo tuna hamu ya kutaka kujua kitakachotokea baadaye. Anaendelea kusema kuwa ni hali ya kusisimua inayompata na kumshika msomaji kiasi cha kuwa na hamu kubwa ya kujua hali au mambo ya baadaye. Pia Senkoro (2011:70) anasema kuwa ujengaji wataharuki hutofautiana kutoka mtambaji mmoja na mwingine, hata kama kisa kinachoelezwa ni kilekile kimoja. Katika riwaya hii mwandishi amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa kuijenga kazi yake kitaharuki toka mwanzo wa riwaya hadi mwisho. Msomaji anakuwa na hamu ya kutaka kujua nini kitakachotokea katika safari ya Bina-Adamu Msafiri katika harakati za kuwatafuta Huntha watatu. Katika riwaya hii msomaji anataka kujua uvumbuzi utakaofanywa na Bina-Adamu.
Kwa mfano katika ukurasa wa1mwandishi anasema:
 “Nilipozaliwa niliwakuta watu wakiogopa kiini cha kijiji chetu na mpaka leo hii unapoisoma hadithi hii bado wanakiogopa.”
Hivyo msomaji hupata dukuduku la kutaka kufahamu juu ya nani Msimuliaji,na ni pahala gani panaposimuliwa na hivyo kuendelea kusoma kazi hiyo ili afahamu juu ya simulizi husika. Pia kazi hii inamjengea taharuki msomaji kwa kutaka kung’amua kuwa P.P ni nani ambaye amechorwa kwa kufumbwa toka mwanzo na jina lake kamili linakuja kujulikana mwishoni kuwa ni Peter Pan. Kwa mfano uk 151,
“Umesema Peter ..e..e..r?Ndiye P.P. kumbe?”
“Ndiye huyu!
“Hiyo P ya pili inamaanisha nini?”
“Jina lake kamili ni Peter P…”
“Kumbe ndio maana anatupa mawe ovyo ovyo tu!”
Hivyo, matumizi ya taharuki humsaidia sana msomaji kupata hamu ya kuendelea kusoma.Vile vile taharuki humtoa uchovu msomaji na kuinua ari mpya ya kusoma.
Kipengele kingine cha mbinu za kibunilizi ambacho kimejidhihirisha katika riwaya hii ya Bina-Adamu ni utomeleaji. Huu ni uchopekaji wa vijitanzu vingine vya fasihi ambavyo ni tofauti na utanzu unaoshughulikiwa. Riwaya ya Bina-Adamuimejengwa kwa utomeleaji ndani yake. Hili linajidhihirisha katika ukurasa wa 87 ambapo mwandishi anaonyesha wimbo ufuatao
“Shusha, shushaa…….thamani ya hela shushaaa!
Bana, banaa….ugavi wa hela banaa!
Kata, kata…..matumizi ya hela kataa!
Hurisha, hurishaa……soko la hela hurishaa!
Punguza, punguzaa……mishahara duni punguzaa!”
Vilevile wimbo umejitokeza katika ukurasa wa 149, ambao unasema:
“Oh nchi hii! Nchi yangu niliyoivumbua……
Enzi yangu, salama uongozwapo na mfalme mmoja
Chimbuko la johari za gharama
Oh, jinsi ulivyotukuka uvumbuzi wako
Kuingia katika duara hii ni kuwa huru
Suala si KUWA, SWALI NI WAPI PA KUWA!”
Pia mwandishi ametumia mbinu ya ujadi. Ujadi ni matumizi ya kauli ambazo hufungamana na jamii husika iliyokusudiwa na mwandishi. Hii inaonekana pale mwandishi anapotumia methali, vitendawili na nahau. Baadhi ya methali hizo ni:
“Haraka haraka haina Baraka” (ukurasa wa 23)
“Hasira hasara” (ukurasa wa 15)
“Msahau jana, kesho humkumbusha” (ukurasa wa 125)
“Matumaini ni chajio kizuri lakini kiamsha kinywa kibaya” (ukurasa wa 88)
Vitendawili, katika ukurasa wa 82 ambapo mwandishi anasema:
“Muda si muda nilishindwa hata kupiga hatua moja kutokana na giza lahuku ng’o na kule ng’o msituni.”
Ufumbaji ni matumizi ya kauli zenye maana fiche katika kazi za fasihi. Mwandishi ametumia mbinu ya ufumbaji kwa kiasi kikubwa. Ufumbaji umejitokeza katika uumbaji wa mandhari, katika lugha, katika maudhui na katika uumbaji wa wahusika.Katika uumbaji wa mandhari, mwandishi amejitahidi kuyaficha sana. Siyo rahisi kuyatambua kwa urahisi pasipo kufanya uchunguzi wa kutosha. Aidha ametumia mandhari ya nchi za kiafrika na yale ya kimagharibi. Kilicho bainisha hapa na kufanya madhari ya kimagharibi kujulikana ni kutumia maneno kama vile jengo la pembe tano ambalo linatufanya tubaini kuwa nchi inayozungumziwa ni Marekani ambako kuna jengo la Mefu na jengo la Pembetano, maarufu kama Pentagonijapokuwa hajaitaja nchi husika kwa uwazi kama ni nchi ipi. Mwandishi anayazungumzia majengo haya katika ukurasa wa 130 na 131. Anathibitisha hili kwa kusema:
“Kwanza kuna jengo la Mefu” (ukurasa wa 130)
“Jengo la pili ni Pembetano” (ukurasa wa 131)
Pia ufumbaji katika mandhari unaojitokeza katika ukurasa wa 133 na 134. Katika ukurasa wa 133, mwandishi anasema:
“Kumbe hata huku wanawapiga risasi watu kwa kuwadhani ni wezi? Je, kama huku msingi wao mkuu ulikuwa rangi, kwetu ulikuwa nini ambako watu wanapigwa risasi na polisi kila mara?”
Katika ukurasa huu mwandishi anaendelea kusema:
“Kila siku P.P anasisitiza hii ndiyo nchi bora katika sayari zote”!
Katika kipengele cha lugha, ufumbaji umejitokeza katika riwaya hii. Mwandishi ametumia lugha iliyojaa taswira, misemo, tamathali za semi, misemo na mbinu mbalimbali katika kipengele hiki jambo ambalo linamfanya msomaji wa riwaya hii kuwa na tafakuri ya hali wa juu ili aweze kubaini kilichokuwa kimekusudiwa na mwandishi. Kwa mfano, katika ukurasa wa 100, mwandishi anatumia lugha ya mafumbo kwa kusema:
“Nilikumbuka vituko kadhaa nilivyopitia huko nyuma kuanzia Zakongwe wazee walinieleza matatizo mengi waliyokabiliana nayo zamani walipokuwa wakipambana na mazimwi yaliyovamia nyumba miaka mingi iliyopita.”
Vilevile ufumbaji umejitokeza katika uumbaji wa wahusika. Mwandishi ametumia wahusika fiche na baadhi yao kuwapa sifa ambazo kiuhalisia hawawezi kuwa kama walivyopewa uhusika wao katika riwaya hii. Kwa mfano ameweza kumchora mhusika Hanna ambaye ana matendo ya ajabu ajabu ambapo anakuwepo mahali fulani kwa wakati fulani na kutoweka ghafla wakati mwingine. Katika ukurasa wa 32, mwandishi anasema:
“Hanna alikuwa ametoweka sasa lakini wale viumbe wa ajabu walikuwa wakiongoza njia,”
Pia amemtumia mhusika P.P ambaye hajipambanui wazi wazi na kujulikana kwa wepesi. Hata Bina-Adamu Msafiri alikuwa na shauku ya kumjua huyu mhusika hadi mwisho wa riwaya hii. Licha ya jina lake kujulikana mwishoni kama Peter Pan; bado siyo rahisi kumwelewa mhusika huyu kama alikuwa anawakilisha mtu gani katika mazingira halisi ya Magharibi.
Mbinu nyingine ya kibunilizi ni matumizi ya dayolojia. Dayolojia ni mazungumzo ya majibizano baina ya wahusika wawil au zaidi wanaozungumza kwa kupokezana.Katika riwaya ya Bina-Adamu mwandishi ametumia mbinu hii ili kuwezesha kuondoa uchovu kwa wasomaji wake.Pia kupitia mbinu hii ya kibunilizi mwandishi ameweza kujiongezea ufundi wa kiutunzi kwa mfano katika ukurasa wa 23 kuna majibizano kati ya Hanna na Bina-Adamu,
“Hapa ni wapi?”
“Umeuliza swali hilo mapema mno! Ulikotoka hukufunzwa haraka haraka haina Baraka”
“Na nani?”
“Na babu!”
“Ala, amemjuaje huyu? Au labda ni mke wangu katika sura nyingine?”
Vilevile dayolojia imejitokeza katika uk 34 mwandishi anasema:
“Wewe ndiye Bina-Adamu msafiri?”
“Ehhh…”
“Tulijua utapita hapa!”
“Mliambiwa na nani?”
“Na babu yako.”
“Babu alikufa miaka mingi iliyopita!”
“Kumbe? Ndiyo maana hata kuongea kwake kulikuwa kwa shida!”
Pia dayolojia imejitokeza katika ukurasa wa 35,47,68,70,71,na72.Tunaona  matumizi haya ya dayolojia yanaonesha kila hatua ambayo mhusika Bina-Adamu msafiri amepitia na vikwazo alivyokutana navyo.Umuhimu wa matumizi ya dayolojia katika masimulizi ni kumuwezesha msomaji kufuatilia kila kinachotokea katika riwaya.Vilevile humfanya msomaji asichoke kusoma kazi husika anayoisoma.
Usawili wa wahusika ni mbinu nyingine ya kibunilizi ambayo hutumiwa na mtunzi kwa lengo la kuwachora, kuwaelezea,kuwafafanua na kuwatambulisha kwa kuwapamajina, dhima, sifa, tabia na matendo. Katika riwaya ya Bina- Adamu mwandishi ametumia mbinu ya maelezo,ulinganuzinausambamba, kuzungumza na hadhira, namajazi kwa nia ya kuwachora na kuwafafanua wahusika wake.
Mbinu ya maelezoniileinayotumia ufundi wa mtunzi katika kuelezea wahusika wake, mbinu hii imetumiwa katika kitabu hiki cha Bina- Adamu katika ukurasa wa 7mpaka 8, unasema:
“Zamani za kale paliishiwakaziwachachesana na labdawatatu. Mmoja alikuwanimhubirialiyeishi upande wa pili unaoelekeana na machweo ya jua. Nyuma yake siku hizi imebakia kuwa bandakuubaada ya mkwewekuondokakwakulalamikachakulakimepotea na wamebakiakulavyakulavinavyotolewa kama sadaka na waumini. Ukiinamia upande wa pili kulikuwa na kichaaaliyeishi upande huo katika kibandakilichofanana na kidungu cha kuwingiandegeshambani; kipompakaleo. Wanakijijiwanasemakichaahuyoalikuwamgangakabla ya wanakijijikumbatizakichaa.Hadithi yake inasimuliwa kwenye vijiji vya mbaliwanakoamini kuwa alikufamiakamingiiliyopita. Mkaziwa tatu hakujulikana kwa jina na watu wengi kijijini. Lakini alikuwanawatotowatatuhuntha; Waliondokazamani na haijulikaniwalikozamia.”
Kutokana namaelezo ya mwandishi tunatambua sifa, tabia na matendo ya wahusika hawawatatu, mbinu hii humfanya mtunzi awe karibu na jamii yake.
Mbinu nyingine ni kuzungumziwa na wahusika wengine ambapo wahusika waliotumika na mwandishi wanatoa sifa na tabia za mhusikamwingine. Mbinu hii imejitokeza katika ukurasa wa 71 unasema:
“Mwalimualiwaeleza ni kwaninihuyo P. P anawatupia watu mawe kwa kumbwewe?
“Alisemaanapendakuchezachezatu”                   
“Kuwatia watu vivimbe vichwani?”
“Tuliambiwa ni mtundu na jeuri”
“Wa kuwagotoa watu vichwa?”
“Labdakwake huo ni mchezo!”
Pia, imejitokeza katika ukurasa wa 24, 55 na 71
Ulinganuzi naUsambamba ni mbinu bunilizi ambayo hutumika na mtunzi kwa njia ya kuwafafanisha na kuwatofautisha kati ya mhusika mmoja au zaidi na wahusika wengine. Mbinu hii imetumika katika ukurasa wa 67:
“Kila kiongozi anakaahuko juu paani, hukondikoanakochumiamatundakwaurahisi na kuwatupia watu walioko chini ambao ndiowaliomshikiangazi ya kupanda juu. Lakini kamawengine ambao wanachofanya ni kulawakashiba kwanza kasha kuyatupa makaka, makokwa na maganda huko chini yanakong’aniwa na umati mkubwa ulioko huko. Wengine wanaibana kuhamishia kwingine, labda ughaibuni”. Katika mbinu hii tunapata sifa, tabia na matendo ya wahusika kwa kuwatofautisha na wahusika wengine.
Wamitila (2006) anasema kuwa, mbinu ya majazi ni mbinu au njia sahali au nyepesi sana ya uhusika, waandishi wa kazi za kifasihi huweza kuyatumiamajina ya wahusika ambayo huakisi mandhari, wasifu, tabia,itikadi pamoja na vionjo vyao.
Hivyo, majazi ambayo mtunzi anawapa wahusika majina kulingana na tabia, sifa, dhima na matendoyao. Hii imetumika katika ukurasa wa 7 na 8.
Mhubirinakichaa ukurasa wa 7 mpaka ukurasa wa 8.
Zamani za kale paliishi wakaziwa chache sana na labda watatu. Mmoja alikuwanimhubirialiyeishi upande wa pili unaoelekeana na machweo ya jua. Nyuma yake siku hizi imebakia kuwa bandakuu baada ya mkwewekuondokakwakulalamikachakulakimepotea na wamebakiakulavyakulavinavyotolewa kama sadaka na waumini. Ukiinamia upande wa pili kulikuwa na kichaaaliyeishi upande huo katika kibandakilichofanana na kidungu cha kuwingiandegeshambani; kipompakaleo. Wanakijijiwanasemakichaahuyoalikuwamgangakabla ya wanakijijikumbatizakichaa.
Mwanasayansi ukurasa wa 53,
“Baada ya muda nilimwona yule mwanayansi na wenzake. Walikuwa wakielekea nilikokuwa nikidhamiria”.
Bina-Adamu Msafiri ni mhusika mkuu katika riwaya hii ambaye alikuwa akisafiri kutafuta ufumbuzi wa jambo kusuhusiana na kijiji chao. Hii imejidhihirisha katika ukurasa wa 34:
“Wewe ni ndiye Bina-Adamu Msafiri?”
“Ehhh…”
“Tulijua utapita hapa!”
“Mliambiwa na nani?”
“Na babu yako”
Hii pia imejitokeza katika ukurasa wa 86. Mbinu hii humsadia msomaji kupata dhamira na ujumbe kwa urahisi zaidi.
Kwa ujumla riwaya hii ya Bina-Adamu, imefanikiwa kufikisha ujumbe kwa kupitia vipengele vya fani na maudhui. Kwa mfano katika dhamira ametoa dhamira ambazo zipo katika jamii yetu ya kiafrika. Dhamira hizi ni kama vile ubaguzi wa rangi, uongozi mbaya, unyonyaji, historia na uhistoria, ukandamizwaji wa nchi za Afrika unaofanywa na nchi za Magharibi. Vipengele vya mielekeo chomozi ya kifani vilivyotumika katika riwaya ya Bina-Adamu ni muhimu sana katika kukikamilisha kipengele maudhui.

MAREJELEO
Madumulla, J.S (2009) Riwaya ya Kiswahili: Nadharia, Historian a Misingi ya Uchambuzi,Sitima Printers and Stationers Ltd, Nairobi, Kenya.
Msokile, M. (1992) Nadharia za Uhakiki wa Fasihi; TUKI, Dar es Salaam.
Senkoro, F.E.M.K. (2011) Fasihi: Mfululizo wa Lugha na Fasihi, Kitabu cha Kwanza, KAUTTU, Dar es Salaam.
TUKI (2010) Kamusi ya Kiswahili Sanifu; TUKI, Dar es Salaam.
Wamitila, K. W. (2002) Bina-Adamu; Phoenix Publishers Ltd, Nairobi.
Wamitila, K.W. (2006) Uhakiki wa Fasihi: Misingi na Vipengele Vyake, Phoenix Publishers Ltd, Nairobi.
Wamitira, K. W. (2003) Kamusi ya Fasihi;Istilahi na Nadharia, Nairobi Focus Publishers, Nairobi.

Print this item

  (MTAGUSANO) NA MBINU ZA KIFANI KATIKA RIWAYA YA MZINGILE YA E.KEZILAHABI (1991)
Posted by: MwlMaeda - 08-27-2021, 06:23 PM - Forum: Riwaya - No Replies

Riwaya ya Mzingile ni riwaya ya kifalsafa iliyojikita katika swali “nini maana ya maisha Katika kujibu swali hili mwandishi amemtumia Kakulu aliyezaliwa katika mazingira ya ajabu kwa kumchora kama neema kwa maana ya kuona kama mkombozi kwa kutatua matatizo ya njaa na magonjwa.

Hata hivyo Kakuru anapoteza maana baada ya watu kuanza kumpinga hivyo anakimbilia mlimani. Pia kwa kutumia swali nini maana ya maisha mwandishi anamlika taasisi za dini ambazo kimsingi ndio mhimili wa maadili zinaposhindwa kudhibitisha hilo kwa viongozi wa dini (mashekhe na mapadri) wanavyokiuka maadili. Kwa kutumia swali hilohilo pia mwandishi anaainisha matatizo yanayotokana na uongozi mbaya unaofanywa na viongozi wabadhilifu na wasiojali  maslahi ya wengi, japo wananchi waliwaamini kwa kuwapa fursa  hiyo kuongoza.Mwandishi amemaliza kwa kueleza kuwa jamii mpya iliyokuwa na unyanyasaji, utabaka na vitu vingine visivyofaa inawezekana pale watu wanapoamua kuungana na kufanya mambo kwa kuelewana na ndio mwanzo hasa wa amani katika jamii.

Tunayaona haya pale kichaa na mwanmke walipoungana pamoja na kujenga jamii mpya isiyokuwa na ubaguzi, unyanyasaji na utabaka. Kwa kifupi riwaya hii inadodosa maana ya maisha ambapo mwandishi anasema maisha ni kama mkufu unaochukua kipande hiki na kile unaviunganisha, kipande kimoja kikikatika unakiacha unachukua kingine kinachokufaa wewe hicho kitamfaa mwingine, siku ya kufa kila mtu atavikwa mkufu wake.
 Mwendo wa riwaya;
Hurejelea suala zima la kasi, mtiririko na mshindilio wa vitushi vya riwaya kwa kuzingatia vigezo vya msuko, maudhui, masafa ya kiwakati na kijografia. Mwendo wa riwaya hii ya “Mzingile” ni mwendo wa taratibu kutokana na kuwa na maudhui yaliyojaa utanzia mwingi,  masafa ya kijiografia  na yale ya kiwakati, yamebainishwa wazi pia kunamshindilio mkubwa wa vitushi. Maudhui ya riwaya hii ni ya kitanzia.

Kwa mfano, msimulizi amekumbwa na matatizo na migogoro mbalimbali katika harakati za safari zake za kumtafuta mzee. Msimuliaji anasema “Giza lilipoingia sikuweza kuziona nyayo tena. Kwa kuogopa kupotea njia nilikata shauri kutafuta mahali pazuri pa kulala. Nilivua shati nikafunikia uso wangu ili mchanga usiingie machoni mwangu. Niliota. Niliota mtu akinisemesha. Mtu aliyekuwa akizungumza nami alikuwa amefunikwa na hali ya mawingumawingu au labda ukungu. Sura yake sikuweza kuitambua.Alinitazama bila kusema neno kwa muda. Nilijaribu
kuinua kichwa lakini kilikuwa kizito. Nilitaka kupiga kelele lakini kinywa kilikataa kufunguka na ulimi ulikuwa mkavu” (uk 9-10) Masafa ya kijiografia yamebainishwa wazi kama vile kijijini kwa mfano “Siku ambayo mama yake aliumwa uchungu, aliitwa mkunga mashuhuri kijijini kuja kumhudumia” (uk1), msituni, kwa mfano “Yasemekana Kakulu alipojiona mzee aliwateua wazee watano, mmoja kila kijiji akaenda nao msituni” mlimani (uk
11).

Masafa ya kiwakati nayo pia yamebainishwa wazi ili kumpa msomaji nafasi ya kujua kile msimuliaji amekikusudia kwa mfano mwandishi anasema “Ilikuwa jioni kama saa kumi nilipoamka. Macho yalikuwa mazito. Katika jitihada ya kutaka kuona niliona mwanamke amesimama karibu name akinitazama” (UK 9). Masafa ya kiwakati yameonekana pia katika (uk 4, 13, 44).
Naratolojia;
Ni taaluma inayohusu suala la usimulizi katika kazi za kiuandishi. Katika taaluma hii ya usimuliaji, kuna masuala mbalimbali yanayojitokeza kama matumizi ya nafsi, suala la wakati na mwendo wa kazi husika. Katika riwaya hii ya “Mzingile” mwandishi ametumia usimulizi shahidi na usimulizi maizi. Usimulizi shahidi umejitokeza ambapo pana matumizi ya nafsi ya kwanza. Mfano, “Safari yangu ilianza asubuhi na mapema wakati ambapo fikra zilikuwa bado kuchoka. Sikujua nielekee upande gani maana hakuna aliyejua kwa hakika mahali alipoishi. Nilifuata silka zangu” (UK 7) pia usimulizi huu umeruhusu kupenyeza matumizi ya nafsi ya pili, katika ukurasa wa pili kunamatumizi ya nafsi ya pili kwa mfano,“Na ninyi mnatafuta umbea! Ondokeni hapa! ” (uk 2).
Usimulizi maizi pia umetumika pale mwandishi alipotumia nafsi ya tatu kwa mfano “Wazee walikumbuka kuwa alipenda sana ubuyu, walianza kutoa sadaka chini ya mibuyu….” (uk 4)
Mtagusano
Ni athari au mwingiliano wa vipengele mbalimbali katika kazi za fasihi, kwa kawaida hii inahusishwa na mwigo au uathiriano wa kazi moja na nyingine. Vipengele hivyo vyaweza kuwa usawiri wa wahusika, lugha, mandhari, na maudhui. Vifuatavyo ni vipengele vya mtagusano kama vilivyojitokeza katika Riwaya ya “Mzingilie”
Usawiri wa wahusika. Usawiri wa wahusika, ni kitendo cha kuwachora, kuwafafanua, kuwatambulisha na kuwajenga wahusika huku wakipewa maneno, matendo, hadhi na uwezo unaolandana na unaowiana. Mwandishi amesawiri wahusika kwa namna ifuatayo;
Mbinu ya mtunzi kumwelezea mhusika, hii ni mbinu ambayo mtunzi huitumia kumwelezea mhusika juu ya matendo yake, mienendo na tabia za mhusika. Kwa mfano, katika riwaya ya “Mzingile” mtunzi amemwelezea Kakulu kama ifuatavyo; “Kakulu alitunza vizuri migomba iliyoachwa na mama yake, alilima viazi na mahindi, akaishi kwa kujitegemea. Alizoea kuwatembelea majirani zake asubuhi na mapema akimung’unya ubuyu…..”(UK 2). Mbinu ya uzungumzaji nafsi, hii ni mbinu ambayo mhusika huzungumza na nafsi yake mwenyewe. Katika riwaya hii ya “Mzingile” mbinu hii imetumika pale Mhusika Kichaa anazungumza na nafsi yake “Ninataka kuwa kichaa!”. Kwa sauti yenye kutisha nilipiga kelele, “Ninaweza kuuwa mtu nikamla mzimamzima!” (UK
20).
Mbinu ya kuzungumza na hadhira, mbinu hii inatumika ambapo mwandishi humchora mhusika akizungumza na hadhira, hadhira huweza kumfahamu mhusika kupitia mazungumzo yake mwandishi ametumia mbinu hii ambapo mhusika Kakulu amezungumza na hadhira kwa mfano mwandishi anasema “…akawakaripia wanaume waliokuwa karibu, ondokeni hapa! Mnachuguliachungulia nini? Hampashwi kuona mwanzo wangu na njia niliyoijia!” (uk 1) pia Kakulu anazungumza na wanawake waliokuwa karibu naye “Na ninyi mnatafuta umbea! Ondokeni hapa! ” (UK 2) Mbinu ya mhusika kuwafafanua wahusika wengine, kwa mfano sehemu ya sita mwandishi amewachora baadhi ya wahusika wakiwazungumzia wahusika wenzao na matendo yao kwa mfano maongezi ya msimulizi na kijana, mfuga mijusi
“Ulimwona?”
“Nani?”
“Mzee”
“Unamjua!”
“Alipita hapa na blanketi lake akiwa amejiharishia. Amezeeka sana
sasa.Alitembea kwa kuyumbayumba kama aliye ndotoni”. (Uk 56)
Mbinu ya majazi, hii ni mbinu ya kuwapa wahusika majina kulingana na sifa zao, tabia au dhima anazotakiwa kupewa. Katika riwaya ya “Mzigile” jina la mhusika Kakulu alipewa kulingna na sifa yake ya kuzaliwa akiwa na uwezo wa kufanya matendo yanayopashwa kufanywa na watu wenye umri mkubwa. Kwa mfano
mwandishi anasimulia “Wanakijiji walimpa jina la Kakulu kwa sababu alizaliwa akiwa na ndevu tayari-Kakulu, kakubwa, kazee” (UK 1)
Mandhari Mandhari iliyotumika ni kama vile; kijijini kwa mfano, “Siku ambayo mama yake aliumwa uchungu, aliitwa mkunga mashuhuri kijijini kuja kumhudumia” (UK 1), mandhari ya msituni uk 4 “Yasemekana Kakulu alipojiona mzee aliwateua wazee watano, mmoja kila kijiji akaenda nao msituni” mlimani uk 11, majini uk, baharini uk… Matumizi ya lugha Ametumia lugha ngumu iliyojaa picha Kwa mfano, ametumia mizinga, nyuki na asali. Mzinga ni nchi, asali ni rasilimali na nyuki ni wananchi (UK 77), kundi la mijsi kubadilika kuwa ng’ombe (UK 55) ni sawa na viongozi wasiowaadilifu kujigeuza na kuonekana kama wanatenda wema kwa wananchi wao, pia ametumia mbinu ya safari ndefu yenye mahangaiko kuwakilisha hali halisi ya maisha ya binadamu na misukosuko waipatayo binadamu Ametumia semi mbalimbali kama vile methali na misemo kwa mfano ametumia methali kama vile “Asiyesikia la mkuu huvujika guu! Ulimwengu huu haukusikia la mkuu” (uk 2), ametumia pia misemo kama vile “mkubwa haibi, anachukua” msanii anasema “Wazee wakaanza kugawana kile kidogo kilichokuwepo. Msemo ukawa mkubwa haibi, anachukua” (uk2), Ametumia tamathali za semi mbalimbali kama vile sitiari, tashibiha, nk kwa mfano, ametumia tashibiha pale aliposema “Maisha ni kama mkufu” (UK 7),”Hata hivyo watu walikufa kama panya” (UK 54), Ametumia pia tashihisi pale mwandishi anasema “Nitakupeleka,”pundamilia alisema (UK 83) Maumizi ya mbinu nyingine za kisanaa kama vile; nidaa (UK 23) Matumizi ya Mbaalaga, kwa mfano mwandishi anasema “Ikafikia hatua ya binadamu kumla binadamu mwenzake” (UK 54) Matumizi ya kejeli, kwa mfano “Kawaimbieni nyimbo hizo wake zenu” (UK 53) Matumizi ya lugha changamani kwa mfano, ametumia maneno ya lugha ya kiingereza kama vile, “Beyond reasonable doubt” (UK 41), well done (UK 47), once more (UK 56)

Mianzo na miisho ya riwaya
Hii ni namna riwaya zinavyofunguliwa au kusanwa na kumalizia. Riwaya inaweza kuanza na taharuki, maswali/kiu au wakati mwingine simulizi. Riwaya ya “Mzingile” sehemu ya kwanza imeanza na simulizi juu ya maisha ya Kakulu na kuzaliwa kwake kimaajabu. Kwa mfano msanii anasema “WALIMWITA Kakulu. Sasa bado tunamwita Kakulu na wajao watamwita hivyohivyo. Ukweli wake ulizingirwa na ukungu wa kisasili. Hakuna mtu aliyewajua barabara wazazi wake. Kuwako kwake kulianza kama mzaha.yasemekana kuzaliwa kwake kulikuwa kwa ajabu”(UK 1) Riwaya hii pia imeishia na hali ya taharuki.

Mtindo katika riwaya ya Mzingile
Ameigawa kazi yake katika sehemu mbalimbali kama vile sehemu ya kwanza (UK1-UK 5), sehemu ya pili(UK6-) sehemu ya tatu sehemu ya nne sehemu ya tano sehemu ya sita  sehemu ya saba Matumizi ya nyimbo kwa mfano katika ukurasa wa 33,na 78. Ambapo kuna matumizi ya wimbo.
“Ninaimba juu ya giza liligubika ulimwengu.
Tumetembea katika msitu wa kurasa potovu
Na kutafuna kila neon na kila aina ya wino.
Tumemeza yapashwayo  kunywewa
Na kucheua yatakiwayo kumezwa.” (UK 33)
Pia ametumia muziki ili kuihaisha kazi yake kwa mfano uk 46 mwandishi anasema “Saa mbili kamili mambo yalianza. Pazia tu lilipoinuliwa tu vifijo vilianza kusikika sehemu ya nyuma. Muziki wa kuingilia uliwekwa. Msichana wa kwanza aliinigia akicheza kwa mwendo wa haraka haraka uliodhihirisha uhai wake…” UK 46 Matumizi ya dayolojia kwa mfano sehemu ya sita (uk 51) kuna mazungumzo ya msimulizi na watoto waliokuwa wanawinda
“Mnakaa peke yenu?”
“Hapana. Yupo kaka”
Kijiji chenu kikubwa? Walitazamana na sikupata jibu
“Kuna kanisa? Niliendelea”
“Kaka ametukataza tusiseme mengi kwa wageni” (UK 51) Matumizi ya barua kwa mfano (uk 64 na 65) mwandishi anasema , juu ya sehemu hii nyeusi maandishi hafifu yaliweza kuonekana. Niliposogea karibu niliweza kuyasoma: “Kwa mtakaosalia. Msifanye makosa tuliyofanya sisi. Tulifunzwa hatukufunzika. Hatukuweza kuongoza mkondo wa sayansi na uchumi, siasa iliposhika hatamu…….”(UK 64) Matumizi ya nafsi zote tatu kwa mfano Pia mwandishi amechanganya lugha ya kiswahili sanifu na maneno ya  lugha za kikabila kama vile neno Kakulu pia maneno ya lugha za kigeni kama vile kiingereza na kilatini kwa mfano, “ Beyond reasonable doubt” (UK 41),  well done (UK 47), once more (UK 56)

UBUNILIZI KATIKA RIWAYA YA MZINGILE 
Ubunilizi ni neno linalotokana na neno buni lenye maana ya kutengeneza kitu kwa mara ya kwanza, gundua, zua au tunga jambo (Kamusi ya Kiswahil Sanifu:34).Hivyo basi fasihi si kazi inayohusu mambo ya kipekee bali ni uwasilishaji wa maisha ya jamii kwa njia bunifu isiyo ya moja kwa moja. Mbinu za kibunilizi zilizotumika katika Riwaya ya “Mzingile” ni kama zifuatazo;

Ufumbaji ni utumiaji wa kauli zenye maana fiche katika kazi ya fasihi. Kauli hizo huwa na maana kinyume na kazi zinazohusika. Katika kazi za fasihi ufumbaji hutumiwa kwa malengo tofautitofauti kama vile; kukwepa mkono wa dola, kuepuka kugusa hisia za wahusika moja kwa moja na pia kuwapa wasomaji nafasi ya kuwafikirisha. Katika riwaya hii ufumbaji umejitokeza katika sehemu mbalimbali. Kwa mfano, ametumia mizinga nyuki na asali (UK 77). Mzinga ni nchi, asali ni rasilimali na nyuki ni wananchi, kundi la mijsi kubadilika kuwa ng’ombe (UK55) ni sawa na viongozi wasiowaadilifu kujigeuza na kuonekana kama wanatenda wema kwa wananchi wao, pia ametumia mbinu ya safari ndefu yenye mahangaiko kuwakilisha hali halisi ya maisha ya binadamu na misukosuko waipatayo binadamu.

Usawiri wa wahusika, ni kitendo cha kuwachora, kuwafafanua,
kuwatambulisha na kuwajenga wahusika huku wakipewa maneno, matendo, hadhi na uwezo unaolandana na unaowiana. Mwandishi amesawiri wahusika kwa namna ifuatayo; Mbinu ya mtunzi kumwelezea mhusika, hii ni mbinu ambayo mtunzi huitumia kumwelezea mhusika juu ya matendo yake, mienendo na tabia za mhusika. Kwa mfano, katika riwaya ya “Mzingile” mtunzi amemwelezea Kakulu kama ifuatavyo; “…Kakulu alitunza vizuri migomba iliyoachwa na mama yake, alilima viazi na mahindi, akaishi kwa kujitegemea. Alizoea kuwatembelea majirani zake asubuhi na mapema akimung’unya ubuyu…..”(UK 2).

Mbinu ya uzungumzaji nafsi, hii ni mbinu ambayo mhusika huzungumza na nafsi yake mwenyewe. Katika riwaya hii ya “Mzingile” mbinu hii imetumika pale Mhusika Kichaa anazungumza na nafsi yake “Ninataka kuwa kichaa!”. Kwa sauti yenye kutisha nilipiga kelele, “Ninaweza kuuwa mtu nikamla mzimamzima!” (UK
20).

Mbinu ya kuzungumza na hadhira, mbinu hii inatumika ambapo mwandishi humchora mhusika akizungumza na hadhira, hadhira huweza kumfahamu mhusika kupitia mazungumzo yake mwandishi ametumia mbinu hii ambapo mhusika Kakulu amezungumza na hadhira kwa mfano mwandishi anasema “…akawakaripia wanaume waliokuwa karibu, ondokeni hapa! Mnachuguliachungulia nini? Hampashwi kuona mwanzo wangu na njia niliyoijia!” (uk 1) pia Kakulu anazungumza na wanawake waliokuwa karibu naye “Na ninyi mnatafuta umbea! Ondokeni hapa! ” (UK 2)

Mbinu ya mhusika kuwafafanua wahusika wengine, kwa mfano sehemu ya sita mwandishi amewachora baadhi ya wahusika wakiwazungumzia wahusika wenzao na matendo yao kwa mfano maongezi ya msimulizi na kijana, mfuga mijusi
“Ulimwona?”
“Nani?”
“Mzee”
“Unanjua!”
“Alipita hapa na blanketi lake akiwa amejiharishia. Amezeeka sana
sasa.Alitembea kwa kuyumbayumba kama aliye ndotoni”. (Uk 56)
Mbinu ya majazi, hii ni mbinu ya kuwapa wahusika majina kulingana na sifa zao, tabia au dhima anazotakiwa kupewa. Katika riwaya ya “Mzigile” jina la mhusika Kakulu alipewa kulingna na sifa yake ya kuzaliwa akiwa na uwezo wa kufanya matendo yanayopashwa kufanywa na watu wenye umri mkubwa. Kwa mfano
mwandishi anasimulia “Wanakijiji walimpa jina la Kakulu kwa sababu alizaliwa akiwa na ndevu tayari-Kakulu, kakubwa, kazee” (UK 1)

Mbinu ya utanzia, ni mbinu ambayo mtunzi hutumia vipengele
mbalimbali vizuavyo huzuni, jitimai, masononeko, masikitiko na mateso kwa hadhira yake. Kipengele hiki ni kinyume na ufutuhi, katika riwaya hii ya Mzingile mwandishi ametumia utanzia kama ifuatavyo; mateso, kifungo, vifo, ugumu wa maisha, magonjwa njaa, ukame na mahangaiko kwa ujumla. Kwa mfano, mwandishi anasimulia jinsi mwanamke wa kiafrika alivyokamatwa, akafungwa jela, akauwawa na pia kunajisiwa. Msanii anasema “Walimfunga, wakampeleka chumbani kwa meneja. Baada ya kumpiga viboko walimfungua. Alianza tena kupigana nao. Walimuua akipigana. Walimnajisi huku akiwa amekufa” (Uk 50), ameongelea pia suala la ukame uliosababisha watu, mimea wanyama na wadudu kufa na kupotea kwa sababu ya ukame uliokikumba kijiji baada ya msimulizi kwenda safari ya kumtafuta mzee msanii anasema “Ukame ukaanza tena, ukaweka chachu ya dhuluma. Wao wakiuana, wanyonge wakifa njaa. Ukame ukaongeza ukakasi. Vifo vikazidi kuongezeka” (uk 51-55).
Mbinu ya ufutuhi, ni mbinu ambayo msanii hutumia ucheshi au furaha kwa hadhira yake.Hii ni kinyume na tanzia. Katika riwaya ya “Mzingile” mwandishi anaonesha ufutuhi pale anaposimulia vituko vya Kakulu aliyekuwa na tabia ya kuwaingilia mapadri, masisita, mashehe kwenye baibui na kanzu zao. Kwa mfano, msanii anasema “Alikuwa mtani wa kila mtu. Mapadri wa siku hizo, masista, wavaa baibui na mashehe walikaogopa, maana kalizoea kufunua makanzu
yao na kuingia miguuni mwao. Ilikuwa vigumu kukaondoa humo. Utawasikia wakipigapiga makanzu yao kama kwamba wanatoa vumbi, We Kakulu acha kufanya hivyo!”. Kalichowafanyia wao wenyewe walijua (UK 3) Pia wenye mabinti walimtania Kakulu awapelekee maji na kuni ili wampatie binti wa kuoa, kwa mfano masnii anasema “Kwa hiyo wenye mabinti wakawa wanakatania. Ukinitafutia kuni nitakupa binti uoe. Jioni hiyo utamwona Kakulu anapeleka mzigo wa kuni uliomzidi kimo” (uk 3) pia Kakulu kumtia mimba mwari kimzaha (uk 3)

Mbinu ya taharuki, taharuki ni matarajio ambapo tunahamu ya kutaka kujua kitakachotokea baadaye Wamitila (2003), hivyo basi, ni hali ya kuwa na dukuduku la kutaka kujua juu ya nini kitafuatia katika usimulizi wa kazi za fasihi, mtunzi huijengea hamu hadhira yake ya kutaka kujua zaidi.Mbinu hii imeoneshwa katika’’ Riwaya ya “Mzingile” pale  mwandishi amekatakata matukio kwa kurukia tukio jingine kwa mfano tukio ……….., kaanza na tukio tokeo (uk 1) na baadae tukio chanzi uk……, msanii ameanza kwa kusema “WALIMWITA Kakulu. Sasa bado tunamwita Kakulu na wajao watamwita hivyohivyo.” Pia anwani yenyewe Mzingile imejengwa kitaharuki kwani pale msomaji aonapo anwani hii atakuwa na shauku ya kuisoma ili apate kujua maana halisi ya anwani hii.

Utomeleaji, ni kuingiza baadhi ya kaida za kazi fulani
kwenye kazi nyingine. Tunatomelea ili kuipa uhai kazi ya fasihi na kuifanya hadhira ijione kuwa ni sehemu ya kazi hiyo au kazi husika. Katika riwaya hii ya Mzingile utomeleaji umejitokeza katika ukurasa wa 33,na 78. Ambapo kuna matumizi ya wimbo.
“Ninaimba juu ya giza liligubika ulimwengu.
Tumetembea katika msitu wa kurasa potovu
Na kutafuna kila neon na kila aina ya wino.
Tumemeza yapashwayo kunywewa
Na kucheua yatakiwayo kumezwa.” (UK 33)
Pia ametumia muziki ili kuihaisha kazi yake kwa mfano uk 46 mwandishi anasema “Saa mbili kamili mambo yalianza. Pazia tu lilipoinuliwa tu vifijo vilianza kusikika sehemu ya nyuma. Muziki wa kuingilia uliwekwa. Msichana wa kwanza aliinigia akicheza kwa mwendo wa haraka haraka uliodhihirisha uhai wake…”
UK 46

Mbinu ya ritifaa, ni mbinu ambayo mtunzi huwasilisha mambo kwa kuwaonesha wahusika wake wakiwasiliana na mtu aliyembali (umbali wa kijiografia au aliyefariki).mfano katika riwaya ya Mzingile
mwandishi amemuonesha.

Dayolojia, hii ni mbinu ya kutumia kauli za kiusemezano kwa lengo la kufikisha ujumbe uliokusudiwa. Mtunzi hutumia vinywa vya wahusika ili kufikisha ujumbe. Katika riwaya ya Mzingile mbinu hii imetumika kama njia ya kuonyesha ufundi wa mtunzi kuweza kusawiri wahusika na hadhi zao pia imesaidia kuwasilisha mawazo kwa hali ya uasilia kwa sababu wahusika wenyewe wamwtamka maneno kwa vinywa vyao wenyewe. Katika riwaya ya Mzingile kuna mazungumzo ya wahusika mbalimbali kwa mfano kuna mazungumzo kati ya msimulizi ma mzee (uk  14)
       “Nimetumwa kuja kukuona”
      “Mimi”
       “Ndio. Wewe”
       “Kuhusu”
  “Kifo cha mwanao. Nimekuja kukujulisha kuwa mwanao ameuawa”
Mbinu ya ujadi, ni utumiaji wa kauli za asili, kauli zinazofungamana sana na jamii inayoandikiwa.Hutumika zaidi ili mwandishi aweze kujipambanua kuwa naye ni sehemu ya jamii ile. Kauli hii hujumuisha methali, nahau, misemo na vipengele vinginevyo vya kimazungumzo, mfano katika Riwaya ya Mzingile ametumia methali kama vile “Asiyesikia la mkuu huvujika guu! Ulimwengu huu haukusikia la mkuu” (uk 2), ametumia pia misemo kama vile “mkubwa haibi, anachukua” msanii anasema “Wazee wakaanza kugawana kile kidogo kilichokuwepo. Msemo ukawa mkubwa haibi, anachukua” (uk2), pia ametumia maneno ya kijadi
kama  vile jina la Kakulu ni la kijadi likiwa na maana ya kakubwa, kazee kalikokomaa. Matumizi ya usihiri pia yandhihirisha  ujadi katika jamii, kwa mfano tukio la mijusi kugeuka kuwa ng’ombe (uk 55). Hivyo basi kupitia mbinu hii ya ujadi hadhira hujiona iko karibu sana na kazi husika waonapo baadhi ya vipengele vya usimulizi wa kijadi wavitumiavyo katika jamii zao vimetumika katika kazi husika

Mbinu ya kisengerenyuma, ni namna ya usimuliaji ambao huanza na tukio- tokeo kisha hufuatia tukiochanzi, mbinu hii mtunzi huelezea kitu na baadae asili au mwanzo wa kitu kile.Mbinu hii imeneshwa pia katika Riwaya ya “Mzingile’’ kuanzia (uk1) anazungumzia habari ya Kakulu kuitwa Kakulu na watu wa kale, waliopo wanamwita kakulu na wajao pia watamwita Kakulu. Kwa mfano mwandishi anasema “WALIMWITA Kakulu. Sasa bado tunamwita Kakulu na wajao watamwita hivyihivyo.” Halafu baadae akasimulia kisa cha Kakulu kuitwa Kakulu

Msuko wa vitushi katika riwaya ya Mzingile
hiki ni kipengele kingine kilichotumiwa na waandishi katika kuwapa wasomaji hamasa ya kuendelea kusoma kazi ya fasihi unajumuisha mambo kama vile muwala na motifu mbalimbali. Mfano, katika Riwaya ya Mzingile
Muwala
Katika riwaya ya mzingile kuna mwendelezano wa vitushi katika kila sehemu, vitushi hivyo vinajengana kiasi cha kuleta mwendelezo wa matukio katika usimulizi. Kwa mfano katika sehemu ya pili kuna vitushi viwili, kitushi cha kwanza kinahusu kifo kilichompelekea msimulizi kuanzisha safari ndefu ya kumtafuta mzee aliyeishi sehemu za mbali, msimulizi anasema “Safari yangu ilianza asubuhi na mapema wakati ambapo fikra zilikuwa bado kuchoka. Sikujua nielekee upande gani mana hakuna aliyejua kwa hakika mahali alipoishi” (uk7) pia kisa cha mzee kuishi mafichoni kimejitokeza katika sehemu hii ya pili (uk 16) kwa mfano mwandishi anasimulia “Kwa kuwa nilikuwa na tuhuma ya kusalitiwa nilijenga nyumba hii ili kujikinga na ghadhabu ya wale ambao wangependa kujilipiza kisasi wakati nimeishiwa nguvu……..Ndiyo maana niko hapa mafichoni” (uk 16) Sehemu ya saba inakamilisha safari yamsimulizi aliyekuwa anapeleka taarifa ya kifo kwa Mzee. Mtirirko wa matukio au vitishi umeleta ujumbe unaoeleweka kwa wasomaji.

Motifu
Motifu ya safari, mwandishi ametumia motifu ya safari kuanziz
sehemu ya pili mpaka sehemu ya saba. Kwa mfano uk 7 msimulizi alianza safari ndefu ya kumtafutaKakulu msanii anasema “Safari yangu ilianza asubuhi na mapema wakati ambapo fikra zilikuwa bado kuchoka. Sikujua nielekee upande gani mana hakuna aliyejua kwa hakika mahali alipoishi” (uk7)

Motifu ya ndoto, mwandishi ametumia motifu hii ya ndoto katika
(uk 9-10) ambapo mwandishi anasema “Giza lilipoingia sikuweza kuziona nyayo tena. Kwa kuogopa kupotea njia nilikata shauri kutafuta mahali pazuri pa kulala. Nilivua shati nikafunikia uso wangu ili mchanga usiingie machoni mwangu. Niliota. Niliota mtu akinisemesha. Mtu aliyekuwa akizungumza name alikuwa amefunikwa na hali ya mawingumawingu au labda ukungu. Sura yake sikuweza kuitambua.Alinitazama bila kusema neon kwa muda. Nilijaribu kuinua kichwa lakini kilikuwa kizito. Nilitaka kupiga kelele lakini kinywa kilikataa kufunguka na ulimi ulikuwa mkavu” (uk 9-10)

Motifu ya majini, msanii ametumia motifu hii katika (uk 8-11) kwa mfano msanii anasema “Nilipotoka majini nilijisugua mwili mzima hadi mapafu yalipohitaji hewa tena. Nilijitumbukiza tena majini, nikaondoa uchafu uliokuwa umekokomolewa na mchanga” (uk 8)
MAREJELEO
Kezilahabi, E (2011), Mzingile, Toleo la tatu: Dar es Salaam University Press: Dar es salaam Tuki (2004), Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Nairobi: Oxford University Press.

Wamitila, K. (2003); Kamusi ya Fasihi: Istilahi na Nadharia. Focus Publications Ltd, Nairobi

Print this item

  UTANZU WA NOVELA
Posted by: MwlMaeda - 08-27-2021, 06:16 PM - Forum: Riwaya - No Replies

Ni utanzu ulio katikati ya riwaya na hadithi fupi. Huu ni utanzu wa kinathari ambao hutambulishwa kwa kiufinyu au ukosefu wa mgogoro au mgogoro finyu na ufinyu wa kimaudhui.

Tofauti kuu kati ya novela na hadithi fupi ni kwamba hadithi fupi aghalabu hujihusisha na kitushi/ tukio moja kuu japo huwepo migogoro kadhaa.Mojawapo ya sifa bainifu za novela ni kujikita kubainisha tukio hali au mgogoro mmoja pekee. Huo mgogoro mmoja aghalabu huibua taharuki ambayo huishia mahali pa mgeuko (turningpoint). Tofauti kuu baina ya riwaya na novela ni kwamba novela huwa na msuko (ploti) mmoja ambao hauruhusu
utokaji nje sana.
Yaani mwandishi hana uhuru wa kuacha kisa kikuu anachokisimulia na kuanzisha kingine katika novela hiyo moja. Kwa upande wa wahusika, novela kwa kawaida hujifunga kwenye wahusika wachache ambapo sifa za ndani au za kisaikolojia hazielezwi.
Mifano ya Novela katika Faishi ya Kiswahili ni kama ifuatavyo:
  1.          Haki Haizami (iliyoandikwa na Ali Njama)
  2.           Kurwa na Doto (ya M.S.Farsy)
  3.           Lila na Fila (ya J.K. Kiimbila)
  4.           Fumbo la Adabu
  5.           Mbio za Maisha
  6.           Miongoni mwa Novela

Print this item