SHAIRI: NAMTAKA BABA YANGU - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi andishi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=7) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=54) +---- Thread: SHAIRI: NAMTAKA BABA YANGU (/showthread.php?tid=1024) |
SHAIRI: NAMTAKA BABA YANGU - MwlMaeda - 08-27-2021 NAMTAKA BABA YANGU Wenzangu nikiwaona, na baba zao nyumbani, Moyo unanisonona, Kama wao natamani, Natafuta kila kona, nikamtia machoni, Mama, baba yuko wapi? Namtaka baba yangu. Wenzangu hupewa pipi, akirejea nyumbani, Nilichokosa ni kipi, nimkose duniani? Baba alienda wapi, na hayumo kaburini, Mama, baba yuko wapi? Namtaka baba yangu. Yananifika madhila, kubakia ukiwani, Tazama ninapolala, mithili ya jalalani, Ninakosa hata ndala, nisitiri miguuni, Mama, baba yuko wapi? Namtaka baba yangu. Lakini Sina makosa, sema Nina kosa gani? Ikiwa alikukosa, na mie kanitendani, Mbona wanitia visa, viso vyangu duniani? Mama, baba yuko wapi? Namtaka baba yangu. Vilaka najibandika, vinisitiri mwilini, Kiatu kinanicheka, ati mie masikini, Ee mama fanya haraka, niondoke ukiwani, Mama, baba yuko wapi? namtaka baba yangu. Kaditama nimefika, baba ninamtamani, Yaniondoke mashaka, nifurahi maishani, Kuishi nae nataka, nikae mbali kwa nini? Mama,baba yuko wapi, namtaka baba yangu. Mtunzi Filieda Sanga Mama B Mabibo Dsm 0753738704 |