MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI

Welcome, Guest
You have to register before you can post on our site.

Username
  
Password
  
Search Forums

(Advanced Search)

Forum Statistics
» Members: 5,481
» Latest member: Kundlimatching
» Forum threads: 2,178
» Forum posts: 2,256

Full Statistics

Online Users
There are currently 106 online users.
» 0 Member(s) | 105 Guest(s)
Bing

Latest Threads
Buy Vilitra 60 Mg |【Get E...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-24-2023, 11:45 AM
» Replies: 0
» Views: 0
How to take Cenforce50?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-19-2023, 12:59 PM
» Replies: 0
» Views: 0
About the Vidalista 60 Mg...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-04-2023, 04:07 PM
» Replies: 0
» Views: 0
What Is Vidalista 60?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-03-2023, 10:49 AM
» Replies: 0
» Views: 0
How to take Cenforce 100 ...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
03-29-2023, 02:37 PM
» Replies: 0
» Views: 66
How is Vidalista 10 Mg us...
Forum: Watunzi wa Kiswahili
Last Post: Kieth_winsett
03-27-2023, 01:26 PM
» Replies: 0
» Views: 117
Obtain Thesis Paper Assis...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Minny02
03-24-2023, 03:01 PM
» Replies: 0
» Views: 200
SEO services for sports f...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Maria Poland
03-17-2023, 01:51 PM
» Replies: 1
» Views: 223
NUKUU ZA KISWAHILI DARASA...
Forum: Nukuu
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:31 PM
» Replies: 0
» Views: 788
NECTA K4 2022
Forum: Mitihani
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:25 PM
» Replies: 0
» Views: 403

  KEJELI KATIKA FASIHI YA KISWAHILI – TANZANIA (3)
Posted by: MwlMaeda - 10-24-2021, 12:50 PM - Forum: Fasihi kwa ujumla - No Replies

3. Kejeli na fasihi ya Kiswahili

Kamusi
ya Wales (2001: 224) inasema kuwa:
Kejeli
hutokea pale ambapo maneno yanayotumiwa yanaelekea kukinzana na maana
inayohitajika katika muktadha maalumu na inayokusudiwa na mwandishi, msemaji au
mtumiaji. (tafsiri ya mwandishi) Hapa tunamaanisha kuwa kejeli huangalia mbinu
ya ulaghai, kinyume cha mambo, udanganyifu au masimulizi yasiyo na ukweli ndani
yake katika kumzungumzia, kumkebehi au kumteta mtu fulani. Mbinu ya kejeli huonyesha
vituko na mbwembwe nyingi zinazopelekea kufurahisha, kuteta, kufunza na kuonya
kiasi kwamba si rahisi kuvitambua, kuvikubali au kuvikataa ndani ya jamii. Mara
nyingi mbinu hii huwepo mahususi kwa lengo la kuteta au kuweka hadharani yale
yaliyo kinyume na matakwa ya jamii. Aghalabu kama semi au maneno haya yatakuwa
yamekusudiwa kumsema au kumwambia mtu fulani huishia kumkejeli mtu huyo si kwa
uwazi. Short (1980: 277) anafafanua mbinu ya kejeli kwamba ni ushirikiano wa
siri kati ya mwandishi au msemaji na msomaji, msikilizaji au hadhira. (tafsiri
ya mwandishi)
Hii
inatutia hamasa pengine kuangalia matumizi ya semi katika maeneo mbalimbali ya
tanzu za fasihi. Kwa mfano, iwapo wewe ni mgeni wa lugha na ukaamua kutembelea
tanzu mbalimbali za fasihi na kuvinjari katika vipera kadhaa vya semi na
kukutana na watu wakisemezana kwa sauti:
Mke
ni nguo, Mgomba kupaliliwa!
Vizee
vyangu viwili kutwa vinatwanga.
Hapa
kunatokea utata wa aina fulani na ambapo wengi huwa wanajiuliza kuwa semi hizi
zinamaanisha nini?
Kwa
hakika ukiziangalia semi hizi, huwezi kuelewa linalosemwa hadi uzame ndani
zaidi katika kuchambua maudhui yake. Hapa semi inamaanisha kuwa ni fungu la
maneno yanayotumiwa katika jamii yakiwa na maana iliyofichika, yenye kutoa
maana fulani. Mara nyingi semi hutumika katika lugha ya uficho ya picha,
tamathali na ishara, hivyo kumfikirisha sana mtu au jamii katika kupata maana
iliyokusudiwa. Kwa upande mwingine, haya ni mafumbo yenye kubeba maudhui yenye
maana zinazofuatana na ibara mbalimbali. Usemi [i]Mke ni nguo, Mgomba kupaliliwa [/i]unaweza kunyambuliwa kuwa: mgomba na
nguo vinasimama upande wa mwanamke, vikimamanisha kuwa ili mke aweze kupendeza
ni lazima atunzwe kwa manufaa ya mwanaume. Hii ni methali yenye kutumia picha.
Usemi
wa pili [i]Vizee vyangu viwili kutwa
vinatwanga
[/i] ni kitendawili, chenye maana iliyofichika. Mwenye kujua maudhui
ya kitendawili hiki atajibu kwamba jibu lake ni [i]kope za macho[/i].
Hapa
tunaweza kusema kuwa, kama hutakuwa na mtu wa kukuelewesha maana iliyofichika
ndani ya maneno haya, utadhania kuwa watu hawa wanatukanana, wanakaripiana au
wanagombana. Hali hii ndiyo unayoweza kukutana nayo wakati unapozungumza,
unaposoma au unaposikiliza masuala yenye kejeli ndani yake.
Kejeli
katika fasihi ya aina hii ni mbinu ya kifani ambayo waandishi wanaitumia ili
kumfanya msomaji afikirie kwa dhati na kwa kina ili aweze kupata ujumbe
uliokusudiwa kwa jamii yake. Waandishi hawa wa fasihi ya Kiswahili wameitumia
mbinu hii ili kumulika, kuchunguza na kuonyesha wazi mambo yaliyokithiri katika
jamii. Mambo hayo yaliyopo kwenye jamii ni pamoja na uongozi mbaya; rushwa;
ubadhirifu, unyang’anyi, wizi wa mali ya umma, ubepari, ubwanyenye, na maovu
mengine mengi yanayofanana na hayo ambayo yanarudisha nyuma maendeleo ya jamii.
[b]3.1. Kejeli na fasihi kabla ya
uhuru
[/b]
Kabla
ya Ukoloni waandishi wa kazi za fasihi ya Kiswahili walitumia mbinu ya kejeli
katika kuwasema wavivu na wale wote waliokuwa wakienda kinyume na maadili ya
jamii. Tanzu za fasihi simulizi kama vile nyimbo, hadithi, ngonjera, methali na
misemo zilitumika katika kuikosoa jamii hiyo. Kejeli ilitumika kama mbinu ya
kusemana, kukosoana, kuonyana na hata kurekebishana katika jamii. Aidha ni
katika mbinu ya kejeli kazi ya fasihi ilitumika kufikirisha hadhira na maudhui
kwa hadhira yake yaliyomo katika jamii ili waweze kujitambua na kujikosoa bila
kutajwa.
Kwa
mfano, upo msemo wa Kiswahili usemao Anapenda mteremko au anapenda dezo
hutumika ukimaanisha kuwa mhusika anapenda vitu vya bure. Msemo huu ni kejeli
kwa watu ambao hawataki kujishughulisha na kazi ngumu au za sulubu, hivyo
hupenda vya bure bila kufanya kazi.
Halikadhalika
kuna misemo kama vile kumwita mtu ambaye hapendi kushirikiana na wenzake katika
kazi Bwana mkubwa. Huku ni kumkejeli kwamba yeye ni mkubwa hivyo hawezi
kushiriki na wenzake katika kazi. Lakini kwa upande mwingine ukiangalia hali ya
mtu huyo anayeitwa Bwana mkubwa huwezi kuona uhusiano kati ya mtu huyu na jina
alilopewa, ila kinachobainishwa hapa ni matendo ya mtu huyu.
Waandishi
wengi walitumia mbinu mbalimbali za kifani katika kufikisha ujumbe wao kwa
jamii. Kwa mfano, wakati wa Ukoloni fasihi ya Kiswahili ilitumika katika
kusawiri hali halisi ya maisha ya wakati huo. Waandishi hawa waligeuza mbinu
zao za uandishi na kutumia mbinu ya kejeli katika kuonesha jinsi jamii
ilivyokuwa ikinyanyasika, ikionewa, na ikitawaliwa kinyama, hali ambayo
ikiwakosesha amani katika maisha yao ya kila siku.
Katika
kazi ya Ruhumbika (1995) ingawa iliandikwa katika kipindi cha baada ya ukoloni,
tunamwona akitumia kejeli katika kuonesha matabaka makuu yaliyokuwepo katika
kipindi cha Ukoloni. Kwa mfano, mwandishi ametumia jina la mhusika Tumbotumbo
kuwakilisha tabaka la mabwenyenye, watawala na wenye mali nyingi. Kwa kutumia
neno Tumbotumbo, mwandishi alifanikiwa sana kuwasema wazungu kuwa walikuwa
wakilionea tabaka la chini kwa manufaa yao. Kwa lugha ya kawaida Tumbotumbo ni
mtu mwenye kupenda sana kula na asiyesumbukia suala jingine isipokuwa tumbo
lake tu. Katika kazi hii anatuonesha kuwa tabaka la Wakoloni lilikuwa
likilidhalilisha, likilitumikisha, likilinyonya na likilikandamiza tabaka la
chini yaani lile la watawaliwa. Mbinu hii imemwezesha mwandishi kufanikisha
suala zima la kifani katika kuonesha kuwa, Wakoloni walikuwa na dhima ya
kujinufaisha wenyewe (matumbo yao) na jamii zao na si kujishughulisha na maisha
ya watawaliwa au walalahoi.
Mbinu
nyingine zilizotumiwa na waandishi hawa ni kwanza, ujenzi wa mandhari ya hisia
kama inavyoonekana katika kazi hizi mbili za Kandoro (1971). Katika kazi hii
tunaona mwandishi ametumia taswira ya mafumbo mazito na kejeli ambazo haikuwa
rahisi kwa Wakoloni kuzigundua kwa urahisi. Kwa mfano, ametumia msemo Siafu
wamekazana (Kandoro 1971: 138) akiwakejeli Wakoloni ili wasifahamu kuwa
Watanzania wamekwishaamshwa na kuanza harakati za kudai uhuru.
Nyoka
amegutuka, ndani ya shimo kutuna,
Tena
amekasirika. hasira zenye kununa,
Nyoka
anababaika, shimoni kwa kujikuna.
Siafu
wamekazana, nyoka amekasirika.
Shimoni
ataondoka, hilo nataja kwa jina,
Nyoka
anajua fika, siafu wakiungana,
Nguvu
zinaongezeka, shimoni watagombana,
Siafu
wameungana, nyoka amekasirika.
Siafu
zikijishika, mshiko kushikamana,
Kwamba
zinampeleka, sultani wao bwana,
Shimoni
zinapojika, nyoka fa kufanya hana.
Siafu
wameungana, nyoka amekasirika.
Siafu
wanapofika, na nyoka wakikutana.
Nyoka
hawezi kufoka, huwa ametulizana,
Ndipo
nyoka hundoka, na wana wakilizana
Hapa
siafu kwa upande mmoja ni neno linawaunganisha wanajamii kwa pamoja ili waweze
kuungana kama siafu kumng’oa Mkoloni. Na kwa upande mwingine neno hili lina
maana ya kuunda jeshi na kuliunganisha ili liwe na nguvu ya kumshambulia
Mkoloni.
Kazi
nyingine zilizotumika katika mapambano dhidi ya ukandamizwaji wa jamii na
Wazungu kwa kuwakejeli ni kama vile misemo na methali mbalimbali. Kwa mfano,
katika kitendawili hiki [i]Wazungu wawili
wanateremka mlima
[/i] jibu likiwa ni [i]Makamasi[/i].
Kwa kuzingatia maana ya kitendawili hiki, kwa upande mmoja tunaona jinsi mzungu
alivyokuwa anakejeliwa kuwa ataondolewa kama kamasi.
 
Katika
kupambana na Wakoloni wa wakati ule, ilifanyika kazi ngumu sana, ndio sababu
waandishi wakaandika mengi katika kuwakejeli Wazungu. Hapa tunamaanisha kwamba,
wapo baadhi yetu miongoni mwa wanajamii waliokuwa wakifurahia kuwepo kwa
Wazungu hao kwa kuyaiga matendo waliyokuwa wakiyafanya. Watu hawa walikejeliwa
kupitia kazi mbalimbali zilizoandikwa na waandishi wa fasihi. Kazi ambazo
ziliwakejeli watu hawa walioacha mila na desturi zao na kufuata utamaduni wa
kigeni zilikuwa nyingi. Miongoni mwa kazi hizi ni nyimbo mbalimbali zilizoimbwa
katika harakati za kudai uhuru kutoka kwa Wakoloni.

Print this item

  KUPELEKEA PIA NI KUSABABISHA
Posted by: MwlMaeda - 10-24-2021, 12:47 PM - Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha - No Replies

BOFYA HAPA CHINI KUFUNGUA >>>>>

Mjadala huu uliendelezwa na wataalamu wengine katika jukwaa na hapa chini naweka michango yao.
Jibu la Mwl. Issaya Lupogo (Chuo Kikuu Mzumbe, Tanzania) kwa Mwl. Abdilatif Abdalla (Harmburg, Ujerumani) Kuhusu PELEKEA na SABABISHA
1.0 Usuli na Utangulizi
Kabla hujasoma andiko hili (jibu kwa Abdilatif Abdalla), yafaa kwanza usome andiko lake (Abdilatif) lenye kurasa takribani 5-6 alilolisambaza au kuliingiza “kuliposti” katika mitandao ya kijamii hususani majamvi ya WhatsApp tarehe 06/11/2019 likianzia katika jamvi la Watetezi wa Kiswahili Tanzania (WAKITA) linaloongozwa na Majid Mswahili.
Kwa ujumla hoja kuu katika makala yake ni kupingana na wanaodai kwamba neno KUPELEKEA si sahihi katika matumizi ya Kiswahili sanifu katika muktadha fulani. Yeye anajenga hoja kwamba matumizi ya neno PELEKEA katika sentensi kama “mvua hii imepelekea kuharibika kwa nyumba nyingi” yapo sahihi kabisa. Anaopingana nao (akiwamo Mwl. Issaya Lupogo na wengine) wanaona kwamba neno PELEKEA katika mfano/muktadha huo si sahihi kisanifu, badala yake neno faafu ni SABABISHA. Hoja alizozitoa kwa ufupi nilivyobahatika kuelewa ninaweza kuzigawa katika kategoria tatu (3). Kwanza, ni hoja ya kiisimujamii au/na mkabala wa kiufafanuzi wa uchambuzi wa lugha “descriptive approach of language analysis”; kwa muda mrefu jamii ya Waswahili imekuwa ikilitumia neno hilo ( PELEKEA) wakiwamo waandishi mbalimbali hususani wa Fasihi (kama ilivyobainika katika mifano ya Abdilatif katika makala yake). Hoja ya pili ni ya kiisimu/kisarufi; ametumia mifano ya maneno aliyodai kuyanyumbua kutoka neno la msingi na kisha maneno hayo kupata maana mpya kabisa; mfano, ona (kutazama) – onea* (hali ya dhuluma/unyanyasaji), shika (kamata/gusa kitu)- shikilia (kung’ang’ania jambo), paa (kupaa juu, na maana nyinginezo katika kidahizo hicho)- paliwa (kupaliwa chakula). Hoja yake ya tatu ni ya kileksikografia; ametumia Kamusi la Kiswahili Fasaha la BAKIZA kueleza kwamba neno hilo (PELEKEA) limo katika kamusi hilo na lina maana sawa na SABABISHA tu.
Kwa hivyo, kwa ujumla Abdilatif anahitimisha na anahimiza kwamba neno PELEKEA lisipigwe vita katika matumizi ya Kiswahili sanifu; huku akiruhusu mjadala na kukiri kwamba yeye bado ni mwanagenzi wa lugha hii adhimu ya Kiswahili.
Katika makala hii, ninatoa majibu “response” kwa kila hoja aliyoitoa.
2.0 Jibu la Hoja za Abdilatif Abdalla
Nitajibu hoja moja baada ya nyingine.
2.1 Hoja ya Kiisimujamii au/na Mkabala wa Kiufafanuzi wa Uchambuzi wa Lugha
Hoja hii ninaikubali pasi na shaka yoyote ile. Huu ni mkabala wa uchambuzi wa lugha unaojikita kuchunguza jinsi jamii inavyotumia lugha yake kisha wataalamu wanachambua na kuhalalisha kinachozungumzwa na wenye lugha yao (jamii). Watumiaji wa lugha wakati mwingine wamekuwa wakikengeuka kanuni na taratibu za kisarufi za lugha, lakini kama ukengeukaji huo unaonekana kushika hatamu, basi wanataalumu wanaoamini katika Mkabala wa Kiufafanuzi wa Uchambuzi wa Lugha wanalihalisha neno hilo au ruwaza hiyo. Kinyume chake, wataalamu wanaoamini katika Mkabala wa Kiuelekezi “Prescriptive Approach of Language Analysis” watazidi kushikilia na kusisitiza kufuatwa kwa kanuni za sarufi husika ya lugha. Suala hili ninalifananisha na maneno ONESHA na ONYESHA. Neno ONESHA linatumika kwa msingi wa Mkabala wa Kiuelekezi kwa sababu mantiki ya dhana husika ni kuona na si kuonya . Neno ONYESHA liko katika msingi wa Mkabala wa Kiufafanuzi; neno hilo licha ya kwamba mantiki yake ni kuonya na si kuona/kuonesha, limekuwa likitumiwa na jamii kwa muda mrefu sana. Na ndio maana matoleo ya sasa ya Kamusi za Kiswahili sanifu yameingiza maneno yote hayo: ONESHA na ONYESHA.
Kama ambavyo niliwahi kuhitimisha katika moja ya mfululizo wa makala zangu (Sehemu ya 12: Je, ni Maonyesho au Maonesho) ninazozisambaza katika akaunti zangu za mitandao ya kijamii, majamvi ya WhatsApp, na kuzichapisha pia katika gazeti la Mwananchi kwenye ukurasa wa Kiswahili Adhimu kila Jumanne; zinazohusu Makosa Yaliyozoeleka katika Matumizi ya Kiswahili Sanifu; nilihitimisha kwamba makundi mawili yanayotumia maneno maonyesho na maonesho watatofautishwa katika misingi ya weledi wa lugha tu. Zaidi bofya hapa kusoma andiko hilo https://www.facebook.com/100002618180434...9/?app=fbl
Vivyohivyo, hitimisho hili nalitoa (kwa kijibu hoja hii na si hoja nyingine ya 2 na 3) kuhusu PELEKEA na SABABISHA ambapo nayafananisha maneno hayo na ONYESHA na ONESHA mtawalia.
2.2 Jibu la Hoja ya Kisarufi
Hoja hii ni nzuri lakini kuna vitu kadhaa havikuzingatiwa wakati inachakatwa labda kwa kutomakinikia sana kamusi aliyokuwa akiitumia au kwa kutotalii vema kamusi hiyo au kwa sababu ambazo mimi sizijui. Abdilatif amejenga hoja za kushawishi neno PELEKEA ni muafaka huku akiliona ni sinonimia au kisawe cha SABABISHA kwa kueleza kwamba neno hilo limetokana na neno kuu PELEKA na baada ya kunyumbuliwa na kuwa PELEKEA, likapata maana mpya ambayo inafanana na SABABISHA. Kwa hivyo, Abdilatif amejenga hoja kwa kutumia mifano mingine anayodai inafafanana na mfano huo kwa kutumia maneno Ona – onea, shika-shikilia na paa-paliwa kama ilivyodokezwa pia katika 2.1.
Mifano hiyo ya maneno aliyoitoa haina mashina yanayooana kama alivyodhani. Neno shika na shikiilia ni maneno tofauti; hata katika kamusi maneno hayo ni vidahizo viwili tofauti kabisa. Halikadhalika, neno ona (kuona) na onea (ya dhuluma) ni vidahizo tofauti katika Kamusi. Vivyohivyo, paa (kupaa na maana nyinginezo alizobainisha katika kidahizo hicho) na palia/paliwa (kupaliwa chakula) ni vidahizo viwili tofauti kabisa katika kamusi. Tumia kamusi vema kuthibitisha hili; kama hili litahojiwa nitarudi na ushahidi kutoka katika kurasa husika za kamusi ambazo vidahizo hivyo vimeoneshwa/vimefafanuliwa. Moja ya kamusi nilizotumia ni Kamusi ya Kiswahili sanifu ya TUKI, toleo la tatu.
Kwa hivyo, hoja hii imekosa ushawishi na ushahidi kutoka vyanzo vilivyotajwa kutumika.
3.0 Jibu la Hoja ya Kileksikografia
Imebanishwa kwamba neno PELEKEA limo katika Kamusi la Kiswahili Fasaha. Ni kweli kuna tofauti nyingi tu kati ya kamusi z/ya BAKIZA na kamusi y/za BAKITA (pamoja na za TUKI na nyinginezo za Tanzania Bara kwa sababu zinaoana). Kuna mjadala mkubwa wa suala hili likiwamo hata la kuwapo kwa Mabaraza ya Kiswahili mawili ndani ya nchi moja. Nisingependa kujiingiza katika mjadala huo kwa sababu ni mzito na mpana, lakini ninachokiona kuna mvuke wa kuwapo kwa lahaja mbili za Kiswahili Sanifu; Kiswahili sanifu cha Zanzibar chini ya BAKIZA na Kiswahili sanifu cha Tanzania Bara chini ya BAKITA.
Kwa hivyo, hitimisho langu kwa hoja ni kwamba kila upande wapo sahihi; Kamusi la Kiswahili Fasaha, BAKIZA wanaoamini KUPELEKEA ni sanifu/fasaha na upande wa Bara (BAKITA, TUKI, n.k) wanaoona KUPELEKEA imengekeuka kanuni na neno sahihi ni SABABISHA
Labda kwa kuwa Mwl. Issaya Lupogo amefunzwa na kufundishwa kwa kutumia miongozo ya Kiswahili sanifu cha Tanzania Bara (BAKITA), ataendelea kuamini hasa upande wa kuliona neno PELEKEA katika muktadha unaojadiliwa si sahihi, na neno sahihi ni SABABISHA. Nafikiri hizi hoja za pande mbili zipimwe/zitathminiwe na mtaalamu wa Kiswahili/lugha ambaye si Mzanzibar wala wa kutoka Tanzania; ili tathmini yake isiwe na ubinafsi.
3.0 Hitimisho la Jumla
Lugha ni pana sana, inatumika katika miktadha mingi. Ni vema kukawepo na makubaliano ya misingi na kanuni za matumizi ya lugha (Kiswahili) katika miktadha rasmi; ambapo bila shaka Kiswahili sanifu kinatakiwa kitumike. Aidha, ninatoa raia kwa Mabaraza yetu mawili (BAKITA na BAKIZA) kuungana na kuwa kitu kimoja katika kuandaa miongozo ya Kiswahili sanifu, mathalani, kuwa na kamusi zisizotofautiana. Mfano, toafauti za kamusi ya BAKITA (Kamusi Kuu la Kiswahili) na kamusi ya BAKIZA (Kamusi la Kiswahili Fasaha) zi/yanatofautina tangu mwanzoni kabisa katika jina la kamusi. Ngeli ya neno kamusi; BAKIZA wameliweka neno “kamusi” katika ngeli ya LI – YA wakati kwa BAKITA ni ngeli ya I-ZI
Mwl. Issaya Lupogo – Chuo Kikuu Mzumbe, Morogoro – Tanzania
+255712143909
lupogoissaya1@gmail.com
Tarehe 08/12/2019
Saa 7:10 Usiku

Print this item

  KEJELI KATIKA FASIHI YA KISWAHILI – TANZANIA (5)
Posted by: MwlMaeda - 10-24-2021, 12:41 PM - Forum: Fasihi kwa ujumla - No Replies

Kwa kutumia mbinu ya majibizano kati ya mtambaji na mlevi, mwandishi ametumia [i]kilima[/i] kama kejeli kwa viongozi. Kwa
mfano, ametumia kilima cha Magharibi, mashariki, kati na Kaskazini. Dhana hii
inaonesha chuki waliyonayo wananchi kutokana na mambo yanayofanywa na viongozi.
Hii imeonekana dhahiri katika ukurasa wa arubaini na tano hadi ule wa arubaini
na sita, mwandishi anadhihirisha haya pale Mwanahego anaposema:

Asiyefanya
kazi wewe uliye juu ya kilima. Juu ya kilima kuna mashamba? (…) kama kuzalisha
mali ni kusema, kwa maneno yako tungeunda ndege. Basi niache Mwanahego niseme…
Tamthilia
hii inatuonesha jinsi hali ngumu ya uchumi inayopelekea kupanda kwa bei za
bidhaa na kwa baadhi ya mazao ya wakulima kukosa soko, hata inafikia hatua ya
wakulima kung’oa mazao yao ya biashara. Penina (1984) anaonyesha viongozi
wanavyohimiza kuzalishwa kwa mazao hayo ili waweze kufaidi wao wenyewe.
Ameonesha jinsi ambavyo wakulima wasivyofaidi vema faida itokanayo na mazao
hayo. Mwishoni tunaoneshwa jinsi wakulima wanavyoonekana kukata tamaa, katika
ukurasa wa arubaini na sita:
Tunasikia
kuna watu hawataki kulima Wanang’oa kahawa, wanang’oa chai, Taifa linategemea
mazao hayo kupatia fedha za kigeni…
Maneno
hayo yanasemwa na kiongozi, kwa kutumia mhusika Sauti. Mwandishi amemtumia
Mlevi Mwanahego katika kukejeli mambo yanayofanywa na viongozi na kuonesha wazi
jamii inakokwenda na ilikotoka.
Katika
kipindi hiki cha miaka themanini, Tanzania ilikumbwa na janga kubwa la njaa.
Hali ya maisha kwa tabaka la chini ilikuwa ya kutisha. Hali hii ya kutisha
ilitokana na tamaa ya viongozi kujilimbikizia mali na kuhujumu njia kuu za
uchumi. Maisha katika kipindi hiki yalifanana na yale ya kipindi cha Ukoloni ,
na hata pengine kuzidi ya kipindi cha Ukoloni. Katika kipindi hiki, fasihi ya
Kiswahili ilisawiri jamii husika kulingana na matukio na mabadiliko
yaliyojitokeza.
Anatumia
nafasi hii kuwakejeli viongozi waliokuwa wakijilimbikizia mali zao kwa wizi,
uporaji na unyang’anyi na huku wakiwakamata wanajamii kama wezi, mafisadi na
wahujumu wa uchumi. Ametutumia kejeli kuonesha kwamba sio wote waliokuwa wazuri
kwa wakati huo.
Mvungi
(1995) katika [i]Mashairi ya Chekacheka[/i],
ametumia kejeli katika kuonyesha yale yaliojitokeza katika kipindi hiki hadi
miaka ya tisini ambapo kulianzishwa mfumo wa vyama vingi. Mvungi ametumia jina
la kitabu [i]Chekacheka[/i] na baadhi ya
vichwa vya mashairi yake katika kukejeli hali halisi ilivyokuwa katika jamii.
Hivyo basi mbinu hii imemwezesha kwa kiasi kikubwa katika kugusa hisia za
wasomaji na kufikisha ujumbe kuhusu masuala ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Kwa mfano, katika shairi la [i]Utu Umekua Kima[/i]
ukurasa wa kumi na nane, mwandishi anafichua wazi matendo ya viongozi walio
katika tabaka la juu wanavyotumia mabavu yao katika kudhulumu na kuwanyonya
tabaka la chini.
Mvungi
amewakejeli wale viongozi wa vyama mbalimbali ambao hujifanya wenye kuwaagiza
walio chini yao kwa kuwalipa ujira mdogo huku waking’ang’ania wakidhani ndiyo
hekima. Tabaka la chini hapa linachekelewa kwa kukejeliwa kuwa hata wakisemwa
namna gani wasiache kutumika. Waendelee tu.
Wakati
mwingine, Mvungi amekuwa akionesha wazi maisha yalivyorudi nyuma kwenye kipindi
cha utumwa. Kwa mfano, katika shairi la [i]Utumwa
Uhuru
[/i] ukurasa wa ishirini na mbili, anaonesha kukosekana kwa demokrasia
baada ya uhuru kupatikana. Bado viongozi wameshikilia enzi za Ukoloni, kichwa
cha shairi hili ni kejeli juu ya uhuru na uongozi wa nchi za Kiafrika. Katika
ubeti wa tatu tunasoma haya:
Pili
ni utumwa huru, Afrika ilobaki
Matabaka
yanadhuru, raia hawana haki
Ni
maisha kwa ushuru, maisha ya shakishaki
Maisha
yenye utupu, watu roho mikononi
Mwandishi
anaonesha kukosekana kwa haki na demokrasia inayotokana na utawala wa chama
kimoja. Katika shairi hili mwandishi anakejeli siasa ya nchi ambayo chama
kimoja kinatawala. Hali hii hairuhusu demokrasia kwa wananchi kwani kila
lisemwalo huwa ni sawa tu bila maamuzi ya wengi.
Vilevile
katika shairi la [i]Gunia la Mikutano[/i]
ukurasa wa ishirini na tano, mwandishi anakejeli uongozi uliokithiri kwa
unyonyaji, ulaghai, unyanyasaji na rushwa. Viongozi wamekuwa watu wa maneno tu
na ziara ambazo huhitaji michango kutoka kwa wananchi. Ametumia neno [i]gunia[/i] kukejeli mikutano na ziara nyingi
wanazofanya viongozi huku wananchi wakiambulia patupu. Haya yanadhihirishwa
katika ubeti wa tatu:
Gunia
la mikutano, pipa la maandamano
Hotuba
kwa mashindano, kazi kubwa ni maneno
Michezo
na michuano, haya ya mshikamano
Matokeo
ni mateso, na kutojali shida.
Hali
kadhalika katika kufichua mfumo mzima wa uongozi mbaya katika jamii mwandishi
Mvungi ametumia kejeli kwa vichwa vya baadhi ya mashairi yake. Kwa mfano,
shairi la [i]Chanzo cha Huo Uozo[/i] ukurasa
wa ishirini na nne, [i]Ulanguzi Umevaa Suti[/i]
urasa wa kumi na tano; na [i]Mtoto Aso
Riziki
[/i] urasa wa ishirini na sita, n.k. Katika mashairi hayo mwandishi
anaonesha rushwa iliyokithiri katika jamii ulaghai wa kisiasa, urasimu na
matumizi mabaya ya mali ya umma. Hivyo basi mwandishi Mvungi katika diwani zake
za [i]Mashairi ya Chekacheka[/i] (1995), [i]Raha Karaha[/i] (1978), na [i]Chungu Tamu[/i] (1985) ametumia kejeli
katika kufichua uozo uliopo katika jamii. Mwandishi ametumia mbinu hii kuonesha
hali ya maisha, demokrasia, utabaka na uongozi mbaya. Hivyo basi mbinu hii
imemuwezesha kwa kiasi kikubwa kufanikiwa kwa kazi zake kifani na kimaudhui.
Pamoja
na fasihi ya Kiswahili kutumia kejeli kusawiri kwa kiasi kikubwa mfumo wa
kiuchumi na kisiasa kwa kuzingatia mabadiliko na matukio mbalimbali katika
jamii; kejeli katika jamii hutumika katika kusawiri duara la maisha ya binadamu
kwa kuwa kuna kupanda na kushuka na pia huwa na mwanzo na mwisho.
Kezilahabi
(1988) katika [i]Karibu Ndani[/i] ametumia
dhana ya [i]chai[/i] kuonesha mzunguko wa
maisha ya binadamu kwamba ni duara hivyo hatuna budi kufanya yaliyo ya
mafanikio wakati wa maisha yetu kwani mwisho wa maisha upo.
Katika
shairi la [i]Chai ya Jioni[/i] ukurasa wa
tatu, ubeti wa kwanza tunasoma:
Wakati
tunywapo chai hapa upenuni
Na
kuwatazama watoto wetu
Wakicheza
bembea kwa furaha
Tujue
kamba ya bembea yetu
Imeshalika
na imeanza kuoza
Na
bado kidogo tutaporomoka
Katika
shairi hili mwandishi amezungumzia maisha ya viongozi walioko madarakani.
Anaonesha wazi jinsi viongozi wanavyofaidi wakiwa madarakani lakini pindi
wang’atukapo hurudi katika hali ya kawaida. Hivyo anawakejeli kwa [i]chai ya jioni[/i] akiwakumbusha kuwa
wasijisahau kuwa ipo siku watayarudia maisha yaliyo sawa na ya wanajamii
wengine. Haya yanadhihirishwa katika ubeti wa mwisho wa shairi:
Lakini
kabla hatujaondoka kimyakimya
kukamilika
nusu duara iliyobakia
tuhakikishe
vyombo vyetu ni safi
Hapa
tunaona kwamba, pamoja na mwandishi kutumia kejeli katika kuonesha mfumo mzima
wa maisha na uongozi, mwandishi ametumia pia mbinu hii katika kuonesha
mabadiliko na mgogoro wa ushairi uliotokea miaka ya sabini.
Katika
shairi la [i]Karibu Ndani[/i] ukurasa wa
thelathini na nne hadi ule wa thelathini na saba, mwandishi anazidi kukejeli
mgogoro wa ushairi wa kimapokeo. Shairi hili la Karibu Ndani ni mwendelezo wa
shairi la [i]Fungueni Mlango[/i] lililo
katika diwani ya [i]Kichomi[/i]. Katika
mashairi haya yote msomaji anakaribishwa ndani ajionee ushairi wa kisasa.
Katika
sehemu ya kwanza ya shairi la [i]Karibu
Ndani
[/i] mwandishi anaukejeli ushairi wa kimapokeo kwa kuufananisha na kibanda
kikuukuu ambacho kinakaribia kuanguka, akimaanisha kuwa ushairi mapokeo hauna
nafasi wakati huu, kwani muda si mrefu utakuwa umekwishapoteza watunzi pamoja
na wasomaji wake.
Washairi
wa mapokeo, sasa wacheza lala salama
katika
mionzi hafifu, ya jua machweoni
Tunaona
jinsi mwandishi anavyowakejeli wale walioshikilia mashairi ya kimapokeo
waingie. Anawashauri katika mashairi ya kisasa yasiojali urari wa vina na
mizani bali kuzingatia zaidi fani na maudhui. Hivyo basi mwandishi anahimiza
washairi hao waende na wakati na kuacha mapokeo ushairi yaliyoigwa kutoka Ulaya
na kufuata yale ya Kiafrika. Haya yapo katika ubeti huu wa pili:
Muda
si mrefu patakuwa kiza tororo.
Kwenye
kiza cha karne pasipo vichochoro mkato
nilikuwa
na nanga yangu, nyimbo mpya natongoa
Mwisho
ukurasa wa thelathini na moja, mwandishi ameukejeli ushairi huo kwa kuulinganisha
na mbwa aliyezeeka na asiye na meno aitwaye Mavina:
Nje
kulikuwa na mwanga, nao ndege wakiimba
Kulikuwa
na njia katikati, wanyama kila upande
Walioinamisha
vichwa, kati nilipopita
Nilipouacha
msitu, nyuma nilitazama
Mbali
nilimwona Mavina, akitangatanga msituni
 
Mwandishi
anatuonyesha kupotea kwa Mavina ambapo hawezi kugundua wala kubahatisha njia ya
kurudi alikotoka. Anaukejeli ushairi wa kimapokeo kwa kuuashiria kupotea kabisa
kwa sababu hauna mashiko na umepwaya.

Print this item

  HALI NA MAENDELEO YA FASIHI YA KISWAHILI KATIKA TANZANIA
Posted by: MwlMaeda - 10-24-2021, 12:33 PM - Forum: Fasihi kwa ujumla - No Replies

Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Utangulizi Tarehe 20 na 21, Agosti 2013, kulifanyika mkutano wa kimataifa wa kukumbuka jitihada za hayati Shaaban Robert za kukuza Kiswahili. Mkutano huo uliofanyika Bukoba, uliandaliwa na Chama cha Ukuzaji Kiswahili na Ushairi Tanzania (UKUTA), wakisaidiana na Baraza la Kiswahili la Taifa – BAKITA, na wapenzi wa Kiswahili toka Taasisi ya Taaluma za Kiswahili – TATAKI. Mkutano ulihudhuriwa na
wataalamu na wapenzi wa Kiswahili toka Tanzania, Kenya na Uganda, ukilenga pia kuadhimisha miaka 50 tokea Shaaban Robert afariki dunia yaani tarehe 20 Juni 1962. Huu ulikuwa ni mkusanyiko muhimu kwa kuwa pia uliwakutanisha pamoja watoto wa magwiji wa Kiswahili, yaani mtoto pekee wa Shaaban Robert, Bw. Ikibal na mtoto wa Sheikh Amri Abeid Kaluta, yaani Sheikh Bakri Abedi Kaluta. Wakati huo huo, Chama cha Kiswahili cha Taifa, Kenya – CHAKITA kiliandaa mkutano Jijini Nairobi wa kukumbuka miaka 50 ya Kiswahili nchini Kenya. Mkutano huo pia ulifanyika tarehe 20 hadi 24 Agosti, 2013. Kwa hiyo, Jarida la HABARI kuamua kujadili kuhusu fasihi ya Kiswahili nchini Tanzania, limekuwa ni jambo jema na linaloendana na matukio yanayohusu mwamko wa Kiswahili Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla. Mwamko ambao sasa umo zaidi miongoni mwa vijana wa sekondari na wale wa vyuoni. Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili wa Vyuo Vikuu vya Afrika mashariki – CHAWAKAMA kitawakutanisha wanafunzi kuendeleza mjadala
kuhusu Kiswahili nchini Rwanda na Afrika mashairiki kwa ujumla mwishoni wa
Agosti 2013. Basi, Jarida la HABARI kweli linaleta habari na taarifa ambazo
zinakwenda na wakati na mambo yalivyo uwandani Afrika mashariki.
Katika makala hii fupi, nitajadili kwa ujumla, hali na maendeleo ya fasihi.
Sitaangalia mawazo kuwa kuna fasihi miongoni mwa Waafrika au la. Mabishano hayo
yamekwisha kuangaliwa mahali pengine hasa tangu miaka ya 1970, na kutokeza
vitabu viwili muhimu katika mjadala huo: kile cha Ruth Finnegan (1970) na
baadaye kile cha Isidore Okpewho (1992) kuhusu fasihi katika Afrika na fasihi
ya Kiafrika. Fasihi ya Kiafrika bado inaendelea kupata mengi kutoka katika
masimulizi, na utafiti mwingi hauna budi kufanyika kuhusu yale ambayo
hayajaandikwa na wala hayafahamiki miongoni mwa wale ambao hasa hupata maarifa
kutoka katika maandishi. Fasihi ya Afrika ni utanzu uliokomaa sasa na
kujipambanua miongoni mwa fasihi za ulimwengu.
Hata hivyo, makala hii itaangalia hali ya fasihi ya Kiswahili nchini Tanzania
katika miaka ya sasa. Tutaangalia kuibuka kwa tanzu simulizi kama vile ushairi
hasa miongoni mwa vijana, maendeleo katika nyimbo za akina mama vijijini,
mashairi simulizi yanayotongolewa radioni na kusikika mahali pengi katika Afrika
mashariki na kuibuka kwa sanaa za maonesho simulizi na vichekesho katika
televisheni na radio. Katika tanzu andishi, tutaangalia zaidi mashairi,
tamthilia, hadithi fupi na riwaya zinavyojadili masuala mbalimbali kuhusu
maisha ya Waswahili hasa miaka hii ya utandawazi.
Hali ya Fasihi Simulizi Fasihi simulizi ni aina ya fasihi ambayo kuwapo kwake
hutegemea sana masimulizi ya mdomo. Fasihi hii ndiyo kongwe zaidi duniani, na
ndiyo mzazi wa fasihi andishi. Jamii zote zenye maandishi zilikuwa, na bado
nyingine zinaendeleza usimulizi. Kupitia katika fasihi hii, wanajamii
husimuliana matukio, huelimishana, huonyana na kupeana taarifa za makuzi na
malezi kwa njia ya kisanaa na ubunifu bila ya kutumia maandishi. “Njia ya
kisanaa na ubunifu” ndiyo maneno ya msingi ambayo huyafanya masimulizi haya
kuwa ya kifasihi. Kwa hiyo, si kila masimulizi ni fasihi, ila tu yale yatumiayo
njia ya kisanaa na ubunifu mkubwa.
Katika miaka ya hivi karibuni utolewaji wa fasihi hii hasa nchini Tanzania
umekumbwa na mabadiliko makubwa. Mabadiliko hayo ni matokeo ya kukua kwa
teknolojia na matumizi ya vyombo vya kielektroniki. Kutoka katika hali ya
kuonana wakiwa pamoja, msimuliaji na wasimuliwaji, sasa fasihi hii imeingia
katika kuhifadhiwa kupitia katika televisheni au radio. Imeweza kuwekwa katika
kanda na katika santuri na video ili wale ambao hawakuwapo wakati wa usimuliaji
waendelee kuisikia au kuona masimulizi husika, muda mwingine.Kwa mfano, kukua huku kwa teknolojia tunaweza kukuona kama hivi: ingawa nchini
Tanzania televisheni imekuwapo tangu mwaka 1973 (Zanzibar), Tanzania bara,
televisheni imeanza mwaka 1994 kama asemavyo Martin Sturmer katika utafiti wake
(1998). Akifafanua hoja hiyo, Moore (1996) anaonesha kuwa kupingwa kwa
televisheni Tanzania bara na kuwapo kwa Radio moja (RTD) tokea miaka ya baada
ya uhuru kulikuwa ni mkakati wa serikali kujenga utamaduni wa Umoja, Udugu na
Utanzania kupitia katika lugha ya Kiswahili. RTD ilijenga na kuuendeleza kwa
makini utamaduni huu. Ndani yake, ilijenga fasihi ya Kiswahili na kuendeleza
lugha sanifu ya Kiswahili. Katikati ya miaka ya 1980, malengo makuu ya kuujenga
Utanzania yalikuwa yamefikiwa, ikiwa ni pamoja na kuwa na idadi kubwa ya watu
wanaojua kusoma na kuandika barani Afrika. Kwa hiyo mwanzoni mwa miaka ya 1990
kama tulivyosema awali, viongozi wa Tanzania waliona wakati ulikuwa umetimia wa
kuruhusu radio nyingi na vituo kadhaa vya televisheni.Leo hii nchini Tanzania kuna televisheni 8, Radio 38, na magazeti 71 kati ya
haya, yale ya kila siku yakiwa 18. Ni katika vyombo hivi vya mawasiliano ambapo
fasihi simulizi hupitia ili kuwafikia wananchi. Katika televisheni kwa mfano,
kipindi maarufu cha “mama na mwana” kilichokuwa kikirushwa na Radio Tanzania,
sasa kimebadilishwa na msimuliaji (mama) anaonekana akiwa na watoto, studioni.
Watoto wengine walioko nje ya studio wanaweza kumwuliza maswali na
wakashirikiana na watoto wenzao kuimba nyimbo au kupiga makofi. Tunaweza kuuona
mchango wa mwanamke katika makuzi ya watoto ukiendelezwa kwa njia za kisasa.
Tunaweza kuona namna usimuliwaji wa fasihi simulizi ulivyojibadilisha
kukubaliana na hali ya kisasa.
Mitaani, nyimbo simulizi katika muziki wa kizazi kipya au kama wauitavyo “bongo
fleva” (Taz. www.bongoflava.com; na Sakawa, 2012) unaendeleza sio uhamasishaji
tu, bali elimu na mawaoni na mjadala kuhusu siasa, kujilinda na magonjwa,
kujadili changamoto za kila siku na mambo yanayowagusa hasa vijana. Katika TV,
filamu za Kiswahili na michezo ya kuigiza, inapendwa sana na wananchi mitaani.
Wananchi wa kawaida na wale wa kipato cha chini wameendelea kuipata fasihi hii
kwa namna ya kipekee. Mapenzi yao kwa fasihi simulizi yamesababisha wachuuzi na
wajasiriamali kufungua vituo vya kuonesha filamu hizo kwa malipo. Vituo hivi si
vile vilivyo rasmi. Wale ambao hawana TV majumbani hukusanyika na kurundikana
katika vyumba ambavyo vina TV na kuona filamu au vichekesho hivyo kwa malipo
kidogo. Tunaweza kulinganisha “utamaduni” huu uliojengeka na ule wa wananchi wa
nchi za magharibi wa kwenda kuangalia sinema katika majumba ya sinema.
Kama vilivyo vituo hivyo vinavyopendwa sana, mashairi na nyimbo radioni ni
tanzu ambazo zimetawanyika katika jamii nyingi za Tanzania kupitia vituo vya FM
ambavyo huwamo karibu katika kila mkoa. Kwa sasa kuna mikoa 30 na wilaya 146.
Kwa hiyo kuwapo kwa radio 38 nchini Tanzania ni ishara kuwa kuna mabadiliko
makubwa ya njia hii ya upashanaji habari. Kupitia katika radio hizi, fasihi
simulizi, ingawa imebadilika kutoka katika gamba la zamani, bado inabeba dhima
ile ile: kuwafanya watu wasikie sauti na kupata ujumbe wa kisanaa na uliojaa
ubunifu mkubwa. Bado watu wengi wanaendelea kupata hadithi katika Kiswahili, na
kuimbiwa mashairi kupitia katika radio hizi.
Yasemwayo na Fasihi Simulizi Kwa ujumla, kupitia katika vyombo hivi vikubwa
yaani Radio na TV, mambo kadhaa huzungumzwa kuhusu yale yanayozigusa jamii. Kwa
mfano, kupitia katika vyombo hivi, Tanzania nzima imeshiriki katika kuelewa
mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi yaani, Albino yanayotokea hasa katika
mikoa ya Shinyanga na Mwanza. Nyimbo zimetungwa kupinga ukatili huu. Nyimbo
zimetungwa kuhamasisha watu kuelewa kinachoendelea na kupinga imani za
kishirikina. Mashairi katika mashule yamesikika yakiitetea sauti ya Albino ili
apate haki ya kuishi na haki ya elimu katika mazingira ya amani.
Jambo jingine ambalo sasa linajadiliwa kifasihi ni lile la kuhimiza watu
kuvumiliana pamoja na kuwa na imani za dini tofauti. Kuwapo kwa dini tofauti
hakukuwahi kuwa ni suala la kujadiliana nchini Tanzania. Hata hivyo, hivi
karibuni vitendo vya kupigana, kuuana na chuki vimeanza kujitokeza kuzungukia
masuala ya kidini. Kwa hiyo, mara moja jamii imeanza kujieleza kupitia katika
fasihi simulizi. Yapo mashairi kadhaa sasa ambayo yanapaza sauti kupinga
uhusiano huu mpya miongoni mwa wanajamii ambao kimsingi ni ndugu. Katika
mikutano mbalimbali, ikitokea kuna vikundi vya waimbaji, basi hutakosa kusikia
nyimbo kuhusu kuvumiliana na kupendana kwa watu wa dini tofauti. Nyimbo hizi
zinasikika si katika vituo vya FM tu, bali pia katika TV zinazokuwa
zimejitokeza kurekodi matukio. Dhamira hii ya kutokugombana kwa sababu za
kidini ni mpya katika fasihi ya Kiswahili.
Mbali ya dhamira hizi, dhamira ambayo sasa imejisimika na kuwa na mizizi katika
jamii ni ile inayojadili ugonjwa wa UKIMWI. Nyimbo, mashairi, ngonjera na
michezo ya kuigiza imeanza kulizungumzia janga hili hasa kutokea mwishoni mwa
miaka ya 1980 (Taz. Mutembei, 2001 na 2002). Kwa sasa nyimbo mbalimbali kuhusu
UKIMWI, dalili zake, madhara yake na hasa jinsi ya kuepukana nao zinaimbwa
karibu kila mkoa. Kwa hiyo, miaka ya sasa inaona kuwa fasihi simulizi
imejitanua kutoka katika dhamira za zamani kama vile kupinga ufukara na ujinga,
na kujielekeza katika mambo ya zama hizi kama ilivyoelezwa. Hata hivyo, hii
haimaanishi kuwa yale mambo ya zamani yameachwa. La hasha! Ufukara bado ni mjadala
miongoni mwa vijana hasa katika nyimbo zao za kizazi kipya. Basi mbali na
dhamira hizi, kuna suala la kisiasa hasa kuhusu vyama na utawala.Katika siasa, nyimbo za kizazi kipya zinaongelea sana suala hili. Labda kuingia
bungeni na kuwa mbunge wa kuchaguliwa, mwimbaji wa nyimbo hizi amezipa hadhi
nyimbo za bongo flava. Leo hii, vijana wanaimba na kujadili kuhusu maana na
kushiriki kwa vyama vingi katika siasa za Tanzania. Wanaimba kuhusu mabadiliko
ya Katiba na upatikanaji wa Katiba Mpya Tanzania. Suala ambalo pia sasa
linajadiliwa ni maana na muundo wa Muungano wa Tanzania. Dhamira hii haikupata
kuwapo kabla. Ilikuwa haiyumkiniki wananchi kuongelea muungano. Wakati fulani
ilichukuliwa kama kosa kubwa na mwiko. Sasa nguvu ya fasihi simulizi imevunja mwiko
huu na serikali imeruhusu mjadala kuwapo. Haya ni machache kuhusu dhima ya
fasihi simulizi katika zama hizi nchini Tanzania. Dhamira hizi pia zinaonekana
katika fasihi ya maandishi.
Yasemwayo na Fasihi andishi Kwanza, watu wengi wamekuwa na mwamko wa kuandika
kuliko ilivyokuwa miaka ya nyuma. Hii pia inatokana na kuwapo kwa uwezekano wa
kuchapishwa kazi za waandishi. Zamani uchapishaji ulikuwa ni wa mashaka.
Maendeleo katika teknolojia, hasa matumizi ya Kompyuta kwa upande mmoja; na
kushamiri kwa biashara kama matokeo ya soko huria, kumesababisha
wafanyabiashara kujiingiza katika eneo hili la utoaji, uuzaji na usambazaji wa
maandishi. Leo hii kuna wachapishaji wengi wa vitabu na magazeti.Katika magazeti (ambayo kama ilivyooneshwa, kuna zaidi ya magazeti 71) kuna
hadithi fupi na mashairi. Baadhi ya hadithi fupi huwa na mfululizo wa matoleo
ambapo kwa kila toleo la gazeti kuna mwendelezo wa hadithji ile ile. Kutoka
katika mfululizo wa aina hii, waandishi maarufu kama Eric Shigongo (Taz.
www.globalpublishers.info) wamejitokeza ili kuhamasisha watu kubadilika kutoka
katika ufukara. (Taz. www.youtube.com/watch?v=1nV4AGsqOgo). Kutokana na
kushiriki kwa watu kama hawa, vijana wananunua magazeti na kusoma, wakitaka
kujifunza namna ya kuishi maisha ya kitajiri.
Mbali na hadithi fupi, kona za mashairi zimeendelea kupewa nafasi katika
magazeti. Hadithi fupi hujadili mambo ya muda mrefu, na visa na mikasa ambayo
imekuwapo katika jamii kwa kipindi kirefu. Haya hivyo, mashairi hujadili
matukio ya hivi karibuni. Ni kama ambavyo tunaweza kuangalia habari kuhusu
matukio motomoto ambayo yanatokea wakati huo (breaking news), ndivyo
inavyotokea katika mashairi. Hii haina maana kuwa mashairi yameacha kujadili
dhamira zilizoota mizizi katika jamii. La hasha! Dhamira hizo bado hujadiliwa
na mashairi. Lakini matuko na habari moto moto huelezwa kifasihi na mashairi
zaidi kuliko hadithi fupi au riwaya.
Mbali na mashairi na hadithi fupi, riwaya (au hadithi ndefu) zimekuwa na mambo
kadhaa kifasihi. Kutoka yale ya kubuni na kuwa ya kifalsafa (kama ya Kusadikika
na Mzimu wa Watu wa Kale) leo hii kuna yale yanayogusa mambo ya vijana kama
riwaya ya Dunia Yao (Said Ahmed Mohamed Khamis, 2006) ambapo mwandishi
anajadili masuala mengi kuhusu vijana katika ulimwengu wa Waswahili wa zama hizi.Licha ya dhamira kuhusu UKIMWI, (riwaya za Kisiki Kikavu, Ua la Faraja, Hadithi
za Kiafrika: kwa wahubiri na walimu, ni mifano michache), katika riwaya, sasa
kuna dhamira mpya. Katika Makuadi wa Soko Huria (2002) Chachage anaandika
kuhusu madhara ya kujiingiza katika soko huria bila kujiandaa na kuwa na watu
wachache waliojaa ufisadi ambao unaiangamiza jamii iliyoinukia katika maelewano
ya kijamaa. Kuna mjadala biashara ya madini (mfano, riwaya ya Pesa za Mawe, ya
Oscar Ulomi, 2006). Hili ni suala ambao limeendelea kuitikisa jamii ya
Kitanzania hadi sasa. Licha ya madini, kuvumbuliwa kwa gesi na mafuta
kumetokeza sauti ya washairi katika mashairi hasa yanayotokeza sasa
magazetini.Aidha, dhamira nyingine ni kuhusu biashara haramu ya madawa ya kulevya na
madhara yake kwa jamii (Taz. Watoto wa mama Ntilie, 2002 cha E. Mbogo).
Mchambuzi anaweza kuona mabadiliko katika jamii ya Tanzania kwa vitabu hivi
vitatu: Kile cha Chachage kinachoongelea ufisadi, cha Ulomi cha biashara ya
madini na cha Mbogo kuhusu madawa ya kulevya. Hali hii ni tofauti na Fasihi ya
Tanzania iliyokumbatia Ujamaa na kusisitiza umoja na maelewano miongoni mwa
jamii. Kwa hakika, uandishi wa Karumuna Mboneko (2004) katika Pambazuko Gizani,
unaonesha mabadiliko kama hayo miongoni mwa asasi za kidini. Mabadiliko makubwa
yanatokea sasa ambapo baadhi ya watu wamefanya Kanisa kuwa aina ya biashara.
Hivyo kuna mfumuko wa makanisa mengi ya “uamsho”. Kutokana na shida za kijamii
na za kibinafsi, wanajamii wengi wana hitaji la kisaikolojia na kimaadili. Watu
wamekata tamaa ya maisha mazuri, na kuporomoka kwa maadili kumezidisha huzuni
miongoni mwa watu. Kwa hiyo, wimbi la makanisa yanayoombea watu kupata neema na
maisha mazuri limekuwa kubwa. Hata hivyo, kama asemavyo Karumuna, viongozi wa
Makanisa haya wengi wamewakatisha tamaa waumini wao, pale ambao ama
wamejihusisha katika maisha kinyume cha maadili yao, au wameshikwa na
kushitakiwa kuhusu biashara haramu waliyoiendesha “nyuma ya altare”. Mambo haya
ni dhamira mpya kabisa katika fasihi andishi.
Licha ya dhamira hizi, suala la ushirikina bado limeendelea kuwa katika dhamira
moto moto za fasihi andishi. Kwa mfano, Gabriel Ruhumbika anaandika kuhusu
ushirikina katika riwaya ya Janga Sugu la Wazalendo, 2002. Na katika hadithi
yake iliyochapishwa mtandaoni na wachapishaji wa Lulu, Lutatinisibwa Kamala
anaadika kuhusu Mauaji ya Albino (2010). Ni mauaji ambayo msingi wake ni imani
za kishirikina kuhusu kupata utajiri wa haraka.
Dhamira hii ya utajiri wa haraka kwa njia za kishirikina inakuzwa zaidi na
kuwapo kwa filamu hasa kutoka Nijeria (Nollywood) ambazo zinatafsiriwa kwa
Kiswahili na kurushwa katika TV. Kama nilivyosema awali, watu wengi hasa
vijijini huziangalia filamu hizi ambazo baada ya kutafsiriwa huwekwa katika
kanda za video na kuuzwa. Waendesha biashara ya video pembezoni mwa miji na
vijiji vyenye umeme, huwavutia sana hasa vijana kwa kuonesha filamu hizi kwa
malipo kidogo.Kuchapishwa kwa tamthilia ya Changamoto (E. Mahenge, 2010) kunaingiza dhamira
nyingine mpya inayoshughulikia haki za watu wenye ulemavu katika jamii. Suala
hili lina uhusiano mkubwa na imani za kishirikina na mauaji ya albino kwa
upande mmoja na mfumuko wa uingizwaji na utazamwaji wa filamu za Kinijeria kama
ilivyoelezwa. Masuala haya yana uhusiano na maisha ya jamii za Watanzania
kutaka utajiri usio wa kufanya kazi, ambao ni kasumba iliyomo katika maisha ya
biashara huria. Uliberali na uliberali mambo leo unaoenezwa kupitia katika
utandawazi umebadilisha maisha ya wanajamii wengi kutaka kuwa matajiri bila ya
kuhangaikia utajiri huo.
Hitimisho Fasihi ya Tanzania, kama yalivyo maisha ya wakati huu inaakisi
matokeo ya utandawazi. Iwe ni fasihi simulizi au fasihi andishi, namna zote
zinayaangalia maisha ya Watanzania kama yaliyo njia panda. Kutoka katika maisha
yaliyosisitiza watu kukaa pamoja na kupendana wakati wa Ujamaa, sasa kuna
maisha ya ubinafsi. Kutoka katika maisha ya watu wengi kuwa na ufukara wa vitu,
sasa kuna maisha yanayodanganya kuhusu uwezekano mkubwa wa watu kuwa na utajiri
wa mali kwa muda mfupi. Mambo haya, si tu yaandikwa katika kazi za kifasihi na
kusimuliwa katika mashairi na hadithi, bali pia yanaoneshwa katika filamu ndani
ya televisheni. Ni maisha ambayo yanadhihakiwa kupitia katika vichekesho ndani
ya radio na katika televisheni. Kutokea kwa vikundi vingi vya vichekesho ni
njia ya wasanii ya kupunguza hali ya ukataji tamaa iliyozikumba jamii maskini
za Kitanzania. Ni njia pia ya kuwacheka wale wanaokimbilia utajiri huku hawataki
kufanya kazi.
Fasihi ya Kiswahili katika Tanzania, na labda katika Afrika ya Mashariki
inapita katika kipindi cha mabadiliko. Suala hili pia linaakisi mabadiliko
katika ujamii na katika elimu na siasa. Kumekuwapo na hamu ya watu wengi zaidi
kutaka kusoma. Hali hii imesababisha kuwapo kwa shule nyingi za sekondari na
vyuo vingi, hata pale ambapo hakuna walimu au vifaa na miundo mbinu ya kutosha.
Kila mtu anataka elimu. Hili si suala baya, lakini linahitaji maandalizi.Fasihi inajadili mwamko huu mpya katika elimu na kaangalia maandalizi duni.
Inajadili madhara ya kutokuwa na elimu na kukimbilia katika imani za
kishirikina. Imani ambazo zinaondoa haki za wale wenye ulemavu na kuingiza woga
katika familia. Woga huu, ndio unaochukuliwa na viongozi wa makanisa mapya ili
kuwatia moyo waumini wao, kuwarudishia hali ya kupenda kuishi, huku viongozi
hao wakijitajirisha kwa pesa za sadaka na mavuno mengine. Haya yote
yanaongelewa katika fasihi ya Kiswahili ambayo imejipatia dhamira mpya kwa
jinsi jamii inavyopita katika kipindi cha mabadiliko.
Baadhi ya Marejeleo 
  • 1. Moore, D. (1996). Reaching the villages: Radio in Tanzania. Journal of the North American Shortwave Association.

  • 2. Sturmer, M. (1998). The Media History of Tanzania. Ndanda Mission Press).

  • 3. Finnegan, R. (1970). Oral Literature in Africa, Oxford: Clarendon Press

  • 4. Okpewho, I. (1992). African Oral Literature. Backgrounds, Character and Continuity, Bloomington: Indiana University Press

  • 5. Sakawa, D.K. (2012). Entertainment-Education Communication Strategy in Tanzania: The Efficacy and Efficiency of Bongo Flava TV programs in Youth behavior influence, LAP Lambert Academic Publishing, Saarbrucken, Germany

Print this item

  SHAIRI: WANAWAKE MALAIKA
Posted by: MwlMaeda - 10-23-2021, 07:46 AM - Forum: Ushairi - No Replies

WANAWAKE MALAIKA
Papara sipaparike, usije pata mashaka,
Situkane wanawake, chonde chonde ewe Kaka,
Wala usifazaike, ukaivuka mipaka,
Wanawake malaika, izingatie miiko.

Ndugu usidanganyike, kwa nchi na mamlaka,
Tena usihadaike, kwa rangi 'kababaika,
Uzuri wa mwanamke, vikorombwezo wataka,
*Wanawake malaika, izingatie miiko.*

Kujipamba apambike, ni fulusi kutumika,
Ubakhili sijivike, kisha vinono wataka,
Yataka utaabike, mahitaji kuyasaka,
Wanawake malaika, izingatie miiko.

Urembo haiba yake, yatengenezwa hakika,
Ajirembe asifike, mrembo asiye shaka,
Ni viunzi uviruke, maisha kwenda yasaka,
Wanawake malaika, izingatie miiko.*

Tama kituo nifike, wanawake malaika,
Matunzo yasikatike, kula kunywa kadhalika,
Na gubu likuondoke, mahaba kukamilika,
*Wanawake malaika, izingatie miiko.*

Khamis S.M. Mataka.

Print this item

  SHAIRI: NAKWENDA KUOA SOMALIA
Posted by: MwlMaeda - 10-23-2021, 07:42 AM - Forum: Ushairi - No Replies

NAKWENDA KUOA SOMALIA
Imenisha hamu Wala Sina gamu
Mwenzenu Sina hamu kuoa Tanzania
Wanawake Tanzania wamenishinda tabia
NAKWENDA KUOA SOMALIA ,

Wanawake Tanzania
Wamenishinda tabia
Kwanza si wazuri,
Hawanukii uturi
Asubuhi kiguu na njia
Mbagala mpaka buza

Akiamka asubuhi
Umeme umemwishia
Simu atakupigia
Madeni umlipie
Vikoba vimemkaba
Wanaume kawapanga
NAKWENDA KUOA SOMALIA,si Nyumbani Tanzania

Hawana Mahaba
Hawajafunzwa kwa Baba
Wewe atakuhadaa
Kwa Mapenzi ya dagaa
Vumbi limewajaa
Mpaka nyota ya jaha
NAKWENDA KUOA SOMALIA ,si Nyumbani Tanzania

Ndoa zipo Somalia
Siyo nyumbani Tanzania
Wanawake hawana Nia
Linawanukia jasho
Na uvundo pia
NAKWENDA KUOA SOMALIA ,si nyumbani Tanzania .

Kutana na Hadija,mery na Rukia
Kifuani watakurukia
Wakijinadi wanajua
Mapenzi wanaigiza
Mbele Kuna Giza ,kumbe yupo
Na Juma,hamadi na Swalehe
Nakwenda kuoa Somalia,si Nyumbani Tanzania .

Naoa Somalia
Wanawake wamefundwa,
Wao hawana inda,
Ujue wameundwa
Malegevu mato yao
Nyenyekevu sauti zao
nakwenda kuoa Somalia ,si Nyumbani Tanzania .

Uturi wananukia
Mapenzi wanayajua
Maungo wamejisitiri
Leo nawapa Siri
Oeni wasomali
Nakwenda kuoa Somalia ,si Nyumbani Tanzania

Kalamu naweka tini
Hemed nashika hatam
Msishike zangu salamu,
Naoa msomali,
Simu zangu nipigie ,Kama wewe msomali
Nakutajia uzishike..0655 250157
https://www.instagram.com/p/CVUxxDIq5WE/...hare_sheet

Print this item

  UKWELI na KWELI
Posted by: MwlMaeda - 10-22-2021, 07:12 PM - Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha - No Replies

UKWELI na KWELI

Kama alivyoeleza Sheikh Khamisi Mataka, kwa upande mmoja kuna tafauti baina ya maneno "ukweli" (kwamba ni nomino/ jina: Huu ni ukweli) na "kweli" (kwamba ni kielezi: Ni kweli leo ni Ijumaa?).  Lakini kwa upande mwengine, na kwa maeneo mengine kuzungumzwako Kiswahili, neno "kweli" ni kielezi na ni nomino/jina pia. Kwa mfano, tuna misemo kama vile, "Kweli ikidhihiri, uongo hujitenga"; "Msema kweli ni mpenzi wa Mngu"; na mengineyo.

Mfano mwengine twauona kwenye tafsiri ya Qur'ani, Aya ya 81 ya Sura Israa (Banuw Israiyl). Sheikh Abdullah Farsy katika Kurani Tukufu amelifasiri neno la Kiarabu alhaqq (الحق) kuwa ni "ukweli"; na Sheikh Ali Muhsin Barwaniy katika tafsiri yake ya Al-Muntakhab  amelifasiri "kweli."?

Naye mshairi Shaaban Robert katika mashairi yake amelitumia neno "kweli" kuwa ni nomino/jina.?
Nami pia nimelitumia hivyo.?

Kwa hivyo, kwa ufupi, mtu ana hiari ya kutumia "ukweli" au "kweli" kuwa ni nomino/jina, na atakuwa hakukipotoa Kiswahili.
-Abdilatif Abdalla,
London,
22.10.2021

Print this item

  SHAIRI: KALAMU YANGU
Posted by: MwlMaeda - 10-22-2021, 07:10 PM - Forum: Ushairi - No Replies

KALAMU YANGU
heko nakupa kalamu, unayenipa kunena,
Ninaposhikwa na hamu, jambo moja kulinena,
Wala sipati ugumu, madhali ninavyo vina,
Ni wewe waniauni, Asante sana kalamu.

Bila wewe singekuwa, na vile sauti sina,
Na waja ningezomewa, wabaki kunitukana,
Lione limepagawa, waja wangesemezana,
Sasa wanipa heshima, Asante sana kalamu.

Fulani bin fulani, naye leo twajuana,
Kunitia masifuni, eti ninajua sana,
Ningekwea jukwaani, niseme najua sana,
Nani angeniamini, Rafiki yangu kalamu?

Neno hili liafiki, Wala tusingejuana,
Wangesema hatutaki, maneno kurushiana,
Kalamu si mnafiki, Mimi nawe twapendana,
Mbali umenipeleka, Asante sana kalamu.

Ofisini nilipita, pengine wangeniona,
Kikumbo wakanipita, mithili wajaniona,
Wangu moyo ulipwita, Cha kufanya ndio Sina,
Libaki kugugumia, hali mpweke kalamu.

Ndipo ukaniambia, andika watakuona,
Na hapo nikaamua, kuandika kikazana,
Ingawa sijatoboa, ninawaza mbali sana,
Popote niende nawe, mwendani wangu kalamu.

Wengine huniuliza, yu wapi huyu kijana,
Ni binti ama ajuza, wanataka kuniona,
Pengine huwashangaza, hivi nivyo msichana,
Wanabaki bumbuwazi, lijue hili kalamu.

Kalamu kipenzi changu, wa ubani maridhia,
Wanipa raha mwenzangu, vile ninakutumia,
Wala hunipi machungu, kwangu huzuni kuzua,
Daima tutabakia, Mimi na wewe kalamu.

Nitapofika ajuza, hapo macho hayaoni,
Kalamu tanitangaza, na kunitia thamani,
Huko utanieleza, Ulaya na Marikani,
Tafadhali niamini, tanikumbuka kalamu.

Wengi tunao galacha, waandishi maarufu,
Tayari wametuacha, weshaenda kwa Raufu,
Maandiko kuyaacha, jambo lenye utukufu,
Mfano huyu Shabani, humkumbuki Kalamu?

Afiki Mimi na wewe, tumezidi pete chanda,
hivi wanipa kiwewe, kalamu umenishinda,
Kama mtu na mkewe, nakupenda wanipenda,
Mwisho wa kutumbuiza, nakuheshimu kalamu.

Mtunzi Filieda Sanga
Mama B
Mabibo Dsm
0753738704

Print this item

  MATANGAZO (VIDEO)
Posted by: MwlMaeda - 10-21-2021, 12:18 PM - Forum: Nukuu - No Replies

Print this item

  UHAKIKI WA MASHAIRI (VIDEO)
Posted by: MwlMaeda - 10-21-2021, 12:13 PM - Forum: Nukuu - No Replies

Print this item