KEJELI KATIKA FASIHI YA KISWAHILI – TANZANIA (5) - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi kwa ujumla (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=73) +--- Thread: KEJELI KATIKA FASIHI YA KISWAHILI – TANZANIA (5) (/showthread.php?tid=1359) |
KEJELI KATIKA FASIHI YA KISWAHILI – TANZANIA (5) - MwlMaeda - 10-24-2021 Kwa kutumia mbinu ya majibizano kati ya mtambaji na mlevi, mwandishi ametumia [i]kilima[/i] kama kejeli kwa viongozi. Kwa mfano, ametumia kilima cha Magharibi, mashariki, kati na Kaskazini. Dhana hii inaonesha chuki waliyonayo wananchi kutokana na mambo yanayofanywa na viongozi. Hii imeonekana dhahiri katika ukurasa wa arubaini na tano hadi ule wa arubaini na sita, mwandishi anadhihirisha haya pale Mwanahego anaposema: Asiyefanya
kazi wewe uliye juu ya kilima. Juu ya kilima kuna mashamba? (…) kama kuzalisha mali ni kusema, kwa maneno yako tungeunda ndege. Basi niache Mwanahego niseme… Tamthilia
hii inatuonesha jinsi hali ngumu ya uchumi inayopelekea kupanda kwa bei za bidhaa na kwa baadhi ya mazao ya wakulima kukosa soko, hata inafikia hatua ya wakulima kung’oa mazao yao ya biashara. Penina (1984) anaonyesha viongozi wanavyohimiza kuzalishwa kwa mazao hayo ili waweze kufaidi wao wenyewe. Ameonesha jinsi ambavyo wakulima wasivyofaidi vema faida itokanayo na mazao hayo. Mwishoni tunaoneshwa jinsi wakulima wanavyoonekana kukata tamaa, katika ukurasa wa arubaini na sita: Tunasikia
kuna watu hawataki kulima Wanang’oa kahawa, wanang’oa chai, Taifa linategemea mazao hayo kupatia fedha za kigeni… Maneno
hayo yanasemwa na kiongozi, kwa kutumia mhusika Sauti. Mwandishi amemtumia Mlevi Mwanahego katika kukejeli mambo yanayofanywa na viongozi na kuonesha wazi jamii inakokwenda na ilikotoka. Katika
kipindi hiki cha miaka themanini, Tanzania ilikumbwa na janga kubwa la njaa. Hali ya maisha kwa tabaka la chini ilikuwa ya kutisha. Hali hii ya kutisha ilitokana na tamaa ya viongozi kujilimbikizia mali na kuhujumu njia kuu za uchumi. Maisha katika kipindi hiki yalifanana na yale ya kipindi cha Ukoloni , na hata pengine kuzidi ya kipindi cha Ukoloni. Katika kipindi hiki, fasihi ya Kiswahili ilisawiri jamii husika kulingana na matukio na mabadiliko yaliyojitokeza. Anatumia
nafasi hii kuwakejeli viongozi waliokuwa wakijilimbikizia mali zao kwa wizi, uporaji na unyang’anyi na huku wakiwakamata wanajamii kama wezi, mafisadi na wahujumu wa uchumi. Ametutumia kejeli kuonesha kwamba sio wote waliokuwa wazuri kwa wakati huo. Mvungi
(1995) katika [i]Mashairi ya Chekacheka[/i], ametumia kejeli katika kuonyesha yale yaliojitokeza katika kipindi hiki hadi miaka ya tisini ambapo kulianzishwa mfumo wa vyama vingi. Mvungi ametumia jina la kitabu [i]Chekacheka[/i] na baadhi ya vichwa vya mashairi yake katika kukejeli hali halisi ilivyokuwa katika jamii. Hivyo basi mbinu hii imemwezesha kwa kiasi kikubwa katika kugusa hisia za wasomaji na kufikisha ujumbe kuhusu masuala ya kisiasa, kiuchumi na kijamii. Kwa mfano, katika shairi la [i]Utu Umekua Kima[/i] ukurasa wa kumi na nane, mwandishi anafichua wazi matendo ya viongozi walio katika tabaka la juu wanavyotumia mabavu yao katika kudhulumu na kuwanyonya tabaka la chini. Mvungi
amewakejeli wale viongozi wa vyama mbalimbali ambao hujifanya wenye kuwaagiza walio chini yao kwa kuwalipa ujira mdogo huku waking’ang’ania wakidhani ndiyo hekima. Tabaka la chini hapa linachekelewa kwa kukejeliwa kuwa hata wakisemwa namna gani wasiache kutumika. Waendelee tu. Wakati
mwingine, Mvungi amekuwa akionesha wazi maisha yalivyorudi nyuma kwenye kipindi cha utumwa. Kwa mfano, katika shairi la [i]Utumwa Uhuru[/i] ukurasa wa ishirini na mbili, anaonesha kukosekana kwa demokrasia baada ya uhuru kupatikana. Bado viongozi wameshikilia enzi za Ukoloni, kichwa cha shairi hili ni kejeli juu ya uhuru na uongozi wa nchi za Kiafrika. Katika ubeti wa tatu tunasoma haya: Pili
ni utumwa huru, Afrika ilobaki Matabaka
yanadhuru, raia hawana haki Ni
maisha kwa ushuru, maisha ya shakishaki Maisha
yenye utupu, watu roho mikononi Mwandishi
anaonesha kukosekana kwa haki na demokrasia inayotokana na utawala wa chama kimoja. Katika shairi hili mwandishi anakejeli siasa ya nchi ambayo chama kimoja kinatawala. Hali hii hairuhusu demokrasia kwa wananchi kwani kila lisemwalo huwa ni sawa tu bila maamuzi ya wengi. Vilevile
katika shairi la [i]Gunia la Mikutano[/i] ukurasa wa ishirini na tano, mwandishi anakejeli uongozi uliokithiri kwa unyonyaji, ulaghai, unyanyasaji na rushwa. Viongozi wamekuwa watu wa maneno tu na ziara ambazo huhitaji michango kutoka kwa wananchi. Ametumia neno [i]gunia[/i] kukejeli mikutano na ziara nyingi wanazofanya viongozi huku wananchi wakiambulia patupu. Haya yanadhihirishwa katika ubeti wa tatu: Gunia
la mikutano, pipa la maandamano Hotuba
kwa mashindano, kazi kubwa ni maneno Michezo
na michuano, haya ya mshikamano Matokeo
ni mateso, na kutojali shida. Hali
kadhalika katika kufichua mfumo mzima wa uongozi mbaya katika jamii mwandishi Mvungi ametumia kejeli kwa vichwa vya baadhi ya mashairi yake. Kwa mfano, shairi la [i]Chanzo cha Huo Uozo[/i] ukurasa wa ishirini na nne, [i]Ulanguzi Umevaa Suti[/i] urasa wa kumi na tano; na [i]Mtoto Aso Riziki[/i] urasa wa ishirini na sita, n.k. Katika mashairi hayo mwandishi anaonesha rushwa iliyokithiri katika jamii ulaghai wa kisiasa, urasimu na matumizi mabaya ya mali ya umma. Hivyo basi mwandishi Mvungi katika diwani zake za [i]Mashairi ya Chekacheka[/i] (1995), [i]Raha Karaha[/i] (1978), na [i]Chungu Tamu[/i] (1985) ametumia kejeli katika kufichua uozo uliopo katika jamii. Mwandishi ametumia mbinu hii kuonesha hali ya maisha, demokrasia, utabaka na uongozi mbaya. Hivyo basi mbinu hii imemuwezesha kwa kiasi kikubwa kufanikiwa kwa kazi zake kifani na kimaudhui. Pamoja
na fasihi ya Kiswahili kutumia kejeli kusawiri kwa kiasi kikubwa mfumo wa kiuchumi na kisiasa kwa kuzingatia mabadiliko na matukio mbalimbali katika jamii; kejeli katika jamii hutumika katika kusawiri duara la maisha ya binadamu kwa kuwa kuna kupanda na kushuka na pia huwa na mwanzo na mwisho. Kezilahabi
(1988) katika [i]Karibu Ndani[/i] ametumia dhana ya [i]chai[/i] kuonesha mzunguko wa maisha ya binadamu kwamba ni duara hivyo hatuna budi kufanya yaliyo ya mafanikio wakati wa maisha yetu kwani mwisho wa maisha upo. Katika
shairi la [i]Chai ya Jioni[/i] ukurasa wa tatu, ubeti wa kwanza tunasoma: Wakati
tunywapo chai hapa upenuni Na
kuwatazama watoto wetu Wakicheza
bembea kwa furaha Tujue
kamba ya bembea yetu Imeshalika
na imeanza kuoza Na
bado kidogo tutaporomoka Katika
shairi hili mwandishi amezungumzia maisha ya viongozi walioko madarakani. Anaonesha wazi jinsi viongozi wanavyofaidi wakiwa madarakani lakini pindi wang’atukapo hurudi katika hali ya kawaida. Hivyo anawakejeli kwa [i]chai ya jioni[/i] akiwakumbusha kuwa wasijisahau kuwa ipo siku watayarudia maisha yaliyo sawa na ya wanajamii wengine. Haya yanadhihirishwa katika ubeti wa mwisho wa shairi: Lakini
kabla hatujaondoka kimyakimya kukamilika
nusu duara iliyobakia tuhakikishe
vyombo vyetu ni safi Hapa
tunaona kwamba, pamoja na mwandishi kutumia kejeli katika kuonesha mfumo mzima wa maisha na uongozi, mwandishi ametumia pia mbinu hii katika kuonesha mabadiliko na mgogoro wa ushairi uliotokea miaka ya sabini. Katika
shairi la [i]Karibu Ndani[/i] ukurasa wa thelathini na nne hadi ule wa thelathini na saba, mwandishi anazidi kukejeli mgogoro wa ushairi wa kimapokeo. Shairi hili la Karibu Ndani ni mwendelezo wa shairi la [i]Fungueni Mlango[/i] lililo katika diwani ya [i]Kichomi[/i]. Katika mashairi haya yote msomaji anakaribishwa ndani ajionee ushairi wa kisasa. Katika
sehemu ya kwanza ya shairi la [i]Karibu Ndani[/i] mwandishi anaukejeli ushairi wa kimapokeo kwa kuufananisha na kibanda kikuukuu ambacho kinakaribia kuanguka, akimaanisha kuwa ushairi mapokeo hauna nafasi wakati huu, kwani muda si mrefu utakuwa umekwishapoteza watunzi pamoja na wasomaji wake. Washairi
wa mapokeo, sasa wacheza lala salama katika
mionzi hafifu, ya jua machweoni Tunaona
jinsi mwandishi anavyowakejeli wale walioshikilia mashairi ya kimapokeo waingie. Anawashauri katika mashairi ya kisasa yasiojali urari wa vina na mizani bali kuzingatia zaidi fani na maudhui. Hivyo basi mwandishi anahimiza washairi hao waende na wakati na kuacha mapokeo ushairi yaliyoigwa kutoka Ulaya na kufuata yale ya Kiafrika. Haya yapo katika ubeti huu wa pili: Muda
si mrefu patakuwa kiza tororo. Kwenye
kiza cha karne pasipo vichochoro mkato nilikuwa
na nanga yangu, nyimbo mpya natongoa Mwisho
ukurasa wa thelathini na moja, mwandishi ameukejeli ushairi huo kwa kuulinganisha na mbwa aliyezeeka na asiye na meno aitwaye Mavina: Nje
kulikuwa na mwanga, nao ndege wakiimba Kulikuwa
na njia katikati, wanyama kila upande Walioinamisha
vichwa, kati nilipopita Nilipouacha
msitu, nyuma nilitazama Mbali
nilimwona Mavina, akitangatanga msituni Mwandishi anatuonyesha kupotea kwa Mavina ambapo hawezi kugundua wala kubahatisha njia ya kurudi alikotoka. Anaukejeli ushairi wa kimapokeo kwa kuuashiria kupotea kabisa kwa sababu hauna mashiko na umepwaya. |