UKWELI na KWELI - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=9) +--- Thread: UKWELI na KWELI (/showthread.php?tid=1354) |
UKWELI na KWELI - MwlMaeda - 10-22-2021 UKWELI na KWELI Kama alivyoeleza Sheikh Khamisi Mataka, kwa upande mmoja kuna tafauti baina ya maneno "ukweli" (kwamba ni nomino/ jina: Huu ni ukweli) na "kweli" (kwamba ni kielezi: Ni kweli leo ni Ijumaa?). Lakini kwa upande mwengine, na kwa maeneo mengine kuzungumzwako Kiswahili, neno "kweli" ni kielezi na ni nomino/jina pia. Kwa mfano, tuna misemo kama vile, "Kweli ikidhihiri, uongo hujitenga"; "Msema kweli ni mpenzi wa Mngu"; na mengineyo. Mfano mwengine twauona kwenye tafsiri ya Qur'ani, Aya ya 81 ya Sura Israa (Banuw Israiyl). Sheikh Abdullah Farsy katika Kurani Tukufu amelifasiri neno la Kiarabu alhaqq (الحق) kuwa ni "ukweli"; na Sheikh Ali Muhsin Barwaniy katika tafsiri yake ya Al-Muntakhab amelifasiri "kweli."? Naye mshairi Shaaban Robert katika mashairi yake amelitumia neno "kweli" kuwa ni nomino/jina.? Nami pia nimelitumia hivyo.? Kwa hivyo, kwa ufupi, mtu ana hiari ya kutumia "ukweli" au "kweli" kuwa ni nomino/jina, na atakuwa hakukipotoa Kiswahili. -Abdilatif Abdalla, London, 22.10.2021 |