MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI

Welcome, Guest
You have to register before you can post on our site.

Username
  
Password
  
Search Forums

(Advanced Search)

Forum Statistics
» Members: 5,481
» Latest member: Kundlimatching
» Forum threads: 2,178
» Forum posts: 2,256

Full Statistics

Online Users
There are currently 82 online users.
» 0 Member(s) | 81 Guest(s)
Bing

Latest Threads
Buy Vilitra 60 Mg |【Get E...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-24-2023, 11:45 AM
» Replies: 0
» Views: 0
How to take Cenforce50?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-19-2023, 12:59 PM
» Replies: 0
» Views: 0
About the Vidalista 60 Mg...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-04-2023, 04:07 PM
» Replies: 0
» Views: 0
What Is Vidalista 60?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-03-2023, 10:49 AM
» Replies: 0
» Views: 0
How to take Cenforce 100 ...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
03-29-2023, 02:37 PM
» Replies: 0
» Views: 66
How is Vidalista 10 Mg us...
Forum: Watunzi wa Kiswahili
Last Post: Kieth_winsett
03-27-2023, 01:26 PM
» Replies: 0
» Views: 117
Obtain Thesis Paper Assis...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Minny02
03-24-2023, 03:01 PM
» Replies: 0
» Views: 200
SEO services for sports f...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Maria Poland
03-17-2023, 01:51 PM
» Replies: 1
» Views: 223
NUKUU ZA KISWAHILI DARASA...
Forum: Nukuu
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:31 PM
» Replies: 0
» Views: 788
NECTA K4 2022
Forum: Mitihani
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:25 PM
» Replies: 0
» Views: 403

  TANZU ZA FASIHI ANDISHI YA KISWAHILI (WATAALAMU MBALIMBALI)
Posted by: MwlMaeda - 10-25-2021, 02:51 PM - Forum: Fasihi kwa ujumla - No Replies

Kama ilivyo kwenye tanzu za fasihi simulizi, haijawa rahisi kueleza tanzu za fasihi andishi kutokana na mikinzano inayoonekana
miongoni mwa wanazuoni.Wataalamu wengi wa awali wa fasihi ya Kiswahili walibainisha kuwa fasihi andishi ina tanzu tatu ambazo ni Ushairi, riwaya na tamthiliya.
MBUNDA MSOKILE 1992: Uhakiki wa fasihi
Yeye anasema tanzu za fasihi andishi zipo tatu; nazo
ni:

Riwaya

Ushairi

Tamthiliya
NKWERA 1976:
Sarufi na Fasihi, Sekondari na vyuo
Anafanana na
Msokile, naye anatambua tanzu tatu ambazo ni:

Riwaya

Ushairi na

Tamthiliya
MULOKOZI 1996
Anaanza kuhoji
uhakiki wa tanzu tatu. Yeye anasema tanzu za fasihi andishi si tatu ni nne;
nazo ni:

Ushairi

Riwaya

Tamthiliya na

Kisa
M’NGARUTHI
2008
Yeye
anakubaliana na Mulokozi kuwa tanzu zipo nne lakini hakubaliana katika majina. Yeye
anatambua:

Ushairi

Hadithi fupi

Riwaya na

Tamthiliya
Kinachoitwa Kisa
na Mulokozi M’ngaruthi anakiita Hadithi
fupi. Wataalamu wa Kenya wanakubaliana na M’ngaruthi, hivyo mfumo wa elimu
ya Kenya unatambua tanzu alizoziainisha M’ngaruthi.
Hata hivyo,
wataalamu wengine wameendelea kuhoji juu ya tanzu nne, kwa sababu novela
nazo zinaingia wapi?
Mfano:
WAMITILA, 2008
Yeye anataja:

Riwaya

Tamthiliya

Novela

Insha

Ushairi

Hotuba

Sira

Masimulizi ya wasafiri
Japokuwa Wamitila
hakiri moja kwa moja kuwa ni tanzu za fasihi andishi lakini anachambua
vipengele hivi kama vinavyojitegemea kila kimoja.
SABABU
YA MIKINZANO YA WANAZUONI JUU YA TANZU ZA FASIHI ANDISHI
1.      Hawakubaliani
katika istilahi/majina ya tanzu mf. Mulokozi kuna utanzu anauita Kisa lakini M’ngaruthi anauita Hadithi fupi.
2.      Hawakubaliani
katika idadi mf. Nkwera (1976)
anasema kuna tanzu tatu wakati Mulokozi (1996) na M’ngaruthi (2008) wanasema
zipo tanzu nne.
 
3.      Kuna
utata katika mpangilio. Yaani ni utanzu
upi uanze, mf. Mulokozi (1996) anaanza na Ushairi, riwaya, Kisa na tamthiliya
wakati M’ngaruthi (2008) anaanza na riwaya, tamthiliya, mashairi andishi na
hadithi fupi.

Print this item

  UTENDAJI SIMULIZI
Posted by: MwlMaeda - 10-25-2021, 02:44 PM - Forum: Fasihi kwa ujumla - No Replies

Usimulizi wa Hadithi katika Afrika
Okpewho anajadili usimulizi wa hadithi
katika Afrika. Anaeleza kuwa msimulizi wa kijadi ni tofauti na msimulizi
anayepatikana katika maandishi. Usimulizi katika Afrika unafanyika wakati
maalumu hasa wakati wa jioni au usiku watu wanapokuwa katika mapumziko baada ya
vipindi maalumu vya kazi.
Usimulizi wa hadithi katika Afrika hufuata
fomula maalumu. Usimulizi wa hadithi hizi huwa na mianzo na miisho ya kifomula
ingawa mianzo na miisho hiyo hutofautiana toka jamii moja hadi nyingine. Kwa
mfano matumizi ya paukwa pakawa, hadithi hadithi n k kutegemeana na utanzu
husika.
 Pia usimulizi wa hadithi unaambatana
na ushiriki wa hadhira ambaye huonyesha kuwa anafuatilia simulizi hiyo.
Kwa jumla, utambaji wa hadithi jukwaani huwa na
sifa kadhaa zinazoutambulisha. Sifa hizi huzitenga hadithi za mapokeo na zile
tunazozisoma vitabuni.  Utendaji huu unaandamana na sifa zifuatazo;
1.
Usemi
halisi. msemaji anasema moja kwa moja
2.
Michepuko:
msimuliaji hutoa kauli za pembeni au maoni yake. Anaiacha hadithi na kusema
mambo ya pembeni au kando kabla ya kuendelea tena kuisimulia. Michepuko hii
inaweza kuwa na jukumu la viliwazo hasa katika hadithi za kusikitisha au za
kitanzia.
3.     Urudiaji
4.
Matumizi
ya wakati uliopo kihistoria/ au uliopita kisimulizi. Utambaji au usimulizi huwa
katika wakati uliopita lakini huchanganya pia na sifa zinazohusishwa na wakati
uliopo ili kuhakikisha kuwa umbali uliopo kati ya hadhira na hadithi yenyewe
umepunguzwa.
5.
Kubadilisha
muundo wa hadithi: mtambaji anauwezo wa kuubadilisha muundo wa hadithi kwa
kuongeza vitushi fulani, kurudia visa fulani, kubadilisha msamiati, kurahisisha
kisa, kutia ucheshi n.k. Kwa hakika kila utambaji hadithi moja huwa ni tofauti
na utambaji wa hadithi hiyo wa mwanzoni yaani inafaraguliwa.

Print this item

  UMILISI KATIKA NADHARIA YA SARUFI ZALISHI
Posted by: MwlMaeda - 10-25-2021, 02:42 PM - Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha - No Replies

Umilisi kama dhana ya msingi moja wapo katika nadharia ya sarufi zalishi haina ulazima wowote kwa mzawa wa Lugha kuwa nayo. Jadili
BOFYA HAPA CHINI KUFUNGUA >>>>>

.docx   CHUO_KIKUU_CHA_MTAKATIFU_AUGUSTINO_TANZA.docx (Size: 23.57 KB / Downloads: 0)

Print this item

  FASIHI, UANDISHI NA UCHAPISHAJI (2)
Posted by: MwlMaeda - 10-25-2021, 02:38 PM - Forum: Fasihi kwa ujumla - No Replies

.pdf   FASIHI, UANDISHI NA UCHAPISHAJI (2).pdf (Size: 122.27 KB / Downloads: 0)

Print this item

  KATEGORIA ZA KISARUFI KWA MKABALA WA KIMAPIKEO
Posted by: MwlMaeda - 10-25-2021, 02:29 PM - Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha - No Replies

.pdf   KATEGORIA ZA KISARUFI KWA MKABALA WA KIMAPIKEO.pdf (Size: 134.71 KB / Downloads: 0)

Print this item

  FASIHI, UANDISHI NA UCHAPISHAJI (9)
Posted by: MwlMaeda - 10-25-2021, 02:19 PM - Forum: Fasihi kwa ujumla - No Replies

SEHEMU YA PILI: UANDISHI
8. Matatizo ya Waandishi Chipukizi
Elieshi Lema
Mada ihusuyo “Matatizo ya Waandishi Chipukizi” ina matatizo yake. Katika mada hii tayari kuna wazo la kificho kwamba kuna matatizo ambayo ni ya kipekee ya waandishi chipukizi, na kwamba matatizo hayo hutoweka mara baada ya mwandishi kufaulu kuchapisha, ama kuwa na mizizi, au kukomaa. Lakini hulka ya uumbaji inafutilia mbali wazo hili kwani kila zoezi la uumbaji ni kitendo kipya, hivyo matatizo ya aina fulanifulani yatajitokeza daima na kuwaathiri waandishi wote. Ni wazi, basi, tofauti kati ya mwandishi chipukizi na yule aliyekomaa imo katika namna mwandishi anavyoyashughulikia matatizo yahusuyo uandishi wa fasihi, katika ujuzi wake wa kutumia vyombo vya kazi yake anapoumba. Baadhi hushindwa katika zoezi hili na kubakia chipukizi daima, na wengine hufaulu na kukomaa.
Makala haya yatajihusisha na waandishi wa riwaya pekee na yatajadili matatizo ya waandishi chipukizi katika mafungu matatu: (1) Matatizo yasiyoisha ya kitendo cha uumbaji, yaani, matatizo yahusianayo na maumbile ya sanaa na dhima yake katika mawasiliano; (2) Matatizo yahusianayo na jamii, kama vile athari ya mazingira kwa mwandishi na katika kazi yake; na (3) Matatizo ya ujumi na usasa; masuala yahusuyo riwaya kama fani na kufaa kwake, na athari za usasa katika kipindi cha kijamii aishicho mwandishi. Makala yatamalizia kwa kutoa maoni kuhusu njia za ufumbuzi wa matatizo yaliyozungumziwa.
1. Matatizo Yasiyoisha Katika Kitendo cha Uumbaji
Sanaa ni mawasiliano. Kuandika ni kuwasiliana, ni itikadi, imani, hisia nzito za mikanganyiko, huzuni au furaha, kupinga yale yasiyo ya haki, au kuyajaribu katika vitendo mawazo mapya yajitokezayo kichwani. Ari ya kuwasiliana na kupeana habari ni tabia iliyokita katika maumbile ya wanadamu, na ni chimbuko la furaha, utambuzi na ukuaji wa nafsi.
Ari ya kuwasiliana ni tofauti na uwezo wa kuwasiliana. Mawasiliano ya dhati yanahitaji utaratibu wa aina yake; yanahitaji utumizi wa lugha na mbinu zake, kama vile ishara, picha, tamathali, n.k., ambazo zinafahamika kwa mwandishi pamoja na wale akusudiao kuwasiliana nao. Msamiati wa lugha hii unatokana na maisha ya kila siku ya mwandishi, tangu utotoni wakati mazingira yanajitokeza kwake kihisia, na kutokana na mwongozo wa watu wazima na wazee wa jamii. Katika ngazi hii ya awali habari na maarifa hutunzwa katika ubongo wa mtu atakayekuwa mwandishi, ubongo ambao daima unajishughulisha. Mwandishi hupata maarifa kutokana na mazingira yake yanayomkuza na huyatumia katika kupanga mawazo yake.
Suala la utaratibu je? Vipi mwandishi anaufikia utaratibu katika kazi ya fasihi ili kuwasiliana? Kwanza yabidi tueleze maana ya utaratibu huu. Kwanza yafaa tuelewe kuwa hadithi ya kubuni si kiini, wahusika na mazingira tu, bali ni ujumla wa mambo yote haya katika mwelekeo wa hadithi nzima yasababishwayo na mahitilafiano, yakuzwayo hadi upeo na hatimaye kufikia mwisho na kutanzuliwa. Huu utaratibu ndio uipayo kazi ya kubuni uzito wake na nguvu yake, na wakati huohuo kuitofautisha kazi ya sanaa na maisha halisi, japokuwa kuna kurandana kwa aina fulani. Pindi mwandishi aufikiapo utaratibu huu katika kazi ya riwaya, umaana wa matendo na kubadilika kwa wahusika hueleweka na kwa hiyo maana ya kazi hiyo kujitokeza. Mtu asomaye hadithi hiyo ataweza kuwatazama wahusika katika mienendo yao kama vile ni watu halisi, msomaji atafuatilia matendo yao na kujitambulisha nao, au kutokubaliana nao au hata kuwahukumu. Hiki kitendo cha msomaji cha kujihusisha, kutokubaliana au kuhukumu mhusika katika riwaya ndicho kimwezeshacho kujifunza na kushiriki kimawazo katika mwenendo wa mabadiliko. Fasihi, kwa hiyo, ina uwezo wa kutupa kile ambacho maisha halisi yasingetupa kirahisi, au yangetupa kwa gharama kubwa. Waandishi wote hutamani kufaulu katika jambo hili na kutoa kazi bora. Hapo ndipo ulipo ugumu kwa waandishi chipukizi walio wengi.
Suala hili lina maana gani kwa waandishi chipukizi? Jambo mojawapo la msingi na muhimu kwa mwandishi yeyote ni uwezo wa kuhisi juu ya mambo yajitokezayo katika mazingira (watu, hali, matukio, n.k.); upeo wa hali ya juu wa kuyachunguza maisha, kuyatafakari na kuyatafsiri (hata kama si kwa usahihi wakati mwingine).
Mwandishi anahitaji ujuzi wa kumwezesha kuyatafsiri kikamilifu yale ayafahamuyo kisanaa. Anahitaji kuelewa, kwa mfano, kwamba bila msomaji kuwa na hamu ya kazi yake, kazi hiyo haitasomwa hata kama jambo liongelewalo ni muhimu sana. Kwa hiyo, kuna umuhimu wa kuelewa nini kitakikanacho katika kubuni hadithi – vitu kama kiini cha hadithi, wahusika, mazingira; jinsi hitilafu zijitokezavyo, upeo na suluhisho; ufundi wa kuchagua kwa makini yale yaliyo muhimu; sauti hai na ulinganifu wa mwendo unaowafanya wasomaji kupata uzoefu kihisia wakati wanaposoma. Mtindo, herufi, sarufi na alama za vituo huiongezea uzuri kazi -iliyoandikwa. Mtindo humwezesha msomaji kupata maana ya kitu kizima na siyo neno mojamoja. Kwa maneno mengine, kile aktfahamucho mwandishi (mtazamo wake wa maisha) lazima kioanishwe vizuri katika kazi yake ya kubuni na kile riwaya yake inachojaribu kukisema. Busara, kipawa na ufundi ni muhimu kwa waandishi wote, na hususa kwa waandishi wachanga ambao inabidi wajitahidi kupita kiasi. Hadi kufikia hapa tunaweza kuelewa kwa nini waandishi wachanga wengi hukwama katika hatua za mwanzo. Siyo kwa sababu hawajui la kusema, au hawana msamiati wa kutosha, bali ni kwamba kunahitajika ujuzi na maarifa ya msingi ya maumbile ya fasihi pamoja na njia maalumu ya kubuni.
2. Matatizo Yatokanayo na Jamii
2.1 Matatizo ya Kluchumi
Hili tatizo halina haja ya kusisitizwa, li wazi kabisa. Hali mbaya ya uchumi wa nchi nyingi za dunia ya tatu ni ya kuhuzunisha. Kijamii na kitaifa hali hii imesababisha mkazo kutiwa katika matatizo yaliyo wazi ya hali ya ujumla na kutozingatia matatizo yampatayo mwandishi. Macho yote yanawatazama wale wanaokufa kwa njaa, mahitaji muhimu ya binadamu, ufutaji wa maradhi, kufa kwa watoto wachanga, kujinasua kiuchumi, n.k.
Sasa mwandishi, na mwandishi mchanga pia, atafanya nini katika hali kama hii? Licha ya sabuni, sukari, mchele, unga, n.k., pia anahitaji karatasi, wmo au peni na kalamu, na mashine ya kutaipu (wengine watasema hiki ni kitu cha anasa, bali mwandishi anahitaji kutaipu kwa sababu wachapishaji wengi wanasisitiza kwamba miswada lazima iwe imetaipiwa). Mwandishi pia anahitaji muda. Hebu mfikirie mwandishi mfanyakazi anayeanza kazi saa mbili asubuhi hadi saa kumi jioni, ujira wake shilingi elfu nne. Hakuna hata haja ya kutazama matumizi ya kiasi kama hiki. Kwa wengi – na hata wale wenye kubana matumizi hasa – kipato hiki kinakuwa kimekwisha baada ya juma la kwanza la mwanzo wa mwezi. Na hapa hatujaweka katika makadirio hayo kahawa, sigara au hata bia, vitu ambavyo katika hali fulanifulani baadhi ya waandishi huvihitaji sana ili kuwasaidia kuyapanga mawazo yao barabara. Baada ya kazi na kuchoka, mwandishi anatamani kuandika kitu kutokana na vidokezo alivyovipata kwa watu au vitu mbalimbali mchana huo, wakati aiipokuwa hana kijidaftari kuweza kuviandika. Lakini anashindwa kuandika, kwani wakati huohuo anawajibika kufanya “mipango” ili aweze kuishi siku inayofuata. Kufikia siku ya pili, vidokezo hivyo huwa vimechuja, mawazo yale hayapendezi tena kama vile alivyohisi jana yake. Bado anahitaji kuandika, lakini matatizo ya kiuchumi yangalipo. Wengi wa waandishi wachanga, katika hali kama hii, wataamua kuchukua njia ya mkato, ambayo daima si nzuri.
2.2 Tatizo la Kutotambuliwa
Hadi hivi leo, Tanzania haijashughulikia suala la nafasi na dhima ya mwandishi katika kukuza na kuathiri maendeleo ya utamaduni. Hata taasisi zinazoshughulikia vitabu – wachapishaji, wachapaji, watawanyaji – zinapewa msaada mdogo sana na serikali. Licha ya hayo, ijapokuwa kumekuwa na kilio kwamba kuna ukosefu wa vitabu, suala la hali au maslahi ya waandishi bado halijashughulikiwa. Hili lina maana kwamba kumekuwepo mteguko kati ya mwandishi na kazi yake – hususa mwandishi wa kazi za kubuni kuliko yule wa kazi za taaluma.
Maana ya hili ni kwamba waandishi wachanga hawafikiriwi kuwa muhimu katika jamii, na jamii haiwajali wala kutilia uzito mapambano yao, hivyo hawana kwa kutegemea au kutoa malalamiko yao. UWAVITA je? Kabla ya kufanyika semina hii, UWAVITA ulikuwa dhaifu na haukufahamika kwa waandishi wachanga wengi hapa nchini.
Kutokuwepo kwa masomo yafundishayo uandishi mashuleni (kinyume cha uchoraji, ufmyanzi, uchongaji na ufundi mwingine), tangu shule za msingi hadi chuo kikuu, ili kuwaendeleza wale wenye vipawa vya uandishi na kuwaongoza hadi wakomae, kunadhihirisha ukosefu wa ufahamu wa suala hili muhimu la kitamaduni. Mtu anafikia hali ya kujiuliza: hii jamii yenye kilio cha ukosefu wa vitabu inatarajia hao waandishi wa vitabu vizuri watoke wapi? Sehemu kubwa ya matatizo haya inaachiwa waandishi wachanga, ambao juhudi zao kubwa zinaishia katika miswada yao kukataliwa na wachapishaji, au hata kama wakipata wachapishaji (kama itokeavyo mara nyingine), kazi zao zinapambana na wahakiki wasomi, wasio huruma, ambao wanazitupa nje kama fasihi finyu au duni.
2.3 Uhusiano wa Mwandishi na Mchapishaji
Hapa tunayafikiria mahusiano ya aina mbili ya mwandishi na mchapishaji. Kwanza ni yale ya kutotoa ahadi thabiti (noncommital). Baada ya mchapishaji kupata muswada, mwandishi anaarifiwa kwamba muswada wake umefika na utasomwa kisha atapelekewa ripoti. Hili ni jambo lifanyikalo wakati wote na hakuna ahadi kutoka kwa mchapishaji kwamba ataichukua kazi hiyo.
Kama muswada unaonyesha hali ya matumaini, mchapishaji anagharamia na kuwapa wasomaji wa kitaalamu wawili nje ya shirika ili wauchunguze na kutoa maoni kwa marekebisho zaidi. Kutokana na maoni ya mhariri na hao wasomaji wawili, kamati ya wahariri huamua kama huo muswada utafaa kuchapishwa. Je kitabu kitauzika? Hili ni jambo muhimu ambalo wachapishaji lazima wazingatie kabla ya kukubali kuchapisha muswada. Kama muswada hauwezi kuchapishwa, japo unaonyesha matumaini au pengine masahihisho yaliyopendekezwa ni mengi, muswada hurudishwa kwa mwandishi pamoja na maelezo. Mchapishaji hawezi kuwasaidia waandishi zaidi ya hapa. Kwa hiyo, mwandishi chipukizi anaachwa peke yake tena kuendelea kutambaa katika uwanja huu mgeni wa sanaa. Baadhi ya waandishi ambao hushindwa kuendelea na kuusahihisha muswada hukata tamaa na kuacha kabisa, na wengine wenye moyo hujaribu kutafuta mchapishaji mwingine.
Kuna matatizo mengine ambayo hutokea hapa, hususa yale ya ucheleweshaji. Japokuwa tatizo hili linamwathiri mwandishi, lakini linahusiana zaidi na matatizo ya uchapishaji.
Mchapishaji hutoa ahadi thabiti kwa mwandishi baada ya kuukubali mswada na baada ya hapo mkataba husainiwa. Uhusiano wa mwandishi na mchapishaji hukomazwa na kuwa wa karibu zaidi mwandishi anapofanya kazi pamoja na mhariri. Na hapa tena tatizo la ucheleweshaji hutokea. Ucheleweshaji huo hutokea kwa sababu ya mambo yafuatayo:
Quote:
(a) Waandishi wachanga wengi huwa na kiherehere na hawajui njia ambazo muswada yabidi upitie. Wanataka kazi yao itoke baada ya mwezi mmoja.
Quote:
(b) Mwandishi anaweza kuwa mgumu kushughulika naye katika masahihisho madogomadogo kwa sababu anaithamini kazi yake kihisia.
Lakini hivi ni vikwazo viwezavyo kuvukwa.
Mrabaha Kablaya Muswada Kuchapishwa au Kuuzwa Msaada wa kifedha kwa mwandishi hutofautiana katika mashirika mbalimbali. Kwa mfano, Tanzania Publishing House hutoa malipo ya awali ya mrabaha kufuatana na vipengele vifuatavyo:
Quote:
(a) Wakati mchapishaji ameridhika na thamani na taadhima ya kazi na mwandishi.
Quote:
(b) Kama mwandishi ana kazi nyingine ambayo iko katika shirika hilo yenye mauzo mazuri, basi mchapishaji hutoa malipo ya awali na kujaribu kulipiza kutokana na kazi ambayo tayari inauzika.
Quote:
© Kama, kutokana na sababu za ugonjwa au umri, mchapishaji anahisi kwamba mwandishi anaweza asiishi muda mreru. Kwa mfano mrabaha wa awali ulitolewa kwa mwandishi wa Myombekere na Bugonoka kutokana na thamani ya kazi na taadhima ya mwandishi pamoja na umri wake.
Waandishi wachanga wengi, kwa bahati mbaya, hawajafikia taadhima kama hiyo katika kazi zao.
2.4 Kutokujua Matokeo
Msimulizi wa hadithi asimuliapo hadithi kwa watoto au watu wazima, kwa kawaida huwepo aina fulani ya itiko – mafarakano, mshangao, machozi katika nyuso za wasikilizaji; huwepo kupiga makofi na kushiriki katika masimulizi;
au huwepo mfadhaiko – wasikilizaji wakizungumza wao kwa wao au wakisinzia. Matokeo ya usimuliaji hujidhihirisha palepale, kiasi kwamba msimulizi hufahamu kama anawagusa wasikilizaji au hapana.
Kuna upungufu mkubwa wa uhakiki wa kazi za fasihi Tanzania. Kundi dogo lililopo la waandishi waliokomaa na wahakiki ambalo ni la kisomi limekazania sehemu ndogo ya fasihi na maarifa yao yamebakia kwao wenyewe na kuishia katika madarasa ya chuo kikuu. Mwandishi mchanga anabakia kurudia makosa na kuendeleza utoaji wa fasihi hafifu. Matokeo ya hali hi’ ni ukosefu wa kichocheo ambacho hutokana na uhakiki wa kazi za fasihi. Na hili linatabiri hali mbaya zaidi, maana fasihi ya Tanzania itakosa mwongozo muhimu, wa kuyasukuma maendeleo ya fasihi katika mweleko fulani. Swali ambalo yabidi tujiulize ni: kama waandishi wenyewe na wahakiki hawajali jambo hili muhimu, nani basi achukue jukumu hili?
Waandishi, na hususa waandishi wachanga, wanahitaji baraza – jarida la fasihi ambalo linatoa kazi zao haraka kuliko katika fani ya kitabu, na ambapo uhakiki wa maana unaweza kufanyika. Jarida la fasihi lingekuwa uwanja wa kufanyia majaribio kwa waandishi wachanga, na matatizo ya kukomaa hayangekuwa na mateso mengi.
3. Matatizo ya Ujumi, Fani na Usasa
Katika sehemu hii tunatoa madokezo tu ili kuibusha maswali ambayo yatazaa mjadala.
Fasihi kama chombo cha utamaduni haibuniwi wala kukua katika ombwe bila uhusiano na vitu vingine. Kuna mambo ya kifalsafa na kiujumi, ambayo yanatoa mwongozo kuhusiana na maana, ukuaji na upanuzi wa fasihi, na kadhalika kutoa kanuni za utambuzi wa manufaa yake.
Ujumi unayakinishwa na utamaduni uliopo, yaani mahusiano ya watu katika jamii kufuatana na wakati na mahali. Utamaduni unaathiri sana matendo ya binadamu dhidi ya mazingira. Kwa mfano, tunafurahia kile kilicho kizuri kifani, kiaina, krosemi, n.k., na kwa maana hii ujumi unakipa kitu thamani na maana.
Maarifa haya yanaweza yasimsaidie mwandishi katika kuandika, lakini yanamsaidia mwandishi kuelewa fasihi katika hali yetu ya kitamaduni. Haya maarifa yanaweza kuathiri kazi za sanaa kama ilivyotokea kwingineko. Bado tunamsoma Aristotle ili kuelewa tanzia. Lakini shujaa aishiaye katika tanzia katika jamii yetu ya Tanzama yukoje? Hatukatai kwamba maarifa ni kwa ajili ya dunia nzima, lakini hata hivyo yanatokana na upekee wa mataifa fulanifulani.
Je, mwandishi mchanga wa Kitanzania ambaye hajapambana na fasihi ya nchi za Magharibi anaitazama fani ya riwaya kama ya kigeni? Hili linaathirije uandishi wake? Labda hapa tunahitaji kutoa heshima kwa Aniceti Kitereza. Mafunzo tuwezayo kupata kutoka kwake ni mengi.
Usasa umebomoa mipaka ya makundi ya jamii za Kiafrika ambazo zilikuwa na misingi ya kuwezesha fasihisimulizi kushamiri. Msimulizi na wasikilizaji walikuwa na lengo moja – wote walitaka utaratibu na upatano katika jamii, na kwa hiyo basi msisitizo ukawa katika mafunzo ya kiitikeli katika hadithi. Wote walikuwa na lugha moja na hata methali. Utunzi ulikuwa ni wa kijumuia.
Makundi ya kijamii ya sasa yako mengi na yenye matakwa tofautitofauti. Hali hii imesababisha kwamba daraja linalounganisha utunzi na usomaji lilegelege: mwandishi yuko peke yake wakati atafutapo lugha ya kumwezesha kuwasiliana na msomaji; na msomaji kwa upande wake hana habari na matatizo haya. Vipi mwandishi, hususa mwandishi mchanga ambaye hana uzoefu, aishughulikie hali kama hii?
Kutofautiana kwa wasomaji, kwa hakika, ni jambo zuri kwa mwandishi, kwani kunasaidia kukuza wasomaji wa aina mbalimbali. Lakini kutofautiana huko kunabadili hali ya mwandishi, kitendo cha kutunga na matokeo yake. Mwandishi anapomaliza kazi yake anapambana na matatizo ya kupata wanunuzi wa kitabu chake au watetezi kwa sababu ya matatizo na mipaka ya mahusiano ya kijamii, ambayo, yeye kama mzalishaji, anayategemea. Hii ndio siasauchumi ya uandishi, kwa maneno rahisi.
4. Ufumbuzi wa Matatizo
Sisi wote tumeona katika uzoefu wetu kwamba njia za ufumbuzi wa matatizo kwa kawaida si halisi. Zipo, lakini pia hazipo. Hata hivyo hapa tumejaribu kutoa maoni.
Quote:
(a) Waandishi, wahakiki, waalimu (hususa wale wa lugha na fasihi) wachukue hatua za kushirikisha na kukuza vipawa na moyo wa kupenda kazi za sanaa mashuleni kwa kufundisha, kuandika, na kufanya mashindano. Taasisi mbalimbali za utamaduni nazo zifanye hivyohivyo au zitoe msaada.
(b) UWAVITA ufanye mpango wa kuendesha karakana za uandishi kila mwaka au baada ya miaka miwili kwa baadhi ya watu watakaochaguliwa ambao wanaonyesha matumaini na ari ya kuandika. Kadhalika umoja huo uanzishe makundi ya waandishi.
© UWAVITA ukiombe Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kianzishe mafunzo ya uandishi, ama kama idara tofauti au katika idara ya fasihi. 

Print this item

  KSW 101: UTANGULIZI WA LUGHA NA ISIMU (MZUMBE)
Posted by: MwlMaeda - 10-25-2021, 02:11 PM - Forum: Nukuu - No Replies

CHUO KIKUU (CHA) MZUMBE (MZUMBE UNIVERSITY)KITIVO CHA SAYANSI ZA JAMII
BOFYA HAPA CHINI KUFUNGUA >>>>>

.pdf   KISWAHILI_ISIMU_JAMII.pdf (Size: 413.27 KB / Downloads: 6)

Print this item

  FASIHI, UANDISHI NA UCHAPISHAJI (11)
Posted by: MwlMaeda - 10-25-2021, 02:07 PM - Forum: Fasihi kwa ujumla - No Replies

SEHEMU YA PILI: UANDISHI
10. Matatizo ya Waandishi Chipukizi
I.C. Mbenna
Utangulizi
Waandishi wowote wale – wa habari, magazeti, vitabu au sanaa yoyote inayoambatana na uandishi – wana mwanzo. Kuna kipindi walipoanza kusimama dede katika uandishi. Walitamani kuandika vizuri, wakashindwa pa kuanzia na kumalizia. Walitamani kuinua majina yao yasomeke na waandishi na wasomaji wenzao, lakini walijikuta wakibweta bila mafanikio. Kazi ya uandishi ilikuwa ngumu, yenye kuhitaji uvumilivu na kujifunza. Mwandishi chipukizi huwa na mazingira kama hayo. Ni nia ya makala haya kumwangalia mwandishi chipukizi katika mazingira ya aina hiyo, kutafakari matatizo yake, kutafuta ufumbuzi.
Dhana ya Mwandishi Chipukizi
Mwandishi chipukizi ni nani? Bila shaka maelezo yangu ya mwanzo yamekupa fikra ya kwamba mwandishi, na hasa mwandishi wa vitabu, ni mwanafunzi asiyejua kikamilifu mambo yanayohusu uandishi, au anayejizoeza tu kama asimamavyo dede mtoto mchanga. Dhana ya mwandishi chipukizi ni pana. Kwa maneno mengine, kinyume cha mwandishi chipukizi ni mwandishi aliyekomaa.
Katika kupima kama mwandishi ni chipukizi au amekomaa, nitatumia vigezo kadhaa. Vigezo hivyo kwa mawazo yangu ni vipengele sita: kipaji, mafunzo, lugha, fikra, vitabu vilivyoandikwa, na soko la mwandishi.
Ni wazo linalokubalika na wengi kwamba kipaji katika sanaa ni jambo muhimu sana. Sanaa ya uandishi inahitaji sana mwandishi mwenyewe awe na kipaji cha kuzaliwa nacho. Kipaji hicho hujitokeza katika nafasi mbalimbali katika maisha yake, na ataonyesha hamu au kupenda sana uandishi na maandishi hata kama hajawahi kuandika. Ili kipaji chake kiwe na maana, hana budi kukilea na kukikuza. Mwandishi chipukizi ama atakuwa na kipaji kilichodumaa au hakipo kabisa. Mtu asiye na kipaji ataonyesha kupenda uandishi. Mchonga kinyago cha Kimakonde asipokuwa na kipaji, atapoteza juhudi na muda wake kwa kazi ambayo haitawapendeza watazamaji au wanunuzi wa kinyago chake. Ukosefu wa kipaji utajionyesha katika matokeo au matunda ya kazi yenyewe ya sanaa.
Aidha, kipaji peke yake hakiwezi kutoa kazi bora sana. Bali mwandishi mwenye kipaji akikifanyia mazoezi ya kuandika na akipata mafunzo kutoka kwa wenzake wenye uzoefu na vipawa zaidi, kipawa chake kitakua na atakuwa na uwezo zaidi.
Yanayomkumba mwandishi chipukizi ni kwamba mara nyingi hajui apate ushauri wapi, na aandikapo maandishi au makala yake, hapati wa kumsaidia. Tatizo hili huwapata waandishi wengi kwani hakuna chombo cha taifa au binafsi kinachotekeleza jambo hili. Vyombo vya uchapishaji hupenda zaidi kushughulikia maandishi yatokayo kwa waandishi wazoefu. Mnda kwao ni mali wasiyopenda kupoteza kwa kuyasoma maandishi yaliyoandikwa ovyoovyo, ya mwandishi chipukizi, ambayo kwa kiasi kikubwa hayafai kuchapwa kitabu au kurekebishwa ili yawe bora. Katika nchi nyingine duniani kama vile Uchina, Urusi, Amerika, Uingereza, vipo ama vyama vya waandishi au wakala (literary agents) mahsusi wa kushughulikia maandishi mbalimbali. Kama ni vyama, basi ni wanachama wanaohudumiwa kwa kuelekezwa. Iwapo ni wakala mwandishi hutekeleza masharti fulani na maandishi yake kusomwa na kupimwa kufaa kwake.
Katika nchi hizo zilizoendelea vipo pia vyuo maalumu vinavyofunza mbinu za uandishi katika nyanja mbalimbali kama vile uandishi habari, hadithi fupi, riwaya, tamthiliya na vitabu.
Jambo jingine linaloonyesha kama mwandishi ni chipukizi au amekomaa ni matumizi ya lugha. Mwandishi bingwa ana msamiati mkubwa sana na matumizi yake ya mbinu za utunzi kama methali, semi, mafumbo na sarufi ni ya kiwango cha juu sana. Hapati taabu katika kujieleza au kueleza tukio au dhama fulani anayoiandikia. Chipukizi, walakini, anababaika; anatumia maneno yaleyale machache ayajuayo au msamiati wake ni maneno magumu sana ambayo pia haelewi maana yake sawasawa. Ni vigumu kutambua hasa kipawa chake ni kipi na nafsi yake haionekani katika maandishi yake.
Sio lazima mtu asome sana ili kuwa tajiri wa lugha; walakini akisoma vya kutosha, uwezo wake unakuwa mkubwa zaidi. Elimu inampa upeo mkubwa na kwa hivyo anaweza kuandika mambo mengi zaidi katika maisha yake. Inaaminika pia kwamba kujua lugha za mataifa zaidi ya moja kunasaidia zaidi.
Lugha ya Kiswahili ni tajiri katika msamiati. Matumizi yake yanakua kila siku. Katika hali kama hii ni dhahiri kwamba Kiswahili kinazidi kukua katika msamiati na kuchukua dhana nzito zaidi ambazo hazikuwepo katika mazingira ya Waswahili hapo awali. Hii ina maana pia kwamba mwandishi hana budi kujifunza, kuijua, na kuisoma lugha aitumiayo katika uandishi wake. Asiridhike na kile anachojua. Hii ni kweli kwa mwandishi chipukizi na aliyekomaa. Wapo wanaosema kuwa Kiswahili ni lugha rahisi sana. Lakini wakipewa vitabu vyake kuvisoma ndipo wanapojua kuwa yawapasa kujifunza. Kuzaliwa Mswahili sio kujua Kiswahili.
Hapo awali nimeeleza kuwa mazoezi na mafunzo ya uandishi ni muhimu. Napenda kusisitiza kuwa mazoezi hayo lazima hatimaye yazae matunda, yaani ‘kitabu’ au ‘makala’. Mwandishi asiyeandika kitu kikajulikana kwa umbo dhahiri atabakia chipukizi aliyejaa nadharia na ndoto za kuwa mwandishi. Uandishi wa vitabu, kwa mfano, hauna maana kama mwandishi ataishia kusema: “Nitaandika kitabu kizuri.” Anaweza kusema maneno kwa nguvu zote, kwa kutamba na kudharau wengine walioandika vitabu. Lakini kama hatakaa chini, kuchukua kalamu na karatasi, na kuandika kurasa kadha wa kadha, hatakuwa mwandishi kamwe.
Ukitaka kuwa mshairi, andika mashairi. Ukitaka kuwa mkulima, lima. Kwa hivyo napenda kuwahimiza waandishi chipukizi kuandika vitabu au makala; huko ndiko kujifunza na kupata stadi zake.
Wapo baadhi ya wananchi waliowahi, na wengine bado wanaendelea, kuandika vitabu. Baadhi ya vitabu hivyo tunaviona madukani, na kwenye vibanda vya kuuzia magazeti. Wasomaji wa kawaida hupima umaarufu wa mwandishi kwa idadi ya vitabu alivyoandika. Mwenye vitabu vingi ndiye mwandishi hodari na aliyepea. Kwa kweli hiki ni kipimo kimojawapo. Lakini anaweza akawa bado ni chipukizi tu. Wingi wa vitabu si hoja kama haulingani na ubora wa kile anachoandika, uzito wa fikra katika maandishi yake, pamoja na ubingwa wa kutumia fikra hizo zimfikie msomaji na kumwelewesha fika. Uzito wa fikra utaonyesha ama ni maandishi ya kitoto au ya kiutu uzima. Ni rahisi sana kuandika uchafu na hata pengine ukapendwa na wachapishaji, wachapaji na wafanyabiashara wenye tamaa ya fedha tu. Na kwa tabia ya binadamu, ni sawa kama nguruwe anayependa kula na kugaragara katika taka. Wapo wasomaji wanaopenda kusoma vitabu vichafu visivyofuata ada, mila zozote au itikadi ya jamii waishimo. Ni dhahiri wanazo sababu zao.
Kigezo kingine unachoweza kutumia katika kumpima mwandishi ni jinsi anavyopokelewa na wasomaji pamoja na jamii yake. Kwa maneno mengine ni jinsi gani maandishi ya mwandishi yanasomwa na kutafakariwa. Wengine husema kuwa mwandishi bora huwa na soko kubwa. Vitabu vyake hununuliwa kwa wingi kila vitokapo. Lakini jambo hili si kweli daima. Pensime mwandishi wa vitabu vichafu atapendelewa sana, na pengine mwandishi bora husongwa na jamii na hata kushtakiwa na serikali yake kwa kuandika mambo fulanifulani.
Matatizo ya Mwandishi Chipukizi
Baada ya kumchambua mwandishi chipukm katika mazingira yake, tumepata pia picha mzuri ya matatizo anayopambana nayo. Matatizo hayo yasipopata utatuzi, yanamfikia pia mchapishaji, yakaathiri uchapaji, utoaji vitabu na usambazaji. Waandishi wana matatizo ya hali na mali. Wanakosa ujuzi; hawazijui taratibu za kufuata; hawana fikra nyingi nzito kutokana na kutojizamisha katika nyanja mbalimbali za uandishi na kutosoma vitabu vingi na mara kwa mara. Pengine hawana elimu ya kutosheleza. Aidha, fikra za waandishi chipukizi huongozwa na lengo la kupata fedha haraka kutokana na kuuza maandishi yao. Hawazingatii madhumuni mufti ya kuandika vitabu ambayo ni pamoja na kuelimisha, kustarehesha, kuchochea wanataaluma, kubadilishana mawazo, kuhifadhi elimu, n.k., hata bila kupata sifa au fedha kwa kazi yao.
Waandishi chipukizi, aghalabu, wanayo matatizo ya ukosefu wa vifaa vya kufanyia kazi ya uandishi. Ni ada sasa kwamba ili maandishi yoyote yasomwe na kutathminiwa na wahariri, hayana budi kuandikwa kwa mashine (tapureta). Ni vigumu kwa mwandishi chipukizi kumudu kununua chombo hiki kwa gharama yake. Pia ni ghali kumkodisha mpiga taipu. Katika nchi zilizoendelea vifaa kama kalamu, karatasi, vitabu vya rejea vya kujisomea kwa ziada kama vile vitabu vinavyozungumzia mbinu mbalimbali za fani za uandishi, si shida. Vinapatikana kila vinapohitajika.
Mwandishi wa Kitanzania anapofanikiwa kuchapishiwa kitabu chake na kikaonekana madukani, anakuwa ametumia juhudi kubwa mno. Tuzo alipatalo ni faraja tu ya kuona kimetoka. Sio jambo linalomsaidia kuinua hali yake ya maisha. Mrabaha ni mdogo mno, hautoi motisha. Hali kadhalika kasi ya uchapishaji na uchapaji katika kampuni za umma na za kigeni ni ndogo sana. Si ajabu kuambiwa kuwa shirika limetoa kitabu kimoja au viwili tu kwa mwaka. Ukiangalia uwiano baina ya wingi wa maandishi yanayomiminika kwa wachapishaji na vitabu vinavyotoka hatimaye, utakatishwa tamaa ya kuandika zaidi.
Mapendekezo ya Ufumbuzi wa Matatizo
Matatizo ya waandishi wa vitabu ni ya miaka mingi sana. Waandishi waliotutangulia kama Sheikh Shabaan Robert na Mathias Mnyampala waliyaeleza mara kwa mara; hata sisi chipukizi tumeendelea kuyarudiarudia katika semina, mikutano na mihadhara kadha wa kadha. Ufumbuzi haujapatikana. Wengi wetu tumekilaumu Chama cha Mapinduzi na Serikali kwa kutamka tu bila kuonyesha vitendo vya kuwasaidia waandishi kwa kutoa fedha au vifaa. Malalamiko yanaonyesha kutotufikisha mbali, hasa katika hali mbaya ya uchumi nchini wakati serikali ina vipaumbele vingi na vya ‘kufa na kupona’ kuliko kuwafikiria akina Ebrahim na Penina wanaotaka tamthiliya zao zichapishwe kwa ajili ya Kidato cha Nne au kisomo cha watu wazima. Serikali itakapolazimika kuchagua katika mipango yake: ama kujenga dispensari Wilaya ya Makete au kuongeza ruzuku kwa Baraza la Kiswahili, au Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, au kuwasaidia wanachama wa UWAVITA, itaona vyombo vya lugha na sanaa havina umuhimu. Ni mawazo ya wanasiasa na wapangaji mipango wengi kwamba mambo ya sanaa yanaweza kusubiri ilimradi wananchi wanapata chakula, wanatibiwa na wanalindwa.
Kwa hivyo, basi, hatuna budi kubuni mikakati mingine ya kuwasaidia waandishi. Waandishi wengi sana tu chipukizi bado. Ni mapendekezo yangu kuwa yafuatayo yatasaidia kuondoa baadhi ya matatizo na kuimarisha uandishi wa vitabu na habari miongoni mwa wananchi Tanzania.
Quote:
1. Chama cha Waandishi Tanzania (UWAVITA) kiimarishwe kwa kutangazwa vya kutosha na waandishi wenyewe kujiunga nacho. Michango yao itasaidia kupata vifaa vidogovidogo na kudumisha mawasiliano na waandishi.
2. Kuanzishwe matawi ya UWAVITA mikoani ya kuwasaidia waandishi ili waweze kukutana na kusaidiana kutatua matatizo yao.
3. UWAVITA uanzishe miradi itakayosaidiwa na wahisani au wafadhili wa nchini na nje. Kwa mfano kuchapisha jarida litakalouzwa na pia kuwa mahali pa kufanyia mazoezi ya uandishi na kupeana mawaidha.
4. UWAVITA uombe hidaya au ruzuku kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Utamaduni, Vijana na Michezo pamoja na mashirika au kampuni zenye ari ya kukuza Kiswahili na sanaa zake.
5. Mashindano ya uandishi wa riwaya, tamthiliya, mashairi, n.k., yafanywe kila inapowezekana kwa kushirikiana na vyama na vyombo vingine vinavyohusika na uandishi, uchapaji na uchapishaji.

Print this item

  FASIHI YA KIAFRIKA
Posted by: MwlMaeda - 10-25-2021, 10:11 AM - Forum: Fasihi kwa ujumla - No Replies

Fasihi ya Kiafrika
Fasihi ya Kiafrika inamaanisha maandiko kuhusu na kutoka Afrika. Kama Yusufu George anavyodokeza katika ukurasa wa kwanza wa sura yake kuhusu Fasihi ya Afrika katika kitabu “Understanding Contemporary Africa”, ‘ wakati mtizamo wa fasihi ya Ulaya kwa ujumla inahusu herufi zilizoandikwa, dhana ya Afrika inahusisha pia fasihi simulizi. 
Kama anavyoendelea kuandika, wakati maoni ya Ulaya kuhusu fasihi yalisisitiza mgawanyo wa sanaa na maudhui, mwamko wa Afrika unajumuisha:
“Fasihi” inaweza pia kuashiria matumizi ya maneno kisanaa kwa ajili ya sanaa pekee. Bila kukana jukumu muhimu la somo la sanaa katika Afrika, tunapaswa kukumbuka kwamba, tangu jadi, Waafrika huwa hawatenganishi sanaa na kufundisha. Badala ya kuandika au kuimba kwa sababu ya uzuri uliomo, waandishi wa Afrika, kwa kufuata fasihi simulizi, hutumia uzuri kusaidia kuwasiliana ukweli na taarifa muhimu na jamii. Hakika, kitu huchukuliwa kizuri kwa sababu ya ukweli kinachoonyesha na jamii kinachosaidia kujenga.
Maandiko ya kale
Misri ya Kale ulikuwa miongoni mwa tamaduni za kale zaidi za Kiafrika zenye desturi ya kuandika, ambao baadhi ya maandishi yake yaliyotumia picha na alamakuashiria kitu au jambo huishi mpaka leo. Kazi kama vile Kitabu cha Wafu cha Misri kawaida hutumiwa na wasomi kama rejeleo la msingi la imani ya kidini ya Misri ya kale na sherehe.
Maandiko ya Kinubi yanakubalika lakini kwa wakati huu hayasomeki. Awali yaliandikwa kwa kutumia picha na alama na hatimaye kwa kutumia alfabeti yenye herufi 23, kutafsiri kumekuwa kugumu.
Fasihi simulizi
Fasihi simulizi inaweza kuwa katika nathari au ushairi.
Mara nyingi, nathari huwa hadithi au historia na inaweza kujumuisha hekaya zenye wahusika bandia. Wasimulizi katika Afrika wakati mwingine hutumia mbinu ya maswali-na-majibu kusimulia hadithi zao.
Mashairi, ambayo mara nyingi huimbwa, hujumuisha: masimulizi ya visa, aya ya shughuli, aya ya kidini, mashairi ya kusifu watawala na watu wengine maarufu. Waimbaji wa sifa husimulia hadithi zao kwa kuimba. Nyimbo za mapendo, za kazi, za watoto, misemo, mithali na vitendawili pia husomwa au huimbwa.
Kwa ujumla fasihi simulizi huundwa kwa tanzu kuu nne (4) ambazo ni: Hadithi/Nathari, Ushairi/Nudhumu, Semi na sanaa za maigizo. Na kila utanzu una vipera vyake.
Fasihi kabla ya Ukoloni
Mifano ya fasihi ya Kiafrika kabla ya ukoloni ni mingi. Fasihi simulizi ya Afrika ya magharibi inajumuisha visa vya Sundiata vilivyotungwa katika Mali ya kale, Visa vya zamani vya Dinga kutoka Dola la kale la Ghana.
Nchini Ethiopia, iliyoandika awali kwa herufi za Ge’ez ni Kebra Negast au Kitabu cha Wafalme.
Aina moja maarufu ya ngano za kiafrika ni hadithi za “ulaghai”, ambapo wanyama wadogo hutumia akili zao kushinda mapambano na wanyama wakubwa. Mifano wa wanyama laghai ni pamoja na Anansi, buibui katika ngano za Waashanti kutoka Ghana; Ijàpá, kobe katika ngano za Wayoruba kutoka Nigeria; na Sungura, ambaye hupatikana katika ngano za Afrika ya Mashariki na Afrika ya kati.
Kazi nyingine zilizoandikwa ni tele, yaani katika Afrika kaskazini, kanda ya Sahel ya Afrika magharibi na pwani ya Kiswahili. Kutoka Timbuktu peke yake, kuna nakala300,000 au zaidi zilizowekwa katika maktaba mbalimbali na mikusanyiko ya binafsi, hasa zilizoandikwa kwa Kiarabu, lakini baadhi yazo katika lugha za wenyeji (yaani Peul na Songhai). Nyingi ziliandikiwa katika Chuo Kikuu maarufu cha Timbuktu. Kazi hizi zinaongelea mada nyingi, ambazo ni pamoja na Unajimu, Ushairi, Sheria, Historia, Imani, Siasa na Falsafa miongoni mwa nyingine.
Fasihi ya Kiswahili vilevile, imehamasishwa na mafundisho ya Kiislamu lakini ilikua katika mazingira ya kienyeji. Kati ya vipande vya fasihi ya Kiswahili vinavyojulikana na vya kitambo sana kimojawapo ni Utendi wa Tambuka au “Hadithi ya Tambuka”.
Katika nyakati za Kiislamu, Waafrika wa Magharibi kama vile ibn Khaldun walitia fora sana katika fasihi ya Kiarabu. Afrika Kaskazini ya kale ilinufaisha Vyuo vikuu kama vile vya Fez na Cairo, kwa kiasi kikubwa mno cha maandiko ili kuongeza yao.
Fasihi ya Kiafrika wakati wa ukoloni
Kazi nzuri za Kiafrika zinazojulikana Ulaya kutoka kipindi cha ukoloni na kile cha biashara ya utumwa ni za masimulizi ya utumwa, kama vile The Interesting Narrative of the Life of Olaudah Equiano (1789) cha Olaudah Equiano.
Katika kipindi cha ukoloni, Waafrika walioathiriwa na lugha za Ulaya walianza kuandika katika lugha hizo. Mwaka 1911, Yusufu Efraimu Casely-Hayford (ajulikanaye pia kama Ekra-Agiman) kutoka Pwani ya Dhahabu (sasa Ghana) alichapisha ile ambayo pengine ni riwaya ya kwanza ya Kiafrika kuandikwa kwa Kimombo, Ethiopia Unbound: Studies in Race Emancipation [9] Ingawa kazi hii iligusia hadithi na utetezi wa kisiasa, uchapishaji na kupitiwa upya na wanahabari wa Ulaya kulimaanisha wakati muhimu katika fasihi ya Kiafrika.
Katika kipindi hiki, tamthilia za Kiafrika zilianza kuibuka. Herbert Isaka Ernest Dhlomo wa Afrika ya Kusini alichapisha tamthilia ya kwanza ya Kiafrika kwa Kiingerezakatika mwaka wa 1935. Mwaka 1962, Ngugi wa Thiong’o kutoka Kenya aliandika mchezo wa kuigiza wa kwanza wa Afrika ya Mashariki, The Black Hermit, hadithi iliyohadhari “ukabila” (ubaguzi kati ya makabila ya Afrika).
Fasihi ya Afrika mwishoni mwa kipindi cha ukoloni (kati ya mwisho wa Vita Vikuu vya Kwanza Vya Dunia na uhuru) iliendelea kuonesha mandhari ya ukombozi, uhuru, na (walau kati ya Waafrika kwenye maeneo yaliyotawaliwa na Ufaransa) kutambua weusi wa Waafrika. Mmoja wa viongozi wa harakati za kutambua weusi, mshairi na hatimaye Rais wa Senegal, Sédar Léopold Senghor, alichapisha mkusanyo wa kwanza wa mashairi ya lugha ya Kifaransa yaliyoandikwa na Waafrika mwaka 1948, Anthologie de la Nouvelle poésie nègre et malgache de langue Française, akishirikisha utangulizi kutoka kwa mwandishi wa Kifaransa Jean-Paul Sartre. [10]
Si kwamba waandishi wa fasihi ya Afrika wakati huo walikuwa mbali na masuala waliyoyakabili. Wengi, kwa hakika, waliteswa kwa undani na pia kwa kuelekezwa: akilaaniwa kwa kuyaweka kando majukumu yake ya kisanaa ili kushiriki kikamilifu katika mapambano, Christopher Okigbo aliuawa katika vita vya Biafra dhidi ya wanaharakati wa Nigeria katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka ya 1960; Mongane Wally Serote aliwekwa kizuizini kati ya miaka 1969 na 1970 chini ya sheria ya Afrika Kusini juu ya Ugaidi ya mwaka 1967, na hatimaye kutolewa bila hata kujibu mashtaka; mwananchi mwenzake Arthur Norje alijiuamjini London mwaka 1970; Jack Mapanje wa Malawi aliwekwa kizuizini bila kesi au tuhuma kwa sababu ya matamko aliyotoa katika baa ya chuo kikuu; na, mwaka 1995, Ken saro-Wiwaalikufa kwa kutiwa kitanzi na serikali ya wanajeshi ya Nigeria.
Fasihi ya Afrika baada ya ukoloni
Kwa ukombozi na kuongezeka kwa kusoma na kuandika kwani mataifa mengi ya Afrika yalipata uhuru wao katika miaka ya 1950 na hasa miaka ya 1960, fasihi ya Afrika imekua kwa kasi kwa wingi na kwa umaarufu, kwa kazi nyingi za Afrika kuonekana katika mitaala ya elimu ya Ulaya na katika orodha ya “vitabu bora” vilivyoandikwa mwishoni mwa karne ya 20. Waandishi wa Afrika katika kipindi hiki waliandika katika lugha za Ulaya (hasa Kiingereza, Kifaransa na Kireno) na pia lugha za jadi za Afrika.
Ali A. Mazrui na wengine hutaja migogoro saba kama mandhari: Farakano kati ya Afrika iliyopita na iliyopo, kati ya Utamaduni na Usasa, kati ya wazawa na wageni, kati ya kujijali na kujali jamii, kati ya Ujamaa na Ubepari, kati ya maendeleo na kujitegemea na kati ya Uafrika na ubinadamu. [11]
Mandhari mengine katika kipindi hiki ni pamoja na matatizo ya kijamii kama vile ufisadi, tofauti za kiuchumi kati ya nchi ambazo zimepata uhuru majuzi, na haki na majukumu ya wanawake. Waandishi wa kike wamewakilishwa vyema katika fasihi ya Afrika iliyochapishwa kuliko walivyokuwa kabla ya uhuru.
Mwaka 1986, Wole Soyinka alikuwa mwandishi wa Afrika wa kwanza baada ya uhuru kushinda Tuzo la Nobel katika fasihi, ingawa Camus Albert, mzaliwa wa Algeria, alipokea tuzo hilo katika mwaka 1957.
Tuzo la Noma
Tuzo la Noma, lilianza mwaka wa 1980, hupatiwa kwa kazi bora ya mwaka katika fasihi ya Afrika.
Riwaya Kuu za Afrika
  • Chinua Achebe, Things Fall Apart (Nigeria)
  • Nuruddin Farah, From a Crooked Rib (Somalia)
  • Alan Paton, Cry, The Beloved Country (Afrika ya Kusini)
  • Gracy Ukala, Dizzy Angel (Nigeria)
  • Daniel Olorunfemi Fagunwa, Ogboju Ode ninu Igbo irunmalẹ (The Forest of a Thousand Demons) (Nigeria)
  • Dalene Matthee, Kringe katika ‘n bos (Circles in a forest) (Afrika ya Kusini)
  • Mariama Ba, si longue Une lettre (Barua Ndefu Kama Hii) (Senegal)
  • Sembène Ousmane, Xala (Senegal)
  • Ngugi wa Thiong’o, A Grain of Wheat (Kenya)
  • Benjamin Sehene, Le Feu sous la Soutane (Fire under the Cassock) (Rwanda)
  • Thomas Mofolo, Chaka (Afrika ya Kusini / Lesotho)
  • Tsitsi Dangarembga, Nervous Conditions (Zimbabwe)
  • Dambudzo Marechera, The House of Hunger (Zimbabwe / Rhodesia)
  • Yvonne Vera, Butterfly Burning (Zimbabwe)
  • Mia Couto, Terra Sonâmbula (A Sleepwalking Land) (Msumbiji)
  • Ayi Kwei Armah, The Beautiful Ones Are Not Yet Born (Ghana)
  • Ben Okri|Ben Okri, The Famished Road (Nigeria)
  • JM Coetzee|JM Coetzee, soni (Afrika ya Kusini)
  • Bessie Head, “When Rain Clouds Gather” (Botswana)
  • Sarah Ladipo Manyika, In Dependence (Nigeria)
  • Chimamanda Ngoye Adichie, Half of a Yellow Sun (Nigeria)
  • Charles Mangua, A Tail in the Mouth (Kenya)
  • Camara Laye, The Tadiance of teh King (Guinea)
  • Nnedi Okorafor, Zahrah ya Windseeker (Nigeria)
  • Monenembo Tierno, King of Kahel (Guinea)
  • Sefi Atta, Everything Good Will Come (Nigeria)
Washairi wakuu wa Afrika
  • Antjie Krog (Afrika Kusini)
  • Chinua Achebe (Nigeria)
  • Georges Andriamanantena (Rado) (Madagaska)
  • Ama Ata Aidoo (Ghana)
  • Jared Angira (Kenya)
  • Kofi Anyidoho (Ghana)
  • Kofi Awoonor (Ghana)
  • Sahlesillasse Birhanemariam (Ethiopia)
  • Dennis Brutus (Afrika Kusini)
  • Glynn Burridge (Shelisheli)
  • Abena Busia (Ghana)
  • John Pepper Clark (Nigeria)
  • José Craveirinha (Msumbiji)
  • Viriato Clemente da Cruz (Angola)
  • Tsegaye Gebremedhin (Ethiopia)
  • Abbe Gubenga (Ethiopia)
  • Don Mattera (Afrika Kusini)
  • Jonathan Kariara (Kenya)
  • Joseph Kariuki (Kenya)
  • Susan Kiguli (Uganda)
  • Ahmadou Kourouma (Ivory Coast)
  • Togara Muzanenhamo (Zimbabwe)
  • Arthur Nortje (Afrika Kusini)
  • Gabriel Okara (Nigeria)
  • Ingrid Jonker (Afrika Kusini)
  • Patricia Jabbeh Wesley (Liberia)
  • K. Moses Nagbe (Liberia)
  • Bai Tamia Moore (Liberia)
  • Prof. Jack Mapanje (Malawi)
  • Nii Parkes (Ghana)
  • Christopher Okigbo (Nigeria)
  • Ben Okri (Nigeria)
  • Okot P’Bitek (Uganda)
  • Lenrie Peters (Gambia)
  • Jean-Joseph Rabearivelo (Madagaska)
  • Jacques Rabemananjara (Madagaska)
  • Elie Rajaonarison (Madagaska)
  • Breyten Breytenbach (Afrika Kusini)
  • Ny Avana Ramanantoanina (Madagaska)
  • Pierre Randrianarisoa (Madagaska)
  • Jean Verdi Salomon Razakandraina (Dox)(Madagaska)
  • David Rubadiri (Malawi, Uganda)
  • Léopold Sédar Senghor (Senegal)
  • Véronique Tadjo (Ivory Coast)
  • Wole Soyinka (Nigeria)
  • Hadraawi (Somalia)
  • Dagnachew Werku (Ethiopia)
  • Bewketu Seyoum (Ethiopia)
  • Adam Small (Afrika Kusini)
  • Getinet Eniyew (Ethiopia)
  • Debede Seyfu (Ethiopia)
  • Eugene Marais (Afrika Kusini)
  • Arménio Vieira (Cape Verde)

Print this item

  TOFAUTI YA SILABI NA NENO
Posted by: MwlMaeda - 10-25-2021, 10:04 AM - Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha - No Replies

        SILABI                                                                                                            NENO
(i) Huwa ni sehemu ya neno                                                                          (i) Huwa ni neno zima
(ii) Hazibebi maana yoyote                                                                           (ii) Hubeba maana katika tungo
(iii) Ni sifa ya kifonolojia (matamshi)                                                         (iii) Ni sifa ya kimofolojia (umbo)
(iv) Hutengwa hata katika mzizi wa neno                                                   (iv) Mzizi wa neno hauguswi
(v) Huweza kuwa huru au funge                                                                 (v) Huweza kuwa huru au changamano
(vi) Hubeba mkazo itokeapo nafasi ya pili mwishoni mwa neno               (vi) Neno zima huwa halibebi mkazo

Print this item