SHAIRI: WANAWAKE MALAIKA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: WANAWAKE MALAIKA (/showthread.php?tid=1356) |
SHAIRI: WANAWAKE MALAIKA - MwlMaeda - 10-23-2021 WANAWAKE MALAIKA Papara sipaparike, usije pata mashaka, Situkane wanawake, chonde chonde ewe Kaka, Wala usifazaike, ukaivuka mipaka, Wanawake malaika, izingatie miiko. Ndugu usidanganyike, kwa nchi na mamlaka, Tena usihadaike, kwa rangi 'kababaika, Uzuri wa mwanamke, vikorombwezo wataka, *Wanawake malaika, izingatie miiko.* Kujipamba apambike, ni fulusi kutumika, Ubakhili sijivike, kisha vinono wataka, Yataka utaabike, mahitaji kuyasaka, Wanawake malaika, izingatie miiko. Urembo haiba yake, yatengenezwa hakika, Ajirembe asifike, mrembo asiye shaka, Ni viunzi uviruke, maisha kwenda yasaka, Wanawake malaika, izingatie miiko.* Tama kituo nifike, wanawake malaika, Matunzo yasikatike, kula kunywa kadhalika, Na gubu likuondoke, mahaba kukamilika, *Wanawake malaika, izingatie miiko.* Khamis S.M. Mataka. |