Neno sadfa katika lugha ya Kiswahili ni nomino: [Ngeli: i-/zi-] yenye maana ya hali ambapo mambo au matukio mawili au zaidi hutokea kwa wakati mmoja bila ya kupangwa au kutarajiwa .
Katika lugha ya Kiarabu, neno hili sadfa( soma: swidfatun/swidfatan/swidfatin صدفة ) ni nomino ya Kiarabu yenye maana ya kukutana bila ya kukubaliana au kuwa na miadi.
Kinachodhihiri ni kuwa neno hili swidfatun/swidfatan/swidfatin صدفة lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno la Kiswahili ' sadfa ' halikubadili maana ya lugha asili - Kiarabu ya kutokea jambo au tukio bila ya kupangwa.
Neno *halmashauri* katika lugha ya Kiswahili lina maana zifuatazo:
1. *Nomino: [Ngeli: i-/zi-]* kikundi cha watu waliochaguliwa au kuteuliwa kufanya kazi ya kuwa watawala, watunga sheria, washauri au kuelekeza jambo fulani.
2. *Nomino: [Ngeli: i-/zi-]* chombo cha kiutawala katika wilaya au mji.
2. *Nomino: [Ngeli: i-/zi-]* kundi la watu waliochaguliwa au kuteuliwa kuelekeza utendaji wa shughuli fulani.
Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *halmashauri* ni naneno mawili ya Kiarabu yaliyowekwa pamoja; neno *ahlu* (soma: *ahlu/ahla/ahli اهل)* lenye maana ya *watu, -enye,* na neno *mashauri* (soma:*mashuuratun /mashuuratan/mashuuratin* *مشورة* ) pia *mash-wara* (soma: *mash-waratun/mash-waratan/mash-waratin مشورة)* lenye maana zifuatazo:
1. Kinachotolewa nasaha kwa rai au namna nyingine.
2. Ushauri.
3. Nasaha, muongozo.
Kinachodhihiri ni kuwa maneno haya mawili *ahlu mashuurat/mash-warat* yaliipoingia katika Kiswahili na kutoholewa, neno jipya la Kiswahili *halmashauri* lilipatikana.
Katika lugha ya Kiarabu neno *shuuraa شورى* linatumika kwa kisawe cha maneno *mashuurat مشورة* na *mash-warat مشورة* na hupatikana misamiati *ahlu al-shuuraa* (soma: *ahlush shuraa اهل الشورى washauri)* na *majlis al-shuuraa* (soma: *majlisush shuraa مجلس الشورى baraza la ushauri; bunge).*
Neno aila katika lugha ya Kiswahili ni nomino: [Ngeli: a-/wa-] yenye maana ya ndugu wa familia moja; familia.
Katika lugha ya Kiarabu, neno hili aila( soma: aailatun/aailatan/aailatin عائلة ) ni nomino ya Kiarabu yenye maana zifuatazo:
1. Neno la jinsi ya kike kwa neno la Kiarabu aail (soma: aailun/aailan/aailin عائل) lenye maana zifuatazo:
a) Mtu mwenye watoto wengi.
b) Mtu anayeishi katika lindi la ufukara.
c) Mmea unaotegemewa na mmea mwengine kwa makuzi na kupata chakula.
d) Familia: Kundi linalokusanya mume, mke, watoto na ndugu wanaowategemea; ndugu wanaoishi nyumba moja.
2. Watu wa nasaba ya babu wa kwanza mmoja; ukoo.
Kinachodhihiri ni kuwa neno hili aailatun/aailatan/aailatin عائلة lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno la Kiswahili ' aila ' lilichukua maana moja inayohusu familia/ukoo na kuacha maana zingine zilizo katika lugha asili - Kiarabu.
Neno aibu katika lugha ya Kiswahili ni nomino: [Ngeli: i-/zi-] yenye maana zifuatazo:
1. Jambo la kumtia mtu fedheha, jambo la kumvunjia mtu heshima.
2. Hali ya mtu kuvaa mavazi yasiyomsitiri vyema.
Kuna nahau: jitia aibu, tia mtu aibu: Alivua nguo mbele ya watu bila kuona aibu.
Kuna methali: Aibu ya maiti aijuaye mwosha: mtu anayezifahamu siri za mtu fulani ni yule aliyenaye karibu.
Katika lugha ya Kiarabu, neno hili aibu( soma: aybun/ayban/aybin عيب ) ni nomino ya Kiarabu yenye maana zifuatazo:
1. Kasoro, upungufu wa sifa: bidhwaa-atun laa aiba fiihaa بضاعة لا عيب فيها bidhaa isiyo kasoro yoyote.
2. Fedheha. Kuna msemo: Alfaqru Laysa Bi Aybin الفقر ليس بعيب ufukara si aibu.
Kinachodhihiri ni kuwa neno hili aybun/ayban/aybin lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno la Kiswahili ' aibu ' halikubadili maana yake katika lugha yake asili - Kiarabu.
Posted by: MwlMaeda - 01-22-2022, 07:46 PM - Forum: Je, wajua ?
- No Replies
FAHAMU MAJINA YA SEHEMU ZA MIJI MAARUFU TANZANIA NA MAANA ZAKE
1. KOLOMIJE.
Inasemekana mahali hapo alifika Mzungu aliyeitwa James, hivyo huyu Mzungu akataka watu wamwite "J" badala ya kutamka jina lote. Hivyo akawaambia CALL ME J, wabantu wakatamka KOLOMIJE na kutengeneza jina la eneo hilo.
2. KARIAKOO
Hii ilitokana na neno Carrier_crop ambalo lilikuwa ni jina la wabeba mizigo wa eneo hilo la sokoni, lakini Waswahili walishindwa kulitamka jina hilo hivyo wakasababisha kutokea kwa jina la Kariakoo.
3. MSASANI.
Hili jina lililotokana na Bwana mmoja aliyeitwa Musa Hassan ambaye alikuwa ni Mnyapara aliyekuwa akisimamia mashamba ya katani ambaye asili yake ni Mtwara, wamakonde wengi wakaamua kuja kumuomba kazi na kwa kwa kuwa walikuwa hawajui anapoishi waliuliza kwa Mucha Hachani, na wakaendelea kuunga unga mpaka kusababisha kutokea kwa jina la Msasani.
4. KAWE.
Hili lilitokana na neno Cow_Way, barabara maarufu kwa kuswagwa ng'ombe kufikishwa hapo Tangaynyika Packers kwa machinjo.
5. KIGOGO
Ilitokana na kigogo halisi kabisa cha kuvuka pale kigogo mwisho kila jumamosi walikuwa wanakusanyika kukiweka "jamani leo siku ya kigogo" (leo pamejengwa daraja).
6. TABATA
Palikuwa na Muarabu aliyekuwa ananunua korosho kwa mali kauli na kuwaahidi wachuuzi waje siku fulani watalipwa kwa kuwaambia "hapana tabu tabata (utapata pesa yako) akabatizwa jina la Mwarabau Tabata, na mwishowe mahali hapo napo pakaanza kuitwa Tabata.
7. ILALA
Jina hili linatokana na makaburi ya pale Karume ambako hakukuwa na mengine hivyo kila alasiri watu walikuwa wakienda kuzika na wimbo wa Haila Illallah! na mwishowe mahala hapo pakaanza kuitwa Ilala.
8. UBUNGO
Majina yafuatayo: bungoni, mikoroshini, na mabibo yote haya yalitokana na uwepo wa miti mingi ya matunda hayo kupatikana maeneo hayo.
9. KIBORILONI
Kiboriloni ni neno lililotokana na maneno mawili KIBO na ALONE. Hii ilikuwa sehemu ambapo wazungu walisimama na kuona kilele cha Kibo pekee bila kukiona kilele cha Mawenzi, Kibo na Mawenzi ni vilele vya Mt. Kilimanjaro.
10. KIBOSHO
Lilitokana na maneno KIBO na SHOW, hii ni sehemu ambapo Kibo kilionekana vizuri zaidi.
11. MWANANYAMALA
Hapo kitambo mitaa ya Mwananyamala kulikuwa na mapori na Simba, kwa hiyo kina mama wa kizaramo walipokuwa wakifika mitaa hiyo wakawa wanawaambia watoto wao wanapolia usiku"Mwana Nyamala" maana yake "Mtoto Nyamaza" ili wasisikiwe na Simba.
12. TABORA
Kambi ya Wafanyabiasha. Walikuwa wakipita na bidhaa zao wanakuta viazi vitamu vilivyopikwa na kukatwakatwa vipande na kuanikwa. Hapo huliwa makavu (Chewing gum) au kupikwa na kuliwa. Haya huitwa Matobolwa au Matovola. Hivyo wakapaita kambi ya Matobolwa au Matovolwa. Hii ilikuwa kugeuka na kuwa Tabora.
13. SUMBAWANGA
Wenyeji wa maeneo hayo walikerwa na vitendo vya ushirikina (tofauti na mtazamo wa watu wengi kwamba wenyeji wanaendekeza ushirikina). Kutokana na kero hiyo waliamua kuwapiga mkwara watu wanaoingia katika mji huo kwamba kama unataka kuja huku, basi Tupa Uchawi i.e Sumba (Tupa) Wanga (Uchawi), ukitupa na kuuacha uchawi wako huko uliko unaruhusiwa kuja hapo Sumbawanga.
14. MTONI KWA AZIZ ALI.
Mtoni kwa Aziz Ali pamepata jina kutokana na mkazi mmoja aliyekuwa maarufu (alwatani) sana marehemu Aziz Ali. Mzee huyu alifariki miaka kadhaa iliyopita.
15. KWA BIBI NYAU.
Kwa Bibi Nyau kulikuwa na ajuza mmoja alikuwa anafuga paka wengi sana.
16. NEWALA.
Waingereza walipofika Mtwara walikuta kisima kilichojengwa na wajerumani ambacho kilikuwa cha kizamani kwa wakati Huo , Hivyo walijenga kisima kipya na kukiita NEW WELL, watanganyika wakatamka NEWALA, hatimaye likawa jina la ile sehemu.
17. CHEKERENI[MOSHI].
Hili ni eneo ambapo barabara inakatiza kwenye reli.Sasa wazungu waliweka alama ya bararani ya tahadhari kabla ya kuvuka reli CHECK THE LINE, watu wakatamka CHEKERENI na kuliita hivyo lile eneo hadi leo.
18 . MAKONGOLOSI
Inatokana na neno la kiingereza MAKING LOSS - Zamani waingereza walipata hasara kutokana na shuguli za uchimbaji wa madini eneo la Makongolosi wilaya ya Chunya mbeya ndipo eneo hilo kubatizwa jina hilo .
19 . GODIMA
Ni kijiji kimoja wapo kilichopo wilaya ya Chunya ambacho jina lake lilitokana na kiingereza ambalo ni GOLD MINE ( Mgodi wa Dhababu
20. MATOMBO
Matombo kwa kiluguru ni matiti. Eneo hilo kuna jiwe lenye mwonekano wa mwanamke mwenye matiti. Ndicho chanzo cha kuitwa matombo.
21. KIPONZERO
Kijiji kilichopo barabara ya Iringa kwenda mbeya ndani ya mkoa wa Iringa.Wakati wa ujenzi wa barabara wapimaji walitumia sana neno KEEP ON ZERO kitu kilichofanya wenyeji wafikiri wale wazungu wanapaita pale keep on zero ambayo wao waliitamka kiponzero.
22.MKONGOTEMA
Kijiji kipo baraba ya Njombe to songea. MKONGO ni mti ,Tema walikuwa na maana ya litema/ matema mashamba ya mazao kama ulezi yanayokuwa milimani. Sasa kutokana na watu kukata miti kwaajili ya matema basi ikawa ukitaka kumwelekeza mtu aliko. Unamweleza " kwavudumula mikongo ya matema kola" kingoni. Basi likaja neno MKONGOTEMA.
23. MBAMBA BAY
Kuna mlima upo hapo unaitwa mlima Mbamba. Kwa kilugha mbamba ni radi. Mlima ule ulikuwa na kawaida ya kupiga sana radi nyakati za masika. Hivyo ukaitwa mlima mbamba. Na kutokana eneo hilo lina ghuba katika ziwa nyasa ( bay) ndipo lilipozaliwa jina Ghuba ya Mbamba yaani MBAMBA BAY.
24. KILOMENI ilitokana na maaguzo wakati wa mapigani mzungu aliagiza askari wakifika pale waue wanaume wote yaani KILL ALL MEN wabongo wakashindwa kutamka ndipo wakaishia KILOMENI
25 GONGO LA MBOTO hili lilitokana na mzee mmoja aliyekuwabakiitwa mzee Mboto alikuwa na kirungu kile chenye kichwa. Alipoenda kuwinda maeneo yale ambayo wakati huo yalikuwa ni porini hakuruni. Wakamtafuta sana lakini hawakumpata mpaka leo isipokuwa waliliona rungo au gongo lake. Ndipo walio liona wakati wa kutafuta wakasema jamanj GONGO LA MBOTO hili hapa. Kuanzia siku hiyo eneo hilo limaitwa GONGO LA MBOTO
26 MIKOCHENI lilitokana na duka la kubadilisha pesa MICRO CHANGE
27 KILIMANJARO limetokana na wazungu kushindwa kutamka KILIMA CHA RUWA
27 MBEZI INN MAGARI SABA ilitokea ajali iliyohusisha magari saba kwa wakati mmoja hapo
28 KIBAHA PICHA YA NDEGE jamaa alitengeneza sanam ya ndege na kuiweka hapo paka pta jina.
29. Sehemu nyungine zinabebe majina ya watu kutokana kwamba wao ndiyo walikuwa maarufu wakati huo au walikuwa wa kwanzq kuhamia maeneo hayo. Mfano Mbezi, Mbezi kwa Yusufu, Kwa Msuguli, kwa Ally Maua, Kwa Tumbo alikuwa na tumbo kubwa, kwa Semangube, kwa Shemsa, Kwa bastola, kwa mfuga mbwa, tegeta kwa ndevu nk
Neno ahirari katika lugha ya Kiswahili lina maana zifuatazo:
1. Nomino: [Ngeli: a-/-wa, wingi: maahirari] yenye maana ya: mtu aliyeachiliwa huru kutoka kifungoni.
2. Kitenzi elekezi: ahirar.i achilia huru aghalabu watu waliokuwa kifungoni au kizuizini; weka huru.
Katika lugha ya Kiarabu, neno hili ahirari( soma: ahraarun/ahraaran/ahraarin احرار ) ni nomino ya Kiarabu ikiwa ni wingi wa neno huru ( soma: hurrun/hurran/hurrin حر ).
Kinachodhihiri ni kuwa neno hili huru ( soma: hurrun/hurran/hurrin حر ) lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa huru lilichukua kutoka lugha ya asili - Kiarabu maana ya mtumwa aliyeachiwa n a ikabuniwa maana mpya ya mwanamke mtawa, mcha-Mungu na mwenye tabia njema , wakati neno la Kiarabu ahraaru/ahraaran/ahraarin lililo wingi wa neno la Kiarabu hurrun/hurran/hurrin lilitoholewa kuwa neno la Kiswahili ahirari likiwa nomino iliyopewa maana mpya ya mtu aliyeachiliwa huru kutoka kifungoni na kitenzi elekezi chenye maana ya achilia huru aghalabu watu waliokuwa kifungoni au kizuizini; weka huru.
Kwa tatizo yake dawa, uanze kulisakama,
Mwishowe kulitatatua, kwa busara na hekima,
Wako moyo utapowa, furaha ukiifuma,
Halina thamani chozi, alinihusia mama.
Wakati tukifiliwa, mfano baba na mama,
Moyo hutaki kutuwa, machozi hujaa pima,
Vipi wanafufuliwa? mwisho vichwa vyatuuma,
Halina thamani chozi, alinihusia mama.
Tupatapo mitihani, ya mabonde na milima,
Mikono huwa kichwani, tulie olele mama,
Mwisho tunapata Soni, kulia mtu mzima.
Nilikuwa bado kinda, alipofariki mama,
Kilio sikukishinda, nililia Kama kinda,
Huku kule nilikwenda, yani aamke mama,
Halina thamani chozi, alinihusia mama.
Siku niliyoamini, chozi halina salama,
Yangu hapo sithamini, kulivisha koja jema,
Machozi ni kitu duni, aminj ninayosema,.
Halina thamani chozi, alinihusia mama.
Kwa heri wanazuoni, ndugu zangu maulama,
Nimefika ukingoni, ndiyo yangu kaditama,
Kulialia ya nini, bure kujitia homa?
Halina thamani chozi, alinihusia mama.