MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'AILA'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO 'AILA'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AILA'

Neno aila katika lugha ya Kiswahili ni nomino: [Ngeli: a-/wa-] yenye maana ya ndugu wa familia moja; familia.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili aila( soma: aailatun/aailatan/aailatin عائلة ) ni nomino ya Kiarabu yenye maana zifuatazo:

1. Neno la jinsi ya kike kwa neno la Kiarabu aail (soma: aailun/aailan/aailin عائل) lenye maana zifuatazo:
a)  Mtu mwenye watoto wengi.

b) Mtu anayeishi katika lindi la ufukara.

c) Mmea unaotegemewa na mmea mwengine kwa makuzi na kupata chakula.

d) Familia: Kundi linalokusanya mume, mke, watoto na ndugu wanaowategemea; ndugu wanaoishi nyumba moja.

2. Watu wa nasaba ya babu wa kwanza mmoja; ukoo.

Kinachodhihiri ni kuwa neno hili aailatun/aailatan/aailatin عائلة lilipoingia katika  Kiswahili na kutoholewa kuwa neno la Kiswahili ' aila ' lilichukua maana moja inayohusu familia/ukoo na kuacha maana zingine zilizo katika lugha asili - Kiarabu.

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)