ETIMOLOJIA YA NENO 'AIBU' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'AIBU' (/showthread.php?tid=2284) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'AIBU' - MwlMaeda - 01-23-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AIBU' Neno aibu katika lugha ya Kiswahili ni nomino: [Ngeli: i-/zi-] yenye maana zifuatazo: 1. Jambo la kumtia mtu fedheha, jambo la kumvunjia mtu heshima. 2. Hali ya mtu kuvaa mavazi yasiyomsitiri vyema. Kuna nahau: jitia aibu, tia mtu aibu: Alivua nguo mbele ya watu bila kuona aibu. Kuna methali: Aibu ya maiti aijuaye mwosha: mtu anayezifahamu siri za mtu fulani ni yule aliyenaye karibu. Katika lugha ya Kiarabu, neno hili aibu( soma: aybun/ayban/aybin عيب ) ni nomino ya Kiarabu yenye maana zifuatazo: 1. Kasoro, upungufu wa sifa: bidhwaa-atun laa aiba fiihaa بضاعة لا عيب فيها bidhaa isiyo kasoro yoyote. 2. Fedheha. Kuna msemo: Alfaqru Laysa Bi Aybin الفقر ليس بعيب ufukara si aibu. Kinachodhihiri ni kuwa neno hili aybun/ayban/aybin lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno la Kiswahili ' aibu ' halikubadili maana yake katika lugha yake asili - Kiarabu. Shukran sana. Khamis S.M. Mataka. |