Mimi sichelei kufa, kudura yake Manani,
Kufa budi nitakufa, mchana ama jioni,
Hufa visivyo na ufa, sembuse aliye duni!
Nakata shingo nusufa, na mkia kiungoni.
Kama kufa ni maafa, naona bwana huponi,
Kiumbe hana sarifa, mauti yamo milini,
Nikifa hupati mafa, furaha yako nini?
Nakata shingo nusufa, na mkia kiungoni.
Ikiwa kufa kashifa, si peke yangu ufuni,
Ikiwa neno la dhifa, sina mfundo moyoni,
Iwapo kufa sharafa, sifi ninangoja nini?
Nakata shingo nusufa, na mkia kiungoni.
Hufa watu wenye sifa, na mafao duniani,
Wapenzi wake latifa, kama Mitume wa dini,
Hufa walaji wa mofa, na walao biriani,
Nakata shingo nusufa, na mkia kiungoni.
Kafa Tumwa Mustafa, patabaki kitu gani?
Maneno yako kifafa, hayana fikira ndani,
Si maneno ya wadhifa, mfano wa punguani,
Nakata shingo nusufa, na mkia kiungoni.
Ebu niambie kaifa, nguvu huletwa na nini?
Siyo yangu taarifa, maneno yenu shetani,
Na nyinyi mwataka sifa, nayo haipatikani,
Nakata shingo nusufa, na mkia kiungoni.
Uchache wa maarifa, ama kasoro kichwani,
Ni neno la takilifa, kwa hukumu na maoni;
Ndoa haina hilafa, ni sheria ni kanuni,
Nakata shingo nusufa, na mkia kiungoni.
Ndoa kitu ashrafa, utumwa wajia nini?
Ndoa jambo mzofafa, huwaje umajinuni!
Ndoa ni lulu nadhifa, nimehuni kitu gani?
Nakata shingo nusufa, na mkia kiungoni.
Mwana kalia kigoda, kabla ya ndoa kupita,
Keti sipoteze muda, muda mwanangu ukuta,
Nikufunze yalo ada, kesho usije kujuta,
Ile chungu ndio tamu, mwanangu mume kahawa.
Nianze kukupongeza, kupata ubavu wako,
Shukuru sana Muweza, uswalipo swala zako,
Kila pande kaangaza, ela kavutika kwako.
Ile chungu ndio tamu, mwanangu mume kahawa.
Mume usije mkwaza, wakanye rafiki zako,
Yao na iwe baraza, wasijue chumba chako,
Maneno mkimaliza, rejea chumbani mwako.
Ile chungu ndio tamu, mwanangu mume kahawa. Unapotoka nyumbani, kichwa usiwache wazi,
Iwe waenda sokoni, au kuona wazazi,
Inamisha macho chini, simkere mkumbazi.
Ile chungu ndio tamu, mwanangu mume kahawa. Sitoke bila kuaga, mwanangu ninakujuza,
Iwe homa yanipiga, au niko kwa jeneza,
Uanze simu kupiga, mumeo kumueleza,
Ile chungu ndio tamu, mwanangu mume kahawa. Hodi hodi vijumbani, kama vile paparazi,
Tuli msubiri hani, lala kama huna kazi,
Kushinda kwa majirani, tamkera laazizi,
Ile chungu ndio tamu, mwanangu mume kahawa. Usilete ushindani, kwa mume nakuusia,
Msikize wa ubani, kila anokuambia,
Lilo kinyume na dini, kukataa si hatia.
Ile chungu ndio tamu, mwanangu mume kahawa. Akikwita itikia, rabeka mpenzi wangu,
Sauti ya kubania, na jicho lako la kungu,
Haraka asije chukia, siku uione chungu,
Ile chungu ndio tamu, mwanangu mume kahawa. Siwate dada wa kazi, mumeo kumpikia,
Sawa azikune nazi, na nyama kukukatia,
Ila kuunga mchuzi, sipende kumuachia,
Ile chungu ndio tamu, mwanangu mume kahawa. Ukae pembeni yake, anapokula chakula,
Kumlisha usichoke, ugali na amarula,
Mume asiwe mpweke, akatafuta badala.
Ile chungu ndio tamu, mwanangu mume kahawa Ugomvi mwishowe ndani, nje wasije sikia,
Usijaribu asilani, ya ndani kusimulia,
Huo ni uhayawani, sidhani nakutania,
Ile chungu ndio tamu, mwanangu mume kahawa. Mume ana hadhi yake, hivyo ataka adabu,
Akiwa na jekejeke, sema naye taratibu
Akitishia mateke, kunywa maji simjibu,
Ile chungu ndio tamu, mwanangu mume kahawa. Kwa mume kuna furaha, nisiyoweza kukupa,
Ela yapo ya karaha, kuzidi yaliyo hapa,
Nisemayo si mzaha, wa kibogoyo na fupa.
Ile chungu ndio tamu, mwanangu mume kahawa. Kuna jambo ulishike, kama wataka thawabu,
Pepo utapata kwake, kwa huyo wako muhibu,
Ukitaka radhi zake, usende kumpa tabu.
Ile chungu ndio tamu, mwanangu mume kahawa. Baada jua kutuwa, mwana usende mahala,
Vyovyote itavyokuwa, uwe wa mwisho kulala,
Rauka kama wajuwa, kazi baada ya swala.
Ile chungu ndio tamu, mwanangu mume kahawa. Siri sito ifukia, nilonayo kwa mtima,
Ingawa nafurahia, kwa mbali moyo wachoma,
Leo zijue hisia, hisia za wako mama,
Ile chungu ndio tamu, mwanangu mume kahawa. Furaha kuoza mwana, mwanangu nakuambia,
Ila ukiwaza sana, majonzi waniachia,
Kule kutegemeana, hivi ndivyo kwaishia,
Ile chungu ndio tamu, mwanangu mume kahawa. Najiona nimechacha, sijiwezi kwa huzuni,
Weye ndio wangu pacha, nikiwepo shughulini,
Jembe langu laniwacha, lenda kwa wake ayuni,
Ile chungu ndio tamu, mwanangu mume kahawa. Nenda kalete mchicha, alafu wende dukani,
Kisha katupe machicha, usafishe na mezani,
Usiku waenda kucha, niko mwenyewe nyumbani.
Ile chungu ndio tamu, mwanangu mume kahawa. Ishirini nimegota, nafunga wangu uneni,
Neno moja nimewata, mwanangu kuna ukweni,
Utaenda kuwakuta, wapende toka moyoni,
Ile chungu ndio tamu, mwanangu mume kahawa.
Posted by: MwlMaeda - 01-11-2022, 09:32 AM - Forum: Ushairi
- No Replies
Dunia rangi rangile, methali hii muhimu
Usione jambo lile, ukadhani la dawamu
Kila chombo na wimbile, hilo mwenzangu fahamu
Usione ukadhani
Usione mtu yule, hana maisha matamu Ukamsonda kwa ndole, kama kaila haramu Aso hili ana lile, nakujuza muadhamu Usione ukadhani Ati kamaliza shule, ana vyeti kemkemu Aranda huku na kule,mithili mwenye wazimu Hawi wa hivyo milele, siku yake itatimu Usione ukadhani Usimuone na yule, juu ni yake sehemu Halipuuzwi nenole, hadhi yake maalumu Hadumu hivyo milele, mpanga mambo Karimu Usione ukadhani Usimwone mwenye ndwele, haponi ukakalimu Dhana hizo ziondole, kichwanimwo zisidumu Hwenda mzima afile, mwele akatabasamu Usione ukadhani Maisha tangia kale, kueleweka vigumu Yataka mwenye makele, kichwani alo timamu Ndipo kunga amanyile, kwa mambo anozuumu Usione ukadhani Tama hapa niketile, nashusha yangu kalamu Haya ndugu yashikile, upate mastakimu Ila kiyatupa kule,utachekesha kaumu Usione ukadhani
Posted by: MwlMaeda - 01-11-2022, 09:20 AM - Forum: Ushairi
- No Replies
WENETU WAMEPOTEA
Wamepotea wenetu, katika ile ajali, kulia ninathubutu, raha imekaa mbali, ni wadogo wanakwetu, wameenda kwa Jalali, msiba ulotufika, ni msiba wa taifa.
Vurugu zile za chama, kwanza zikae pembeni,
Tuziepushe lawama, kama zile za chamani,
Tumuombeni karima., roho ziende peponi
Maafa yalotufika, ni maafa ya taiga.
Wenetu liliwajaza, gari lile maluuni,
Mwishowe limetuliza, wazazi huku nyumbani,
Tunabaki tunawaza,Hii ni ajabu gani??
Msiba ulotufika, ni msiba wa taifa.
Pia lilikuwa bovu, mesikia karibuni
Enyi muwe wasikivu,Na niwahadithieni,
Lilijaa na ubovu,Lilitoka gerejini,
Ni msiba wa wenetu, kila mtaa kilio.
Kifo ni kifo jamani, cha wenetu kinauma, wenetu Hawa jamani, wamepoteza uzima, wamehama duniani, kwa mola wende SALAMA,
Msiba ni wetu site, tuwaombee kwa mungu.
Tunataka hatutaki, hakuna ataegoma,
Hayuko ataebaki,sisi na watu wazima, ni kuanzia samaki, binadamu na wanyama, tuwaombee wenetu, wende jannatu naima.
Kumbukumbu ya ajali ya wanafunzi wa shule ya Lucky ya Arusha iliyotokea Rhotia –Marera
Posted by: MwlMaeda - 01-11-2022, 08:46 AM - Forum: Ushairi
- No Replies
W. I. V. U ???????
Wivu ni yake asili,
Mapenzini kujivisha,
Aliye wivu mkweli,
Penzi hajabahatisha,
Asiyewivu tapeli,
Penzini anakuchosha. ???????
Wivu waleta mapenzi,
Mapenzi yaleta wivu,
Mwenye wivu anaenzi,
Hatokuacha mkavu,
Mwenye wivu mjenzi,
Penzi litaota shavu. ???????
Ila wivu na karaha,
Daima havipatani,
Wivu mwenzie furaha,
Karaha sio penzini,
Utanawiri wajiha,
Asowivu limbukeni. ???????
Uonyeshe wivu wako,
Na katu usiogope,
Onyesha mpenzi wako,
Mapenzi sio mapepe,
Wakisema watu wako,
Maneno yao yatupe. ???????
Mwenye wivu nahodha,
Kwa jahazi ya mapenzi,
Wivu si kufanya adha,
Mwenye wivu si mshenzi,
Mwenye wivu analadha, ???????