MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'SADFA' - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
ETIMOLOJIA YA NENO 'SADFA' - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16)
+--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'SADFA' (/showthread.php?tid=2296)

ETIMOLOJIA YA NENO 'SADFA' - MwlMaeda - 01-25-2022

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'SADFA'

Neno sadfa katika lugha ya Kiswahili ni nomino: [Ngeli: i-/zi-] yenye maana ya hali ambapo mambo au matukio mawili au zaidi hutokea kwa wakati mmoja bila ya kupangwa au kutarajiwa .

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili sadfa( soma: swidfatun/swidfatan/swidfatin صدفة ) ni nomino ya Kiarabu yenye maana ya kukutana bila ya kukubaliana au kuwa na miadi.

Kinachodhihiri ni kuwa neno hili swidfatun/swidfatan/swidfatin صدفة lilipoingia katika  Kiswahili na kutoholewa kuwa neno la Kiswahili ' sadfa ' halikubadili maana ya lugha asili - Kiarabu ya kutokea jambo au tukio bila ya kupangwa.

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.