ETIMOLOJIA YA NENO 'AILA' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'AILA' (/showthread.php?tid=2287) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'AILA' - MwlMaeda - 01-24-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AILA' Neno aila katika lugha ya Kiswahili ni nomino: [Ngeli: a-/wa-] yenye maana ya ndugu wa familia moja; familia. Katika lugha ya Kiarabu, neno hili aila( soma: aailatun/aailatan/aailatin عائلة ) ni nomino ya Kiarabu yenye maana zifuatazo: 1. Neno la jinsi ya kike kwa neno la Kiarabu aail (soma: aailun/aailan/aailin عائل) lenye maana zifuatazo: a) Mtu mwenye watoto wengi. b) Mtu anayeishi katika lindi la ufukara. c) Mmea unaotegemewa na mmea mwengine kwa makuzi na kupata chakula. d) Familia: Kundi linalokusanya mume, mke, watoto na ndugu wanaowategemea; ndugu wanaoishi nyumba moja. 2. Watu wa nasaba ya babu wa kwanza mmoja; ukoo. Kinachodhihiri ni kuwa neno hili aailatun/aailatan/aailatin عائلة lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno la Kiswahili ' aila ' lilichukua maana moja inayohusu familia/ukoo na kuacha maana zingine zilizo katika lugha asili - Kiarabu. Shukran sana. Khamis S.M. Mataka. |